22-0710 Aina Tatu Za Waamini

UJUMBE: 63-1124E Aina Tatu Za Waamini

PDF

pakua – m4a

pakua – amr

BranhamTabernacle.org

Mpendwa mwamini,

Hebu wazia jambo hilo, Mungu, ambaye aliumba vitu vyote na kuviweka katika mpangilio, alishuka na kufanyika mwili miongoni mwetu, apate kutukomboa. Na ndipo angetuheshimu sana kwa Uwepo Wake mtukufu, hata angesimama hapa kwenye dunia hii yenye dhambi katika siku za mwisho , na kuthibitisha Neno Lake kuwa hivyo, kwa sababu Yeye ana wajibu kwa Neno hilo.

Roho Mtakatifu amelihuisha Neno hilo kwetu. Nalo Limekuwa hai. Kwa imani tunaliona. Tunajua ni hivyo kwa sababu Neno lilisema hivyo, naye Roho analihuisha Neno hilo kwetu. Sasa tunaunganishwa na Neno la Mungu lililodhihirishwa katika mwili, kama vile tu nabii alivyosema lingefanya.

Mwamini huliamini, anaamini (kitu gani?) Neno. Si kanuni za imani; Neno! Si madhehebu; Neno! Si kile anachosema mtu mwingine; kile lisemacho Neno! Naam, kumbukeni, huyo ni mwamini. Mwamini haulizi. Mwamini hasemi, “Inawezekanaje? Laiti ningaliweza kulielezea !” Huyo ni asiyeamini . A-ha. Ni mwamini, ambaye, haidhuru ni kitu gani, “Kama ni Neno, Ni Neno! Hilo ni kweli.” Huyo ndiye mwamini.

Huna budi kuamini kila nukta na kila yodi, na kila kitu kilichosemwa Humo ndani. Hakina budi kuwa ni kweli. kama Ukisema, “Siamini Jambo hilo. Baadhi ni Mungu, baadhi ni mwanadamu, baadhi ni hadithi za kuwinda tu.” Vema, basi wewe ni Asiyeamini. Mwamini haulizi. Mwamini huliamini Hilo, haidhuru linasikika namna gani ama lo lote mtu ye yote asemalo juu Yake, jinsi linavyoonekana lisilowezekana , SISI TUNALIAMINI!

Kila mtu aliyepo hapa, aliyeko, kila mtu anayesikiliza kanda hii; na hata ingawa siku moja sina budi kuondoka humu duniani, kanda hizi zingali zitaendelea. Hiyo ni kweli. Mnaona? Nanyi mmo katika moja ya tabaka hizi. Huna budi kuwa katika moja ya hizo.

Tunaishi katika siku za mwisho na yakubidi uangalie maisha yako na uone ni tabaka gani la watu ulilomo. Je! unasema, “Ninaamini Mungu alimtuma nabii ambaye amethibitishwa kwa Nguzo ya Moto?” yeye Alituambia tuamini kila Neno. Kusema HASA kile kilicho kwenye kanda na kutobadili hata Neno moja. Tutahukumiwa kwa yale YEYE ALIYOSEMA, si kwa yale ambayo mtu fulani aliyosema ati alisema, ama yale mtu fulani anasema alimaanisha, bali kwa yale kanda zisemavyo.

Au, utaambatana pamoja na Kora na Dathani, na wale wanaosema, “Yeye siye mtu pekee aliye mtakatifu. Kuna wengine wameitwa kufanya mambo haya aliyofanya. Unamtukuza sana nabii wa Mungu. Roho Mtakatifu ndiye anayetuongoza hivi sasa. Huu ni wakati tofauti.”

Wewe umo katika moja ya tabaka hizi. Katika hali yako ya sasa hivi, hali yako ya sasa ya akili, kwamba, ninyi mlio hapa katika mkutano huu unaoonekana, nanyi mtakaokuwa katika mikutano isiyoonekana ya kanda hii, hali yako ya sasa ya akili baada ya kuisikiliza kanda hii, inakuthibitishia uko katika tabaka gani. Inakwambia mahali ulipo hasa, iwapo wewe ni mwamini katika Neno na utadumu Nalo, kama ungeondoka uende zako, ama kufunga kanda hiyo.

Jina la Bwana lihimidiwe, sisi ndio WAAMINI Halisi, si mtu aliyeshawishiwa na mtu mwingine; si kwa jambo lingine, bali Roho Mtakatifu ametufunulia Neno Lenyewe. Tunaona Neno likiwekwa wazi, Likithibitishwa na kudhihirishwa.

Tunajaribiwa kwa hayo majaribu, zile barabara zenye mavumbi, joto la jua la mateso, lakini uaminifu wa mioyo yetu unavifua vitu hivyo vya Neno. Sasa tunakuwa tayari kufinyangwa. Sisi ni Watoto wa Mungu, tumetengenezwa barabara kwa Neno Lake. Sisi ni mifano iliyo hai, nalo Neno la Mungu likiishi kupitia kwetu. Jaribio huja kututikisa, kutuweka kule chini kabisa, kuona mahali tutakaposimama. Lakini hatutaondoshwa, Tunasimama kwenye Kila Neno.

Sikiliza anapokuambia wewe ni nani.

Kumbuka tu ya kwamba kila sehemu yako ilikuwa hapa, wakati Mungu aliponena ulimwengu ukawa. Yeye aliuweka mwili wako wakati uo huo. Wala hakuna kitu kinachoweza kuuondoa ila Mungu.

Hakuna kinachoweza kuliondoa hilo kutoka kwako. Hakuna mtu anayeweza kupachukua mahali pako, haidhuru ni padogo namna gani. Unasema, “Mimi ni mke wa nyumbani tu.” Hakuna mtu anayeweza kupachukua mahali pako. Mungu, katika uchumi Wake mkuu, ameweka jambo hilo hivyo, Mwili wa Kristo, katika utaratibu, hata hapana mtu anayeweza kupachukua mahali pako.

Utukufu… Haleluya… Kusikiliza Chakula cha Mungu kilichowekwa ghalani kunazidi kuwa kukuu zaidi na ZAIDI . Kadiri tunavyomsikia Mungu akinena kupitia mjumbe wake mteule akituambia sisi ni nani, ndivyo Imani yetu inavyokuwa kubwa zaidi. Furaha kubwa ya kujua:

. Sisi ndio “WAAMINI HALISI”
. Sisi ndio “WAMOJA WAO”
. Sisi ndio “BIBI-ARUSI “

Ningependa KUKUALIKA KUBONYEZA PLAY pamoja nami, pamoja na Maskani ya Branham, pamoja na sehemu ya Bibi-arusi kutoka ulimwenguni kote saa 6:00 SITA MCHANA , saa za Jeffersonville, ( ni Saa 1:00 MOJA JIONI Ya Tanzania), Wakati tutakapokusanyika kutoka Mashariki, Magharibi, Kaskazini na Kusini Kusikia: Aina Tatu za Waamini 63-1124E . Hivi ndivyo Roho Mtakatifu anavyotuongoza kufanya. Kwetu sisi, huu ndio mpango wa Mungu.

. Bonyeza Play: Kanda yoyote ambayo Mungu anaweka moyoni mwako.

. Bonyeza Play : Sikiliza wakati wowote utakaochagua.

. BONYEZA PLAY : Ndiyo ujumbe wangu kwako.

Ndugu. Joseph Branham.

Maandiko ya kusoma kabla ya ibada :

Yohana Mtakatifu 6:60 – 71