Category Archives: Uncategorized

22-0206 Muhuri Wa Pili

Ujume: 63-0319 Muhuri Wa Pili

PDF

BranhamTabernacle.org

Mpendwa Tawi Jipya,

Kimetendeka; kile ambacho watakatifu wote walio tutangulia wamekuwa wakingojea. Ule Mti wa Asili sasa umetoa tawi jipya. Tumewasili. Sisi ndilo hilo Tawi Jipya. Roho Mtakatifu ameshuka, na Roho wa Mungu yuko juu yetu. Ile Imani ya Asili, ya Kipentekoste, ya kimitume imerejeshwa na malaika Wake wa 7. Sasa, nabii Wake anaenda nyumba kwa nyumba, akimega mkate pamoja nasi. Kuna ishara kuu, maajabu, na Ufunuo juu ya Ufunuo unaomwagwa juu yetu.

Tunaziweka taa zetu zikiwa zimetengenezwa na zimejaa Mafuta. Tunadumu na Neno la Asili, kama alivyotuambia tufanye. Wengine wanaweza kutaka Kanisa, lakini sisi HATUTAKI LOLOTE ILA SAUTI YA MUNGU YA ASILI.

Sasa, hebu wazia tu jambo hilo sasa. Hebu tuninii tu—tujaribu kuyaingiza yale tunayoamini kwamba Roho Mtakatifu angetutaka tujue .
Sasa kumbukeni , “ Hakuna lo lote linaloweza kufunuliwa; Mungu hatafanya neno lo lote, hata kidogo, mpaka kwanza alifunue kwa watumishi Wake, manabii.” Na kabla ya Yeye hajafanya neno lo lote, hulifunua .

Hakuna kinachoweza kufunuliwa kwa Bibi-arusi; ikiwa si na nabii Wake kwanza. Kama kuna siri zozote zitakazofunuliwa, ufunuo wowote mpya, cho chote tunachohitaji ili kuwa Bibi-arusi Wake na kunyakuliwa, Ni lazima kwanza umjie nabii ndipo YEYE atatufunulia jambo Hilo, Bibi-arusi Wake.

Kufunua nini? Siri ya Ngurumo Saba. Hilo lina maanisha nini? Inamaanisha moja ya mambo mawili. Labda tayari ipo kwenye kanda na itafunuliwa ufikapo wakati wake kufunuliwa kwetu.

Lakini nawazia, wakati siri hizo zinapoanza kufunuliwa, Mungu alisema, “Zifiche sasa. Ngoja kidogo. Nitazifunua katika siku hiyo. Usiziandike, hata kidogo, Yohana, maana zitawakwaza. Zi—ziache tu, unaona. Lakini nitazifunua katika siku ile ambayo kuna haja ya kuzijua .”

Ama, atamtuma nabii Wake kurudi duniani ili kututambulisha Kwake, ndipo nabii Wake atatufunulia siri ya zile Ngurumo Saba.

Na ndipo kunakuja Ngurumo saba za siri ambazo hata hazijaandikwa kamwe. Hiyo ni kweli. Nami naamini ya kwamba, kupitia Ngurumo hizo Saba, zitafunuliwa katika siku za mwisho ili kumkusanya Bibi-arusi pamoja kwa ajili ya kupata imani ya kunyakuliwa. Kwa sababu, ile tuliyo nayo sasa hivi, ha—hatungeweza kufanya jambo hilo. Kuna jambo fulani. Hatuna budi kupiga hatua mbele zaidi.

Haitakuwa ni kundi la watu ambao watakaofunua siri hiyo, Itakuwa ni Malaika-mjumbe Wake wa 7, William Marrion Branham. Hiyo si kwa sababu “MIMI ” nilisema hivyo; ni kwa sababu NENO LINASEMA HIVYO!!

“ Anachukua kile Kitabu na, cha Mihuri, na kuzivunja,” na kumwonyesha malaika wa saba ; kwa kuwa hii pekee, siri za Mungu, ndiyo huduma ya yule malaika wa saba .

Inasema yote hapo. Huduma ya Siri za Mungu si ya mwingine ila malaika wa saba. Zile Ngurumo Saba zitamkusanya Bibi-arusi pamoja na kutupa imani ya kunyakuliwa.
Ikiwa Ngurumo ndizo zitamkusanya Bibi-arusi pamoja, na siri ya Ngurumo haina budi kutoka kwa malaika wa 7, basi hakuna jambo la muhimu zaidi kwa Bibi-arusi kufanya kuliko KUBONYEZA PLAY . Hilo ndilo litakalomkusanya Bibi-arusi pamoja kwa ajili ya Unyakuo.

Dumu na Neno la Asili kwenye kanda. BONYEZA PLAY .

Na kanda zitafunua mengi Yake, wakati unajifunza .

Jina la Bwana libarikiwe! Utukufu kwa Mungu! Tunaipenda hisi hiyo tamu tunayopata kutokana na kusikia Sauti ya Mungu ikizungumza nasi kwenye kanda. Tunamsikia tu Roho Mtakatifu akifurika pande zote kutuzunguka tunapotembea Nayo. Tunaenda nayo nyumbani. Tunaishikilia kwenye mto wetu.

Njoo usikilize pamoja nasi Jumapili saa 6:00 Sita Mchana , saa za Jeffersonville, ( ni Saa 2:00 mbili Usiku ya Tanzania), Roho Mtakatifu anapokuja kwa uvumi majumbani mwetu na kutufunulia yote tunayohitaji, tunaposikia: Muhuri wa Pili 63-0319.

Ndugu. Joseph Branham

Maandiko ya kusoma kabla ya kusikiliza Ujumbe:

Mathayo Mtakatifu 4:8 / 11:25-26 / 24:6

Marko Mtakatifu 16:16

Yohana Mtakatifu 14:12

2 Wathesalonike 2:3

Waebrania 4:12

Ufunuo 2:6 / 6:3-4 / Sura ya 17 yote nzima / 19:11-16

Yoeli 2:25

Amosi 3:6-7

22-0130 Muhuri Wa Kwanza

Ujume: 63-0318 Muhuri Wa Kwanza

PDF

BranhamTabernacle.org

Mpendwa Malkia wa Mbinguni,

MIMI , Mfalme wenu, nitanguruma kwenu NINYI siku ya Jumapili na kuwaambia NINYI , NINYI ndiyo Bibi-arusi Wangu. Nimewachagua NINYI kimbele. nimewakomboa NINYI. Nimewahesabia haki NINYI na Niliyaweka majina yenu kwenye Kitabu changu cha Uzima cha Mwana-Kondoo kabla ya kuwekwa misingi ya ulimwengu. WEWE ni Malkia Wangu Kipenzi.

Nimewangojea na kuwangojea NINYI ili niweze kurejesha yote ambayo Adamu wangu wa kwanza alipoteza. Urithi wake wote ambao alipoteza. Ushirika wake wote na haki ya Uzima. Nilikuwa nimempa mamlaka makuu kamili juu ya dunia. Yeye Alikuwa mungu wa dunia nikiwa mimi ndiye Mungu wa ulimwengu wote.

Yeye alikuwa na mamlaka juu ya dunia hii. Angeweza kunena, aliweza kutoa majina, aliweza kusimamisha maumbile, aliweza kufanya lo lote alilotaka kufanya. Lakini alipoteza hayo Yote.

Sasa, kama nilivyokuahidi WEWE katika Neno Langu, Nimerudisha yote aliyopoteza na nimekurudishia WEWE. Yamekombolewa. Umilikaji halali wa yote yaliyopotezwa na Adamu sasa ni YAKO. Umilikaji wa halali wa hiyo hati-miliki ya kuwazika ya Uzima wa Milele, ambayo inamaanisha ya kwamba WEWE una kila kitu ambacho Adamu alikipoteza.

Nimekuwa aliye jamaa yako wa karibu. Nilidai kilicho Changu. Nilikitwaa kitabu cha ukombozi kutoka kwenye Mkono wa Baba Yangu, nikachana ile mihuri kutoka katika kitabu hicho na nikakituma kwa malaika-mjumbe wangu wa saba ili akufunulie WEWE. Atakurudishia WEWE Imani ya asili ya Biblia na atakufunulia WEWE siri Zangu zote.

Nimekuhakikishia na kukuthibitishia mambo haya kupitia Adamu Wangu wa kwanza aliyerejeshwa kikamilifu; Malaika wangu wa saba nabii-mjumbe. Angeweza kunena na kuwaumba kindi, kumrudishia samaki uhai , kudhibiti hali ya hewa na kuirudisha Tufani kule ilikotoka. Angeweza kunena na kuwafufua wafu. Hata nilipigwa picha YANGU pamoja naye ili kuonyesha ulimwengu, huyu ndiye Adamu Wangu wa kwanza aliyerejeshwa, msikieni yeye. Sasa WEWE, Malkia Wangu, una kila kitu ambacho Adamu alikipoteza.

Kumbuka, malaika-mjumbe wangu wa saba atakuwa duniani wakati wa Kuja Kwangu. Atakutambulisha KWANGU. Parapanda hiyo ya mwisho italia na waliokufa katika Kristo watafufuka. Wale walio hai na waliosalia watanyakuliwa pamoja nao, ili kunilaki hewani wakati ule ule malaika Wangu wa saba anapotoa Ujumbe wake. Muhuri wa mwisho unafunguliwa. Ile Parapanda ya mwisho italia; Nitakuja kudai mali yangu, WEWE, na ndipo nitakupeleka WEWE kwenye Karamu YETU ya Harusi.

Malkia wangu mpendwa, njoo unisikie Nikizungumza NAWE na kukufunulia kila kitu unachohitaji. Nimekuhifadhia WEWE Chakula hiki ili WEWE uwe Malkia Wangu. Nitazungumza na WEWE saa 6:00 Sita mchana, saa za Jeffersonville, ( ni Saa 2:00 Mbili Usiku Ya Tanzania), ambapo nitanguruma KWAKO Muhuri wa Kwanza 63-0318 .

Ndugu. Joseph Branham

Maandiko ya kusoma ili kujitayarisha kwa ajili ya kusikiliza Ujumbe:

Mathayo Mtakatifu10:1 / 11:1-14 / 24:6 / 28:19

Yohana Mtakatifu12:23-28

Matendo 2:38

2 Wathesalonike 2:3-12

Waebrania 4:12

Ufunuo 6:1-2 / 10:1-7 / 12: 7-9/ 13:16 / 19:11-16

Malaki Sura ya 3 yote na sura ya 4 yote

Danieli 8:23-25 ​​/ 11:21 / 9:25-27

22-0123 Pengo Kati Ya Nyakati Saba Za Kanisa Na Ile Mihuri Saba

Ujume: 63-0317e Pengo Kati Ya Nyakati Saba Za Kanisa Na Ile Mihuri Saba

PDF

BranhamTabernacle.org

Mpendwa Bibi-arusi anayepiga vifijo na kufurahi,

Tuko katika Neno na tuna wakati mkuu zaidi katika maisha yetu yote. Kufundisha, kujiweka wakfu, na ufunuo. Hakuna kitu muhimu zaidi kuliko kusikia Sauti ya Mungu kwenye kanda.

Ujumbe huu ni kila kitu kwetu sisi. Unatupa kuridhika kukamilifu. Kitu pekee kinachoweza kuzima kiu ya nafsi zetu ni kumsikia Mungu akisema nasi kupitia nabii wake.

Kila siku anatupa ufunuo zaidi wa Yeye Mwenyewe na sisi wenyewe. Uhakikisho wa kina zaidi kwamba, kwa “Kubonyeza Play,” tunasikia Neno Lake na tunafanya kama vile Yeye alivyotuamuru kufanya. Sisi ni kondoo wake, na kondoo hawezi kujiongoza mwenyewe; inabidi awe na kiongozi. Na Roho Mtakatifu anatuongoza Kwake, Sauti Yake inenayo Maneno ya kutoweza kukosea kwenye kanda.

Si kwa bahati kwa sisi kusikiliza Jumbe hizi pamoja, Yeye alituchagua sisi kufanya hivyo. “hatua za wenye haki huongozwa na Bwana.” Kuna sababu fulani. Hatuwezi kusaidia. Ujumbe kwenye kanda ndio tu Bibi-arusi anaotaka. Kwa kuusikia, inatupa mkono wenye nguvu wa Imani kushikilia na kuamini kila Neno.

Kwa nini tunaamini ni muhimu sana kwa wote wanaojiita “Bibi-arusi wa Mungu” kuzisikiliza kanda ?

Neno linatuambia wazi kwamba Biblia yenyewe iliandikwa na manabii. Hayakuwa mawazo yao, wala fikra zao, bali Roho Mtakatifu akiwasukuma kuandika Biblia. Biblia pia inatuambia kwamba Bwana Mungu hatafanya neno LOLOTE mpaka atakapolifunua Neno Lake kwa nabii Wake. Wengine wanaweza kunena Hilo na kulitangaza, lakini wanaweza kusema TU yale ambayo nabii wa Mungu amekwisha kusema.

Kama unaamini ya kwamba William Marrion Branham ni Malaika-mjumbe wa 7 aliyethibitishwa na Mungu, basi kile alichosema KWENYE KANDA si maneno yake, bali ni mawazo yenyewe hasa ya Mungu Mwenyewe yaliyotambulishwa. Unaweka Kikomo chako cha Milele kwenye kila Neno alilonena kwenye hizo kanda, kama unavyoamini hiyo kuwa ni BWANA ASEMA HIVI. Haiwezi kuongezwa kwake wala kuondolewa kutoka kwake, wala halihitaji kufasiriwa; Ni Mwana wa Adamu akizungumza kupitia kwa mtu aliyemchagua ili kutimiza Neno Lake.

Bibi-arusi wa kweli anajua umuhimu wa kuzisikiliza kanda. Kwetu sisi, kanda hizi ni kuu na huduma nyingine zote ni ndogo. Kila mtu lazima wajiulize kama kikomo chao cha Milele kinategemea kuamini kila Neno ambalo nabii wa Mungu alilonena. Kama ninaamini ni Sauti ya Mungu inayonena na kumwita Bibi-arusi Wake, basi hakuna kitu cha maana zaidi kuliko KUBONYEZA PLAY, kwani nitahukumiwa kwa kila Neno ambalo NABII WA MUNGU ALILOSEMA…si kwa lile mtu fulani alilosema kwamba nabii wa Mungu alisema.

Kama unaamini unahitaji zaidi ya hizi kanda , basi kwako huoni umuhimu kuweka msisitizo wa kuzisikiliza kanda, bali unaweka umuhimu zaidi kwenye huduma. Unaweza kuwa na mkuu mmoja tu.

Tutakaposikiliza kanda Jumapili hii, Mungu Mwenyewe atazungumza nasi na kutuambia tuna umiliki wa halali wa hati-miliki ya kuwazika ya Uzima wa Milele. Tuna kila kitu ambacho Adamu na Hawa walikipoteza. Kitaletwa kwetu katika ufunuo, na kutoka katika Mkono wa Mungu kwa kuthibitishwa.

Kisha atatuambia nini kiliendelea Mbinguni. Jinsi Yesu Mwenyewe alivyokitwaa kile Kitabu, akaichana muhuri, kisha akakipeleka kwa nabii aliyemchagua na akamwambia ampe Bibi-arusi Wake….Nena kuhusu vifijo !!!! Kila kitu duniani na Mbinguni kitatusikia tukipiga vifijo na kupiga vigelegele tunapoona majina yetu yameandikwa kwenye Kitabu cha Uzima cha Mwana-Kondoo.

Naye akakitwaa kile Kitabu, (utukufu!) akakifungua kile Kitabu, na kuichana ile Mihuri; na kukituma duniani, kwa malaika Wake wa saba, kukifunua kwa watu Wake! Haya basi. Loo! jamani! Ni kitu gani kilichotukia? Vigelegele, vifijo, zile haleluya, watiwa mafuta, nguvu, utukufu, dhihirisho!

Na maskini Yohana, aliyekuwa amesimama pale, ndugu yetu, akilia! “Mbona,” yeye akasema, “kila kitu Mbinguni, kila kitu duniani, na kila kitu chini ya bahari, vilinisikia nikisema kwa sauti kuu, ‘Amina! Amina! Baraka, heshima, na uweza, na nguvu, ziwe Kwake Yeye aishiye milele na milele.’”

Unaweza kuusikia wapi ufunuo huu mkuu? KWENYE KANDA TU. Kuna jambo la Kipekee kwa Bibi-arusi wanapomsikia Mungu Mwenyewe akisema kupitia midomo ya mwanadamu na kuwaambia, “WEWE NDIWE BIBI-ARUSI WANGU KIPENZI.”

Njoo uketi katika uwepo wa Roho Mtakatifu kwa Kubonyeza Play , Jumapili saa 6:00 sita Mchana, saa za Jeffersonville,( ni saa 2:00 Mbili Usiku ya Tanzania) tunaposikia Malaika-mjumbe Wake wa saba akileta: Pengo Kati ya Nyakati Saba za Kanisa Na Ile Mihuri Saba 63-0317E .
Tutakuwa tukipiga vifijo na kushangilia na kusema haleluya.

Ndugu. Joseph Branham

Maandiko ya kusoma kwa maandalizi ya kusikiliza Ujumbe:

Mambo ya Walawi: 25:47-55

Yeremia: 32:1-15

Zekaria: 3:8-9 / 4:10

Warumi: 8:22-23

Waefeso: 1:13-14 / 4:30

Ufunuo: 1:12-18 / Sura ya 5 yote / 10:1-7 / 11:18

22-0116 Mungu Akijificha Kwa Urahisi, Halafu Akijifunua Kwa Jinsi Hiyo

Ujume: 63-0317M Mungu Akijificha Kwa Urahisi, Halafu Akijifunua Kwa Jinsi Hiyo

PDF

pakua – m4a

pakua – amr

BranhamTabernacle.org

Mpendwa Kundi dogo la Eliya ,

 Sisi ni watu wateule, wakipekee na wasio wa kawaida  kwa ulimwengu, na kwa waaminio wengi, lakini hata hivyo, sisi ni ukuhani wa kiroho, taifa la kifalme, tukimtolea Mungu dhabihu za kiroho, pamoja na matunda ya midomo yetu tukilisifu Jina Lake.  Tunataka kuuambia ulimwengu kwamba tuna furaha sana, tunashukuru sana, na kuheshimika sana kuwa Wamoja Wao.

 Tumeuza lulu zetu nyingine zote, Yeye alipotupa Lulu ya thamani kuu, Ufunuo Wa Yeye Mwenyewe.  Tunaona Neno lenyewe la Mungu likidhihirishwa.  Ahadi ile ile ya siku za mwisho, Nuru za jioni zile zile ambazo zingeangaza.

 Imefunuliwa kilindi kabisa mioyoni mwetu kwamba Sauti tunayoisikia kwenye kanda ni Mwana wa Adamu akijifunua Mwenyewe.  Sauti hiyo ilituambia: Kaeni hapa, Angalieni Chakula Hiki kilichohifadhiwa ambacho nimewawekea kwenye hizo kanda.  Ikiwa una maswali yoyote, Rudi kwenye kanda hizi.  Inaweza hata kukushangaza kidogo, lakini cheza tena kanda na usikilize kwa makini.  Kama wewe ni Bibi-arusi, Roho Mtakatifu atakufunulia jambo Hilo.  Kumbuka, kanda hazihitaji kufasiriwa kokote, sema tu kile kilicho kwenye hizo kanda.  Mimi ni mchungaji wenu na ninyi ni kundi langu dogo, Dumuni na mafundisho ya kanda.

 Najua wengi sana hawaelewi tunachofanya kwa kusikiliza Ujumbe uleule wote kwa wakati mmoja, lakini ni sawa, bado ni ndugu na dada zetu nasi tunawapenda na hatupaswi kamwe kusema dhidi yao.  Kila Mtu lazima afanye kama wanavyohisi wanaongozwa Na Bwana kufanya.  Mungu hufanya kazi na kutuongoza kama watu binafsi.

 Nabii alituambia lazima tuchunguze kila kitu kwa Neno, na kukithibitisha kwa Neno, kama tu alivyofanya.  Neno la wakati huu, Ni na daima imekuwa, Biblia.  Biblia inatuambia katika siku za mwisho angefunua kikamilifu siri na mafumbo yote katika Biblia yake kwa nabii ambaye atamtuma.  Yeye Mwenyewe angenena kupitia nabii huyu na kujidhihirisha Mwenyewe katika mwili kama alivyofanya kwa Ibrahimu.  Neno Lake lisingekuwa maneno ya mwanadamu, bali  Maneno yenyewe ya Mungu Mwenyewe.  Ingekuwa BWANA ASEMA HIVI, kwa hiyo Biblia na Sauti hiyo zingekuwa kitu kimoja na sawa.

 Kuna Kilindi  kikiita kilindi  ndani ya mioyo yetu kusikia hiyo Sauti iliyothibitishwa.  Tunataka kusikia Sauti ya Mungu moja kwa moja kutoka kwa nabii Wake Aliyechaguliwa.  Kuna upendo kama huu mioyoni mwetu kusikia Sauti hiyo na kustarehe tu tukijua hatuhitaji kuhoji chochote tunachosikia, inabidi tu kuamini KILA NENO.

 Hakuna mahali pengine ambapo tunaweza kufanya hivyo.  Sio kwamba mtu fulani angetuambia jambo lisilo  sahihi au kutupotosha, kwa vile wao pia wana Roho Mtakatifu, Lakini tunajua kwamba wanaweza kutuambia jambo Lisilo Sahihi bila kupenda.  Lakini tunaposikia Sauti ya Mungu iliyothibitishwa kwenye kanda, hata kama hatuelewi kinachosemwa, Baba Mungu alisema inatupasa tu kusema AMINA, TUNAAMINI KILA NENO.  Hatuwezi kufanya hivyo kwa sauti nyingine yoyote.

 Tuliamriwa na Sauti hiyo pia:

 Msinisikilize mimi , bali sikilizeni kile nilichosema. Nilichosema ni ujumbe . Msimjali mjumbe kamwe; angalieni ujumbe. Kazeni macho yenu, si juu ya mjumbe, lakini juu ya ujumbe—kile ulichosema . Hilo ndilo jambo la kuangalia `“ .

 Alichosema NI Ujumbe wa wakati huu.  Tunapaswa kukaza macho yetu juu ya Ujumbe;  Ndilo jambo la kuangalia .

 Anatufunulia mambo kuliko hapo awali.  Kila Ujumbe tunaosikia unasikika kama Ujumbe mpya ambao hatujawahi kamwe kuusikia.  Ingawa tumezisikia mara mamia hapo awali, hatuwezi kueleza, ni kama tunausikia kwa mara ya kwanza naye anatupa Ufunuo zaidi na zaidi.

 Hatuwezi tu kuwazia mtu yeyote Asitake kusikia Jumbe hizi pamoja nasi.  Kuna muungano kama huo na Umoja pamoja na Bibi-arusi na Neno Lake.  Tumeridhika kabisa zaidi ya wakati mwingine maishani mwetu.

 Kwa mara nyingine tena tuko chini ya matarajio makubwa.  Ni kana kwamba Mihuri inafunguliwa sasa hivi.  Anaenda kutuonyesha mambo ambayo hatujawahi kamwe kuyaona hapo awali na kuleta Nuru kwa mambo ambayo tumesikia mara nyingi ,nyingi sana hapo awali;  lakini sasa, tutaliona waziwazi.

 Tunajua ya kwamba kila kitu tunachohitaji kwa ajili ya Unyakuo Wake ujao hivi karibuni, ni ile Sauti kwenye hizo kanda.

 Mungu alimtuma nabii Wake kwa ono upande wa nyuma wa jangwa huko Arizona ambako alitwaliwa juu na malaika saba, kisha akarudishwa Jeffersonville kufunua siri zilizofichwa za ile Mihuri Saba kwa Bibi-arusi.

 Njoo usikilize pamoja nasi Mungu anapozungumza nasi mdomo kwa sikio Jumapili hii saa 4:00 nne Asubuhi., saa za Jeffersonville,( ni saa 12:00 kumi na mbili jioni ya Tanzania),  nasi tutasikia: Mungu Akijificha  Kwa Urahisi, Halafu Akijifunua Kwa Jinsi  Hiyo 63-0317M .

 Tutauanza Ujumbe huu kwenye aya ya #94, baada ya ibada ya kuweka wakfu.

 Ndugu.  Joseph Branham

 1 Mambo ya Nyakati 17:1-8

 Isaya 35:8 / 40:1-5 / 53:1

 Malaki Sura ya 3 yote

 Mathayo Mtakatifu 11:10, 11:25-26

 Yohana Mtakatifu 14:1-6

 1 Wakorintho Sura ya 13 yote

 Ufunuo Sura ya 21 yote

22-0109 Hii Ndiyo Ishara Ya Mwisho, Bwana?

Ujume: 62-1230E Hii Ndiyo Ishara Ya Mwisho, Bwana?

PDF

pakua – m4a

pakua – amr

BranhamTabernacle.org

Mpendwa Hekalu la Mungu,

 Ujumbe huu hauna kikomo katika nguvu. Wenyewe Ni Mkamilifu ndani yake.  Ni Neno la mwisho juu ya mambo yote.  Hakuna kitu kingine kwa Bibi-arusi ila ile Sauti ambayo imerekodiwa kwenye kanda.  Ni Ujumbe wa Mungu uliothibitishwa wa wakati huu.  Ni Yakini yetu.

 Tuko safarini mwetu kuelekea Nchi ya Ahadi, tukiongozwa na Roho Mtakatifu, Nguzo ya Moto.  Chakula chetu cha Kiroho kimehifadhiwa ili kutuhifadhi  katika safari yetu.  Yote tunayohitaji yametolewa.

 Daudi alitayarisha kwa wingi kabla ya kifo chake vitu vyote vilivyohitajika ili kujenga nyumba ya Bwana .  Aliamuru kwamba lazima iwe ya ukuu kupindukia, ya umaarufu, na ya utukufu, katika nchi zote.

 Kisha akazungumza na Sulemani, na kumpa yote ambayo alikuwa ametayarisha kwa ajili ya ujenzi wa Hekalu la Bwana.  Akampa mfano wa ukumbi, na nyumba zake, wa hazina, na vyumba vya juu, na vyumba vya ndani, na mahali pa kiti cha rehema.

 Akampa kielelezo cha vyote alivyokuwa navyo kwa roho, vya nyua za nyumba ya Bwana.  Vyumba vyote vilivyozunguka pande zote, hazina za nyumba ya Mungu, na hazina za vitu vilivyowekwa wakfu.

 zamu za makuhani na Walawi, na kwa ajili ya kazi yote ya utumishi wa nyumba ya Bwana.  Pia akampa vyombo vyote vya utumishi katika nyumba ya Bwana .  Dhahabu na fedha kwa vyombo vyote vya huduma za kila namna.  Uzani wa dhahabu na fedha kwa kila kinara.  dhahabu na fedha kwa kila meza ya mikate ya wonyesho, ndoana, mabakuli, vikombe na mabakuli.

 kwa ajili ya madhabahu ya uvumba, dhahabu safi kwa uzani;  na dhahabu kwa mfano wa gari la makerubi, walionyosha mabawa yao, na kulifunika sanduku la agano la BWANA.

 Yote yalikuwa yametayarishwa na kuhifadhiwa kwa ajili ya jengo hilo.  Hakukuwa na chochote kilichopungua.  Ni lazima afuate Ramani kwa usahihi  kulijenga Hekalu la Bwana.

 Lakini katika wakati wetu, Mungu anajenga Hekalu lingine, Bibi-arusi Wake.  Hekalu hili halitaharibiwa, bali litaishi Milele pamoja Naye.  Ametayarisha na kuhifadhi kwa wingi kwa kila kitu kinachohitajika ili kujenga Hekalu Lake jipya.

 Uungu, Uzao wa Nyoka, Majuma Sabini ya Danieli, Nyakati Saba za Kanisa, Mihuri Saba, Kutambua Siku Yako, Ndoa na Talaka, Kufunuliwa Kwa Mungu, Ile Ishara, Yakini, Watiwa-Mafuta, Chakula cha Kiroho, Kristo ni Siri, na mamia na mamia zaidi .  ambazo lazima zifuatwe kwa usahihi .

 Amehifadhi kila kitu tunachohitaji, lakini ni lazima tufuate Ramani kwa usahihi, bila kubadilisha yodi moja au nukta moja.

 Sasa, huku ni, jambo ninalonena asubuhi hii, ni kuhifadhi Chakula, kuhifadhi Chakula, ili kwamba mpate kitu cha kula, ili kwamba mpate kitu cha kufanyia karamu. Kiwekeni Hicho kwenye kanda zenu; mkaziweke katika chumba chenye baridi. Pengine wakati mrefu baada ya kuondoka kwangu, mngali mtakumbuka mambo haya ni kweli. Ketini chumbani mwenu mkazisikize. Mnaona? Na hiki ni Chakula, kihifadhini Hicho katika ghala.

 Alisema katika maskani huhisi kama nyumbani kwake kuliko mahali pengine popote.  Palikuwa ni Mahali ambapo Chakula kilihifadhiwa.

 Kule nje kwenye mikutano ninakoenda, hamnisikii nikihubiri Jumbe hizi. La, niliwaahidi, kuja kwenye Maskani hii. Papa hapa ndipo mimi huhubiria jumbe zangu. Nina tatu ama nne zaidi hapa, ambazo Bwana amenipa mimi, nina Maandiko juu yake, ambayo nisingethubutu kuhubiri mahali pengine po pote ila papa hapa. Hapa ndipo Neno la Mungu lilipoanzia. Na, hata Mungu atakapolibadili, ninakaa papa hapa na kuutoa papa hapa. Hiyo ni kweli.

 Nabii wa Bwana alinena na kusema kulikuwa na kundi la watu wanaomwamini, na walio na njaa na kushikilia kila neno alilosema. Ninyi ndilo kundi hilo la watu. Ninyi ndilo kusanyiko lake.  Ninyi ndilo hilo kundi lake dogo.

 Nimekuwa katika maombi na kuhisi Bwana anatuongoza kufuata Jumbe alizoziweka kwa wingi nabii Wake katika ghala Lake ili kumjenga Bibi-arusi Wake.

 Tutaendelea kumfuata nabii Wake tunaposikiliza:  Hii ​​Ndiyo Ishara ya Mwisho, Bwana?  62-1230E .  Ningependa kukualika uungane nasi Jumapili saa 4:00 nne Asubuhi ., saa za Jeffersonville,( ni saa 12:00 kumi na mbili jioni ya Tanzania), kusikia Chakula hiki kilichotayarishwa na kuhifadhiwa maalum ambacho kitakujenga ndani ya Hekalu la Bwana.

  “ Wakati umekwisha .” Kama ndivyo ilivyo, hebu na tujiandae, marafiki, kumlaki Mungu wetu. Kumekwisha wekwa chakula kingi sana sasa; hebu na tukitumie. Hebu na tukitumie sasa.

 Ndugu.  Joseph Branham

22-0102 Yakini

Ujume: 62-1230m Yakini

PDF

pakua

BranhamTabernacle.org

Mpendwa Bibi arusi wa Ujumbe wa Mtu Mmoja,

 Huu Umekuwa mwaka Mkuu jinsi gani kwa Bibi-arusi.  Ametuunganisha kutoka ulimwenguni kote kwa kitu pekee kinachoweza kuleta Bibi-arusi Wake pamoja, Ujumbe wa wakati huu, Sauti yenyewe ya Mungu ikimwita Bibi-arusi Wake atoke .

 Na sasa, naamini uko tayari kugonga kilele kile cha mwisho kule kuleta imani ambayo italinyakua Kanisa hata Utukufuni; na lipo katika hizo Jumbe!

 Ufunuo wa Ujumbe huu sasa umetia nanga ndani kabisa ya mioyo yetu.  Matendo yetu yanaambatana kabisa na Neno.  Tunajua fundisho letu ni kamilifu na Neno, haliongezi chochote Kwake wala kuondoa lolote Kwake.  Kwetu sisi, si kingine ila Neno kwenye kanda.

 Amekuwa akitutayarisha kwa ajili ya kilele cha mwisho kwa kutupa Imani tunayohitaji kwa ajili ya Unyakuo.  Imani hiyo, iko ndani yetu SASA.  Uhai wa Kristo umezalishwa karibu katika njia ya kufanyika mwili, kupitia sisi, kama ilivyokuwa ndani ya Kristo.

 Tunaweza kuona maisha yake.  “Kazi nizifanyazo mimi nanyi mtazifanya, yeye aaminiye.”  Si yeye ajifanyaye anaamini, si yeye ajidhaniaye kuwa anaamini, bali, “Yeye aaminiye.”  “Yeye aniaminiye Mimi, kazi nizifanyazo Mimi yeye naye atazifanya.”  Kwa nini?  Ametiwa nanga kwenye Mwamba uleule.  Mwamba ulikuwa nini?  Neno, daima.  Umetiwa nanga hapo.  Ni Nyota yako ya kaskazini unapopotea baharini .

 Tumetia nanga sana kwenye Mwamba huo.  Tuna hakika nalo.  Tumeyakinika nalo.  Hatuchukui Neno la mtu mwingine, tunadumu na Bwana Asema hivi.  Tumekuja kwenye Yakini Yetu.

 Tumeridhika kabisa na tumetosheka. Hakuna kushangaa tena kama ilivyokuwa katika siku za Waamuzi, na kwa walio wengi sana leo, ambapo kila mtu alifanya lililo sawa machoni pake mwenyewe, ambapo kila mtu alikuwa na yakini yake mwenyewe na kufanya yale tu aliyotaka kufanya.  Mungu habadilishi kanuni zake, hawezi na awe Mungu.  Ikiwa Mungu atawahi kusema lolote au kufanya jambo lolote, ni lazima afanye vivyo hivyo kila wakati.

 Mungu daima hutuma nabii kuwaongoza watu wake.  Alitutumia Nabii Wake malaika wa 7 ;  Mwana wa Adamu akijifunua Mwenyewe katika mwili wa mwanadamu, kumwita Bibi-arusi Wake atoke na kumwongoza .  Kanda ni Sauti ya Mungu kwa Bibi-arusi Wake.  HIYO NDIO YAKINI YETU.

 Akapanda akaenda kule…Alijua…Nami napenda hilo, jinsi alivyokuja; alifikia kwenye yakini yake, nguzo yake ya kujishikilia.

 Mungu anamwita Bibi-arusi Wake pamoja. Yeye Hatabadilisha mpango Wake. Yeye Hatatuma kundi la watu kumkusanya Bibi-arusi Wake.  Bibi-arusi Wake ataungana tu kwenye Neno safi, hiyo ni Sauti ya Mungu kwenye hizo Kanda.  Ni huduma ya kweli ya Mungu kwa ajili  ya siku hii .

Hakuna njia bora ya kuanza Mwaka Mpya kuliko kukusanyika pamoja na kusikia nguzo yetu yakushikilia , Yakini yetu, ikizungumza nasi. Ningependa kuwaalika kila mmoja kuja kusikiliza pamoja nasi Jumapili saa 4:00 nne Asubuhi ., saa za Jeffersonville,( ni Saa kumi na mbili jioni ya Tanzania), ili kusikia Ujumbe: Yakini 62-1230M.

 Kama hamwezi kuungana nasi, ninawatia moyo kuchagua Ujumbe wa kucheza katika nyumba zenu, au mtie moyo mchungaji wenu kuchagua Ujumbe ambao ninyi pia mnaweza kuketi  pamoja, chini ya upako huu mkuu uliopo, na kusikia yakini ya Bibi-arusi iliyothibitishwa.

 Ndugu.  Joseph Branham

21-1226 Kwa Nini Bethlehemu Mdogo

Ujume: 63-1214 Kwa Nini Bethlehemu Mdogo

PDF

pakua

BranhamTabernacle.org

Wapendwa darasa,

Ningependa kuwahubiria na kuwafundisha leo kwa njia ya barua yangu. Hebu kwanza tupitie yale tuliyojifunza Jumapili iliyopita.

Je, unawezaje kuupata ule uzao wa Mungu uliochaguliwa tangu zamani? BONYEZA PLAY .

Yoshua aliwaambia wahudumu wake wafanye nini? Ingieni Yeriko, wahudumieni watu kwa KUBONYEZA PLAY, na yako na nyumba yako itaokolewa.

Wajumbe wake walirudi, wakasema, “Nimezitii amri zako. Nasi tulimpata mwanamke kule, tulipozicheza kanda.

Hatuonei haya. Hatujali ni nani anayeiona. Tulitaka kila mtu aione na kuisikia. Tumeiweka majumbani mwetu, katika makanisa yetu, kila mahali tunapoenda, ili kila mtu anayepita ajue ya kwamba tunatambulishwa na Ishara yetu; Yesu Kristo, Neno Lake, Roho Mtakatifu, Ujumbe wa saa hii, hizi Kanda, Sauti ya Mungu.

Tunaweza kuona ya kwamba hasira iko tayari kupitia juu ya uso wa nchi, na cho chote kisicho chini ya hiyo Ishara kitaangamia.
Bali atakapoiona Ishara, atapita juu yetu. Ndiyo masharti ya Mungu ya wakati huu. Ujumbe wa wakati wa jioni, ni kupaka Ishara.

Je, darasa alituambia ingefanana sana kiasi gani?

. Kusema tu ninaamini… hakutoshi.

. Kutembea mahali ilipo… hakutoshi, inakufanya kuwa mbaya zaidi.

. Siibi.

. Ninauzuria kwenye Maskani ya Branham.

. NAAMINI UJUMBE.

. NINAAMINI KILA NENO ULILOSEMA NDUGU BRANHAM…WOW !!!

Hilo ni sawa, bali hiyo ni uwezo tu wa kusoma

Usifikie tu umbali huu, ukasema, “Naamini Ujumbe.” Tii Mjumbe! Ingia katika Kristo!
Chukua Ujumbe, uingize moyoni mwako, ya kwamba huna budi kupata ile Ishara, Uhai ule ule uliokuwemo katika Kristo uwe ndani yako. “Nitakapoiona hiyo, nitapita juu yenu.”

Mungu amekuwa akimwambia nini Bibi-arusi wake Ujumbe baada ya Ujumbe? KANDA , KANDA, KANDA. kuhubiri Ujumbe na kufundisha Ujumbe ni sawa, lakini ni lazima UCHEZE UJUMBE.

Je, mtu anawezaje kusema anaupenda Ujumbe na hataki kuucheza Ujumbe mbele ya watu? Hawana uhusiano wa upendo ule nilio nao kwa ujumbe huu, kama ni pendavyo kila mmoja kuja pamoja na kusikia hilo likithibitishwa na sauti ya Nguzo ya Moto.

Tuna IMANI isiyotikisika katika Neno lake. Sisi sio Hawa. Sisi sio mabwana mashaka au kuridhiana na Shetani. Tunashikilia kila Neno la Mungu katika Biblia, na kila Neno kwenye Kanda. Kwa maana hizi kanda ni hasa mawazo yenyewe ya Mungu, yaliyonenwa na kufunuliwa kwa Bibi-arusi Wake, na haihitaji kufasiriwa kokote. Ndipo mahali pekee tunajuapo tunapoweza kusema AMINA kwa kila Neno.

Ujumbe huu ni mkate mpya unaoshuka kutoka Mbinguni, kwa ajili ya safari yetu. Ni Mkate wa Uzima, na kila siku tunapokea upya kutoka kwa Kristo, kutoka Mbinguni, Roho Mtakatifu, akija na kujaza nafsi zetu.

Tumeketi pamoja tukiwa na lengo moja, Neno la Mungu, nasi tunakula Neno Hilo. Tuko katika Bethlehemu ya kiroho ya Mungu, tukila Mkate wa kiroho wa Mungu, na nafsi zetu zinaitikia kila Neno alilosema, kwa “Amina!” Tunafurahia Chakula hiki cha malaika wa Mbinguni ambacho kimehifadhiwa kwa ajili yetu ili tukile.

Njoo uungane nasi Mezani Pake na kula pamoja nasi kile chakula cha malaika wa Mbinguni Jumapili hii saa 4:00 nne Asubuhi ., saa za Jeffersonville.( ni saa 12:00 Kumi na mbili jioni ya Tanzania).

Kama nyinyi watu wa kanda hapa, mnaosikiliza kanda, ningewatakeni msikilize huo: Ni Kwa Nini Ilibidi Yesu Kuja Bethlehemu. Ni kwa nini ilimbidi kufanya hivyo?

Baba amekwishanena nasi kupitia nabii Wake kwa mara nyingine tena na kuwaalika ninyi nyote Watu wa kanda kuja kusikiliza Ujumbe: Kwa nini Bethlehemu Mdogo 63-1214.

Mahubiri yangu na kufundisha kwangu sasa kumekwisha, sasa hebu na TUBONYEZE PLAY .

Ndugu. Joseph Branham

21-1219 Ile Ishara

UJUMBE: 63-0901M Ile Ishara

PDF

BranhamTabernacle.org

Mpendwa Bibi-arusi wa Ishara,

Haijawahi kutokea wakati kama huu hapo awali katika historia ya ulimwengu. Ulimwengu wote ulilazimika kushuhudia jambo hilo, kwani sayari tano zilijipanga zenyewe pamoja. Kuna jambo lililokuwa likitukia mnamo Desemba 12, 2021 katika mbingu, huku jambo fulani likiendelea duniani. Bibi-arusi waliungana wenyewe pamoja kutoka ulimwenguni kote kama vile Mungu alivyonena kupitia kwa nabii Wake, na Bibi-arusi Wake alikuwa na Ushirika na Kutawazana Miguu kwa pamoja katika nyumba zao.

Ni hali na uwepo wa Bwana ulioje uliokuwa ndani ya nyumba zetu. Baadhi ya vijana wa kanda waliingia ndani ya nyumba zetu nasi tukaifanya nyumba yetu kuwa kanisa la Bwana. Tuliweka Ishara kwa nyumba zetu na kwa familia zetu. Roho Mtakatifu aliijaza nyumba yetu, mioyo yetu, na nafsi zetu kwa uwepo wake. Ilikuwa kana kwamba sisi ni wana wa Israeli tukijiandaa kwa safari yetu ya kutoka.

Neno lilikuwa likisema nasi kupitia malaika wake na lilitumika kwenye nyumba zetu. Mauti ilikuwa imetuzunguka, lakini tulijua tulikuwa salama na ingepita juu ya nyumba zetu. Tulikuwa tunajiandaa kuondoka kuelekea Nchi YETU ya Ahadi.

Hatujawahi kamwe kuhisi ukaribu kama tulivyohisi usiku ule. Tulijua jambo fulani Lilikuwa likitendeka. Tulijua alikuwa anatutayarisha kwa ajili ya Kuja Kwake, lakini ilibidi iwe wakati huu, siku hii, mwezi huu, mwaka huu. Kila kitu kilikuwa kikamilifu na mahali pake. Ilikuwa na maana. Ilikuwa inatokea kama ishara kwa ulimwengu.

Kila tukio la kiroho ni ishara kutoka kwa Mungu. Iweni waangalifu. Tazameni hilo, mnaona. Tazameni, kila tukio la kiroho, kila kitu kinachotendeka, ni ishara. Hatuko hapa kwa bahati. Mambo haya hayatendeki kwa bahati. Ni ishara. Ni ishara, kuingia—ingieni mahali pa salama, upesi. Nuhu alikuwa ishara kwa kizazi chake; Elija alikuwa ishara kwa chake; Yohana alikuwa ishara kwa chake. Mnaona? Kila kitu, Ujumbe wa wakati huu, ni ishara. Uchunguze, tazama unachofanya. Unaona? Ni ishara. Kila kitu kina maana yake.

Musa alipoanza huduma yake katika Israeli, kwa ishara kuu, waona, Israeli walikusanyika upesi toka kila sehemu ya Misri kuenda Gosheni, wakirudi nyumbani kwao, kwa maana walijua kitu fulani kilikuwa karibu kutukia. Lo, ni mfano jinsi gani!

Ni mfano mkamilifu jinsi gani leo hii, Bibi-arusi anapokusanyika kwenye Neno safi lisiloghoshiwa la wakati huu; kwa sababu sisi pia tunajua, kuna jambo linakaribia kutukia.

wanakuja kutoka Mashariki na Magharibi, Wanatoka nchi za mbali; Kula karamu pamoja na Mfalme, kula kama wageni Wake, kwenye Chakula Chake Kilichohifadhiwa MEZANI PAKE.

Alimtuma malaika Wake nabii akiwa na Ujumbe kumwita atoke na kumwongoza Bibi-arusi Wake kwenye Nchi ya Ahadi. Amejitambulisha Mwenyewe miongoni mwetu kwa Nguzo ya Moto. Kisha, Yeye ametuma Ishara Yake ili Bibi-arusi Wake akae chini ya hiyo, kwa maana Yeye anaitambua Ishara hiyo Pekee.

Ishara ni nini leo hii?

Yeye hutambua tu I—Ishara. Huo ndio Ujumbe wa wakati huu! Huo ndio Ujumbe wa siku hizi! Huo ndio Ujumbe wa wakati huu! Katika Jina la Yesu Kristo, upokeeni !

Bibi-arusi na Kristo wanakuwa Mmoja. Huduma ya Bibi-arusi, na huduma ya Kristo, ni sawa. Mungu Mwenyewe Anatambua Ujumbe wa mjumbe Wake. Amemtambua Bibi-arusi Wake. Hasi inakuwa chanya. Kila ahadi katika Neno Lake ni YETU. Ni lazima itutii.

Tunakuwa Bibi-arusi Neno mkamilifu kwa njia iliyoandaliwa na Mungu kwa siku ya leo: Sauti Yake, Neno Lake, kwenye Kanda. Mungu kamwe habadilishi mpango Wake. Daima amemtuma nabii kuwaongoza watu wake. Alikuwa na wengine walioitwa na kutiwa mafuta, bali wao wangeweza kusema TU yale nabii aliyosema, kwa maana Maneno yake yalikuwa BWANA ASEMA HIVI kwa watu.

Unawezaje kuwa na UHAKIKA asilimia 100% kwamba unalosikia ni Neno KAMILIFU la Mungu? Kuna njia moja tu kwangu mimi: Bonyeza Play.

Hakika kuna wengine ambao wameitwa kuhubiri Neno, kwa maana limo ndani ya Neno na haliwezi kupingwa, lakini wanaweza tu kuhubiri Neno ambalo wamesikia kwenye Kanda kutoka kwa mjumbe wa Mungu. Hawawezi kuhubiri, kufundisha, kufasiri, kuondoa au KUONGEZA CHOCHOTE KWAKE kwani ni NENO KAMILIFU LA MUNGU. Hivyo ndivyo Neno lisemavyo.

Si vibaya kumsikia mhudumu, kama wengine wasemavyo, wala si vibaya kwenda kanisani. Unapaswa kwenda kanisani, Lakini Bibi-arusi anataka kusikia chakula cha kondoo, na wengi wanaamini njia pekee ya kusikia Neno safi ni Kubonyeza Play.

Mungu awabariki na huduma yao Mungu aliyowaitia. Kwa maana mimi siko kinyume chao na ninawapenda nakuamini nitatumia Umilele pamoja na Bibi-arusi Wake wote aliyechaguliwa tangu awali. Mimi niko tu kwa ajili ya huduma ya kanda.

Wengi husema ni lazima uwe na mhudumu ili uwe Bibi-arusi. Ninakubali , ninaye , William Marrion Branham, kwa maana yeye ndiye mhudumu mkuu sana aliye na huduma kuu sana kuliko zote ulimwenguni. Kwa maana si neno lake, ujumbe wake, mawazo yake, wala si fasiri yake. Ndilo Neno pekee la Mungu lililothibitishwa kwa ajili ya Wakati wetu. Na ndiyo, ndio HUDUMA kuu sana HAI iliyopo .

Maswali yangu ni: Je! Unaweza tu kusikiliza Kanda na kuwa Bibi-arusi wa Kristo, au je, inanibidi kuwa na kitu zaidi ya Sauti ya Mungu kwenye kanda?

Mimi na nyumba yangu, sisi ni NYUMBA YA KANDA, na tunaamini sisi ni Bibi-arusi Wake na Kila TUNACHOHITAJI ni Sauti ya Mungu kwenye kanda.

Ikiwa ungependa kuungana nasi nyumbani kwako, kanisani, garini au popote pale ambapo Bwana yuko nawe, ili kusikia Bwana Asema hivi, uungana nasi Jumapili saa 3:00 Tatu asubuhi, saa za Jeffersonville, ( ni saa 11:00 kumi na moja jioni ya Tanzania), kusikia Neno la Mungu likimkamilisha Bibi-arusi Wake na kutuletea Ujumbe: Ile Ishara 63-0901M

Ndugu. Joseph Branham

Maandiko ya kusoma kabla ya kusikia Ujumbe:

Mwanzo 4:10

Kutoka sura ya 12 yote

Yoshua sura ya 12 yote

Matendo 16:31 / 19:1-7

Warumi 8:1

1 Wakorintho 12:13

Waefeso 2:12 / 4:30

Waebrania 6:4 / 9:11-14 / 10:26-29 / 11:37 / 12:24 / 13:8,10-20

Yohana Mtakatifu 14:12