23-0827 Muhuri Wa Sita

UJUME: 63-0323 Muhuri Wa Sita

PDF

pakua – m4a

pakua – amr

Wapendwa Watu wa Nabii Wa Mungu,

Sikilizeni, nina jambo fulani tu la kuwaambia. Ni zuri sana, linanichoma tu ndani kabisa moyoni mwangu. Ninatumaini hamjalisahau, mnaona. Hebu niseme jambo hili, mbele Zake. Kwa neema Yake, Yeye aliniruhusu pia kuwaona WATU WANGU, si muda mrefu uliopita, wakiwa katika mavazi meupe.

Kutoka Pwani ya Mashariki hadi ya Magharibi, kote nchini, tunakusanyika pamoja. Tuko umbali wa saa mengi, Bali tuko pamoja kama watu wa Nabii wa Mungu. Sisi ni JAMII MOJA.

Wakati nabii wa Mungu alipokuwa hapa duniani, mahali pekee palipo pakuu sana, na mahali ambapo Bibi-arusi alitaka kuwa, ilikuwa ni kuungana pamoja kwenye mawasiliano ya simu, wakingojea kusikia sauti hiyo ikisema, “Habari za Asubuhi Marafiki.”

Jinsi gani wangependa kukaa katika umati huo kwenye kona ya barabara ya Nane na Penn. Wangefurahia kutumia usiku kucha kwenye maegesho ili tu kupata kiti, ama kuweza kusimama na kuegemea ukutani kwa masaa. Wangeuza vyote walivyokuwa navyo, wangepoteza kazi zao, kama ingebidi ili tu kuwa katika ibada hiyo moja.

Maisha yao yote yalikuwa yakitegemea kila Neno ambalo nabii alilonena. Hawakutaka kukosa kitu. Ingawa walijua ya kwamba siku moja wangeweza kupata kanda hiyo, walitaka kuungana na Bibi-arusi wakati ule ule Mungu alipokuwa akinena kupitia midomo ya mwanadamu.

Haya ndiyo yalikuwa maisha yao. Hili ndilo walilongojea kila wiki. Hakuna kilichokuwa cha maana zaidi kwao ila kusikia Ujumbe unaofuata. Jinsi gani walivyojaa furaha kwa kujua, SASA, walikuwa na nafasi ya kusikia wao wenyewe, wote kwa wakati mmoja, Neno kwa Neno, yale ambayo nabii malaika-mjumbe wa Mungu aliyosema.

Mungu alikuwa ameandaa njia. Alitaka Bibi-arusi Wake aungane pamoja kwenye Sauti Yake. Alitaka Bibi-arusi Wake aisikie Sauti Yake wote kwa wakati mmoja. Alijua Sauti Yake iliyonenwa kupitia malaika-mjumbe Wake ndiyo Sauti pekee ambayo ingemuunganisha Bibi-arusi Wake.

Mpango wake mkuu ulikuwa ukitendeka.

Wachungaji kutoka kote Marekani walihakikisha kwamba makanisa yao yameunganishwa kwa njia ya simu. Walikuwa wamelipata lile ono ya kwamba HAKUNA KITU kilicho muhimu zaidi kuliko kusikia Sauti Hiyo.

Hivyo ndivyo walivyokuwa wamefundisha makusanyiko yao. “Mungu amemtuma nabii akiwa na Bwana Asema Hivi. Amethibitishwa na Nguzo ya Moto. Hii ni Sauti ya Mungu kwenu. Hii ni Malaki 4, na Ufunuo 10:7. Yeye ndiye mtu aliyeitwa na Mungu kumwongoza Bibi-arusi Wake. Huyu ndiye nabii yule niliyewaambia habari zake zote. Sasa hatuna budi sote kumsikiliza. Kama vile Yohana wa kale, sina budi kupungua na yeye ataongezeka.

Mpango wa Mungu ungali bado unatimizwa. Bibi-arusi angali bado anaungana kwenye Sauti Yake. Lakini sasa tunaungana KUTOKA ULIMWENGUNI KOTE. Kila Jumapili, sehemu ya Bibi-arusi Wake wanangojea kwa matarajio makubwa kusikia kila Neno, wote kwa wakati mmoja.

Labda tumeusikia Ujumbe mara mia moja hapo kabla, lakini wakati huu unajisikia kana kwamba ni MARA YA KWANZA. Tunajua tutapata Ufunuo MKUBWA kuliko hapo awali.

Hakuna mahali pengine tunapotaka kuwa. Hakuna kitu kingine kilicho muhimu zaidi. Kwetu sisi, Hili ​​ndilo Lile. Huu ni mpango wa Mungu KWETU. Sauti hii inaita, inaunganisha na kumkamilisha Bibi-arusi Wake…NA SISI NDIO HUYO BIBI-ARUSI.

Ninawaalika kuungana nasi Jumapili hii, saa 06:00 SITA MCHANA, saa za Jeffersonville,( ni saa MOJA JIONI ya Afrika Mashariki ) tunapoungana KUSIKIA Sauti ya Mungu Anapotufunulia:   Muhuri wa Sita 63-0323.

Ndugu. Joseph Branham

Maandiko ya kusoma kabla ya kusikia Ujumbe:

Kutoka 10:21-23
Isaya 13:6-11
Danieli 12:1-3
Mathayo 24:1-30
Mathayo 27:45
Yohana 10:27
Ufunuo 6 yote
Ufunuo 11:3-6