23-0730 Muhuri Wa Pili

UJUMBE: 63-0319 Muhuri Wa Pili

PDF

pakua – m4a

pakua – amr

BranhamTabernacle.org

Mpendwa, Bibi-arusi

Bibi-arusi hashangai kuhusu Ujumbe huu wala mjumbe Wake tangu mwaka 1933, wakati Nguzo ya Moto ilipotokea kwenye Mto Ohio siku hiyo. Tumejua ya kwamba William Marrion Branham ndiye malaika-mjumbe wa 7 mwenye nguvu wa Mungu aliyemtuma duniani kumwita Bibi-arusi Wake atoke.

Tangu siku hiyo, Mungu amekuwa akimkusanya Bibi-arusi Wake pamoja kwa ajili ya Kuja Kwake. Tuko chini ya matarajio hayo makubwa; maana tunajua itakuwa tu siku yo yote sasa.

Yeye amekuwa akiijenga Imani yetu kuliko hapo awali, akituambia, akituhakikishia, sisi ni Bibi-arusi Wake mwaminifu. Tunajua kwa sisi kukaa na Chakula Chake Kilichohifadhiwa ghalani, cho chote tunachohitaji kipo HAPO, KWENYE KANDA.

Tunajuaje jambo hilo kwa uhakika? Neno linasema MUNGU hatafanya NENO LO LOTE mpaka atakapolifunua kwa watumishi wake manabii. Kwa hiyo tunajua ikiwa Mungu atatufunulia jambo lo lote, ama kufanya jambo lo lote, kutupa Imani ya kunyakuliwa, Yeye atalinguruma kupitia nabii wetu, na nabii Wake peke yake.

Siku za kujiuliza-uliza zimekwisha. Bibi-arusi amechukua msimamo. Hakuna jambo lililo muhimu zaidi kuliko kumsikia Mungu akinena na Bibi-arusi Wake kwenye Kanda. Ndiyo Maneno pekee yaliyothibitishwa na Mungu Mwenyewe kuwa Bwana Asema Hivi.

Muda umeenda sana nasi tunaweza kuhisi ule uzito wa pumzi chafu ya adui yetu kutuzunguka pande zote. Vita vimepamba moto naye Shetani anashambulia kila upande, lakini Mungu asifiwe tunacho Chakula cha Kiroho, nasi tunaketi kwenye Meza ya Bwana mchana na usiku, tukila hiyo Mana Iliyofichwa. Anaendelea kutufunulia zaidi na zaidi kila siku anapotuambia, “Yote yako sawa kipenzi. Nipo pamoja nawe. Nilikuambia sitakuacha kamwe wala sitakupungukia. Kazana. Wafukuze hao pepo. Ninakupa bomu Langu la atomiki, Neno Langu, litumie. Nililiwaza. Ndipo likaandikwa, na sasa, katika siku Yenu, Nimelinena ili upate kunisikia MIMI nikikuambia WEWE, Bwana Asema Hivi, Wewe ni Bibi-arusi Wangu. Wewe ni Neno lililofanyika mwili.”

Mungu amenena kupitia midomo ya mwanadamu na ametupa Neno lake; hatuna cha kuogopa. Si Neno letu, mawazo yetu, mitazamo yetu, Ni Neno la Mungu alilotupa SISI. IMANI yetu iko katika Neno lake nalo Neno lake haliwezi KUSHINDWA KAMWE!

Sasa, tunapoisikia Mihuri hii ikifunguliwa, Roho Mtakatifu anazungumza nasi kwa mara nyingine tena nasi tunaweza kuyaona majina yetu yameandikwa humo kwenye Kitabu cha Uzima cha Mwana-Kondoo. Hatuwezi kabisa kujizuia…NDIYO, ni jina langu lililoandikwa humo. Anazungumza kunihusu MIMI.

Njooni muungane nasi Jumapili hii saa 6:00 SITA MCHANA, saa za Jeffersonville, ( Ni saa 1 MOJA JIONI ya Afrika Mashariki ) Na Kuusikia Muhuri wa Pili 63-0319, Wakati Sauti ya Mungu inapowaambia kuwa majina yenu yameandikwa katika Kitabu cha Uzima cha Mwana-Kondoo.

Ndugu. Joseph Branham

Maandiko ya kusoma kabla ya kusikiliza Ujumbe:

Mathayo Mt 4:8 / 11:25-26 / 24:6
Marko 16:16
Yohana 14:12
2 Wathesalonike 2:3
Waebrania 4:12
Ufunuo 2:6 / 6:3-4 / Sura ya 17 / 19:11-16
Yoeli 2:25
Amosi 3:6-7