Category Archives: Uncategorized

23-0723 Muhuri Wa Kwanza

UJUMBE: 63-0318 Muhuri Wa Kwanza

PDF

pakua – m4a

pakua – amr

BranhamTabernacle.org

Wapendwa…Nitawaita Bibi-arusi,

Mungu, Muumba Mkuu, Alfa na Omega, Nyiroro ya mabondeni, Ua la Sharoni, Nyota yenye Kung’aa ya Asubuhi, Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu, Nguzo ya Moto, Mungu Mwenyewe, alikuja duniani na kunena nasi kupitia midomo ya mwanadamu, UTUKUFU!, Akaiweka kwenye kanda ya sumaku, ili Ninyi mweze kumsikia YEYE Akiwaita… “NINYI” BIBI-ARUSI WAKE.

Lioneni kwa picha dhairi jambo hili enyi marafiki. Bwana wetu Yesu Kristo, akiwatazama machoni na kuwaambia: “Ninyi ni Bibi-arusi Wangu. Nawapenda. Nimewangojea kwa muda mrefu sana. Kwangu Mimi, ninyi ni wakamilifu. Ninyi ni nyama ya nyama Yangu, mfupa wa mfupa Wangu. Niliwachagua ninyi kabla sijaumba Dunia au nyota. Nawapenda sana. Tutaishi Milele pamoja. Sasa, ninakuja kuwachukua.”

Hilo peke yake linapaswa kumpa kila mmoja wetu Imani ya Kunyakuliwa. Ni kitu gani ibilisi anaweza kuwarushia, kuwaambia, kukiweka juu yenu ambacho kinaweza kuwadhuru? HAKUNA CHOCHOTE, NINYI NI BIBI-ARUSI WA KRISTO! Ninyi ni Neno Lake lililofanyika mwili, ninyi ni Bibi-Yesu Kristo.

Anawezaje mtu yeyote, katika lugha yoyote, kuandika na kutuelezea nini maana yake? Huwezi kabisa.

Hakuna mahali popote duniani unapoweza kuwa na heshima na majaliwa hayo ya kusikia Maneno haya isipokuwa uwe na Ufunuo sahihi na UBONYEZE PLAY.

Yale matukio makuu zaidi ambayo ulimwengu umekuwa ukingojea tangu mwanzo wa wakati, yanatukia sasa hivi, nasi tu sehemu ya hilo. Yeye ameingojea siku hii, saa hii, watu hawa; NINYI, kuutimiza na kuutekeleza Mpango Wake Mkuu.

Ufunuo wa ile siri ya ile Mihuri Saba, zile Ngurumo zikifunuliwa, ukamilifu wetu, Adamu Wake aliyerejeshwa kikamilifu, Kuja Kwake, mambo haya yote yanadhihirishwa na yanatimia SASA HIVI, ndani YENU, BIBI-ARUSI WAKE!

Si katika siku za Musa. Si katika siku za Nuhu. Si katika siku za Yesu, Si hata katika siku za Yohana ama Paulo; Inatukia sasa, SASA HIVI, KWENU NINYI.

Hatutaki kulikosa. Tunataka kuwa tayari kwa ajili ya huku Kuja Kwake. Ili kufanya jambo hilo, tumeagizwa kwenda kwenye NENO kupata majibu yetu. Si wazo langu, ama wazo la mtu fulani ama mafikara yake, bali Yale Neno la Mungu lililothibitishwa linasemayo.

Tunajua Bibi-arusi yampasa kusema “amina” kwa kila Neno na kuungana pamoja kuwa Mmoja. Kwa hiyo ni lazima tuangalie katika Neno la Mungu ili tuone ni kitu gani kitakachomuunganisha Bibi-arusi pamoja.

Na ndipo kunakuja Ngurumo saba za siri ambazo hata hazijaandikwa kamwe. Hiyo ni kweli. Nami naamini ya kwamba, kupitia Ngurumo hizo Saba, zitafunuliwa katika siku za mwisho ili kumkusanya Bibi-arusi pamoja kwa ajili ya kupata imani ya kunyakuliwa.

Papo hapo liko katika Neno. Hizo Ngurumo Saba zitafunuliwa katika siku yetu ili kumkusanya Bibi-arusi pamoja kwa ajili ya kupata imani ya kunyakuliwa.

Kisha swali linalofuata tunalohitaji kujua ni: Je, hizo Ngurumo ni nini?

Wakati, ile “iliponguruma.” Kumbuka, sauti kuu ya kishindo cha Ngurumo ni Sauti ya Mungu. Hivyo ndivyo Biblia isemavyo, unaona, “kishindo cha Ngurumo.” Wao walidhani ilikuwa ni ngurumo, lakini ilikuwa ni Mungu. Yeye aliielewa, kwa maana ilifunuliwa Kwake. Unaona? Ilikuwa ni Ngurumo.

Kwa hiyo zile Ngurumo ni Sauti ya Mungu itakayomkusanya Bibi-arusi pamoja na kuwapa (SISI) imani ya Kunyakuliwa. Hilo hapo jibu letu.

Ni nani aliye Sauti ya Mungu kwa Bibi-arusi?
William Marrion Branham.

Sasa, mimi ni ndugu yenu tu, kwa neema ya Mungu, lakini pindi huyo Malaika wa Bwana anaposhuka, inakuwa, basi, Sauti ya Mungu kwenu…Mimi siwezi kusema neno lolote mwenyewe, ila kile Yeye anachonionyesha, Mimi Nakisema. Ninyi aminini jambo hilo na mwone kinachotokea.

Liaminini jambo hilo na mwone kile kitendekacho na kutukia Jumapili hii, tutakapokusanyika pamoja, kupokea imani ya kunyakuliwa, kumsikia Yeye Akinguruma kwa Bibi-arusi Wake.

Nena “kuhusu kuketi sasa katika ulimwengu wa Roho”? Itakuwaje! Kama tunaweza kujisikia hivi, hali tumeketi hapa duniani, kabla ya kuja kwa Kunyakuliwa, katika hali hii tuliyo nayo sasa; nasi tunaweza kufurahi, na tukisimama kando-kando ya kuta, na kusimama kwenye mvua, ili tu kusikia jambo Hili; itakuwaje tutakapomwona Yeye ameketi pale! Loo! jamani! Loo! utakuwa ni wakati wa fahari kweli.

Usikose katika wakati huu mtukufu. Umealikwa kukusanyika pamoja nasi tunaposikia: Muhuri wa Kwanza 63-0318, saa 06:00 SITA MCHANA, saa za Jeffersonville.( ni saa 1:00 MOJA JIONI ya Afrika Mashariki)

Ndugu. Joseph Branham

Maandiko ya Kusoma Kwa Maandilizi ya Kusikiliza Ujumbe:

Mtakatifu Mathayo 10:1 / 11:1-14 / 24:6 / 28:19
Yohana 12:23-28
Matendo 2:38
2 Wathesalonike 2:3-12
Waebrania 4:12
Ufunuo 6:1-2 / 10:1-7 / 12:7-9 / 13:16 / 19:11-16
Malaki Sura ya 3 na ya 4
Danieli 8:23-25 ​​/ 11:21 / 9:25-27

23-0716 Pengo Kati Ya Nyakati Saba Za Kanisa Na Ile Mihuri Saba

UJUMBE: 63-0317E Pengo Kati Ya Nyakati Saba Za Kanisa Na Ile Mihuri Saba

PDF

pakua – m4a

pakua – amr

BranhamTabernacle.org

Wapendwa Yungiyungi dogo za Kidimbwi,

Tumejipenyeza hadi juu ya maji yenye matope na kutandaza mbawa zetu. Petali zetu ndogo zimetokeza na sasa linaakisi ua la Uwandani . Tumeweka maisha yetu kikamilifu kwa Mungu na Neno lake.

Tuko katika wakati wa mwisho tukitoka Mashariki na Magharibi, Kaskazini na Kusini, tukijiweka tayari kwa ajili ya huo Unyakuo. Tukijishikilia imara kwa dakika chache mpaka kila mshipa umejazwa na Roho Mtakatifu. Tunajiweka tayari KUPAA JUU.

Siku yenyewe imefika. Anawaita watu Wake pamoja Kwake katika umoja wa kweli na Yeye Mwenyewe. Ni Yesu Kristo akiishi pamoja na Roho wake katika mwili wetu, akifanya mambo yale yale aliyoyafanya kama bendera kwa ulimwengu.

Jambo lililo tukufu zaidi katika Maandiko linatendeka katika wakati wetu. tendo, ambalo hata Malaika, hakuna kitu, kingaliweza kufanya jambo hilo, ila Mwana-Kondoo. Alikuja na kukitwaa kile Kitabu kutoka katika mkono wa kuume wa Yeye aliyeketi juu ya kile Kiti cha Enzi, akakifungua, akaichana ile Mihuri, na kukituma duniani, kwa malaika Wake wa saba, atufunulie SISI, Bibi-arusi Wake.

Mambo yanayotukia; Neno analotufunulia kila siku, hayaelezeki. Tunapaza sauti zetu, na kupiga vifijo na vigelegele, Haleluya! Upako, nguvu, utukufu, dhihirisho, Ufunuo huu wa Neno Lake ni mkuu kuliko ulivyopata kuwa tangu mwanzo wa wakati.

Pamoja na kila kiumbe kilichoko mbinguni, na juu ya nchi, na chini ya nchi, ndani ya bahari, na vyote vilivyomo ndani yake, tunapaza sauti: Baraka, heshima, utukufu, uweza, ni kwake Yeye aketiye juu ya kile kiti cha enzi, na Mwanakondoo milele, amina! Amina, na amina!

Kila kiumbe, kila mtu tangu mwanzo wa wakati walingojea siku hii ifike. Hata Mungu Mwenyewe alingojea mpaka malaika Wake mteule alipofika duniani kabla ya Yeye kujitokeza kukitwaa kile Kitabu, kukifungua na kuzifunua siri Zake zote kwa Bibi-arusi Wake mteule.

Sasa tunajua yale ambayo hakuna mwanadamu duniani, tangu mwanzo wa wakati, amewahi kujua. Kila kitu kilichopotezwa katika lile anguko. Kila kitu ambacho kimefichwa katika Neno Lake. Kila kitu ambacho Bibi-arusi anachohitaji kimerekodiwa na kimewekwa katika ghala moja dogo la Mungu.

Ametuonyesha Kule ng’ambo ya pili ya pazia la Wakati nasi tunajiona wenyewe tukiwa pamoja Naye kule upande wa Pili. Bibi-arusi amejifanya tayari kwa kusikia Neno.

Tumekuwa katika mafunzo. Tumevaa silaha zote za Mungu. Hakuna kinachoweza kutuondosha. Hakuna kinachoweza kututisha. Hakuna kinachoweza kutudhuru. Hakuna kinachoweza kutufanya kupatana hata kwenye Neno moja. SISI NI NENO.

Tunamngojea huku tukiwa na shada letu la maua mikononi mwetu. Muda umefika. Ile Saa ya kale inayoyoma. Tunasikia farasi wakienda shoti, mchanga ukivingirishwa chini ya gurudumu. Lile gari la Kale la farasi liko karibu kusimama.

Atakapokuja tutaruka kutoka katika ulimwengu huu wa kale nakuangukia Mikononi mwake. Atatunyakua na kusema, “Nilikuwa nimekwenda kuwaandalia mahali, lakini yote yamekwisha sasa, mpenzi”.

Kuja Kwake kumekaribia sana. Tuko chini ya matarajio zaidi ya hapo kabla. Tunayo furaha sana kwa anavyotaka tuisikie ile Mihuri Saba kwa mara nyingine tena. Tunajua tutapokea Ufunuo zaidi, kwa sababu kila Ujumbe tunaousikia ni kana kwamba kamwe hatujawahi kuusikia hapo awali.

Kuishi leo hii na kusikia Ujumbe huu ni hata kuu zaidi kuliko wakati uliporekodiwa. Yeye Anatufunulia hata na zaidi sasa hivi. Ni kitu gani kingeweza kutokea?

Njoo ukusanyike pamoja nasi saa 06:00 SITA MCHANA, saa za Jeffersonville,( Ni saa 1:00 MOJA JIONI ya Afrika Mashariki),na Kufurahia kusikiliza:  
63-0317E Pengo Kati ya Nyakati Saba za Kanisa na Ile Mihuri Saba. Ni Chakula Kilichohifadhiwa alichokiandaa Bwana kwa ajili ya Bibi-arusi kula.

Ndugu. Joseph Branham

Maandiko ya kusoma kwa maandalizi ya kusikiliza Ujumbe:

Mambo ya Walawi 25:47-55
Yeremia 32:1-15
Zekaria 3:8-9 / 4:10
Warumi 8:22-23
Waefeso 1:13-14 / 4:30
Ufunuo 1:12-18 / Sura ya 5 yote/ 10:1-7 / 11:18

23-0709 Mungu Akijificha Kwa Urahisi, Halafu Akijifunua Kwa Jinsi Hiyo

UJUMBE: 63-0317M Mungu Akijificha Kwa Urahisi, Halafu Akijifunua Kwa Jinsi Hiyo

PDF

BranhamTabernacle.org

Wapendwa Watu Wateule, Wa kipekee, Wasio wa kawaida, Ukuhani wa Kiroho, Taifa la Kifalme,

Ni wakati ulio wa fahari jinsi gani ambao Yeye Amekuwa akimpa Bibi-arusi Wake, akifunua Neno Lake zaidi ya hapo nyuma. Kila Ujumbe tunaousikia inaonekana kana kwamba hatujawahi kamwe kuusikia hapo awali. Mioyo na nafsi zetu zimejaa furaha tunapofanyia karamu Mana Mpya ishukayo kutoka Mbinguni. Inaonekana kama onyesho letu la awali la Karamu yetu ya Harusi inayokuja hivi karibuni anapotulisha Ufunuo baada ya Ufunuo.

Tunamtolea Mungu dhabihu za kiroho, kwa matunda ya midomo yetu, tukilisifu Jina Lake. Tumetwaa nafasi zetu kama nyota za mbinguni.

Ametuunganisha pamoja katika ulimwengu wa roho, akimimina Roho Wake Mtakatifu juu yetu, akitutayarisha kwa ajili ya Kuja kwake hivi karibuni. Ndio yote tunayoweza kuwazia. Ndio yote tuliyo nayo akilini mwetu. Yote tunayotaka kufanya ni KUSIKIA NENO. Yeye anatuambia tena na tena sisi ndio Bibi-arusi Wake. Haya ndio Mapenzi yake Makamilifu kwa kukaa na Njia yake iliyoandaliwa.

Sisi ni askari katika Idara ya Huduma Yake ya kanda, nasi tunajivunia jambo hilo. Ni beji ya heshima. Tunatamani kulisema kwa sauti na kuuambia ulimwengu, NDIYO, SISI NI MMOJA WAO.

Ametupa Chakula kilichohifadhiwa ili tupate kula. Ile Mana ya Mungu Mwenyewe akinena na Bibi-arusi Wake, akitujulisha sisi tuko katika jeshi Lake.

Tunakusanyika chini ya dari kuu la mbinguni katika upatano sana, hata Roho Mtakatifu amemweka kila mshirika wa ule Mwili hata kumekuwa na uponyaji unaobubujika wenyewe wa nafsi na mwili.

Tunalichukua Neno la Mungu na kumshinda ibilisi na nguvu zake. Tunamkatakata vipande-vipande kwa Neno hilo. Kapteni wetu Mkuu alituambia: “Wewe ni Neno. Usiogope. Nenda moja kwa moja hadi kwa Ibilisi na useme, ‘IMEANDIKWA.’”

Ametuchagua tuwe askari wake. Tumekuwa katika mafunzo, tumeimarishwa na Neno Lake. Sasa tumevaa na tuko tayari kwa mapambano. Jenerali wetu mwenye Nyota 5 ametuamuru nini la kufanya: Shikilieni kabisa hayo mafundisho Yangu ya kanda.

Nanyi mwe na hakika, semeni tu yale tu kanda inayosema. Msiseme jambo lingine lo lote. Mnaona? Maana, sisemi jambo Hilo kwa nafsi yangu mwenyewe. Yeye Ndiye anayesema Hilo , mnaona. Na mara nyingi sana, vurugu, watu wanainuka na kusema, “Vema, Fulani alisema ilimaanisha hivi-na-hivi.” Liache tu jinsi lilivyo.

Si yale William Branham anayotuambia kwenye kanda, ni yale MUNGU anayomwambia Bibi-arusi Wake kwenye kanda. Haya ni MAAGIZO yake. Kuna njia moja tu ya kutii maagizo haya kutoka kwa Jenerali wako mwenye Nyota 5 na uliache jinsi lilivyo, KUBONYEZA PLAY.

Tuko katika jeshi la Mungu, kwa hivyo lazima tutii maagizo yetu Neno kwa Neno. Tunasonga mbele. Sisi ni watu mashujaa, watu wa imani, watu wenye nguvu, watu wenye ufahamu, watu wa Ufunuo.

Tunakuwa katika ushirika mkamilifu na Baba tena, tukisimama upande ule mwingine wa shimo, bila kumbukumbu la dhambi dhidi yetu. Adamu wake aliyerejeshwa.

Ni Mungu katika urahisi kwa mara nyingine tena. Si kwa ajili ya kila mtu, Bibi-arusi Wake peke yake, nasi tunaliona waziwazi na dhahiri kabisa.

Ninayo matazamio makuu ya kuisikia ile Mihuri Saba kwa mara nyingine tena. Yeye atakuwa akitufunulia Neno Lake zaidi ya hapo awali. Tutakuwa tukipokea Ufunuo ulio mkuu zaidi wa Neno Lake.

Yeye amengojea hadi siku hii ya leo ili kutufunulia sisi mengi zaidi. Yote tunayohitaji yamerekodiwa na yanapatikana kwa ajili yetu kuyasikia kwa mguso tu wa kidole chetu.

Ujumbe huu ndio zile Ngurumo Saba zitakazomkamilisha Bibi-arusi; kwa maana SIRI ZOTE ZA MUNGU ZITAFUNULIWA NA MALAIKA-MJUMBE WETU WA 7 KWA BIBI-ARUSI.

Huu ni wakati wenye fahari mno katika historia ya ulimwengu. Tuko ukingoni mwa kuja Kwake kumjia Bibi-arusi Wake. Ulimwengu unatarajia mambo haya yote yaliyonenwa katika Maandiko; kama jua kutua mchana na mambo ya kila namna kutukia. Lakini imepita tayari, na hawakujua.

Kumbukeni, kimetiwa muhuri na hizo Ngurumo Saba za siri. Unaona?

Mambo makuu yanaenda kutukia tunapokusanyika kwa mara nyingine tena ili kumsikia Mungu Akinguruma na kumfunulia zaidi Bibi-arusi Wake kwenye ile Mihuri Saba.

Ninakualika uungane nasi saa 06:00 SITA MCHANA, saa za Jeffersonville, ( Ni saa 1:00 MOJA JIONI ya Afrika Mashariki ) tunapoanza mfululizo huu mkuu kwa Ujumbe:
63-0317M Mungu Akijificha Kwa Urahisi, Halafu Akijifunua kwa jinsi hiyo.

Wakati Ndugu Branham anapoweka wakfu upya kwa Mungu Maskani ya Branham na watu, hebu na tujiweke wenyewe wakfu upya Kwake, nyumba zetu, makanisa yetu, ama popote tunapokusanyika.

Ndugu. Joseph Branham

Maandiko ya Kusoma kwa maandalizi ya Kusikiliza Ujumbe:

1 Mambo ya Nyakati 17:1-8
Isaya 35:8 / 40:1-5 / 53:1
Malaki Sura ya 3
Mathayo 11:10, 11:25-26
Yohana 14:1-6
1 Wakorintho Sura ya 13
Ufunuo Sura ya 21

23-0702 Vita Vikuu Sana Vilivyowahi Kupiganwa

UJUMBE: 62-0311 Vita Vikuu Sana Vilivyowahi Kupiganwa

PDF

pakua – m4a

pakua – amr

BranhamTabernacle.org

Wapendwa Vikosi Maalum vya Huduma ya Kanda.

Hebu na tuungane pamoja kwa ajili ya kipeo kikuu cha wikendi ya ajabu ya mafunzo ambayo tumekuwa nayo, tunapomsikia Jenerali wetu mwenye Nyota 5 akizungumza kupitia malaika Wake mteule wa duniani na kutuelekeza jinsi ya kupigana na kushinda Vita Vikuu Sana Vilivyowahi Kupiganwa 62-0311.

Wapi: Makao Makuu (Kiti cha Enzi cha Mungu)

Muda gani: Saa 8:00 NANE MCHANA. Masaa ya JEFFERSONVILLE ( ni saa 3:00 TATU USIKU ya Afrika Mashariki )

Ndugu. Joseph Branham

23-0625 Hii Ndiyo Ishara Ya Mwisho, Bwana?

Ujume: 62-1230E Hii Ndiyo Ishara Ya Mwisho, Bwana?

PDF

BranhamTabernacle.org

Mpendwa Bibi-arusi Neno kwa Neno,

Hakuna nabii, hakuna mtume, kamwe, katika wakati wo wote, aliyewahi kuishi katika wakati kama huu tunaoishi sasa. Huu ndio wa mwisho. Ile Nguzo ya Moto imerudi. Ile Nguzo ya Moto ambayo iliwaongoza wana wa Israeli; Ile ile iliyompiga Sauli ikamwangusha akienda zake Dameski. Ile ile imekuja na Nguvu ile ile, ikifanya mambo yale yale, na ikifunua Neno lile lile, ikidumu Neno kwa Neno na Biblia!

Siri zote zilizofichwa zilifunuliwa kwake yeye. Je, umeona, Siri ZOTE. Hakuna jipya, hakuna kilichoachwa, hakuna kitakachofunuliwa kutoka kwa mtu mwingine ye yote; YOTE yalifunuliwa kwa malaika-mjumbe Wake wa saba na hayo tumepewa SISI, Bibi-arusi Wake, kwenye Kanda.

Ndiyo YOTE Bibi-arusi anayohitaji; ANGALIA TENA, YOTE BIBI-ARUSI ANAYOHITAJI . Wengine wanahitaji vitu vingine, nao wamepewa vitu hivyo. Lakini tunachohitaji sisi kimerekodiwa na tumepewa hicho kwenye Kanda NACHO kinatupa IMANI ya Kunyakuliwa.

Sisi ndilo kanisa lile ambalo Bwana Mungu alimpa. Haya ndiyo makao yake makuu. Hapa ndipo Yeye alipotuambia tukae. Si jengo, KANDA. Sisi ndio kundi lile la watu wanaoamini, na wenye njaa na wanaoshikilia kila Neno. Alituambia tukae hapa na tuliangalie lile Jiwe Jeupe, Jiwe gumu sana, NENO KWENYE HIZI KANDA.

Sauti kutoka Mbinguni ilinena naye na kusema, “Lete Chakula. Kihifadhi mle ndani. Hiyo ndiyo njia pekee ya kuwaweka hapa, ni kuwapa Chakula”. Yeye Hakusema tafuteni kitu kingine, ama ya kwamba kutakuwa na mafunuo mapya kutoka kwa mtu mwingine; angalieni CHAKULA HIKI KILICHOHIFADHIWA KWENYE KANDA, KAENI HAPO.

Lakini kama tu vile walivyofanya katika ndoto zote alizofunua, baadhi yao wakaenda huko; baadhi yao wakachukua njia moja, na wengine nyingine. Wachache sana ndio waliobakia na wakaendelea kuangalia kile ambacho YEYE aliwaambia.

Sasa linganisha hilo na zile nyingine, zile ndoto. Hili lilikuwa ono. Kile chakula; hiki hapa. Mahali penyewe ni hapa.

Asingeweza kuwa wazi zaidi kwa Bibi-arusi Wake zaidi ya hapo. Hili lilikuwa ono, si ndoto, ONO. Chakula kiko hapa: KANDA. Mahali penyewe ni hapa: KANDA. Tunafanya vile hasa alivyotuambia tufanye: Kuzisikiliza KANDA!

Inahitaji Ufunuo wa Kiroho kuelewa mambo haya. Itahitaji Ufunuo wa Kiroho kuamini na kuelewa yote atakayotuambia Jumapili hii. Utakuwa ni wakati uliyotukuka kwa Bibi-arusi.

Kuna mambo mengi sana Mungu anatuambia na kutufunulia kwenye Ujumbe huu. Ninataka kunakili nukuu baada ya nukuu na kuwapeni, lakini najua atawafunulia kila kito cha thamani kwa sababu alisema huyu ndiye ninyi mlikuwa:

Hili ndilo kanisa ambalo Bwana Mungu alinipa. Hapa ndipo makao makuu yangu. Hapa ndipo ninapokaa…kuna kundi la watu hapa wanaoamini na wana njaa na wangali wanashikilia.

Sisi ndio kundi hilo ambalo lina njaa na linaloshikilia. Watu Wengi hawatuelewi na wanatufanyia mzaha, lakini hiyo ni sawa, tunawapenda na kuwaombea; bali sisi tunataka SAUTI MOJA tu kutuongoza.

Nisamehe, lakini sina budi kukupa nukuu hii.

“Aanzapo kupiga baragumu, siri itatimizwa”. Sasa, angalia: Basi wakati umewadia wa kufunuliwa kwa zile Sauti za Muhuri Saba za Ufunuo 10. Mnaelewa? Wakati siri zote za kile Kitabu zimemalizika, na Biblia ilisema hapa kwamba angetimiza zile siri .

Nani ambaye angetimiza zile siri? Mchungaji wako? Kundi? Mimi? Malaika-Mjumbe wa Saba: William Marrion Branham. Hakuna mtu kabla yake, kipindi chake, ama baada yake. ANGETIMIZA ZILE SIRI.

Huenda ikawa ni wakati wa mwisho. Huenda ikawa wakati umewadia wa pinde za mvua kupita angani na tangazo toka mbinguni likisema, “Wakati umekwisha.” Kama ndivyo ilivyo, hebu na tujiandae, marafiki, kumlaki Mungu wetu.

Ndiyo, Bwana, tunataka kujiandaa kukulaki wewe. Tunataka kufanya yote tuwezayo. Tunataka kuwa katika Mapenzi Yako makamilifu. Tafadhali tuambie Baba, tufanye nini ili tuweze kujiandaa?

Kumekwisha wekwa chakula kingi sana sasa; hebu na tukitumie. Hebu na tukitumie sasa.

Asante Baba kwa Chakula ulichokihifadhi kwa ajili ya Bibi-arusi Wako na ule Ufunuo Wake. Tunakitumia kila siku.

Naomba msamaha kwa kanisa langu dogo hapa, ambako Wewe umenituma kulielekeza na kuliongoza. Wabariki, Bwana. Nimetenda kulingana na yale maono na ndoto na kadhalika vimesema kadiri nijuavyo mimi. Nimehifadhi chakula chote, vizuri nijuavyo, kwa ajili yao , Bwana. Hata iwe nini, Bwana, sisi tu Wako.

Asante Bwana, umetuambia kwa mara nyingine tena, umekihifadhi Chakula chote tunachohitaji kwa safari yetu.

Ni Vigumu kwangu kungojea kusikia, Hii ​​Ndiyo Ishara ya Mwisho, Bwana? 62-1230E, pamoja na kila mmoja wenu Jumapili saa 06:00 SITA MCHANA saa za Jeffersonville.( Ni saa 1:00 MOJA JIONI masaa ya Afrika Mashariki),Najua mambo yatafunuliwa kwetu zaidi ya hapo awali. Hii inaweza kuwa mara ya mwisho sisi kusikia jambo hili.

Vipi kama ni kitu cha kutujulisha jinsi ya kuingia katika imani ya kunyakuliwa! Sio? (Tutakimbia na kuruka juu ya kuta?) Kuna jambo lililo tayari kutukia, na hii miili ya kale iliyoharibika, mipotovu, itabadilishwa? Naweza kuishi nipate kuliona, ee Bwana? Lipo karibu sana kwamba nitaliona? Hiki ndicho kizazi kile? Mabwana, ndugu zanguni, ni wakati gani? Tuko wapi?”

Ndugu. Joseph Branham

23-0618 Wakati wa Kanisa La Laodikia

UJUMBE: 60-1211E Wakati wa Kanisa La Laodikia

PDF

BranhamTabernacle.org

Wapendwa Waamini wa Neno lisilokosea,

Jinsi gani imekuwa ni jambo lakupendeza sana kusikia na kusoma Nyakati hizi Saba za Kanisa. Kwa kila Ujumbe tunaousikia, kila sura tunayosoma, Yeye anatupa Ufunuo zaidi. Tunajiona waziwazi tukishuka kuja kupitia kila wakati wa kanisa…Bibi-arusi Wake, ambaye alidumu na Neno la asili.

Katika nyakati zote tunaziona roho hizo mbili kwa uwazi; Udanganyifu na uongo wa Shetani, kulipotosha Neno la Mungu, kuwadanganya, kuwapotosha na kuwashinda watu. Lakini wakati wote kumekuwa na kundi dogo la Mungu la watu waaminifu, Bibi-arusi Wake, wakishikilia kila Neno.

Wakati wote kuna onyo moja la daima linalotolewa kwa watu, yawabidi KUDUMU NA NENO. Mara tu unapopata kutoka nyuma ya Neno hilo, unanaswa katika utando wa buibui mkuu wa Shetani; kama Hawa alivyofanya tangu mwanzo. Alishindwa kulitumia Neno. Adamu alishindwa katika kutolitii Neno moja kwa moja. Lakini Yesu, katika Maisha Yake binafsi, akishindana na nafsi yake, alishinda kwa utii kwa Neno la Mungu.

Alisema kama tunataka kuketi katika kiti Chake cha enzi, lazima tuwe Neno lililo hai. Maombi yetu, kufunga kwetu, au hata toba zetu hazitatupa majaliwa hayo. Bibi-arusi NENO tu ndiye atakayejaliwa.

Kunayo mengi ningependa kusema, na nukuu nyingi ningependa kuzishiriki na kila mmoja wenu; hayaishi. Ninajua Ujumbe Huu unawaka katika kila mojawapo wa mioyo yenu na mnapenda kila Neno, jinsi tu nami ninavyolipenda. Yote Tunayotaka kufanya ni kuzungumza na kulishiriki. Tunataka ulimwengu ujue: Ndiyo, sisi ni watu wa kanda. Ndiyo, sisi tunabonyeza Play . Ndiyo, sisi tunaamini ile Sauti iliyo kwenye kanda hizi ndio itakayomkamilisha Bibi-arusi. Ndiyo, kanda ndizo zitakazomuunganisha Bibi-arusi. Ndiyo, Kubonyeza Play ndio Mapenzi Makamilifu ya Mungu. Ndiyo, mimi ndiye Bibi-arusi Wake.

Ninajua mimi ninarudia Kwa barua nyingi, lakini nina furaha sana, ninashukuru kweli, ni hakika … ni jambo lisilo na shaka, huu ndio Mpango wa Mungu kwa Bibi-arusi Wake.

Kwa kila Ujumbe tunaousikia, tunashangaa kwa mshangao, Wao Wanakosaje kuona, kusoma au kusikia yale tunayosikia? Liko papo hapo, kwenye kanda, kanda baada ya kanda, baada ya kanda. Inanifanya nijisikie kuwaambia wao kama vile Yesu alivyomwambia Nikodemo: “Je! wewe u mwalimu wa Israeli, na mambo haya huyafahamu?”

Hebu Sikiliza jinsi gani malaika huyu anavyolifanya rahisi.

Juu ya msingi wa tabia za wanadamu peke yake, mtu ye yote anajua ya kwamba palipo na watu wengi kuna hata na maoni yasiyopatana juu ya mambo madogo-madogo ya fundisho muhimu ambalo wote wanashikilia pamoja.

Juu ya msingi wa tabia za wanadamu PEKE YAKE, hakuna ufahamu wa kiroho unaohitajika, mtu ye yote anajua watu wawili watakuwa na maoni yasiyopatana juu ya MAMBO MADOGO- MADOGO ya fundisho muhimu.

Wote wanaweza kukubaliana na kusema kama watu hawafanyi wanalosema wao, ama wakiondoka, basi maangamizi yatafuata. Lakini nabii wa kweli daima atamwongoza mtu kwenye Neno na kuwafunga watu kwa Yesu Kristo naye hatawaambia watu wamwogope yeye ama yale anayosema, Lakini waogope yale Neno lisemayo.

Neno linasemaje? Nitawapelekea Eliya nabii. Katika siku za SAUTI. Kutakuwa na nabii wa Neno MMOJA…MMOJA tu…kwa kuwa Mungu ameukabidhi Ufunuo kwa HUYO MMOJA PEKE YAKE. Yeye ndiye atakayemrudisha Bibi-arusi Wangu.

Jinsi kulivyo na sauti nyingi hivi na maoni mengi na nukuu nyingi, mtu anawezaje kuwa na HAKIKA?

Ni nani basi atakayekuwa na mamlaka ya kutokosea ambayo itarudishwa katika wakati huu wa mwisho, kwa kuwa wakati huu wa mwisho utarudi kwenye kumdhihirisha Bibi-arusi wa Neno Halisi?

Huyo ndiye ambaye Bibi-arusi anataka kumsikiliza, huyo aliye na mamlaka ya kutokosea; kwa maana Yeye atakuwa ndiye wa KUMRUDISHA Bibi-arusi. Yeye Hatakuwa na maoni yasiyopatana, Yeye ni Neno.

Swali: Bwana, tunataka kujua, ni nani mtu huyo atakayekuwa na Maneno ya kutokosea?

Nitakwambia ni nani atakayekuwa nalo. Itakuwa ni nabii aliyethibitishwa kinaganaga, ama hata aliyethibitishwa kinaganaga zaidi kuliko nabii ye yote katika nyakati zote tangu Henoko hata siku hii, kwa sababu mtu huyu itambidi kuwa na huduma ya jiwe la kifuniko , na Mungu atamtambulisha. Haitambidi kujitetea , Mungu atamtetea kwa sauti ya ishara. Amina.

Jibu: William Marrion Branham.

Hebu nikutie moyo leo Ewe Bibi-arusi Mteule. HUWEZI, NA HAUTA, PUMBAZWA. Je, ulilipata jambo hilo? Hakuna mtu anayeweza kukupumbaza. Paulo hangeweza kumpumbaza mteule ye yote, kama angalikuwa amekosea. Hata katika wakati ule wa kanisa la kwanza la Efeso, wateule hawakuweza kupumbazwa. Waliwajaribu mitume wa uongo na manabii wa uongo na kuwaona kuwa ni waongo na Wakawaondosha.

UTUKUFU EWE BIBI-ARUSI …. Wewe ni Kondoo WAKE nawe unaisikia Sauti yake na kumfuata YEYE. WEWE NI BIBI-ARUSI-NENO LILILO HAI!!

Hakuna kitu kilicho kikuu zaidi kuliko kujua Maneno haya. Kujua ndani ya moyo wako na nafsini mwako, kuwa wewe ni Bibi-arusi Wake. Siku zile ambazo ulimwengu ulikuwa ukingoja zimefika. Bibi-arusi anajitambua naye anafanyika MMOJA NA YEYE; sisi ni UUMBAJI MPYA WA MUNGU.

Kwa mara nyingine tena ninawasihi, ISIKILIZENI SAUTI YA MUNGU siku ya Jumapili, popote mkutanikapo. Haijalishi ni Ujumbe gani Mnaousikiliza mradi tu mnasikiliza Sauti ya Mungu iliyothibitishwa. Sauti hiyo ilikuwa ndio Sauti ambayo Mungu aliyoiita na kuichagua kumrudisha na kumkusanya Bibi-arusi Wake.

Kwa makanisa yote, watu wote, mnaalikwa kusikiliza pamoja nasi Jumapili hii saa 06:00 SITA MCHANA.,masaa ya Jeffersonville,( ni saa 1:00 MOJA JIONI ya Afrika Mashariki) tunaposikia:  Wakati wa Kanisa la Laodikia 60-1211E.

Ndugu. Joseph Branham

23-0611 Wale Wanawali Kumi, Na Wayahudi Mia Na Arobaini Na Nne Elfu

UJUMBE: 60-1211M Wale Wanawali Kumi, Na Wayahudi Mia Na Arobaini Na Nne Elfu

PDF

BranhamTabernacle.org

Wapendwa, Wapendao Mana,

Tuna furaha kwa sababu kwamba tunaweza kula Chakula kisicho na mfupa wala mbegu ndani yake. Mikate myembamba ilishuka kutoka Mbinguni, iitwayo “Mana,” inafunika kila mahali kwa utamu wa Mbinguni.

Kwa Ufunuo wa Kiroho, Yeye ametufunulia kuna mahali pamoja tu tunaweza kupata hii Mana Safi isiyo na mbegu: kwa kuisikia Sauti ya Mungu aliyoiandaa kwa ajili ya Bibi-arusi Wake.

Ni ombi lake la daima katika kila wakati kwamba makanisa waisikie Sauti ya Bwana. Katika Wakati huu wa mwisho, ombi Lake ni la nguvu zaidi kuliko wakati mwingine wo wote ; kwa maana hii ndio siku ya Kuja kwa Bwana. Ametuonya, kwa dharura yote, kwamba hatuna budi kuisikia Sauti Yake ya kweli, iliyothibitishwa.

Loo! kuna sauti nyingi sana ulimwenguni—shida nyingi sana na mahitaji yanapaza sauti yapate kushughulikiwa; lakini kamwe hakutakuweko na sauti iliyo muhimu sana na inayostahili kushughulikiwa kama sauti ya Roho. Kwa hiyo, “Yeye aliye na sikio la kusikia, na alisikie Neno hili ambalo Roho ayaambia makanisa.”

Hilo hapo, onyo lake kwa makanisa, jinsi gani ilivyo muhimu kusikia SAUTI ya Roho. Hakika hapo ndipo adui atakaposhambulia, akijaribu kuondoa kwa watu umuhimu wa kuisikia SAUTI HIYO.

Yeye anatuambia kuna SAUTI NYINGI. Kuna shida nyingi sana na mahitaji, yanapaza sauti yapate kushughulikiwa, lakini usisahau kamwe, lazima usikie SAUTI YAKE ILIYOTHIBITISHWA.

Ikiwa niliwahudhi kwa kusema hivyo, nisameheni, lakini, nilihisi yaweza kuwa huko ni kuchukizwa, lakini, mimi ni Sauti ya Mungu kwenu.

Hilo hapo jibu: MIMI NI SAUTI YA MUNGU KWENU.

Ni wazi sana kwa Bibi-arusi Wake. Halijafichwa, Liko papo hapo wazi kabisa; mtu yeyote anaweza kulisoma. Mimi Siwaambii watu jambo ambalo Yeye Hakusema… mimi silibuni jambo hili. Yeye anatuambia waziwazi ni jambo gani lililo muhimu zaidi tunalopaswa kufanya. Mapenzi makamilifu ya Mungu ni KUSIKIA SAUTI YAKE NA YEYE NDIYE SAUTI YA MUNGU KWETU.

Ndugu na dada, sisemi kuwa hamwezi kuwasikia wachungaji wenu. Sisemi kwamba ni wa uwongo ama ni makosa ikiwa watahudumu. Ni wazi Bwana ametuweka hapa ili tuwe msaada kwa Bibi-arusi na kuwaelekeza ninyi KURUDI kwenye Neno la asili; kuiweka Sauti hiyo mbele zenu kuwa iliyo muhimu zaidi mnayopaswa kuisikia. Tunatakiwa kurudi kwenye MAPENZI MAKAMILIFU YA MUNGU. Yule Adamu aliyerejeshwa kikamilifu, akilindwa na Neno. Mungu alinena kila siku na Adamu mdomo kwa sikio katika ile Bustani, na leo hii, Yeye Anafanya jambo lile lile.

Tunapaswa kuwa tukisimama katika pengo na kusema, “Sisi ni ndugu!” Hatujagawanyika, Sisi sote ni mwili mmoja; Mmoja katika tumaini na fundisho, (Fundisho la Biblia.)

Sisi ni ndugu. Mimi Sijaribu kuyagawanya Makanisa, ninajaribu kutuleta pamoja kwa jambo PEKEE linaloweza kumleta Bibi-arusi pamoja. Hatuwezi sote kukubaliana na MTU YOYOTE, AMA KUNDI LA WAHUDUMU; wote wametofautiana, na wanasema mambo yaliotofautiana. Kuna malaika-mjumbe wa saba MMOJA tu . Kuna Sauti ya Mungu MOJA tu . Sauti ambayo Mungu ameiandaa kwa ajili ya Bibi-arusi Wake kwenye kanda.

Nitakuwa wazi. Ufunuo wangu ni: Kusikiliza Sauti ya Mungu kwenye kanda NDIO MAPENZI MAKAMILIFU YA MUNGU.

Kama katika siku za Samweli, wakati watu walipomwendea na kumwambia walitaka mfalme wakuwatawala. Ilihuzunisha moyo wake. Alimwendea Mungu na kumwambia kile walichotaka. Mungu alimwambia Samweli, hawakukukataa wewe, Samweli, wamenikataa Mimi, ili Nisiwe mfalme juu yao .

Je, Yeye alikuwa akiwatawala namna gani? KWA NABII WAKE, SAMWELI. Hayo yalikuwa ndio MAPENZI YAKE MAKAMILIFU, nao wakamkataa. Ili uwe Bibi-arusi Wake ni lazima Urudi kwenye Mapenzi Makamilifu ya Mungu. Huwezi kuwa na MAPENZI MAKAMILIFU 2.

Jinsi gani ningependa Bibi-arusi wote wakusanyike pamoja kutoka ulimwenguni kote ili kusikia Sauti ya Mungu wote kwa wakati mmoja. Si kwa sababu “Mimi” nasema hilo, bali kwa sababu Mungu ANAFANYA HIVYO. Ndilo jambo pekee la kumkusanya Bibi-arusi Wake pamoja.

Ninakualika uje kusikiliza pamoja na sehemu ya Bibi-arusi, Jumapili saa 06:00 SITA MCHANA, saa za Jeffersonville( Ni saa 1:00 MOJA JIONI ya Afrika Mashariki), kusikia: Wale Wanawali Kumi, Na Wayahudi Mia Na Arobaini na Nne Elfu 60-1211M.

Ikiwa huwezi kuungana nasi, mtie moyo mchungaji wako msikilize Sauti ya Mungu Jumapili hii asubuhi kanisani mwenu. Je! Waweza kuwazia, Bibi-arusi kote ulimwenguni, katika kila kanisa, kila nyumba, ama popote ulipo, wakisikia Mana Mpya ikifunika kila mahali kwa utamu wa Mbinguni.

Ndugu. Joseph Branham

23-0604 Wakati Wa Kanisa La Filadelfia

UJUMBE: 60-1210 Wakati Wa Kanisa La Filadelfia

PDF

BranhamTabernacle.org

Mpendwa Bibi Yesu Kristo,

Je! hilo halisikiki lakupendeza? Mwana-Kondoo na Bibi-arusi Wake wametulia milele katika ukamilifu wote wa Mungu. Ati tutoe sifa ya jambo hilo? Tunalifikiri. Tunaliota. Tunasoma kile Neno lisemacho kulihusu. Tunamwona Yeye akishiriki Utakatifu Wake NASI. Ndani yake, tumekuwa haki halisi ya Mungu.

Inatuletea furaha jinsi gani wakati tunapobonyeza Play, na kumsikia Mungu Mwenyewe akizungumza nasi kupitia malaika Wake mwenye nguvu na kutuambia mambo haya.

Hakuna kitu cho chote katika maisha haya, hata kiridhishe namna gani, kiwe kizuri na chema vipi, ila utapata jumla ya ukamilifu wote katika Kristo. Kila kitu hufifia kabisa mbele Zake.

Yeye anatuambia tutakuwa na jina jipya, Jina Lake. tutapewa jina lake wakati atakapotupeleka kwake. Itakuwa lakupendeza sana kuliko tunavyoweza kuwazia. Tutaenda popote Bwana-arusi alipo. Hatutaachwa Naye kamwe. Hatutaondoka Ubavuni mwake. Tutashiriki kiti cha enzi pamoja naye. Tutatiwa taji kwa utukufu na sifa zake.

Na wakati anapojithibitisha Mwenyewe kwa ulimwengu, na ulimwengu wote unasujudu miguuni Pake, wakati huo ulimwengu wote utasujudu miguuni pa watakatifu, ikithibitisha ya kwamba walikuwa sahihi katika msimamo wao pamoja Naye. Mungu na abarikiwe milele!

Yeye alitujua tangu zamani kwa uamuzi wa Kiungu ya kwamba tungekuwa Bibi-arusi Wake. Yeye Alituchagua SISI; hatukumchagua Yeye. Yeye ndiye Aliyetuita SISI ; hatukuja kwa hiari yetu. Yeye Alitufia SISI. Alitusafisha katika Damu Yake Mwenyewe. Yeye Alitununua SISI . Sisi ni mali yake, na wake peke yake. Tumejitoa Kwake kabisa naye Anakubali jukumu hilo. Yeye ni kichwa CHETU. Yeye Ananena nasi kupitia malaika wake nasi tunatii, kwani hiyo ndiyo furaha yetu.

Tangu mwanzo hata mwisho, Ujumbe ulio kwenye kanda yote ni MUNGU kwetu SISI. Hebu hayo Maisha na yawe ndani YETU. Hebu na iwe ni Damu yake inayotuosha SISI. Hebu iwe ni Roho Wake anayetujaza SISI. Hebu na liwe ni Neno lake ndani ya moyo na mdomo WETU. Na yawe ni Mapigo Yake yanayotuponya SISI. Na iwe ni Yesu, na Yesu peke yake. Si kwa matendo ya haki, ambayo tumefanya. Kristo ndiye uzima wangu. Ujumbe huu ni uzima wetu, kwa maana ni Kristo.

Loo! kuna sauti nyingi sana ulimwenguni—shida nyingi sana na mahitaji yanapaza sauti yapate kushughulikiwa; lakini kamwe hakutakuweko na sauti iliyo muhimu sana na inayostahili kushughulikiwa kama sauti ya Roho. Kwa hiyo, “Yeye aliye na sikio la kusikia, na alisikie Neno hili ambalo Roho ayaambia makanisa.”

Mungu anayo Sauti kwa ajili ya siku hii. Imethibitishwa na Nguzo ya Moto kuwa ni Sauti ya Mungu. Kamwe hakutakuwa na Sauti ILIYO MUHIMU SANA NA YENYE THAMANI SANA KUSHUGHULIKIWA kama ile Sauti iliyo kwenye kanda kwa ajili ya siku ya leo.

Njoo uungane nasi Jumapili saa 06:00 SITA MCHANA, saa za Jeffersonville. ( Ni saa 1:00 MOJA JIONI ya Afrika Mashariki )Tuna mfuko mzima wa maandiko uliyojaa Asali. Tutaiweka kwenye Mwamba, si juu ya kanisa lolote; juu ya Mwamba, Kristo Yesu. Basi ninyi kondoo anzeni kuiramba. Hakika mtapata afya mara moja. Shida zote za dhambi zitakwisha utakapouramba Mwamba. Hivyo tu ndivyo unavyopaswa kufanya, njoo uisikie Sauti ya Mungu ikituambia yote kuuhusu: Wakati wa Kanisa la Filadelfia 60-1210.

Ndugu. Joseph Branham

23-0528 Wakati Wa Kanisa La Sardi

UJUMBE: 60-1209 Wakati Wa Kanisa La Sardi

PDF

BranhamTabernacle.org

Wapendwa Wanaostahili, Wenye Haki,

Enyi Tai, mko tayari kukusanyika pamoja Jumapili hii kusikia Sauti tamu ya Yesu ikinena nanyi na kusema:

“ninyi Mnastahili.” “Ninyi ni wangu.” “Ninyi ni wenye Haki.” “Mtatembea pamoja nami katika mavazi meupe.” “Majina yenu yameandikwa Mbinguni.”

Haya si maneno yangu, bali ni Maneno hasa ya Baba yetu wa Mbinguni akinena na WEWE, Bibi-arusi Wake mteule. Roho Mtakatifu amekuja tena na kuishi katika mwili wa mwanadamu, ili aweze kunena mdomo kwa sikio na Bibi mteule wake Maneno haya ya ajabu.

Inapendeza kuyasikia kutoka kwangu, au mtu ye yote ambaye angesema “Yesu alisema”, lakini kumsikia YEYE akisema kupitia Sauti yake teule; ile
aliyozoea kukuambia, kibinafsi… hakuna kabisa kilicho kikuu zaidi.

Kuna sauti nyingi ambazo Mungu hutumia kuleta Neno lake ulimwenguni. Amewachagua na kuwaweka wawe baraka kwa ulimwengu na kwa Bibi-arusi Wake.

Yesu alipokuwa hapa duniani katika mwili wa mwanadamu, Alikuwa pia amewachagua watu, mitume Wake, wamfuate Yeye na kusema kwa niaba Yake yale walioona kuzidiwa na waliosikia. Watu hawa ndio aliowatuma kuieneza Injili, habari njema kwamba Masihi amekuja; Alikuwapo, duniani pamoja nao. Aliwatuma wawili wawili kutangaza Habari Njema hii na kuwaleta watu wote kwake yeye.

Alipokuwa amewakusanya pamoja usiku mmoja, aliwauliza, “Watu huninena mimi kuwa ni nani?” Wakamjibu, “Wengine husema Wewe ni Eliya; wengine husema Wewe ni Yohana Mbatizaji.” Lakini yeye akasema, “Lakini NINYI MNASEMA Mimi kuwa ni nani?” Ndipo Petro akanena maneno hayo makuu, “Wewe ndiwe Kristo, Mwana wa Mungu aliye hai.” Yesu akamjibu, akasema, Mwili na damu havikukufunulia hili, Petro, bali Baba yangu aliye mbinguni amekufunulia hili, na juu ya mwamba huu(Ufunuo) nitalijenga kanisa langu.”

Ulimwengu umejikwaa pande zote kwenye siri hii kuu. Watu wengine wanaamini alikuwa akimaanisha Petro. Wengine wanaamini kuwa ni mwamba uliokuwa umelala pale. Wengine wanaamini ilikuwa ni Yesu. Lakini kwa Ufunuo, tuliopewa na Roho Mtakatifu, tunajua ulikuwa ni UFUNUO WA YEYE ALIKUWA NANI.

Baada ya kifo cha Yesu, kuzikwa na kufufuka, siku ya Pentekoste, walitumwa kuuambia ulimwengu Habari hii Kuu. Petro alichaguliwa tena kuwa msemaji na kwenda mbele ya watu na kutangaza jinsi ya kupokea Roho wake Mtakatifu. Alisema, hamna budi kutubu na kubatizwa katika Jina la Bwana Yesu Kristo.

Ni nafasi iliyoje ambayo Roho Mtakatifu alikuwa ameweka juu ya Petro. Tunaweza tu kuwazia jinsi watu walivyomtazama. Yeye alitembea pamoja na Yesu alipokuwa hapa duniani katika mwili. Yeye alikuwa rafiki Yake. Alikuwa kando Yake kila siku. Yule ambaye alikuwa amemchagua kumpa ule Ufunuo. Lakini Mungu alikuwa amemchagua MTU MWINGINE kuwa nabii Wake: Paulo.

Wakati Petro alipofika Antiokia kuwa pamoja na Paulo, alikuwa akila na kunywa pamoja na watu wa mataifa. Lakini kundi la watu lilipokuja kutoka kwa Yakobo, alijitenga na kuogopa. Paulo alimkemea waziwazi mbele ya wale wengine na kusema haenendi sawa sawa na ile kweli naye alistahili hukumu. Ndugu Branham alisema Petro alizidiwa na wale wa Dini ya Kiyahudi.

Je, jambo hili linatuambia nini kwa ajili ya siku hii? Haijalishi ni nani. Kiasi gani walivyo na Roho Mtakatifu. Wana mamlaka gani ama wito gani. NI LAZIMA UKAE NA NABII MTEULE WA MUNGU KUWA YAKINI YAKO. KWA MAANA YEYE, NA YEYE PEKE YAKE, NDIYE MFASIRI WA KIUNGU WA NENO LA MUNGU.

Hili si kinyume na Petro au mwanafunzi yeyote aliyechaguliwa na Mungu, wakati huo ama sasa. Wamechaguliwa kueneza Injili, lakini Mungu alikuwa amemchagua MTU MMOJA juu ya Kanisa Lake. Yeye peke yake ndiye aliyekuwa nabii aliyechaguliwa na Mungu akiwa na Bwana Asema hivi, si wao. Wana mahali pao, lakini Yeye ana NABII MMOJA wa kuliweka Kanisa Lake katika utaratibu, akiwa na Neno la mwisho kwa ajili Bibi-arusi Wake.

Hili linatuonyesha jinsi gani tunavyopaswa kuwa waangalifu kuisikia Sauti ya Mungu iliyothibitishwa kwa ajili ya wakati wetu. YULE Aliyemchagua kuwa mfasiri wa kiungu wa Neno Lake. HAKUNA KITU KIKUBWA kuliko kuisikia Sauti yake ikinena kupitia malaika Wake; Sauti ya chaguo Lake , si letu.

Tunaona katika nyakati zote jinsi Mungu alivyo na kundi teule la watu ambao wangekaa NA NENO LAKE na mjumbe Wake mteule. Sauti hiyo inatutangazia sisi kila siku sisi ni nani, MMOJA WAO.

Yeye angetuma watengenezaji kwenye kanisa Lake, lakini LEO HII, Yeye alimtuma mrejeshaji Wake; “Nitarejesha, asema Bwana, nami nitaigeuza mioyo ya watoto, kwa kuwa ninayo mengi ya kuwaambia katika siku za Sauti Yangu.”

Umealikwa kuja kuisikiliza hiyo Sauti, Jumapili saa 6:00 SITA MCHANA, saa za Jeffersonville, ( ni saa 1:00 MOJA JIONI ya Afrika Mashariki ) anapozungumza nasi na kutuonyesha Lile Kanisa la Kweli na la uwongo Katika kipindi cha: Wakati wa Kanisa la Sardi 60-1209.

Ndugu. Joseph Branham

23-0521 Wakati Wa Kanisa La Thiatira

UJUMBE: 60-1208 Wakati Wa Kanisa La Thiatira

PDF

BranhamTabernacle.org

Wapendwa Nyota Katika Taji Yake,

Furahi Bibi-arusi. Tunakuwa mmoja na Yeye. Kila siku, Anatupa Ufunuo zaidi wa yeye Mwenyewe na wetu sisi. Tunazidi kufahamu zaidi ile Nguvu ya Kuhuisha inayoishi na kukaa ndani yetu.

Hatuwezi hata kueleza jinsi tunavyojisikia. Tumemezwa na Roho wake. Ndio yote tuwazayo. Hakuna kitu kingine muhimu kwetu. Tunaona Neno Lake likifanyika Neno ndani yetu. Linalisha nafsi zetu. Tunaishi kila siku kumwabudu yeye, kumsifu, na kumshukuru kwamba tunaweza kusikia Sauti yake ikinena nasi.

Tunaposoma Kitabu chetu cha nyakati za Kanisa, ni vigumu kwetu kukiweka chini; mioyo yetu inalipuka. Kila siku huleta Ufunuo zaidi. Tunataka kuruka juu na kupaza sauti, kukimbia huku na huku chumbani na kupiga kelele: “Utukufu, Haleluya, Bwana apewe sifa.” “je, umelisoma hili?” “Nimeliwekea alama kwenye marejeo yangu pendwa, lakini sijawahi, KAMWE, kulisoma kama hivi hapo awali.” Yeye anatufunulia Biblia nzima kutoka Mwanzo hadi Ufunuo, nami najiona SISI WENYEWE KATIKA NENO LAKE.

Tunamwona Bibi-arusi huyo wa Kweli ambaye aliyedumu na Neno katika nyakati zote na hakudanganywa na udanganyifu mkuu wa Shetani. Alitaka kuabudiwa kama Mungu. Lakini wakati wote kulikuwa na yule BIBI-ARUSI WA KWELI, akidumu mwaminifu kwa Neno Lake. Hilo kundi dogo teule lililokaa na mjumbe Wake. Kama sisi tu, hawakuweza, na wasingeweza, kupatana. Walijua kulikuwa na NJIA MOJA PEKEE ya kuwa na hakika: kudumu na Njia Yake aliyoiandaa, Neno Lake, malaika Wake.

Jinsi gani Shetani amekuwa akidanganya wakati wote. Amefanya kazi katika Nyakati mbalimbali za Kanisa mpaka ametimiza malengo yake. Yeye Sasa amefanana sana na YULE ALIYE MKAMILIFU ili aweze kuwapoteza walio wateule kama yamkini….lakini Mungu apewe sifa, HAIWEZEKANI, HATUDANGANYIKI. Kwa nini? TULIKAA NA SAUTI YA MUNGU, NENO LAKE LILILOFANYIKA MWILI.

Hakuna njia ya mkato. Sauti ya Mungu ndiyo Njia Yake aliyoiandaa kwa ajili ya wakati huu. Tumeendelea kufanya kazi zake kwa uaminifu hadi mwisho. Tumepewa mamlaka juu ya mataifa, na ni watawala wenye nguvu, wenye uwezo, wasiokunjika ambao wanaoweza kukabiliana na hali yoyote kwa nguvu sana. Hata adui yetu aliyedhikika sana amevunjika. Udhihirisho wetu wa utawala, kwa Nguvu zake, ni kama ule wa Mwana.

Loo, jinsi tulivyotamani tungeweza kueleza kwa maneno jinsi tunavyojisikia. Siku moja tutafanya hivyo enyi marafiki. Tutaishi Milele na Bwana wetu, Malaika Wake, na sisi kwa sisi.

Kama yule bibi mzee mweusi huko Memphis, nasi tulijua alikuwa ndiye tulipomsikia. Kwa nini? Loo, sisi ni MMOJA WAO.

Je, ungependa Roho Mtakatifu azungumze nawe na kukuambia wewe ni nani? Njoo ujionee uwepo wa Bwana pamoja nasi Jumapili hii saa 06:00 SITA MCHANA, saa za Jeffersonville,( ni saa MOJA JIONI ya Afrika Mashariki ) tunaposikia: Wakati wa Kanisa la Thiatira 60-1208 . Itabadilisha maisha yako.

Ndugu. Joseph Branham