22-0116 Mungu Akijificha Kwa Urahisi, Halafu Akijifunua Kwa Jinsi Hiyo

Ujume: 63-0317M Mungu Akijificha Kwa Urahisi, Halafu Akijifunua Kwa Jinsi Hiyo

PDF

pakua – m4a

pakua – amr

BranhamTabernacle.org

Mpendwa Kundi dogo la Eliya ,

 Sisi ni watu wateule, wakipekee na wasio wa kawaida  kwa ulimwengu, na kwa waaminio wengi, lakini hata hivyo, sisi ni ukuhani wa kiroho, taifa la kifalme, tukimtolea Mungu dhabihu za kiroho, pamoja na matunda ya midomo yetu tukilisifu Jina Lake.  Tunataka kuuambia ulimwengu kwamba tuna furaha sana, tunashukuru sana, na kuheshimika sana kuwa Wamoja Wao.

 Tumeuza lulu zetu nyingine zote, Yeye alipotupa Lulu ya thamani kuu, Ufunuo Wa Yeye Mwenyewe.  Tunaona Neno lenyewe la Mungu likidhihirishwa.  Ahadi ile ile ya siku za mwisho, Nuru za jioni zile zile ambazo zingeangaza.

 Imefunuliwa kilindi kabisa mioyoni mwetu kwamba Sauti tunayoisikia kwenye kanda ni Mwana wa Adamu akijifunua Mwenyewe.  Sauti hiyo ilituambia: Kaeni hapa, Angalieni Chakula Hiki kilichohifadhiwa ambacho nimewawekea kwenye hizo kanda.  Ikiwa una maswali yoyote, Rudi kwenye kanda hizi.  Inaweza hata kukushangaza kidogo, lakini cheza tena kanda na usikilize kwa makini.  Kama wewe ni Bibi-arusi, Roho Mtakatifu atakufunulia jambo Hilo.  Kumbuka, kanda hazihitaji kufasiriwa kokote, sema tu kile kilicho kwenye hizo kanda.  Mimi ni mchungaji wenu na ninyi ni kundi langu dogo, Dumuni na mafundisho ya kanda.

 Najua wengi sana hawaelewi tunachofanya kwa kusikiliza Ujumbe uleule wote kwa wakati mmoja, lakini ni sawa, bado ni ndugu na dada zetu nasi tunawapenda na hatupaswi kamwe kusema dhidi yao.  Kila Mtu lazima afanye kama wanavyohisi wanaongozwa Na Bwana kufanya.  Mungu hufanya kazi na kutuongoza kama watu binafsi.

 Nabii alituambia lazima tuchunguze kila kitu kwa Neno, na kukithibitisha kwa Neno, kama tu alivyofanya.  Neno la wakati huu, Ni na daima imekuwa, Biblia.  Biblia inatuambia katika siku za mwisho angefunua kikamilifu siri na mafumbo yote katika Biblia yake kwa nabii ambaye atamtuma.  Yeye Mwenyewe angenena kupitia nabii huyu na kujidhihirisha Mwenyewe katika mwili kama alivyofanya kwa Ibrahimu.  Neno Lake lisingekuwa maneno ya mwanadamu, bali  Maneno yenyewe ya Mungu Mwenyewe.  Ingekuwa BWANA ASEMA HIVI, kwa hiyo Biblia na Sauti hiyo zingekuwa kitu kimoja na sawa.

 Kuna Kilindi  kikiita kilindi  ndani ya mioyo yetu kusikia hiyo Sauti iliyothibitishwa.  Tunataka kusikia Sauti ya Mungu moja kwa moja kutoka kwa nabii Wake Aliyechaguliwa.  Kuna upendo kama huu mioyoni mwetu kusikia Sauti hiyo na kustarehe tu tukijua hatuhitaji kuhoji chochote tunachosikia, inabidi tu kuamini KILA NENO.

 Hakuna mahali pengine ambapo tunaweza kufanya hivyo.  Sio kwamba mtu fulani angetuambia jambo lisilo  sahihi au kutupotosha, kwa vile wao pia wana Roho Mtakatifu, Lakini tunajua kwamba wanaweza kutuambia jambo Lisilo Sahihi bila kupenda.  Lakini tunaposikia Sauti ya Mungu iliyothibitishwa kwenye kanda, hata kama hatuelewi kinachosemwa, Baba Mungu alisema inatupasa tu kusema AMINA, TUNAAMINI KILA NENO.  Hatuwezi kufanya hivyo kwa sauti nyingine yoyote.

 Tuliamriwa na Sauti hiyo pia:

 Msinisikilize mimi , bali sikilizeni kile nilichosema. Nilichosema ni ujumbe . Msimjali mjumbe kamwe; angalieni ujumbe. Kazeni macho yenu, si juu ya mjumbe, lakini juu ya ujumbe—kile ulichosema . Hilo ndilo jambo la kuangalia `“ .

 Alichosema NI Ujumbe wa wakati huu.  Tunapaswa kukaza macho yetu juu ya Ujumbe;  Ndilo jambo la kuangalia .

 Anatufunulia mambo kuliko hapo awali.  Kila Ujumbe tunaosikia unasikika kama Ujumbe mpya ambao hatujawahi kamwe kuusikia.  Ingawa tumezisikia mara mamia hapo awali, hatuwezi kueleza, ni kama tunausikia kwa mara ya kwanza naye anatupa Ufunuo zaidi na zaidi.

 Hatuwezi tu kuwazia mtu yeyote Asitake kusikia Jumbe hizi pamoja nasi.  Kuna muungano kama huo na Umoja pamoja na Bibi-arusi na Neno Lake.  Tumeridhika kabisa zaidi ya wakati mwingine maishani mwetu.

 Kwa mara nyingine tena tuko chini ya matarajio makubwa.  Ni kana kwamba Mihuri inafunguliwa sasa hivi.  Anaenda kutuonyesha mambo ambayo hatujawahi kamwe kuyaona hapo awali na kuleta Nuru kwa mambo ambayo tumesikia mara nyingi ,nyingi sana hapo awali;  lakini sasa, tutaliona waziwazi.

 Tunajua ya kwamba kila kitu tunachohitaji kwa ajili ya Unyakuo Wake ujao hivi karibuni, ni ile Sauti kwenye hizo kanda.

 Mungu alimtuma nabii Wake kwa ono upande wa nyuma wa jangwa huko Arizona ambako alitwaliwa juu na malaika saba, kisha akarudishwa Jeffersonville kufunua siri zilizofichwa za ile Mihuri Saba kwa Bibi-arusi.

 Njoo usikilize pamoja nasi Mungu anapozungumza nasi mdomo kwa sikio Jumapili hii saa 4:00 nne Asubuhi., saa za Jeffersonville,( ni saa 12:00 kumi na mbili jioni ya Tanzania),  nasi tutasikia: Mungu Akijificha  Kwa Urahisi, Halafu Akijifunua Kwa Jinsi  Hiyo 63-0317M .

 Tutauanza Ujumbe huu kwenye aya ya #94, baada ya ibada ya kuweka wakfu.

 Ndugu.  Joseph Branham

 1 Mambo ya Nyakati 17:1-8

 Isaya 35:8 / 40:1-5 / 53:1

 Malaki Sura ya 3 yote

 Mathayo Mtakatifu 11:10, 11:25-26

 Yohana Mtakatifu 14:1-6

 1 Wakorintho Sura ya 13 yote

 Ufunuo Sura ya 21 yote