22-0227 Muhuri Wa Tano

Ujume: 63-0322 Muhuri Wa Tano

PDF

BranhamTabernacle.org

Mpendwa Mwili Mmoja Mkuu wa Kristo,

Ni nini kinachotukia leo? Neno la Mungu linatimizwa. Siku ambazo Bibi-arusi alizongojea kwa muda mrefu sasa zinadhihirishwa mbele ya macho yetu. Siku ambazo nabii wa Mungu alituonya zinakuja, sasa zimefika.

Muhuri unafunguliwa. Ni kitu gani hicho? Siri inafunguliwa. Mnaona? Na wakati siri inapofunuliwa, basi baragumu inalia. Inatangaza vita. Pigo linashuka, na wakati wa kanisa ukaanza .

. Urusi
. Vita
. Ukomunisti
. Mafuta
. Mapigo

Wakati Urusi inapoenda huko kupata mafuta hayo, jihadhari .

Urusi, ukomunisti hauteki cho chote! Neno la Mungu haliwezi kushindwa. Urumi utauteka ulimwengu .

Malaika wa maangamizi anaushikilia mkono wa Urusi, ulioshika mabomu ya atomiki ; mpaka Kanisa la Mungu litakapoungana pamoja, na Mwili mmoja mkuu wa Kristo . “ Siwezi kufanya neno lo lote hadi utakapoingia huku.” Loo, kama hilo si dhamana iliyobarikiwa !

Kanisa, Bibi-arusi Wake, anaungana pamoja kutoka ulimwenguni kote kama Mwili Mmoja Mkuu wa Kristo, wakimsikiliza Mungu akinena na kufunua Neno Lake. Tunaona Neno likitimizwa katika ulimwengu unaotuzunguka, lakini pia tunaona Neno likitimizwa na kudhihirishwa ndani yetu.

Tunapokea changamko kwa Ufunuo kuliko hapo awali wakati nabii hizi zinapotimizwa.

Dunia iko katika hofu na wasiwasi . Wanangojea, wanatazama na kushangaa, nini kitatokea baadaye? Kesho ina kitu gani?
Je, haya yote yanamaanisha nini? Je, Urusi itateka? Vipi kuhusu uchumi?

Wakati huohuo, Bibi-arusi yuko kwenye AMANI. TUNAPUMZIKA, tukiwa tumejazwa na Roho wake Mtakatifu, tukimsikiliza akinena kupitia malaika wake mkuu mwenye nguvu akituambia: Msiogope kitu chochote Enyi kundi langu dogo, ninyi ni Kipenzi wangu Waliochaguliwa . Ninyi ni:

Waliochaguliwa kabla ya kuwekwa misingi ya ulimwengu. Amina! Nao ni waaminifu kwa Neno. Amina! Whiu! Ninapenda jambo hilo. “Wanaitwa, waliochaguliwa, kabla ya kuwekwa misingi ya ulimwengu.” Na halafu, ni waaminifu kwa Neno, kwa uchaguzi wao, wote wamechangamshwa na divai mpya na Mafuta, wamepanda farasi tu moja kwa moja, wakishuka kuja kukabiliana na yeye. Wao wanajua zile Ngurumo zitatoa jambo hilo kwa ajili yetu, karibuni sana .

Anatambua kwamba sisi ni waaminifu kwa Neno lake. Tumefanya hivyo kwa uchaguzi wetu. Sasa tumepanda farasi tu moja kwa moja , tukijua zile Ngurumo zitatoa jambo hilo kwa ajili yetu karibuni sana, Naye atakuja na kutupeleka kwenye Makao yetu Mapya.

Kuna mengi zaidi anayotaka sisi tujue. Kitu fulani kinawaka tu moyoni mwake anataka kutuambia. Hawezi kusubiri zaidi kwani anajua itatupa Changamko. Kwa neema ya Mungu, alimruhusu nabii Wake atuone sisi, watu wake, kule ng’ambo ya pili pamoja naye. Akasema, “Nilipowaona ninyi nyote mlikuwa na NGUO NDEFU NYEUPE .”

Tulikuwa  tumekusanywa pamoja naye. Tulimchukua na kumketisha mahali pa juu kwenye kitu kikubwa na kirefu. Tulimwambia, “duniani, ulikuwa kiongozi wetu”.

Kulikuwa na mamilioni yetu sisi tukimkimbilia na kumkumbatia tukimwita “Ndugu”. Mara moja Sauti kutoka juu ilinena na kusema, “Watu hawa ni waongofu wako ambao umewaongoza. Utahukumiwa kwa yale uliyowaambia”.

Nabii alinena na kusema, “Kama kundi la Paulo likiingia, na langu pia , maana nimehubiri Neno lile lile kabisa.” Na sisi sote tukapaza Sauti WOTE MARA MOJA, KWA SAUTI MOJA:

” Tunategemea Jambo Hilo !”

Jina la Bwana lihimidiwe, tunategemea kila Neno alilonena kupitia nabii Wake. Tutahukumiwa kwa Neno hilo. Tulikuwa watu wa nabii. Alikuwa kiongozi wetu aliyetuongoza kwa Kristo. Sisi Sote tulikuwa na Nguo ndefu Nyeupe. Hatukutegemea kile mtu fulani alichosema ati Alisema , au kile mtu fulani alichosema inamaanisha , tulitegemea kila Neno Yeye alilosema.

Ni siku na wakati wa jinsi gani wa kuishi, Bibi-arusi. Ukisikia taarifa ya habari leo hii, utajua kilichotokea jana. Bonyeza Play, nawe utasikia kile kitakachotokea kesho, na siku inayofuata, na siku inayofuata, na siku inayofuata.

Njoo ukusanyike pamoja na Mwili Mmoja Mkuu Wa Kristo saa 6:00 Sita Mchana , saa za Jeffersonville, ( Ni saa 2:00 mbili Usiku ya Tanzania) Kusikia: Muhuri wa Tano 63-0322. Hakuna Kushangaa, hakuna kudhania , Bali ni KUJUA unasikia BWANA ASEMA HIVI kutoka kwenye Sauti ya Mungu kwa ajili ya wakati wetu.

Ndugu. Joseph Branham

Maandiko ya kusoma kabla ya kusikiliza Ujumbe:

Danieli 9:20-27

Matendo 15:13-14

Warumi 11:25-26

Ufunuo 6:9-11 / 11:7-8 / 22:8-9