Category Archives: Uncategorized

24-0204 Yupo Mtu Hapa Anayeweza Kuiwasha Taa

UJUMBE: 63-1229M Yupo Mtu Hapa Anayeweza Kuiwasha Taa

PDF

pakua – m4a

pakua – amr

BranhamTabernacle.org

Mpendwa Sura ya Yesu Kristo,

Watu wanafikiri sisi ni wendawazimu, tunavyoketi katika nyumba zetu na makanisa, kuzisikiliza kanda. Wanafikiri tunakufa kwa njaa. Hawatambui kuwa tumeketi katika uwepo wa Nuru ya Mwana ya Agosti , tukiivishwa, na kulishwa Chakula Kilichohifadhiwa kama ndama zizini.

Sisi ndio ile Ngano iliyoendelea zaidi, tuko tayari kulipokea. Ikiwa wanataka kuishi katika mapokeo yao, na waendelee. Sio SISI, sisi tunaishi katika Nuru ya siku yetu.

Nuru ya siku yetu ni nini? Mungu alimtuma ulimwenguni malaika wake wa saba mwenye nguvu kumwongoza Bibi-arusi wake. Yeye alikuwa nani? Alikuwa nabii. Yale aliyosema yalitimia. Yeye alikuwa Neno la Mungu lililodhihirishwa. Yeye alikuwa dhihirisho la Nuru ya Neno la Mungu. Yeye alikuwa Nuru ya Mungu kwa ajili ya siku hii.

Musa aliendelea tu hata hivyo, kwa sababu alikuwa ile Nuru. Alikuwa Nuru ya saa ile. Kile alichokuwa nacho, kilikuwa nini? Mungu akidhihirisha Neno Lake lililoahidiwa kupitia kwa Musa, na Musa alikuwa Nuru.

Eliya alikuwa Nuru…Alikuwa nini? Ile Nuru. Haleluya! Alikuwa Nuru, ile Nuru; alikuwa Neno la Mungu lililodhihirishwa.

Yohana, alipokuja duniani… Basi alipojitokeza Yesu alisema alikuwa Taa angavu inayong’ara. Haleluya! Kwa nini? Alikuwa Neno lililodhihirishwa.

Basi kulingana na Neno, Nuru ya siku yetu ni nabii wa Mungu, William Marrion Branham. Yeye yule aliaye katika nyika ya Babeli “Tokeni kwake, enyi watu wangu, msishiriki dhambi zake.”

Yeye alikuwa kutimizwa kwa Malaki 4:5, na Ufunuo 10:7. Yeye alinena tu na kusema, “itakuwa pale,” nayo ilikuwa pale, bila kitu chochote ndani yake. Hakuwa kamwe amempata kindi; hapakuwa na yeyote hapo. Yeye alisema tu, “Na iwe,” na ikawa.

Neno la Mungu halikosei, nalo halina budi kutimia. Tumeiona Nuru; Neno Lake aliloahidi kwa ajili ya siku hii. Limethibitishwa na kuhakikishwa ya kwamba ni Kweli. Ni Nuru ya saa hii.

Hakuna kibadala katika kujua kile tunachosikiliza ni Neno lililodhihirishwa kwa ajili ya siku hii. HALINA WAFURUKUTA MIKIA NDANI YAKE… HATA CHEMBE. Ikiwa wengine watosheka na kitu kingine, na waendelee, lakini sio sisi.

Haimaanishi kuwa huwezi kumsikiliza mchungaji wako, ama kwamba mhudumu hawezi kuhubiri; sivyo hata kidogo, lakini LAZIMA uchuje kila neno unalosikia kupitia chujio kuu la Mungu, UJUMBE HUU KWENYE Kanda.

Wanaposema siku za Ujumbe wa mtu mmoja zimepita, hao ni WAFURUKUTA MKIA. Wanaposema Ujumbe huu sio Yakini yao, hao ni WAFURUKUTA MKIA. Wanaposema kusikiliza kanda haitoshi, hao ni WAFURUKUTA MKIA.

Hakuna kitu kikubwa zaidi ya Kubonyeza Play tu, kujua unaweza kusema AMINA kwa kila neno. Hakuna mahali pengine unapoweza kufanya hivyo isipokuwa kusikiliza Ujumbe wa saa hii.

Sasa sisi ni sura ya Yesu Kristo kwa ajili ya siku hii. Sisi ni Neno Lake lililodhihirishwa. Sisi ndio wale aliowachagua kupokea Ufunuo Wake mkuu wa wakati wa mwisho. Sisi ndio BIBI-ARUSI WAKE.

Ni Bibi-arusi Wake peke yake ndiye atakayekuwa na Ufunuo wa kweli wa Nuru ya siku hii. Watajua, Nuru hii itawakamilisha. Nuru hii ni Roho Mtakatifu akinena kupitia malaika-mjumbe Wake.

Je! ungependa kuketi katika uwepo wa Nuru ya Mungu ya saa hii? Basi ninakualika uje uungane nasi Jumapili saa 6:00 SITA MCHANA saa za Jeffersonville,( Ni saa 2:00 MBILI USIKU ya Afrika Mashariki ) tunaposikia  Yupo Mtu Hapa Anayeweza Kuiwasha Taa 63-1229M.

Ndugu. Joseph Branham.

Maandiko ya kusoma kabla ya ibada:

Mwanzo 1:3, Sura ya 2
Zaburi 22
Yoeli 2:28
Isaya 7:14, 9:6, 28:10, 42:1-7
Mathayo 4:12-17, Sura ya 24 na ya 28
Marko Sura ya 16
Ufunuo Sura ya 3

24-0128 Aina Tatu Za Waamini

UJUMBE: 63-1124E Aina Tatu Za Waamini

PDF

pakua – m4a

pakua – amr

BranhamTabernacle.org

Mpendwa Mwamini,

Jinsi inavyopendeza kusema, MIMI NI MWAMINI. Si wa kanuni za imani; Neno! Si wa madhehebu; Neno! Si wa kile anachosema mtu mwingine; bali kile lisemacho Neno!

Sisi hatuulizi kitu, tunaliamini tu. Haidhuru Linasikika namna gani ama lolote mtu ye yote asemalo juu yake, sisi ni waamini halisi. Tuna ufunuo wa kiroho wa Neno.

Tunaiona ile saa tunayoishi. Tunauona ule Ujumbe wa saa hii. Tunamwona yule mjumbe wa saa hii. Tunamwona Mungu akijifunua Mwenyewe katika Neno Lake. Tunaona hakuna kitu kingine ila Ujumbe Huu, Mjumbe Huyu, Neno Hili.

Mwamini halisi hasikii kitu ila Neno. Hakuna zaidi. Yeye huliangalia Neno. Hatafuti mianya. Yeye hatafuti viinimacho. Anamwamini Mungu, na hilo latosha, naye anaendelea tu. Mnaona? Huyo hapo mwamini.

Sisi hatuwezi kusikia kitu kingine ila Neno; Neno linalomjia nabii peke yake. Si mianya, si fasiri ya mtu fulani, Neno Safi lililonenwa na kuwekwa kwenye kanda kwa ajili ya Bibi-arusi.

Roho amelihuisha Neno hilo ndani yetu nalo limekuwa hai. Kwa imani, tunaliona na kuliamini. Itakuja sauti kutoka Mbinguni ambayo italeta ubatizo mkubwa sana wa Roho Mtakatifu katika Bibi-arusi, ambao utatuondoa duniani, katika Neema ya Kunyakuliwa. Mungu aliahidi jambo hilo.

Tunawekwa majaribuni kila wakati, kila siku. Shetani anajaribu kutuambia majaribu na mitihani yetu ni Mungu anatuadhibu. Lakini MUNGU ASIFIWE, sivyo ilivyo, ni Shetani anayefanya jambo hilo naye Mungu analiruhusu.

Mungu anatujaribu, na kutufinyanga ili aone kile tutakachofanya. Jaribio huja kututikisa, kutuweka kule chini kabisa, kuona mahali tutakaposimama. Lakini tunashinda kila vita, kwa kuwa sisi ni mifano iliyo hai; Neno la Mungu linaishi ndani yetu na kupitia kwetu.

Sisi tuna umuhimu jinsi gani machoni pake?

Hakuna mtu anayeweza kupachukua mahali pako, haidhuru ni padogo namna gani. Unasema, “Mimi ni mke wa nyumbani tu.” Hakuna mtu anayeweza kupachukua mahali pako. Mungu, katika uchumi Wake mkuu, ameweka jambo hilo hivyo, Mwili wa Kristo, katika utaratibu, hata hapana mtu anayeweza kupachukua mahali pako.

Hilo ni lakupendeza jinsi gani? Kila mmoja wetu ana mahali. Kila mmoja wetu alikuwa hapa wakati Mungu aliponena ulimwengu ukawa. Aliweka mwili wetu hapa wakati huo huo. Mungu alituweka sisi duniani katika wakati huu ili kulitimiza Neno lake na kutupa Uzima wa Milele.

Kila mmoja anapaswa kufanya uamuzi. Unasimama wapi kuhusu Neno hili, Ujumbe huu, mjumbe huyu? Ni muhimu jinsi gani kulisikia Neno linalonenwa kwenye kanda?

Kwenye sehemu mbalimbali ulimwenguni, kanda hizi zinakopita, huduma za kanda.

Ni huduma ya kanda iliyotumwa kwa Bibi-arusi Wake ulimwenguni kote kutoka kwa Mungu. Inakuambia mahali ulipo hasa, wewe ni nani, na iwapo wewe ni mwamini katika Neno.

Wewe umo katika moja ya tabaka hizi. Katika hali yako ya sasa hivi, hali yako ya sasa ya akili, kwamba, ninyi mlio hapa katika mkutano huu unaoonekana, nanyi mtakaokuwa katika mikutano isiyoonekana ya kanda hii, hali yako ya sasa ya akili baada ya kuisikiliza kanda hii, inakuthibitishia uko katika tabaka gani.

Baada ya wewe kusikiliza kanda hii, inathibitisha uko katika tabaka la watu gani. Baadhi wanaamini unahitaji zaidi ya Neno safi tu lililonenwa kwenye kanda. Wengine wanaamini kwamba siku za Ujumbe wa mtu mmoja zimepita; ni lazima umsikilize mchungaji wako vinginevyo umepotea.

Mgawanyiko mkuu sana katika Ujumbe siku hizi ni umuhimu uliowekwa katika kuzisikiliza kanda. Baadhi wanafundisha kuwa ni makosa kuzicheza kanda kanisani; ni mchungaji pekee yake ndiye anayepaswa kuhudumu. Wengine wanasema kuna ulingalifu, lakini kamwe hawazichezi kanda kanisani, na kama wakizicheza ni mara chache sana.

Kulivyo na mitazamo mingi, mawazo mengi, fasiri nyingi za Neno, ni nani aliye sahihi? Ni yupi utakaye mwamini? Hilo ndilo swali ambalo kila mmoja wetu anapaswa kujiuliza.

Nabii alituambia tulichunguze kwa NENO, sio yale mtu yeyote asemayo. unalifanyaje jambo hilo? KUNA NJIA MOJA TU PEKEE ya kufanya jambo hilo, BONYEZA PLAY.

Lazima kuwe na jibu sahihi, njia sahihi. Kila mtu lazima aamue mwenyewe. Jumapili hii itaamua wakati ujao wa wote wanaosikia Ujumbe huu.

Jambo unalopaswa wewe mwenyewe kujiuliza: Ni nani pekee aliye na Bwana Asema Hivi? Nguzo ya Moto ilimthibitisha nani? Ni nani atakaye tutambulisha kwa Yesu? Ni nani aliyenena Neno la kutokukosea? Ni maneno ya nani yaliyonenwa duniani yalikuwa muhimu sana, yakarudisha mwangwi mbinguni?

Iwapo ungependa kupata majibu sahihi, ningependa kukualika uje kusikiliza Jumapili hii saa 06:00 SITA MCHANA, saa za Jeffersonville,( ni saa 2:00 MBILI USIKU ya Afrika Mashariki ) kusikiliza Ujumbe:   63-1124E —Aina Tatu za Waamini.

Ndugu. Joseph Branham

Yohana Mtakatifu 6:60-71

24-0121 Nimtendeje Yesu Aitwaye Kristo?

UJUMBE: 63-1124M Nimtendeje Yesu Aitwaye Kristo?

PDF

pakua – m4a

pakua – amr

BranhamTabernacle.org

Wapendwa Wapenda Kanda,

Tunaupenda Ujumbe huu kwa moyo wetu wote. Ni utamu wa miwa ya Mungu. Ni Neno la Mungu ambalo limethibitishwa kinaganaga, na kuhakikishwa, tena na tena. Ujumbe huu ni jibu la Neno la Mungu. Ni Kristo yeye yule aliyetiwa mafuta, lile Neno lililotiwa mafuta la siku yetu.

Tuna Neno la Mungu lililothibitishwa hapa, likithibitisha, kuhakikishwa na Roho, ya kwamba Yeye ametupokea na kutupa Ubatizo wa Roho Mtakatifu. Tumebatizwa katika Jina la Yesu Kristo. Injili ile ile, ishara zile zile, maajabu yale yale, huduma ile ile, hata Nguzo ya Moto ile ile ikionekana mbele zetu, ikionyesha ishara na maajabu. Hakuna udhuru, mahali po pote.

Ni wakati wa kuungana kwa Mungu na Bibi-arusi Wake. Bibi-arusi wa Kristo amekwishaitwa. Tumetiwa muhuri katika Ufalme wa Mungu. Mitambo iko hapa tunangojea tu Nguvu za Utendaji zitakazotuondoa kwenye dunia hii kuingia Utukufuni, katika Kunyakuliwa.

Hizo Nguvu za utendaji ni kujazwa tena kwa Roho Mtakatifu. Jiwe la Kufunika litashuka na kuungana na ule Mwili. Ndipo, wakati Kichwa hicho na Mwili huo vinapoungana pamoja, zile nguvu kamili za Roho Mtakatifu zitatuinua SISI juu na waliokufa katika Kristo watafufuka katika uzuri wa utakatifu Wake, na kuruka kwenda hewani.

Saa hiyo inawadia haraka sana. Wakati umefika mwisho. Maamuzi ya mwisho hayana budi kufanywa. Utafanya nini na Neno lililotiwa mafuta la siku hii? Msimamo wako ni upi juu ya Ujumbe wa saa hii?

Je, hivi utasema tu: “Ninaamini Ujumbe. Ninaamini Mungu alimtuma nabii.”

Usifikie tu umbali huu, ukasema, “Naamini Ujumbe.” Tii mjumbe.

Iwapo huna budi KUMTII mjumbe: ANGALIA, alisema tii mjumbe. Basi ni muhimu jinsi gani kuamini na kusikia kila Neno ambalo mjumbe huyo alilosema?

Unasema, “ Vema, Naamini kila neno lililosemwa, Ndugu Branham.” Hilo ni sawa, bali hiyo ni—hiyo ni uwezo tu wa kusoma.

Kwa nini watu wasiridhike na kanda? Kila mtu hawezi kuwa nabii. Kuna nabii mmoja tu, na Neno huja kwa nabii huyo.

Kanisa lilifanya vizuri mpaka walipoanza kulihoji hilo; ama walitaka sauti zingine kuwaambia, na kuwafasiria, yale ambayo nabii huyo aliyosema. Walitaka Kora na Dathani wa sasa.

Mnaona, ilianza na upotoshaji mdogo tu wa Neno, na, jambo lile lile, inaishia vile vile.

Kama ilianza hivyo, na itaishia hivyo, upotoshaji mdogo tu wa Neno, hakika mnatambua jinsi gani MNAVYOPASWA kukaa na kanda. Hakika mnaona kwa nini Mungu alihakikisha kuwa Ujumbe huu umerekodiwa na kuhifadhiwa kwa ajili ya Bibi-arusi.

Sisemi mambo haya kuwashusha wachungaji wenu, au kusema msimsikilize mchungaji wenu, HAPANA, bali kuwaonyesha umuhimu wa kubonyeza play na kuusikia Ujumbe huu kwenye kanda.

Jinsi Kanisa linapaswa kuwa linahakikisha tena, na tena, na tena, na tena! Tunakungojea Kuja Kwake. Tunaamka, tunakungojea kule kuondoka. Inatubidi kulichunguza kwa Neno, si kile mtu fulani alichosema. Hakikisha unajua, wewe mwenyewe, kama tukio la kibinafsi pamoja na Kristo. Lichunguze tena, na tena, na tena.

AMESEMAJE? Inatubidi kulichunguza kwa Neno tena, na tena, na tena. Unalichunguzaje kwa Neno? Neno la siku hii ni lipi? Ni lile lile kama lilivyokuwa tangu mwanzo, Biblia.

Mungu anasema ni nani aliye mfasiri wa Neno Lake? ni Mimi? Ni Mchungaji wako? HAPANA, nabii wa Mungu aliyethibitishwa wa wakati huu ndiye mfasiri pekee wa Neno. Kwa hiyo, ni lazima ulichunguze kwa KANDA kila Neno analosema mtu yeyote tena, na tena, na tena!

Ikiwa tamshi hilo ni la kweli, na unaamini kwamba jambo lililo muhimu zaidi ambalo mtu yeyote, au mchungaji yeyote analoweza kufanya, ni KUBONYEZA PLAY, Basi kwa nini hilo ni gumu sana kwa yeyote anayedai kuamini Ujumbe kusema hivyo? Kwa sababu tu hawaliamini.

Uamuzi WAKO wa mwisho ni upi? Kwangu mimi na nyumba yangu, tutabaki na Ujumbe huu na mjumbe wa Mungu, Kanda hizi. Tunaamini hakuna kitu muhimu zaidi kuliko kusikiliza Sauti ya Mungu kwenye kanda.

  • Kuna Sauti MOJA tu ya Bwana Asema Hivi.
  • Kuna Sauti MOJA tu ambayo Nguzo ya Moto iliithibitisha.
  • Kuna malaika-mjumbe wa saba MMOJA tu.
  • Kuna Sauti MOJA tu ambayo Bibi-arusi wote wanayoweza kukubaliana kwake.
  • Kuna Sauti ya Mungu MOJA tu kwa ajili ya kizazi hiki.

Kama unao Ufunuo huo huo, njoo uungane nami na kundi dogo la waaminio ulimwenguni kote wanaoamini jinsi hiyo hiyo, Jumapili saa 6:00 SITA MCHANA, saa za Jeffersonville,( Ni saa 2:00 MBILI USIKU ya Afrika Mashariki ) tunaposikia na kufanya uamuzi wetu wa mwisho: Nimtendeje Yesu Aitwaye Kristo? 63-1124M.

Ndugu. Joseph Branham

24-0114 Yeye Aliye Ndani Yenu

UJUMBE: 63-1110E Yeye Aliye Ndani Yenu

PDF

pakua – m4a

pakua – amr

BranhamTabernacle.org

Wapendwa Waamini wenye Imani Kamilifu,

Kila siku mioyo yetu inaenda mbio kwa matarajio makubwa. Tunangojea ile saa ifike ya kule Kuja Kwake hivi karibuni. Hofu zote zimetoweka. Hakuna kujiuliza-uliza tena, “Je! sisi ni Bibi-arusi Wake”? Imetiwa nanga ndani ya mioyo yetu zaidi ya hapo nyuma, SISI NI BIBI-ARUSI WAKE.

Tumeshikwa katika hali ya Kimbinguni, tukisikiliza huduma ya Yesu Kristo, aliyefanyika mwili upya katika Kanisa Lake. Ujumbe huu umethibitishwa kotekote na Neno la Mungu, hivi kwamba hawezi kuwa ni mwanadamu, haina budi kuwa ni Mungu akinena mdomo kwa sikio na Bibi-arusi Wake.

Sisi tunaamini si mwanadamu anayenena nasi kwenye kanda hizi, ni Mungu.

Ninachojaribu kusema, “Usife moyo.” Usimruhusu Shetani akuambie ubaya kunihusu mimi; sababu ana mengi. Bali wewe shikilia matumaini hayo; sababu, usipoyashikilia, haitatendeka. Usiniangalie mimi, kama mwanadamu; mimi ni mwanadamu, nimejaa makosa. Bali tazama yale ambayo ninayosema kumhusu Yeye. Ni Yeye. Yeye Ndiye.

Yakubidi kuamini na kuwa na matumaini katika yale ANAYOSEMA, LA SIVYO HAITATENDEKA. Hatumwangalii nabii wa Mungu kama mwanadamu, kama wengi wanavyofikiri tunafanya hivyo. Tuko nyuma ya pazia la mwili wa mwanadamu, na yote tunayoyaona na kusikia ni Mungu akinena kupitia midomo ya mwanadamu, NA TUNAYO MATUMAINI NA KUAMINI KILA NENO.

Huo ndio Ufunuo wa Yesu Kristo kwa ajili ya siku hii. Kuamini kuwa ni Mungu, si mwanadamu, anayenena kwenye kanda. Ukilikosa jambo hilo, rafiki, umeukosa Ujumbe wa wakati huu na huwezi kuwa Bibi-arusi.

Shetani anaweka fasiri yake kwenye jambo hilo, na asilimia 99% ya wakati ananukuu Ujumbe kama tu vile alivyomfanyia Hawa, bali Hawa aliamriwa kukaa na Neno; yale Adamu aliyomwambia ndio Mungu aliyosema, si yale ambayo mtu mwingine aliyosema ati yalimaanisha. Hawa alipaswa kukaa na Sauti ya Mungu.

Hii ndio siku iliyo kuu ambayo ulimwengu umewahi kujua. Maisha ya Yesu Kristo, yale aliyoishi na kujifunua Mwenyewe katika maisha ya nabii Wake, sasa yanaishi katika mwili ndani YETU, Bibi-arusi Wake.

Tunafanya vile hasa Yeye alivyotuamuru kufanya: kukaa na Neno kwa kukaa na Sauti ya Mungu iliyo kwenye kanda. Ndio huduma ya kanda ya Mungu na mpango wa Mungu wa siku hii.

Ikiwa kweli unaamini William Marrion Branham alikuwa ndiye malaika-mjumbe wa saba aliyechaguliwa na Mungu, yule ambaye Mungu alimchagua kunena na kufunua siri zote zilizofichwa katika Neno, aliye Sauti ya Mungu kwa kizazi hiki, mtu aliyekuwa na imani kuliko mtu mwingine yeyote yule, yule ambaye malaika wa Bwana alimwambia “ikiwa utawafanya watu WAKUAMINI, hakuna kitu kitakachosimama mbele ya maombi yako”, basi Jumapili hii itakuwa siku kuu kuliko.

HAKUNA KITU ambacho kinachoweza kamwe kuuondoa Ufunuo wa Ujumbe Huu kwetu sisi, HAKUNA. Hatuwezi KAMWE kuutilia shaka. Kama Yeye aliusema, sisi tunauamini. Huenda tusiuelewe Wote, lakini tunauamini hata hivyo.

Yesu mwenyewe alituambia: “Yeye aliye ndani yenu ni mkuu kuliko yeye aliye katika ulimwengu.” hebu hilo na lizame mioyoni mwetu. Roho Wake anaishi ndani yetu. Je, twaweza kulishika hilo? Sasa hivi, unaposoma Barua hii, Roho Mtakatifu, Mungu Mwenyewe, Nguzo ya Moto, anaishi na kukaa ndani yetu? Tunajuaje kuwa hiyo ni kweli? MUNGU ALISEMA HIVYO!!

Shetani anaendelea kutuambia kwamba sisi ni watu walioshindwa. Na yuko sahihi, ndivyo tulivyo. Anatukumbusha, hatupo mahali tunapotakiwa kuwa katika Neno. Sahihi tena, hatuko. Tunafanya mambo tunayojua vyema kuliko kuyafanya. Tusamehe Bwana, yuko sahihi.

Lakini hata pamoja na makosa yetu yote, madhaifu yetu yote, kushindwa kwetu kote, haibadilishi ukweli wa mambo, SISI NI BIBI-ARUSI. TUNAAMINI KILA NENO!

Hatujitazami sisi wenyewe ama chochote tunachoweza kufanya, sisi ni mchafuko. Sisi tunajua tu kwamba Yeye alituchagua na kutupa Ufunuo wa Neno Lake na hakuna kitu kinachoweza kuuondoa Ufunuo huo kwetu. Huo umewekwa ndani ya mioyo na roho zetu.

Yeye alituambia inatupasa kuwa na IMANI KAMILIFU. Tunayo Bwana, IMANI KAMILIFU katika Neno Lako. Tuna imani katika Yale Nabii Wako aliyosema kuwa ni Bwana Asema Hivi. Si neno lake, bali Neno lako kwetu sisi.

Nabii Wako alituambia chochote tunachohitaji, kama tu tutaamini, na kuwa na imani katika Neno Lako, tunaweza kupata chochote tunachohitaji. TUNAAMINI.

Bwana, ninalo hitaji. Ninakuja mbele Zako nikiwa na imani yote niliyo nayo katika Neno Lako, kwa maana haiwezi kushindwa. Lakini leo, Bwana, siji mbele Zako nikiwa tu na imani yangu, bali na imani uliyompa malaika-mjumbe wako wa saba mwenye nguvu.

Ee Bwana Mungu, nakuomba uturehemu. Na jalia kila mwanamume na mwanamke ambaye ameketi sasa, ambaye ana namna yo yote ya maradhi au mateso; na kama vile Musa alivyojitupa mwenyewe katika pengo, kwa ajili ya watu, usiku wa leo ninaweka moyo wangu mbele Zako, Bwana. Na kwa imani yote niliyo nayo, ambayo iko ndani Yako, ambayo Wewe umenipa, ninawapa.

Nami ninasema: nilicho nacho, nawapa wasikizi hawa! Kwa Jina la Yesu Kristo wa Nazareti, kataeni magonjwa yenu, kwa sababu Yeye aliye ndani yenu ni mkuu, kuliko huyo Ibilisi anayejaribu kuyatwaa maisha yenu. Ninyi ni wana wa Mungu. Mmekombolewa.

Imekwisha. Neno Lake haliwezi kushindwa. Chochote tunachohitaji, tunaweza kukipokea.

Njooni muungane nasi Jumapili saa 6:00 SITA MCHANA, saa za Jeffersonville, ( Ni saa 2:00 MBILI USIKU ya Afrika Mashariki) kupokea baraka hii kuu na upako kutoka kwa Mungu pindi sehemu ya Bibi-arusi watakapokusanyika kutoka duniani kote kusikiliza Sauti ya Mungu akiweka IMANI yake pamoja na IMANI yetu.

Ndugu. Joseph Branham

63-1110E Yeye Aliye Ndani Yenu

24-0107 Nafsi Zilizo Kifungoni Sasa

UJUMBE: 63-1110M Nafsi Zilizo Kifungoni Sasa

PDF

pakua – m4a

pakua – amr

BranhamTabernacle.org

Wapendwa Watu Waliotengwa,

Mungu amekuja katika wakati wetu na kujifunua katika mwili wa mwanadamu, katika mtu aitwaye William Marrion Branham, ili aweze kulitimiza Neno Lake. Huo ndio Ufunuo wa Yesu Kristo katika wakati wetu.

Kuisikiliza Sauti hiyo na kuamini kila Neno ndiyo Njia pekee iliyoandaliwa na Mungu kwa ajili ya siku hii. Alituma ulimwenguni watu wengi waliopakwa mafuta na Roho wake Mtakatifu, lakini Yeye alituma na kunena kupitia mtu mmoja tu kufunua Neno Lake na kumwongoza Bibi-arusi Wake.

Yeye kamwe habadilishi Mpango Wake wala Njia Yake ya kufanya mambo. Jinsi alivyolifanya mara ya kwanza, Yeye hulifanya jinsi hiyo kila wakati. Yeye huwaongoza watu Wake Mwenyewe, kwa Nguzo ya Moto.

Usisahau kamwe, WEWE NI Bibi-arusi mteule wa Mungu na hakuna kitu shetani anachoweza kufanya au kusema ambacho kinaweza kuliondoa hilo kutoka kwako, HAKUNA! Alikuchagua wewe tangu asili kabla ya kuwekwa misingi ya ulimwengu. Alikujua tangu wakati huo, nawe ulikuwa pamoja Naye. Alijua jina lako. Alijua kila kitu kukuhusu. Alijua heri na shari zako. Alijua kushindwa kwako, makosa yako, na bado alikupenda na kukuchagua wewe kwa kuwa ulikuwa sehemu yake.

Nafsi yako inaweza tu kujilisha kwenye Neno Lake. Hakuna kinachoweza kukutosheleza ila Neno Lake. Unapenda kusoma Neno Lake na kumtafakari Yeye, ukiomba kutoka katika kilindi cha moyo wako. Unaposikia Sauti Yake ikizungumza nawe moja kwa moja, inakuinua hadi ng’ambo ya pazia la wakati. Kwa maana unajua umeketi naye katika ulimwengu wa roho wakati anaponena nawe mdomo kwa sikio, akifunua Neno lake, akikukumbusha, WEWE NI BIBI-ARUSI WANGU.

Ibilisi aweza kukutwanga na kukutwanga. Waweza kushushwa moyo sana wakati mwingine na kuhisi wewe ni aliye shindwa kabisa; ujisikie kana kwamba umemkosa Yeye zaidi ya yeyote yule. Wewe ndiye mbaya zaidi kuliko wabaya wote, lakini mahali fulani, chini kabisa ndani ya nafsi yako, unasikia ile Sauti Ndogo Tulivu ikikuambia: “Hakuna kitu kinachoweza kukutenganisha na MIMI, WEWE NI NENO LANGU. Nililiweka jina lako kwenye Kitabu Changu Cha Uzima cha Mwana-Kondoo, Mimi Mwenyewe .”

Naweza kusema nini kuwatia moyo leo?

Kaeni tu katika Neno. BONYEZENI PLAY kila siku na mwisikie Sauti ya Mungu ikisema Bwana Asema hivi na kuwaambia; Ninawaunganisha katika Neno Langu. Mnaweza kushinda CHOCHOTE, kwa maana Neno Langu linaishi na kukaa ndani yenu. Nimewathibitishieni, mnayo IMANI KAMILIFU. Mmeiweka ile Ishara, nayo imewaweka katika Kudhikika. Nitasimama nyuma ya Neno Langu. Nitafanya kile nilichosema kuwa nitafanya.

Maneno Yake ni ya ajabu jinsi gani anayosema nasi kwenye Kanda. Tunajua si mtu fulani, mtu wa kimwili ambaye yuko miongoni mwetu. Ni Mungu wa Milele anayezungumza nasi, Bibi-arusi Wake.

Mnaalikwa kuungana na Bibi-arusi Jumapili hii saa 06:00 MCHANA, saa za Jeffersonville,( Ni saa MBILI USIKU ya Afrika Mashariki ) tunapokusanyika kusikiliza ile Sauti Ndogo Tulivu:  63-1110M Nafsi Zilizo Kifungoni Sasa.

Ndugu. Joseph Branham

Maandiko ya kusoma kabla ya ibada:

Mwanzo 15:16
Mathayo 23:27-34
Yohana 4:23-24 / 6:49 / 14:12
1 Petro 3:18-22
2 Petro 2:4-5
Yuda 1:5-6

23-1231 Kukata Tamaa

UJUMBE: 63-0901E Kukata Tamaa

PDF

pakua – m4a

pakua – amr

BranhamTabernacle.org

Baba mpendwa,

Tumecheza muda mrefu vya kutosha. Tumehudhuria kanisa muda mrefu vya kutosha. Tangu kuusikia Ujumbe, ile Ishara, imemtupa Bibi-arusi Wako katika hali ya kudhikika.

Tunajua jambo fulani linakaribia kutukia. Wakati umekaribia. Tunataka Uje ututoe katika ulimwengu huu. Tunataka kuwa pamoja na Wewe. Tunahisi hali ya kudhikika ndani kabisa ya nafsi zetu.

Je! hivi tutalizungumzia tu? Je! tumedhikika vya kutosha? Je! tunakulilia Wewe mchana na usiku kama tunavyopaswa?

Loo, Kanisa, amka na ujitikise! Finya dhamira yako, amka katika saa hii! Hatuna budi kukata tamaa ama tutaangamia! Kuna jambo linalokuja kutoka kwa Bwana! Ninajua jambo hilo kwamba ni BWANA ASEMA HIVI. Kuna jambo linalokuja, na ni afadhali tukate tamaa. Ni kati ya uzima na mauti. Litapita katikati yetu wala hatutaliona.

Tunajua inahitaji hali ya kudhikika kukuleta Wewe jukwaani. Hatuna budi Tulipate sasa hivi ama tuangamie. Bwana, tujalie tudhikike kuliko hapo awali, ndipo utajitokeza jukwaani na kuja kumchukua Bibi-arusi Wako anayengoja.

Tusaidie Baba kujiingiza kwa nguvu. Si kutembea tu na kuingia ndani Yake kwa urahisi, bali kujiingiza ndani yake kwa nguvu. Sio tu kulizungumzia na kuendelea na maisha yetu ya kila siku. Tunataka kukutafuta kwa mioyo yetu yote, kwa roho zetu zote na kwa akili zetu zote. Bwana, tusaidie.

Tunajua tumekukosa mara nyingi, Bwana, lakini ulituambia kama tukishindwa, hilo halina uhusiano wo wote na jambo hilo; sisi ni wenye kushindwa kwanza, lakini tuna Wewe umesimama hapo na mkono wenye nguvu na unaweza kutushika chini na kutuinua juu ya maji.

Nabii alitutangazia ya kwamba Wewe ungepita juu yetu wakati tu unapoona ile Ishara ikiwa imewekwa. Bwana, tumefuata maagizo Yako na tumeiweka ile Ishara na kufanya nyumba zetu kuwa Kanisa la Kanda, tukisikiliza na kuamini kila Neno.

Yeye hutambua tu I—Ishara. Huo ndio Ujumbe wa wakati huu! Huo ndio Ujumbe wa siku hizi! Huo ndio Ujumbe wa wakati huu! Katika Jina la Yesu Kristo, upokeeni!

Sisi tuna Hakika kabisa, na tunaamini na kuweka kila kitu kulingana na yale nabii aliyotuambia.

Tunaamini kila kitu kinafanyika na hutokea kwa wakati Wako mkamilifu. Hakuna kitu kilicho nje ya mahali. Tumeiona miujiza Yako yote, nasi tumesikia na kuja chini ya ushahidi wa ile Ishara.

Sasa wakati tukiwa chini ya ushahidi wa ile Ishara, tutaula Ushirika Jumapili hii katika hali ya kudhikika. Kwa maana tunajua Wewe uko tayari kutoa hukumu.

Jalia tuule kama mfano wa Pasaka, wakati ilipoliwa kwa dharura, katika wakati wa kudhikika. Tupo katika kudhikika tena leo Baba.

Tunashukuru, Bwana, kwamba tunaweza kutazama nyuma kwenye mwaka huu na kuona yote ambayo umetufanyia. Umelifunua Neno Lako na kutupa Ufunuo juu ya Ufunuo kuliko hapo awali.

Sasa tunajua sisi ni wana na binti Zako. Sisi ndiye Bibi-arusi-Neno kamilifu Wako ambaye Umemngojea kwa muda mrefu sana. Ni Wewe, unayeishi na kukaa ndani yetu. Ulituchagua, ukatujua sisi tangu zamani na sasa unakuja kutuchukua.

Bwana, jalia tukutafute mchana na usiku. Na tuwe wenye kudhikika sana kukulilia Wewe. Jalia tujiingize kwa nguvu zaidi ya tulivyowahi kufanya hapo awali. Huu ukawe ndio mwaka wewe utakaokuja kutuchukua. Tunakupenda Baba, na tunataka kuwa katika Mapenzi yako makamilifu. Njoo uwe nasi tunapoungana saa 11:00 KUMI NA MOJA JIONI, saa za Jeffersonville, kuizunguka Sauti Yako na kukusikia Wewe ukituambia jinsi ya kuingia katika : Kudhikika (Kukata Tamaa) 63-0901E. Kisha uwe pamoja nasi tunaposhiriki katika kudhikika, Meza ya Bwana.

Hizi ndizo siku kuu za maisha yetu Baba. Kwa maana tunajua Unakuja upesi kutupeleka kwenye Makao yetu ya Baadaye pamoja nawe. Tunatazamia kila siku kwa hamu kubwa wale watakatifu ambao wametutangulia. Tunajua pindi tuwaonapo, ule wakati wa kuja kwako umefika….UTUKUFU!!!

Tuko katika hali ya Kudhikika kwa ajili ya siku hiyo, Baba.

Ndugu. Joseph Branham.

Maandiko ya kusoma kabla ya ibada:

Kutoka 12:11
Yeremia 29:10-14
Luka 16:16
Yohana 14:23
Wagalatia 5:6
Yakobo 5:16

23-1224 Kwa Nini Bethlehemu Mdogo?

UJUMBE: 58-1228 Kwa Nini Bethlehemu Mdogo?

PDF

BranhamTabernacle.org

Mpendwa Bibi-arusi Aliyeweka Ile Ishara,

Ningependa sote tujitayarishe kwa ajili ya ibada ya kipekee sana ya Ushirika wa Nyumbani katika Mkesha wa Mwaka Mpya, Jumapili, Tarehe 31 Desemba. Tutausikia Ujumbe, 63- 0901E Kudhikika, ambao Ndugu Branham anaingia katika ibada ya Ushirika na ya kutawadhana Miguu kuelekea mwisho wa kanda.

Kwenye Voice Radio Ujumbe utachezwa(kwa Kiingereza peke yake), na mfuate mpangilio wa ibada kama jinsi tulivyofanya katika ibada zilizopita za Ushirika wa Nyumbani, ikiwemo muziki wa piano wakati wa sehemu ya ibada ya Ushirika, na Nyimbo za Injili wakati wa Kutawadhana Miguu. Tutaanza ibada saa 11:00 KUMI NA MOJA JIONI. majira ya Jeffersonville. Kwa wale ninyi mlio nchi za ng’ambo, tafadhali jisikieni huru kuicheza kanda hii na kushiriki Ushirika katika masaa ya nchi zenu ili mshiriki Ushirika kabla ya saa sita usiku ya 2023.

Siwezi kufikiri njia bora zaidi tunayoweza kuumaliza mwaka huu wa 2023, na kuuanza mwaka mpya wa kumfanyia kazi Bwana katika 2024, kuliko kunyamaza mbele zake, kudhikika zaidi Kwa ajili yake, kushiriki Meza Yake, kuombea na kusameheana mmoja kwa mwingine, kuiosha miguu ya watakatifu Wake, na kulisikia Neno Lake. Hii itakuwa jioni ya kipekee iliyoje.

Zilizoorodheshwa hapa chini ni anuani za njia za kupata na kutayarisha divai na mkate wa Ushirika.

Ninashukuru sana kwamba Bwana ameiandaa njia kwa sisi kuungana pamoja kwa ajili ya hili tukio takatifu jinsi hii. Hakika natazamia kukutana nanyi nyote Mezani Pake.

Jumapili hii, tutasikia ujumbe wa Krismasi: Kwa nini Bethlehemu Mdogo? 58-1228 saa 6:00 SITA MCHANA. saa za Jeffersonville.( Ni saa 2:00 MBILI USIKU ya Afrika Mashariki)

Mungu awabariki,

Ndugu Joseph Branham

Jumapili, Desemba 24, 2023

58-1228 Kwa Nini Bethlehemu Mdogo?
saa 6:00 SITA MCHANA. Saa za Jeffersonville ( Ni saa 2:00 MBILI USIKU ya Afrika Mashariki )

Jumapili, Desemba 31, 2023

63- 0901E Kudhikika/pamoja na Ushirika wa Nyumbani na Kutawadhana Miguu
Saa 11:00 KUMI NA MOJA JIONI saa za Jeffersonville

https://branhamtabernacle.org/en/streaming/viewservice/259609A1-17BB-458F-A4AC-C3EBFF4D53E8

https://branhamtabernacle.org/en/articles/view/1212021_InstructionsToObtainCommunionWineFeetWashingBins

23-1217 Ile Ishara

UJUMBE: 63-0901M Ile Ishara

PDF

BranhamTabernacle.org

Mpendwa Kipenzi Changu,

Moyo wangu unabubujika tu ninapowaona ninyi nyote mkikusanyika pamoja kuizunguka Sauti Yangu, mkisikia Neno Langu, ninapozungumza nanyi kupitia malaika Wangu.

Inanifurahisha sana kujua kwamba mnao Ufunuo wa ni nani niliyemchagua kuwa Sauti Yangu kwenu. Kuamini kila Neno alilonena halikuwa neno lake, bali Neno Langu kwenu.

Hiyo ilikuwa ni ya muhimu sana Kwangu, Nikaifanya irekodiwe na kuhifadhiwa kwa ajili yenu, ili mweze kuisikia tena na tena. Sikutaka kamwe msahau nilichosema kutoka moyoni Mwangu. Nilijua ya kwamba hiyo ingekuwa ndio njia pekee ningeweza kuwapa ninyi ile Imani Kamilifu mliyohitaji, ili tuweze kuwa pamoja.

Daima nimemtumia mtu mmoja kunena na kulifunua Neno Langu kwa Bibi-arusi Wangu. Jinsi ile tu nilivyofanya na Musa. Kile alichoagiza, ndicho alichopata, kwa maana alinena tu Maneno Yangu. Hata nilimwambia yeye, nitakufanya wewe mungu. Utakuwa mungu, na Haruni atakuwa nabii wako. Nitachukua sauti yako, nami nitaumba kwa kukutumia wewe. Nami nitanena, nao watu hawawezi kuikana. Lolote UTAKALOSEMA, litatendeka.

Sasa mmeipata Imani Kamilifu katika Neno Langu, si kwamba mnatambua tu ni nani Niliyewatumia kuwa Sauti Yangu, lakini sasa mnatambua kwamba Neno Langu linaishi na kukaa ndani yenu, hilo limekupa IMANI KAMILIFU.

Mnajua ninyi ni nani.
Mnakaa ndani Yangu, na Neno Langu ndani yenu. Ombeni mtakalo; nanyi mtapewa. katika Jina Langu mtatoa pepo; si, Mimi nitatoa, NINYI MTATOA. Kama NINYI mkiuambia mlima huu; si kama Mimi Nikiuambia, Kama NINYI mkiuambia mlima huu.

Adui yako hana nguvu tena juu yako. Wewe na Neno Langu ni MMOJA. Ikiwa una watoto ama wapendwa wako ambao hawako mahali wanapopaswa kuwa, wadai. Kama Ilifanya kazi kwako, basi itumie IMANI yako KAMILIFU katika NENO LANGU KAMILIFU linalokaa ndani yako, nawe waweza kupokea uombacho.

Lo, nimengoja kwa muda mrefu sana wewe kujitambua ni nani. Kukuona ukijiweka mwenyewe tayari kwa kulisikia Neno Langu. Nimefurahishwa sana hatimaye wakati huo umefika.

Hilo Neno Kamilifu nililonena na kuwahifadhia ninyi ndilo Ishara Yangu kwa kila mwamini leo. Ni Roho Mtakatifu; si damu, kemia, bali ni Roho Wangu Mtakatifu, Neno Langu, linaloishi na kukaa ndani yenu.

Saa ambayo hiyo Ishara haina budi kuonyeshwa waziwazi imewadia. Huna budi kuibeba Ishara pamoja nawe usiku na mchana; sio tu Jumapili, huna budi Kubonyeza Play wakati wote.

Yeye hutambua tu I—Ishara. Huo ndio Ujumbe wa wakati huu! Huo ndio Ujumbe wa siku hizi! Huo ndio Ujumbe wa wakati huu! Katika Jina la Yesu Kristo, upokeeni!

Nje huko kuna jumbe nyingi, lakini Sauti Yangu ndio Ujumbe wa wakati huu. Huna budi kupokea na kuamini kila Neno. Haina budi kuwekwa wakati wa jioni.

Ninyi kote ulimwenguni, mnaosikiliza kwenye kanda, ishara ya wakati huu iko hapa. Kuna Ishara ambayo haina budi kuwekwa, na haingalikuja wakati mwingine wo wote …mnalipata?

Njoo uiweke ile Ishara Yangu maishani mwako pamoja na Bibi-arusi wangu Jumapili hii saa 6:00 saa SITA MCHANA, saa za Jeffersonville (Ni saa 2:00 MBILI USIKU ya Afrika Mashariki ) tunapousikia Ujumbe Wangu kwa Bibi-arusi: ile Ishara 63-0901M.

Ndugu. Joseph Branham

Maandiko ya kusoma kabla ya kusikiliza Ujumbe:

Mwanzo 4:10
Kutoka sura ya 12
Yoshua sura ya 12
Matendo 16:31 / 19:1-7
Warumi 8:1
1 Wakorintho 12:13
Waefeso 2:12 / 4:30
Waebrania 6:4 / 9:11-14 / 10:26-29 / 11:37 / 12:24 / 13:8, 10-20
Yohana 14:12

23-1210 Imani Kamilifu

UJUMBE: 63-0825E Imani Kamilifu

PDF

BranhamTabernacle.org

Mpendwa Bibi-arusi mwenye Imani Kamilifu,

IMANI yetu huja kwa kusikia, kulisikia Neno. Neno humjia nabii.

Nabii ni:

Neno lililofanyika mwili! Haleluya! Neno likitenda kazi katika mwili wa mwanadamu, kwa ishara za kimwili kwa ishara za vitu, kwa ishara za Kimaandiko, kikamilifu, kuwaleteeni Imani Kamilifu kwa ajili ya Kunyakuliwa Kukamilifu.

Sisi tunafanya kile hasa Neno linasema tufanye kwa kuisikia Sauti ya Mungu pekee iliyothibitishwa ikinena na kufunua Neno Lake kupitia mwili wa mwanadamu ili kutupa Imani Kamilifu.

Inakupasa…masikio yako ni bubu kwa kinginecho chote isipokuwa neno analosema Roho. Unaona? “Kwake yeye aliye na sikio ( linalosikiza ), aone neno ambalo Roho ayaambia makanisa”; yeye aliye na mahali pa kusikizia, ambapo panapokea neno ambalo Roho ayaambia makanisa. Waona?

Sisi ndio mahali pake pa kusikizia ambapo panalipata na kuliamini kila Neno. Anapotupa amri: “Semeni tu yale yaliyo kwenye hizo kanda. MIMI NI Sauti ya Mungu kwenu. Mnaniita mimi mchungaji wenu, nanyi mwanena vema, maana ndivyo Nilivyo.” Sisi tunayatekeleza. Cho chote Asemacho, hamna tashwishi kamwe tunatembea moja kwa moja. Lolote Bwana anenalo kupitia nabii Wake, hamna mtu ulimwenguni anayeweza kutushawishi vinginevyo, tunaendelea vivyo hivyo.

Sasa unafikia Imani Kamilifu , ukamilifu mtimilifu usioweza kushindwa. Imani hiyo haishindwi.

Sasa tunayo Imani Kamilifu katika Neno Lake. Sisi hatujitazami wenyewe. Hatuogopi lolote, kama Ayubu. Hatuogopi kuyatazama mawimbi makubwa na kuzama ndani ya maji kama Petro. Siku hizo zimepita. SASA tunalitazama lile Neno Kamilifu linaloishi na kukaa ndani yetu. Tunafikia asili ya Bibi-arusi. Tunafikia katika hali ya kunyakuliwa.

Tunapoomba, tunaamini kwamba tunapokea kile tunachoomba, nasi tutakipokea; tutapewa. Wakati, mahali, hakuna kitu kitakachokibadilisha. Tunajua imetendeka. imekwisha Tayari. Tunajuaje? Kwa sababu si Neno letu, bali ni NENO LAKE, ambalo amesema na kutupa sisi. Tuna NGUVU NA IMANI KAMILIFU YA KULINENA.

Kama vile Yesu alivyofanya kwa ajili yake Mwenyewe, tunatambua mahali petu; sisi ni nani. Jambo pekee tunalopaswa kufanya basi, ni kuwa na imani na kile tulicho. Tuwe na imani katika kile NENO linasema tulicho! Ndipo Neno la Mungu linakuja ndani yetu na kujidhihirisha Lenyewe; kwa maana sisi ni waamini. Na mwamini ni “imani ya Mungu inayotenda ndani yetu.”

Na sasa, tunakuwa watiwa mafuta kwa Roho yuyo huyo, masihi watiwa mafuta, masihi wa siku za mwisho, kuangaza ufufuo wa Yesu Kristo; kuonyesha ya kwamba si mfu, bali yuko katika umbo la Roho Mtakatifu, yu ndani ya watu Wake, akitembea kati ya Bibi-arusi Wake, akimfanyia mapenzi, akijimwaga Mwenyewe Kwake. Wanakuwa mmoja kwa ajili ya Karamu ya Arusi; na ishara zile zile, zilizoahidiwa na Mungu yule yule, katika Neno lile lile zinafanya madhihirisho yale yale Yake.

Hamna kilichobaki kwetu ila kuliamini, na kwa Kuliamini ndiyo hakika ya mambo inayoumba Imani Kamilifu. Sikiliza hilo tena, KWA KULIAMINI NDIYO HAKIKA YA MAMBO INAYOUMBA IMANI KAMILIFU.

Je! kunacho kiungo katika mwili wako kinachotilia shaka hata Neno moja: HAPANA
Je! unaamini kila Neno: Ndiyo
Je! Amekupa Ufunuo wa Ujumbe huu: Ndiyo
Je! Ni Bibi-arusi peke yake ndio watakaokuwa na huo Ufunuo wa kweli: Ndiyo
Je! unajua wewe ni Bibi-arusi Wake: Ndiyo
Je! Alisema kwa kuamini kila Neno itakupa Imani Kamilifu: Ndiyo
BASI WEWE NDIYE BIBI-ARUSI-NENO MWENYE IMANI KAMILIFU!!

Ee Bwana tuandae zaidi ya wakati mwingine tunapokusanyika pamoja Jumapili hii kusikia Neno lako. Tusaidie tusijitazame wenyewe tena, bali tu kuamini Neno Lako ulilonena kwa ajili yetu. Tumeuona Mvuto wa Tatu ukitenda kazi nasi tunajua unakaa ndani yetu. Yatubidi tuwe tunalinena na kuliamini Neno Lako.

Tunajua unamjia hivi karibuni Bibi-arusi-Neno Wako mkamilifu. Lolote tunalohitaji, Baba, LOLOTE TUNALOHITAJI, tunajua tutalipokea. Kwa maana Ni Neno Lako ambalo umekwisha kulinena kwa ajili yetu. Hakuna lingine lakufanya ila KULIAMINI tu. Tunaliamini Baba, tunaliamini. Sasa hebu na tulitendee kazi NENO LAKO.

Tunakiri kushindwa kwetu, dhambi na makosa yetu yote. Tutazame kupitia Damu ya Mwanao ambapo tunahesabiwa haki kwa Neema na rehema zako. Jalia kuwe na badiliko ndani ya Bibi-arusi Wako zaidi ya hapo awali. Na Utumiminie Roho wako Mtakatifu na kutupa yote tunayohitaji.

Wagonjwa wataponywa magonjwa yote. Aliyerudi nyuma atarudi kwenye Neno. Bibi-arusi wako ulimwenguni kote wataona njia yako iliyoandaliwa kwa ajili ya siku hii na kuamini.

Kama huna mtu wa kukuwekea mikono…wewe jiwekee mikono yako mwenyewe…wewe ni mwaminio. Umekuwa Neno; unakuwa Neno, unapolipokea Neno.

Njoo Bwana Yesu, Bibi-arusi Wako anajiweka mwenyewe tayari kwa kukaa katika uwepo wa Neno Lako, kuivishwa. Tunataka kupambwa na kuvikwa kwa Neno lako.

Njoo ututie mafuta zaidi ya hapo kabla Jumapili hii saa 6:00 SITA MCHANA, saa za Jeffersonville, ( Ni saa 2:00 MBILI USIKU ya Afrika Mashariki ) wakati sehemu ya Bibi-arusi wako inapokusanyika kukusikiliza WEWE ukinena na kutufunulia jinsi ya kupata: Imani Kamilifu 63-0825E.

Ndugu. Joseph Branham

Maandiko ya kusoma kabla ya ibada:

Marko 11:22-26 / 16:15-18
Yohana 14:12 / 15:7
Waebrania 11:1 / 4:14
Yakobo 5:14
1 Yohana 3:21

23-1203 Ninawezaje Kushinda?

UJUMBE: 63-0825M Ninawezaje Kushinda?

PDF

BranhamTabernacle.org

Mpendwa Yungiyungi la Kidimbwini,

Jinsi gani mioyo yetu ilivyoruka kwa furaha Jumapili tulipomsikia Bwana wetu akinena na kutuambia kile kinachotendeka sasa hivi. Tunaungana na Neno na kuwa MMOJA Naye. Hivi karibuni sana tutaungana na watakatifu waliotutangulia kuwa WAMOJA nao. Kisha sisi sote pamoja tutaungana na Kristo kama MMOJA kwenye Karamu ya Arusi ya Mwana-Kondoo.

Ni furaha iliyoje iliyojaza nafsi zetu wakati Alipotuambia kuwazia kwamba katika dakika moja, katika kufumba na kufumbua jicho, ulimwengu hata hautajua kinachoendelea; lakini kwa ghafula, tutawaona mbele ya macho yetu wapendwa wetu walioondoka, nasi tutaungana nao tena.

Ni matarajio yaliyoje yanayojaza mioyo yetu kuwazia, kwa ghafula, tutawaona wamesimama mbele yetu baba zetu, mama zetu, kaka, dada, waume, wake, watoto, hata nabii wetu. TUTAWAONA, KATIKA MWILI!!

Tutajua papo hapo, hili NDILO; wakati umefika, tumefaulu, IMEKWISHA. Nena kuhusu changamko kwa Ufunuo!! Nikiliwazia na kulinena tu sasa hivi, naweza kuwasikia mkipaza sauti, UTUKUFU, HALELUYA, JINA LA BWANA LIHIMIDIWE.

Ni Wakati wa jinsi gani tunaokuwa nao, tukila barua hizi za mapenzi tulizoachiwa. Barua za mapenzi tunazoweza kuzichomoa wakati wowote tunapotaka na kuzisoma tena na tena na tena. Si hivyo tu, bali na KUBWA ZAIDI, tunaweza KUMSIKIA Bwana wetu Mwenyewe akisema kupitia midomo ya mwanadamu na kutuambia, “Nilizihifadhi barua hizi za mapenzi kwa ajili yako tu, kipenzi Changu. Nilijua wakati ungefika ambao ungehitaji kunisikia Mimi nikikuambia jinsi ninavyokupenda na kwamba wewe ni Wangu.”

“Nilitaka kukuambia kila siku adui anapokushambulia, unapopitia mitihani na majaribu yako yote, WEWE NI WANGU. Tayari nimelipa ile gharama. Tayari nimeshinda chochote kile…umenisikia kipenzi? CHOCHOTE unachokihitaji, nimekwisha kushinda kwa ajili yako, kwa sababu Nakupenda”.

“Nilikujua kabla hata ulimwengu haujawepo. Wewe ulikuwa sehemu Yangu WAKATI HUO. Hukumbuki hilo sasa, lakini Mimi ninakumbuka. Usisahau nilichokuambia, wewe ni Mwili wa Mwili Wangu, Roho wa Roho Yangu, Mfupa wa Mfupa Wangu”.

“Ule wakati umefika sasa ambao nimekuwa nikiwaambia. Hakutakuwa na huzuni tena, hakutakuwa na mitihani na majaribu tena; siku hizo zimekwisha. Sasa ni sisi sote tu pamoja Milele yote”.

“Jipe moyo. Endelea kusonga. Kule Kupambazuka kwa siku ile kumekaribia. Mvutano wote unaopitia kila siku ni wa kukuleta karibu na Mimi”.

“Wakati jambo lolote linapokujia, na unaanza kuhisi umevunjika moyo sana, umechoka na huwezi, na kuonekana kama huwezi kuendelea mbele, inakubidi usisahau kamwe, Mimi Niko hapo pamoja nawe. Neno Langu linaishi ndani yako. Wewe ni Neno Langu.”

“Niliwaambia, mnene Neno. Lo lote mtakalo, mkisali, aminini ya kwamba mtalipokea, nanyi mtalipata. Mtapewa jambo hilo. Tayari Mimi nimekwishawashindia jambo hilo”.

Maneno haya yanamaanisha nini kwetu. Yanatuhifadhi kila siku. Linaziinua Roho zetu na kutuweka katika ulimwengu wa Roho pamoja Naye. Tunamwishia tu Mungu na Neno Lake. Tuna kusudi moja, hilo ni Yesu Kristo. Nje ya Hilo, hakuna jambo lingine linalojalisha.

Tumelipata lile Ono. Pazia limevutwa nyuma nasi tunamwona Yeye, Neno Lake lililofanyika mwili, akizungumza nasi kupitia midomo ya mwanadamu. Tuna mapenzi na Neno hili, Ujumbe huu, Sauti hiyo.

Njoo uungane nasi Jumapili saa 6:00 SITA MCHANA, saa za Jeffersonville,( Ni saa 2:00 MBILI USIKU ya Afrika Mashariki ) upate uzoefu uliyo mkuu maishani mwako. Usikie jinsi ya kushinda kila vita ambavyo Shetani anatupa mbele yako. Ujaze moyo wako kwa furaha na shangwe kujua wewe ni Bibi-arusi wa Yesu Kristo.

Ndugu. Joseph Branham

63-0825M Ninawezaje Kushinda?

Maandiko ya Kusoma kabla ya ibada :

Ufunuo 3:21-22