21-1204 Unyakuo

Ujume: 65-1204 Unyakuo

PDF

pakua – m4a

pakua – amr

BranhamTabernacle.org

Mpendwa Bibi-arusi wa Sauti,

Ninaamini ninaweza kunena kwa niaba ya kila mmoja wetu ninaposema, tumekuwa na wikendi kuu sana ya Shukrani ya maishani mwetu. UTUKUFU!!

Tulisikia Neno juu ya Neno, Ufunuo juu ya Ufunuo. Kiu Yetu ilitulizwa na kitu pekee kinachoweza: Neno Lake, Ujumbe wa wakati huu, Kristo Mwenyewe akinena na Bibi-arusi Wake.

Sasa tunaona Neno lile lile lililoahidiwa, la Luka, la Malaki, ahadi hizi nyingine zote za siku ya leo, zikifanyika mwili, zikikaa kati yetu, ambazo tulisikia kwa masikio yetu; sasa tunamwona Yeye (kwa macho yetu) akifasiri Neno Lake Mwenyewe, hatuhitaji Fasiri yo yote ya mwanadamu. Ee kanisa la Mungu Aliye Hai! mlio hapa na kwenye simu! amkeni upesi, kabla hamjachelewa sana! Mungu awabariki.

Je! tunaweza kuwazia Hilo ya kwamba tungeweza kuwa tunatazama kwa macho yetu wenyewe, Neno lililo hai la Mungu lililodhihirishwa? Tukilitazama Neno lililo hai lililofasiriwa katika umbo la mwili, Mungu kati yetu! Si ajabu wahenga wote wa kale waliitazamia siku hii, lakini SASA, tunaishi katika siku hizo zilizoahidiwa, tukiona na kusikia jambo Hilo likiwa limedhihirishwa kwa masikio na macho yetu wenyewe.

Tumesikia habari Zako, ya kwamba Wewe ungeweza kuumba kuchakuro; Tumesikia habari Zako, ya kwamba Wewe ungeweza kuumba kondoo dume; lakini sasa Tunakuona Wewe, kwa jicho letu Wenyewe! Dhihirisho hilo, ono kufanywa lionekane.

Yeye ni nini basi? Neno lililofasiriwa ni dhihirisho la Jina la Mungu .

Haijalishi wakosoaji wanasema nini, Sisi tuko katika Mapenzi Yake Makamilifu kwa kukusanyika katika nyumba zetu, katika makanisa yetu, au popote tunapokusanyika, tukisikiliza Sauti Yake.

Kama mimi siamini kwenda kanisani, basi kwa nini niwe na makanisa? Tulikuwa nayo kila mahali nchini, yameunganishwa hivi majuzi usiku, kila maili mia mbili mraba kulikuwapo na kanisa langu .

Makanisa YAKE yameunganishwa kote ulimwenguni ili kusikia Sauti ya Mungu ikinena, na kumwita Bibi-arusi Wake atoke. Hakuna chachu miongoni mwetu, jambo Hilo linaleta utimilifu wote wa Uungu kwa jinsi ya mwili miongoni mwetu. Mwana wa Adamu anadhihirishwa, anafunuliwa, akilirudisha Kanisa pamoja na Uungu wote wa Mungu miongoni mwetu. Anatuonyesha ishara zile zile zionekanazo na Dhihirisho la Yeye Mwenyewe kama alivyofanya hapo mwanzo alipodhihirishwa duniani katika umbo la Mungu-Nabii.

Aliahidiwa na Malaki 4, aliahidiwa na Maandiko hayo mengine. Unaabudia wapi? Nyumba ya Mungu, umeketi (katika wakati uliopo).

Ninamshukuru sana Bwana kwa yote anayomfanyia Bibi-arusi Wake katika siku hizi za mwisho. Amekuwa akitutia moyo, akituhakikishia, kwamba sisi ni Wateule Wake waliokuwa ndani Yake kabla ya kuwekwa misingi ya ulimwengu. Ni wakati wa ajabu jinsi gani kwa Bibi-arusi Wake.

Bwana ameweka moyoni mwangu kuendelea na Jumbe hizi za mwisho ambazo zilizohifadhiwa kwa ajili ya Bibi-arusi Wake. Ninahisi kubarikiwa sana kufikiria, Baba alitoa njia ambayo sote tungeweza kuungana pamoja, kutoka kote ulimwenguni, kusikia Jumbe hizi. Huu hakika ni, Muungano Usioonekana wa Bibi-arusi wa Kristo.

Tangu wakati hatukuweza kuwa na ibada pamoja ya mahali, kwa sababu ya Corona na ujenzi wa patakatifu papya, kuna mambo mawili ambayo sisi sote tunayakosa na tunatamani kuyafanya. Ni mambo hayo mawili ambayo Bwana aliamuru kwa Bibi-arusi Wake kufanya hadi kurudi Kwake: Ushirika na Kutawazana Miguu.

Nilipokuwa nikiomba na kumtafuta Bwana, Aliweka moyoni mwangu tuwe na vyote viwili Ushirika na Kutatawazana Miguu pamoja na familia zetu. Nilibarikiwa sana na kufurahishwa sana Alipoweka Jambo hilo moyoni mwangu, na jinsi tunavyoweza kulifanya. Tutakuwa tukiufanya katika tarehe kamili ya ibada ya mwisho ya Ushirika ambayo Ndugu Branham aliyokuwa nayo alipokuwa hapa pamoja nasi, tarehe 12 Desemba 1965. Pia tutabarikiwa kwa yeye kutuongozea ibada ya Ushirika na kutawazana Miguu kwa mara nyingine tena.

Nitakuwa nikikutumia barua, na kuchapisha kwenye tovuti ya Branham Tabernacle, maelezo yote katika siku chache. Ninaweza kukuahidi utakuwa ni wakati ambao Bibi-arusi hatasahau. Niko chini ya matarajio Haya ya baraka zake kuu ambazo atakuwa akitupatia.

Kuanzia Jumamosi hii, tutakuwa tukisikiliza Sauti yetu ikituletea Ujumbe: Unyakuo 65-1204 , saa 3:00 Tatu Asubuhi., saa za Jeffersonville( ni Saa 11:00 Kumi na Moja jioni ya Tanzania) . Itakuwa ni miaka 56 hadi siku hii ambapo Mungu alinena kupitia kwa mjumbe Wake na kuweka Sauti Yake kwenye kanda ya sumaku, ili Bibi-arusi apate kula kwenye Hiyo na kuiva Mwenyewe, akijifanya Mwenyewe tayari kwa ajili ya Unyakuo unaokuja hivi karibuni.

Tutaendeleza ratiba kwa kukusanyika Jumapili saa 8:00 Nane mchana, saa za Jeffersonville, ( ni Saa 4:00 nne usiku ya Tanzania) ili kusikia: Mambo Yatakayokuwapo 65-1205 .

Kisha Jumatatu tutasikia: Matukio ya Sasa Yakidhihirishwa Na Unabii 65-1206 , na

Jumanne : Uongozi 65-1207. Unaweza kuusikiliza siku hiyo wakati wowote unaofaa kwako na familia yako.

Kama tu wiki iliyopita, tutakuwa tukiweka jumbe hizi kwenye Voice Radio( iliyo kwenye app ya Lifeline ya vgr) saa 3:00 Tatu Asubuhi za Jeffersonville ( ni Saa 11:00 kumi na Moja jioni ya Tanzania)

na saa 1:00 Moja jioni ya Jeffersonville ( ni Saa 9:00 Tisa Usiku ya Tanzania) .

Ilioambatishwa hapa ni kalenda yenye siku, majira na Jumbe ambazo tutakazosikia. Katika siku chache zijazo, nitakuwa nikikutumia barua na kuchapisha ratiba ya Ibada yetu ijayo ya Ushirika.

Nikitazamia kuwa pamoja nawe, Bibi-arusi Wake Asiyeonekana, kwenye Kiti Chake cha Enzi.

Bwana na akubariki,

Ndugu. Joseph Branham