23-0806 Muhuri Wa Tatu

UJUMBE:63-0320 Muhuri Wa Tatu

PDF

pakua – m4a

pakua – amr

BranhamTabernacle.org

Mpendwa Bibi-arusi mwenye Changamko,

Jitayarisheni, Jumapili hii mtapata Changamko kwa Ufunuo zaidi kuliko ambavyo mmewahi kupata maishani mwenu. Mtakuwa mkilewa tu kwenye Neno. Itakuwa nzuri sana, na kusikika vizuri…na hata dhahiri zaidi kuliko wakati Alipoizungumza. Na kuna njia moja tu ya kulipata, yakubidi Ubonyeze Play!

Chukueni kanda, zisikilizeni kwa makini sana. Kwa sababu,
utalipata kwenye kanda, kwa sababu wamekuwa wakizicheza kanda hizo, na ni nzuri zinasikika vizuri. Kwa hiyo, mtalisikia vizuri zaidi humo.

Malaika-mjumbe wa saba wa Mungu ametoka kusema nini? Yule ambaye Mungu alimchagua kumfunulia siri zote za Biblia; yule aliyemchagua kutoa Ufunuo wa ile Mihuri Saba, zile Ngurumo, na Neno Lake lote. Malaika yule aliyemchagua kumwita Bibi-arusi Wake atoke. Yule aliyemchagua kuwa Sauti Yake katika siku za mwisho.

Hebu tusome tu nukuu hiyo kwa mara nyingine tena ili kuhakikisha kwamba tunaelewa kile alichotoka kusema kwamba tufanye.

“Utalipata kwenye”, WAPI?
“Utalisikia vizuri zaidi”, WAPI?

Nena kuhusu jinsi ilivyo muhimu Kubonyeza Play na kuzisikiliza Kanda. UTUKUFU!! Hili si neno langu, hili ni NENO la MUNGU akimwambia Bibi-arusi Wake, LIPATE HUMO…KWENYE KANDA. Enyi Wahubiri, ondokeni mgongoni kwangu.

Mtu ye yote anayedai kuwa anaamini Ujumbe huu anawezaje kusema kwamba kuzicheza kanda si jambo lililo KUU ZAIDI ambalo Bibi-arusi analotakiwa kufanya? mchungaji anawezaje kuweka huduma yake kuwa juu ya ile ya nabii? Sio tu kuinukuu….Ninafanya hivyo sasa hivi pia, bali kuicheza Sauti hiyo kwa kundi lake ili waweze “KULISIKIA VIZURI ZAIDI HUMO”.

Huduma iliyo kuu zaidi ulimwenguni ni Huduma ya Kanda. Hakuna kitu kilicho kikubwa zaidi kuliko Kubonyeza Play. Kuna Sauti moja tu ambayo imeamriwa na Mungu kuwa Bwana Asema Hivi kwa Bibi-arusi Wake, ni Sauti iliyo kwenye kanda.

Hebu niseme wazi kwa mara nyingine tena. Mimi SIPINGANI na mhudumu yeyote anayehubiri, wala sihisi mhudumu hawezi kuhubiri ama kufundisha. Lakini kwangu mimi na huduma yangu, nimeitwa kuuambia ulimwengu mzima kusikiliza Neno lililofanyika mwili, ambalo limerekodiwa na kuhifadhiwa kwenye kanda ya sumaku. Ninaamini ni Sauti ya Mungu, na ni HILO, na HILO peke yake, linalojibu maswali yako yote. Litakupa kila kitu unachohitaji, ikijumuisha na Imani ya Kunyakuliwa, kwa maana ni BWANA ASEMA HIVI.

Bibi-arusi hahitaji neno langu, ninanukuu tu Neno kama wahudumu wengine wote. Ninyi mnanukuu na kusema jinsi ilivyo muhimu kusikia huduma yenu na wito wenu, Bwana asifiwe. Mimi Ninawaambia watu huduma ILIYO MUHIMU ZAIDI ni Sauti ya Mungu iliyo kwenye Kanda. Hakuna kilicho kikuu zaidi yake. Wao Hawapaswi kuwa na kitu kingine chochote.

Sisemi mambo haya ili watu wawe na roho mbaya au mtazamo mbaya kwa mhudumu yeyote ama huduma yoyote, Mungu apishe mbali. Ninawapenda. Wao ni ndugu zangu. Mungu ameweka wito katika maisha yao. Je! nithubutu kunena dhidi ya watiwa mafuta wa Mungu, LAKINI nalazimika kunena na kusema kwamba wengi wameweka mkazo sana kwenye huduma YAO na hawakuiweka Sauti ya Mungu iliyo kwenye kanda kuwa ndiyo SAUTI ILIYO MUHIMU ZAIDI ambayo Bibi-arusi anayotakiwa kuisikia.

Nilisema kwa urahisi, “Mrudisheni Ndugu Branham kwenye mimbara zenu,” na wengi wa wahudumu wamevalia njuga kuwaambia watu wao ati Ndugu Branham hakusema jambo hilo kwenye kanda, na HAO wameitwa kulichukua Neno na kuwapa watu; wanatoa visingizio vya KUTOCHEZA KANDA MAKANISANI MWAO.

Wanasema ni MAKOSA ikiwa mchungaji anacheza kanda kanisani mwao, wanawakosoa watu wanasema, ikiwa wanasikiliza tu kanda katika makanisa yao, na sio wahudumu, wao si Bibi-arusi.

Nimesikia visingizio vingi sana wanavyotumia na kuwaambia watu. Kamwe hawatawaambia watu wao, “KANDA NDILO JAMBO LILILO MUHIMU SANA MNALOPASWA NINYI KUSIKILIZA”. Kama wangefanya hivyo, basi hao watu wangeuliza… “basi kwa nini hatuzichezi kanda kanisani mwetu kama ndio muhimu ZAIDI?”

Huyu ndiye tutakayemsikiliza Jumapili:

Mungu alijidhihirisha katika Mwanadamu, na akatambua ni nani aliyekuwa nyuma Yake; na yale Sara aliyotenda, akicheka hemani. Na Maandiko haya yote, ya Malaki, na kadhalika, yaliyobashiriwa katika siku za mwisho. Waebrania 4 ilisema, wakati “Neno” litakaporudi. Malaki 4 ilisema Hilo lingerudi kwa njia ya mtu.

Neno hilo limerudi kwa njia ya mtu nasi tuna Sauti Yake imerekodiwa kwenye Kanda na Tutaisikia KILA JUMAPILI.

Ninayo furaha kutangaza kwamba kwa mara nyingine tena, Jumapili hii saa 06:00 SITA MCHANA, saa za Jeffersonville,( Ni saa 1:00 MOJA JIONI ya Afrika Mashariki ) tutasikiliza Neno lililofanyika mwili na kurekodiwa kwenye kanda ya sumaku. Linatupa Ufunuo juu ya: Muhuri wa Tatu 63-0320.

Ni wakati uliyoje tutakaokuwa nao, Bibi-arusi. Ni furaha iliyoje itakayojaza mioyo yetu. Ni amani iliyoje itakayofariji nafsi zetu, tunaposikia yale ambayo Mungu Mwenyewe aliyomwambia Shetani: “Waache. Kama ukimshika mmoja wao, Wa Kondoo zangu waliojazwa na Mafuta Yangu na Divai ya Neno lililo safi, usiwalazimishe kusema ‘Salamu Maria’ yo yote, ama baadhi ya kanuni zako za imani. Usiwaguse. Wanajua wanakoenda, kwa maana wametiwa Mafuta Yangu na wana divai ya furaha, maana wanajua Neno Langu la ahadi. ‘Nitawafufua tena.’ Usidhuru Hao! Usiende ukajaribu kuwachafua…Usiwakaribie tu hata kidogo.”

Hatuna cha kuogopa. Tuna Neno. SISI NI NENO. Hatusimami kwa lolote. Sisi ni Wana na Binti za Mungu. Shetani, pisha njia, KILA kitu ni mali yetu. Mungu Alisema Hivyo. Imeandikwa!

Ndugu. Joseph Branham

Maandiko ya Kusoma kabla ya Kusikiliza Ujumbe:

Mathayo Mt 25:3-4
Yohana Mt 1:1, 1:14, 14:12, 17:17
Matendo Sura ya 2 yote
I Timotheo 3:16
Waebrania 4:12, 13:8
1 Yohana 5:7
Mambo ya Walawi 8:12
Yeremia Sura ya 32 yote
Yoeli 2:28
Zekaria 4:12