22-0213 Muhuri Wa Tatu

Ujume:: 63-0320 Muhuri Wa Tatu

PDF

BranhamTabernacle.org

Mpendwa Bibi-arusi Bikira,

 Nimekuwa nikiomba na kumuuliza Bwana kile ambacho angenitaka niandike na kusema ambacho kingeweza kuwa baraka na faraja kwako, Bibi-arusi Wake.  Sina maneno, na sijui niseme nini.  Ninajiona sistahili hata kuandika maneno machache niandikayo, lakini ni heshima kuu sana  ya maishani mwangu kufanya chochote kwa ajili Yake.

 Ninaamini wakati wa kusikia Mihuri hii Saba ni mkamilifu sana.  Tunaweza kuona mpango mkuu wa Mungu ukifunuliwa na kuwekwa wazi mbele zetu.  Ujumbe baada ya Ujumbe unakuwa Ufunuo mkuu zaidi baada ya Ufunuo.  Tunamwona yeye akijifunua mwenyewe kwetu na kutuongoza.  Tunajua tunafanya yale hasa yeye aliyotuambia tufanye, “kudumu na Neno.”  Hakuna njia kuu zaidi ya kufanya hivyo kuliko Kubonyeza Play .

 Ninahisi wito alioweka moyoni mwangu ni kudumisha Ujumbe huu, sauti Yake, kanda hizi mbele yenu daima;  ili kukueleza umuhimu wa kuzisikiliza kanda.  Najua siwezi kulifikisha ipasavyo, lakini NAJUA niko sahihi kuwaambia “Bonyeza Play,” kwani si fikira zangu, wazo langu, wala maneno yangu, bali ni Maneno ya Mungu Mwenyewe anenayo kupitia malaika-mjumbe Wake wa 7, akituambia :

  Wakati mwingine wakati tunaposoma tu, na, sasa, iweni waangalifu sana. Na wakati unaposoma, chukueni kanda, zisikilizeni kwa makini sana. Kwa sababu, utalipata kwenye kanda, kwa sababu wamekuwa wakizicheza kanda hizo, na ni nzuri zinasikika vizuri . Kwa hiyo, mtalisikia vizuri zaidi humo .

 Kama nilivyosema mara nyingi sana hapo awali, sipingi huduma au chochote ambacho Mungu ameweka katika kanisa Lake.  Hiyo ingekuwa ni kwenda kinyume na Neno la Mungu.  Ninaamini wametiwa mafuta na wameitwa na Mungu.  Lakini ninaamini ya kwamba kusikiliza na kuweka Sauti yenyewe hasa ya Mungu mbele ya watu halina budi kuwa jambo la muhimu sana mtu yeyote aliyeitwa na Mungu angeweza kufanya.

 Haitoshi kusema tu, “Ninawaambia kusanyiko langu kuzicheza kanda.”  Ikiwa unaamini:

 . Hakuna upako mkuu kuliko kusikia Sauti ya Mungu kwenye kanda.

 . Ufunuo wote lazima utoke kwenye Sauti hiyo.

 . Imani ya Kunyakuliwa tunayohitaji itakuja kutoka kwenye kile isemacho Sauti hiyo.

 Mhudumu yeyote anawezaje kutotaka kuisikiliza Sauti hiyo, pamoja na kanisa lao, na kusema AMINA KWA KILA NENO?

 Kila mmoja lazima wawe na Kitu fulani wanachohisi na kuamini kuwa ni jambo la MUHIMU ZAIDI wanaloweza kufanya ili kuwa Bibi-arusi wa Kristo.  Kitu fulani lazima Kiwe cha MUHIMU SANA  cha Mungu na  Mapenzi yake Makamilifu.  Je, hiyo ni huduma ya mchungaji wako?  Ni Kusikiliza  wahudumu wengine?  Si kusema hilo ni kosa, la hasha, na hilo ni sawa kabisa kulingana na Neno, Lakini je! unaamini jambo la MUHIMU ZAIDI ni kusikiliza Sauti ya Mungu iliyothibitishwa kwenye kanda?

 Ikiwa hilo ndilo unaloamini kuwa ndilo jambo MUHIMU SANA ungeweza kufanya, basi kwa nini huduma haitaki kucheza na kusikiliza huo UJUMBE  MUHIMU SANA NA MKAMILIFU pamoja na makusanyiko yao?

 Jiulize mwenyewe , au muulize mchungaji wako swali hili: Je, unaamini kuwa nukuu hii ni ya kweli, au je, hili ni kosa na ni kutokuelewa kwa Ndugu Branham, au kujaribu kujisifu mwenyewe?

 Unaona, ni vile vile ambavyo ingetukia sasa! Na, kwa kanisa, ni Kitu gani ? Neno lililofanyika mwili likifanywa mwili miongoni mwa watu Wake tena ! Unaona? Nao hawaliamini Hilo kamwe .

 Ikiwa unaamini kuwa nukuu hii ni ya kweli, na kwako wewe ni SAUTI YA MUNGU, Neno lililofanyika mwili, basi ni jinsi gani mtu ye yote asingeweza kuona kwamba HAKUNA KITU CHA MUHIMU zaidi Ya Kuisikia Sauti hiyo .

 Amka ewe bikira aliyelala, je nawe una Ufunuo huu au uko kama alivyosema: ”  Huliamini hilo kamwe . ”

 Kama vile nabii alivyotuambia, sisi ni Kitabu kipya cha Matendo, lile Tawi jipya, Wateule Wake.  Hivyo, wengi wanahisi kwamba Roho Mtakatifu sasa hivi anatuongoza kama watu binafsi au anatuongoza kwa huduma, wala si kwa nabii Wake.

 Kuna ukweli mwingi katika hili, LAKINI nabii alilisahihisha hili pia, na akatufunulia ukweli.

 Mtu fulani alikuwa akizungumza nami hapa si muda mrefu uliopita.  Kasema, “Lakini Ndugu Branham…” [Ndugu Branham anasafisha koo lake—Mh.] Samahani.  Kasema, “baada ya Roho Mtakatifu kuja, hakuna Malaika wanaoliongoza kanisa, ama kuelekeza watu binafsi.  La, bwana.”  Kasema, “Ni Roho Mtakatifu anayetuongoza.”

 Huko ni kutokuelewa kati ya Malaika na Roho Mtakatifu .  HILO NI KOSA, Malaika waliliongoza Kanisa kote kote, na wangali wanaliongoza Kanisa. Sahihi kabisa .

 Malaika wake analiongoza na kulielekeza Kanisa Lake.  Sote tuna nafasi zetu na wito wetu, lakini malaika peke yake ndiye anapaswa kumwongoza Bibi-arusi.

 Sikiliza kile nabii wa Mungu alichosema kuhusu huduma zingine zote ukilinganisha na kile ambacho Mungu ALICHOMWITIA YEYE KUFANYA,

 Ni kama tu mtu ambaye anafanya kazi ya—ya opareta wa simu, yeye si fundi umeme kabisa. Yeye huenda akafanya kazi ndogo ya umeme. Na kama vile, kama mtu ni mlinda nyaya za umeme, vema, bila shaka yeye…Mtu akiwa ni mchimba mashimo ya nguzo za umeme, naye hajafanya kazi yo yote ya ulinzi wa nyaya za umeme, afadhali asizikaribie; lakini huenda akafanya kazi ndogo ya kurekebisha ama jambo fulani lile .

 Lakini wakati lile Jambo halisi litakapofunuliwa katika siku ya mwisho, ya sehemu ya mwisho ya Kanisa, ni wakati Mungu amesema ya kwamba Yeye angetutumia, kulingana na Maandiko. Nasi tumeyachunguza kindani kabisa, ya kwamba Yeye alibashiri ya kwamba Roho ya Eliya ingerudi juu ya mtu fulani .

 Wakati Mtu fulani anapojaribu kubishana nawe na kukuambia, “inahitaji zaidi ya kusikiliza kanda tu.  Ndugu Branham kamwe hakusema kuzicheza kanda kanisani.  Itahitaji huduma kumkamilisha Bibi-arusi;”  ama chochote kile ambacho mtu ye yote anaweza kukuambia, ili kujaribu na kukufanya utilie shaka na ya kwamba kusikiliza Sauti ya Mungu iliyothibitishwa kwenye kanda kanisani mwenu ni makosa…

 Kama tu vile jamaa fulani anavyoanza, kujaribu kubishana nawe ;  ikiwa unajua pa kusimama, Tambua kile anachoamini .

 Kama wanadai kuamini  kuwa , “Ujumbe Huu ni Neno.  William Marrion Branham ni malaika-mjumbe wa Saba wa Mungu.  Ujumbe huu ndio Yakini Yao.  Ujumbe huu ni Mwana wa Adamu akijifunua mwenyewe katika mwili kama alivyoahidi angefanya…”

 Ni kama tu kumchukua sungura na kumwachilia awe huru kwenye zizi, na umeziba kila tundu. Wewe simama tu langoni; lazima arudi. Imekwisha. Unaona? Hana budi kurudi langoni tena, maana hiyo ndiyo njia pekee anayoweza kutokea. Atatokeza kichwa chake apenyeze hapa, na karibu avunje shingo yake; halafu aende kule, mahali kule. Wewe simama tu na umwangalie, naye atarudi moja kwa moja. Unaona? Imekwisha .

 Shikilieni Mafundisho hayo ya Kanda.  Semeni tu kile kanda zinachosema.  Msibadili Neno moja.  Msiongeze kwake, wala kuondoa Neno moja.  Ni Sauti ya Mungu kwenu.  Ni Neno Lililofanyika Mwili.  Ni Maneno yasiyoweza kukosea.  Yeye ni mchungaji wenu.  Malaika wake anawaongoza.  Ni  Bwana Asema Hivi .

 Maadamu uko katika Neno hilo, uko salama .

 Njoo Utengeneze taa yako na kuijaza Mafuta Jumapili hii saa 6:00 Sita Mchana , saa za Jeffersonville, ( ni saa 2:00 mbili Usiku ya Tanzania), wakati malaika mteule wa Mungu anaponguruma na kuuvunja  Muhuri wa Tatu 63-0320 , na kuufunua kwa Bibi-arusi Wake.

 Ndugu.  Joseph Branham.

 Maandiko ya kusoma ili kujitayarisha kusikia mahubiri, “ Muhuri wa Tatu .”

 Maandiko:

 Mathayo Mtakatifu 25:3-4

 Yohana Mtakatifu 1:1, 1:14, 14:12, 17:17

 Matendo Sura ya 2 yote

 I Timotheo 3:16

 Waebrania 4:12, 13:8

 1 Yohana 5:7

 Mambo ya Walawi 8:12

 Yeremia  Sura ya 32 yote

 Yoeli 2:28

 Zekaria 4:12