22-0717 Yupo Mtu Hapa Anayeweza Kuiwasha Taa

UJUMBE: 63-1229M Yupo Mtu Hapa Anayeweza Kuiwasha Taa

PDF

BranhamTabernacle.org

Mpendwa Sura ya Yesu Kristo,

Kama yule mvulana mdogo aliyejitazama kwenye kioo na asitambue kwamba alikuwa akijiangalia mwenyewe, sasa tunatazama katika Kioo cha Mungu, Neno Lake, na tunatambua, BABA, HUYO NI MIMI, Mimi ni Sura ya Neno Lako. Mimi ni Neno Lako lililodhihirishwa. Mimi ni mwamini, mimi ndiye Bibi-arusi Wako!

Kila Ujumbe tunaosikia huinua Imani yetu hadi viwango vipya. Alituambia lazima tujitokeze katika mojawapo ya makundi matatu: Waamini, waamini wakujifanya au wasioamini. Tulipotazama kwenye kioo Chake tulipaza sauti, “Naona, bila kivuli cha shaka, sisi ndio Waamini. Hakika Mwamini ndiye atakayeamini kila nukta na kila yodi; BABA, HUYO NI MIMI.”

Hakuna kitu kinachoweza kuturidhisha na kutupa Uzima ila Neno la Mungu lililonenwa kwenye kanda. Ndiyo njia pekee Uzima unapoweza kuja, kupitia Neno Lake lililonenwa, Sauti ya Mungu kwa ajili ya wakati wetu.

Jitayarishe, kuna mengi zaidi yajayo Jumapili hii, Julai 17, 2022. Kuna mtu hapa ambaye atakaye iwasha Taa, na atakapofanya hivyo, sote tutakuwa na maumivu ya koo kwa kupiga kelele na kupaza sauti, Amina, Haleluya, Jina la Bwana lisifiwe, Utukufu kwa Mungu, kwa sababu Mungu Mwenyewe atakuwa akizungumza nasi moja kwa moja na kulifunua zaidi Neno Lake.

Kama vile lile jua linaloangaza leo litaivisha nafaka kwa ajili ya mavuno mwezi wa Julai. Mwaona ninayomaanisha? Bali Nuru ya leo haitafaa lolote kule nyuma Julai . Ina nguvu zaidi ; ngano imeendelea zaidi. Iko tayari kulipokea. Amina! Hakika iko hivyo .

Mavuno yameiva! Tumeendelea zaidi na tayari zaidi kulipokea. Yesu ana meza iliyotandazwa, ambapo watakatifu wa Mungu wanalishwa kwa Chakula kilichoiva cha siku hii. Nuru ya Injili ikithibitisha na kuhakikisha kwamba Yeye yuko hapa leo pamoja nasi. Watakatifu wanakula Chakula cha kiroho ambacho kimehifadhiwa, wakijiandaa kwa ajili ya Unyakuo.

Wakati Mchungaji wetu, Roho Mtakatifu anapozungumza kupitia kwa nabii Wake aliyethibitishwa, anabonyeza swichi hiyo na kuwasha nuru ya Ufunuo, Yeye atatuambia Yeye ni nani hasa katika wakati wetu. Atapaza sauti na kutuonya,
Natumaini hamjalala.

Nuhu alikuwa Nuru katika siku yake. Musa alikuwa ni Nuru ya saa yake, sasa Nimewatumia nabii mwenye Nguvu katika Wakati wenu, nami ninalidhihirisha Neno Langu lililoahidiwa kupitia kwake. Yeye ni Neno la Mungu lililodhihirishwa katika siku yenu. Yeye ndiye Nuru ya Wakati huu.

Nilipokuwa hapa duniani katika mwili mara ya mwisho, nilichukua ile mikate mitano ya shayiri na kuanza kuimega ile mikate. Kutoka ile ya asili, nilitengeneza mikate na kuwalisha elfu tano.

Kisha nikapata samaki, na kutoka kwa samaki huyo, nikafanya samaki mwingine na samaki mwingine, nikawalisha elfu tano.

Lakini Katika wakati wako, sikuwa na kitu. Nilinena tu na kusema , “Sema itakuwepo,” na ilikuwa pale, bila kuwa na kitu. Yeye alinena tu na kusema, “Sema itakuwapo!” na ilikuwa pale bila kuwa na kitu. Sikuwa na kindi; hapakuwa na mmoja pale. Yeye alisema tu, “Wawepo!” wakawa! Neno Langu haliwezi kukosea na Lazima litimie.
.

Kama wana wa Israeli, walipokuwa safarini, walikuwa wakila mana mpya kila siku. Walikuwa wakitembea katika Nuru ya Nguzo ya Moto. Hiyo Nguzo ya Moto ilikuwa ni Yesu Kristo.

Leo yuko pamoja nasi kwa mara nyingine tena, Nguzo ile ile ya Moto, akifanya mambo yale yale ambayo Yeye alifanya alipokuwa hapa duniani akilitimiza Neno Lake.

Tunakualika uungane nasi Jumapili saa 06:00 SITA MCHANA, saa za Jeffersonville, ( ni saa 1:00 MOJA JIONI ya Tanzania) wakati mchungaji wetu, Roho Mtakatifu, ile Nguzo ya Moto, anapowasha Nuru Yake ya Ufunuo, tunaposikia : 63-1229M “Yupo Mtu hapa Anayeweza Kuiwasha Taa “.

Ndugu. Joseph Branham

Maandiko ya kusoma kabla ya ibada ni:

Mwanzo 1:3, Sura ya 2 yote

Zaburi 22 yote
Yoeli 2:28
Isaya 7:14, 9:6, 28:10, 42:1-7

Mathayo 4:12-17, Sura ya 24 yote na Sura ya 28 yote

Marko Mtakatifu Sura ya 16 yote.

Ufunuo Sura ya 3 yote