24-0211 Tazama Aliko Yesu

UJUMBE: 63-1229E Tazama Aliko Yesu

PDF

pakua – m4a

pakua – amr

BranhamTabernacle.org

Mpendwa Mbegu Iliyorutubishwa,

Je! mwaweza kuwazia jinsi gani ingekuwa ni jambo la kupendeza kuketi na kumsikia malaika-mjumbe wa saba wa Mungu akiwaambia jinsi ambavyo hakujiepusha na kuwahubiria habari ya Kusudi lote la Mungu? Akiingia kwa undani sana kuhusu Mvuto wa Tatu, na kuwahakikishia jinsi ambavyo sasa ulivyothibitishwa?

Jinsi Mungu alivyonena na kindi wakatokea; kama vile tu alivyomnena kondoo dume kwa ajili ya Ibrahimu. Jinsi ambavyo Sauti ile ile ilivyomwambia amweleze maskini dada mnyenyekevu aitwaye Hattie, ambaye aliyesema neno sahihi, na kumwambia ya kwamba Sauti ile ile ambayo ilinena kuhusu wale kindi wakawepo ilisema ampe kile alichotaka na aone kama hakitatokea mara moja.

Jinsi ambavyo siku moja wakati alipokuwa akiwinda nyikani pamoja na rafiki zake, dhoruba kali ilitokea ambayo ingemlazimu kuondoka. Lakini jinsi Mungu alivyozungumza naye, mdomo kwa sikio, na kusema, “Niliumba mbingu na nchi. Nilituliza zile pepo zenye nguvu juu ya bahari.”

Jinsi alivyoruka juu na kuvua kofia yake wakati ile Sauti ilipomwambia, “Iambie tu dhoruba, nayo itakoma. Lo lote utakalosema, hivyo ndivyo itakavyokuwa.”

Yeye kamwe hakuihoji hiyo Sauti, bali alinena na kusema, “Dhoruba, koma. Nawe, jua, waka kama kawaida kwa siku nne, hadi tutakapokuwa tumetoka hapa.”

Kabla hajamaliza kusema hayo, ile mvua ya theluji, theluji na kila kitu kilisimama. Jinsi ambavyo katika dakika moja jua kali lilikuwa linawaka mgongoni mwake. pepo zilibadilika na mawingu, kama kitu cha siri, yakiinuka juu angani, na jua lilikuwa linawaka katika dakika chache.

Kisha angewaambia ambavyo miaka 16 kabla hata haujadhihirika, Mungu alimwonyesha kulikuwa na uvimbe kwenye kifuko cha kushoto cha mayai cha Dada Branham, na kwa nini huo ulikuwepo pale. Jinsi walivyoomba na kuomba Mungu auondoe. Ndipo, akatambua kuwa ni Mungu tu anayeijaribu imani yao.

Ndipo tu kabla haujaondolewa kwa upasuaji, alikuwa akizungumza na Mungu na Kumwambia jinsi gani amekuwa mke mzuri sana kwake. Jinsi ambavyo hakuwahi kulalamika kuhusu yeye kutokuwepo nyumbani. Jinsi ambavyo daima alivyotayarisha kila kitu kwa ajili yake wakati alipotaka kwenda kuwinda, kupumzika na kuzungumza na Bwana.

Kisha akasikia kitu fulani chumbani. Alipoinua macho, ile Sauti ikasema, “Simama,” na kumwambia, “Basi lolote utakalosema, hivyo ndivyo itakavyokuwa.”

Alisubiri kwa dakika moja tu, kisha akasema, “Kabla mkono wa daktari haujamgusa, Mkono wa Mungu utaondoa ule uvimbe, na hata hautaonekana.”

Sekunde moja kabla ya mkono wa daktari haujaweza kumgusa, aliponywa. Jinsi daktari alivyomwambia, “Ninataka kukuhakikishia, Bibi Branham, ya kwamba huo uvimbe haupo. Huna uvimbe wowote.”

Jinsi lilivyo Kamilifu Neno la Bwana!

Kumsikia Yeye akiwaambia hakuna shaka tena niani mwake, anajua ule Mvuto wa Tatu ni nini, na anajua unayotenda. Kwa maoni yake, utakuwa kile kitu ambacho kitaanzisha ile imani ya Kunyakuliwa, kwa ajili ya kuondoka.

Kwetu sisi ni kuwa na kicho, na kukaa kimya tu, kwa kuwa ile saa itawadia hivi karibuni ambapo Mungu atatutendea mambo fulani makuu. wakati huo ujapo, wakati kule kufinywa kutakaposhuka, ndipo mtaona, yale mmeona kwa kitambo, yakidhihirishwa katika ule utimilifu wa nguvu zake.

Tutakuwa na baraka hiyo kuu Jumapili hii saa 06:00 SITA MCHANA., saa za Jeffersonville. ( Ni saa 2:00 MBILI USIKU ya Afrika Mashariki ) Ningependa kuwaalika kuungana pamoja nasi tunaposikia: Tazama Aliko Yesu 63-1229E.

Hatutakusanyika pamoja ili kumsikiliza mwanadamu; kuna watu wengi sana barabarani, na wote wanafanana. Hatutakuwa tunatazama na kusikia mhudumu tu, ama mchungaji, tutakuwa tukimtazama na kumsikiliza Yesu. Tutaungana pamoja kutoka ulimwenguni kote kumsikia Yule Mtu, Yule Mtu wa Mungu, Yule Yesu wa Nazareti wa mwili, akiwa Mungu, akinena na Bibi-arusi Wake.

Yakubidi ujiulize mwenyewe, unatazama nini leo? Unaona nini unapotazama? Unaweza tu kumwona Yeye unapomtazama Yeye kupitia kwenye Neno.

Alichokuwa wakati alipotembea Galilaya, ni jambo lile lile alilo huku Jeffersonville, jambo lili alilo kwenye Maskani ya Branham. Unaangalia uone nini, mwanzilishi, mtu wa kimadhehebu? Hutaona jambo hilo katika Yesu. Unatazama umwone mtu mkuu wa kikasisi? Hutaona jambo hilo katika Yesu. La. Unamwonaje Yesu? Kwenye Neno la Mungu likidhihirishwa, kwa maana Yeye alikuwa Neno la Mungu lililodhihirishwa. Alivyokuwa wakati huo, ndivyo alivyo usiku wa leo, na atakuwa hivyo milele.

Mtazame Yesu hivi sasa upate kuishi;
Kwa maana imeandikwa katika Neno Lake, haleluya!
Ni kwamba tu “tunatazama na kuishi.”

Ndugu. Joseph Branham

Maandiko ya kusoma ili kujitayarisha kusikiliza Ujumbe:

Hesabu 21:5-19
Isaya 45:22
Zekaria 12:10
Yohana 14:12