24-0204 Yupo Mtu Hapa Anayeweza Kuiwasha Taa

UJUMBE: 63-1229M Yupo Mtu Hapa Anayeweza Kuiwasha Taa

PDF

pakua – m4a

pakua – amr

BranhamTabernacle.org

Mpendwa Sura ya Yesu Kristo,

Watu wanafikiri sisi ni wendawazimu, tunavyoketi katika nyumba zetu na makanisa, kuzisikiliza kanda. Wanafikiri tunakufa kwa njaa. Hawatambui kuwa tumeketi katika uwepo wa Nuru ya Mwana ya Agosti , tukiivishwa, na kulishwa Chakula Kilichohifadhiwa kama ndama zizini.

Sisi ndio ile Ngano iliyoendelea zaidi, tuko tayari kulipokea. Ikiwa wanataka kuishi katika mapokeo yao, na waendelee. Sio SISI, sisi tunaishi katika Nuru ya siku yetu.

Nuru ya siku yetu ni nini? Mungu alimtuma ulimwenguni malaika wake wa saba mwenye nguvu kumwongoza Bibi-arusi wake. Yeye alikuwa nani? Alikuwa nabii. Yale aliyosema yalitimia. Yeye alikuwa Neno la Mungu lililodhihirishwa. Yeye alikuwa dhihirisho la Nuru ya Neno la Mungu. Yeye alikuwa Nuru ya Mungu kwa ajili ya siku hii.

Musa aliendelea tu hata hivyo, kwa sababu alikuwa ile Nuru. Alikuwa Nuru ya saa ile. Kile alichokuwa nacho, kilikuwa nini? Mungu akidhihirisha Neno Lake lililoahidiwa kupitia kwa Musa, na Musa alikuwa Nuru.

Eliya alikuwa Nuru…Alikuwa nini? Ile Nuru. Haleluya! Alikuwa Nuru, ile Nuru; alikuwa Neno la Mungu lililodhihirishwa.

Yohana, alipokuja duniani… Basi alipojitokeza Yesu alisema alikuwa Taa angavu inayong’ara. Haleluya! Kwa nini? Alikuwa Neno lililodhihirishwa.

Basi kulingana na Neno, Nuru ya siku yetu ni nabii wa Mungu, William Marrion Branham. Yeye yule aliaye katika nyika ya Babeli “Tokeni kwake, enyi watu wangu, msishiriki dhambi zake.”

Yeye alikuwa kutimizwa kwa Malaki 4:5, na Ufunuo 10:7. Yeye alinena tu na kusema, “itakuwa pale,” nayo ilikuwa pale, bila kitu chochote ndani yake. Hakuwa kamwe amempata kindi; hapakuwa na yeyote hapo. Yeye alisema tu, “Na iwe,” na ikawa.

Neno la Mungu halikosei, nalo halina budi kutimia. Tumeiona Nuru; Neno Lake aliloahidi kwa ajili ya siku hii. Limethibitishwa na kuhakikishwa ya kwamba ni Kweli. Ni Nuru ya saa hii.

Hakuna kibadala katika kujua kile tunachosikiliza ni Neno lililodhihirishwa kwa ajili ya siku hii. HALINA WAFURUKUTA MIKIA NDANI YAKE… HATA CHEMBE. Ikiwa wengine watosheka na kitu kingine, na waendelee, lakini sio sisi.

Haimaanishi kuwa huwezi kumsikiliza mchungaji wako, ama kwamba mhudumu hawezi kuhubiri; sivyo hata kidogo, lakini LAZIMA uchuje kila neno unalosikia kupitia chujio kuu la Mungu, UJUMBE HUU KWENYE Kanda.

Wanaposema siku za Ujumbe wa mtu mmoja zimepita, hao ni WAFURUKUTA MKIA. Wanaposema Ujumbe huu sio Yakini yao, hao ni WAFURUKUTA MKIA. Wanaposema kusikiliza kanda haitoshi, hao ni WAFURUKUTA MKIA.

Hakuna kitu kikubwa zaidi ya Kubonyeza Play tu, kujua unaweza kusema AMINA kwa kila neno. Hakuna mahali pengine unapoweza kufanya hivyo isipokuwa kusikiliza Ujumbe wa saa hii.

Sasa sisi ni sura ya Yesu Kristo kwa ajili ya siku hii. Sisi ni Neno Lake lililodhihirishwa. Sisi ndio wale aliowachagua kupokea Ufunuo Wake mkuu wa wakati wa mwisho. Sisi ndio BIBI-ARUSI WAKE.

Ni Bibi-arusi Wake peke yake ndiye atakayekuwa na Ufunuo wa kweli wa Nuru ya siku hii. Watajua, Nuru hii itawakamilisha. Nuru hii ni Roho Mtakatifu akinena kupitia malaika-mjumbe Wake.

Je! ungependa kuketi katika uwepo wa Nuru ya Mungu ya saa hii? Basi ninakualika uje uungane nasi Jumapili saa 6:00 SITA MCHANA saa za Jeffersonville,( Ni saa 2:00 MBILI USIKU ya Afrika Mashariki ) tunaposikia  Yupo Mtu Hapa Anayeweza Kuiwasha Taa 63-1229M.

Ndugu. Joseph Branham.

Maandiko ya kusoma kabla ya ibada:

Mwanzo 1:3, Sura ya 2
Zaburi 22
Yoeli 2:28
Isaya 7:14, 9:6, 28:10, 42:1-7
Mathayo 4:12-17, Sura ya 24 na ya 28
Marko Sura ya 16
Ufunuo Sura ya 3