22-0123 Pengo Kati Ya Nyakati Saba Za Kanisa Na Ile Mihuri Saba

Ujume: 63-0317e Pengo Kati Ya Nyakati Saba Za Kanisa Na Ile Mihuri Saba

PDF

BranhamTabernacle.org

Mpendwa Bibi-arusi anayepiga vifijo na kufurahi,

Tuko katika Neno na tuna wakati mkuu zaidi katika maisha yetu yote. Kufundisha, kujiweka wakfu, na ufunuo. Hakuna kitu muhimu zaidi kuliko kusikia Sauti ya Mungu kwenye kanda.

Ujumbe huu ni kila kitu kwetu sisi. Unatupa kuridhika kukamilifu. Kitu pekee kinachoweza kuzima kiu ya nafsi zetu ni kumsikia Mungu akisema nasi kupitia nabii wake.

Kila siku anatupa ufunuo zaidi wa Yeye Mwenyewe na sisi wenyewe. Uhakikisho wa kina zaidi kwamba, kwa “Kubonyeza Play,” tunasikia Neno Lake na tunafanya kama vile Yeye alivyotuamuru kufanya. Sisi ni kondoo wake, na kondoo hawezi kujiongoza mwenyewe; inabidi awe na kiongozi. Na Roho Mtakatifu anatuongoza Kwake, Sauti Yake inenayo Maneno ya kutoweza kukosea kwenye kanda.

Si kwa bahati kwa sisi kusikiliza Jumbe hizi pamoja, Yeye alituchagua sisi kufanya hivyo. “hatua za wenye haki huongozwa na Bwana.” Kuna sababu fulani. Hatuwezi kusaidia. Ujumbe kwenye kanda ndio tu Bibi-arusi anaotaka. Kwa kuusikia, inatupa mkono wenye nguvu wa Imani kushikilia na kuamini kila Neno.

Kwa nini tunaamini ni muhimu sana kwa wote wanaojiita “Bibi-arusi wa Mungu” kuzisikiliza kanda ?

Neno linatuambia wazi kwamba Biblia yenyewe iliandikwa na manabii. Hayakuwa mawazo yao, wala fikra zao, bali Roho Mtakatifu akiwasukuma kuandika Biblia. Biblia pia inatuambia kwamba Bwana Mungu hatafanya neno LOLOTE mpaka atakapolifunua Neno Lake kwa nabii Wake. Wengine wanaweza kunena Hilo na kulitangaza, lakini wanaweza kusema TU yale ambayo nabii wa Mungu amekwisha kusema.

Kama unaamini ya kwamba William Marrion Branham ni Malaika-mjumbe wa 7 aliyethibitishwa na Mungu, basi kile alichosema KWENYE KANDA si maneno yake, bali ni mawazo yenyewe hasa ya Mungu Mwenyewe yaliyotambulishwa. Unaweka Kikomo chako cha Milele kwenye kila Neno alilonena kwenye hizo kanda, kama unavyoamini hiyo kuwa ni BWANA ASEMA HIVI. Haiwezi kuongezwa kwake wala kuondolewa kutoka kwake, wala halihitaji kufasiriwa; Ni Mwana wa Adamu akizungumza kupitia kwa mtu aliyemchagua ili kutimiza Neno Lake.

Bibi-arusi wa kweli anajua umuhimu wa kuzisikiliza kanda. Kwetu sisi, kanda hizi ni kuu na huduma nyingine zote ni ndogo. Kila mtu lazima wajiulize kama kikomo chao cha Milele kinategemea kuamini kila Neno ambalo nabii wa Mungu alilonena. Kama ninaamini ni Sauti ya Mungu inayonena na kumwita Bibi-arusi Wake, basi hakuna kitu cha maana zaidi kuliko KUBONYEZA PLAY, kwani nitahukumiwa kwa kila Neno ambalo NABII WA MUNGU ALILOSEMA…si kwa lile mtu fulani alilosema kwamba nabii wa Mungu alisema.

Kama unaamini unahitaji zaidi ya hizi kanda , basi kwako huoni umuhimu kuweka msisitizo wa kuzisikiliza kanda, bali unaweka umuhimu zaidi kwenye huduma. Unaweza kuwa na mkuu mmoja tu.

Tutakaposikiliza kanda Jumapili hii, Mungu Mwenyewe atazungumza nasi na kutuambia tuna umiliki wa halali wa hati-miliki ya kuwazika ya Uzima wa Milele. Tuna kila kitu ambacho Adamu na Hawa walikipoteza. Kitaletwa kwetu katika ufunuo, na kutoka katika Mkono wa Mungu kwa kuthibitishwa.

Kisha atatuambia nini kiliendelea Mbinguni. Jinsi Yesu Mwenyewe alivyokitwaa kile Kitabu, akaichana muhuri, kisha akakipeleka kwa nabii aliyemchagua na akamwambia ampe Bibi-arusi Wake….Nena kuhusu vifijo !!!! Kila kitu duniani na Mbinguni kitatusikia tukipiga vifijo na kupiga vigelegele tunapoona majina yetu yameandikwa kwenye Kitabu cha Uzima cha Mwana-Kondoo.

Naye akakitwaa kile Kitabu, (utukufu!) akakifungua kile Kitabu, na kuichana ile Mihuri; na kukituma duniani, kwa malaika Wake wa saba, kukifunua kwa watu Wake! Haya basi. Loo! jamani! Ni kitu gani kilichotukia? Vigelegele, vifijo, zile haleluya, watiwa mafuta, nguvu, utukufu, dhihirisho!

Na maskini Yohana, aliyekuwa amesimama pale, ndugu yetu, akilia! “Mbona,” yeye akasema, “kila kitu Mbinguni, kila kitu duniani, na kila kitu chini ya bahari, vilinisikia nikisema kwa sauti kuu, ‘Amina! Amina! Baraka, heshima, na uweza, na nguvu, ziwe Kwake Yeye aishiye milele na milele.’”

Unaweza kuusikia wapi ufunuo huu mkuu? KWENYE KANDA TU. Kuna jambo la Kipekee kwa Bibi-arusi wanapomsikia Mungu Mwenyewe akisema kupitia midomo ya mwanadamu na kuwaambia, “WEWE NDIWE BIBI-ARUSI WANGU KIPENZI.”

Njoo uketi katika uwepo wa Roho Mtakatifu kwa Kubonyeza Play , Jumapili saa 6:00 sita Mchana, saa za Jeffersonville,( ni saa 2:00 Mbili Usiku ya Tanzania) tunaposikia Malaika-mjumbe Wake wa saba akileta: Pengo Kati ya Nyakati Saba za Kanisa Na Ile Mihuri Saba 63-0317E .
Tutakuwa tukipiga vifijo na kushangilia na kusema haleluya.

Ndugu. Joseph Branham

Maandiko ya kusoma kwa maandalizi ya kusikiliza Ujumbe:

Mambo ya Walawi: 25:47-55

Yeremia: 32:1-15

Zekaria: 3:8-9 / 4:10

Warumi: 8:22-23

Waefeso: 1:13-14 / 4:30

Ufunuo: 1:12-18 / Sura ya 5 yote / 10:1-7 / 11:18