23-0813 Muhuri Wa Nne

UJUME: 63-0321 Muhuri Wa Nne

PDF

pakua – m4a

pakua – amr

BranhamTabernacle.org

Wapendwa Wana Tai,

Sauti ya Mungu inatupaisha kwenye kilele ambacho hatujawahi kufika hapo awali, na kufunua Neno Lake. Tumeichimbia midomo yetu midogo ndani ya Mbawa Zake kuu anapotupeleka juu angani. Tunapaa juu zaidi ya anga zote zenye mawingu. Tunaweza kuona mbali sana katika umilele. Ni Ufunuo mpya kabisa kwetu. Kadiri anavyotupeleka juu zaidi, ndivyo inavyokuwa wazi zaidi. Tunapiga kelele: NALIONA…NALIONA.

Sasa amechukua Mabawa Yake yenye nguvu, akayatikisa sana na kutuambia, “RUKENI ENYI WANANGU, RUKENI. Mwanzoni tuliogopa sana. Yule adui alikuwa akizijaza akili zetu mashaka mengi sana. Siwezi, Siwezi kabisa. Kisha tukamsikia Yeye akitupazia sauti na kurudia kunguruma, “MNAWEZA, NYINYI NI WANA TAI WANGU, ANZENI TU KUYAPIGA MABAWA YENU!!”

Kisha, yote kwa pamoja mabawa yetu madogo kwa kawaida huanza kupiga-piga. Kadiri tunavyosikiliza Neno Lake hutuhakikishia sisi ni nani, na nini cha kufanya, na ndivyo mabawa yetu yanavyozidi kuwa na nguvu. Piga, piga, piga….Bonyeza Play, Bonyeza Play, Bonyeza Play …kisha ghafla, tunaruka. Sisi ni Tai.

Wakati Hofu kidogo inapojaribu kuingia niani mwetu, tuliangalia tu huku na kule na kuanza kusikiliza Sauti Yake. Huyo hapo, akiruka karibu nasi ili kutukamata ikiwa tutaanza kuanguka. Tunatambua hatuna cha kuogopa, Baba Tai yuko papo hapo pamoja nasi. Yeye anaangalia kila hatua tunayofanya. Hataruhusu chochote kitupate.

Uhuru na hakikisho jinsi hii ambao kiasi kwamba hatujawahi kuuhisi hapo awali. Yeye anaendelea kutuambia, Ninyi ni wana tai Wangu. Mnatii na kufanya kile hasa Nilichowaambia mfanye kwa kukaa na Sauti Yangu Niliyowaachia.

Yeye anajua anapotuambia jambo lo lote kwenye kanda, tutaenda kulifanya, kwa maana tunajua ni Neno Lake. Yeye atasimama moja kwa moja nyuma ya Jambo hilo. Hata kama halikuandikwa katika Biblia, Yeye ataliunga mkono, hata hivyo.

Tunajua, kama liko nje ya jambo hilo, Yeye atalifunua kwa nabii Wake. Tunatambua ya kwamba siri zote za Mungu zinajulishwa kwa nabii Wake, na yeye peke yake, kwa hiyo lo lote tunalohitaji kujua, Liko kwenye kanda.

Nena kuhusu nguvu za Ufunuo unaoleta changamko. Tunataka kupiga makelele kwa sauti zetu zote. Tunataka ulimwengu ujue, Mimi ni tai wa Kanda!

Mawazo ya Mungu yakawa uumbaji wakati yaliponenwa, kwa Neno. Hapo ndipo wakati anapoyaleta kwa—kwako kama wazo, wazo Lake, nalo linafunuliwa kwako. Halafu, lingali ni wazo mpaka wewe utakapolinena.

Imefunuliwa kwetu. Utukufu. Sasa tunataka kulinena. Sisi ni Bibi-arusi wa Yesu Kristo. Alinijua mimi, alinichagua tangu zamani kabla ya kuwekwa misingi ya ulimwengu. Mimi ni Neno Lake lililo hai lililofanyika mwili. Aliniambia OMBA nawe utapokea. Bisha, utafunguliwa. Chochote tunachokihitaji, TUNAKINENA.

Huu ni Wakati wa Tai na sisi ndio Wana Tai Wake. Hatujawahi kuwa na furaha ama kuridhika zaidi katika maisha yetu. Bila hofu. Bila wasiwasi.

Ninakualika uje uruke umbali wa upeo mpya pamoja nasi Jumapili hii saa 06:00 SITA MCHANA, saa za Jeffersonville, ( Ni saa 1:00 MOJA JIONI ya Afrika Mashariki ), Wakati tai mwenye nguvu wa Mungu anapopaza sauti na kufunua Muhuri wa Nne 63-0321.

Ndugu. Joseph Branham

Maandiko ya kusoma ili kujitayarisha kusikia ujumbe wa Muhuri wa Nne 63-0321:

Mathayo Mt. sura ya 4 yote
Luka Mt. 24:49
Yohana Mt. 6:63
Matendo 2:38
Ufunuo 2:18-23, 6:7-8, 10:1-7, 12:13, 13:1-14, 16:12-16, 19:15-17
Mwanzo 1:1
Zaburi 16:8-11
2 Samweli 6:14
Yeremia sura 32 yote
Yoeli 2:28
Amosi 3:7
Malaki sura ya 4 yote