UJUMBE: 63-0318 Muhuri Wa Kwanza
Category Archives: Uncategorized
25-0119 Ufunuo, Mlango Wa Tano Sehemu Ya I
UJUMBE: 61-0611 Ufunuo, Mlango Wa Tano Sehemu Ya I
Wapendwa Wana Wenye Mamlaka,
Ni Majira ya baridi ya ajabu jinsi gani tuliyonayo Roho Mtakatifu anavyoangazia Neno Lake kuliko hapo awali. Mambo ambayo labda tumeyasikia, kuyasoma na kujifunza maisha yetu yote sasa yanawekwa wazi na kufunuliwa zaidi ya hapo awali.
Mwanadamu amengojea kwa maelfu ya miaka kuifikia siku hii hasa. Wote walitamani na kuomba ili kusikia na kuyaona mambo tunayoyaona na kusikia. Hata manabii wa kale waliitamani siku hii. Jinsi gani walivyotaka kuona kule kutimizwa na kuja kwa Bwana.
Hata wanafunzi wa Yesu, Petro, Yakobo, na Yohana, watu waliotembea na kuzungumza Naye, walitamani kuona na kusikia yote yaliyokuwa yamefichwa. Waliomba lifunuliwe na kudhihirishwa katika siku yao, katika wakati wao.
Kote katika zile Nyakati Saba za Kanisa, kila mjumbe, Paulo, Martin, na Luther, walitaka kuzijua zile siri zote zilizokuwa zimefichwa. Haja yao ilikuwa ni kuona kule kutimizwa kwa Neno kukitendeka kipindi wawapo hai. Walitaka kuona kule kuja kwa Bwana.
Mungu alikuwa na mpango. Mungu alikuwa na wakati. Mungu alikuwa na watu aliokuwa akiwangojea…SISI. Katika nyakati zote, wote walishindwa. Bali Yeye alijua, kwa kujua Kwake tangu zamani, kungekuwako na watu: Bibi-arusi wa Neno Lake tukufu na kamilifu. WAO HAWANGEMWANGUSHA YEYE. Hawangepatana HATA KWA NENO MOJA. Wangekuwa Bibi-arusi Neno Wake aliye bikira safi.
Sasa huu ndio wakati. Sasa haya ndio majira. Sisi ndio wale wateule ambao Yeye amewangojea tangu Adamu alipoanguka na kupoteza haki yake. SISI NI BIBI-ARUSI WAKE.
Mungu alimwonyesha Yohana kuonekana kimbele kwa yote ambayo yangetukia, lakini hakujua maana zote. Naye alipoitwa juu, aliona katika mkono wa kuume wake yeye aliyeketi juu ya kile kiti cha enzi kitabu kilichoandikwa ndani, kilichotiwa muhuri saba, lakini hapakuwa na mtu ye yote aliyestahili kukifungua hicho kitabu.
Yohana alipiga kelele na kulia sana kwani yote yalikuwa yamepotea, hakukuwepo na tumaini. Lakini Bwana asifiwe, mmoja wa wale wazee akamwambia, “Usilie, kwa maana tazama, Simba wa kabila la Yuda, Shina la Daudi, Yeye ameshinda kukifungua kile kitabu, na kuifungua muhuri zake saba”.
Huo ulikuwa ndio wakati. Hayo yalikuwa ndio majira. Huyo alikuwa ndiye mtu ambaye Mungu alikuwa amemchagua kuyaandika yote aliyoyaona. Lakini bado, Haikujulikana maana Yake yote.
Mungu alikuwa akingojea na kungojea chombo Chake kiteule, malaika-mjumbe Wake wa saba, aje duniani, ili Yeye aweze kuitumia sauti yake kuwa Sauti Yake, kwa Bibi-arusi Wake. Yeye alitaka kunena mdomo kwa sikio ili KUSIWEKO KUTOELEWA. Yeye Mwenyewe, alitaka kunena na kuzifunua siri Zake zote kwa Bibi-arusi Wake Kipenzi, mpendwa, aliyechaguliwa tangu awali, mkamilifu…SISI!!
Jinsi ambavyo Yeye ametamani kutuambia mambo haya yote ya ajabu. Kama vile mwanamume anavyomwambia mke wake kwamba anampenda mara kwa mara, na yeye hachoki kulisikia hilo, Yeye anapenda kutuambia mara kwa mara kwamba anatupenda, alituchagua, alitungojea, na sasa anakuja kutuchukua.
Yeye alijua jinsi gani tungependa kumsikia Yeye Akilisema tena na tena, kwa hiyo akaifanya Sauti Yake irekodiwe, hivyo Bibi-arusi Wake angeweza ‘Kubonyeza Play’ siku nzima, kila siku, na kulisikia Neno Lake likiijaza mioyo yao.
Bibi-arusi Wake kipenzi amejiweka tayari kwa kujilisha Neno Lake. Hatutasikiliza kitu kingine cho chote, Sauti Yake tu. Tunaweza tu kutumia Neno Lake Safi lililotolewa.
Tuko chini ya matarajio makubwa. Tunalihisi hilo ndani ya nafsi zetu. Yeye anakuja. Tunausikia muziki wa harusi ukicheza. Bibi-arusi anajitayarisha kutembea kwenye marefu ya ukumbi. Kila mtu asimame, Bibi-arusi anakuja kuungana na Bwana Arusi wake. Yote yamekwisha tayarishwa. Wakati umefika.
Yeye anatupenda zaidi ya yeyote yule. Tunampenda zaidi ya yeyote yule. Tunakwenda kuwa Mmoja na Yeye, na wale wote tuwapendao, milele.
Unaalikwa kuja kujiweka mwenyewe tayari kwa ajili ya harusi pamoja nasi Jumapili saa 06:00 SITA MCHANA, saa za Jeffersonville,(Ni saa 2 MBILI USIKU ya Afrika Mashariki) tunapoisikia Sauti ya Mungu ikifunua Ufunuo, Mlango Wa Tano Sehemu ya I 61-0611.
Ndugu. Joseph Branham
21-0117 Pengo Kati Ya Nyakati Saba Za Kanisa Na Ile Mihuri Saba
UJUMBE: 63-0317E Pengo Kati Ya Nyakati Saba Za Kanisa Na Ile Mihuri Saba
- 25-0309 Pengo Kati Ya Nyakati Saba Za Kanisa Na Ile Mihuri Saba
- 23-0716 Pengo Kati Ya Nyakati Saba Za Kanisa Na Ile Mihuri Saba
- 22-0123 Pengo Kati Ya Nyakati Saba Za Kanisa Na Ile Mihuri Saba
- 21-0117 Pengo Kati Ya Nyakati Saba Za Kanisa Na Ile Mihuri Saba
- TAI WANAKUSANYIKA PAMOJA
- 19-0324 Pengo Kati Ya Nyakati Saba Za Kanisa Na Ile Mihuri Saba – Preliminari
- 17-0319 Pengo Kati Ya Nyakati Saba Za Kanisa Na Ile Mihuri Saba
21-0110 Mungu Akijificha Kwa Urahisi, Halafu Akijifunua Kwa Jinsi Hiyo
UJUMBE: 63-0317M Mungu Akijificha Kwa Urahisi, Halafu Akijifunua Kwa Jinsi Hiyo
- 25-0302 Mungu Akijificha Kwa Urahisi, Halafu Akijifunua Kwa Jinsi Hiyo
- 23-0709 Mungu Akijificha Kwa Urahisi, Halafu Akijifunua Kwa Jinsi Hiyo
- 22-0116 Mungu Akijificha Kwa Urahisi, Halafu Akijifunua Kwa Jinsi Hiyo
- 21-0110 Mungu Akijificha Kwa Urahisi, Halafu Akijifunua Kwa Jinsi Hiyo
- 19-0317 Mungu Akijificha Kwa Urahisi, Halafu Akijifunua Kwa Jinsi Hiyo
- 17-0318 Mungu Akijificha Kwa Urahisi, Halafu Akijifunua Kwa Jinsi Hiyo – Preliminari
21-0103 Ufunuo, Mlango Wa Nne Sehemu Ya III
UJUMBE: 61-0108 Ufunuo, Mlango Wa Nne Sehemu Ya III
21-0101 Ufunuo, Mlango Wa Nne Sehemu Ya II
UJUMBE: 61-0101 Ufunuo, Mlango Wa Nne Sehemu Ya II
20-1231 Ufunuo, Mlango Wa Nne Sehemu Ya I
UJUMBE: 60-1231 Ufunuo, Mlango Wa Nne Sehemu Ya I
20-1227 Wakati wa Kanisa La Laodikia
20-1225 Zawadi Ya Mungu Iliyofungwa
UJUMBE: 60-1225 Zawadi Ya Mungu Iliyofungwa
20-1220 Wale Wanawali Kumi, Na Wayahudi Mia Na Arobaini Na Nne Elfu
UJUMBE: 60-1211M Wale Wanawali Kumi, Na Wayahudi Mia Na Arobaini Na Nne Elfu
- 24-1201 Wale Wanawali Kumi, Na Wayahudi Mia Na Arobaini Na Nne Elfu
- 23-0611 Wale Wanawali Kumi, Na Wayahudi Mia Na Arobaini Na Nne Elfu
- 20-1220 Wale Wanawali Kumi, Na Wayahudi Mia Na Arobaini Na Nne Elfu
- NUKUU YA LEO KWA KISWAHILI
- 19-0303 Wale Wanawali Kumi, Na Wayahudi Mia Na Arobaini Na Nne Elfu
- 16-0403 Wale Wanawali Kumi, Na Wayahudi Mia Na Arobaini Na Nne Elfu – Preliminari