22-0306 Muhuri Wa Sita

Ujume: 63-0323 Muhuri Wa Sita

PDF

BranhamTabernacle.org

Wapendwa Kondoo wa Mungu,

Ni jambo gani kubwa zaidi liwezalo kuwa, tunaweza kuwa watu waliyotunukiwa zaidi vipi , kuliko kuwa na Mfalme wa wafalme , Bwana wa mabwana miongoni mwetu ?

Hebu fikiria jambo hilo. Uwepo wa Mfalme wa wafalme, Bwana wa mabwana uko pamoja nasi. Ametufunulia kuwa TUMEWASILI. Tumefika! Ufunuo aliotupa unatoka kwa Mungu. Ni kweli. Sisi ni Bibi-arusi Wake na Kondoo waliochaguliwa.

Tunasikia barua Zake za upendo kila wiki zikituambia: “Wana-Kondoo wangu wapendwa, nimefanya mwito Wangu wa kondoo. Mbuzi hawaujui, bali ninyi mmeutambua. Mmedumu waaminifu, kwa maana kondoo Wangu wananijua mimi na mgeni hawatamfuata. Haina budi kuwa ni ishara Yangu ya kiroho Sauti iliyothibitishwa PEKE YAKE .”

Hamkuchezeana kimahaba huko au hata kumtazama mwingine; mmedumu waaminifu kwa Sauti Yangu. Ninyi Ndio wale Nimekuwa nikingojea. Najua mmefanyiwa mzaha na kutoeleweka, lakini niliwaambia Mimi nitarudi kwa ajili yenu kama MTADUMU NA NENO LANGU, nanyi mmedumu nalo. SASA NAKUJA KWA AJILI YENU kama nilivyowahidi ningefanya. Neno ambalo mmekuwa mkilimwagilia maji linakuja kuwapeleka kwenye Makao Yetu Mapya.

Wengine wanaweza kutokuwa na ufunuo sisi tulio nao na kusema kuwa tunaonyesha heshima ya kibinadamu ; au kumwabudu mwanadamu na sio Bwana wetu. Wao ni vipofu jinsi gani . Ikiwa hiyo ni kweli, basi Bibi-arusi wa Kristo ng’ambo ya pazia la wakati pia walikuwa wamekosea.

Wakati Nabii alipomwona Bibi-arusi wakimkimbilia na kusema, “ndugu yetu mpendwa,” walimtwaa juu na kumketisha Mahali pa Juu . Nini…je BIBI-ARUSI wa Kristo alikuwa akionyesha heshima ya kibinadamu kwa nabii kwa kumweka Mahali pa Juu? Je Unasema hawakupaswa kufanya hivyo?

Kisha baada ya hayo, Bibi-arusi wote walikuwa wamesimama pale wakiwa wamevaa nguo zao ndefu nyeupe na kuanza kupaza Sauti, “Kama usingalijitokeza na Injili, tusingalikuwa hapa.” Kama yeye asingalijitokeza wasingalikuwa kule?

Ndipo Sauti kutoka juu ikasema tutahukumiwa kulingana na NENO alilotuhubiria, kisha atatukabidhi kwake.
Sauti haikusema kwamba tutahukumiwa kwa yale mtu fulani aliyosema au yale mtu fulani aliyofafanua kuwa alisema , bali yale Yeye aliyosema . Ndipo yeye atatukabidhi Kwake.

Naweza kuchukua nafasi hii kuzungumza kwa niaba ya sehemu ya Bibi-arusi walio na Ufunuo ule ule nilio nao, na niseme jinsi tunavyohisi. Kama tutahukumiwa kwa Neno hilo , na KIKOMO CHETU CHA MILELE kinategemea Neno ambalo Mungu alilonena kupitia nabii Wake, basi hatuna budi kulisikia PEKE YAKE Neno hilo kutoka kwenye Sauti ya Mungu kwa ajili ya wakati wetu. Hatuwezi, na hatutaweka kikomo chetu cha Milele juu ya yale mtu Fulani anafafanua, au kusema, bali yale ALIYOSEMA. TUNAWEZA KUSIKIA TU SAUTI YA MUNGU PEKE YAKE , na William Marrion Branham ndiye SAUTI PEKEE YA MUNGU…MUNGU ALISEMA HIVYO.

Niliwaudhi kwa kusema hivyo, samahani , lakini, nilihisi huenda nilakuchukiza, lakini, mimi ni Sauti ya Mungu kwenu .

Kwa hiyo tuna furaha na tunamshukuru Bwana kwamba tunafanya kama vile wale Bibi-arusi walivyokuwa wakifanya upande wa pili. Utukufu, Heshima na Sifa zote zinamwendea BWANA wetu MMOJA NA WA PEKEE YESU KRISTO. Kama vile nabii wa Ufunuo 22:9 alivyotuambia, mwabudu Mungu … TUNAFANYA HIVYO na kumpenda sana.

Muda umechelewa . Maandiko yanatimizwa haraka kuliko tunavyoweza kusoma yote yanayotendeka. Anakuja kwa ajili ya Bibi-arusi Wake upesi. Ulimwengu unaungana. Bibi-arusi anaungana. Jukwaa linaandaliwa kwa ajili ya Unyakuo.

Tunamsifu Bwana kwa ajili ya watu walioitwa na Mungu wanaohubiri Neno, Lakini wahudumu, wekeni Sauti hiyo nafasi ya Kwanza ambayo ninyi na watu wenu mtahukumiwa kwayo. Kusanyikeni katika makanisa yenu na msikie Sauti pekee ya Mungu iliyothibitishwa ikinena. Bonyeza Play.

Tunawaalika wote ambao wangetaka kuja ndani ya Safina na kuokolewa pamoja nasi tunapoungana na kusikia Sauti ya Mungu ikinena Maneno tutakayohukumiwa kwayo, saa 6:00 sita mchana , saa za Jeffersonville, ( ni saa 2:00 Mbili Usiku ya Tanzania) na kusikia Muhuri wa Sita 63-0323 .

Ni Chakula cha Kondoo kwa Kondoo wa Mungu. Hakuna kilichoongezwa, hakuna kilichoondolewa na hakuna kilichofafanuliwa, ni CHAKULA safi cha KONDOO kisichoghoshiwa.

Ndugu. Joseph Branham.

Kutoka 10:21-23
Isaya 13:6-11
Danieli 12:1-3
Mathayo 24:1-30
Mathayo 27:45
Yohana 10:27
Ufunuo sura ya 6 yote
Ufunuo 11:3-6