23-0723 Muhuri Wa Kwanza

UJUMBE: 63-0318 Muhuri Wa Kwanza

PDF

pakua – m4a

pakua – amr

BranhamTabernacle.org

Wapendwa…Nitawaita Bibi-arusi,

Mungu, Muumba Mkuu, Alfa na Omega, Nyiroro ya mabondeni, Ua la Sharoni, Nyota yenye Kung’aa ya Asubuhi, Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu, Nguzo ya Moto, Mungu Mwenyewe, alikuja duniani na kunena nasi kupitia midomo ya mwanadamu, UTUKUFU!, Akaiweka kwenye kanda ya sumaku, ili Ninyi mweze kumsikia YEYE Akiwaita… “NINYI” BIBI-ARUSI WAKE.

Lioneni kwa picha dhairi jambo hili enyi marafiki. Bwana wetu Yesu Kristo, akiwatazama machoni na kuwaambia: “Ninyi ni Bibi-arusi Wangu. Nawapenda. Nimewangojea kwa muda mrefu sana. Kwangu Mimi, ninyi ni wakamilifu. Ninyi ni nyama ya nyama Yangu, mfupa wa mfupa Wangu. Niliwachagua ninyi kabla sijaumba Dunia au nyota. Nawapenda sana. Tutaishi Milele pamoja. Sasa, ninakuja kuwachukua.”

Hilo peke yake linapaswa kumpa kila mmoja wetu Imani ya Kunyakuliwa. Ni kitu gani ibilisi anaweza kuwarushia, kuwaambia, kukiweka juu yenu ambacho kinaweza kuwadhuru? HAKUNA CHOCHOTE, NINYI NI BIBI-ARUSI WA KRISTO! Ninyi ni Neno Lake lililofanyika mwili, ninyi ni Bibi-Yesu Kristo.

Anawezaje mtu yeyote, katika lugha yoyote, kuandika na kutuelezea nini maana yake? Huwezi kabisa.

Hakuna mahali popote duniani unapoweza kuwa na heshima na majaliwa hayo ya kusikia Maneno haya isipokuwa uwe na Ufunuo sahihi na UBONYEZE PLAY.

Yale matukio makuu zaidi ambayo ulimwengu umekuwa ukingojea tangu mwanzo wa wakati, yanatukia sasa hivi, nasi tu sehemu ya hilo. Yeye ameingojea siku hii, saa hii, watu hawa; NINYI, kuutimiza na kuutekeleza Mpango Wake Mkuu.

Ufunuo wa ile siri ya ile Mihuri Saba, zile Ngurumo zikifunuliwa, ukamilifu wetu, Adamu Wake aliyerejeshwa kikamilifu, Kuja Kwake, mambo haya yote yanadhihirishwa na yanatimia SASA HIVI, ndani YENU, BIBI-ARUSI WAKE!

Si katika siku za Musa. Si katika siku za Nuhu. Si katika siku za Yesu, Si hata katika siku za Yohana ama Paulo; Inatukia sasa, SASA HIVI, KWENU NINYI.

Hatutaki kulikosa. Tunataka kuwa tayari kwa ajili ya huku Kuja Kwake. Ili kufanya jambo hilo, tumeagizwa kwenda kwenye NENO kupata majibu yetu. Si wazo langu, ama wazo la mtu fulani ama mafikara yake, bali Yale Neno la Mungu lililothibitishwa linasemayo.

Tunajua Bibi-arusi yampasa kusema “amina” kwa kila Neno na kuungana pamoja kuwa Mmoja. Kwa hiyo ni lazima tuangalie katika Neno la Mungu ili tuone ni kitu gani kitakachomuunganisha Bibi-arusi pamoja.

Na ndipo kunakuja Ngurumo saba za siri ambazo hata hazijaandikwa kamwe. Hiyo ni kweli. Nami naamini ya kwamba, kupitia Ngurumo hizo Saba, zitafunuliwa katika siku za mwisho ili kumkusanya Bibi-arusi pamoja kwa ajili ya kupata imani ya kunyakuliwa.

Papo hapo liko katika Neno. Hizo Ngurumo Saba zitafunuliwa katika siku yetu ili kumkusanya Bibi-arusi pamoja kwa ajili ya kupata imani ya kunyakuliwa.

Kisha swali linalofuata tunalohitaji kujua ni: Je, hizo Ngurumo ni nini?

Wakati, ile “iliponguruma.” Kumbuka, sauti kuu ya kishindo cha Ngurumo ni Sauti ya Mungu. Hivyo ndivyo Biblia isemavyo, unaona, “kishindo cha Ngurumo.” Wao walidhani ilikuwa ni ngurumo, lakini ilikuwa ni Mungu. Yeye aliielewa, kwa maana ilifunuliwa Kwake. Unaona? Ilikuwa ni Ngurumo.

Kwa hiyo zile Ngurumo ni Sauti ya Mungu itakayomkusanya Bibi-arusi pamoja na kuwapa (SISI) imani ya Kunyakuliwa. Hilo hapo jibu letu.

Ni nani aliye Sauti ya Mungu kwa Bibi-arusi?
William Marrion Branham.

Sasa, mimi ni ndugu yenu tu, kwa neema ya Mungu, lakini pindi huyo Malaika wa Bwana anaposhuka, inakuwa, basi, Sauti ya Mungu kwenu…Mimi siwezi kusema neno lolote mwenyewe, ila kile Yeye anachonionyesha, Mimi Nakisema. Ninyi aminini jambo hilo na mwone kinachotokea.

Liaminini jambo hilo na mwone kile kitendekacho na kutukia Jumapili hii, tutakapokusanyika pamoja, kupokea imani ya kunyakuliwa, kumsikia Yeye Akinguruma kwa Bibi-arusi Wake.

Nena “kuhusu kuketi sasa katika ulimwengu wa Roho”? Itakuwaje! Kama tunaweza kujisikia hivi, hali tumeketi hapa duniani, kabla ya kuja kwa Kunyakuliwa, katika hali hii tuliyo nayo sasa; nasi tunaweza kufurahi, na tukisimama kando-kando ya kuta, na kusimama kwenye mvua, ili tu kusikia jambo Hili; itakuwaje tutakapomwona Yeye ameketi pale! Loo! jamani! Loo! utakuwa ni wakati wa fahari kweli.

Usikose katika wakati huu mtukufu. Umealikwa kukusanyika pamoja nasi tunaposikia: Muhuri wa Kwanza 63-0318, saa 06:00 SITA MCHANA, saa za Jeffersonville.( ni saa 1:00 MOJA JIONI ya Afrika Mashariki)

Ndugu. Joseph Branham

Maandiko ya Kusoma Kwa Maandilizi ya Kusikiliza Ujumbe:

Mtakatifu Mathayo 10:1 / 11:1-14 / 24:6 / 28:19
Yohana 12:23-28
Matendo 2:38
2 Wathesalonike 2:3-12
Waebrania 4:12
Ufunuo 6:1-2 / 10:1-7 / 12:7-9 / 13:16 / 19:11-16
Malaki Sura ya 3 na ya 4
Danieli 8:23-25 ​​/ 11:21 / 9:25-27