23-0820 Muhuri Wa Tano

UJUME: 63-0322 Muhuri Wa Tano

PDF

pakua – m4a

pakua – amr

BranhamTabernacle.org

Mpendwa Bibi-arusi Neno Mkamilifu,

Mungu ametuma nguvu yake ya mwisho. Amemleta tai Wake mkuu ili aturudishe kwenye ile Imani ya asili ya baba zetu. Huu ni wakati wa tai. Hakuna Wanyama wengine tena. Hakuna wajumbe wengine tena. Hakuna kundi lingine la watu tena. Wamekwisha. Tuko mwisho. Sauti ya Ufunuo 10:7 imewasili Naye amemtumia nabii-tai wake mkuu kumwita Bibi-arusi Wake atoke.

Kama ungalimsikiliza mchungaji wetu Jumapili, yule tai mkuu wa Mungu, ungemsikia akikuambia kama alivyotuambia sisi:

“ Ninyi ndilo kundi lile ambalo litakalozichukua hizo Ngurumo Saba; Neno la Mungu mwenyewe, na kukata vipande-vipande na kukata na hata kuzifunga mbingu. Mnaweza kufunga hiki, ama kufanya vile, lo lote mnalotaka kufanya. Adui anauawa kwa Neno litokalo katika kinywa chenu, kwa maana ni kali kuliko upanga wenye makali kuwili. Mnaweza kuagiza tani bilioni mia moja za inzi kama mkitaka. Lo lote mtakalosema, litatukia, kwa maana ni Neno la Mungu likitoka katika kinywa cha Mungu. Ni Neno Lake, lakini daima Yeye hutumia mwanadamu kulifanyiza kazi.”

Ninawezaje kusisitiza vya kutosha umuhimu wa Kubonyeza Play; kumsikia yule tai aliyetumwa na Mungu? Ujumbe huu ni muhimu sana, mkamilifu sana…MKAMILIFU SANA, hivi kwamba hata hangeweza kuuweka mikononi mwa Malaika. Hapakuwa na mtu mwingine, hapakuwa na kundi lingine la watu, HAKUNA MTU YE YOTE Yeye angaliweza kumpa Hilo, ILA NABII-TAI WAKE MKUU.

Tunaweza kuzungumza kulihusu, kulifundisha, na hata kulihubiri, lakini kuna SAUTI MOJA PEKEE iliyo na “Bwana Asema Hivi,” nawe huna budi kuamini kila Neno. Kuna Sauti moja tu unayoweza kuweka kikomo chako cha milele kwake. Kuna SAUTI MOJA tu ambayo Mungu aliyoichagua kumwongoza Bibi-arusi Wake, na NI BIBI-ARUSI WAKE PEKE YAKE NDIYE ATAKAYEKUWA NA UFUNUO HUO.

Kulikuwa na nabii-tai mmoja tu aliyemchagua kabla ya kuwekwa misingi ya ulimwengu kumfunulia NENO LAKE LOTE …WILLIAM MARRION BRANHAM, na yeye, na yeye peke yake, ndiye tai-mjumbe wa Mungu kwa ajili ya siku hii. Yeye, na yeye peke yake, ndiye aliyetumwa kumwongoza Bibi-arusi wa Mungu.

Wito wangu Mimi, ama wito wa wahudumu wo wote, ni jambo moja tu: KUWAONGOZENI NINYI KWAKE YEYE, YULE TAI MKUU WA MUNGU. Yule aliyemchagua. Yule aliyemthibitisha kwa Nguzo Yake ya Moto. Yule aliyemchagua wakati alipokifungua kile Kitabu, na kuivunja ile Mihuri, na kukituma duniani, ili akifunue kwetu sisi, Watu Wake.

Maneno hayo aliyosema kwenye kanda si maneno yake yeye, ni Mawazo hasa ya Mungu mwenyewe yaliyonenwa na kurekodiwa kwenye kanda ili Bibi-arusi Wake asikie; na ni WEWE tu, Bibi-arusi WAKE uliye na Ufunuo wa kweli wa jambo hilo.

Bibi-arusi, hebu fikiria jambo hilo! Tumewasili. Hakuna cha zaidi. Utafiti wa kisayansi umethibitisha jambo Hilo. Thibitisho la Neno limehakikisha jambo Hilo. Nasi tumewasili! Na Ufunuo huu unatoka kwa Mungu, nao ni Kweli. Na kwa sababu mnalitambua jambo Hilo, SISI NI wana na binti zake waliorejeshwa kikamilifu.

Hakuna kushangaa tena. Hakuna kujiuliza-uliza tena. SISI NI BIBI-ARUSI NENO WAKE MKAMILIFU. Tunajitambua sisi ni nani. Sisi ndio wale, kwa Neema ya Mungu, aliyomruhusu tai Wake kuwaona wote wakiwa wamevaa nguo ndefu nyeupe.

Jipe moyo Bibi-arusi. Tumekaribia. Tunaweza kuliihisi hilo. Ni halisi zaidi kwetu sasa kuliko hapo awali. Adui anatuchukia, LAKINI MUNGU ANATUPENDA. Si kwamba yeye yuko nasi tu, YUKO NDANI YETU. SISI NI NENO LAKE LILILOFANYIKA MWILI.

Yeye anamthibitishia Shetani, SISI HATUWEZI, NA HATUTASHINDWA. Kuna IMANI na shaka tu. Sisi tuna IMANI TU. Si katika sisi wenyewe, KATIKA NENO LAKE, NALO haliwezi kushindwa. Kwa nini? SISI NI NENO. Mungu alisema hivyo!!

Wewe hukumchagua Yeye, ALIKUCHAGUA WEWE. Shetani anawezaje kukufanyia lo lote, MUNGU ALIKUCHAGUA. Yeye alikuchagua wewe kwa sababu ALIJUA hungeshindwa kuamini Neno Lake. Shetani anakuambia, “lakini unashindwa, unashindwa, unashindwa”… uko sahihi, nashindwa katika mwili wangu, lakini NIMEHESABIWA HAKI, nami sitashindwa kuamini KILA NENO.

Tunapata kujaribiwa na kupitia mitihani kwa ajili ya MUNGU, ili apate KUMTHIBITISHIA, ADUI YAKE NA ADUI YETU… SISI NI BIBI-ARUSI NENO WAKE MKAMILIFU.

Roho Mtakatifu Mkuu na ajaze nyumba zenu, makanisa yenu, ama popote mlipo Jumapili hii saa 6:00 SITA MCHANA, saa za Jeffersonville,( ni saa 1:00 MOJA JIONI ya Afrika Mashariki) tunapomsikia tai mkuu wa Mungu akileta Ufunuo kwa:  Muhuri wa Tano 63-0322.

Ndugu. Joseph Branham

Maandiko ya kusoma kabla ya Kusikiliza Ujumbe:

Danieli 9:20-27
Matendo 15:13-14
Warumi 11:25-26
Ufunuo 6:9-11 / 11:7-8 / 22:8-9