23-0406 IBADA MAALUM YA USHIRIKA

Ujume: 57-0418 IBADA MAALUM YA USHIRIKA

pakua – m4a

pakua – amr

BranhamTabernacle.org

Mpendwa Mti wa Bibi-arusi Uliyorudishwa,

Kwa muda wa mwaka mzima, nimetazamia kwa hamu wikendi ninayoweza kufungia nje ulimwengu kabisa, kuzima vifaa vyangu vyote, kuomba siku nzima, kusikia Sauti Yake ikizungumza na moyo wangu, kushiriki Ushirika Naye, na kuweka wakfu upya maisha yangu kwa ukamilifu Kwa ajili ya Huduma yake. KILA SIKU inapaswa kuwa siku ya Pasaka kwetu, lakini wikendi hii ni tukio la kipekee sana, fursa takatifu; wakati uliotengwa kwa Bibi-arusi kukusanyika pamoja na Kuabudu. NIMESISIMKWA SANA kuhusu jambo hilo Enyi marafiki. Siwezi kungoja zaidi ili kujifungia na Mungu mahali pa siri, hapo katika Roho, nikiutazama Uso Wake; nikiungana na Bibi-arusi wa Kristo ulimwenguni kote, tukiketi katika mahali pa mbinguni. Lihimidiwe Jina la Bwana! Kwa kweli inapaswa kuwa wikendi inayotarajiwa sana na takatifu katika maisha yetu.

Loo, hebu tusimame dakika moja tu zaidi hapa. “Mahali pa Mbinguni.” Sasa, si popote pale, bali mahali pa Mbinguni. Tumekusanyika katika “Mbingu,” ina maana kwamba hapo ndipo mahali pa mwaminio. Basi, kama nimeomba vya kutosha, nawe umeomba vya kutosha, au kanisa limeomba vya kutosha, na tuko tayari kwa Ujumbe, nasi tumekusanyika pamoja kama watakatifu, walioitwa wakatoka, waliobatizwa na Roho Mtakatifu, wamejazwa na baraka za Mungu, wameitwa, wakateuliwa, wameketi pamoja mahali pa Mbinguni sasa, sisi ni wa Kimbinguni katika nafsi zetu. Roho zetu zimetuleta katika hali ya Kimbinguni. Loo, ndugu! Haya basi, hali ya Kimbinguni! Loo, nini kingetokea usiku wa leo, kungetokea nini usiku wa leo kama tungekuwa tumeketi hapa katika hali ya Kimbinguni, huku Roho Mtakatifu anatembea katika kila moyo ambao umezaliwa upya na ukawa kiumbe kipya katika Kristo Yesu? Dhambi zote zikiwa chini ya Damu, katika ibada kamilifu, huku tumemwinulia Mungu mikono yetu na mioyo yetu imeinuliwa, tumeketi katika mahali pa Mbinguni katika Kristo Yesu, tukiabudu pamoja katika mahali pa Mbinguni.

Je, umewahi kuketi mahali kama hapo? Loo, mimi nimeketi hata ningelia kwa furaha na kusema, “Mungu, kamwe usiniache nikaondoka hapa.” Mahali pa Mbinguni tu katika Kristo Yesu!

Akitubariki na Nini? Uponyaji wa Kiungu, kutangulia kujua, ufunuo, maono, nguvu, lugha, tafsiri, hekima, maarifa, baraka zote za Kimbinguni, na furaha isiyoneneka na iliyojawa na Utukufu, kila moyo umejazwa na Roho, tukitembea pamoja, tukiketi pamoja katika mahali pa Mbinguni, hakuna wazo moja baya kati yetu, hakuna hata sigara moja inayovutwa, hakuna nguo moja fupi, hakuna jambo hili, lile au lingine, hakuna wazo moja baya, hakuna aliye na neno dhidi ya mwingine, kila mtu akizungumza katika upendo na upatanifu, kila mtu katika moyo mmoja na mahali pamoja, “ndipo kukaja ghafla toka Mbinguni uvumi kama wa upepo wa nguvu ukienda kasi.” Haya basi, “Ametubariki kwa baraka zote za rohoni.”

Bwana Yesu pokea ibada zetu kwako wikendi hii ya Pasaka. Hebu na tuingie katika mahali pa mbinguni katika Kristo Yesu; na tupasue kuingia katika Patakatifu pa Patakatifu. Hakuna wazo moja baya, hakuna kizubaishi chochote, bali kwa nia moja, katika Mahali pamoja; basi kuwe na sauti kutoka Mbinguni ikija kama uvumi wa upepo wa nguvu uendao kasi katika kila moja ya nyumba zetu. “Njoo Bwana Yesu”, tuko tayari kukuona uso kwa uso.

Kwa maana Bibi-arusi amerudishwa kupitia Ujumbe wa Nuru ya jioni ya siku yetu; kupitia Ujumbe wa Malaki 4. Tunakushukuru Bwana kwa dhihirisho kamili la Kristo katika Kanisa Lake, si kanisa lililojengwa kwa mikono, bali dhihirisho kamili la Kristo aliyedhihirishwa ndani ya mtu, nabii wako, kwa ishara kuu na maajabu, naye amefunua Neno lote la Mungu tena. Na sasa linaishi ndani ya Bibi-arusi Wako ulimwenguni kote. Asante kwa kutuwezesha kuishi ili kuona Nuru hii kuu ya jioni, kulingana na unabii.

Basi Nuru ya jioni imetokea kwa ajili gani? Nuru ya jioni ni ya nini? Kurudisha. Whiu! Mnalipata? [Kusanyiko linasema, “Amina.”—Mh.] Nuru ya jioni ni kwa ajili ya kusudi lile lile la Nuru ya asubuhi, kurudisha kile kilichokatiliwa mbali na Nyakati za Giza, kupitia Roma. Mungu anaenda kurudisha, kwa kuangaza Nuru ya jioni (ya nini?), kulirudisha Neno lote la Mungu tena, dhihirisho kamili la Kristo katika Kanisa Lake. Kila kitu alichofanya Yeye, vile vile hasa alivyofanya, itakuwa hivyo tena katika Nuru ya jioni. Mnaona ninayomaanisha? Loo, hilo si ni zuri sana? [“Amina.”] Na kujua ya kwamba tunaishi papa hapa kuiona sasa, Nuru ya jioni, kulingana kabisa na unabii.

Bibi-arusi wa kweli haishii katika Kuhesabiwa haki, ingawa anajua dhambi zake ni kana kwamba hakuwahi kuzitenda kamwe; Yeye haishii katika Utakaso, ingawa Ametakaswa na kutengwa kwa ajili ya utumishi; Haishii katika Pentekoste, ingawa amepokea ubatizo wa Roho Mtakatifu; bali anaendelea hadi kwenye NENO LA SIKU YETU: Malaki 4, Neno Lenyewe lililofanyika mwili tena katika mwanadamu. Ile, “Nitarudisha asema Bwana,” ambayo italeta Imani ya Kunyakuliwa kwa Bibi-arusi. Na Neno hilo lililodhihirishwa linaweza TU kuja kwa kuzisikia Kanda, Jina Lake la ajabu na lisifiwe.

Mmoja wao, Martin Luther, yeye alianza kuiangaza Nuru. Kulikuwako na Nuru ndogo, nguvu kidogo sana, ya kuhesabiwa haki.

Ndipo akaja Wesley, nguvu zaidi, utakaso.

Baada ya Wesley, akaja aliye na nguvu zaidi kuliko yeye, Pentekoste, ule ubatizo wa Roho Mtakatifu, katika nabii mwingine mkuu. Unaona?

Lakini katika siku za mwisho, za Malaki 4, Eliya atakuja pamoja na Neno lile lile. “Neno la Bwana lilimjia nabii.” Katika Nuru za jioni, atatokea, apate kurudisha na kurejesha. Kitu gani? “Kuirudisha mioyo ya watoto iirudie Imani ya Mungu.” Nuru ya nne!

Njooni mkusanyike kulizunguka Neno, majumbani mwenu, wakati wa wikendi ya Pasaka na hebu tumwabudu Bwana. Zimeni simu zenu isipokuwa kupiga picha, kusikiliza Nukuu ya Leo, na kuzicheza kanda kwenye programu ya The Table , programu ya Lifeline, au anuani ya kupakulia.

Ningependa sote tuungane kwenye ratiba ifuatayo:

ALHAMISI

Ilikuwa ni Alhamisi usiku ambapo Bwana Yesu alikuwa na Karamu ya Mwisho pamoja na wanafunzi wake, katika ukumbusho wa Pasaka kabla ya kule kutoka kwa wana wa Israeli. Ni fursa iliyoje tuliyo nayo ya kufanya ushirika na Bwana katika nyumba zetu, kabla ya wikendi yetu takatifu, na kumwomba yeye atusamehe dhambi zetu, na kutupa sisi sote kile tunachohitaji katika safari yetu.

Mungu, chunguza mioyo yetu sasa. Je, ile Damu iko humo Bwana? Kama haimo, twaomba kuwa—kuwa utaiweka sasa hivi, ukiondoa dhambi zetu na kuzifunika, nazo zitatengwa nasi, Bwana, dhambi za ulimwengu huu, ili tuwe watakatifu na wa kupendeza mbele za Baba yetu sasa tunapokuja kula ule—ule mwili wa Damu iliyomwagwa ya Mwana-Kondoo wetu, Mwana wa Mungu, Mwokozi wetu.

Asante kwa kuturuhusu kuishi katika kuona Nuru hii kuu ya jioni, kulingana na Unabii.

Kwa ndugu na dada zangu wa nchi za ng’ambo,

Hebu sote tuanze saa 12:00 KUMI NA MBILI jioni . kwa masaa ya nchi na eneo unaloishi, kusikia Ushirika 57-0418. na kisha tuende katika Ibada yetu maalumu ya Ushirika itakayokuwa ikicheza kwenye programu ya Lifeline ama unaweza kupakua Ujumbe kwa Kiingereza ama lugha zingine kwa kubofya kwenye anuani hapa chini.

Kufuatilia Ujumbe, tutakusanyika na familia zetu majumbani mwetu na kushiriki Meza ya Bwana.

Hivi karibuni tutakuwa na anuani ya kupakua vyote kanda na ibada ya Ushirika, au, itapatikana kwenye Voice Radio .

IJUMAA

Hebu tuende katika maombi pamoja na familia zetu saa  3:00 TATU asubuhi ( ni saa 10:00 KUMI jioni ya Tanzania)., na kisha tena saa   6:00 SITA mchana( ni saa 1:00 MOJA JIONI ya Tanzania ), tukimualika Bwana kuwa pamoja nasi na kujaza nyumba zetu na Roho Mtakatifu tunapojiweka wakfu Kwake.

Mawazo yetu na yarudi huko nyuma hadi siku ile pale Kalvari, zaidi ya miaka 2000 iliyopita, na kumwona Mwokozi wetu akining’inia msalabani, na kisha tujitoe vivyo hivyo kufanya daima yale yanayompendeza Baba:

Sasa tunaona ya kwamba ilimwakisi kikamilifu. Yule Mchongaji sasa alikuwa amelifanya Neno kuakisi kwenye kile Kipeo tena, kilichoitwa Mwanawe, Mungu, Imanueli. Wazia tu, ya kwamba, mtu ambaye amejidhili sana mpaka Mungu akajitambulisha Mwenyewe mle ndani, katika mwili huo, Naye akawa…Yeye na Mungu wakawa mmoja. “Mimi na Baba Yangu ni Mmoja. Baba Yangu anaishi ndani Yangu. Mimi daima hufanya lile linalomfurahisha Baba.”

Vipi kama Mkristo siku hizi angeweza kuwa na ushuhuda kama huo? Ungekuwa ni kipeo papa hapa Yuma, mtaani. Kama wewe ni dobi mwanamke huko nje nyuma beseni la kufulia, ungali utakuwa ni kipeo kwa Mungu, wakati unapoweza kusema, “Daima nafanya kile kinachompendeza Mungu,” na ulimwengu mzima unaweza kuona ka—kazi ya Yesu Kristo ikiakisi ndani yako.

Kisha saa  6:30 Sita na Nusu Mchana.,(  ni saa 1:30 MOJA na NUSU jioni ya Tanzania ), tuungane pamoja katika nyumba zetu ili kusikia, Ukamilifu 57-0419.

Kisha Hebu na tuungane tena pamoja katika maombi saa 9:00 TISA alasiri.( ni saa 4:00 Nne Usiku ya Tanzania). katika ukumbusho wa kusulubiwa kwa Bwana wetu.

JUMAMOSI

Hebu sote kwa mara nyingine tena tuungane katika maombi saa 3:00 TATU Asubuhi ( ni saa 10:00 kumi jioni ya Tanzania )., na  saa 06:00 SITA Mchana( ni saa 1:00 Moja jioni ya Tanzania)., na tutayarishe mioyo yetu kwa ajili ya mambo makuu atakayotutendea miongoni mwetu.

Bwana! Tafadhali, Bwana! Loo, naweza nikaimba kupita kiasi. Huenda nikahubiri kupita kiasi. Huenda nikapaza sauti kupita kiasi. Huenda nikalia kupita kiasi. Lakini kamwe sitaomba kupita kiasi. Ee Mungu, nichunguze na unijaribu.

Nilikuwa tu nikizungumza, muda mfupi uliopita, kuhusu madimbwi ya kina kirefu, jinsi yanavyoziakisi nyota; tia kina cha Roho wako ndani yetu, Bwana, kama nabii Daudi alivyosema, “Uniongoze kando ya maji matulivu,” sio maji yanayotiririka. Maji matulivu, niongoze huko, Bwana. Ninyamazishe.

Kisha saa  6:30 SITA na NUSU Mchana ( ni Saa 1:30 moja na Nusu jioni ya Tanzania )., Sote tutakusanyika pamoja kusikia NENO:
Kuzikwa 57-0420.

Hii itakuwa SIKUKUU ILIYO MUHIMU ilioje kwa Bibi-arusi Wake ulimwenguni kote.

Kisha tuungane tena pamoja katika maombi saa 9:00 TISA alasiri . ( ni Saa 4:00 Nne Usiku ya Tanzania )

JUMAPILI

Ni Siku kamilifu jinsi gani kusikia na kushiriki Kurejeshwa Kwa Mti wa Bibi-arusi. Kwanza Hebu na tuamke mapema kama vile Ndugu Branham alivyofanya asubuhi ile wakati rafiki yake mdogo, yule robin, alipomwamsha
saa 11:00 KUMI na MOJA asubuhi .. Hebu na tumshukuru Bwana kwa kumfufua Yesu kutoka kwa wafu:

Saa kumi na moja asubuhi ya leo, rafiki yangu mdogo mwenye kifua chekundu aliruka dirishani akaniamsha. Ilionekana kana kwamba moyo wake mdogo ungepasuka, akisema, “Amefufuka.”

Saa  3:00 TATU asubuhi .( ni saa 10:00 kumi jioni ya Tanzania)  hebu na tuungane kwa mara nyingine tena katika mnyororo wetu wa maombi, tukiombeana sisi kwa sisi na kujitayarisha kuisikia Sauti ya Mungu.

Saa  6:30 Sita na Nusu mchana .(ni Saa 1:30 Moja na Nusu jioni ya Tanzania )tutakusanyika pamoja kusikia Ujumbe wetu wa Pasaka:  Kurudishwa Kwa Mti wa Bibi-arusi 62-0422.

Baada ya Ibada hii, Hebu na tuungane tena katika maombi, tumshukuru kwa WIKENDI YA AJABU ALIOTUPATA KUWA PAMOJA NAYE NA PAMOJA NA BIBI-ARUSI WAKE ULIMWENGUNI KOTE.

Kwa ndugu na dada zangu walio nchi za ng’ambo, kama mwaka jana,

Ningependa kuwaalika kuungana nasi kwa matukio haya kwa saa za Jeffersonville, kwa vipindi vyote vya maombi kwenye ratiba hii na kwa kanda itakayochezwa   Jumapili Alasiri . Ninatambua, hata hivyo, kwamba kucheza Kanda Alhamisi, Ijumaa, na Jumamosi alasiri katika wakati wa Jeffersonville kungekuwa vigumu sana kwa wengi wenu, kwa hivyo tafadhali jisikie huru kucheza Jumbe hizo wakati wowote wa mchana unaokufaa. Ningependa, hata hivyo, tuungane wote pamoja Jumapili saa 6:30 Sita na Nusu mchana., saa za Jeffersonville, ( Ni saa 1:30 moja na Nusu jioni ya Tanzania )ili kusikia Ujumbe wetu wa Jumapili kwa pamoja.

Ningependa pia kukualika wewe na watoto wako kuwa sehemu ya karatasi za vipindi vya Creations na video za Maelekezo, na majaribio ya YF, ambayo familia yako yote inaweza kufurahia pamoja. Tunaamini mtayapenda kwa kuwa yote yanahusu NENO tutakalosikia wikendi hii.

Kwa ratiba ya wikendi, taarifa kuhusu kujiandaa kwa ajili ya ibada ya Ushirika, nyenzo zitakazohitajika kwa ajili ya vipindi vya Creations, majaribio ya Pasaka, na taarifa nyinginezo, tazama anuani zilizopo hapa chini.

Ni heshima kubwa kwangu kukualika wewe na familia yako kukusanyika pamoja na Bibi-arusi duniani kote kwa wikendi iliyojaa KUABUDU, SIFA NA UPONYAJI. Ninaamini kweli ni wikendi ambayo itabadilisha maisha yako milele.

Ndugu Joseph Branham