22-0206 Muhuri Wa Pili

Ujume: 63-0319 Muhuri Wa Pili

PDF

BranhamTabernacle.org

Mpendwa Tawi Jipya,

Kimetendeka; kile ambacho watakatifu wote walio tutangulia wamekuwa wakingojea. Ule Mti wa Asili sasa umetoa tawi jipya. Tumewasili. Sisi ndilo hilo Tawi Jipya. Roho Mtakatifu ameshuka, na Roho wa Mungu yuko juu yetu. Ile Imani ya Asili, ya Kipentekoste, ya kimitume imerejeshwa na malaika Wake wa 7. Sasa, nabii Wake anaenda nyumba kwa nyumba, akimega mkate pamoja nasi. Kuna ishara kuu, maajabu, na Ufunuo juu ya Ufunuo unaomwagwa juu yetu.

Tunaziweka taa zetu zikiwa zimetengenezwa na zimejaa Mafuta. Tunadumu na Neno la Asili, kama alivyotuambia tufanye. Wengine wanaweza kutaka Kanisa, lakini sisi HATUTAKI LOLOTE ILA SAUTI YA MUNGU YA ASILI.

Sasa, hebu wazia tu jambo hilo sasa. Hebu tuninii tu—tujaribu kuyaingiza yale tunayoamini kwamba Roho Mtakatifu angetutaka tujue .
Sasa kumbukeni , “ Hakuna lo lote linaloweza kufunuliwa; Mungu hatafanya neno lo lote, hata kidogo, mpaka kwanza alifunue kwa watumishi Wake, manabii.” Na kabla ya Yeye hajafanya neno lo lote, hulifunua .

Hakuna kinachoweza kufunuliwa kwa Bibi-arusi; ikiwa si na nabii Wake kwanza. Kama kuna siri zozote zitakazofunuliwa, ufunuo wowote mpya, cho chote tunachohitaji ili kuwa Bibi-arusi Wake na kunyakuliwa, Ni lazima kwanza umjie nabii ndipo YEYE atatufunulia jambo Hilo, Bibi-arusi Wake.

Kufunua nini? Siri ya Ngurumo Saba. Hilo lina maanisha nini? Inamaanisha moja ya mambo mawili. Labda tayari ipo kwenye kanda na itafunuliwa ufikapo wakati wake kufunuliwa kwetu.

Lakini nawazia, wakati siri hizo zinapoanza kufunuliwa, Mungu alisema, “Zifiche sasa. Ngoja kidogo. Nitazifunua katika siku hiyo. Usiziandike, hata kidogo, Yohana, maana zitawakwaza. Zi—ziache tu, unaona. Lakini nitazifunua katika siku ile ambayo kuna haja ya kuzijua .”

Ama, atamtuma nabii Wake kurudi duniani ili kututambulisha Kwake, ndipo nabii Wake atatufunulia siri ya zile Ngurumo Saba.

Na ndipo kunakuja Ngurumo saba za siri ambazo hata hazijaandikwa kamwe. Hiyo ni kweli. Nami naamini ya kwamba, kupitia Ngurumo hizo Saba, zitafunuliwa katika siku za mwisho ili kumkusanya Bibi-arusi pamoja kwa ajili ya kupata imani ya kunyakuliwa. Kwa sababu, ile tuliyo nayo sasa hivi, ha—hatungeweza kufanya jambo hilo. Kuna jambo fulani. Hatuna budi kupiga hatua mbele zaidi.

Haitakuwa ni kundi la watu ambao watakaofunua siri hiyo, Itakuwa ni Malaika-mjumbe Wake wa 7, William Marrion Branham. Hiyo si kwa sababu “MIMI ” nilisema hivyo; ni kwa sababu NENO LINASEMA HIVYO!!

“ Anachukua kile Kitabu na, cha Mihuri, na kuzivunja,” na kumwonyesha malaika wa saba ; kwa kuwa hii pekee, siri za Mungu, ndiyo huduma ya yule malaika wa saba .

Inasema yote hapo. Huduma ya Siri za Mungu si ya mwingine ila malaika wa saba. Zile Ngurumo Saba zitamkusanya Bibi-arusi pamoja na kutupa imani ya kunyakuliwa.
Ikiwa Ngurumo ndizo zitamkusanya Bibi-arusi pamoja, na siri ya Ngurumo haina budi kutoka kwa malaika wa 7, basi hakuna jambo la muhimu zaidi kwa Bibi-arusi kufanya kuliko KUBONYEZA PLAY . Hilo ndilo litakalomkusanya Bibi-arusi pamoja kwa ajili ya Unyakuo.

Dumu na Neno la Asili kwenye kanda. BONYEZA PLAY .

Na kanda zitafunua mengi Yake, wakati unajifunza .

Jina la Bwana libarikiwe! Utukufu kwa Mungu! Tunaipenda hisi hiyo tamu tunayopata kutokana na kusikia Sauti ya Mungu ikizungumza nasi kwenye kanda. Tunamsikia tu Roho Mtakatifu akifurika pande zote kutuzunguka tunapotembea Nayo. Tunaenda nayo nyumbani. Tunaishikilia kwenye mto wetu.

Njoo usikilize pamoja nasi Jumapili saa 6:00 Sita Mchana , saa za Jeffersonville, ( ni Saa 2:00 mbili Usiku ya Tanzania), Roho Mtakatifu anapokuja kwa uvumi majumbani mwetu na kutufunulia yote tunayohitaji, tunaposikia: Muhuri wa Pili 63-0319.

Ndugu. Joseph Branham

Maandiko ya kusoma kabla ya kusikiliza Ujumbe:

Mathayo Mtakatifu 4:8 / 11:25-26 / 24:6

Marko Mtakatifu 16:16

Yohana Mtakatifu 14:12

2 Wathesalonike 2:3

Waebrania 4:12

Ufunuo 2:6 / 6:3-4 / Sura ya 17 yote nzima / 19:11-16

Yoeli 2:25

Amosi 3:6-7