All posts by admin5

RATIBA YA KRISMASI!

Ndugu na Dada Wapendwa,

Kwa sababu ya Krismasi kuwa kwenye siku ya Jumapili mwaka huu, nimejisikia moyoni mwangu kutokuwa na wakati maalum wa sisi kusikiliza Ujumbe siku hiyo. Familia nyingi zina watoto wadogo ambao huchangamka sana kufungua zawadi zao asubuhi ya Krismasi, na itakuwa vigumu sana kwao kutulia kusikiliza Ujumbe au kuwafanya wangoje hadi wakati fulani baadaye.

Na, hata hivyo, kwenye Krismasi, mwajua, watoto wadogo, huwezi kuwaambia vinginevyo. Wao, ninii tu, ni wakati wa Krismasi kwao. Nao wasingetaka maskini soksi zao zitundikwe, kungekuwa na kitu fulani. Ni desturi, hata katika taifa letu, kwamba wanatundika soksi, na kitu kingine. Mbona, nilifanya hivyo, nilipokuwa mtoto, na—na ingawa liko mba—mbali sana na Maandiko, njia iliyowekwa kama lilivyo. Hata hivyo, watoto ni ninii, wanasikia watoto wengine wakisema, “Vema, nilipata hiki kwa ajili ya Krismasi. Nilipata hiki.” Jamaa hao wadogo wanasimama huku, wanaangalia, mwajua. Huwezi, huwezi kuwafanya waelewe. Unaona? Kwa hiyo, kwamba tu, Krismasi itadumu. Naam.

Pia kunaweza kuwe na wengine ambao wangependelea kuamka mapema na kusikiliza Ujumbe, kama walivyopanga na washiriki wengine wa familia zao baadaye siku hiyo. Kwa hiyo nimeamua kwa kila familia kuchagua wakati ambao ungelingana vyema na ratiba yao ya kusikiliza Ujumbe. Tutatangaza Ujumbe huo kwenye Lifeline mara tatu tofauti Siku ya Krismasi:  Saa 3:00 Tatu Asubuhi . – Saa 06:00 Sita Mchana. – Saa 11:00 Kumi na moja Jioni. Tafadhali usijisikie kuwa ni lazima usikilize wakati mmojawapo wa nyakati hizi, lakini chagua wakati unaofaa zaidi kwako au kwa familia yako. Jambo muhimu zaidi ni, KUBONYEZA PLAY.

Inaweza ionekane kwa namna fulani inachekesha, asubuhi hii, kuvaa kabuti langu jukwaani, bali nilifurahia sana ku—kuonyesha hilo kabuti zuri nililopewa na kanisa hili. Nilimuona Ndugu Neville hapa juzijuzi, amevaa ile suti ya kupendeza, jinsi ilivyomkaa vizuri mno, na nikawaza, vema, ni…Ilionekana nzuri mno, na kusanyiko langu linazungumzia habari zake, nikafikiri, “Nitavaa tu kabuti jukwaani.”

Unajua, ninaamini kamwe hatukui. Sikuzote tu…Nami sitaki kukua. Unalionaje hilo, Ndugu Luther? La, kamwe hatutaki kukua, tunapenda siku zote tu kudumu tukali watoto.

Bwana na awape Sikukuu yakupendeza iliyojaa Uwepo Wake.

Ndugu. Joseph Branham

22-1218 Je! Mungu Hubadilisha Nia Yake Kuhusu Neno Lake?

Ujume: 65-0418E Je! Mungu Hubadilisha Nia Yake Kuhusu Neno Lake?

PDF

pakua – m4a

pakua – amr 13MB (use Firefox to download)

BranhamTabernacle.org

Wapendwa Masihi Wadogo,

Sisi ni watiwa-mafuta wa Mungu; waliotiwa mafuta na Roho Wake yule yule, kwa kazi zile zile, kwa Nguvu zile zile, kwa ishara zile zile. Imetoka tai hadi tai, kutoka Neno hadi Neno mpaka utimilifu wa Yesu Kristo udhihirishwe katika kila mmoja wa miili yetu kwa hitaji la kimwili , kiroho, au hitaji lolote tunalohitaji. Hizo Nguvu za kuhuisha zinaishi na kukaa ndani yetu. Sisi ni Masihi wadogo wa Mungu.

Kila wiki Ufunuo wa Ujumbe huu; sisi ni nani, wapi tunatoka, na wapi tunakoenda, unakuwa mkubwa zaidi na zaidi. Twajiuliza kwa matarajio makuu, lawezaje kuwa tukufu zaidi? Laweza kuwa wazi zaidi kiasi gani? Lakini kwa kila kanda mpya tunayosikia, Mungu ananena nasi mdomo kwa sikio na kutufunulia zaidi Neno Lake, na kutuhakikishia, SISI NI NANI.

Shauku kubwa ya moyo wa kila mwamini ni kuwa katika MAPENZI MAKAMILIFU ya Mungu. Kamwe hatutaki kuwa katika mapenzi Yake ya kuruhusia. Mioyo yetu huvunjika na kupondeka ikiwa tunahisi tumefanya jambo lolote ambalo litamchukiza. Tunajua Mungu anayo Mapenzi makamilifu, nasi tunataka tu kuwa katika MPANGO WA MAPENZI YAKE MAKAMILIFU.

Katika maisha yangu, nimekuwa na msimamo mkali kwa kusema ninaamini jambo lililo muhimu zaidi ambalo kila mshiriki wa Bibi-arusi analoweza kufanya, washirika na wahudumu vilevile , ni KUBONYEZA PLAY . Ninaamini ndiyo Sauti ya Mungu PEKEE iliyothibitishwa kwa ajili ya Siku yetu ambayo lazima usikie na kutii kila Neno.

Nimesema ninaamini wahudumu wanahitajika kumrudisha Ndugu Branham kwenye mimbara zao na kucheza kanda katika makanisa yao, kwa kuwa Ndiyo Sauti moja muhimu sana iliyopo ambayo watu hawana budi kuisikia.

Nimepokea shutuma nyingi maishani mwangu kwa kuchukua msimamo huu kwa kile ninachoamini kuwa Mpango Wake na Mapenzi yake Makamilifu. Imeeleweka vibaya na kusemwa kwamba siamini katika huduma tano ya Waefeso 4.

Nimeeleza mara nyingi, nyingi sana huo ni uongo. Sijawahi kamwe kusema, wala sijawahi kuamini jinsi hiyo. Kuna wengi ambao wamepindisha maneno yangu na kuwaambia watu mambo ambayo sijawahi kusema ama kuamini, lakini hilo ni jambo la kutarajiwa.

Lazima kuwe na Kweli ya Neno la Biblia. Ikiwa unadai unaamini Ujumbe huu, basi hatuna budi kuchukua yale nabii aliyosema, kwani ndiyo fasiri halisi hasa ya Neno la Mungu. Kwa maana yeye ndiye mfasiri PEKEE wa Neno hilo.

Ikiwa ningewauliza kila mmoja wenu, “Ni nani anayetaka kuwa katika mapenzi makamilifu ya Mungu?”
Kila mmoja wenu angesema, “NDIYO, hiyo ndiyo haja ya moyo wangu.” Hivyo ni lazima tuangalie kwenye kile nabii alichosema ni Mapenzi Makamilifu ya Mungu.

KUMBUKA: Ikiwa Ujumbe huu ulio kwenye kanda si Yakini yako, na huamini kila Neno, ACHA KUSOMA BARUA HII. Kwangu mimi, wewe si mwamini, kwa hivyo sio kwa ajili yako. Mimi Ninaweza tu kukaa na yale Mungu aliyosema kwenye kanda.

Tunataka alichosema Yeye; si kile kanisa lilisema, kile alichosema Daktari Jones, kile alichosema mtu mwingine. Tunataka kile BWANA ASEMA HIVI ilichosema, kile Neno lilichosema.

Inatupasa kujikabidhi wenyewe kwenye mapenzi Yake na kwenye Neno Lake. Hatupaswi Kulitilia swali. Yatubidi Kuliamini tu. Usijaribu kutafuta njia ya kuliepa. Lichukue tu jinsi lilivyo.

Watu wengi wanajaribu kuepa, kupitia njia nyingine. Nawe unapofanya jambo hilo, Mungu atakuwa akikubariki, bali unafanya kazi katika mapenzi Yake ya kuruhusia wala si mapenzi Yake makamilifu, ya Kiungu. Mungu atakuruhusu kufanya jambo fulani, na hata akubariki katika kulifanya, bali hata hivyo si mapenzi Yake makamilifu.

Mungu alimtuma malaika-mjumbe wake wa saba duniani kumwita Bibi-arusi Wake atoke . Tunaamini ilikuwa ni Mwana wa Adamu akijifunua Mwenyewe katika mwili wa mwanadamu. Ni Sauti yenyewe hasa ya Mungu ambayo imerekodiwa na kuhifadhiwa kwa ajili ya Bibi-arusi Wake.

Mungu mwenyewe alimwambia nabii wake, ukiwafanya watu WAKUAMINI , hakuna kitakachosimama mbele zako. Alikuwa ndiye aliyechaguliwa na Mungu kumwongoza Bibi-arusi Wake. Hakuna anayeweza kupachukua mahali pake. Haidhuru ni akina Kora wangapi walioinuka, ama Dathani wangapi, ilikuwa ni William Marrion Branham ambaye Mungu alimwita kumwongoza Bibi-arusi Wake. Huu ndio Mpango wa Mungu na MAPENZI YAKE MAKAMILIFU.

Iwapo watu hawatatembea katika mapenzi Yake makamilifu, Yeye ana mapenzi ya kuruhusia atakayokufanya uende kwayo.

Sasa, Mungu ni mwema…Yeye hutuma Neno Lake . Kama hutaamini Neno Lake, Basi ndipo anaweka katika Kanisa ofisi tano tofauti : Kwanza, mitume, manabii, walimu, wachungaji, wainjilisti. Ni kwa ajili ya kulikamilisha Kanisa.

Kwa hivyo, wahudumu waliinuliwa tu kwa sababu watu katika nyakati zote hawakukubali MPANGO WA MAPENZI MAKAMILIFU ya Mungu; Neno Lake lililonenwa na nabii Wake. Tunapaswa kuamini tu Neno ambalo nabii wa Mungu alilonena. Hatuhitaji mtu mwingine yeyote au kitu kingine chochote.

Basi kazi ya wahudumu ni KUWARUDISHA watu kwenye Mpango wa Mapenzi Yake Makamilifu, ambao ni: KAENI NA HIZO KANDA, KWA MAANA NI MAPENZI MAKAMILIFU YA MUNGU. Kisha weka MPANGO HUO WA MAPENZI MAKAMILIFU mbele zao kila wakati kwa: KUBONYEZA PLAY.

Huna budi kurudi na kuanzia mahali ulipoanzia, ama mahali ulipoachia, na kuchukua kila Neno la Mungu.

Kwa hivyo unapaswa kufanya nini ili uwe katika MAPENZI YAKE MAKAMILIFU : Kubonyeza Play .

Wachungaji wanapaswa kufanya nini ili wawe katika MAPENZI YAKE MAKAMILIFU: Kubonyeza Play.

Nabii wa Mungu alikuwa anafanyaje akienda kwenye mikutano? Kuombea tu wagonjwa, na kila kitu namna hiyo? Angesema mambo kwa njia isiyo dhahiri ambayo kondoo wangesikia, kwa sababu tunajua kile anachozungumzia. Ama kweli, ilikuwa tu ni chambo kwenye ndoano. Aliwaonyesha ishara kama utambuzi, na alijua siri za mioyo yao, ili tu kuwachochea watu. Lakini kisha akasema jambo muhimu zaidi lilikuwa ni :

Muda si muda, kanda inaangukia nyumbani mwao. Imelenga penyewe, basi. Kama yeye ni kondoo, anakuja moja kwa moja Nalo. Kama yeye ni mbuzi, anapiga hiyo kanda teke.

Je, Wewe ni kondoo au ni mbuzi? Kundi dogo la Mungu moyo wake uko kwenye Neno hilo. Tuko katika Mapenzi Yake Makamilifu kwa Kubonyeza Play kwa kuwa huo ulikuwa, na ndio, Mpango wake wa asili.

Kaa moja kwa moja na Neno Lake, maana hilo ndilo litakalotokea mwishoni, lile Neno, Neno kwa Neno. “Ye yote atakayeondoa Neno moja Kwake, ama kuongeza neno moja Kwake!” Halina budi kudumu, Neno hilo.

Ninamshukuru sana Bwana kujua, kwa Ufunuo wa kiroho, ya kwamba niko katika Mapenzi Yake Makamilifu kulingana na Neno Lake. Siongezi fasiri yangu Kwake, ama ufahamu wangu Kwake, bali ninasikia kwa masikio yangu BWANA ASEMA HIVI na Mapenzi Yake Makamilifu ni kitu gani .

Ninakualika uje Ukatafute madini pamoja nasi Jumapili hii saa 6:00 SITA MCHANA , saa za Jeffersonville,(Ni saa 2:00 MBILI USIKU ya Tanzania ) tunaposikia: Je! Mungu Hubadilisha Nia Yake Kuhusu Neno Lake? 65-0418E . Kuna vito vingi vya thamani sana katika Ujumbe huu, utakuwa TAJIRI katika Roho wake Mtakatifu tukimaliza.

Ndugu. Joseph Branham

Maandiko ya Kusoma Kabla ya Kusikiliza Ujumbe :

Kutoka sura ya 19 Yote
Hesabu 22:31
Mathayo Mtakatifu 28:19
Luka 17:30
Ufunuo sura ya 17 yote

22-1211 Ni Kuchomoza Kwa Jua

Ujume: 65-0418M Ni Kuchomoza Kwa Jua

PDF

pakua – m4a

pakua – amr 14MB (use Firefox to download)

BranhamTabernacle.org

Mpendwa Hekalu la Nguvu za Utendaji ,

Mwanadamu daima ametamani moyoni mwake kuwa kama Ibrahimu alipokuwa ameketi nyumbani kwake karibu saa 11:00. Aliiinua macho na kuwaona wanaume watatu wakija kwake wakiwa na vumbi kwenye mavazi yao. Akawakimbilia upesi, na kusema, “Bwana Wangu.” Aliyesimama pale mbele zake, katika mwili wa mwanadamu akinena, alikuwa ni Melkizedeki Mkuu.

Jumapili hii, shauku hiyo katika mioyo yetu itatimia kwa kila mmoja wetu. Sisi sote tutakusanyika pamoja kutoka ulimwenguni kote, tukimsikiliza Melkizedeki yule yule mkuu akizungumza NASI. Mtu ambaye hakuwa na baba, wala mama, hana mwanzo wa siku zake au mwisho wa uhai, Mungu,  en morphe , akizungumza nasi kupitia midomo ya mwanadamu, kama jinsi Alivyofanya siku hiyo kwa Ibrahimu.

Hakuna njia nyingine ya kusikia Sauti hiyo isipokuwa UBONYEZE PLAY. Hakujawahi kuwa na wakati katika historia ambapo Bibi-arusi ameungana kutoka kote ulimwenguni kuisikia Sauti ya Melkizedeki ikinena kwa wakati huohuo mmoja . Mungu anamuunganisha Bibi-arusi Wake kwa Sauti hiyo.

Tumekuwa, kwa miaka, na Neno la Mungu. Sasa tunaye Mungu wa Neno, mnaona, na papa hapa akiliishi Neno Lake. Kwa hiyo ni kweli, moja ya ishara kuu za mwisho zilizoahidiwa Kanisa kabla ya Kuja kwa Bwana.

Jumapili hii, Bibi-arusi atakuwa na Ujumbe wa Pasaka Desemba hii; na ni Ujumbe ulioje tutakaosikia.

Mitambo. Nguvu za utendaji. Nguvu za kuhuisha. Kristo aliyefufuka. Wana wa Mungu Waliodhihirishwa. Roho yule yule aliyekaa ndani ya Kristo anakaa ndani yetu. Uhai ule ule, nguvu zile zile, baraka zile zile, alizokuwa nazo, tunazo. Hati ya kumiliki. Ile Mbegu ya kwanza iliyopevuka inatikiswa mbele ya watu. Sisi sasa tu nyama ya nyama yake, mfupa wa mfupa Wake; uhai wa uhai wake, Nguvu za Nguvu Zake! Sisi ni Yeye!

Yesu Kristo aliyefufuka; Melkizedeki Mwenyewe, atatoa mlio na kutuambia, “Nilirekodi Sauti yangu na kuiweka kwenye kanda ya sumaku ili niweze kuwavuta ninyi kwangu, nami ningeweza kusema nanyi kama vile nilivyomfanyia Ibrahimu. Ninawataka msikie moja kwa moja kutoka Kwangu .”

Ninyi ndilo Kanisa langu lililochaguliwa na kukusudiwa tangu zamani! Miili yenu ni hekalu la Nguvu za Utendaji , kwa sababu tangu mwanzo mlikuwa sehemu ya ile Mitambo.

Huo ni ule ufunuo wa Kiungu wa Neno lililofanyika mwili. Kama lilikuwa mwili katika siku hiyo kwa njia ya Mwana, Bwana Arusi, ni mwili leo kwa Bibi-arusi. Mnaona?

Hizo Nguvu za Kuhuisha zinaishi ndani yetu. Hatupaswi kuogopa KITU. Roho yule yule aliyekuwa ndani Yake, sasa yu ndani yetu na anaihuisha miili yetu ipatikanayo na mauti. Hatutumaini hivyo, TUNAJUA HIVYO. Tayari tumefaulu, yeye alifaulu kwa ajili yetu.

Kisha, ili kuhitimisha alasiri, Melkizedeki atazungumza kwa mara nyingine tena na kusema;

Watu hawa, ambao ni raia wenzangu wa Ufalme, wenye kumiliki Nguvu za kuhuisha, lihuishe kwao, Bwana, sasa hivi . Naomba Roho aende kutoka tai hadi tai, kutoka kwenye Neno hadi Neno, mpaka utimilifu wa Yesu Kristo udhihirishwe katika kila mmoja wa hiyo miili, kwa ajili ya haja za kimwili, za kiroho, ama haja zo zote walizo nazo, tunapowekeana mikono. Katika Jina la Yesu Kristo.

Kutoka tai hadi tai, Neno hadi Neno, utimilifu wa Yesu Kristo utadhihirishwa katika kila mmoja wa miili yetu. UTUKUFU!!

Hili linaweza tu kutukia kwa KUBONYEZA PLAY, kwa hivyo njoo uungane nasi na ushiriki katika Yubile ya mlo bora wa Chakula kilichohifadhiwa , tunaposikia Sauti Hiyo, Jumapili saa 6:00 SITA MCHANA , saa za Jeffersonville, ( ni saa 2:00 MBILI USIKU ya Tanzania ) ikituletea Ujumbe, Ni Kuchomoza Kwa Jua 65-0418M .

Ndugu. Joseph Branham

Maandiko ya kusoma Kabla ya Kusikiliza Ujumbe :

Mambo ya Walawi 23:9-11
Mathayo 27:51 / 28:18
Marko 16:1-2
Luka Mtakatifu 17:30 / 24:49
Yohana Mtakatifu 5:24 / 14:12
Matendo 10:49 / 19:2
Warumi 8:11
1Wathesalonike 4:16
Waebrania 13:8
Ufunuo 1:17-18

22-1204 Huyu Melkizedeki Ni Nani?

UJUMBE: 65-0221E Huyu Melkizedeki Ni Nani?

PDF

BranhamTabernacle.org

Mpendwa Mawazo ya Mungu,

Natumai uko tayari kwa Jumapili hii. Nena kuhusu jinsi mioyo yetu itakavyowaka ndani yetu anaponena nasi njiani katika nyumba zetu na makanisa yetu…SUBIRI TU!

Katika mwezi huu uliopita Ametuambia tuhakikishe tunaingia katika Merikebu sahihi…na tuko. Alituambia ya kwamba Uzao halisi wa Mungu hautarithi pamoja na kapi…ndipo akasema, SISI NDIYO UZAO HUO. Kisha, tukasikia kwa masikio yetu, Mungu akinena kupitia mwanadamu na kututangazia, Leo, Maandiko haya yametimia mbele ya yaya haya macho yetu.

Alituambia Jumapili iliyofuata kwamba tuko katika Mahali palipoandaliwa na Mungu pa Kuabudia, na kwa sababu tuko, HATUJAFANYA uzinzi na Neno Lake. Kwa hiyo, sisi ni Bibi-arusi Neno Bikira Safi wake.

Jumapili hii, Yeye atatuunganisha sisi sote kwa mara nyingine tena na kunena kupitia Malaika-Nabii Wake mkuu na kutuambia, MIMI NDIMI HUYU MELKIZEDEKI, nami ninajidhihirisha kwenu katika mwili wa kibinadamu, kama vile nilivyosema nitafanya katika Neno Langu.

UTUKUFU! Je, umefuraishwa? Je, umebarikiwa Kusikotamkika? Vema, KUNAYO MENGI ZAIDI YAJAYO. Anaenda kukamilisha hadithi hii kuu.

Wazia Hilo, TULIKUWA katika mawazo hasa ya Mungu tangu mwanzo. Miaka elfu nne kabla ya Yesu hajaja duniani, na miaka elfu kadhaa kabla hujaja duniani, Yesu, katika Mawazo ya Mungu, alikufa kwa ajili ya dhambi zetu. NA KISHA , MAJINA YETU yakawekwa kwenye Kitabu cha Uzima cha Mwana-Kondoo.

Je, hilo linazama niani mwako? Majina yetu yaliteuliwa na Mungu na kuwekwa kwenye Kitabu cha Uzima cha Mwana-Kondoo kabla kabisa ya kuwekwa misingi ya ulimwengu. Alijua macho yetu, kimo chetu, chochote tulicho. Tulikuwa katika mawazo Yake hapo mwanzo….katika mawazo ya Mungu! Basi, kitu pekee tulicho ni Neno la Mungu lililodhihirishwa. Baada ya Yeye kuliwaza, akalinena, nasi hawa hapa.

Ni vigumu kuelewa. Mungu akituambia mambo haya yote. Alitupenda sana hivi kwamba alitaka kuhakikisha kwamba tutalisikia moja kwa moja kutoka Kwake Mwenyewe , hivyo akafanya irekodiwe ili kwamba Jumapili, Desemba 4, 2022, Angeweza tena kumleta Bibi-arusi Wake pamoja na kutuambia: “Nilifanya haya yote kwa ajili yako wewe. Nilitaka ulisikie moja kwa moja kutoka Kwangu. NAKUPENDA. WEWE NI BIBI-ARUSI WANGU. NAKUJA KUKUCHUKUA HIVI KARIBUNI .”

Ndiyo maana tunajua tunapoingia katika Uwepo wa Mungu, kitu fulani ndani yetu kinatuambia ya kwamba tunatoka mahali fulani, nasi tunarudi tena kwa Nguvu hizo zinazotuvuta.

Mungu ameondoa kinyago kwenye kitu hicho chote na tunaweza kukiona. Mungu, en morphe, aliyetiwa kinyago katika Nguzo ya Moto. Mungu, en morphe, katika Mtu aliyeitwa Yesu. Mungu, en morphe, katika Kanisa Lake. Mungu juu yetu, Mungu pamoja nasi, Mungu ndani yetu; Mungu Anayejidhili.

Hatuna chochote cha kuogopa. Hakuna cha kuhofia, hata kifo. Tunapoondoka hapa, hata hatujafa. Nyumba ya maskani yetu iliyo ya dunia hii  ikiaribiwa, tuna nyingine TAYARI inayotungoja, En morphe.

Ni Vigumu Kwangu kungojea kumsikia akizungumza nasi na kufunua mambo haya yote Jumapili hii saa 6:00 SITA MCHANA , saa za Jeffersonville. (Ni saa 2:00 MBILI USIKU ya Tanzania) Njoo uungane nasi Katika mahali pekee unapoweza kusikia SAUTI YA MUNGU iliyothibitishwa ikikuambia mdomo kwa sikio Yeye NI NANI , sisi ni NANI na tunaelekea wapi. BONYEZA PLAY.

Huyu Melkizedeki Ni Nani? 65-0221E

Ndugu. Joseph Branham

Maandiko ya kusoma Kabla ya Kusikiliza Ujumbe :

Mwanzo Sura ya 18 yote
Kutoka 33:12-23
Yohana Mtakatifu 1:1
Warumi 8:1
2 Wakorintho 5:1
2 Wathesalonike 4:13-18
1Timotheo 3:16 / 6:15
Waebrania 7:1-3 /13:8
Ufunuo 10:1-7 / 21:16

22-1127 Ndoa Na Talaka

UJUMBE: 65-0221M Ndoa Na Talaka

PDF

BranhamTabernacle.org

Mpendwa kundi la Nabii,

Kumbuka, ninasema jambo hili kwa kundi langu tu. Na huko nje hewani, ninasema hili kwa wafuasi wangu mwenyewe. Ujumbe huu ni kwa ajili yao tu, na yale nitakayosema hapa.

Mhudumu ye yote, yeye, hao ni wake, ndiyo, yeye ni mchungaji wa kundi, acha atende cho chote anachotaka. Hilo ni juu yake na Mungu. Kasisi ye yote, mhubiri ye yote, hiyo ni juu yako, ndugu yangu.

Ninazungumza tu hapa Jeffersonville, mahali pekee ambapo ningezungumzia jambo hili , ni kwa sababu ni kundi langu mwenyewe . Ndilo kundi ambalo Roho Mtakatifu amenipa kulifahamu na kuwa msimamizi wake , ataniwajibisha kwa ajili yake . Na watu hawa wangu wamekuwa waongofu hapa kutoka nchini kote, ambao nimewaongoza kwa Kristo .

Ni jiwe la kifuniko kwa wikendi ya Shukrani jinsi gani . Ninashukuru sana kuwa sehemu ya kundi hilo dogo ambalo bado analisimamia pamoja na kila mmoja wenu. Hakuna mahali pengine ambapo tunaweza kwenda.

Baba ametutumia tai mkuu arukaye ili kumwongoza Bibi-arusi Wake. Kuna sauti nyingi zinazowatia moyo watu na kunena Maneno ambayo yaliyonenwa na nabii wake, lakini kuna SAUTI MOJA tu iliyotumwa kumuongoza na kumuunganisha Bibi-arusi Wake.

Maneno ambayo nabii wa Mungu aliyonena kwenye Kanda ni Yakini yetu. Tunaeleweka vibaya kwa sababu tunasema tunaamini KILA NENO, lakini tuliamriwa na nabii wa Mungu kufanya hivyo hasa.

Nasema vivyo hivyo katika Jina la Yesu Kristo. Usiongeze kitu. Usiondoe—kuliwekea mawazo yako. Wewe sema tu yaliyosemwa katika kanda hizo. Tenda sawasawa kabisa na vile Bwana Mungu amekuamuru kutenda. Usiongezee Kwake.!

Amka ulimwengu. Muda umekaribia. Maneno aliyosema nabii wa Mungu, MUNGU AMETUAMURU ; Kuamini, kusema na kutenda, HASA yale aliyosema kwenye kanda. Si kile ninachosema, si kile kuhani ama wahubiri wenu wanayosema, bali yale nabii wa Mungu aliyosema KWENYE KANDA .

Hakuna kitu muhimu zaidi kuliko kusikia Sauti Hiyo kwenye kanda, HAKUNA. Tutaenda kuhukumiwa kwa yale yaliyonenwa KWENYE KANDA . Sio kwa niliyosema, bali yale ALIYOSEMA YEYE .

Nakutakia YALIYO BORA SANA. Maneno yangu machache ni ya kuwatia moyo, kama vile mchungaji yeyote apaswavyo, kuamini kila Neno. Siwafundishi : kutilia shaka jambo lolote mnalosikia kwenye kanda, kuna makosa kwenye kanda, hamna budi kunisikia mimi kadiri mpaswavyo kumsikia nabii. Nawaandikia maneno machache ya kuwatia moyo DUMUNI NA NENO LA ASILI, BONYEZA PLAY. Ninawataka muwe Bibi-arusi Neno safi, asiyeghoshiwa.

Mungu aliruhusu Maneno Yake yarekodiwe katika siku hii ili kila kiumbe hai kiweze kusikia Sauti Yake. Katika siku za Paulo, walikuwa na waandishi wa kuandika yale aliyokuwa akihubiri, ambayo ni Biblia. Lakini LEO, Mungu alitaka iwe KUU zaidi. Tunaweza Kubonyeza Play na kumsikia kwa masikio yetu wenyewe Yesu Kristo aliyefufuka akizungumza nasi, mdomo kwa sikio.

Ni siku ya jinsi gani tunayoishi. Huku ulimwengu wa kawaida ukiporomoka karibu nasi, tuna mahali palipoandaliwa ambapo tunaweza kwenda na kupumzika tu. Tunapapata kwenye KANDA. Tumeziweka katika vyumba vyetu baridi na kufanyia karamu Chakula Kilichohifadhiwa ambacho kimehifadhiwa katika ghala. Nabii wetu anaweza kuwa ameondoka muda mrefu, lakini bado tunangali tunakumbuka mambo haya ni kweli, na tunafanya kama vile Mungu alivyotuamuru kufanya, DUMUNI NA HIZO KANDA.

Njoo uwe na karamu iliyo bora ya Shukrani ambayo hujawahi kamwe kula Jumapili hii saa 06:00 SITA MCHANA , saa za Jeffersonville, ( Ni Saa 2:00 MBILI USIKU ya tanzania) Wakati Sauti ya Mungu inapozungumza nasi Ujumbe: Ndoa Na Talaka 65-0221M .

Ndugu. Joseph Branham

Maandiko ya kusoma Kabla ya Kusikiliza Ujumbe :

Mathayo Mtakatifu 5: 31-32 / 16: 18 / 19: 1-8 / 28:19
Matendo 2:38
Warumi 9:14-23
1Timotheo 2:9-15
1Wakorintho 7:10-15 / 14:34
Waebrania 11:4
Ufunuo 10:7
Mwanzo sura ya 3 yote
Mambo ya Walawi 21:7
Ayubu 14:1-2
Isaya 53 yote
Ezekieli 44:22

22-1120 Mahali Alipopachagua Mungu Pa Kuabudia

Ujume: 65-0220 Mahali Alipopachagua Mungu Pa Kuabudia

PDF

pakua – m4a

pakua – amr 8 MB (use Firefox to download)

BranhamTabernacle.org

Mpendwa Bi Yesu Kristo,

Jinsi tunavyopenda kusikia majina yetu yakiitwa. Kufikiri tu, sisi ndio wale Anaowajia. Bibi-arusi wa Kifalme kwa Mwana aliyeahidiwa wa Kifalme. Uzao wake maalumu wa Kifalme wa Ibrahimu ambao umekuwa mkweli na mwaminifu kwa kila Neno.

Hatujafanya uzinzi, wala hata kukonyezana, na neno lingine lo lote; tumejiweka tu wasafi na tumekaa na kila Neno.

Kuna wanawake Wakristo wengi wazuri ulimwenguni leo, wanawake waaminifu; Bali kuna Bi Yesu Kristo mmoja tu. Sisi ndio tunaenda Nyumbani pamoja Naye. Sisi ndio Mke wake Aliyeteuliwa .

Alituambia katika Neno Lake kwamba angekuja mara nyingine tena, kama jinsi tu alivyokuja hapo awali. hapo yeye alisimama, akijifunua katika mwili wa mwanadamu, akisoma Neno na kutuambia, “Leo Maandiko haya yametimia machoni penu,” nasi tukamtambua, na tukawa Bi Yesu Kristo wake.

Imefunuliwa kwetu ya kwamba M-w-a-n-a yule yule wa Mungu aliyetokea mashariki na kujithibitisha Mwenyewe kama Mungu aliyefanyika mwili ndiye M-w-a-n-a yule yule wa Mungu aliyeko katika kizio cha magharibi cha dunia ambaye anajitambulisha Mwenyewe kati ya Bibi-arusi wake. Ile nuru ya jioni ya Mwana imekuja.

Na kama ningeuliza swali kuhusu cho chote, yapaswa kuwe na jibu la kweli. Kwaweza kuwe na lililo la karibu nalo; lakini yapaswa kuwe na jibu la kweli, la moja kwa moja kwa kila swali. Kwa hiyo, basi, kila swali linalozuka maishani mwetu, yabidi kuwe na jibu la kweli na sahihi.

Katika wakati wetu kuna maswali mengi na mabishano miongoni mwa watu.

. Je, ni muhimu jinsi gani kusikiliza kanda za nabii wa Mungu?

. Je, ni muhimu jinsi gani kusikia na kuamini kila Neno?

. Yakini yetu ni nini? Je! Ni yale aliyosema kwenye kanda, ama Roho Mtakatifu humwongoza kila mtu kuamua lipi ni Neno na lipi si Neno.

. Je, ni lazima tuwe na mtu, au kundi la watu, kutuvunjia-vunjia ?

. Je! Neno linasema baada ya Yeye kumtuma Eliya nabii, Yeye atatuma kundi la watu ambalo halina budi kuwafafanulia Hilo?

. Je, tunahitaji mtu fulani wa kutufasiria Neno au kulivunja-vunja ?

. Je, tunapaswa kuzisikiliza tu kanda katika nyumba zetu, magari, na vituo vya mafuta, na kisha kumsikia mhudumu tunapoenda kanisani?

. Je, tucheze kanda katika makanisa yetu?

. Je, ni Sauti ya Mungu kwa ajili ya wakati wetu au la?

Sasa, kama ni swali la Biblia, basi lapaswa liwe na jibu la Biblia. Halingepaswa kuweza kuja kutoka kundi la watu, kutoka kwenye ushirika wo wote ule, au kutoka kwa mwalimu fulani, au kutoka kwa madhehebu fulani. Lapaswa litoke moja kwa moja katika Maandiko…

Kwa hiyo, ikiwa tunataka kupata jibu sahihi kwa maswali yetu, ni lazima twende kwenye Maandiko. Kisha, ni lazima tuamue, ni nani aliye mfasiri wa Kiungu wa Maandiko. Je, kila mtu anajiamulia kivyake?

Nabii haimaanishi kunena Neno tu, bali pia ni kutabiri, na ni mfasiri wa Kiungu wa Neno, Neno la Kiungu lililoandikwa.

Kwa hiyo kama nabii ndiye mfasiri wa Kiungu wa Maandiko, basi kile nabii huyo alichosema ni Neno la Mungu kwa Bibi-arusi Wake ambalo limekwisha kufasiriwa, NI HAYO TU.

Hilo haliondoi wahudumu, au nafasi ambayo Mungu amewaitia. Wameitwa na Mungu kudumisha Neno hilo lililonenwa na nabii wa Mungu mbele ya kundi lao. Wawaelekeze watu wao kwa huyo mjumbe na Ujumbe wa Saa hii.

Kila neno wanalohubiri lazima lipimwe kwa Maneno ambayo nabii wa Mungu aliyosema kwenye kanda. Hawapaswi kubadilisha, wala hata kuweza kufasiri hata NENO MOJA. Maandiko ya Mungu yanafasiriwa TU na nabii Wake.

Sasa, kila moja yao, bila shaka, ungeweza kuona wazo lao, nami siwezi kuyalaumu. Kila moja hudai kwamba wao ndio ile kweli, wana ile kweli. Na watu ambao ni washiriki wa makanisa hayo wanapaswa kuiamini hiyo, kwa sababu wamesalimisha kikomo cha—chao, kikomo chao cha Milele, juu ya mafundisho ya kanisa lile. Nayo yanatofautiana sana, moja kwa lingine, mpaka inazusha maswali mbalimbali mia tisa na kitu.

Ikiwa Ujumbe huu ulionenwa na nabii wa Mungu si Yakini yako, bali ni kile ambacho mtu ama watu fulani wasemayo ndio Neno, Basi kikomo chako cha Milele kinategemea yale WANAYOSEMA.

Maneno yangu yanaonekana kupingana kabisa na ye yote na wahudumu wote. Siwapingi. Ninaamini Mungu ameweka watu halisi katika Kanisa Lake na kuyaangalia makundi Yake kuweka Ujumbe huu mbele yao. Ninaamini wanahubiri na kuamini Ujumbe huu. Lakini kwa nini hawataki kumweka Ndugu Branham nyuma ya mimbara zao Kama Sauti iliyo muhimu sana yakusikia? Kwa nini wanaweka huduma yao kuwa sawa na, pia muhimu kama ile Sauti?

Malaki 3 ilisema, “Namtuma mjumbe Wangu mbele ya uso Wangu kuitengeneza njia.” Na yule ambaye alipelekwa kuitengeneza ile njia, alimtambua Yeye pale. “Huyo Ndiye! Hakuna kosa. Huyo Ndiye! Ninaona ishara ikimfuata Yeye. Najua kwamba huyo Ndiye; Nuru ikishuka kutoka Mbinguni na kukaa juu Yake.” Ilikuwa dhahiri, huyo alikuwa Ndiye.

Basi, ndugu yangu, nataka kukuuliza wewe jambo fulani, katika kufunga. Tungeweza kusema hivi. Hivi katika Malaki 4, hatukuahidiwa tai mwingine, Nguzo ya Nuru itafuata , kuonyesha kanisa lililokosea siku hii kwamba Yeye ni Waebrania 13:8, “yeye yule jana, leo, na hata milele”? Hivi hatukuahidiwa mwingine atakayeruka aje kutoka nyikani?

Je, tunapaswa kufuata nini? Nguzo hiyo ya Nuru. Hiyo Nguzo ya Nuru ni nani? Yule tai, Malaki 4. Ni nani aliyekuwa na Nguzo ya Moto juu ya kichwa chake kumthibitisha yeye alikuwa nani? William Marrion Branham.

Kila wakati tunapokusanyika, hatuna budi kuiweka Sauti hiyo mbele ya watu. Ni lazima tuipe Sauti ya Mungu NAFASI YA KWANZA. Si kumwabudu mtu huyo, bali kumwabudu yule Mungu Aliye Katika mtu huyo.

Huyo ndiye mtu ambaye Mungu amechagua kumwongoza Bibi-arusi Wake. Mtu huyo ndiye mtu ambaye Mungu amechagua kufasiri Neno Lake. Mtu huyo ndiye mtu ambaye Mungu amechagua kufunua kwake siri zake zote. Mtu huyo ndiye ambaye Mungu alisema, “Wafanye watu WAKUAMINI ”, SI MTU MWINGINE YE YOTE AU ASEMAYO MTU AWAYE YOTE YULE, WEWE, WILLIAM MARRION BRANHAM . Mtu huyo ndiye atakayetutambulisha kwa Yesu Kristo.

Mwanamume au mwanamke anayeongeza lo lote kwa yale ninayosema, haamini yale nisemayo.

Njoo na uwe Bi Yesu Kristo pamoja nasi Jumapili hii saa 06:00 SITA MCHANA , saa za Jeffersonville, ( Ni Saa 2:00 MBILI USIKU ya Tanzania) tunaposikia kinywa cha Mungu kilichochaguliwa kikinena na kutuambia:  Mahali Alipopachagua Mungu Pa Kuabudia 65-0220 .

Ndugu. Joseph Branham

Maandiko ya kusoma kabla ya kusikiliza Ujumbe :

Kumbukumbu la Torati 16:1-3
Kutoka 12:3-6
Malaki Sura ya 3 & 4
Luka 17:30
Warumi 8:1
Ufunuo 4:7

22-1113 Leo Maandiko Haya Yametimia

UJUMBE: 65-0219 Leo Maandiko Haya Yametimia

PDF

BranhamTabernacle.org

Mpendwa Uzao wa Kifalme wa kiroho wa Ibrahimu,

Ni kanisa gani unaloweza kwenda na kujua, bila shaka yo yote, ya kwamba kila Neno unalosikia ni Bwana Asema Hivi? Hakuna mahali popote, isipokuwa tu usikilize Sauti ya Mungu ikisema nawe kwenye kanda.

Sisi ni tai wa Mungu na hatutapatana hata kwa Neno moja. Tunataka tu Mana mpya kila ibada na Haiji tena mpya kuliko kuisikia moja kwa moja kutoka kwa Mungu Mwenyewe. Tunaruka juu zaidi na zaidi tunaposikia kila Ujumbe. Kadiri tunavyoenda juu zaidi , ndivyo tunavyoweza kuona zaidi . Kama hakuna Mana katika kanisa hili, tai wa Mungu wanapaa juu kidogo mpaka waipate.

Jinsi gani mioyo yetu inavyoruka kwa furaha tunapomsikia Mungu akizungumza nasi na kutuambia ya kwamba sisi ndio Kanisa Lake halisi, Kanisa la Mungu, lililozaliwa mara ya pili, ambalo linaloamini kila Neno la Mungu mbele ya kitu chochote kile, bila kujali ni kitu gani, kwa sababu sisi ni Bibi-arusi-Neno Bikira Wake Asiyeghoshiwa.

Kuna msukosuko mwingi miongoni mwa watu leo. Kama ilivyokuwa katika siku za Yesu, wale waliojiita waamini walikuwa wakichukua mafafanuzi ya yale makuhani walikuwa Wamesema kuhusu Maandiko. Walikuwa wakiamini mafafanuzi ya Neno ya Watu. Hiyo ndiyo ilisababisha wakose kuiona ile Kweli ya Mungu, kwa sababu kulikuwa na mafafanuzi mengi sana yaliyotengenezwa na Wanadamu ya Neno la Mungu. Mungu hahitaji mtu yeyote afafanue Neno Lake. Yeye ni Mfafanuzi Wake Mwenyewe.

Je, unaamini kama ungeishi wakati wa Yesu, ungeamini kila Neno alilosema, bila kujali kuhani wako alisema nini? Je, ungemwambia kuhani wako kwamba kumsikiliza Yesu ndilo jambo muhimu zaidi unaloweza kufanya? Je, ungemwambia Maneno ya Yesu hayahitaji kufasiriwa? Kama wangekuwa na kanda za Mahubiri ya Yesu, je! ungalimwambia kuhani wako unataka abonyeze play ili uweze kusikia yale hasa Yesu aliyosema na jinsi alivyoyasema?

Vema, hilo halikuwa kwa ajili ya wakati wako; huu ni wakati wako, huu ndio wakati wako. Biblia yasema, ni Yeye yule jana, leo, na hata milele. Kile Unachofanya na kusema hivi sasa ndivyo hasa ungefanya wakati huo.

Tunaamini kwamba M-w-a-n-a wa Mungu yule yule aliyetokea mashariki na kujithibitisha Mwenyewe kama Mungu aliyefanyika mwili, ndiye M-w-a-n-a yule yule wa Mungu Aliyeko katika kizio cha magharibi cha dunia ambaye anajitambulisha Mwenyewe miongoni mwetu. Tunaamini Leo Maandiko haya yametimia mbele yetu.

Hakika ninaamini huu ndio mwaka uliokubaliwa, mwaka wa yubile. (ama mwaka wa Sikukuu). Ikiwa Unatamani kubaki mtumwa na kutoamini Ujumbe huu kuwa ni Bwana Asema Hivi ; Ikiwa Ujumbe huu sio Yakini yako; ikiwa unaamini inahitaji mtu kuufafanua Ujumbe huu; Ikiwa unaamini ni makosa kuzicheza kanda kanisani mwako; Basi itakubidi upelekwe na shimo litatobolewa masikioni mwako kwa msharasi, Na ndipo itakupasa kumtumikia huyo mwenye watumwa siku zako zote.

Lakini Kanisa la kweli la Bibi-arusi linaamini Neno lote la Mungu katika utimilifu Wake na katika nguvu Zake. Sisi ndio lile Kanisa Teule ambalo linajiondoa na kuwekwa kando kutoka kwenye mambo hayo, nalo dhihirisho la Mungu limeuvutia usikivu wetu. Sisi ndio ule Uzao wa Kifalme wa kiroho wa Ibrahimu.

Kwa hivyo tuna shukrani kwenu kuwa hapa mkafurahie ushirika huu pamoja nasi, ambao tunatarajia Mungu atatupa katika mkutano huu.

Kwa hivyo tunakualika uungane nasi Jumapili saa 6:00 SITA MCHANA , saa za Jeffersonville, ( Ni Saa 2:00 MBILI USIKU ya tanzania) tunaposikia 65-0219 Leo Maandiko Haya Yametimia . Tunatarajia Kile Mungu anachofanya wakati wa mikutano hii. Ile Nuru ya jioni ya Mwana imekuja.

Ndugu. Joseph Branham

Maandiko ya kusoma :

Yohana Mtakatifu Sura ya 16 yote
Isaya 61:1-2
Luka Mtakatifu 4:16

22-1106 Ile Mbegu Haitarithi Pamoja Na Kapi

UJUMBE: 65-0218 Ile Mbegu Haitarithi Pamoja Na Kapi

PDF

BranhamTabernacle.org

Mpendwa Bibi-arusi-Neno Bikira ,

Tuko hapa. Tumefika. Muda umekaribia. Kapi limejitenga na Mbegu. Tumekuwa tukikaa katika Uwepo wa Mwana, tukiiva. Tutakaa katika Uwepo huo mpaka kundi letu dogo litakapoiva sana kwa Kristo, mpaka tuwe mkate kwenye meza Yake. Bwana Ashukuriwe!

Ujumbe huu umethibitisha Malaki 4, umethibitisha Luka 17:30, umethibitisha Waebrania 13:8, umethibitisha Yohana Mtakatifu 14:12, umethibitisha Ufunuo sura ya 10, kufunguliwa kwa ile Mihuri Saba, siri za Mungu, uzao wa nyoka, ndoa na talaka. na siri hizi nyingine zote ambazo zilikuwa zimefichwa chini ya nguzo kwa miaka hii yote.

Sisi ni mabikira kwa Neno. Hatuwezi na hatutagusa kitu kingine chochote. Kwa kila Ujumbe tunaosikia, ni msafi na mpya; Mana mpya ambayo ndio kwanza imeshuka kutoka Mbinguni.

Lakini alituonya kwamba katika wakati wa mwisho kutakuwa na roho mbili ambazo zingefanana sana, zingewapoteza walio wateule , kama Yamkini. Hivyo, ni lazima tuwe macho kwa roho hiyo kwani itaonekana kuwa kama Bibi-arusi mwenyewe.

Tazama, ona zinavyofanana. Mathayo ilisema—Mathayo Mt. 24:24, ilisema kwamba hizo roho mbili katika siku za mwisho , roho ya kanisa ya watu wa kanisa na Roho ya watu wa Bibi-Arusi , zitafanana sana hata ingewapoteza, kama yamkini, walio Wateule. Hivyo ndivyo jinsi zinavyofanana.

Alisema ROHO ya watu wa kanisa na ROHO ya watu wa Bibi-arusi zitafanana sana moja kwa nyingine . Hiyo ingemaanisha kwamba roho ya watu wa kanisa ingepaswa kusema wanaamini Ujumbe wa wakati huu ili KUFANANA JINSI HIYO.

Hiyo haingekuwa methodisti, Baptisti, presbiteri, au hata wapentekoste; Wao wako mbali sana na Neno na hata wanaukataa Ujumbe. Hakuna hata mmoja wao aliye na roho inayofanana na Bibi-arusi.

Shetani amejaribu, na amefanikiwa sana, kuwa mdanganyifu sana. Hata tangu hapo mwanzo, alisema tu, “Hakika,” hivyo akimwambia Hawa atumie hoja yake naye amsikilize yeye na si Neno tu. Kuna jambo moja tu aliloamriwa kufanya: kukaa na Neno.

Ukweli:

Ikiwa una swali, lazima kuwe na jibu. Hivyo ndivyo nabii alivyotuambia. Jibu lazima litoke katika Neno. Neno huja kwa nabii peke yake. Nabii ndiye mfasiri pekee wa Neno. Ikiwa mwanamume au mwanamke yeyote atakupatia jibu, lazima liwe vile nabii alivyokwishasema . Haiwezi kuwa fasiri yao , wazo au ufahamu wao. Hawana budi waliunganishe kwa Neno lililonenwa na nabii wa Mungu aliyethibitishwa. Wala Sio neno la nabii pamoja na, ni kile tu nabii alichosema.

Kuna itikadi mbili sasa hivi .

1 : Ni lazima uamini kila Neno kwenye hizo kanda kwani ndizo Jumbe muhimu sana unazopaswa kusikia.

2 : Wala Huhitaji kuamini kila Neno kwenye hizo kanda, na wahudumu sasa wao wanazo jumbe muhimu sana unazopaswa kusikia.

Kunazo tofauti nyingi, nyingi kwa hiyo itikadi ya pili: Roho Mtakatifu ataniongoza mimi au mchungaji wangu kutuambia kile ambacho ni Neno na kisichokuwa Neno. Tunahitaji zaidi ya yale tu aliyosema Ndugu Branham kwenye kanda. Huna budi kuwa na wahudumu wa kufafanua au kulivunja-vunja Neno. Bila ya wahudumu huwezi kuwa Bibi-arusi.

Kuna Mbegu za Hitilafu nyingi zaidi, lakini haiwezekani kuziorodhesha zote. Lakini hakuna tofauti ama mbegu za hitilafu kwa Ile namba ya kwanza. Ni AMINI KILA NENO, hivyo tu.

Mkiwa Kama waamini wa Ujumbe huu wa wakati wa mwisho, lazima mjiulize maswali haya:

1 : Je, unaamini kile nabii alichosema kwenye kanda ndio Yakini yako, au unaamini ni Roho Mtakatifu kupitia wewe au mchungaji wako?

2 : Je, unaamini kwamba huduma tano ina jumbe muhimu zaidi ambazo Bibi-arusi anazohitaji kusikia, au ni Ujumbe uliyo kwenye kanda?

Iwapo mchungaji wako, mhubiri, mwalimu, mwinjilisti au nabii hakuambii kwamba kuzisikiliza kanda ndizo JUMBE MUHIMU SANA unazopaswa kusikia, yeye ni wa UWONGO, NA ILE ROHO AMBAYO NABII ALITUONYA INGEKUJA.

Ikiwa anasema HIZO NDIZO Jumbe muhimu sana mnazoweza kusikia, lakini bado anakataa kuzicheza kanda katika kanisa lake, HAPO KUNA KASORO FULANI. Ikiwa anaamini kweli kwamba kuzisikiliza kanda ndilo jambo muhimu zaidi mnaloweza kufanya, basi angezicheza kanda KWANZA, kisha ahubiri ikiwa anahisi kuongozwa.

Mfano rahisi:

Kama ningekuambia, kunywa maji safi ndilo jambo moja muhimu zaidi uwezalo kufanya kwa ajili ya afya yako, na kuna maji MAMOJA tu ya kunywa yaliyothibitishwa na kuhakikishwa…lakini ujapo nyumbani kwangu kula chakula cha jioni, Nami sikuhudumii hayo maji yaliyothibitishwa. Ninakuambia, “unaweza kunywa maji hayo huko nyumbani kwako lakini nyumbani kwangu, lazima unywe kile Mimi ninachokupa .”

Ikiwa maji hayo ndio KITU BORA ninachoweza kukupa kwa ajili ya afya yako, ambayo yatakupa uhai, basi jambo la kwanza nitakalokupa unapoingia nyumbani Mwangu ni maji hayo safi ya kunywa.

Je, nimekosea kwa kusema, “CHEZENI KANDA KATIKA MAKANISA YENU, ndilo jambo bora sana muwezalo kufanya kwa watu wenu. Ni Bwana Asema Hivi.”

Au, wanakosea kwa kusema, “Ni makosa kucheza kanda kanisani, Ndugu Branham hakusema kamwe kucheza kanda kanisani mwenu. Tunawaambia watu wacheze kanda majumbani mwao, kwenye magari yenu, kila wakati, LAKINI kanisani lazima wanisikie MIMI.”

Ni Roho gani anayekuongoza? Je, Unasema, “kinachosemwa kwenye kanda ni Yakini yangu na ndilo jambo muhimu zaidi niwezalo kusikia”? Au, Unasema, “Kanda hizo hazitoshi. Sio Yakini yangu na sio jambo lililo muhimu zaidi kusikia, je ni Wahudumu ”?

Sasa, ni wakati wa mbegu au wakati wa Bibi-Arusi. Makapi yamekufa, yale makapi tayari yamekwisha kukauka. Ni wakati wa Neno bikira, lisilogoshiwa. Ni bikira, Kumbuka, wakati wa Neno bikira.

Njoo usikie Manna mpya ambayo ndio kwanza imeshuka kutoka Mbinguni Jumapili hii saa 06:00 SITA MCHANA , saa za Jeffersonville, ( Ni saa 2:00 MBILI USIKU Ya Tanzania),Tunaposikia :  
65-0218 Ile Mbegu Haitarithi Pamoja na Kapi.

Ndugu. Joseph Branham

22-1030 Mtu Anayejiepusha Na Uso Wa Bwana

UJUMBE: 65-0217 Mtu Anayejiepusha Na Uso Wa Bwana

PDF

BranhamTabernacle.org

Wapendwa Wana-kondoo wa Bwana,

Jinsi mioyo yetu inavyotamani siku hii kila wiki tunapoweza kuungana pamoja kutoka ulimwenguni kote ili kusikia Sauti ya Mungu ikizungumza nasi Neno la Uzima wa Milele. Hakuna kitu kingine kinachoshibisha nafsi zetu na kukata kiu yetu ila Sauti ya Mungu.

Ulituambia, Baba, kwamba mashamba Makubwa ya mavuno ni meupe, yameiva, na nafaka iko tayari sasa kwa ajili ya ule wakati mkuu wa kupura. Nafaka sasa inakaa katika Uwepo wa Mwana na ikiiva kwa ajili ya Ufalme wa Mungu.

Baba, Tunatetea tunayoamini kuwa ni Kweli; Sauti Yako kwenye kanda ndiyo Sauti PEKEE ambayo itatukamilisha sisi, Bibi-arusi Wako.

Ni ngumu kwani tunaeleweka vibaya sana kwa ndugu na dada zetu. Tunawasihi na kuwaomba wasijiepushe na Uwepo Wake, bali wakimbilie kuingia katika Uwepo Wake.

Tunajua kuna watu wengi watiwa-mafuta uliowachagua na kuwaweka waangalie kundi Lako, wanaopenda Ujumbe huu kwa mioyo yao yote, Lakini Baba, wanashindwa kuweka Sauti Yako iliyothibitishwa kwenye kanda mbele yao. Wanashindwa kuwaambia kwamba huu ni Ujumbe wa mtu mmoja na kwamba Wewe ulimchagua mtu huyo kumwongoza Bibi-arusi Wako. Wanashindwa kuwaambia kwamba Sauti Yako ndiyo Sauti PEKEE itakayomunganisha na kumkamilisha Bibi-arusi Wako.

Lazima “Nipige kelele juu yake.” Nipige kelele juu ya kila kitu, na kila mtu, ambaye anapinga kucheza Kanda Zako katika makanisa yao. Nipige kelele juu ya matendo yao, nipige kelele juu ya kanisa lao, nipige kelele juu ya manabii wao, nipige kelele juu ya wahudumu wao, nipige kelele juu ya makasisi wao. Lazima nipige kelele juu ya kitu hicho chote!

“Aisee, nimeshuka kuja kujiunga nanyi enyi jamaa. Mnajua, naamini nitawaambia nitakachofanya. Nina kitu kidogo tu hapa naamini ninaweza kuifanya ninino…kutuunganisha sote pamoja, na kufanya hivi, vile, ama vinginevyo.”

Lazima nipige kelele juu ya jambo hilo, kwani Neno Lako pekee, lililonenwa na nabii Wako, ndilo linaloweza kutuleta PAMOJA. Mahubiri yao yanawezaje? Wote hawakubaliani mmoja kwa mwingine na wanaona mambo kwa njia tofauti mmoja kwa mwingine, isipokuwa jambo moja, wote wanalokubaliana kwalo… KUTOCHEZA KANDA KATIKA MAKANISA YAO. Hilo lawezaje , Baba?

Ulituambia ni lazima tuwe na YAKINI MOJA, ambayo ni Neno lako. Ulituambia Neno Lako humjia nabii Wako, PEKE YAKE. Ulituambia yeye ndiye Mtu PEKEE anayeweza kulifasiri Neno Lako. Ulituambia kwamba kila mhudumu, kila mshiriki wa kawaida, kila mwanadamu, anaweza TU KUSEMA ALICHOSEMA. Sauti Yake ndiyo SAUTI PEKEE ambayo imethibitishwa na Nguzo Yako ya Moto kuwa Bwana Asema Hivi .

Sisemi kwamba ni wa uwongo au hawapaswi kuhubiri. Wala sisemi Bwana hayuko pamoja nao, au hawajatiwa mafuta na kuitwa kuhubiri, Lakini lazima niwapigie kelele wakati hawatawaambia watu wao kwamba kusikiliza kanda ndilo jambo muhimu zaidi wanaloweza kufanya.

Kubadilisha yodi moja au nukta moja ni kifo. Umeandaa njia kwa ajili ya Bibi-arusi wako kusikia Bwana Asema hivi kwa masikio yao wenyewe. Wanawezaje Kutowahubiria watu wao kwamba huu Ndio Ujumbe uliyo muhimu sana uwapasao Kusikia? Ndio Ujumbe pekee ninaoweza kusema AMINA kwa kila Neno, kwa kuwa si Neno la mwanadamu, au fasiri ya mwanadamu ya Neno Lako, ni Neno Lako Safi.

Ulisema Ujumbe na mjumbe ni kitu kimoja . Nabii wako alinena Hilo nawe ungelitimiza. Neno Lako lililonenwa na nabii Wako HALIHITAJI fasiri kwa kuwa ni Mwana wa Adamu akizungumza moja kwa moja na Bibi-arusi Wake.

Yanipasa niwasihi watu, rudini kwenye upendo wenu wa kwanza. Rudini kwenye kile mnachojua ni BWANA ASEMA HIVI. Ikiwa umekuwa unajiuliza ni njia gani ya kwenda au nini cha kufanya, njoo, ingia katika Merikebu pamoja nasi usiku wa leo. Tunashuka kwenda Ninawi, ili kupiga kelele. Tuna wajibu mbele za Mungu, huo ni Ujumbe huu kwenye kanda.

Tunaamini ya kwamba Kuja kwa Bwana kumekaribia, Naye atakuwa na Bibi-arusi, nasi tunajitayarisha. Hatutaki chochote ila Neno Safi la Mungu lililonenwa na nabii Wake. Tunaenda Utukufuni, njoo tuungane katika Merikebu yetu.

Ikiwa unaamini Ujumbe huu ni Kweli, na unaostahili kuuishia, unaostahili kuufia, njoo uungane nasi Jumapili hii saa 06:00 SITA MCHANA , saa za Jeffersonville, (Ni saa 1:00 MOJA JIONI Ya Tanzania), tunaposikia Ujumbe tunaoamini ni muhimu na wa haraka kwetu kuusikia: Mtu Anayejiepusha Na Uso Wa Bwana 65-0217.

Ninyi ni wana-kondoo wangu. Mwaonaje? Ninyi ni wana-kondoo wa Bwana ambao ameniruhusu kuwalisha .

Ndugu. Joseph Branham.

Maandiko ya kusoma kabla ya Kusikiliza Kanda :

Yona 1:1-3
Malaki sura ya 4 yote
Yohana Mt. 14:12
Luka 17:30

22-1023 Maswali na Majibu #4

UJUMBE: 64-0830E Maswali na Majibu #4

PDF

pakua – m4a

pakua – amr

BranhamTabernacle.org

Mpendwa Ndugu Joseph,

 1. Nimekusikia ukisema kwamba unaamini KILA NENO la Ujumbe huu ni BWANA ASEMA HIVI.

 Kutoka kilindi cha moyo wangu na kila mshipa katika mwili wangu NINAAMINI HILO.  Ni Sauti yenyewe hasa ya Mungu ikinena mdomo kwa sikio kwa Bibi-arusi Wake.

 Mungu alinena kupitia nabii wake na kusema:

  Nasema vivyo hivyo katika Jina la Yesu Kristo. Usiongeze kitu. Usiondoe—kuliwekea mawazo yako. Wewe sema tu yaliyosemwa katika kanda hizo. Tenda sawasawa kabisa na vile Bwana Mungu amekuamuru kutenda. Usiongezee Kwake .

 Ikiwa unadai unaamini Ujumbe huu wa wakati wa mwisho, wewe pia lazima uamini KILA NENO ili uwe Bibi-arusi Wake.  Shetani anajaribu kulipiga msasa Kupitia Wahudumu na kusema, “Ndugu Branham alipokuwa akisimulia hadithi za kuwinda au kusema ‘mnaye mpishi bora zaidi nchini’, au ‘Sina Maandiko kwa jambo hilo, lakini nitakuambia kile ninachofikiri;’ Haikupasi  kuamini sehemu hiyo.  Roho Mtakatifu yuko hapa kutuongoza kuelewa kile ambacho ni Neno na kisichokuwa Neno .”  HUYO NI IBILISI YULE YULE ALIYEONGEA NA HAWA NA KUSEMA, HAKIKA…. HAKUMAANISHA KILA NENO.  Je, linasikika kama unalifahamu?

 Wanafanya yale ALIYOWAAGIZA wasifanye.  Alisema SEMA YANAYOSEMWA kwenye kanda hizo, usiliwekee mawazo yako au uelewa wako.  Hakusema, “Kila kitu ISIPOKUWA sehemu hii na ile, na mchungaji wako atakuambia ni wakati gani alipokuwa Roho Mtakatifu  akizungumza na wakati gani alikuwa ni mimi tu.”  Mimi ni moja ya changarawe ndogo tu pwani kati ya mawe haya makubwa.

  2. Je, unafikiri Ndugu Branham na/au kanda zake ndizo Yakini?

 Ndugu Branham si Yakini Yangu bali Ujumbe alionena kwenye kanda ndiyo Yakini yangu Kabisa.

 Watu wengi husema hiyo si sahihi, Biblia ndiyo Yakini.  Rafiki yangu, Biblia na Ujumbe uliyo kwenye kanda ni kitu kimoja.  Hicho ndicho kiini hasa cha Ujumbe.  Ujumbe uliyo kwenye kanda ndiyo fasiri ya Biblia.  Hivyo ni kitu kimoja na jambo lile lile .

 Ukweli rahisi ni kwamba,  1: Biblia ni Neno.  2: Neno humjia nabii.  3: Nabii ndiye Mfasiri PEKEE wa Kiungu wa Neno.   4: Nabii wetu, William Marrion Branham, ndiye Neno lililodhihirishwa la siku yetu na alitumwa kulifasiri Neno.  5: Neno la Mungu halihitaji kufasiriwa.  Anachosema kupitia nabii wake kwenye kanda  NDIYO FASIRI YA NENO LAKE.

 Biblia inatuambia kwamba alikuwa anakuja tena na kuishi katika mwili kama alivyofanya na Ibrahimu na Yesu Kristo.  Alisema alikuwa na mambo mengi ya kutuambia.  Alisema angefunua siri hizi zote kuu ambazo zimefichwa katika Neno Lake.  Alisema hazihitaji fasiri yoyote.  Hakusema kamwe angetuma kundi kuongoza na kuwaunganisha watu Wake, YEYE MWENYEWE ANGEWAONGOZA WATU KUTUMIA NABII WAKE KAMA ALIVYOFANYA DAIMA.  NENO LAKE HALIWEZI KUBADILIKA.

 3. Je, unaamini kwamba wachungaji wanapaswa kucheza kanda katika makanisa yao?

 Kila mchungaji yampasa afanye kama anavyojisikia kuongozwa na  Bwana kufanya, kwa kuwa kila kanisa linajitawala lenyewe .  Ninaamini, na nimesema mara nyingi mimbarani, ya kwamba wachungaji wanapaswa kumrudisha Ndugu Branham kwenye mimbara zao kwa kuzicheza kanda.  Sijawahi kusema yawapasa waache kuhubiri, wacheze tu kanda.  Lakini wanatumia kila kisingizio cha kutocheza Sauti ya Mungu katika makanisa yao.

 Nitamwacha nabii aseme jinsi ninavyohisi kuhusu wachungaji ambao hawataicheza Sauti hiyo katika makanisa yao.

  Sasa, Ndugu Junior Jackson alikuwa na haki ya kutokukubaliana na hayo. Yeye ataka kanisa lake…Watu wote wanataka kunena kwa lugha na mengineyo mkutanoni. Hizo ni taabu za Ndugu Junior; hiyo ni—hiyo ni juu yake. Lakini Junior Jackson anaamini Ujumbe huu sawasawa kama wengine wetu wote wafanyavyo. Yeye ni mmoja wetu.

 4. Je, unaamini kwamba wahudumu wanapaswa kuacha kuhubiri?

 Hapana, sijawahi kusema hivyo wala siamini hivyo.  Neno linatuambia, na Ndugu Branham amekuwa wazi kabisa kwenye Jumbe hizi za Maswali na Majibu, kwa wahudumu kuendelea.

 Najisikia tu kuongozwa, kwa kanisa langu, kufanya utangulizi wa haraka;  ama kwa barua kwa sasa, kisha Kubonyeza Play na kusikia Sauti PEKEE ya Mungu  iliyothibitishwa kwa siku hii.  Nimesema mara nyingi kwamba nina huduma kuu zaidi ulimwenguni, napata kutambulisha Sauti ya Mungu kanisani kwangu kila Jumapili.

5. Watu wanasema unahisi  Usipojiunganisha na ibada za Maskani ya Branham wewe si Bibi-arusi?

 Sijawahi KAMWE kusema hivyo au hata kufikiria hivyo, ndugu na dada zangu.  Yeyote anayeweza kusema kitu kama hicho ni makosa . Nikiwa Kama mchungaji wa Maskani ya Branham, najisikia nikiongozwa kucheza kanda za Ndugu Branham.  Ninaamini hiyo Sauti ndiyo kitu pekee kitakachomuunganisha Bibi-arusi.

 Kama nilivyosema awali, ninaamini kila kitu kwenye kanda hizi ni Bwana Asema hivi na hakihitaji fasiri yoyote.  Ninaweza kusema amina kwa kila Neno ninalosikia.  Ninaamini William Marrion Branham alitumwa kumwita Bibi-arusi atoke .  Nafasi yangu katika huduma tano ni kuwaelekeza watu kwa mjumbe huyo na kisha Kubonyeza Play . Hakuna kitu kikubwa zaidi ya kuisikia Sauti hiyo.  Upako mkuu zaidi uko kwenye kanda, kwa hiyo kwa nini nitake kulipatia kanisa langu kitu kingine?

 Kila Jumapili ninaualika ulimwengu kusikiliza Ujumbe ambao Bwana ameweka moyoni mwangu ili kuucheza kwa kanisa langu.  Kila mtu anakaribishwa kusikiliza kwa wakati mmoja.

 Ninatumia kama kiongozi wangu kile Ndugu Branham alichosema kwenye kanda hizi .

Nasi tuna mfumo huu wa simu sasa, ambao ni mzuri sana, sana. Watu wanaweza kuketi moja kwa moja nyumbani mwao ama nini hii mwao…wakusanyike makwao, makanisani mwao, na kadhalika, na kusikiliza ibada. Nafurahia jambo hilo.

Sasa, ewe mchungaji, nataka ujue jambo hilo, ya kwamba, ninazungumza haya kwa ajili ya kusanyiko langu peke yake. Nami nina haki ya kutenda jambo hilo, kwa maana nimewekwa na Roho Mtakatifu kuwachunga kondoo hawa.

Ujumbe huu, na Jumbe zote zingine ambazo ninazungumzia, zinaelekezwa kwenye kusanyiko langu. Si kwa ajili ya kusanyiko lako isipokuwa wawe wanataka kulipokea. Bali limeelekezwa kwa watu hawa hapa.

Na hilo ni kote kote ulimwengu mzima. Na watu huamka usiku wa manane usiku, katika nchi za kale, hufanya mnyororo huo wa maombi kwa wakati mmoja.  Kwa hakika, makumi elfu na maelfu kwa maelfu wanaomba kwa wakati mmoja.  Mungu hana budi kusikia;  wewe ni—unaivumisha tu Mbingu kwa maombi, unaona, kwa hiyo hana budi kusikia.

 6. Je, ni kosa kwenda kanisani ?

 Sijawahi kusema hivyo wala kuamini hivyo.  Ikiwa niliamini hivyo kwa nini ningekuwa na kanisa?  Katika Maskani ya Branham tulikuwa na ibada 3 kwa wiki hadi ikawa vigumu sana kwangu kuwa na ibada nyingi jinsi hiyo kila wiki na kufanya kazi katika VGR.  Ndipo tukawa na ibada 2 kwa wiki katika Maskani hatimaye isingewezekana kutosha watu .  Kwa hiyo tulihamia kwenye jengo letu tulilotumia kwa ajili ya vijana wetu, ambalo lilikuwa jumba la mazoezi.

 Bwana alikuwa ameweka moyoni mwangu kutoa tamko Jumapili moja asubuhi.  Nilisema hata ikiwa siku moja wangefunga milango ya kanisa hili , hatutakosa hata mpigo kwani mchungaji wetu angeweza kuzungumza nasi popote tulipo.  Mwezi mmoja baadaye,  CORONA Ikaja ambayo ilifunga makanisa kote ulimwenguni.

 Nilijisikia kuongozwa kwamba wakati huo, tungekuwa na fursa nzuri ya kurekebisha ukumbi wa mazoezi, kwani tulihitaji mahali pakuabudia.  Kwa hivyo, tumekuwa na furaha katika nyumba zetu, kuungana na kumsikiliza nabii wa Mungu kwenye kanda pamoja na sehemu ya Bibi-arusi duniani kote, wakati kanisa linarekebishwa.

 Sasa hivi tunamalizia jengo, lakini kama vile tu wakati Ndugu Branham alipokuwa hapa kwenye Maskani ya Branham, tayari tumepita eneo la ziada la maegesho tulilojenga.  Itatubidi tu kuomba na kuona jinsi Bwana aongozavyo.

 Najua kuna maswali mengi, mengi zaidi kwenye mioyo ya watu.  Kuna mambo mengi niliyosema yameeleweka vibaya.  Ikiwa Ndugu Branham Walimwelewa vibaya, ni kiasi gani zaidi basi mimi nitakavyoeleweka vibaya?

 Ninaweza kuwa nimekosea katika kile nilichosema.  Ningeweza kuyasema vizuri zaidi au ningekuwa wazi zaidi kwa jinsi nilivyoyawasilisha.  Ila kuna jambo moja NAJUA ni sahihi, UJUMBE HUU NI MKAMILIFU .  Sio lazima unisikilize mimi au Kile nisemacho, lakini YAKUPASA UBONYEZE PLAY NA UAMINI KILA NENO.

 Kwa mara nyingine tena, ninakualika uungane na Maskani ya Branham Jumapili hii saa 06:00 SITA MCHANA , saa za Jeffersonville, (Ni saa 1:00 MOJA JIONI Ya Tanzania) tunaposikia: Maswali na Majibu #4 64-0830E .

 Ndugu.  Joseph Branham