Category Archives: Uncategorized

22-1106 Ile Mbegu Haitarithi Pamoja Na Kapi

UJUMBE: 65-0218 Ile Mbegu Haitarithi Pamoja Na Kapi

PDF

BranhamTabernacle.org

Mpendwa Bibi-arusi-Neno Bikira ,

Tuko hapa. Tumefika. Muda umekaribia. Kapi limejitenga na Mbegu. Tumekuwa tukikaa katika Uwepo wa Mwana, tukiiva. Tutakaa katika Uwepo huo mpaka kundi letu dogo litakapoiva sana kwa Kristo, mpaka tuwe mkate kwenye meza Yake. Bwana Ashukuriwe!

Ujumbe huu umethibitisha Malaki 4, umethibitisha Luka 17:30, umethibitisha Waebrania 13:8, umethibitisha Yohana Mtakatifu 14:12, umethibitisha Ufunuo sura ya 10, kufunguliwa kwa ile Mihuri Saba, siri za Mungu, uzao wa nyoka, ndoa na talaka. na siri hizi nyingine zote ambazo zilikuwa zimefichwa chini ya nguzo kwa miaka hii yote.

Sisi ni mabikira kwa Neno. Hatuwezi na hatutagusa kitu kingine chochote. Kwa kila Ujumbe tunaosikia, ni msafi na mpya; Mana mpya ambayo ndio kwanza imeshuka kutoka Mbinguni.

Lakini alituonya kwamba katika wakati wa mwisho kutakuwa na roho mbili ambazo zingefanana sana, zingewapoteza walio wateule , kama Yamkini. Hivyo, ni lazima tuwe macho kwa roho hiyo kwani itaonekana kuwa kama Bibi-arusi mwenyewe.

Tazama, ona zinavyofanana. Mathayo ilisema—Mathayo Mt. 24:24, ilisema kwamba hizo roho mbili katika siku za mwisho , roho ya kanisa ya watu wa kanisa na Roho ya watu wa Bibi-Arusi , zitafanana sana hata ingewapoteza, kama yamkini, walio Wateule. Hivyo ndivyo jinsi zinavyofanana.

Alisema ROHO ya watu wa kanisa na ROHO ya watu wa Bibi-arusi zitafanana sana moja kwa nyingine . Hiyo ingemaanisha kwamba roho ya watu wa kanisa ingepaswa kusema wanaamini Ujumbe wa wakati huu ili KUFANANA JINSI HIYO.

Hiyo haingekuwa methodisti, Baptisti, presbiteri, au hata wapentekoste; Wao wako mbali sana na Neno na hata wanaukataa Ujumbe. Hakuna hata mmoja wao aliye na roho inayofanana na Bibi-arusi.

Shetani amejaribu, na amefanikiwa sana, kuwa mdanganyifu sana. Hata tangu hapo mwanzo, alisema tu, “Hakika,” hivyo akimwambia Hawa atumie hoja yake naye amsikilize yeye na si Neno tu. Kuna jambo moja tu aliloamriwa kufanya: kukaa na Neno.

Ukweli:

Ikiwa una swali, lazima kuwe na jibu. Hivyo ndivyo nabii alivyotuambia. Jibu lazima litoke katika Neno. Neno huja kwa nabii peke yake. Nabii ndiye mfasiri pekee wa Neno. Ikiwa mwanamume au mwanamke yeyote atakupatia jibu, lazima liwe vile nabii alivyokwishasema . Haiwezi kuwa fasiri yao , wazo au ufahamu wao. Hawana budi waliunganishe kwa Neno lililonenwa na nabii wa Mungu aliyethibitishwa. Wala Sio neno la nabii pamoja na, ni kile tu nabii alichosema.

Kuna itikadi mbili sasa hivi .

1 : Ni lazima uamini kila Neno kwenye hizo kanda kwani ndizo Jumbe muhimu sana unazopaswa kusikia.

2 : Wala Huhitaji kuamini kila Neno kwenye hizo kanda, na wahudumu sasa wao wanazo jumbe muhimu sana unazopaswa kusikia.

Kunazo tofauti nyingi, nyingi kwa hiyo itikadi ya pili: Roho Mtakatifu ataniongoza mimi au mchungaji wangu kutuambia kile ambacho ni Neno na kisichokuwa Neno. Tunahitaji zaidi ya yale tu aliyosema Ndugu Branham kwenye kanda. Huna budi kuwa na wahudumu wa kufafanua au kulivunja-vunja Neno. Bila ya wahudumu huwezi kuwa Bibi-arusi.

Kuna Mbegu za Hitilafu nyingi zaidi, lakini haiwezekani kuziorodhesha zote. Lakini hakuna tofauti ama mbegu za hitilafu kwa Ile namba ya kwanza. Ni AMINI KILA NENO, hivyo tu.

Mkiwa Kama waamini wa Ujumbe huu wa wakati wa mwisho, lazima mjiulize maswali haya:

1 : Je, unaamini kile nabii alichosema kwenye kanda ndio Yakini yako, au unaamini ni Roho Mtakatifu kupitia wewe au mchungaji wako?

2 : Je, unaamini kwamba huduma tano ina jumbe muhimu zaidi ambazo Bibi-arusi anazohitaji kusikia, au ni Ujumbe uliyo kwenye kanda?

Iwapo mchungaji wako, mhubiri, mwalimu, mwinjilisti au nabii hakuambii kwamba kuzisikiliza kanda ndizo JUMBE MUHIMU SANA unazopaswa kusikia, yeye ni wa UWONGO, NA ILE ROHO AMBAYO NABII ALITUONYA INGEKUJA.

Ikiwa anasema HIZO NDIZO Jumbe muhimu sana mnazoweza kusikia, lakini bado anakataa kuzicheza kanda katika kanisa lake, HAPO KUNA KASORO FULANI. Ikiwa anaamini kweli kwamba kuzisikiliza kanda ndilo jambo muhimu zaidi mnaloweza kufanya, basi angezicheza kanda KWANZA, kisha ahubiri ikiwa anahisi kuongozwa.

Mfano rahisi:

Kama ningekuambia, kunywa maji safi ndilo jambo moja muhimu zaidi uwezalo kufanya kwa ajili ya afya yako, na kuna maji MAMOJA tu ya kunywa yaliyothibitishwa na kuhakikishwa…lakini ujapo nyumbani kwangu kula chakula cha jioni, Nami sikuhudumii hayo maji yaliyothibitishwa. Ninakuambia, “unaweza kunywa maji hayo huko nyumbani kwako lakini nyumbani kwangu, lazima unywe kile Mimi ninachokupa .”

Ikiwa maji hayo ndio KITU BORA ninachoweza kukupa kwa ajili ya afya yako, ambayo yatakupa uhai, basi jambo la kwanza nitakalokupa unapoingia nyumbani Mwangu ni maji hayo safi ya kunywa.

Je, nimekosea kwa kusema, “CHEZENI KANDA KATIKA MAKANISA YENU, ndilo jambo bora sana muwezalo kufanya kwa watu wenu. Ni Bwana Asema Hivi.”

Au, wanakosea kwa kusema, “Ni makosa kucheza kanda kanisani, Ndugu Branham hakusema kamwe kucheza kanda kanisani mwenu. Tunawaambia watu wacheze kanda majumbani mwao, kwenye magari yenu, kila wakati, LAKINI kanisani lazima wanisikie MIMI.”

Ni Roho gani anayekuongoza? Je, Unasema, “kinachosemwa kwenye kanda ni Yakini yangu na ndilo jambo muhimu zaidi niwezalo kusikia”? Au, Unasema, “Kanda hizo hazitoshi. Sio Yakini yangu na sio jambo lililo muhimu zaidi kusikia, je ni Wahudumu ”?

Sasa, ni wakati wa mbegu au wakati wa Bibi-Arusi. Makapi yamekufa, yale makapi tayari yamekwisha kukauka. Ni wakati wa Neno bikira, lisilogoshiwa. Ni bikira, Kumbuka, wakati wa Neno bikira.

Njoo usikie Manna mpya ambayo ndio kwanza imeshuka kutoka Mbinguni Jumapili hii saa 06:00 SITA MCHANA , saa za Jeffersonville, ( Ni saa 2:00 MBILI USIKU Ya Tanzania),Tunaposikia :  
65-0218 Ile Mbegu Haitarithi Pamoja na Kapi.

Ndugu. Joseph Branham

22-1030 Mtu Anayejiepusha Na Uso Wa Bwana

UJUMBE: 65-0217 Mtu Anayejiepusha Na Uso Wa Bwana

PDF

BranhamTabernacle.org

Wapendwa Wana-kondoo wa Bwana,

Jinsi mioyo yetu inavyotamani siku hii kila wiki tunapoweza kuungana pamoja kutoka ulimwenguni kote ili kusikia Sauti ya Mungu ikizungumza nasi Neno la Uzima wa Milele. Hakuna kitu kingine kinachoshibisha nafsi zetu na kukata kiu yetu ila Sauti ya Mungu.

Ulituambia, Baba, kwamba mashamba Makubwa ya mavuno ni meupe, yameiva, na nafaka iko tayari sasa kwa ajili ya ule wakati mkuu wa kupura. Nafaka sasa inakaa katika Uwepo wa Mwana na ikiiva kwa ajili ya Ufalme wa Mungu.

Baba, Tunatetea tunayoamini kuwa ni Kweli; Sauti Yako kwenye kanda ndiyo Sauti PEKEE ambayo itatukamilisha sisi, Bibi-arusi Wako.

Ni ngumu kwani tunaeleweka vibaya sana kwa ndugu na dada zetu. Tunawasihi na kuwaomba wasijiepushe na Uwepo Wake, bali wakimbilie kuingia katika Uwepo Wake.

Tunajua kuna watu wengi watiwa-mafuta uliowachagua na kuwaweka waangalie kundi Lako, wanaopenda Ujumbe huu kwa mioyo yao yote, Lakini Baba, wanashindwa kuweka Sauti Yako iliyothibitishwa kwenye kanda mbele yao. Wanashindwa kuwaambia kwamba huu ni Ujumbe wa mtu mmoja na kwamba Wewe ulimchagua mtu huyo kumwongoza Bibi-arusi Wako. Wanashindwa kuwaambia kwamba Sauti Yako ndiyo Sauti PEKEE itakayomunganisha na kumkamilisha Bibi-arusi Wako.

Lazima “Nipige kelele juu yake.” Nipige kelele juu ya kila kitu, na kila mtu, ambaye anapinga kucheza Kanda Zako katika makanisa yao. Nipige kelele juu ya matendo yao, nipige kelele juu ya kanisa lao, nipige kelele juu ya manabii wao, nipige kelele juu ya wahudumu wao, nipige kelele juu ya makasisi wao. Lazima nipige kelele juu ya kitu hicho chote!

“Aisee, nimeshuka kuja kujiunga nanyi enyi jamaa. Mnajua, naamini nitawaambia nitakachofanya. Nina kitu kidogo tu hapa naamini ninaweza kuifanya ninino…kutuunganisha sote pamoja, na kufanya hivi, vile, ama vinginevyo.”

Lazima nipige kelele juu ya jambo hilo, kwani Neno Lako pekee, lililonenwa na nabii Wako, ndilo linaloweza kutuleta PAMOJA. Mahubiri yao yanawezaje? Wote hawakubaliani mmoja kwa mwingine na wanaona mambo kwa njia tofauti mmoja kwa mwingine, isipokuwa jambo moja, wote wanalokubaliana kwalo… KUTOCHEZA KANDA KATIKA MAKANISA YAO. Hilo lawezaje , Baba?

Ulituambia ni lazima tuwe na YAKINI MOJA, ambayo ni Neno lako. Ulituambia Neno Lako humjia nabii Wako, PEKE YAKE. Ulituambia yeye ndiye Mtu PEKEE anayeweza kulifasiri Neno Lako. Ulituambia kwamba kila mhudumu, kila mshiriki wa kawaida, kila mwanadamu, anaweza TU KUSEMA ALICHOSEMA. Sauti Yake ndiyo SAUTI PEKEE ambayo imethibitishwa na Nguzo Yako ya Moto kuwa Bwana Asema Hivi .

Sisemi kwamba ni wa uwongo au hawapaswi kuhubiri. Wala sisemi Bwana hayuko pamoja nao, au hawajatiwa mafuta na kuitwa kuhubiri, Lakini lazima niwapigie kelele wakati hawatawaambia watu wao kwamba kusikiliza kanda ndilo jambo muhimu zaidi wanaloweza kufanya.

Kubadilisha yodi moja au nukta moja ni kifo. Umeandaa njia kwa ajili ya Bibi-arusi wako kusikia Bwana Asema hivi kwa masikio yao wenyewe. Wanawezaje Kutowahubiria watu wao kwamba huu Ndio Ujumbe uliyo muhimu sana uwapasao Kusikia? Ndio Ujumbe pekee ninaoweza kusema AMINA kwa kila Neno, kwa kuwa si Neno la mwanadamu, au fasiri ya mwanadamu ya Neno Lako, ni Neno Lako Safi.

Ulisema Ujumbe na mjumbe ni kitu kimoja . Nabii wako alinena Hilo nawe ungelitimiza. Neno Lako lililonenwa na nabii Wako HALIHITAJI fasiri kwa kuwa ni Mwana wa Adamu akizungumza moja kwa moja na Bibi-arusi Wake.

Yanipasa niwasihi watu, rudini kwenye upendo wenu wa kwanza. Rudini kwenye kile mnachojua ni BWANA ASEMA HIVI. Ikiwa umekuwa unajiuliza ni njia gani ya kwenda au nini cha kufanya, njoo, ingia katika Merikebu pamoja nasi usiku wa leo. Tunashuka kwenda Ninawi, ili kupiga kelele. Tuna wajibu mbele za Mungu, huo ni Ujumbe huu kwenye kanda.

Tunaamini ya kwamba Kuja kwa Bwana kumekaribia, Naye atakuwa na Bibi-arusi, nasi tunajitayarisha. Hatutaki chochote ila Neno Safi la Mungu lililonenwa na nabii Wake. Tunaenda Utukufuni, njoo tuungane katika Merikebu yetu.

Ikiwa unaamini Ujumbe huu ni Kweli, na unaostahili kuuishia, unaostahili kuufia, njoo uungane nasi Jumapili hii saa 06:00 SITA MCHANA , saa za Jeffersonville, (Ni saa 1:00 MOJA JIONI Ya Tanzania), tunaposikia Ujumbe tunaoamini ni muhimu na wa haraka kwetu kuusikia: Mtu Anayejiepusha Na Uso Wa Bwana 65-0217.

Ninyi ni wana-kondoo wangu. Mwaonaje? Ninyi ni wana-kondoo wa Bwana ambao ameniruhusu kuwalisha .

Ndugu. Joseph Branham.

Maandiko ya kusoma kabla ya Kusikiliza Kanda :

Yona 1:1-3
Malaki sura ya 4 yote
Yohana Mt. 14:12
Luka 17:30

22-1023 Maswali na Majibu #4

UJUMBE: 64-0830E Maswali na Majibu #4

PDF

pakua – m4a

pakua – amr

BranhamTabernacle.org

Mpendwa Ndugu Joseph,

 1. Nimekusikia ukisema kwamba unaamini KILA NENO la Ujumbe huu ni BWANA ASEMA HIVI.

 Kutoka kilindi cha moyo wangu na kila mshipa katika mwili wangu NINAAMINI HILO.  Ni Sauti yenyewe hasa ya Mungu ikinena mdomo kwa sikio kwa Bibi-arusi Wake.

 Mungu alinena kupitia nabii wake na kusema:

  Nasema vivyo hivyo katika Jina la Yesu Kristo. Usiongeze kitu. Usiondoe—kuliwekea mawazo yako. Wewe sema tu yaliyosemwa katika kanda hizo. Tenda sawasawa kabisa na vile Bwana Mungu amekuamuru kutenda. Usiongezee Kwake .

 Ikiwa unadai unaamini Ujumbe huu wa wakati wa mwisho, wewe pia lazima uamini KILA NENO ili uwe Bibi-arusi Wake.  Shetani anajaribu kulipiga msasa Kupitia Wahudumu na kusema, “Ndugu Branham alipokuwa akisimulia hadithi za kuwinda au kusema ‘mnaye mpishi bora zaidi nchini’, au ‘Sina Maandiko kwa jambo hilo, lakini nitakuambia kile ninachofikiri;’ Haikupasi  kuamini sehemu hiyo.  Roho Mtakatifu yuko hapa kutuongoza kuelewa kile ambacho ni Neno na kisichokuwa Neno .”  HUYO NI IBILISI YULE YULE ALIYEONGEA NA HAWA NA KUSEMA, HAKIKA…. HAKUMAANISHA KILA NENO.  Je, linasikika kama unalifahamu?

 Wanafanya yale ALIYOWAAGIZA wasifanye.  Alisema SEMA YANAYOSEMWA kwenye kanda hizo, usiliwekee mawazo yako au uelewa wako.  Hakusema, “Kila kitu ISIPOKUWA sehemu hii na ile, na mchungaji wako atakuambia ni wakati gani alipokuwa Roho Mtakatifu  akizungumza na wakati gani alikuwa ni mimi tu.”  Mimi ni moja ya changarawe ndogo tu pwani kati ya mawe haya makubwa.

  2. Je, unafikiri Ndugu Branham na/au kanda zake ndizo Yakini?

 Ndugu Branham si Yakini Yangu bali Ujumbe alionena kwenye kanda ndiyo Yakini yangu Kabisa.

 Watu wengi husema hiyo si sahihi, Biblia ndiyo Yakini.  Rafiki yangu, Biblia na Ujumbe uliyo kwenye kanda ni kitu kimoja.  Hicho ndicho kiini hasa cha Ujumbe.  Ujumbe uliyo kwenye kanda ndiyo fasiri ya Biblia.  Hivyo ni kitu kimoja na jambo lile lile .

 Ukweli rahisi ni kwamba,  1: Biblia ni Neno.  2: Neno humjia nabii.  3: Nabii ndiye Mfasiri PEKEE wa Kiungu wa Neno.   4: Nabii wetu, William Marrion Branham, ndiye Neno lililodhihirishwa la siku yetu na alitumwa kulifasiri Neno.  5: Neno la Mungu halihitaji kufasiriwa.  Anachosema kupitia nabii wake kwenye kanda  NDIYO FASIRI YA NENO LAKE.

 Biblia inatuambia kwamba alikuwa anakuja tena na kuishi katika mwili kama alivyofanya na Ibrahimu na Yesu Kristo.  Alisema alikuwa na mambo mengi ya kutuambia.  Alisema angefunua siri hizi zote kuu ambazo zimefichwa katika Neno Lake.  Alisema hazihitaji fasiri yoyote.  Hakusema kamwe angetuma kundi kuongoza na kuwaunganisha watu Wake, YEYE MWENYEWE ANGEWAONGOZA WATU KUTUMIA NABII WAKE KAMA ALIVYOFANYA DAIMA.  NENO LAKE HALIWEZI KUBADILIKA.

 3. Je, unaamini kwamba wachungaji wanapaswa kucheza kanda katika makanisa yao?

 Kila mchungaji yampasa afanye kama anavyojisikia kuongozwa na  Bwana kufanya, kwa kuwa kila kanisa linajitawala lenyewe .  Ninaamini, na nimesema mara nyingi mimbarani, ya kwamba wachungaji wanapaswa kumrudisha Ndugu Branham kwenye mimbara zao kwa kuzicheza kanda.  Sijawahi kusema yawapasa waache kuhubiri, wacheze tu kanda.  Lakini wanatumia kila kisingizio cha kutocheza Sauti ya Mungu katika makanisa yao.

 Nitamwacha nabii aseme jinsi ninavyohisi kuhusu wachungaji ambao hawataicheza Sauti hiyo katika makanisa yao.

  Sasa, Ndugu Junior Jackson alikuwa na haki ya kutokukubaliana na hayo. Yeye ataka kanisa lake…Watu wote wanataka kunena kwa lugha na mengineyo mkutanoni. Hizo ni taabu za Ndugu Junior; hiyo ni—hiyo ni juu yake. Lakini Junior Jackson anaamini Ujumbe huu sawasawa kama wengine wetu wote wafanyavyo. Yeye ni mmoja wetu.

 4. Je, unaamini kwamba wahudumu wanapaswa kuacha kuhubiri?

 Hapana, sijawahi kusema hivyo wala siamini hivyo.  Neno linatuambia, na Ndugu Branham amekuwa wazi kabisa kwenye Jumbe hizi za Maswali na Majibu, kwa wahudumu kuendelea.

 Najisikia tu kuongozwa, kwa kanisa langu, kufanya utangulizi wa haraka;  ama kwa barua kwa sasa, kisha Kubonyeza Play na kusikia Sauti PEKEE ya Mungu  iliyothibitishwa kwa siku hii.  Nimesema mara nyingi kwamba nina huduma kuu zaidi ulimwenguni, napata kutambulisha Sauti ya Mungu kanisani kwangu kila Jumapili.

5. Watu wanasema unahisi  Usipojiunganisha na ibada za Maskani ya Branham wewe si Bibi-arusi?

 Sijawahi KAMWE kusema hivyo au hata kufikiria hivyo, ndugu na dada zangu.  Yeyote anayeweza kusema kitu kama hicho ni makosa . Nikiwa Kama mchungaji wa Maskani ya Branham, najisikia nikiongozwa kucheza kanda za Ndugu Branham.  Ninaamini hiyo Sauti ndiyo kitu pekee kitakachomuunganisha Bibi-arusi.

 Kama nilivyosema awali, ninaamini kila kitu kwenye kanda hizi ni Bwana Asema hivi na hakihitaji fasiri yoyote.  Ninaweza kusema amina kwa kila Neno ninalosikia.  Ninaamini William Marrion Branham alitumwa kumwita Bibi-arusi atoke .  Nafasi yangu katika huduma tano ni kuwaelekeza watu kwa mjumbe huyo na kisha Kubonyeza Play . Hakuna kitu kikubwa zaidi ya kuisikia Sauti hiyo.  Upako mkuu zaidi uko kwenye kanda, kwa hiyo kwa nini nitake kulipatia kanisa langu kitu kingine?

 Kila Jumapili ninaualika ulimwengu kusikiliza Ujumbe ambao Bwana ameweka moyoni mwangu ili kuucheza kwa kanisa langu.  Kila mtu anakaribishwa kusikiliza kwa wakati mmoja.

 Ninatumia kama kiongozi wangu kile Ndugu Branham alichosema kwenye kanda hizi .

Nasi tuna mfumo huu wa simu sasa, ambao ni mzuri sana, sana. Watu wanaweza kuketi moja kwa moja nyumbani mwao ama nini hii mwao…wakusanyike makwao, makanisani mwao, na kadhalika, na kusikiliza ibada. Nafurahia jambo hilo.

Sasa, ewe mchungaji, nataka ujue jambo hilo, ya kwamba, ninazungumza haya kwa ajili ya kusanyiko langu peke yake. Nami nina haki ya kutenda jambo hilo, kwa maana nimewekwa na Roho Mtakatifu kuwachunga kondoo hawa.

Ujumbe huu, na Jumbe zote zingine ambazo ninazungumzia, zinaelekezwa kwenye kusanyiko langu. Si kwa ajili ya kusanyiko lako isipokuwa wawe wanataka kulipokea. Bali limeelekezwa kwa watu hawa hapa.

Na hilo ni kote kote ulimwengu mzima. Na watu huamka usiku wa manane usiku, katika nchi za kale, hufanya mnyororo huo wa maombi kwa wakati mmoja.  Kwa hakika, makumi elfu na maelfu kwa maelfu wanaomba kwa wakati mmoja.  Mungu hana budi kusikia;  wewe ni—unaivumisha tu Mbingu kwa maombi, unaona, kwa hiyo hana budi kusikia.

 6. Je, ni kosa kwenda kanisani ?

 Sijawahi kusema hivyo wala kuamini hivyo.  Ikiwa niliamini hivyo kwa nini ningekuwa na kanisa?  Katika Maskani ya Branham tulikuwa na ibada 3 kwa wiki hadi ikawa vigumu sana kwangu kuwa na ibada nyingi jinsi hiyo kila wiki na kufanya kazi katika VGR.  Ndipo tukawa na ibada 2 kwa wiki katika Maskani hatimaye isingewezekana kutosha watu .  Kwa hiyo tulihamia kwenye jengo letu tulilotumia kwa ajili ya vijana wetu, ambalo lilikuwa jumba la mazoezi.

 Bwana alikuwa ameweka moyoni mwangu kutoa tamko Jumapili moja asubuhi.  Nilisema hata ikiwa siku moja wangefunga milango ya kanisa hili , hatutakosa hata mpigo kwani mchungaji wetu angeweza kuzungumza nasi popote tulipo.  Mwezi mmoja baadaye,  CORONA Ikaja ambayo ilifunga makanisa kote ulimwenguni.

 Nilijisikia kuongozwa kwamba wakati huo, tungekuwa na fursa nzuri ya kurekebisha ukumbi wa mazoezi, kwani tulihitaji mahali pakuabudia.  Kwa hivyo, tumekuwa na furaha katika nyumba zetu, kuungana na kumsikiliza nabii wa Mungu kwenye kanda pamoja na sehemu ya Bibi-arusi duniani kote, wakati kanisa linarekebishwa.

 Sasa hivi tunamalizia jengo, lakini kama vile tu wakati Ndugu Branham alipokuwa hapa kwenye Maskani ya Branham, tayari tumepita eneo la ziada la maegesho tulilojenga.  Itatubidi tu kuomba na kuona jinsi Bwana aongozavyo.

 Najua kuna maswali mengi, mengi zaidi kwenye mioyo ya watu.  Kuna mambo mengi niliyosema yameeleweka vibaya.  Ikiwa Ndugu Branham Walimwelewa vibaya, ni kiasi gani zaidi basi mimi nitakavyoeleweka vibaya?

 Ninaweza kuwa nimekosea katika kile nilichosema.  Ningeweza kuyasema vizuri zaidi au ningekuwa wazi zaidi kwa jinsi nilivyoyawasilisha.  Ila kuna jambo moja NAJUA ni sahihi, UJUMBE HUU NI MKAMILIFU .  Sio lazima unisikilize mimi au Kile nisemacho, lakini YAKUPASA UBONYEZE PLAY NA UAMINI KILA NENO.

 Kwa mara nyingine tena, ninakualika uungane na Maskani ya Branham Jumapili hii saa 06:00 SITA MCHANA , saa za Jeffersonville, (Ni saa 1:00 MOJA JIONI Ya Tanzania) tunaposikia: Maswali na Majibu #4 64-0830E .

 Ndugu.  Joseph Branham

22-1009 Maswali na Majibu #2

UJUMBE: 64-0823E Maswali na Majibu #2

PDF

pakua – m4a

pakua – amr

BranhamTabernacle.org

Mpendwa Bikira Safi aliyeposwa,

Mungu anatupenda sana hata akamfanya nabii wake ajibu maswali yetu YOTE, na akaweka majibu kwenye kanda. Wakati Tunapoyahitaji, yote tunayopaswa kufanya ni KUAMINI NA KUBONYEZA PLAY.

Je, ninaye Roho Mtakatifu?

Ishara ya Roho Mtakatifu, Mungu anapokufunulia na unaliona, BWANA ASEMA HIVI na kulikubali.

Basi ninaye Bwana, ulivyonifunulia Ujumbe huu na nimeukubali kama Bwana Asema Hivi !

Lakini, inaonekana kama ninakosea sana…na vipi kuhusu maisha yangu ya nyuma?

Si vile ulivyo, vile ulivyokuwa, au lo lote lile, ni yale Mungu amekufanyia wewe sasa. Hiyo ndiyo ishara.

Bwana, huyaoni maisha yangu ya nyuma na hata huyaoni makosa yangu mengi, mengi sasa, Unasikia sauti yangu tu; Utukufu Bwana, NINAYE ROHO MTAKATIFU.

Ndugu Branham, najua ulisema wewe siye changarawe pekee pwani, lakini ni nani atakayekuwa akimuongoza Bibi-arusi wa Kristo katika wakati wa mwisho?

Kwa msaada wa Mungu, naamini kuwa ninamuongoza Bibi-arusi wa Yesu Kristo.

Nina mambo mengi moyoni mwangu, nifanye nini?

Hakuna kilicho muhimu sasa ila kuwakusanya watoto wote wa Mungu pamoja na kusema, “Haya twendeni.”

Asante Bwana, tunafanya hivyo tu. Hakuna kitu kingine kilicho muhimu kwetu ila Neno Lako. Roho Wako Mtakatifu anatuongoza kupitia nabii Wako na tunakusanyika kulizunguka Neno Lako kutoka ulimwenguni kote, nasi tuko tayari Kwenda.

Nina maswali mengi, ninahitaji mwongozo, msaada, na majibu. Nitayapata wapi hayo?

Niko hapa kujaribu kuwasaidia, kwa sababu nawapenda. Ninyi ni watoto wangu niliomzalia Kristo. Nadai kila mmoja wenu. Nadai ninyi usiku huu; nadai ninyi wakati wote; mimi kila mara huwadai ninyi kisha—kama ndugu yangu na dada.

Tunakupenda pia Ndugu Branham. Tunajua Mungu alikutuma utuongoze na kutuelekeza. Tumelichunguza kwa Neno nalo linajipanga kikamilifu.

Ni nani Aliye Baba yangu katika Injili?

Ninyi ni watoto wangu; mi—mimi ni baba yenu katika Injili, si baba kama vile kasisi angalikuwa, mimi—mimi ni baba yenu katika Injili kama Paulo alivyosema pale.

Tunajua ni Roho Mtakatifu akuongozaye wewe kutuongoza, Ndugu Branham. Unasema kama vile tu Paulo alivyosema katika Biblia, kufuata hasa kabisa yale uliyosema, kwa kuwa ni Kweli, nasi hatupaswi kubadili yodi moja au nukta moja.

Utafanya nini Ndugu Branham?

Nimewazaa ninyi kwa Kristo, na sasa na—nawaposea ninyi Kristo; hilo ni kufanya ninyi muweke nadhiri ya ndoa kwa Kristo kama bikira wasafi. Msiniaibishe! Msiniaibishe! Ninyi iweni bikira safi.

Umetuposa sisi kwa Kristo kama mabikira kwa Neno Lake. Hatuwezi, na hata hatutavutiwa na mwingine. Tunakagua kila kitu tunachosikia na tunachofanya kwa Neno Lako lililohifadhiwa.

Je, ni jambo gani muhimu zaidi ninaloweza kufanya ili kuwa Bibi-arusi Wake, Ndugu Branham?

Kaa moja kwa moja na Neno.

Majibu yote kwa maswali yetu yanaweza kufupishwa kwa maneno haya:

KAA MOJA KWA MOJA NA NENO.

Ujumbe huu NI Neno la wakati wetu. Ndugu Branham ndiye Sauti ya Mungu kwa Wakati wetu. Kila kitu lazima kiendane na Neno. Neno halihitaji Kufasiriwa kwokwote. TUNAPOBONYEZA PLAY, YOTE TUNAYOHITAJI YANATOLEWA HAPO, KWENYE HIZO KANDA.

Je, Una jambo fulani moyoni mwako unalohitaji jibu? Njoo uungane nasi Jumapili
saa 6:00 SITA MCHANA , saa za Jeffersonville, (Ni Saa 1:00 MOJA JIONI Ya Tanzania) tunapopata majibu yetu yote tunaposikia : 64-0823E – Maswali Na Majibu #2.

Ndugu. Joseph Branham

22-1002 Maswali na Majibu #1

UJUMBE: 64-0823M Maswali na Majibu #1

PDF

pakua – m4a

pakua – amr

BranhamTabernacle.org

Mpendwa Maskani ya Branham,

Kama hamwezi kuja hapa maskanini, tafuteni kanisa fulani mahali fulani; enendeni kwalo. Ikiwa huwezi kuzisikiliza kanda pamoja nasi, Zisikiliza kanda mahali fulani. Kucheza na kuzisikiliza Kanda ndilo jambo muhimu zaidi ambalo mhubiri, mwalimu, mtume, nabii, mwinjilisti au wewe unaloweza kufanya.

Hiki ndicho kituo changu cha nyumbani; haya ndiyo makao yangu makuu; hapa ndipo tumeimarika. Sasa, shikilia hilo mawazoni haijalishi itakuwaje. Sasa, kama mna busara, mtashika jambo fulani. Haijalishi itakuwaje, haya ndiyo makao yetu makuu, papa hapa! Na wekeni hilo mawazoni na mrejee kwenye kanda hii siku fulani, ambamo mlinisikia nikifanya unabii. Vema, kumbukeni hayo.

Nabii alikuwa akifanya nini? Akihifadhi Chakula. Akihifadhi Chakula ili kwamba tupate Kitu cha kula, ili kwamba tupate Kitu cha kufanyia karamu. Tumekiweka hicho kwenye kanda zetu tumeziweka katika chumba chetu chenye Baridi.

Alisema kulikuwa na ghala moja tu ndogo katika nchi hii yote , ghala moja ndogo. Aliweka tu Akiba nyingi ; Ile Ishara, Yakini, Mihuri, Nyakati Saba za Kanisa, Makao ya Baadaye ,kuthibitisha Neno Lake, yote kwa ajili yetu, kwa hiyo tungekaa hapa tu na kusikiliza Atakapokuwa ameondoka.

Yaonekana yuko mbali sana, lakini bado tunakumbuka, mambo haya ni kweli. Haya ni maisha ambayo yatubidi kutembea peke yetu.

Ghala ZIMEJAA . Hakuna Chakula kingine ambacho kimethibitishwa na Mungu mwenyewe kuwa ni NENO SAFI ambalo halijavunda.

Ikiwa ungependa kufanya karamu pamoja nasi, tunakukaribisha uungane nasi, Jumapili hii saa 6:00 SITA MCHANA . Saa za Jeffersonville (Ni saa 1:00 jioni ya Tanzania) tunapokuja Mezani na kula kama wageni Wake.

Maswali na Majibu 64-0823M

Ndugu. Joseph Branham

22-0925 Kuthibitisha Neno Lake

UJUMBE: 64-0816 Kuthibitisha Neno Lake

PDF

BranhamTabernacle.org

Mpendwa Chumvi ya Dunia ,

Wakati tu inaonekana kana kwamba haiwezi kuwa bora zaidi, Yeye anatupa Mzigo mwingine wa Kanda wa mafunuo. Tuna uwakilisho kwa kuchaguliwa tangu awali. Hiyo ndiyo sababu tunatoka mashariki na magharibi, kaskazini na kusini, ili kusikia Neno lililo hai likidhihirishwa.

Mungu alipoumba ulimwengu, tulikuwa katika mawazo yake. Wakati mshitaki wetu anapoendelea kutunyooshea kidole na kumwambia Baba, “walifanya hivi, walifanya hivi, walifanya hivi,” Damu ya Bwana wetu Yesu inatufunika. Tunapoomba, Mungu hatuoni, Yeye husikia tu sauti zetu kupitia Damu ya Yesu.

Shetani hawezi kusumbua; ama, anaweza kukujaribu, bali hawezi kumpata Mkristo aliyezaliwa mara ya pili. Kwa maana, Mungu, tangu kuwekwa misingi ya ulimwengu, alitangulia kumwona, na akamtuma Yesu kumkomboa, nayo ile Damu inanena kwa niaba yake. Anawezaje kufanya dhambi wakati, hata, haiwezi kuonekana na Mungu? Yeye hata haninii…Kitu pekee anachosikia ni sauti yako. Yeye huona uwakilisho wako. Amina! Hiyo ni kweli. Mnaona?

Nabii wa Mungu alituambia mambo haya. Hakuwa yeye aliyekuwa Akinena ; alionyesha tu mawazo ya Mungu, sifa Zake za mambo ambayo hayana budi kutendeka . Anatumia mdomo wake kuyaeleza. Na baada ya yeye kuyaeleza ,  lazima yatimie . “Mbingu na nchi zitapita, bali Neno Langu halitashindwa kamwe.”

Amethibitisha Neno Lake kwetu tena na tena. Je, hajatuthibitishia kuwa: Mwana wa Adamu aliyefanyika mwili kati yetu? Je! hajatuthibitishia: Nabii wetu anatimiza kila andiko linalomuhusu ? Je, hajatuthibitishia: Sisi ni Bibi-arusi Wake? Je, hajatuthibitishia: Tunao ushahidi wa kweli wa Roho Mtakatifu?

Tuna wasiwasi wa nini basi? Ametuthibitishia, ikiwa tutamshindania Naye, Atatushindania . Neno Lake haliwezi kushindwa kamwe.

Wote wanaoamini Ujumbe huu na mjumbe wa wakati huu wataokolewa. Wote wasiouamini Ujumbe na Mjumbe, wataangamia pamoja na ulimwengu .

Sikilizeni kwa makini enyi kanisa. Wengi sana hawaelewi, ama hawana Ufunuo wa Neno. Wanahisi tunamtukuza sana mtu huyu. Ikiwa kweli unaamini Ndugu Branham ni nabii wa Mungu, basi fungua moyo wako na nafsi yako na usikilize kile isemacho Bwana Asema Hivi .

Ni kitu gani kitakachomleta Bibi-arusi pamoja? Ni nini kitakachomuunganisha Bibi-arusi kuwa Mmoja na Mungu?

“ Katika siku hiyo Mwana wa Adamu atafunuliwa.” Nini? Kuliunganisha Kanisa kwa kile Kichwa, kuliunganisha, arusi ya Bibi-arusi. Wito wa Bwana Arusi utakuja hapa , wakati Mwana wa Adamu atakaposhuka aje katika mwili wa mwanadamu kuunganisha hivyo viwili pamoja. Kanisa halina budi kuwa Neno, Yeye ni Neno, na hivyo viwili vitaungana pamoja, na kufanya hivyo, itachukua dhihirisho la kufunuliwa kwa Mwana wa Adamu.

Itachukua dhihirisho la kufunuliwa kwa Mwana wa Adamu. Si wazo lako, si uelewa wako, si mawazo yako wala mahubiri yako. Mwana wa Adamu atamuunganisha Bibi-arusi pamoja na Bwana-arusi, nalo linatendeka HIVI SASA .

Hivi sasa tuko kwenye Karamu ya Harusi na Bwana Harusi na hivi karibuni tutaondoka kwenda kwenye Karamu yetu ya Arusi na Fungate.

Neno na Kanisa wanakuwa mmoja. Lo lote afanyalo Mwana wa Adamu, Yeye alikuwa Neno, Kanisa linafanya jambo lile lile .

Tunaweza tu kuishi kwa kila Neno litokalo katika Kinywa cha Mungu! Mungu amethibitisha kwamba nabii wetu ndiye Mnenaji wa Mungu kwa ajili ya wakati huu. Tunajuaje kuwa ni Neno la Mungu? Yeye amesema hivyo, ndipo akalithibitisha kwa Neno Lake.

Sisi ndio Kanisa-Bibi-arusi Aliye tayari katika siku za mwisho. Aliyeitwa kutoka katika mengine yote; yule ndege mwenye madoadoa kwa Damu Yake.

Baba, mioyo yetu inarukaruka, na moyo wangu unapigapiga, ninapowazia hayo na kujua ya kwamba maneno yako ni kweli, hamna hata moja linaloweza kushindwa .

Hii ndiyo njia pekee iliyoandaliwa na Mungu kwa siku hii. Ndiyo njia PEKEE ya kutobadilisha Neno moja. Kumbuka, Roho Mtakatifu anaweza kuja na kumtia mtu mafuta, na bado ni nje ya Mapenzi ya Mungu. NI LAZIMA TUDUMU NA NENO LA ASALI LILILOLITHIBITISHWA.

Ikiwa ungependa kudumu na Neno hilo na kusikia Sauti ya Mungu pamoja nasi, ninakualika uungane nasi Jumapili hii saa 6:00 SITA MCHANA , saa za Jeffersonville,(ni Saa 1 :00 MOJA JIONI Ya Tanzania),tunaposikia: Kuthibitisha Neno Lake  64-0816 .

Si lazima uungane nasi au hata kusikia kanda ile ile kwa wakati mmoja pamoja nasi, lakini ninakusihi, msikie nabii wa Mungu.

Ndugu. Joseph Branham

Maandiko ya kusoma kabla ya ibada:

Mathayo Mt 24:24

Marko Mt 5:21-43 / 16:15

Luka Mt 17:30 / 24:49

Yohana Mt 1:1 / 5:19 / 14:12

Warumi 4:20-22

I Wathesalonike 5:21

Waebrania 4:12-16 / 6:4-6 /13:8

1 Wafalme 10:1-3

Yoeli 2:28

Isaya 9:6

Malaki 4

22-0918 Makao Ya Baadaye Ya Bwana Arusi Wa Mbinguni Na Bibi-Arusi Wa Duniani

UJUMBE: 64-0802 Makao Ya Baadaye Ya Bwana Arusi Wa Mbinguni Na Bibi-Arusi Wa Duniani

PDF

pakua – m4a

pakua – amr

BranhamTabernacle.org

Rafiki wapendwa kwa Nabii ,

Moyo wangu unabubujika kwa furaha ninapowazia kuhusu sisi kukusanyika pamoja Jumapili hii ili kusikia Sauti ya Mungu ikisema nasi. Hakuna furaha kubwa maishani mwangu kuliko kuwa katika uwepo wa Roho Mtakatifu na kumsikia akisema na Bibi-arusi Wake, mdomo kwa sikio.

Hakuna kitu kingine katika ulimwengu huu kinachonipa furaha na amani, ila Neno Lake. Ninaposikia tu, “Habari za Asubuhi Marafiki,” mimi huketi tu, nikastarehe, na kunywa kutoka kwenye Kisima hicho kinachofoka maji kikiniambia Maneno ya Uzima wa Milele. Kuwazia, Mungu alimtuma kwangu MIMI NA WEWE, nasi ni MARAFIKI wa nabii wa Mungu na mjumbe.

Anatupenda sana hivi kwamba Alimtuma nabii Wake atuambie yote yahusuyo Makao yetu ya Baadaye. Alifurahishwa sana kutuambia yote yahusuyo hilo, hata kwa undani zaidi kuliko alivyoambiwa Yohana. Ametufunulia, Si mji wenye umbo la mraba, bali ni mji wenye umbo la piramidi, ambako Mwana-Kondoo atakuwa juu yake na Nuru ya ulimwengu.

Anatujulisha barabara zitajengwa kwa dhahabu na nyumba tutakazoishi zitakuwa za dhahabu safi sana. Yeye anaweka kila kitu kidogo jinsi tunavyopenda hasa, jinsi tungetaka tu. Hajaacha kitu chochote. Mjenzi wa Kiungu ameubuni kwa ajili yetu SISI, Mpendwa wake.

Miti ya Uzima itakuwako kule, nayo itazaa aina kumi na mbili za matunda. Na hayo Malango ya mji hayatafungwa usiku, kwa maana hakuna usiku kule, Yeye atakuwa ndiye Nuru yetu.

Ni nani atakayekuwa kule?

Ni akina nani waliokuja kwenye nchi mpya pamoja na nabii Nuhu? Hao walioingia pamoja naye safinani. Hiyo ni kweli? Hao ndio wanaotoka na kutembea mle. Mnaona? Hao walioingia pamoja na Nuhu, kwa ujumbe wake, hao ndio waliotoka wakatembea juu ya nchi mpya baada ya ubatizo wake wa maji .

Anazungumza kuhusu SISI marafiki zangu! Tuko ndani ya Safina yetu ya siku hii; Neno Lake, Ujumbe Huu, pamoja na Nuhu wetu Nabii . Na huko ng’ambo katika Nchi hiyo, Mji ule ambako Mwana-Kondoo ndiye Nuru, yeye atatujua SISI. Sisi ni watu wake, vito katika taji yake. Tumetoka Mashariki na Magharibi, kuja kwenye mji uliojengwa mraba. Mji ule ambao Ibrahimu alikuwa anautafuta.

Huku nikiona Neno likijidhihirisha Lenyewe , ninajua, bila shaka hata kidogo, vito vya taji yangu vitang’aa kuliko kitu cho chote kile ulimwenguni, katika Siku ile.

Je! twaweza hata kuanza kuwazia… Nabii wa Mungu alisema, ALIJUA, bila shaka hata kidogo , ya kwamba SISI ni vito vya taji yake, na tutang’aa kuliko kitu chochote kile ulimwenguni katika siku ile . Haleluya… Utukufu…Jina la Bwana lisifiwe.

Marafiki, kama tunafikiri ni la ajabu, tukiketi pamoja kutoka kote ulimwenguni, tukisikiliza na kula Neno Lake katika kanda hizi, itakuwaje tutakapoishi katika mji ule pamoja Naye!

Nabii wa Mungu atakuwa jirani yetu wa karibu, na tutakapokula hiyo miti, na tutakapotembea kwenye barabara hizo, tutakapotembea kwenye barabara hizo za dhahabu kwenye chemchemi, kunywa kutoka kwenye chemchemi, kutembea katika paradiso za Mungu, huku Malaika wanarukaruka kuizunguka dunia, wakiimba nyimbo za sifa.

Loo, itakuwa ni Siku ya namna gani! Inastahili kwa vyote. Njia inaonekana inaparuza, wakati mwingine inakuwa ngumu, lakini, loo! itakuwa kitu kidogo sana nitakapomwona Yeye, kidogo sana. Vipi yale majina mabaya na mambo ambayo wao wamesema, hayo yatakuwa nini nitakapomwona Yeye katika Mji ule mzuri, mzuri sana wa Mungu?

Marafiki, siwezi kusubiri kuona, na kuwa katika mji ule. Ninatamani kuwa kule pamoja na Bwana na Mwokozi wetu, nabii Wake, na pamoja na kila mmoja wenu.

Ninaelekea kwenye Mji ule mzuri
Bwana wangu ameuandaa kwa walio Wake ;
Wakati wote Waliokombolewa wa nyakati zote Wataimba “Utukufu!”
Wakikizunguka Kiti Cheupe cha Enzi
Wakati mwingine ninatamani Mbinguni sana, Na utukufu nitakaouona kule
Itakuwa ni furaha jinsi gani nitakapomwona Mwokozi wangu ,
Katika Mji ule mzuri wa dhahabu!

Ninaualika ulimwengu uje kuungana na sisi, marafiki wa nabii, tunapokusanyika kukizunguka Kiti Chake cha Enzi ili kusikia Sauti ya Mungu ikisema nasi saa 6:00 SITA MCHANA , saa za Jeffersonville,( ni Saa 1:00 MOJA JIONI Ya Tanzania) tunapomsikia Yeye akituambia yote kuhusu : Makao Ya Baadaye ya Bwana Arusi wa Mbinguni na Bibi-arusi wa Duniani 64-0802 . Naweza kukuahidi, itakuwa Sikukuu katika maisha yako.

Ndugu. Joseph Branham

Maandiko ya kusoma kabla ya kusikiliza Ujumbe :

Mathayo Mt. 19:28

Yohana Mt. 14:1-3

Waefeso 1:10

2 Petro 2:5-6 / Sura ya 3 yote

Ufunuo 2:7 / 6:14 / 21: 1-14

Mambo ya Walawi 23:36

Isaya Sura ya 4 yote / 28:10 / 65:17-25

Malaki 3:6

22-0911 Mabirika Yavujayo

UJUMBE: 64-0726E Mabirika Yavujayo

PDF

pakua – m4a

pakua – amr

BranhamTabernacle.org

Wapendwa Wanywaji wa Maji ya Kisima Kinachofoka Maji.

Hatukupandikizwa, sisi ni sehemu ya uzao asili wa Neno. Roho Mtakatifu Mwenyewe, ameivisha, amethibitisha, na kujidhihirisha Mwenyewe kwetu. Tumelikubali kwa utimilifu Wake, kwa uwezo wa thibitisho lake na Ufunuo wa kile lilicho, nasi tumekuwa sehemu Yake. Ni zaidi ya uhai kwetu.

Roho Mtakatifu Mwenyewe alinena kupitia chombo kinyenyekevu, kisichostahili na kusema, “Hii hapa Fimbo Yangu ya kifalme , Neno Langu, lichukue, uende zako, na uupeleke Ujumbe.” Alichukua Neno Lake na kutubangua, kutufanya kuwa Bibi-arusi Wake.

Imewasumbua makasisi kuona watu wakitoka makanisani na kwenda kucheza kanda. Walisema, “Ikiwa yeyote wenu atahudhuria hiyo mikutano, utatupwa nje , tutakuweka nje ya shirika letu”.

Jibu lao ni: Mnaweza pia kutuachilia, tutaendelea hata hivyo! Tuko safarini pamoja na Bwana Yesu, Mwamba wetu uliopigwa, tukila Chakula cha malaika, mana iliyohifadhiwa ghalani kutoka juu, na kunywa kutoka kwenye Mwamba huo. Hatupaswi kamwe kuhangaikia kile tunachokunywa, Si chochote ila NENO SAFI.

Daima tumekuwa na uamsho unaoendelea. Chemchemi yetu daima inabubujika tena na tena, na tena na tena. Hakuna mwisho wake.
Tunapata kinywaji safi na baridi cha maji kila tunapobonyeza Play. Tunakitegemea na tunaishi kwacho. Jambo likupasalo kufanya tu ni kwenda kule na Unywe.

Tunaishi kwa chemchemi hiyo kila siku! Haitubidi kuvuta, kuchimba, kuvuta kwa mashine, au chochote kile; tunashiriki tu katika njia aliyoiandaa yeye , bure . Unaweza kuchukua taratibu zako zote zakujitengenezea unazotaka, visima vyako vyote vya kale vya maji yanayooza; kwetu sisi, tumekuja kwenye Chemchemi yake safi. Ni Furaha yetu. Ni Nuru na Nguvu zetu.

Yeye ndiye furaha yangu. Yeye ndiye Nuru yangu. Yeye ni—Yeye ni nguvu zangu. Yeye ni Maji yangu. Yeye ni Uzima wangu. Yeye ni Mponya wangu. Yeye ni Mwokozi wangu. Yeye ni Mfalme wangu. Kila ninachohitaji kinapatikana Kwake. Kwa nini niwe na hamu ya kukiendea kitu kingine?

Kwetu sisi hakuna mahali pengine pa kwenda ila moja kwa moja kwenye Chemchemi iliyotolewa na Mungu. Hatuna hofu kamwe tutakunywa nini. Haitulazimu kuweka kitambaa cha kale cha kuchujia ambacho kinaweza kutoa vitu vikubwa, lakini huacha juisi mbaya. TUNAPATA TU MAJI SAFI YA KISIMA KINACHOFOKA MAJI YENYE MADINI NA VIRUTUBISHO VYOTE TUNAVYOHITAJI.

Ametuhakikishia: Watoto wangu wachanga , msiwe na wasiwasi tena, mnao ushahidi wa kweli wa Roho Mtakatifu. Mmenithibitishia Mimi ya kwamba mnaamini kila Neno. Mmelipokea, NINYI NI WANGU. SISI NI KITU KIMOJA. MUME NA MKE.

Ninakuja kwa ajili yenu katika muda mfupi, katika kufumba na kufumbua jicho. Ninawaandalia Makao mapya. Mtapenda jinsi nilivyoyafanya.
Najua ni ngumu sana kwenu sasa, na mna mitihani mingi na majaribu na mizigo yenu ni mizito. Lakini msisahau, hamna chochote cha kuhofia , Nimewapa Neno Langu. Ninyi ni Neno Langu . Tayari nimefanya kila kitu kwa ajili yenu. Nena Neno na msiwe na shaka. Mnayo Imani yenu, pamoja na nabii Wangu aliwapa Imani yake.

Ningependa uungane nasi Jumapili hii saa 06:00 SITA MCHANA , saa za Jeffersonville, ( Ni saa 1:00 MOJA JIONI Ya Tanzania) kusikia 64-0726E Mabirika Yavujayo , na kunywa kutoka kwenye Chemchemi hii inayofoka maji inapobubujisha Neno Safi ambalo halihitaji chujio.

Ndugu. Joseph Branham

Maandiko ya kusoma kabla ya kusikiliza ibada

Zaburi 36:9
Yeremia 2:12-13
Yohana Mtakatifu 3:16
Ufunuo Sura ya 13 yote.

22-0904 Kutambua Siku Yako Na Ujumbe Wake

UJUMBE: 64-0726M Kutambua Siku Yako Na Ujumbe Wake

PDF

pakua – m4a

pakua – amr

BranhamTabernacle.org

Wapendwa Waliokatwa Watoke,

Nataka kila mtu ajue kwanini tunafuraha sana jinsi hii!!

Tumelikubali Neno la Bwana. Neno lililofunuliwa lililonenwa, na nabii wa Mungu wa Malaki 4. Sisi ni Bibi-arusi wa Yesu Kristo. Sisi Ndio ambao tumedumu waaminifu kwa Sauti Yake iliyothibitishwa. Sisi ndio ambao Aliyowapa Lulu ya thamani kuu, Ufunuo wa kweli wa Ujumbe Wake na mjumbe Wake.

Mungu amechukua Neno la nabii Wake na kumbangua Bibi-arusi anayeamini kila nukta na kila yodi. Ametukata, kama alivyoahidi atafanya. Sisi ni kondoo wa Mungu, na tunaisikia tu Sauti ya Mungu! “Kondoo Wangu huisikia Sauti Yangu,” tunapobonyeza Play.

Tuna Washiriki kutoka kote nchini; kutoka New York, kutoka Massachusetts, hadi Boston, Maine, Tennessee, Georgia, Alabama, na kote nchini. Kutoka Afrika hadi Mexico, Ulaya hadi Australia, tunakusanyika pamoja, chini ya Ujumbe Mmoja, Sauti Moja, nayo inamuunganisha Bibi-arusi kwa ajili ya Kunyakuliwa.

Nabii wetu, mjumbe wa Mungu, Mwana wa Adamu akijifunua Mwenyewe katika mwili, anapaza sauti, “Shetani, ondoka njiani, nina Ujumbe wa Mfalme. Mimi ni Mjumbe wa Mfalme. Nina Neno lililothibitishwa la siku hii. Nimekusudiwa kumwita Bibi-arusi Wake atoke na Kumwongoza.”

“Ninajaribu kuwavuta watu fulani, kuwakata niwaondoe kwenye mambo haya. kuwavuta watoke; kuwaonyesha, kwa Maandiko, ya kwamba Mungu amesimama hapa; pamoja na thibitisho la Nguzo ya Moto”

Mungu ametambua ya kwamba kuna watu fulani ulimwenguni ambao aliwakusudia Uzima. Alitambua ulikuwa ni wakati wa kumtuma mjumbe Wake kumwita Bibi-arusi Wake atoke, Hivyo Yeye Akamtuma . Sisi Ndio wale Waliotambua jambo hilo. Sisi ndio wale Aliojua tungeamini kila Neno.

Ibrahimu alitambua ya kwamba Mungu alikuwa akisema naye katika mwili wa Kibinadamu. Alitambua ishara Yake na kumwita B-W-A-N-A, Elohim, na akabarikiwa na Bwana. Tumetambua ya kwamba kama ilivyokuwa katika siku hiyo, ndivyo itakavyokuwa wakati Mwana wa Adamu atakapodhihirishwa, Elohim, akinena katika mwili wa kibinadamu.

Sisi ni sehemu yake, na Mwanawe, na tutadumu naye milele. Si kwa wito wetu au uchaguzi wetu, bali kwa uchaguzi wake. Hatukuwa na uhusiano wowote nalo. Yeye ndiye aliyetuchagua kabla ya kuwekwa misingi ya ulimwengu.

Haidhuru utahubiri namna gani, hata ufanye nini, haliwezi kuivishwa, haliwezi kudhihirishwa, haliwezi kuthibitishwa; ila tu na Yeye aliyesema, “Mimi Ndimi Nuru ya ulimwengu,” lile Neno. Kwa hiyo hakuna budi kutokee Nguvu fu—fu—fulani, Roho Mtakatifu Mwenyewe, kuivisha, ama kuthibitisha, ama kuhakikisha, ama kudhihirisha ya kwamba yale ambayo Yeye amebashiri yangetukia katika siku hii. Nuru ya jioni inaleta hilo. Ni wakati wa jinsi gani!

Alituona katika lile ono tulipokuwa tukipita mbele yake. Tulipitia mahali pale pale alipopitia Bibi-arusi wakati alipopitia hapo mwanzo, Alfa na Omega. Alikuwa akiangalia wengine wakitoka mstarini, na alikuwa akijaribu kumvuta , lakini sisi ndio Wale tuliopaza Sauti, “Tunategemea jambo Hilo.”

Angalia, “Kama vile Yane na Yambre pia walivyompinga Musa,” yeye atakuja moja kwa moja, baadhi yao . Si , sasa, yeye hazungumzi kuhusu Mmethodisti, Mbaptisti, hapa; wao wako nje ya picha . Unaona? “Lakini kama vile Yane na Yambre walivyoshindana na Musa na Haruni, vivyo hivyo hao nao; watu walioharibikiwa na akili zao kuhusu ile Kweli.” wamepotoka wakaingia katika mafundisho ya sharti na mafundisho ya kanisa, badala ya Biblia.

Jinsi inavyotupasa kuwa waangalifu sana kudumu na Neno la kweli, lililothibitishwa la siku yetu. Ni lazima kila wakati tukumbuke na kutambua Neno humjia nani. Ni nani aliye mfasiri pekee wa kiungu wa Neno? Ni nani Aliye Neno la siku yetu ?

Roho wa Mungu, ambaye ni Neno la Mungu, “Neno Langu ni Roho na Uzima,” litamweka Bibi-arusi mahali Pake. Kwa maana, Yeye Atatambua nafasi yake katika Neno, ndipo anakuwa ndani ya Kristo, litamweka kwenye nafasi yake .

Umealikwa kuja kusikiliza Sauti pekee ya Mungu iliyothibitishwa ya siku yetu, na kutambua nafasi yako katika Neno na kuwekwa mahali pako tunapomsikia Elohim akisema kupitia nabii Wake na kutuletea Ujumbe: Kutambua Siku Yako na Ujumbe Wake 64-0726M , saa 06:00 MCHANA , saa za Jeffersonville (Ni Saa 1:00 MOJA JIONI Ya Tanzania.)

Ndugu. Joseph Branham

Maandiko ya kusoma kabla ya kusikia Ujumbe:

Hosea: Sura ya 6 yote

Ezekieli: Sura ya 37 yote

Malaki: 3:1 / 4:5-6

2 Timotheo: 3:1-9

Ufunuo: Sura ya 11 yote

Mungu, umba ufufuo ndani yangu! Jalia niwe huo ufufuo. Jalia kila mmoja wetu awe huo ufufuo, ufufuo ndani yangu. Nifanye mimi, Bwana, nipate njaa, nifanye nione kiu. Umba ndani yangu, Bwana, kile ambacho kinahitajika ndani yangu. Nijalie, tangu saa hii na kuendelea, niwe wako; mtumishi aliyewekwa wakfu zaidi, mtumishi bora, aliyebarikiwa zaidi na Wewe; mwenye uwezo zaidi, mnyenyekevu zaidi, mwema zaidi, mwenye kupenda kufanya kazi zaidi; mwenye kuangalia zaidi mambo ambayo ni ya kweli, na kusahau mambo yaliyo nyuma, na mambo yasiyo ya kujenga. Jalia nikaze mwendo kuelekea kwenye mede ya wito mkuu wa Kristo. Amina.

Rev. William Marrion Branham