23-0716 Pengo Kati Ya Nyakati Saba Za Kanisa Na Ile Mihuri Saba

UJUMBE: 63-0317e Pengo Kati Ya Nyakati Saba Za Kanisa Na Ile Mihuri Saba

PDF

pakua – m4a

pakua – amr

BranhamTabernacle.org

Wapendwa Yungiyungi dogo za Kidimbwi,

Tumejipenyeza hadi juu ya maji yenye matope na kutandaza mbawa zetu. Petali zetu ndogo zimetokeza na sasa linaakisi ua la Uwandani . Tumeweka maisha yetu kikamilifu kwa Mungu na Neno lake.

Tuko katika wakati wa mwisho tukitoka Mashariki na Magharibi, Kaskazini na Kusini, tukijiweka tayari kwa ajili ya huo Unyakuo. Tukijishikilia imara kwa dakika chache mpaka kila mshipa umejazwa na Roho Mtakatifu. Tunajiweka tayari KUPAA JUU.

Siku yenyewe imefika. Anawaita watu Wake pamoja Kwake katika umoja wa kweli na Yeye Mwenyewe. Ni Yesu Kristo akiishi pamoja na Roho wake katika mwili wetu, akifanya mambo yale yale aliyoyafanya kama bendera kwa ulimwengu.

Jambo lililo tukufu zaidi katika Maandiko linatendeka katika wakati wetu. tendo, ambalo hata Malaika, hakuna kitu, kingaliweza kufanya jambo hilo, ila Mwana-Kondoo. Alikuja na kukitwaa kile Kitabu kutoka katika mkono wa kuume wa Yeye aliyeketi juu ya kile Kiti cha Enzi, akakifungua, akaichana ile Mihuri, na kukituma duniani, kwa malaika Wake wa saba, atufunulie SISI, Bibi-arusi Wake.

Mambo yanayotukia; Neno analotufunulia kila siku, hayaelezeki. Tunapaza sauti zetu, na kupiga vifijo na vigelegele, Haleluya! Upako, nguvu, utukufu, dhihirisho, Ufunuo huu wa Neno Lake ni mkuu kuliko ulivyopata kuwa tangu mwanzo wa wakati.

Pamoja na kila kiumbe kilichoko mbinguni, na juu ya nchi, na chini ya nchi, ndani ya bahari, na vyote vilivyomo ndani yake, tunapaza sauti: Baraka, heshima, utukufu, uweza, ni kwake Yeye aketiye juu ya kile kiti cha enzi, na Mwanakondoo milele, amina! Amina, na amina!

Kila kiumbe, kila mtu tangu mwanzo wa wakati walingojea siku hii ifike. Hata Mungu Mwenyewe alingojea mpaka malaika Wake mteule alipofika duniani kabla ya Yeye kujitokeza kukitwaa kile Kitabu, kukifungua na kuzifunua siri Zake zote kwa Bibi-arusi Wake mteule.

Sasa tunajua yale ambayo hakuna mwanadamu duniani, tangu mwanzo wa wakati, amewahi kujua. Kila kitu kilichopotezwa katika lile anguko. Kila kitu ambacho kimefichwa katika Neno Lake. Kila kitu ambacho Bibi-arusi anachohitaji kimerekodiwa na kimewekwa katika ghala moja dogo la Mungu.

Ametuonyesha Kule ng’ambo ya pili ya pazia la Wakati nasi tunajiona wenyewe tukiwa pamoja Naye kule upande wa Pili. Bibi-arusi amejifanya tayari kwa kusikia Neno.

Tumekuwa katika mafunzo. Tumevaa silaha zote za Mungu. Hakuna kinachoweza kutuondosha. Hakuna kinachoweza kututisha. Hakuna kinachoweza kutudhuru. Hakuna kinachoweza kutufanya kupatana hata kwenye Neno moja. SISI NI NENO.

Tunamngojea huku tukiwa na shada letu la maua mikononi mwetu. Muda umefika. Ile Saa ya kale inayoyoma. Tunasikia farasi wakienda shoti, mchanga ukivingirishwa chini ya gurudumu. Lile gari la Kale la farasi liko karibu kusimama.

Atakapokuja tutaruka kutoka katika ulimwengu huu wa kale nakuangukia Mikononi mwake. Atatunyakua na kusema, “Nilikuwa nimekwenda kuwaandalia mahali, lakini yote yamekwisha sasa, mpenzi”.

Kuja Kwake kumekaribia sana. Tuko chini ya matarajio zaidi ya hapo kabla. Tunayo furaha sana kwa anavyotaka tuisikie ile Mihuri Saba kwa mara nyingine tena. Tunajua tutapokea Ufunuo zaidi, kwa sababu kila Ujumbe tunaousikia ni kana kwamba kamwe hatujawahi kuusikia hapo awali.

Kuishi leo hii na kusikia Ujumbe huu ni hata kuu zaidi kuliko wakati uliporekodiwa. Yeye Anatufunulia hata na zaidi sasa hivi. Ni kitu gani kingeweza kutokea?

Njoo ukusanyike pamoja nasi saa 06:00 SITA MCHANA, saa za Jeffersonville,( Ni saa 1:00 MOJA JIONI ya Afrika Mashariki),na Kufurahia kusikiliza:  
63-0317E Pengo Kati ya Nyakati Saba za Kanisa na Ile Mihuri Saba. Ni Chakula Kilichohifadhiwa alichokiandaa Bwana kwa ajili ya Bibi-arusi kula.

Ndugu. Joseph Branham

Maandiko ya kusoma kwa maandalizi ya kusikiliza Ujumbe:

Mambo ya Walawi 25:47-55
Yeremia 32:1-15
Zekaria 3:8-9 / 4:10
Warumi 8:22-23
Waefeso 1:13-14 / 4:30
Ufunuo 1:12-18 / Sura ya 5 yote/ 10:1-7 / 11:18