23-0709 Mungu Akijificha Kwa Urahisi, Halafu Akijifunua Kwa Jinsi Hiyo

UJUMBE: 63-0317M Mungu Akijificha Kwa Urahisi, Halafu Akijifunua Kwa Jinsi Hiyo

PDF

pakua – m4a

pakua – amr

BranhamTabernacle.org

Wapendwa Watu Wateule, Wa kipekee, Wasio wa kawaida, Ukuhani wa Kiroho, Taifa la Kifalme,

Ni wakati ulio wa fahari jinsi gani ambao Yeye Amekuwa akimpa Bibi-arusi Wake, akifunua Neno Lake zaidi ya hapo nyuma. Kila Ujumbe tunaousikia inaonekana kana kwamba hatujawahi kamwe kuusikia hapo awali. Mioyo na nafsi zetu zimejaa furaha tunapofanyia karamu Mana Mpya ishukayo kutoka Mbinguni. Inaonekana kama onyesho letu la awali la Karamu yetu ya Harusi inayokuja hivi karibuni anapotulisha Ufunuo baada ya Ufunuo.

Tunamtolea Mungu dhabihu za kiroho, kwa matunda ya midomo yetu, tukilisifu Jina Lake. Tumetwaa nafasi zetu kama nyota za mbinguni.

Ametuunganisha pamoja katika ulimwengu wa roho, akimimina Roho Wake Mtakatifu juu yetu, akitutayarisha kwa ajili ya Kuja kwake hivi karibuni. Ndio yote tunayoweza kuwazia. Ndio yote tuliyo nayo akilini mwetu. Yote tunayotaka kufanya ni KUSIKIA NENO. Yeye anatuambia tena na tena sisi ndio Bibi-arusi Wake. Haya ndio Mapenzi yake Makamilifu kwa kukaa na Njia yake iliyoandaliwa.

Sisi ni askari katika Idara ya Huduma Yake ya kanda, nasi tunajivunia jambo hilo. Ni beji ya heshima. Tunatamani kulisema kwa sauti na kuuambia ulimwengu, NDIYO, SISI NI MMOJA WAO.

Ametupa Chakula kilichohifadhiwa ili tupate kula. Ile Mana ya Mungu Mwenyewe akinena na Bibi-arusi Wake, akitujulisha sisi tuko katika jeshi Lake.

Tunakusanyika chini ya dari kuu la mbinguni katika upatano sana, hata Roho Mtakatifu amemweka kila mshirika wa ule Mwili hata kumekuwa na uponyaji unaobubujika wenyewe wa nafsi na mwili.

Tunalichukua Neno la Mungu na kumshinda ibilisi na nguvu zake. Tunamkatakata vipande-vipande kwa Neno hilo. Kapteni wetu Mkuu alituambia: “Wewe ni Neno. Usiogope. Nenda moja kwa moja hadi kwa Ibilisi na useme, ‘IMEANDIKWA.’”

Ametuchagua tuwe askari wake. Tumekuwa katika mafunzo, tumeimarishwa na Neno Lake. Sasa tumevaa na tuko tayari kwa mapambano. Jenerali wetu mwenye Nyota 5 ametuamuru nini la kufanya: Shikilieni kabisa hayo mafundisho Yangu ya kanda.

Nanyi mwe na hakika, semeni tu yale tu kanda inayosema. Msiseme jambo lingine lo lote. Mnaona? Maana, sisemi jambo Hilo kwa nafsi yangu mwenyewe. Yeye Ndiye anayesema Hilo , mnaona. Na mara nyingi sana, vurugu, watu wanainuka na kusema, “Vema, Fulani alisema ilimaanisha hivi-na-hivi.” Liache tu jinsi lilivyo.

Si yale William Branham anayotuambia kwenye kanda, ni yale MUNGU anayomwambia Bibi-arusi Wake kwenye kanda. Haya ni MAAGIZO yake. Kuna njia moja tu ya kutii maagizo haya kutoka kwa Jenerali wako mwenye Nyota 5 na uliache jinsi lilivyo, KUBONYEZA PLAY.

Tuko katika jeshi la Mungu, kwa hivyo lazima tutii maagizo yetu Neno kwa Neno. Tunasonga mbele. Sisi ni watu mashujaa, watu wa imani, watu wenye nguvu, watu wenye ufahamu, watu wa Ufunuo.

Tunakuwa katika ushirika mkamilifu na Baba tena, tukisimama upande ule mwingine wa shimo, bila kumbukumbu la dhambi dhidi yetu. Adamu wake aliyerejeshwa.

Ni Mungu katika urahisi kwa mara nyingine tena. Si kwa ajili ya kila mtu, Bibi-arusi Wake peke yake, nasi tunaliona waziwazi na dhahiri kabisa.

Ninayo matazamio makuu ya kuisikia ile Mihuri Saba kwa mara nyingine tena. Yeye atakuwa akitufunulia Neno Lake zaidi ya hapo awali. Tutakuwa tukipokea Ufunuo ulio mkuu zaidi wa Neno Lake.

Yeye amengojea hadi siku hii ya leo ili kutufunulia sisi mengi zaidi. Yote tunayohitaji yamerekodiwa na yanapatikana kwa ajili yetu kuyasikia kwa mguso tu wa kidole chetu.

Ujumbe huu ndio zile Ngurumo Saba zitakazomkamilisha Bibi-arusi; kwa maana SIRI ZOTE ZA MUNGU ZITAFUNULIWA NA MALAIKA-MJUMBE WETU WA 7 KWA BIBI-ARUSI.

Huu ni wakati wenye fahari mno katika historia ya ulimwengu. Tuko ukingoni mwa kuja Kwake kumjia Bibi-arusi Wake. Ulimwengu unatarajia mambo haya yote yaliyonenwa katika Maandiko; kama jua kutua mchana na mambo ya kila namna kutukia. Lakini imepita tayari, na hawakujua.

Kumbukeni, kimetiwa muhuri na hizo Ngurumo Saba za siri. Unaona?

Mambo makuu yanaenda kutukia tunapokusanyika kwa mara nyingine tena ili kumsikia Mungu Akinguruma na kumfunulia zaidi Bibi-arusi Wake kwenye ile Mihuri Saba.

Ninakualika uungane nasi saa 06:00 SITA MCHANA, saa za Jeffersonville, ( Ni saa 1:00 MOJA JIONI ya Afrika Mashariki ) tunapoanza mfululizo huu mkuu kwa Ujumbe:
63-0317M Mungu Akijificha Kwa Urahisi, Halafu Akijifunua kwa jinsi hiyo.

Wakati Ndugu Branham anapoweka wakfu upya kwa Mungu Maskani ya Branham na watu, hebu na tujiweke wenyewe wakfu upya Kwake, nyumba zetu, makanisa yetu, ama popote tunapokusanyika.

Ndugu. Joseph Branham

Maandiko ya Kusoma kwa maandalizi ya Kusikiliza Ujumbe:

1 Mambo ya Nyakati 17:1-8
Isaya 35:8 / 40:1-5 / 53:1
Malaki Sura ya 3
Mathayo 11:10, 11:25-26
Yohana 14:1-6
1 Wakorintho Sura ya 13
Ufunuo Sura ya 21