23-0402 Unyakuo

Ujume: 65-1204 Unyakuo

PDF

pakua – m4a

pakua – amr

BranhamTabernacle.org

Mpendwa Neno Juu ya Neno,

Makanisa mengi yametatizika, yana mshangao , yameduwazwa, yamepigwa na butwaa, yamefadhaika, yamechanganyikiwa na hata kushangazwa na kile kinachoendelea kwa hawa “ Watu wa Kanda ” kutoka ulimwenguni kote kila Jumapili.

Ni Muungano Usioonekana wa Bibi-arusi wa Kristo, tukiketi katika uwepo wa Mwana, kuivishwa, tukijiweka wenyewe tayari. Bwana Arusi Wetu wa Mbinguni amekuwa akituambia yote kuhusu Makao yetu ya Baadaye Pamoja Naye.

Majuma machache tu yaliyopita Alituambia: “Dunia hii si Makao yako, ni Edeni ya Shetani, nami nitaiteketeza kwa moto. Wewe ni kipenzi changu, ambaye Nimekuchagua kabla ya kuwekwa misingi ya ulimwengu kuwa Bibi-arusi wangu. Sasa, Jumapili hii nitakuambia yote kuhusu Unyakuo Wangu unaokuja hivi karibuni.”

Tuko chini ya matarajio makubwa sana. Tunaweza kulihisi jambo hilo hewani. Mambo yanatukia haraka sana.

Vile vile hasa Biblia ilivyosema ingetendeka katika siku hii, inatendeka, siku baada ya siku. Mbona, inalundikana upesi sana huko nje, katika yale majangwa, na mambo yanayotendeka, hata nisingeweza kufuatilia jambo hilo. Tuko karibu na kule Kuja kwa Yesu, kuunganishwa na Kanisa Lake, ambapo Neno linafanyika Neno.

Haya yote yanatendeka kwa ajili yetu, Bibi Mteule wake, Bibi-arusi wa siku hii. Sisi ndio pekee tunaoona mambo haya yakijifunua.

Ametuchagua tangu zamani kwa ajili ya wakati huu na hakuna mtu yeyote anayeweza kupachukua mahali petu. Sasa Sisi ni wana na binti waliodhihirishwa ili tuweze kushirikiana Naye; hicho ndicho yeye Anachotaka.

SISI ni Neno juu ya Neno, chembe hai juu ya chembe hai, Uhai juu ya Uhai, na kimo kikamilifu cha Bibi-arusi wa Bwana Yesu Kristo.

Kama unalo hitaji, litamke . Wewe ni Neno juu ya Neno. Usiangalie utusitusi huu katika ulimwengu unaotuzunguka; magonjwa, maradhi, mauaji, kukata tamaa, ukichaa wa watu ambao hawajui ikiwa wao ni mwanamume au mwanamke. SISI NI BIBI-ARUSI , tuliochaguliwa tangu zamani , tumehesabiwa haki, Bibi-arusi aliyedhihirishwa wa Bwana Yesu Kristo.

Usiogope LOLOTE. Kuwa mwenye furaha na kushangilia. Muda umekaribia. Tunajiandaa kuondoka kwenye nyumba hii ya wadudu, UTUKUFU !!!

Njoo ujiweke tayari pamoja nasi kwa ajili ya Unyakuo , Jumapili saa 06:00 SITA MCHANA , saa za Jeffersonville ( ni saa 1:00 MOJA JIONI ya Tanzania). Kamwe Hutabaki kama ulivyokuwa.

Ndugu. Joseph Branham.

Maandiko ya kusoma Kabla ya Kusikiliza Ujumbe :

Zaburi 27:1-5