All posts by admin5

21-0919 Watiwa Mafuta Katika Wakati Wa Mwisho

UJUMBE: 65-0725m Watiwa Mafuta Katika Wakati Wa Mwisho

PDF

pakua

BranhamTabernacle.org

Mpendwa Bibi-arusi Aliyeteuliwa,

Sababu ya Walioteuliwa, Yesu alisema, hawatadanganywa, ni kwa sababu wao ndio Neno hilo. Hawawezi kuwa kitu kingine. Hawawezi kusikia kitu kingine. Hawajui kitu kingine.

Hakuna kitu kikubwa maishani kuliko kujua kwamba Mungu alimchagua nabii Wake kabla ya kuwekwa misingi ya ulimwengu kunena Maneno haya. Kisha, Aliruhusu Sauti Yake kurekodiwa, kwa hivyo sisi, Bibi-arusi Wake aliyechaguliwa kimbele , tunaweza kurejea nyuma na kusikia Sauti Yake ambayo iliyorekodiwa na kuhifadhiwa, kwa sababu alitaka tujue:

. Sisi ni Neno.
. Hatuwezi kudanganywa.
. Hatuwezi kuwa kitu kingine.
. Hatuwezi kusikia kitu kingine.
. Hatujui kitu kingine.

Yeye Alijua tungehitaji kutiwa moyo leo zaidi ya siku nyingine yoyote katika historia. Vita vingerindima zaidi ya hapo awali. Bibi-arusi wake angejaribiwa. Bali kama angeweza kumkumbusha Bibi-arusi wake wao ni akina nani, wangefurahi mioyoni mwao wakijua wao ndio Wapenzi Wake katika mapenzi Yake Makamilifu.

Chochote kile Shetani anachotutupia, lolote lile tunalopitia,
sasa tunajua, Yeye Anachagua Bibi-arusi, na sisi ndio Bibi-arusi huyo. Hatuonei haya Ufunuo wetu wa Neno. Hatutajaribu kamwe Kumtendea Mungu kazi Bila Mapenzi Yake. Kwetu sisi, ni Chakula cha Kiroho Kwa wakati Wake. Tunatambua kwamba kutakuwepo na Watiwa mafuta katika Wakati wa Mwisho, lakini sisi Tuta KAA NA NENO.

Ikiwa ungependa hakikisho lili hili, njoo uungane nasi Jumapili saa 8:00 nane mchana , saa za Jeffersonville, ( ni saa 3:00 tatu Usiku ya Tanzania) kusikia: 65-0725M Watiwa mafuta Katika Wakati wa Mwisho.

Ndugu. Joseph Branham

Maandiko ya kusoma :

Mathayo Mtakatifu 5: 44-45 / 7:21 / 24: 15-28

Luka Mtakatifu 17:30 / 18: 1-8

Yohana Mtakatifu 14:12

Waefeso 1: 5

2 Timotheo 3: 1-8

Waebrania 6: 1-8 / 11: 4

Ufunuo 10: 1-7 / 16: 13-14

Malaki 4: 5

I Wafalme 22: 1-28

Yeremia: Sura ya 27 yote na 28 yote

21-0912 Chakula cha Kiroho kwa Wakati Wake

UJUMBE: 65-0718e Chakula Cha Kiroho Kwa Wakati Wake

PDF

pakua

BranhamTabernacle.org

Tai wanakusanyika Pamoja.

Mpendwa Kondoo wa Zizi la kondoo wa Mungu,

Katika siku ambazo Bwana wetu Yesu alipokuwa hapa duniani katika mwili, wakosoaji na wasioamini walimwambia:

Hata Lini utatuhangaisha Nafsi Zetu? Kama wewe ndiwe Kristo, utuambie waziwazi.

Kwa mara nyingine, Atazungumza nasi waziwazi na kuwaambia wakosoaji Wake na Bibi-arusi Wake, “Mimi ni mtu anayetoka kwa Mungu, aliyetumwa kutoka kwa Mungu, aliyeteuliwa na Mungu, nikiwa na BWANA ASEMA HIVI ya Kweli . Nimekaa kwa muda mrefu sana katika uwepo wake , nitanena na wewe kama Mungu mwenyewe.

Nataka kusiwe na shaka, na kwako wewe kuamini, mimi ni mjumbe wa Mungu kwako. Ujumbe ambao mimi Ninaounena , na mjumbe, ni kitu kile kile . Sisi ni Mmoja na kitu kimoja. Alinituma kwako kuwakilisha BWANA ASEMA HIVI, Neno kwa Neno.

Kumbuka, Neno la Mungu linasema Yeye hatafanya neno lolote mpaka kwanza anifunulie mimi. Watu wanataka kuweka fasiri zao wenyewe kwa yale ninayosema, lakini Maneno ambayo ninayo Nena na wewe hayahitaji Fasiri yoyote. Wewe sema TU Yale ninayosema.

Nataka pia utambue kwamba Neno lile lile ninalokuambia, pia linaishi ndani yetu. Una mamlaka ya Mungu aliye hai ndani yako. Wewe ndiye Bibi-arusi Kanisa Lililo Hai.

Baada ya Mimi kuondoka, lakini kabla ya ukame kuanza, Mungu amekuandalia mahali pa siri pa kujificha kabla ya hukumu kuipiga dunia. Utakuwa pale unasubiri, unakula Chakula hiki kilichofichwa ambacho atakachokuachia. Utakuwa ukiishi juu ya wema na rehema za Ufunuo wa Yesu Kristo anavyojithibitisha kwako kila siku.

Kwenu ninyi , Kitakuwa Chakula cha Rohoni kwa wakati wake. kingewachefua wengine tumbo. Nitakuwa mnono sana kwao. Lakini kwa ajili yenu, Kondoo Wake, Utakuwa ni Mkate wa Uzima, Yesu Kristo yeye yule jana, leo, na hata milele.

Usisahau, nitakulisha “HUKO”; si mahali pengine, “HUKO”. Watu watakucheka na kusema wewe una kichaa, lakini kile wanachokiita kichaa na Upuuzi , Mungu ataita kikuu . “

Alituambia kwamba huduma kuu ambayo Mungu aliyompa ilikuwa vinafanana kabisa na wakati wa Eliya. Baada ya ukame kuwa unakaribia kwisha, yeye Alimwita atoke na kumpeleka kwenye NYUMBA ya mjane mpaka ukame ulipoisha.

Alisema mjane huyu hakuwa Ameshirikiana na wasioamini au kuchukua alama ya mnyama wakati wa ukame, kwa hiyo alimwita Eliya kumlisha huyu mjane . Alikuwa tayari kufa kwani alikuwa amebaki na keki moja ndogo, kitu kimoja kidogo yule mama alichokuwa anashikilia.

Eliya akamwita huyo mwanamke , “Nipe hicho mimi, kwanza. Kwa kuwa, BWANA ASEMA HIVI, lile pipa halitapunguka wala ile chupa haitaisha, hata siku ile Bwana Mungu atakapoleta mvua juu ya nchi.”

Ilimbidi kumweka Mungu kwanza . Ilimbidi kuamini na kushikilia kila Neno ambalo mjumbe huyo alilosema. Alijua kwamba mjumbe na Ujumbe wake walikuwa kitu kimoja. Maneno aliyomwambia yangetimia , kwa maana ilikuwa Bwana Asema Hivi.

Ndivyo ilivyo leo, ya kwamba Chakula cha Uzima ambacho watoto wanakula, kinafuata Ujumbe wa Mungu, kuwahifadhi katika wakati wa ukame.

Neno lilo hilo limekuja kwetu na liko ndani yetu na tunakula mambo ya siri ya Mungu ambayo ulimwengu umefichwa. Ametufunulia kwamba Ujumbe na mjumbe ni kitu kimoja. Chakula cha kiroho kiko tayari, na kiko katika wakati sasa.

Unakaribishwa kwenye SIKU SIKUU NYINGINE KWA AJILI YA BIBI-ARUSI . Tutatwaa chupa la Mafuta, na Litakuwa Limefurika tena . Kisha tutachota ndani ya pipa la unga, na litajaa tena mpaka juu. Tutaketi mahali pamoja katika ulimwengu wa Roho kutoka kote ulimwenguni, tukiwa tumefichwa mahali petu pa siri, tukiifurahia mana iliyofichwa wakati Mungu anapojithibitisha mwenyewe kwetu.

Njoo ukusanyike katika zizi la Kondoo pamoja nasi Jumapili saa 8:00 nane Mchana , saa za Jeffersonville, (ni saa 3:00 tatu Usiku ya Tanzania)
Tunaposikia Mjumbe wa Mungu akituletea Ujumbe wa Mungu: Chakula cha Kiroho Kwa Wakati Wake 65-0718E.

Sisi tukiwa na dola moja
na senti themanini za kujenga Maskani , watu wengi wa gereji tayari walikuwa wameamua itakuwa gereji yao. Lakini ingali ni zizi la kondoo kwa ajili ya Kondoo wa Mungu.

Ndugu. Joseph Branham

Maandiko ya kusoma

1 Wafalme 17: 1-7
Amosi 3: 7
Yoeli 2:28
Malaki 4: 4
Luka 17:30
Yohana Mtakatifu 14:12

21-0905 Kumtendea Mungu Kazi Bila Mapenzi Yake

UJUMBE: 65-0718m Kumtendea Mungu Kazi Bila Mapenzi Yake

PDF

pakua

BranhamTabernacle.org

Tai wanakusanyika Pamoja.

Mpendwa Kanisa la Sauti Ya Mungu,

Sisi ni Kanisa lake la Sauti Ya Mungu, kipenzi chake Bibiarusi_Neno, na tunangoja kwa hamu kusikia kile Baba atakachonena na kutufunulia Jumapili hii.

Tunayo Sauti ya Mungu iliyo hai kiganjani mwetu. Kwa mguso mmoja wa kidole chetu tunaweza kumsikia Mungu akinena kupitia midomo ya mwanadamu, Maneno ya uzima wa Milele. Kwa kidole kimoja Anasema nasi na kutufunulia siri zote zilizokuwa zimefichwa tangu kuwekwa misingi ya ulimwengu.

Kwa kidole kimoja Anajibu swali lolote tulilo nalo mioyoni mwetu. Kwa kidole kimoja Anatuambia chochote tunachohitaji kujua. Kwa kidole kimoja tunaweza kusikia Sauti ya Mungu ikisema nasi na kutupa Imani ya Kunyakuliwa . Kwa kidole kimoja tunaweza kumsikia Mungu akinena na kutuambia, umeponywa.

Wakati adui anatuambia sisi sio Bibi-arusi wa Mungu, wewe ni uliyeshindwa tu, kwa kidole kimoja tunabonyeza Play na tunaweza kumsikia Baba akinena nasi na kutuhakikishia, “WEWE ni Bibi-arusi wangu mteule. Nilikuchagua kabla ya kuwekwa misingi ya Ulimwengu. ”

Tunaposhushwa Moyo na adui anatushambulia kutoka kila kona, kwa kidole chetu kimoja tunaweza kumsikia akisema nasi na kutamka tu, “Habari za asubuhi Marafiki,” na Amani ya Roho Mtakatifu inakijaza chumba.

Tunaposikia ADUI ANASEMA ninyi mnamfuata tu mtu na mnaweka mengi kumhusu , kwa kidole kimoja tu tunasikia Sauti ya Mungu ikituambia:

Yeye aliniambia ikiwa nitawafanya watu waniamini. Hilo linaonekana kuwa la ajabu mimi kusema hivi, “Unaniamini ?” Kasema, “Je! Haikubidi kumwamini Mungu ?” Unapaswa kuamini hilo. Yakubidi umwamini Mungu na umwamini Kristo, na umwamini Roho Mtakatifu. Halafu baada ya kuwaamini wote, Mungu anakutaka uniamini .

Wakati adui anajaribu kutuambia, “Si Maandiko na ni makosa kukusanyika kwa wakati fulani na kusikiliza tu kanda,” kwa kidole kimoja tu tunasikia Sauti ya Mungu ikituambia:

Na kwa kanisa hili, na kwenye kanda— watu wanaosikiza kanda , na watu katika sehemu zilizounganishwa kwa redio wanaosikiza nchini kote, nawatakeni msikilize hili kwa makini na msikose .

Wakati adui anaposema Ndugu Branham alisema kaa na Neno, sio kanda, kwa kidole kimoja tunasikia Sauti ya Mungu IKIPIGA KELELE kusema:

Nasema vivyo hivyo katika Jina la Yesu Kristo : Usiongeze kitu. Usiondoe—kuliwekea mawazo yako. Wewe sema tu yaliyosemwa katika kanda hizo. Tenda sawasawa kabisa na vile Bwana Mungu amekuamuru kutenda. Usiongezee Kwake!

Sauti hiyo hata hivyo inatueleza jinsi ya kulichunguza kwa Neno ili tusikosee.

Lazima zako tano ndizo hizo. Lazima iwe hivyo;

. Wakati Wake
. Majira Yake
. Mtu yule aliyemchagua
. Lazima ije kwa nabii
. Nabii yule lazima awe nabii aliyethibitishwa

Nabii wetu ni Yesu Kristo.

Neno lililothibitishwa la saa hii !
Neno lililothibitishwa la siku za Musa lilikuwa Yesu. Neno lililothibitishwa la siku za Isaya, Eliya, Yohana, wote, lilikuwa Yesu. Na Neno lililothibitishwa leo ni Yesu, yeye yule jana, leo na hata milele .

Kwa kidole kimoja tunaweza kubonyeza play na kumsikia Yesu Kristo mwenyewe akinena na kutufunulia:

. Huu ndiyo wakati ,
. Haya ndiyo Majira ,
. Huyu ndiye mtu niliyemchagua,
. Huyu ndiye nabii wangu,
. Nabii huyu amethibitishwa zaidi ya manabii Wangu wote wengine .

Leo, sio tu kwamba tuna yule Mungu wa Mbinguni anayetuzungumzia , lakini yeye yuko ndani yetu, anakaa, na anaishi Maisha yake kupitia sisi. Inapita ufahamu wetu.

Hebu na Tujiweke Tayari. Wakati umekaribia. Tunaona Maandiko yakitimizwa kila siku. Ujumbe unasomeka kama habari ya leo:

” Mshangao wa wakati huo, dhiki kati ya mataifa, matetemeko ya nchi mahali mahali, bahari ikivuma, na moyo wa mwanadamu ukikoma kwa hofu “

Hata maumbile yenyewe hutuambia leo, tunapoona mataifa yakivunjika, dunia ikididimia, maandiko kwenye ukuta.

Tunaona kanisa na hali lilimo. Twamuona Bibi-arusi na hali aliyomo. Nasi twajua kwa mambo ya asili kwamba Kanisa linajiweka tayari kuondoka.

UTUKUFU, tunajiandaa kuondoka. Kwa kidole kimoja tu unaweza kujifanya mwenyewe tayari. Ninakualika uungane nasi Jumapili saa 8:00 nane mchana , saa za Jeffersonville,(ni saa 3:00 tatu Usiku ya Tanzania) kusikia: Kumtendea Mungu Kazi Bila Mapenzi Yake 65-0718M.

Ndugu. Joseph Branham

Maandiko ya kusoma Kabla ya ibada :

Kumbukumbu la Torati 4: 1-4 / 4: 25-26
1 Mambo ya Nyakati 13
1 Mambo ya Nyakati 15:15
Zaburi 22
Marko Mtakatifu 7: 7
Yoeli 2:28
Amosi 3: 7
Malaki 3
Mathayo Mtakatifu11: 1-15
1 Wakorintho 13: 1

21-0829 Kuonea Haya

UJUMBE: 65-0711 Kuonea Haya

PDF

pakua

BranhamTabernacle.org

Tai wanakusanyika Pamoja.

Wapendwa Maskani ya Branham,

Tunashukuru sana alituteua Sisi Tangu Asili kuchagua kanisa linalofaa kuziingiza familia zetu.

kama nilikuwa ninachagua kanisa, ningalichagua kanisa la kweli, lenye mafundisho ya kimsingi, linaloamini Injili Yote, kanisa la Biblia, kama ningelikuwa nachagua moja kuwaingiza familia yangu.

Tunashukuru sana tunauambia ulimwengu mchungaji wetu ni Nani, na kwamba tunatenda tu kama yeye.

kama utachunguza tabia ya hilo kanisa, hebu mwangalie tu mchungaji kwa muda mfupi, na mara nyingi utaona ya kwamba kanisa hutenda kama mchungaji wake .

Tunashukuru sana haijalishi tuko wapi ulimwenguni, Yeye hukutana nasi .

Aliahidi kukutana nao popote wawili watatu wamekusanyika pamoja. Hakika. Hapo ndipo mwaminio wa kweli huweka matumaini yake, ni katika hilo Neno la Mungu linalodhihirishwa katika Kweli.

Tunashukuru sana tunamwamini Nabii Wake, na kila Neno lililonenwa.

Kama unaniamini mimi kuwa nabii wa Mungu, sikiliza yale niliyokwambia.

Je! Nabii wake alikuwa ahubiri nini?

Ujumbe mkamilifu , kurudi kwenye Neno ,

Alitumwa kwa kusudi gani?

“ Nenda ukamlete Bibi-arusi huyo!” Ndilo jukumu. Hiyo ndiyo sababu ya mimi kuwapo hapa. Hilo ndilo ninalojaribu kufanya , ni kumwita Bibi-arusi atoke .

Je! Vipi Ikiwa tutatoka nje ya Mstari?

Na hivyo ndivyo nilivyopaswa kufanya , kumweka Bibi-arusi huyo kwenye mstari, nimtafute mtu huyo.

Sasa Baba amemwekea Akiba nini Bibiarusi wake?

Ninarudi nyumbani, nifanye upya nadhiri zangu tena, na kuanza upya.” Kwa hiyo hilo ndilo tunalopanga kufanya, hiyo ndiyo sababu nipo hapa.

Bwana asifiwe, tunaanza lini ibada zetu za kufanya upya?

Halafu basi, Bwana akipenda, Jumapili ijayo asubuhi tutaanza ibada. Nanyi nyote mnisaidie, nasi tutaomba, kwa maana lilikuwa moyoni mwangu kujaribu…Wao walisema, “Vema, tungeenda Louisville ama tungeshuka twende huko New Albany.” Lakini mkutano huo ulipaswa kuwa ni wa Jeffersonville. Nitaenda Louisville na New Albany, katika nyakati tofauti, lakini huu unapaswa kuwa hapa Jeffersonville.

Tuko tayari Baba. Tai wako watakusanyika na kusikiliza. Ni kitu Gani kitakachotukia wakati huu?

“… Ninafikia mahali, ninahitaji imani zaidi.” Hiyo ndiyo sababu niko nyumbani sasa ni kupata ujazo m—mpya wa imani.

Bwana asifiwe, hilo ndilo tunalohitaji pia Baba, Ujazo Mpya wa IMANI.
Tunajua imani huja kwa kusikia, kusikia Neno lako, na Neno lako Linamjia Nabii.

Ujumbe huu, Nguvu za Mwenyezi Mungu , Zimeenea kote ulimwenguni , lakini wakati wa Kutengana unatukia sasa. Mungu anamwita Bibi-arusi, naye shetani analiita kanisa. Sisi ni sehemu ya Ujumbe huu, Neno Lake, Bibi-arusi Wake!

Tuna hakikisho na tunajua tunalozungumzia. Hatuonei haya kwamba tunaamini Ujumbe huu na Mjumbe Wake, kwa kuwa wao ni kitu kimoja. Hatu haya kusema: “Tunaamini kila Neno”. Hatuonei haya kusema: “Tunacheza kanda kanisani mwetu”. Hatuonei haya kusema: “Sisi ni Watu wa Kanda”.

Ni ngumu kwetu kuelewa kwamba mwamini yeyote, au mhudumu wa huduma tano, anayedai kuamini Ujumbe huu, na kusema Ndugu Branham ni Nabii na Mjumbe wa Mungu, Kisha Angeamini na kuwaambia watu kuwa ni makosa na sio kulingana na Neno kucheza hasa Sauti ya Mungu iliyothibitishwa katika kanisa Lao.

Na tuwe tayari, wakati ufaao na wakati usiofaa; karipia, kemea na … kwa uvumilivu wote na mafundisho. Kwa sababu utakuja wakati watakapoyakataa mafundisho yenye uzima ;

ila kwa kuzifuata nia zao wenyewe watajipatia pamoja waalimu makundi makundi ; kwa kuwa wana masikio ya utafiti ;

Nao watageuzwa … _
wasisikie yaliyo kweli ,…
watazigeukia hadithi za uongo .

Inapofikia Neno la Mungu Halisi, lisiloghoshiwa, lililothibitishwa na Mungu, Sauti ya Mungu iliyothibitishwa, Inaonekana kulitahayarisha hata kundi hilo lingine. Wana tahayari kwa jambo hilo nao wanaamini Kwamba kuwa Kanisa la Kanda ni kuwa kinyume cha Neno.

Bali kwetu sisi, Ni Halisi. Hatuonei haya. Wakati tulipopokea Ufunuo huo, kulikuwa na kitu ambacho kilitulia ndani yetu, na sasa hakuna kinachoweza kupachukua Mahali pake. Tunajivunia kuitwa Mmoja wao, Kanisa la Kanda, Kundi la Kanda, Watu wa Kanda.

Tunakualika uje kusikiliza pamoja na Maskani ya Branham kwenye huduma ya Kanda ya Mungu, Jumapili saa 8:00 Nane Mchana, saa za Jeffersonville,( Ni Saa 3:00 Usiku ya Tanzania) tunapokusanyika kwa matarajio makubwa; kuzifanya upya nadhiri zetu tena, na kuanza upya, kwa kusikia: Kuonea Haya 65-0711 .

Ndugu. Joseph Branham

Marko Mtakatifu 8: 34-38

21-0822 Kuchagua Bibi-Arusi

Ujumbe: 65-0429e Kuchagua Bibi-Arusi

PDF

pakua – m4a

pakua – amr

BranhamTabernacle.org

Tai wanakusanyika Pamoja.

Mpendwa Bibi-arusi aliyechaguliwa na Mungu,

Baba alimchagua Bibi-arusi Wake kabla ya kuwekwa misingi ya ulimwengu. Alitaka Bibi-arusi atakayeonyesha tabia Yake. Alitaka Bibi-arusi ambaye angevutia usikivu Wake kwa kushika Neno Lake.

Bibi-arusi ambaye angejitolea sana Kwake na kwa Neno Lake lililoahidiwa, hata Nia ile ile iliyokuwa ndani Yake ingekuwa ndani yao. Wangekuwa mwili Wake uleule, mifupa ile ile, Roho yule yule, kila kitu kile kile, wamejengwa sawa sawa kabisa mpaka hao wawili wangekuwa Mmoja.

Alitaka kuunda tabia Yake hasa ndani yao, kwa maana Anatakiwa awe kama tu Yeye . Amengojea tangu alipoweka Adamu na Hawa wake wa kwanza duniani ili kumrejesha Bibi-arusi wake mkamilifu. Amekuwa akimfikiria sana, kumrudisha katika Dhihirisho lake kamilifu; kwa maana watakuwa Bibi-arusi _Neno Lililonenwa wake.

Alipomwona bibi-arusi, Alifurahi sana, Hatimaye alikuwa na Bibi-arusi ambaye hatapatana hata kwa Neno moja. Bibi-arusi ambaye hangetilia shaka hata moja wapo ya hilo , bali Atalichukua vile tu lilivyo. Wangeuambia ulimwengu Halihitaji Fasiri yo yote, kwa maana ni Sauti Safi Ya Mungu.

Alipokuwa akimwangalia Mke wake kipenzi mdogo mkamilifu , Alijisifia kwa ajili yake, Ilibidi tu amwonyeshe wazi. Kwa hivyo alimwita malaika wake wa 7 mwenye nguvu, ili aweze Kumkagua huyo bibi-arusi kimbele . Alimtaka amwone bibi-arusi, na amwonyeshe wazi, ili aweze kumwelezea huyo Bibi-arusi jinsi alivyo mzuri. Kwa hivyo angeweza kumtia moyo bibi-arusi na kumfanya atambue kwamba yeye Anamjua bibi-arusi ni nani.

Kwa hivyo Alimchukua malaika Wake na kumweka mahali pa juu ili aweze kumkagua bibiarusi kimbele. Alipotazama, Roho wa Mungu akamwambia kusema, “ Huyo hapo Bibi-arusi.” Akatazama, na akawaona NINYI pale. Moyo wake Ulifurahi.

Kila mmoja WENU alikuwa amevaa vazi la kitaifa la huko ambapo mnakotoka: Uswizi, Ujerumani, kote ulimwenguni, kila taifa. Nywele ndefu zilizotengenezwa vizuri huku nyuma, nguo zenye mikono mirefu, na sketi ndefu Nadhifu. NANYI mlikuwa Mkipiga Hatua Taratibu, ” Twendeni, Askari Wakristo, tukitembea kama waendao vitani.” Alipotazama, Tulianza kupiga hatua hata Angani; Tulikuwa Neno.

Asante Baba. Jinsi gani jambo hilo linavyotutia moyo mioyo yetu leo hii. Tunakupenda wewe na Neno lako kwa yote yaliyo ndani yetu. Tunaamini kila Neno. Ujumbe huu unatutoshea kama glavu mkononi.

Tunataka kuwa Bibi-arusi-Neno wako Mkamilifu. Hatujui njia nyingine ya kufanya jambo hilo ila kukaa na Neno lako, hii manna iliyohifadhiwa uliyomwachia Bibi-arusi wako ili ajifanye Mwenyewe tayari.

Tunaona wakati huo umekaribia. Ulimwengu unatetemeka chini yetu kwa Matetemeko ya ardhi. Malaika wako wapelelezi wote wanazunguka karibu . Ulimwengu umepinduliwa-juu-chini. Vita, mapigano, mauaji, virusi na magonjwa kila mahali. Adui anakasirika bila kukoma, anajaribu kumtesa Bibi-arusi Wako, lakini Mke wako kipenzi aliyechaguliwa yuko THABITI akishikilia Neno Lako.

Tusaidie Baba tusitoke nje ya hatua. Hebu na tukuangalie wewe na kushikilia Mkono Wako usiobadilika. Ongeza IMANI yetu, utupe kile tunachohitaji. Njoo uwe na Bibi-arusi wako Jumapili hii, saa 8:00 Nane mchana, saa za Jeffersonville,( ni saa 3:00 Tatu usiku ya Tanzania) tunapokusanyika kuizunguka Sauti Yako kwa ajili ya siku hii na kukusikia Ukinena: Kuchagua Bibi-arusi 65-0429E.

Haya ni Maombi yetu Baba:

Ee Mungu wa Mbinguni, hurumia ulimwengu wenye dhambi na watu wenye dhambi, Bwana, kama tulivyo usiku wa leo. Mungu, ninajaribu kusimama pengoni na kuomba rehema ya Kiungu, kwamba utalizungumzia kundi hili usiku wa leo na kumhamasisha Bibi-arusi Wako, Bwana, akapige hatua taratibu si kwa ishara za kanuni zozote za imani, bali kwa sauti ya Injili ya Bwana Yesu Kristo. Tujalie, Ee Mungu. Na ijulikane, usiku wa leo, ya kwamba Wewe ni Mungu, na Neno Lako ni Kweli. Huku, kwa uchaji, mbele ya macho ya watu hawa, tunawahamasisha Neno Lako.

Ndugu. Joseph Branham

Mwanzo 24: 12-14
Ufunuo 21: 9

21-0815 Ile Mbegu Haitarithi Pamoja na Kapi

Ujumbe: 65-0429b Ile Mbegu Haitarithi Pamoja na Kapi

PDF

pakua

BranhamTabernacle.org

Tai wanakusanyika Pamoja.

Mpendwa Mwili wa Mwili Wake,

Nina furaha sana kwamba Mungu habadilishi nia Yake kuhusu Neno Lake. Yeye ni yeye yule jana, leo na hata milele. Jinsi alivyofanya mambo tangu mwanzo, anafanya vile vile leo. Mungu, Mwenyewe, aliyejidhihirisha katika mwili wa mwanadamu, kwa Damu ya Yesu Kristo, kutakasa maisha ili Aweze kujiakisi mwenyewe kupitia huo .

Mjumbe wetu leo hii ​​ana Utambulisho wake wa Kimaandiko kati yetu. Ni Roho Mtakatifu, Mwenyewe, akijifasiria Mwenyewe. Hakuna haja ya kwenda kutoka kwa hili kwenda kwa Lile ili kupata ukweli au fasiri; Roho Mtakatifu amelipa Kanisa Lake Waefeso 4, yote katika mtu mmoja, nabii Wake aliyethibitishwa.

Mtume : Mtume maana yake ni “aliyetumwa,” au, “mmishenari.” Mimi ni mmishenari.

Nabii : Je! Unaniamini mimi kuwa nabii wa Mungu?

Mwinjilisti : “ Fanya kazi ya mhubiri wa injili. Timiliza huduma yako. Utakuja Wakati watakapoyakataa mafundisho Yenye uzima. “

Mchungaji : Mwaniita, “mchungaji wenu”; nanyi mwasema vema, kwa maana ndivyo nilivyo.

Mwalimu : Nataka kuzungumza juu ya Neno, ama kufundisha somo hili la shule ya Jumapili, juu ya Neno la Ile Ishara .

Ni sawa na = Ninajua ninyi, ndugu zetu, mnanitazama mimi kuwa Yakini kwa kile… maadamu ninamfuata Mungu, kama vile Paulo alivyosema katika Maandiko, “nifuateni mimi, kama mimi ninavyomfuata Kristo.”

Ujumbe huu ni Yakini yetu, hivyo tunamfuata yeye kama anavyomfuata Kristo.

Wala Sipuuzi kuwa kuna wengi ambao Mungu anawaita Waefeso 4 watu ambao wamewekwa na kuitwa na Mungu kutimiza ofisi hizi; kwa NEEMA YAKE, mimi ni mmoja wao. Lakini sisi ni wadogo, nabii malaika wa 7 wa Mungu ndiye MKUU.
Kwa wale ambao kote ulimwenguni huiita “Maskani ya Branham ” “kanisa Lao la nyumbani”: mchungaji wetu, huduma yetu iliyo hai, Yakini yetu, Waefeso 4 yetu yote ipo kwenye kanda. Tunaamini ni huduma ya asili ambayo alikuwa nayo wakati alipokuwa hapa duniani.

Ni amani iliyoje, pumziko jinsi gani, hatujawahi kuwa na wasiwasi au kumvuka kiongozi wetu au chujio letu wakati tunaposikia Neno. Ni Neno la Mungu lililohakikishwa na lililothibitishwa, mana safi kila tunapolisikia na tunachotakiwa kufanya ni kuketi chini na kufurahiya mioyo yetu ikiwaka ndani yetu anapozungumza nasi njiani.

Na wote alionipa Baba, watakuja. Kondoo wangu, hua Wangu, huisikia Sauti Yangu. Mgeni hawatamfuata.” Na Sauti ya Mungu ni nini? Ni Neno la Mungu. Sauti ya mtu ye yote ni nini ila ni neno lake? Ni Neno la Mungu; watalisikia Neno la Mungu .

Halafu bado kuna mengi ZAIDI kwa ajili ya Kanisa Lake. Sio tu kwamba tunatambua siku hii na mjumbe wake, Neno la siku hii, Bali furaha kuu ambayo mwanadamu aliyowahi kupewa hatimaye imetimia. SISI NI sehemu ya Roho Wake, sehemu ya Mwili wake; nyama ya nyama Yake, mfupa wa mfupa Wake; Neno la Neno Lake, Maisha ya Maisha yake, SISI NI Bibi-arusi wa Kristo!

Utukufu !! Lisifikiwe Jina la Bwana !! Haleluya !! Bibi-arusi Wake Amejitambua na Anajifanya Mwenyewe Tayari kwa Neno Lake.

Hivyo ndivyo kanisa linavyofanya siku hizi, kwa kuwa Yesu ni Neno Naye ni Bwana Arusi, na Bibi-arusi ni sehemu ya Bwana Arusi. Kwa hiyo Neno ambalo itapaswa litimizwe siku hii ni sehemu ile ile ya Neno lililotimizwa katika siku Zake, na ni Neno lile lile, tukio lile lile, Maisha yale yale .

Njoo upate uzoefu wa Neno lile lile, tukio lile lile, Maisha yaleyale Jumapili hii saa 8:00 Nane mchana, saa za Jeffersonville,( ni Saa 3:00 tatu usiku ya Tanzania) kusikia: Ile Mbegu Haitarithi Pamoja Na Kapi 65-0429B.

Ndugu. Joseph Branham

Maandiko ya Kusoma:

Mathayo 1: 18-20 / 24:24
Luka 17:30
Yohana mtakatifu 5:24
Wagalatia 4: 27-31
Mwanzo 2:15
Isaya 9: 6
Malaki 4

21-0808 Je! Mungu Hubadilisha Nia Yake?

Ujumbe: 65-0427 Je! Mungu Hubadilisha Nia Yake?

PDF

pakua

BranhamTabernacle.org

Tai wanakusanyika Pamoja.

Mpendwa Bibi_arusi wa Mapenzi Makamilifu,

Ee Mungu mpendwa, hatutaki mapenzi Yako ya kuruhusia, Baba. Jalia tutembee katika mapenzi Yako makamilifu. Hebu tuninii tu—tusichukue tu Neno moja hapa na pale, na kulifanya liafikiane na fundisho fulani la sharti ama kanuni fulani ya imani, ama jambo fulani. Hebu na tuchukue Neno jinsi lilivyo, tukiamini Injili kamili, yote ambayo Yesu alitufundisha kufanya .

Hiyo ndiyo hamu yetu kubwa na ya kina kabisa, ni kuwa katika mapenzi Makamilifu ya Mungu. Hatutaki kamwe kumchukiza, bali kumpendeza katika yote tunayosema na tunayofanya. Tunataka kuwa wana na binti zake wenye Mamlaka na waliyodhihirishwa.

Ni wapi tunapata kujua jinsi ya kuwa katika mapenzi yake Makamilifu na kumpendeza? Ni Lazima tuende kwenye Neno Lake, kwani tunajua Neno Lake ndio kweli na uzima. Neno Lake daima ni lile lile, mpango Wake daima ni ule ule, kwani Yeye hawezi kubadilika.

Neno linatuambia, jinsi alivyofanya mambo mara ya kwanza, atafanya vile vile kila wakati. Lazima yeye abaki vile vile milele. Kusudi lake daima limekuwa lile lile. Matendo yake daima yamekuwa yale yale . Jinsi anavyofanya mambo, jinsi anavyowaponya watu, na jinsi anavyowaongoza watu Wake, daima atabaki vile vile .

Biblia inatuambia katika Neno Lake lisilobadilika kuwa Neno la Bwana huja kwa manabii Wake peke yao. Yeye kamwe hawafunulii makasisi ama mwanatheolojia, manabii Wake tu. Alisema pia hakufanya neno lolote mpaka kwanza alipowaonyesha hilo manabii wake .

Mwanadamu daima amekuwa akitaka mfumo uliotengenezwa na mwanadamu, kundi la watu kuwaongoza. Lakini hiyo kamwe haikuwa njia ya Mungu , Yeye daima alimtuma kiongozi wa kiungu aliyeitwa, nabii aliyeteuliwa akiwa na Neno kuwaongoza watu Wake. Nabii huyo alithibitishwa na alichaguliwa kuwa kiongozi wao wa saa hiyo.

Mungu alichagua na kuweka viongozi wengine wengi waliowekwa wakfu waliojazwa na Roho Mtakatifu; na wana nafasi zao, lakini aliwaonya hao viongozi, “Kaeni mbali na hiyo Nguzo ya Moto.” Je! Nguzo hiyo ya Moto hufanya nini… HUONGOZA WATU MCHANA NA USIKU.

Kisha Neno linatuambia, “Kama ilivyokuwa katika siku za Sodoma, Hivyo ndivyo itakavyokuwa siku Ile atakayofunuliwa Mwana wa Adamu .” Kulingana na Neno Lake katika Malaki 4, na Maandiko mengi, atarudi tena katika Kanisa Lake katika umbo la mwili; katika watu, katika wanadamu, kwa njia ya kuwa nabii.

Tutamtambuaje nabii huyu? Yeye atathibitisha yeye ni nani kwa Neno. Yeye atajua siri za mioyo. Atawafunulia watu Neno lote. Atathibitishwa na Nguzo ya Moto kumwongoza Bibi-arusi. Mungu hata atapigwa picha pamoja na nabii wake.

Wengine watakuwa kama Yohana kwenye kisiwa cha Patmo na kujaribu kumwabudu, lakini atasema, “Angalia usifanye hivyo, mimi ni mjoli wako, na wa manabii, mwabudu Mungu.” Bibi-arusi atajua sio kumwabudu yeye, yule mtu, lakini kumwabudu Mungu KATIKA MTU HUYO.

Atatambua kuwa ndiye yule aliyechaguliwa na Mungu kunena Maneno ya kutokukosea. Atatambua kuwa alikuwa yule malaika_mjumbe wa 7 aliyechaguliwa na Mungu. Ulimwengu utaona na kusikia Sauti ya Mungu ikinena kupitia Yeye na utaona Adamu wa kwanza aliyerejeshwa Kikamilifu.

Atamwongoza Bibi-arusi kwa Nguzo ya Moto. Atakuwa akipata taarifa yake kutoka kwa Logos na kumpa Bibi_arusi njiani mwao kuelekea nchi ya ahadi. Bibi-arusi atakuwa na Ufunuo na kutambua huyu ni mjumbe aliyeandaliwa na Mungu. Hii ndio njia iliyoandaliwa na Mungu. Haya ni MAPENZI MAKAMILIFU ya Mungu .

Njoo uungane nasi Jumapili saa 8:00 Nane Mchana, saa za Jeffersonville (Ni saa 3:00 Tatu Usiku ya Tanzania), Kusikia: Je! Mungu Hubadilisha Nia Yake? 65-0427.

Ndugu. Joseph Branham

Hesabu 22:31

21-0801 Kuthibitisha Neno Lake

Ujumbe: 65-0426 Kuthibitisha Neno Lake

PDF

pakua

BranhamTabernacle.org

Tai wanakusanyika Pamoja.

Wapendwa Watoto Wachanga Wanaoweza kujifunza,

Ni Hali ya kimbinguni jinsi gani tulikuwa tumeketi siku ya Jumapili wakati Bibi-arusi wa Kristo alipokusanyika pamoja katika Uwepo wa Roho Mtakatifu. Tungeweza kuhisi Ikihuisha miili yetu inayokufa.

Hakuna upako mkuu zaidi, hakuna hali kuu zaidi, kuliko wakati Ukibonyeza Play na kusikia Sauti ya Mungu ikizungumza nawe. Mungu ameweka masikio yetu kusikia na kuamini kila Neno, kwani si mwingine isipokuwa El, Elah, Elohim, Yule aliyekuwepo, anayejitosheleza, mwenye nguvu, akiongea na kila mmoja wetu na kutufunulia sisi Kuwa ni wana na binti zake waliodhihirishwa.

Jinsi gani ilivyokuwa yenye nguvu wakati Uzao wa Mungu uliochaguliwa awali, kutoka kote ulimwenguni, walipoweka mikono yao mitakatifu juu ya mmoja kwa mwingine. Nyumba zetu na makanisa yetu yalijazwa na Uwepo wa Roho Mtakatifu. Imani yetu ilikuwa imejengwa, kwani tulijua ni nani anayesema nasi. Kisha akatuambia kuwa ile nguvu ya kuhuisha ilikuwa NDANI YETU. Tuliamini kwa mioyo na roho zetu zote, kwa sababu alisema hivyo.

Ndipo akatuambia tuseme, “Bwana Mungu, naamini kwa moyo wangu wote.” Tulirudia kila Neno kutoka kwenye kina cha mioyo yetu. Alisema, “Ugonjwa hauwezi kusimama katika kundi kama hili.” Roho yetu ilifurahi tuliposikia Maneno haya, kwa maana tulijua kilichokuwa kinatendeka.

Alisema, “Kila mtu anayemtaka Roho Mtakatifu, inua mikono yako, POPOTE ULIPO unayetaka hilo… ninaamini kwamba Mungu atamjaza kila mmoja wenu, SASA HIVI, na Roho Mtakatifu.”
Wakati huo huo, tulijazwa, na kujazwa upya, na Roho Wake Mtakatifu, Sauti ya Mungu ilitamka hivyo.

Kisha kwa wale ambao waliyohitaji uponyaji katika miili yao, Alisema, “Ninakuamuru, katika Jina la Yesu Kristo, simama kwa miguu yako na kukubali uponyaji wako.” Wakati huo huo, kila mwamini, kutoka kote ulimwenguni, ambaye alikuwa na IMANI na aliamini, ALIPONYWA.

Je! Hili lilitendeka wapi? Katika kundi moja dogo la watu lililokusanyika pamoja? Hapana, ilikuwa kutoka ULIMWENGUNI kote wakati Bibi-arusi alipoketi pamoja katika Ulimwengu wa Roho kusikiliza Sauti ya Mungu kwa ajili ya siku yetu.

HAIWEZEKANI kwa mtu yeyote, au kundi la watu, kumuunganisha Bibi-arusi namna hiyo. Ni Roho Mtakatifu peke yake ndiye anayeweza kufanya hivyo kwa kunena kupitia mjumbe wake aliyeandaliwa kwa ajili ya siku hii. Ujumbe huu ni BWANA ASEMA HIVI. Hakuna kushangaa, hakuna kubahatisha, Mungu amethibitisha hii ndiyo njia yake iliyoandaliwa kwa ajili ya leo hii.

Tunalo pumziko na amani jinsi gani. Hatujawahi kamwe kuwa na wasiwasi au kuhoji kile tunachoambiwa. Hatujawahi kamwe kurudi kwenye Neno kulikagua, maana tunasikiliza Neno la Mungu lililothibitishwa kwa ajili ya siku yetu. Tunaketi tu, tukifungulia mioyo yetu, akili na roho zetu, na kusema AMINA, AMINA, AMINA.

Hapana, hatustahili. Hapana, hatuelewi kila kitu. Lakini Tuna AMINI kila Neno. Alisema hiyo ilikuwa ndiyo ishara ya kweli kwamba una Roho Mtakatifu, na ni Bibi-arusi Wake peke yake ndiye atakayeamini na kukaa na kila Neno. SISI NDIYO BIBI_ARUSI HUYO….Haleluya !.

Linapita juu ya wanaodhaniwa kwamba wana akili nyingi sana, na unalifunulia watoto wachanga wanaoweza kujifunza .

Ninashukuru sana ya kuwa mimi ni mtoto mchanga Ninayeweza kujifunza.

Amethibitisha kupitia karne zote Kuwa yeye alikuwa Nani katika kila kizazi. Yeye alithibitisha jambo Hilo kupitia kwa manabii Wake. Alilithibitisha hilo wakati alipokuja katika mwili, akachukua dhambi zetu na kutundikwa msalabani, kisha akafufuka na Akamtuma Roho Mtakatifu.

Sasa amethibitisha katika siku yetu kwa kurudi na kujifunua mwenyewe katika mwili wa mwanadamu Kwa mara nyingine tena kama alivyoahidi angefanya katika Neno Lake. Alijithibitisha kuwa ni Mwana wa Adamu, huduma ya Yesu Kristo Mwenyewe, ikiwa imefichwa katika mwili wa mwanadamu.

Na sasa, sura Yake ya mwisho, sababu yenyewe ya mpango huu mkuu, kuja kwetu, Bibi-arusi Wake aliyerejeshwa Kikamilifu, aliyethibitishwa, ambaye aliyekaa Na Neno.

Je! Ungalipenda Kuwa kwenye mlima siku hiyo wakati Yesu alipoongea na wale 5000? Je! Ungalipenda kumwona akiuthibitishia ulimwengu kuwa Yeye alikuwa nani kwa kutoa mikate na samaki? Je! Ungalipenda kukaa chini ya upako huo, kusikia tu Sauti Yake ikifariji moyo wako kwa Maneno Yake ya Uzima wa Milele?

Unaweza, ikiwa unaamini Ujumbe huu kwa moyo wako wote.

Njoo uketi pamoja nasi chini ya upako huo juu ya mlima Jumapili hii saa 8:00 Nane mchana, saa za Jeffersonville ( Ni saa 3:00 tatu usiku ya Tanzania), na umsikie Mungu akiuthibitishia ulimwengu kuwa Yeye ni nani katika siku yetu. Luka 17:30 Akinena nawe na kukuambia B-R-A-N-H-A-M ni Sauti Yangu iliyothibitishwa na iliyochaguliwa kwako. Njoo umsikie Yeye: Kuthibitisha Neno Lake 65-0426 .

Ndugu. Joseph Branham

Maandiko ya kusoma:

Mathayo Mtakatifu 11: 4-19 / 28:20
Marko Mtakatifu 11: 22-26
Luka Mtakatifu 8: 40-56 / 17:30
Yohana Mtakatifu 14:12
Waebrania 4: 12-15 / 13: 8
Malaki 4

21-0724 Mahali Pa Kuabudia Palipoandaliwa Na Mungu

Ujume: 65-0425 Mahali Pa Kuabudia Palipoandaliwa Na Mungu

PDF

pakua

BranhamTabernacle.org

Tai wanakusanyika Pamoja.

Wapendwa Waliyouishwa ,

Jinsi gani tunavyopenda kukusanyika pamoja kila wiki kula Manna ya Kiroho aliyowaandalia Bibi-arusi Wake. Inatupa nguvu tunayohitaji kwa ajili ya safari yetu. Ni Maisha yenyewe ya Masihi, yaliyodhihirishwa, yakifanya Kanisa Lake liwe tayari kwa Unyakuo.

Nguzo ya Moto imetuita kutoka, na inatuongoza kwenda kwenye Nchi ya Ahadi, chini ya upako wa nabii Wake Mwenye nguvu, William Marrion Branham.

Ndugu Branham sio ile Nguzo ya Moto. Yeye Ndiye kiongozi aliyepakwa mafuta, chini ya ile Nguzo ya Moto. Nguzo ya Moto inathibitisha tu Ujumbe wake kwa ishara na maajabu. Ni Roho wake Mtakatifu Mkuu aliyejidhihirisha kati yetu na ni mara elfu zaidi ya manabii wengine wote wa hapo awali.

Hivi huwezi kumwona Mwana wa Adamu, Mwana wa Adamu katika mfano wa Ujumbe wa kinabii, akirudi tena katika Kanisa Lake, katika unabii, akimfunua Yesu Kristo kwamba ni yeye yule jana, leo, na hata milele? Halijawahi kufanyika kote katika wakati huu, mpaka kufikia saa hii.

Akili zetu za Kiroho zimelishika. Tunaliona na tunaamini kila Neno. Ujumbe Huu, Kanda hizi, ni Njia iliyoandaliwa na Mungu ili kuikamata akili hiyo huko nje ambapo mbegu hiyo imepandwa. Tumesikia Sauti hiyo na Nuru imetugusa na tumetwaa Uzima.

Inatuketisha katika makao ya kimbinguni, SASA HIVI. Sio tutakuwa, tuko sasa. Tayari tumefufuliwa, Nguvu tendaji na mitambo ipo kazini. Imetuhuisha katika Uwepo wa Mungu, alipo Roho Wake. Sio kile utakachokuwa, tayari uko! Ni shetani tu akijaribu kutufumba kutoka Kwenye hilo.

Swali: Je! Umekuwa Hai?
J: Ndio

Swali: Je! Kristo amekuwa halisi kwako?
J: Ndio

Swali: Je! Nguvu za Mungu zimedhihirishwa?
J: Ndio

Swali: Je! Uko katika Kanisa hilo, Kanisa lililoandaliwa na Mungu?
J: Ndio

Swali : Unakuaje ndani Yake, unajuaje kuwa umehuishwa ndani Yake?
J : Mawazo yetu yote; Utu wetu wote, uko ndani ya Kristo. Kristo yuko katikati yetu, akijithibitisha kuwa hai, akithibitisha kuwa yuko hapa.

Sisi ni nyama ya nyama Yake, na mfupa wa mfupa Wake, mwili wa mwili Wake, Jina la Jina Lake, Bibi-arusi Wake. Tuko ndani yake. Sisi ni mwili Wake na mifupa yake.

Hatuwezi kufa, tumehuishwa. Nguvu ile ya kuhuisha iliyotufufua kutoka kwenye maisha ya dhambi, na kubadilisha Utu wetu, imetufufua kwa uwezekano katika Kristo Yesu, ambapo, ufufuo utatuleta katika ukomavu kamili.

Tumezaliwa mara ya pili na kuzaliwa upya, tumebatizwa na Roho Mtakatifu, ndani ya Yesu Kristo. Tumehuishwa kwa kila Neno. Tunaitikia kila Neno kwa “amina”.

Tunapokusanyika pamoja katika Yesu Kristo; kwa nia moja, na kwa umoja , chochote tunachohitaji, ikiwa tutakuwa na IMANI na kuamini, Yeye atatupatia.
Hebu na tutambue ya kwamba Yeye atakuwa katika kila moja ya nyumba zetu, makanisa yetu, au mahali popote tutakapokusanyika, kwani sisi ni wana na binti zake, Kanisa la Bibi-arusi Wake.

Ninajua Yeye yuko hapa. Nina hakika Yeye yuko hapa. Ninajua ya kwamba sasa kuna nguvu za kuhuisha ndani ya Kanisa kumponya kila mtu anayeketi hapa .

Je! Unaamini Ujumbe huu? Je! Unaamini ni Njia ya Mungu ya leo? Je! Unaamini ni Mwana wa Adamu akijifunua mwenyewe katika mwili wa mwanadamu? Je! Unaamini kila Neno?

Ikiwa unahitaji uponyaji wa mwili, uponyaji wa roho, au CHOCHOTE ambacho unaweza kuhitaji, basi ninakupa changamoto kuamini sauti ya Mungu iliyotiwa mafuta nakuthibitishwa kwa ajili ya siku yetu:

Jalia sasa ya kwamba nguvu hizo za kuhuisha zitaihuisha imani yao, Bwana, kwa yale wanayofanya. Kuna mwamini aliyeweka mikono yake juu ya mwamini, mwili kwa mwili, nguvu kwa nguvu. Na ni nguvu za Mungu, kwa mwana wa Mungu ama binti ya Mungu, kwa Mwana wa Mungu. Ee Mungu, jalia Shetani awaachilie watu hawa! Jalia waponywe alasiri ya leo, kwa nguvu hizo za kufufuka, kuhuisha kwa Uwepo uliotambulishwa, Yesu Kristo. Katika Jina la Yesu Kristo, na iwe hivyo!

Njoo uungane nasi chini ya: Mahali Pa Kuabudia Palipoandaliwa na Mungu 65-0425, na upokee uponyaji wako, utiwe mafuta na Roho Mtakatifu, roho yako ifurahi unapoketi katika makao ya kimbinguni na kumsikia Mwana wa Adamu akizungumza Jumapili hii saa 8:00 Nane mchana , saa za Jeffersonville ( ni saa 3:00 Tatu usiku ya Tanzania).

Ndugu. Joseph Branham

Maandiko ya kusoma kabla ya kusikia Ujumbe:

Kumbukumbu la Torati 16: 1-6
Malaki 4: 5
Mathayo Mtakatifu 1:23
Marko Mtakatifu 16:17
Luka Mtakatifu 17:30
Yohana Mtakatifu 4:23 / 10: 1-7
Warumi 8: 1-11
1 Wakorintho 12:13
Waefeso 1:21
1Wathesalonike 4:16
Waebrania 13: 8
Ufunuo 22:19