Category Archives: Uncategorized

23-0312 Makao Ya Baadaye Ya Bwana Arusi Wa Mbinguni Na Bibi-Arusi Wa Duniani

UJUMBE: 64-0802 Makao Ya Baadaye Ya Bwana Arusi Wa Mbinguni Na Bibi-Arusi Wa Duniani

PDF

pakua – m4a

pakua – amr

BranhamTabernacle.org

Mpendwa Bibi-arusi wa Duniani,

Malaki 4 ni Neno la Mungu, nayo imezaa kwa jinsi yake, SISI, Bibi-arusi Wake. Ni Roho Mtakatifu, Utu wa Yesu Kristo, katika matendo , aliyewekwa ndani ya mioyo yetu. Tumehuishwa kwa KILA Neno alilonena, kwa kuwa “Kondoo Wangu huisikia Sauti Yangu; mgeni hawatamfuata.”

Imekuwa ya ajabu jinsi gani miezi hii iliyopita , kumfuata nabii huko Jeffersonville. Mungu amekuwa akizungumza kupitia malaika wake mwenye nguvu na kutulisha kwa Chakula chake kilichohifadhiwa Ghalani kutoka kwenye GHALA LAKE MOJA DOGO katika nchi yote. Ni Mana Iliyofichwa, ni kwa ajili ya Bibi-arusi Wake tu.

Kwa kila Ujumbe tunaousikia, tunashiriki na kufurahi pamoja; “Najua nimezisikia Jumbe hizi mara nyingi sana hapo awali, lakini KAMWE sijawahi kuzisikia kama hivi sasa”. Hakika ni chemchemi ya Maji yaliyo Hai yanayobubujika ndani yetu. Hatuwezi kujizuia. Ndiyo yote tunayotaka kuzungumzia. Hatukuwahi kuwa na uhakika katika maisha yetu, wakujua sisi ni nani na wapi tunaelekea.

Hakuna kujiuliza tena:
“ Mimi Sijui tu. Nimefanya mambo mengi ya kutisha maishani mwangu. Nimemkosea Bwana mara nyingi sana. Inaonekana DAIMA mimi hujichafua.”

Hakuna kutumai tena :
“Natumai kweli kuwa mimi ni mtoto wa Mungu. NINATAKA kuwa. Naomba niwe.”

Siku hizo ZIMEKWISHA . Sasa TUNAJUA . Utukufu kwa Mungu!!

Tunajuaje? Mungu amekuwa akizungumza nasi moja kwa moja kwa Sauti Yake iliyo kwenye kanda, akituambia tena na tena, “Mimi niko ndani yenu, ninyi mko ndani Yangu. Sisi ni MMOJA. Niliwachagua NINYI kabla ya kuwekwa misingi ya ulimwengu. Ninyi ni nyama ya Nyama Yangu , mfupa wa Mfupa Wangu”.

Ni Ujumbe mkamilifu jinsi gani Mungu aliyotuzungumzia siku ya Jumapili kutuambia yote kuhusu jinsi ulimwengu huu tunaoishi si wetu, ni Edeni ya Shetani. Jinsi alivyomdanganya Hawa hapo mwanzo kuhoji na kutilia shaka NENO MOJA tu. Alivua utaji mtakatifu wa Mungu, na kujivika utaji wa maarifa, ndipo macho yake yakafumbuliwa naye akajua alikuwa yu uchi.

Shetani alipotosha Neno la asili, na sasa amempofusha kwamba bado yu uchi wala hajui. Amekuwa malkia wa Shetani na dunia hii ndiyo Edeni ya ufalme wake.

Jumapili, Bwana-arusi wetu wa Mbinguni anataka kumkumbusha Bibi-arusi Wake wa duniani mahali Makao yetu ya baadaye yalipo na vile yatakavyokuwa. “Mpendwa Kipenzi , kwa kuwa sasa nimekwisha kuambia yote kuhusu ulimwengu huu na jinsi Edeni ya Shetani ilivyo, ninataka kukuambia KWA MARA NYINGINE TENA kuhusu Makao YAKO ya Baadaye na mimi .

Nataka kuwaambieni kinaganaga. Najua mmenisikia nikiwaambia juu Yake mara nyingi, lakini ngojeni tu, wakati huu itakuwa kana kwamba hamjawahi kunisikia nikiwaambieni hapo kabla.

Nataka kuingia kwa undani sana. Ninataka kuwafunulia Ninyi mko katika Mapenzi yangu Makamilifu kwa kukaa na Neno langu na nabii Wangu. Ninataka kuwapa mfano wa kile mnachofanya leo hii kama mfano mkamilifu wa ule mji mpya mtakaoishi ndani yake.

Tutaingilia jambo fulani hakika. Nitawadondoshea kitu fulani kidogo; Naamini mtalikamata. Mtaishi katika Mji huo pamoja Nami. Nabii wangu ataishi karibu nanyi . Atakuwa jirani yako. Mtatembea kwenye barabara hizo za dhahabu na kunywa kutoka kwenye Chemchemi Yangu. Mtatembea katika paradiso za Mungu, huku Malaika wakirukaruka na kuimba nyimbo za sifa.

Ninyi mtakuwa vito kwenye taji ya nabii Wangu. Mtang’aa kuliko kitu chochote kile ulimwenguni, katika Siku ile. Kuna mengi nataka kuwafunulieni Jumapili. Ni siku ya ajabu iliyoje tutakayokuwa nayo pamoja”.

Anayo mengi sana ambayo ametuwekea akiba katika wiki chache zijazo, kama hatakuja na kutuchukua kabla ya wakati huo. Wiki baada ya wiki, akituambia, sisi ni akina nani, tunakoelekea, jinsi kutakavyokuwa kule. Atakuwa akituongoza hadi kwenye wiki iliyo tukufu sana ya Pasaka ambayo hatujawahi kamwe kuwa nayo, iliyojawa na si kingine ila kumsifu na kumwabudu yeye.

Ni wakati wa kusisimua jinsi gani . Tunaona unabii ukitimia mbele ya macho yetu. Tunaona Neno likidhihirishwa NDANI YETU. Kuja Kwake kunaweza kutokea wakati wowote. Tunasimama mlangoni tukiwa na shada la maua mikononi mwetu. Tunaweza kusikia farasi wakienda shoti na mchanga ukivingirishwa chini ya magurudumu.

Lile gari la Kale la Farasi litasimama hivi karibuni. Tutaruka kutoka kwenye mlango wa mwili huu mzee na kurukia mikononi Mwake. Atatutazama na kusema, “Yote yamekwisha sasa, mpenzi, nitakupeleka sasa kwenye Makao yako ya Baadaye.”

Unaalikwa kuwa sehemu ya siku zilizo kuu ambazo ulimwengu haujawahi kuona. Wana tai watakusanyika kutoka ulimwenguni kote ili kusikia Sauti ya Mungu ikizungumza na Bibi-arusi Wake na kumwambia yote kuhusu: Makao Ya Baadaye ya Bwana-arusi Wa Mbinguni na Bibi-arusi wa Duniani 64-0802 , saa 06:00 SITA Mchana , saa za Jeffersonville. ( Ni saa 1:00 MOJA JIONI Ya Tanzania na Kenya pia ).

Ndugu. Joseph Branham

Ukumbusho: Msisahau kuhusu badiliko la saa ya Akiba ya mchana.

Maandiko ya kusoma kabla ya kusikia Ujumbe:

Mathayo 19:28
Yohana 14:1-3
Waefeso 1:10
2 Petro 2:5-6 /Sura ya 3 yote.
Ufunuo 2:7 / 6:14 /21:1-14
Walawi 23:36
Isaya Sura ya 4 yote / 28:10 / 65:17-25
Malaki 3:6

23-0305 Edeni ya Shetani

UJUMBE: 65-0829 Edeni ya Shetani

PDF

pakua – m4a

pakua – amr

BranhamTabernacle.org

Watoto Wangu Wapendwa,

Ninyi ni sifa Yangu, Baba yenu wa Mbinguni. Mlikuwa ndani yangu tangu mwanzo. Hamkumbuki hilo sasa, lakini mlikuwemo humo pamoja Nami . Nilitamani sana kuwajua kwa sababu nilitaka kuwasiliana nanyi, nizungumze nanyi, niwapende, na kuwapa mkono.

Kama mtoto wangu, wewe ni sehemu Yangu, uliyefanyika mwili, kama vile nilivyofanyika mwili, ili tushirikiane mmoja na mwengine kama familia ya Mungu duniani. Hilo ndilo lilikuwa kusudi Langu na ndilo nililotaka tangu mwanzo.

Niliwatengenezea Bustani ya Edeni ili tuweze kuwa na ushirika , lakini adui Yangu akaingia kimya kimya kwa udanganyifu , na kuutawala ulimwengu huu kwa kufasiri vibaya mpango wangu kwenu.

Ni saa danganyifu mnayoishi ndani yake, lakini pia ni wakati mzuri zaidi ya nyakati zote, kwa sababu sasa mnaelekea ule Utawala mkuu wa Miaka Elfu tena; mnaelekea Edeni tena.

Roho wangu si kitu ambacho mmeelimishwa. Ni kitu ambacho Mimi nilikiweka ndani yenu kwa kujua kwangu tangu awali kwa mkono Wangu wenye nguvu. Sasa mwito Wangu wa mwisho unatoka kumshika Bibi-arusi Wangu; “Tokeni kati yao, mkatengwe nao”.

Leo wao hawajaribu kuliimarisha Neno Langu katika mioyo ya watu, wanajaribu kujiimarisha wao wenyewe . Makanisa yanajaribu kuimarisha fundisho la kanisa ndani ya moyo wa mtu. Kila mtu akisema, “Nilitenda hili. Mimi, mie, langu, dhehebu langu, mimi, hili.” Wanajiimarisha wao wenyewe na si Neno Langu lililonenwa kupitia nabii wangu.

Haiwabidi kuelewa yote Nisemayo, inawabidi kuliamini tu kwa sababu nilisema hivyo, na hilo latosha milele.

Roho wangu Mtakatifu anatenda kazi ndani yenu. Ni Uzima uliyo ndani yenu, si msisimko wa mwili ; sio namna fulani ya uhakika wa matendo ya kimwili, Bali ni Mtu, MIMI, Yesu Kristo, Neno la Mungu, lililowekwa mioyoni mwenu, nalo linahuisha kila Neno la wakati huu. Ni Roho Wangu Mtakatifu akitenda kazi ndani yenu kulingana na Neno.

Bibi-arusi wangu wa kwanza alianguka kwa kusikiliza hoja za Shetani, lakini Nimewakomboa ninyi kwa nafsi Yangu, ambalo ni Neno lililofanyika mwili. NINYI HAMTANIANGUSHA. Ninyi ni Bibi-arusi-Neno Bikira Wangu ambao hamtasikiliza hoja za Shetani. Mtakaa na Neno Langu.

Baada ya ule Utawala wa Miaka Elfu kumalizika, basi kutakuweko na Edeni iliyowekwa tena; Ufalme wangu mkuu utarudishwa tena. Niliupigania dhidi ya Shetani katika bustani ya Gethesemane, nami nikainyakua Edeni Yangu. Sasa nimeenda kuiandaa Edeni yenu Mpya huko Mbinguni. Nitarudi tena kuwachukueni hivi karibuni, kwa hivyo msifadhaike mioyoni mwenu.

Hakutakuwa na Bahari tena, kwa maana mbingu za kwanza na nchi ya kwanza zitapita. Nitaifanya upya kwa ubatizo wa Moto ambao utaua kila mdudu mbaya , kila maradhi, kila ugonjwa, na kila uchafu uliowahi kuwa duniani.

Dunia itapasuka, kutatokea Dunia Mpya . Mbingu hii ya kwanza na nchi ya kwanza zitapita. Kutakuwa na Yerusalemu Mpya ikishuka kutoka Kwangu Mimi kutoka Mbinguni. Hapo nitakuwa pamoja nanyi, sifa Zangu za kweli, Wanangu wa kiume na wakike. Tutakuwa na ushirika katika utakatifu, macho yenu yakiwa yametiwa upofu yasione dhambi yo yote.

Nimewajieni tena kama nilivyowaahidi ningefanya. Nimelitimiza Neno langu kwenu. Nililirekodi Neno Langu kwenye kanda ya sumaku ili kusiwe na mkanganyiko, hakuna swali, Neno langu safi tu kwa ajili yenu; kwa kuwa ni Bwana Asema Hivi.

Wekeni dhamiri zenu ziwe safi. Ifunikeni mioyo yenu. macho yenu
yafunikwe yasione mambo ya ulimwengu ya kufanywa mtu mkubwa fulani .

Msisahau kamwe, nitageuka huko magharibi na kurudi tena, mojawapo ya siku hizi. Mpaka wakati huo, peleka Jina Langu ; Litafurahisha moyo, peleka, uendako, kwa Kubonyeza Play.

Msipatane hata kwa Neno moja. Neno Langu kwenye kanda halihitaji kufasiriwa. Ninyi ni sehemu Yangu, sifa Yangu. Ulimwengu huu ni Edeni ya Shetani, lakini nimewafanyia Edeni Mpya ambamo tutaishi milele pamoja. Hadi wakati huo, unganeni kwenye Neno Langu. Pendaneni.

Njoo uungane nao katika Maskani ya Branham Jumapili hii saa 06:00 SITA MCHANA saa za Jeffersonville, ( ni saa 2:00 MBILI USIKU ya Tanzania na Kenya pia ) , na mnisikie mimi Nikinena kupitia nabii Wangu niliyemchagua na kufunua Neno Langu mnaposikia; Edeni ya Shetani 65-0829.

Kwa Niaba Yake,
Ndugu Joseph Branham

Maandiko ya kusoma kabla ya Kusikiliza Ujumbe :

2 Timotheo 3:1-9
Ufunuo 3:14
2 Wathesalonike 2:1-4
Isaya 14:12-14
Mathayo 24:24

23-0226 Chujio La Mtu Mwenye Busara

Ujume: 65-0822e Chujio La Mtu Mwenye Busara

PDF

pakua – m4a

pakua – amr

BranhamTabernacle.org

Wapendwa Kusanyiko la Ndugu Branham,

Ningependa kualika ulimwengu kuungana nasi kwa njia ya mawasiliano ya simu Jumapili hii saa 06:00 SITA MCHANA , saa za Jeffersonville, (ni Saa 2:00 MBILI USIKU ya Tanzania) Wakati sisi Tai tunapokusanyika pamoja kila maili mia mbili mraba katika mojawapo ya makanisa ya nabii. Tutamsikia Mungu akinena kupitia malaika-mjumbe wake wa saba na kutuambia:

Ujumbe huu, na Jumbe zote zingine ambazo ninazungumzia, zinaelekezwa kwenye kusanyiko langu. Si kwa ajili ya kusanyiko lako isipokuwa wawe wanataka kulipokea. Bali limeelekezwa kwa watu hawa hapa.

Yeye anazungumza nasi, UTUKUFU, kusanyiko lake. Si ninyi mnaosema, “Ndugu Branham ni nabii, bali yeye si mchungaji wetu. Mchungaji wetu anasema kuzicheza kanda kanisani hakulingani na Neno la Wakati huu.” “Mchungaji wetu anatuambia yatupasa tumsikilize Yeye. Kulingana na Neno, anatuongoza sasa hivi kwa Roho Mtakatifu .”

Nabii aliwaeleza ninyi na mchungaji wenu.

kwa ajili ya wahudumu wo wote mahali po pote, wakati wo wote, hili halielekezwi kwa madhumuni ya kudharau mafundisho yenu, hili hata halielekezwi kwa kondoo wenu.

Hatutaki kubishana nanyi ndugu na dada. Tunaelewa, halielekezwi kwenu, bali kwetu sisi, tunaoamini kwamba Roho Mtakatifu amemweka malaika-mjumbe Wake wa saba kuwa mchungaji wetu na kutuongoza sisi, kanisa Lake. Tunaamini kuzicheza kanda ndiyo NJIA PEKEE YA KWELI. Mko sahihi na mnafanya kile nabii alichowaambia NINYI mfanye:

Na sikuzote mimi huwarejesha, kama wao ni washiriki wa kanisa fulani, “Mwoneni mchungaji wenu.”

Yawabidi mfanye jinsi mchungaji wenu anavyosema.

Kisha nabii anamwambia mchungaji wenu kwa mara nyingine tena, ili tu kuhakikisha ameelewa.

Sasa, ewe mchungaji, nataka ujue jambo hilo, ya kwamba, ninazungumza haya kwa ajili ya kusanyiko langu peke yake. Nami nina haki ya kutenda jambo hilo, kwa maana nimewekwa na Roho Mtakatifu kuwachunga kondoo hawa.

Yeye Ametumwa kutuchunga sisi, kondoo wake; wale ambao Mungu amempa KUWATUNZA. Roho Mtakatifu ndiye mchungaji wetu anapotuzungumzia na kutuongoza kila siku kwa Sauti yake iliyothibitishwa.

Hivi ndivyo Bwana atuongozavyo kufanya. Hatuko dhidi yenu ama mchungaji wenu, au jinsi mnavyohisi kuongozwa na Bwana kufanya. Kila mmoja yampasa kufanya jinsi anavyohisi Bwana anamwongoza kufanya kulingana na Neno.

Tuna chujio moja, UJUMBE HUU. Kila kitu tunachokisikia lazima kipitie kwenye chujio hilo. Sauti tunayoisikia kwenye kanda hizi ndiyo Sauti pekee tunayoamini kwa 100% kuwa Bwana Asema Hivi.

Hivi unaamini ya kwamba huko kutiwa mafuta juu ya watu hao kunamaanisha ya kwamba ni upako wa Roho Mtakatifu?” Naam, bwana, Roho Mtakatifu halisi wa Mungu juu ya mtu, na hata hivyo wao ni wa uongo.

Kikomo chetu cha milele kinategemea kile YEYE ALICHOSEMA KWENYE KANDA, si kile mtu mwingine yeyote ama kundi la watu wanachosema. Kwa hiyo, hatuwezi, na hatutamsikiliza mtu mwingine . anawezaje Mtu yeyote kubahatisha ?

Njooni mkusanyike pamoja nasi zaidi sana kama mwonavyo ile siku ikikaribia.

Watu wanaweza kuketi moja kwa moja nyumbani mwao ama nini hii mwao…wakusanyike makwao, makanisani mwao, na kadhalika, na kusikiliza ibada.

Hilo, marafiki , kulingana na nabii wa Mungu, si kulingana na fasiri ya mtu fulani ya kile Biblia inachosema, ni kukusanyika pamoja kulizunguka Neno zaidi sana kama tunavyoona ile siku ikikaribia.

Sanduku lina faida gani bila Mungu? Ni sanduku tu la mbao, meza mbili za mawe.

Njoo ukusanyike pamoja nasi tunaposikiliza chujio lililoandaliwa na Mungu, anapotuletea Ujumbe: Chujio La Mtu Mwenye Busara 65-0822E.

Ndugu. Joseph Branham

Chunguzeni kile mnachopigania. Chunguzeni kilichowaleta hapa. Chunguza kwa nini unaenda kanisani. Nini kinachowafanya… Ni vyema kwenda kanisani, bali usiende kanisani tu; jambo hilo halitawaokoa.

23-0219 Kristo Amefunuliwa Katika Neno Lake Mwenyewe

Ujume: 65-0822M Kristo Amefunuliwa Katika Neno Lake Mwenyewe

PDF

pakua – m4a

pakua – amr 13MB (use Firefox to download)

BranhamTabernacle.org

Kundi langu Dogo,

Nawasalimu na ninyi mliyo kwenye mfumo huu wa simu, ambao ni mzuri sana, sana. Ninamshukuru sana Bwana mnaweza kuketi moja kwa moja majumbani mwenu, mkusanyike makwenu, makanisani mwenu, na kusikiliza ibada. Kila mahali sauti yangu inapokuja, jalia kundi hilo dogo libarikiwe.

Leo, nataka kuwaandikia barua ndogo ya mapenzi kutoka moyoni mwangu ili kuwatia moyo. Ninyi ndiyo wale ambao Mungu aliyowachagua kuwa Bibi-arusi Wake kabla ya kuwekwa misingi ya ulimwengu; ninyi mnaosikiliza kanda hizi. Nimewaambia mara nyingi sana, kanda hizi ni kwa ajili yenu tu, ninyi ndiyo kusanyiko langu. Mimi Siwajibiki na wale ambao Mungu aliowapa wahudumu wengine kuwachunga; Mimi Ninawajibika tu na aina ya Chakula ninachowalisha ninyi. Kanda hizi ni kwa ajili yenu, maskani yangu pekee , wale ambao Mungu amenipa mimi kuwa mchungaji wenu. Ni Mana iliyofichwa, hao wengine hawawezi kuila.

Sasa, kama watu wanataka kutengeneza chakula cha kisasa na kadhalika huko nje, waache wapate ufunuo kutoka kwa Mungu na wafanye yale ambayo Mungu anawaambia wafanye, wale cho chote wanachotaka. Nitafanya jambo lilo hilo. Bali Jumbe hizi ni kwa ajili yenu ninyi tu.

Ninajaribu sana niwezavyo kudumu kwa unyofu na Neno, kwa ajili yenu ninyi ambao mmewekwa mikononi mwangu kutoka kwa Mungu, maana kondoo huhitaji chakula cha kondoo. “Kondoo Wangu huisikia Sauti Yangu.” Na hilo ndilo tunaloishi kwalo, kila Neno litokalo. Si Neno moja mara hii na mara nyingine, bali kila Neno litokalo kinywani mwa Mungu. Hilo ndilo ambalo ninyi watakatifu mnaishi kwalo.

Kila mtu hana budi kuwa na kitu fulani ambacho wanashikilia. Kitu fulani kinapaswa kuwa nguzo ya kushikilia, kwa maneno mengine, Mkataa. Na kila mtu hana budi kuwa na mkataa ama Yakini. Kwangu mimi, na kwa wale ambao ninatumaini ninawaongoza kwa Kristo, na kwa njia ya Kristo, Biblia ndiyo mkataa wetu.

Basi, tunatambua ya kwamba Mungu alitutumia manabii Wake. Hiyo ndiyo njia aliyokuwa nayo yakulileta Neno Lake kwa watu, kwa kinywa cha nabii Wake. Sasa katika siku hizi za mwisho, Yeye ameahidi kujidhihirisha Mwenyewe katika utimilifu tena, wa mwili Wake, katika Roho. Ni Mungu Mwenyewe katika maumbile ya herufi, sura ya nabii, akidhihirishwa katika mwili.

Sina budi kuishi daima katika uwepo wa yule Mwandishi nikiwa na kalamu yangu tayari wakati wo wote kuandika lo lote yeye Analosema. Nimeelekeza nia yangu daima kwenye mawazo Yake; si vile mwanadamu anavyofikiri, vile wakati huu unavyofikiri, vile kanisa linavyofikiri, vile ufalme unavyofikiri. Mawazo ya Mungu tu! Ninatamka tu mawazo ya Mungu kwa Neno.

Wakati Mungu anapoyafunua mawazo Yake Kwangu , mimi ninayatamka katika Neno kwenye kanda, “BWANA ASEMA HIVI.” Si, “ Mimi Nasema Hivi .” Ni, “BWANA ASEMA HIVI!” Ninaweza tu kulifasiri jinsi vile Mwandishi anavyotaka niwafasirie ninyi ; maana ni Neno la Mungu lisilokosea.

Kuna wengine wengi wanaojaribu kuniiga, kama makuhani, ama kadhalika. Nao wanafanya nini? Wanachafua tu, hivyo tu. Wasingeweza kufanya jambo hilo. Mungu alinituma mimi, nabii Wake, kumwongoza Bibi-arusi Wake; si mtu mwingine, wala si kundi la watu.

Maneno ninayonena, na vile ninavyotenda, itawapofusha wengine, lakini itayafungua macho ya wengine. Alinivalisha kwa namna ya mavazi ambayo ningevaa, tabia yangu, shauku yangu, kila kitu jinsi tu ilivyonipasa kuwa. Alinichagua kikamilifu kwa ajili yenu. Wengine wangesimama na kuangalia waseme, “Vema, siwezi. Kuna…Si—siwezi kuona.” Wao wamepofushwa.

Yeye atajifunua kwa yule yeye atakayemfunulia Hilo . Amelifanya hivi kwamba anaweza kujificha mwenyewe katika Maandiko, kwa mwanatheolojia mwenye akili sana aliyeko. Yeye Anaweza tu kujificha mwenyewe , akae papo hapo katika Maandiko, nao wanaweza kuyatazama siku nzima na wasiweze kuyaona; wayatazame maishani mwote, na wasiyaone kamwe. Anaweza tu Mwenyewe kujificha, akiketi pale.

Jambo lililopo sasa ni wale wanaoupokea Ujumbe mioyoni mwao, hawana budi kukaa katika Uwepo wa Mwana, wapate kuivishwa. Bonyeza Play halafu umwache Mwana aukaushe ubichi wote ukutoke, awafanye Wakristo waliokomaa.

Wakati yeye alipokuja mara ya kwanza, alikuwa mwanadamu. Alipokuja mara ya pili, akiwa na sehemu maradufu, alikuwa mwanadamu. Alipokuja kama Yohana Mbatizaji, alikuwa mwanadamu. Aliahidi kuja katika siku hii na kuishi na kujidhihirisha kwa mara nyingine tena ndani ya mwanadamu; Mwana wa Adamu akiishi katika mwili wa mwanadamu.

Sasa tuko katika wakati wa jicho, kinabii, ya Malaki 4. Hakuna kitu kingine kilichosalia kuja ila Yeye Mwenyewe kuingia ndani ya kitu hicho, ’ maana hilo ndilo jambo la mwisho lililopo.

Sikilizeni enyi wana-kondoo wangu wadogo, ninyi ambao Mungu amenipa kuwa mchungaji wenu. Wakati umeenda sana . Anakuja upesi kuwachukua ninyi , Bibi-arusi Wake. Kaeni na hizo kanda, hazihitaji kufasiriwa.

Ninawaalika ninyi Tai wadogo mje kuungana nami kwenye jambo pekee litakalomleta Bibi-arusi Wake pamoja Jumapili hii, saa 6:00 SITA MCHANA , saa za Jeffersonville.( Ni saa 2:00 MBILI USIKU ya Tanzania na Kenya pia ) Mtasikia Bwana Asema Hivi wakati Mungu anaponena kupitia mimi na kufunua: Kristo Amefunuliwa Katika Neno Lake Mwenyewe 65-0822M.

Kumbuka, KAENI NA HUDUMA YA KANDA . BONYEZA PLAY KILA SIKU.

Ndugu Branham

Maandiko ya kusoma kabla ya kusikiliza Ujumbe:

Kutoka 4:10-12
Isaya 53:1-5
Yeremia 1:4-9
Malaki 4:5
Luka Mtakatifu 17:30
Yohana Mtakatifu 1:1 / 1:14 / 7:1-3 / 14:12 / 15:24 / 16:13
Wagalatia 1:8
2 Timotheo 3:16-17
Waebrania 1:1-3 / 4:12 / 13:8
2 Petro 1:20-21
Ufunuo 1:1-3 / 10:1-7 / 22:18-19

23-0212 Nawe Hujui

UJUMBE: 65-0815 Nawe Hujui

PDF

pakua – m4a

pakua – amr 11MB (use Firefox to download)

BranhamTabernacle.org

Mpendwa Bibi-arusi Anayengoja,

Nami najua ya kwamba, baada ya kuondoka kwangu kutoka dunia hii, hizo kanda na vitabu vitaendelea kuwepo, na wengi wenu ninyi watoto wadogo mtaona, katika siku zijazo, ya kwamba jambo hili ni Kweli kabisa, kwa maana nanena katika Jina la Bwana.

Njoo ukusanyike pamoja na sisi, Tai, Jumapili saa 06:00 SITA MCHANA Saa Za Jeffersonville,( Ni Saa 2:00 MBILI USIKU ya Tanzania na Kenya pia ) . tunaposikia 65-0815 – Nawe Hujui.

Ndugu. Joseph Branham

23-0205 Matukio Yakidhihirishwa Na Unabii

Ujume: 65-0801e Matukio Yakidhihirishwa Na Unabii

PDF

pakua – m4a

pakua – amr 11MB (use Firefox to download)

BranhamTabernacle.org

Wapendwa Watu wa Wakati huu,

Baba, tunakupenda sana. tunawezaje kuanza kueleza jinsi tunavyojisikia? Ulituchagua, ukatukusudia tangu zamani, nawe ukafanyika Mwanadamu aliye hai ili kutoa Maisha Yako kwa ajili yetu.

Ulituandikia mawazo Yako yenyewe kwetu kupitia manabii Wako, ili tupate Neno Lako. Ndipo, kama ulivyoahidi, ulikuja tena , ukijifunua Mwenyewe katika mwili wa mwanadamu kwa matukio yanayodhihirishwa na unabii, kufasiri na kufunua Neno Lako.

Kwa kujichagulia wewe mwenyewe, ulimchagua William Marrion Branham kuwa mtu wa wakati huu. Ulimchagua ili kuvutia usikivu wetu. Uliongoza mikono yake. Uliongoza macho yake katika maono. Hakuweza kusema kitu cho chote ila kile ulichokuwa unamwonyesha.

Hakuweza kusema kitu cho chote ila kile ulichoweka kinywani mwake. Ulitawala kabisa ulimi wake, vidole vyake, na kila kiungo cha mwili wake. Yeye Alikuwa katika utawala wako mkamilifu .

Kisha, kwa kuchagua Kwako kwa mara nyingine tena, ulituchagua tuwe watu wa wakati huu. Kundi lako dogo la walio wachache limekusanyika kwa upako wa Neno Lako, likidhihirisha tena maisha ya Yesu Kristo. Sisi ni Neno Lako tukiungana na Neno. Hatuwezi kufanya kitu kingine .

Baba, tunataka kuwa katika Mapenzi yako makamilifu; hakuna kitu kingine muhimu kwetu. Hatutaki mawazo yetu, fikra zetu, au kile mtu mwingine ye yote asemacho, mapenzi Yako tu.

Tumeliendea Neno Lako ili kuona kile ulichosema tunapaswa kufanya ili kuwa Bibi-arusi Wako. Ulisema utauhukumu ulimwengu siku moja kwa Neno Lako. Ulituambia Neno Lako huwajilia manabii Wako PEKE YAO , ambao walichaguliwa tangu awali na kuamriwa tangu zamani na Wewe.

Ulituambia halimjii kamwe mwanatheolojia wala kundi la watu, bali kwa nabii Wako. Yeye Atakuwa mfasiri wako pekee wa kiungu wa Neno. Si mawazo yake, fikra zake, fasiri yake, bali Wewe ukinena kupitia kwake, ukilifasiri Neno Lako Mwenyewe.

Katika kila wakati, watu wanawaachilia watu waweke fasiri yao wenyewe kwenye Neno Lako, na inawafanya kuwa vipofu . Inafanya jambo lile lile lililofanyika kwa Mafarisayo na Masadukayo. Hiyo ndiyo sababu watu wanashindwa kulipata leo hii. Wao Wanasikiliza kile mtu mwingine anachosema juu Yake, badala ya kusikiliza Neno kama vile nabii Wako alivyowaambia wafanye.

Ulisema, kwanza Ninatuma Neno Langu, halafu kama watu hawataamini Neno Langu, basi Ninawapelekea wahudumu. Pia ulisema katika kila wakati wahudumu hupotoka ; si wote, bali wengi wao, na kuwaongoza watu kwao. Sisi tunataka kuwa katika Mpango Wako wa asili.

Inachanganya sana, wahudumu hawawezi kukubaliana wao kwa wao. Ndugu X hawezi kukubaliana na Ndugu Y; Ndugu Y hawezi kukubaliani na ndugu Z. Hawawezi kukubaliana  wao kwa wao. Wanaonekana kukubaliana juu ya jambo moja tu, hatupaswi kucheza kanda kanisani.
Ni Babeli tena, inachanganya sana. Tunaamini kuna Mchoro mmoja tu na ni lazima tujichonge wenyewe ili kueneana na Mchoro huo, sio kujaribu kukata Mchoro huo ili utuenee.

Kumekuwa na huduma nyingi sana ambazo zimeibuka na mawazo yao wenyewe, fasiri zao wenyewe na mafundisho. Wote wamekuwa si kitu. Kumekuwa na wahudumu wakubwa waliowekwa wakfu waliyoinuka wanaosema wanahubiri na kunukuu Ujumbe wa wakati huu, na huduma yao ndio Njia iliyoandaliwa na Mungu kwa ajili ya wakati huu, na sio kanda.

Wana watu waaminifu wanaoenda kwenye makanisa yao, wakiwasikiliza kwa miaka mingi. Wana wahudumu wengi wanaowatembelea, mikutano, miamsho, mahubiri, wakisema wanachosema wao ndio Njia Yako iliyoandaliwa, na sio kanda. Ndipo siku moja wanasema, Ujumbe huu si kweli.

Je, hawakuwa wanachunguza alichokuwa anasema kwa kutumia kanda hizo? Je! walikuwa wakichukua tu kile alichosema kuwa ni Neno, Njia iliyoandaliwa na Mungu kwa ajili ya wakati huu? Kama angalizicheza kanda, Sauti Yako iliyothibitishwa kwa watu, badala yake wao wenyewe wakijiweka kama sauti iliyo muhimu sana, wangejua waliyekuwa wakimsikiliza ni mpakwa mafuta wa uongo katika mafundisho ya wakati wa mwisho.

Hiyo haimaanishi kuwa huhitaji mchungaji. Haimaanishi wote ni wachungaji watiwa mafuta wa uongo. Hilo Halimaanishi kuna wengi wanaohubiri kile hasa Ndugu Branham alichosema. Bali inamaanisha jambo lililo muhimu sana unalopaswa kusikia ni Ujumbe uliyo kwenye kanda; Ndio BWANA ASEMA HIVI PEKEE.

Ni Mwongozo. Ni Yakini. Ni Neno la mwisho. Ndilo Neno Kamilifu pekee. Isipokuwa mchungaji, kiongozi wako wa kiroho, anasikiliza Neno hilo safi pamoja na watu wake, kuna kitu kitaenda kombo.

Kwa nini wahudumu hawataki kucheza Sauti Yako iliyothibitishwa katika makanisa yao? Wanawezaje kusema ni makosa huku wanadai wanaamini kuwa ni Neno? Kwa nini wanatoa kila aina ya visingizio na kusema huduma yao ndiyo Njia Yako iliyoandaliwa kwa ajili ya Wakati huu, na sio Sauti Yako iliyothibitishwa kwenye kanda?

Kwa nini wanawatisha watu kwa kusema kwa sababu tunasema “BONYEZA PLAY” ili kuisikia Sauti yako, tunamwabudu mtu na sio Wewe unenaye kupitia mtu huyo?

Sisi tunakuabudu WEWE TU BABA. Tunalikagua kwa Neno lako tena na tena. Unatuambia kupitia nabii Wako kwa kila Ujumbe tunaosikia kwenye kanda: Ndiyo Njia Yako pekee iliyoandaliwa kwa ajili ya Wakati huu.

Wapi pengine ambapo Bibi-arusi Wako angeweza kwenda isipokuwa kuongoza moja kwa moja kwenye Neno Lako. Sisi ni Bibi-arusi- Neno Bikira wako. lazima tudumu na Nguzo Yako ya Moto. Ndipo mahali pekee tunapoweza kuridhika na kusema amina kwa kila Neno tunalosikia.

Baba, tunakuona Wewe ukiwa nje ya kanisa lako ukijaribu kuingia ndani, na hilo linaivunja mioyo yetu. Komeo liko kwa ndani nasi tumekufungulia mlango uingie. Hatujui kitu kingine . Hatutaki kitu kingine. Hatuwezi kuchukua kitu kingine. Tumetiwa mimba na Neno lako.

Asante Baba kwa Ufunuo wa Neno Lako. Hatumpingi yeyote, tuko kwa ajili ya Neno lako tu lililodhihirishwa na unabii. Tutasimama mbele zako siku moja kwenye hukumu. Kwa mioyo yetu yote tunataka kusema, “Baba, tumedumu na Neno Lako.”

Mtie moyo mchungaji wako, kiongozi wako wa kiroho, Kubonyeza Play Jumapili hii kusikia Sauti ya Mungu. Utahukumiwa siku moja kwa yale Neno la Mungu lisemayo kwenye kanda. Unawezaje kukipa nafasi kitu kingine cho chote?

Umealikwa kuja kuuungana nasi Jumapili hii saa 06 :00 SITA MCHANA , saa za Jeffersonville, ( Ni saa 2:00 MBILI USIKU ya Tanzania na Kenya pia ), kusikia: Matukio Yakidhihirishwa Na Unabii 65-0801e , Mungu anapozungumza kupitia midomo ya mtu aliyejichagulia. Yule ambaye alimpa tabaka yake, karama zake. Alimpa tabia yake, mwenendo wake, na cho chote kile, jinsi anavyojieleza, cho chote afanyacho. Yeye Alimfanya William Marrion Branham mtu wa wakati huu ili kuwashika watu wa wakati huu, nasi ndio WATU WA WAKATI HUU.

Ndugu. Joseph Branham

Maandiko Ya Kusoma Kabla Ya Kusikiliza Ujumbe :

Mwanzo 22:17-18
Zaburi 16:10 / Sura ya 22 yote / 35:11 / 41:9
Zekaria 11:12 / 13:7
Isaya 9:6 / 40: 3-5 / 50:6 / 53:7-12
Malaki 3:1 / sura ya 4 yote
Yohana Mtakatifu 15:26
Luka Mtakatifu 17:30 / 24:12-35
Warumi 8:5-13
Waebrania: 1:1 / 13:8
Ufunuo: 1:1-3 / Sura ya 10 yote

23-0129 Mungu Wa Wakati Huu Mwovu

UJUMBE: 65-0801m Mungu Wa Wakati Huu Mwovu

PDF

pakua – m4a

pakua – amr 13MB (use Firefox to download)

Mpendwa kundi dogo Neno-Bikira wa Kristo,

Hatuwezi kuwa kitu kingine. Hatuwezi kusikia kitu kingine. Hatujui kitu kingine. Hatutaki kitu kingine. Palipo na Nyama mbichi, KUBONYEZA PLAY, ambalo ni Neno la majira haya, Hapo ndipo Tai watakapokusanyika. Neno linakuwa hai ndani yetu.

Sisi hatuko sawa na mtu mwingine yeyote ! Ninyi ni watu waliotengwa, watakatifu kwa Bwana, waliowekwa wakfu kwa Neno na Roho wa Mungu, kuzaa matunda ya ahadi Yake ya siku hii. Tunazidi kukomaa na kuivishwa kwa kusikia Sauti ya Mungu.

Nabii alituambia turejee kwenye kanda hizi. Kama una kinasasauti, kusanya kundi la watu pamoja na ukaicheze, na msikilize kwa makini. Kusikiliza Sauti Yake, kile anachotuambia. Neno la Mungu halihitaji kufasiriwa; Yeye hujifasiria Mwenyewe. “Mimi ni Sauti ya Mungu kwenu.”

Nalo ndilo Hili, Biblia, neno moja lisiongezwe Kwake au kuondolewa Kwake. Dumuni waaminifu tu kwa Sauti hiyo. “Mgeni hawatamfuata,”

Anawezaje mtu yeyote kutoona Njia ya Mungu iliyoandaliwa kwa ajili ya siku hii? Lakini utukufu kwa Mungu, tunaweza kuiona, kwa sababu tumechaguliwa kuiona . Hatuta, na hatuwezi kudanganywa, kwa sababu sisi ni Neno Lake lililodhihirishwa.

Ndugu na dada, hebu hilo nalizame ndani kwa dakika moja, SISI NI NENO LILILODHIHIRISHWA!! Mungu Mwenyewe, akinena kupitia midomo ya mwanadamu, anatuambia SISI NI NENO. Hatuna chochote cha kuogopa. Kila kitu tunachohitaji ni chetu.

Kila wiki tuko chini ya matarajio makubwa ya Bwana kutuzuru. Hatuna nafasi hapa ya kuketi kila mmoja, wala kila mmoja hawezi kuja Jeffersonville, kwa hiyo inatubidi tu kuwatumia Neno kupitia njia ya mtandao.

Tuko majumbani mwetu, makanisani mwetu, kwenye magari yetu, tumekusanyika kuzunguka vipaza sauti vyetu vidogo kutoka ulimwenguni kote, tukingojea Kuja kwa Bwana.

Wamekusanyika pamoja nasi huko katika Afrika, wakingojea Kuja kwa Bwana. Wamekusanyika pamoja nasi huko Mexico, wakingojea Kuja kwa Bwana. Huko Ulaya, Skandinavia, Australia, Mashariki ya kati, Amerika ya Kusini, kutoka pembe nne za dunia, wakingojea Kuja kwa Bwana.

Nasi tumekusanyika hapa kwenye kanisa la nyumbani, maskani, tukingojea Kuja kwa Bwana. Tuko umbali wa masaa mengi, Bali tuko pamoja kama JAMII MOJA, waamini, tukisikiliza Sauti ya Mungu, tukingojea Kuja kwa Masihi.

SISI NDIO watu walioitwa na waliochaguliwa na Mungu kutoka katika wakati huu mwovu kwa ajili ya Jina Lake. Tunajaribiwa na kuthibitishwa kwa Shetani kwamba sisi ni Neno. Sisi ni sehemu ya ule Mti wa Bibi-arusi wa Asili. Tunatazama maisha yetu yakidhihirishwa na Neno hilo.

Ni rahisi kwa kila mtu kuamini kwamba Yesu alikuwa jawabu la moja kwa moja kwa kila unabii uliokuwa utimie ndani Yake, kwa sababu wanatazama nyuma kuona hayo yakitukia. Lakini katika wakati huu mwovu uliopo sasa, wanafanya jambo lile lile walilofanya wakati huo, kwa kulifasiri kwa njia nyingine, na wamewafanya watu waingie katika nguvu za upotevu wauamini uongo. Laiti wangetambua ni Neno lile lile la wakati huu likidhihirishwa.

Kuna jambo moja tu linaloweza kumleta Bibi-arusi pamoja, Ujumbe huu. Kuna jambo moja tu ambalo sote tunaweza kukubaliana kwalo, Ujumbe huu. Kuna Sauti moja tu ambayo imethibitishwa kuwa Bwana Asema hivi, Sauti ya Mungu kwenye kanda.

Sasa, makanisa tu baridi, ya kawaida, magumu, na kadhalika, ya theolojia za kujitengenezea, hayo hayangeweza; walio Wateule wasingewajali. Lakini ni kule juu karibu sana na jambo lililo halisi. Kuacha tu Neno moja ndivyo tu unavyopaswa kufanya. Lililoahidiwa kwa wakati huu; wakati mkuu sana!Enyi Wakristo, kila mahali, jihadharini na saa tunayoishi! Andikeni, na someni, na msikilize kwa makini.

Mungu wa wakati huu mwovu anafanya yote awezayo kuwadanganya watu kwa kuizuia Sauti Yake iliyothibitishwa isiwafikie. Anajaribu kuwafanya wasiamini Neno moja tu, kama alivyomfanyia Hawa hapo mwanzo.

Lakini Bibi-arusi-Neno wa Kristo anakuja kilipo Kichwa. Tunaungana tena kwa Mwenzi wetu pale tulipoanzia. Wakati wa kutoka umefika. Mungu anakuja kwa ajili Bibi-arusi Wake yule anayedumu na Neno Lake.

Roho Mtakatifu yuko hapa akimwita Bibi-arusi wa Kristo atoke. Yeye anafanya hivyo kwa kumthibitishia Neno Lake la ahadi Kwake, kwa ajili ya wakati huu, akionyesha ya kwamba Hilo ni Kristo.

Hakuna jambo lililo kuu kuliko kuungana na Bibi-arusi ulimwenguni kote, Kusikiliza Sauti ya Mungu ikinena nawe moja kwa moja. Hakuna haja ya kutumaini, kushangaa au hata kuomba ikiwa kile unachosikia ni kweli. Kwa maana Ndiyo SAUTI PEKEE ILIYOTHIBITISHWA YA BWANA ASEMA HIVI.

Njoo uungane nasi ukasikilize:

Baada ya hayo naliona malaika mwingine, akishuka kutoka mbinguni, mwenye mamlaka kuu; na nchi ikaangazwa kwa utukufu wake.

Saa 6:00 SITA MCHANA , saa za Jeffersonville,( ni Saa 2:00 MBILI USIKU YA Tanzania na Kenya pia) tunaposikia: Mungu wa Wakati Huu Mwovu 65-0801M.

Ndugu. Joseph Branham

Maandiko ya kusoma kabla ya kusikiliza Ujumbe:

Mathayo Mtakatifu sura ya 24 yote /27:15-23
Luka Mtakatifu 17:30
Yohana Mtakatifu 1:1 / 14:12
Matendo 10:47-48
1 Wakorintho 4:1-5 / sura ya 14 yote
2 Wakorintho 4:1-6
Wagalatia 1:1-4
Waefeso 2:1-2 / 4:30
2 Wathesalonike 2:2-4 / 2:11
Waebrania sura ya 7 yote
1 Yohana Sura ya 1 yote / 3:10 / 4:4-5
Ufunuo 3:14 / 13:4 / Sura ya 6-8 na 11-12 zote / 18:1-5
Mithali 3:5
Isaya 14:12-14

23-0115 Watiwa Mafuta Katika Wakati Wa Mwisho

Ujume: 65-0725M Watiwa Mafuta Katika Wakati Wa Mwisho

PDF

Server S
Server G

pakua – m4a

pakua – amr 18MB (use Firefox to download)

Wapendwa Wakusanyikao Katika Zizi La Kondoo,

Nimeridhishwa na kumshukuru sana Bwana kwa kukusanyika pamoja na kila mmoja wenu katika zizi la Kondoo wa Mungu kila wiki, ambapo tumefichwa mahali petu pa siri, tukijilisha na kuishi kwa Chakula hicho Kilichofichwa. Ni Ufunuo wa Yesu Kristo, akijithibitisha na kujidhihirisha Mwenyewe kwetu.

Amejificha ili kwamba wengine waliangalie moja kwa moja na bado wasilione, bali kwetu sisi, Bibi-arusi Wake mteule, tunaliona waziwazi na kuamini kila Neno. Tumekaa na Neno Lake na nabii Wake kwani wao ni Mmoja na kitu kile kile .

Na iwapo wewe ni mwana wa Mungu, utakaa pamoja na nabii wa Biblia hii. Ni Neno.

Manabii wengi waliotiwa mafuta siku hizi wanasema “Ni Roho Mtakatifu ndiye unayepaswa kukaa naye, si nabii.” Kama manabii wa kale, kama tuna swali, inabidi kuwe na jibu sahihi. Ni lazima twende KWENYE NENO kuona kile nabii aliyetutangulia alichosema.

Lakini kuna Kristo mmoja aliye halisi, Roho, na huyo ni Neno lililofanyika mwili kama alivyoahidi kufanya.

Kristo MMOJA aliye halisi, Roho, ambaye Yeye aliahidi, Malaki 4, Luka 17, Mwana wa Adamu akijifunua Mwenyewe katika mwili wa mwanadamu.

Ndiyo, kuna watu waliotiwa mafuta. Ndiyo, wana wito. Ndiyo, wana Roho Mtakatifu halisi. Ndiyo, wana nia na makusudi sahihi.

Basi tutajuaje wa kweli na wa uongo?

Angalia, wanafanana. Wametiwa mafuta namna ile ile. Lakini angalia, “Kwa matunda yao…”

Sipendi kusema mambo haya lakini saa imechelewa sana na wakati unaenda. Hili ndilo linalosemwa na kuhubiriwa leo na wale mbwa-mwitu wakali Paulo alilionya kanisa kuwahusu, na wale wapakwa mafuta wa uongo ambao Ndugu Branham aliyosema wangekuja. Wako hapa kati yetu, kama tu walivyosema.

Hapa kuna kipande kidogo cha barua iliyoandikwa kutoka kwa mhudumu . Matunda yao yanajaribu kutilia shaka juu ya nabii wa Mungu. Wanawaonya watu wao kuwa sisi ni miungu watu kwa sisi kumfuata nabii na Kubonyeza Play.

Sikiliza jinsi hili lilivyodanganyifu.

Nimekerwa kwamba pepo huyu amepenya tabaka zetu za ujumbe hivi kwamba sasa tunaita vitabu vya mahubiri ya William Branham SAUTI YA MUNGU. William Branham hakuwa sauti halisi ya Mungu , bali ni sauti ya mwanadamu ambayo Mungu aliyotumia. Biblia haisemi kamwe kwamba Yeye alikuwa ni sauti ya Mungu, bali Biblia inamtambulisha kama sauti ya malaika wa 7. ( Ufu 3:14; 10:7 ).

Hebu twende kwenye NENO na tumwache nabii wa Mungu ayaanike wazi mafundisho haya ya uongo.

Ikiwa kwa kusema hivyo niliwakera, mnisamehe, lakini, nilihisi kwamba hilo laweza kuchukiwa, lakini, MIMI NI SAUTI YA MUNGU KWENU .

Sasa utamwamini nani, nabii huyu wa uongo aliyetiwa mafuta, au MALAIKA-MJUMBE WA SABA WA MUNGU ALIYETHIBITISHWA ? Unawezaje kukaa chini ya mhudumu yeyote ambaye anayeamini au anayekufundisha mambo kama hayo? Afadhali uingie katika Neno wakati ungalipo.

Kosa la kutisha limefanywa na jumuia ya ujumbe katika kumfanya William Branham kuwa mungu kwa kumfanya kuwa yakini. William Branham hakuwa kamwe yakini! Neno la Mungu ndilo Yakini.

Amina, Neno la Mungu NDIYO Yakini yetu. Neno lilikuja kwa nani, kwako wewe au kwake YEYE? Ni nani aliye mfasiri wa kiungu wa NENO LA MUNGU, wewe au YEYE? Ni nani ambaye Nguzo ya Moto ilimthibitisha kuwa Bwana Asema hivi, wewe au YEYE?

Kwa sababu ukiwa na watu wawili, una maoni mawili.

Hatuhitaji watu wawili wala maoni yao, tunahitaji tu kile nabii wa Mungu alichosema kwenye kanda.

Yapasa kuwe na Yakini moja thabiti , na Yakini yangu ni Neno, Biblia .

Hilo hapo, kama vile ulivyosema, Biblia ni Yakini yake na yetu, lakini kisha anasema:

Najua ninyi ni Ndugu , mnanichukua mimi kama Yakini Yenu .

Kwa hivyo subiri kidogo, hilo linasikika kinyume na ULICHOSEMA. Alisema kwamba tunamchukua yeye kama Yakini Yetu.

Mradi ninamfuata Mungu kama Paulo alivyosema katika Maandiko , “ Mnifuate mimi kama ninavyomfuata Kristo .”

Je, huyo si aliyetiwa mafuta? Je, hakujua alichokuwa anazungumzia?

Hivi Nabii wa Mungu alituambia nini wiki iliyopita?

Tunaona ya kwamba mtu anapokuja, ametumwa kutoka kwa Mungu, amechaguliwa na Mungu, akiwa na BWANA ASEMA HIVI ya kweli, ujumbe huo na mjumbe huyo ni mmoja na kitu kimoja .

Alisema huwezi kuwatenganisha, ni kitu kimoja, lakini unasema tunapaswa kuwatenganisha?

William Branham hana tofauti na mwanadamu ye yote apatikanaye na mauti, kwa maana alikuwa mtu wa tabia moja na Eliya alivyokuwa .

Amina, alikuwa mwanadamu tu hakika, lakini alikuwa NDIYE MTU ambaye Mungu alimchagua kufunua Neno Lake lote kwake , na kutuongoza kwenda kwenye Nchi ya Ahadi. Yeye ndiye ambaye Mungu alisema, wafanye watu WAKUAMINI.

Kitu kile kile, wametiwa mafuta, wakihubiri Injili ya Pentekoste, bali wakiikana ahadi ya siku hii ya Neno kuthibitishwa , “ Yesu Kristo yeye yule jana, leo, na hata milele .”

Tutajuaje tofauti ikiwa wao ni wapakwa mafuta wa kweli wa Roho Mtakatifu? Anatupa mifano ili tujue kati ya manabii wa uongo na nabii wa kweli.

Balaamu na Musa. Mikaya na Zedekia. Yeremia na
Hanania. Katika kila kisa wote wawili walikuwa manabii waliotiwa mafuta wa Mungu, lakini alituambia tufanye nini, TUDUMU NA NABII WA MUNGU ALIYETHIBITISHWA. Hiyo ndiyo njia PEKEE ya kuwa na uhakika kwamba unafuata Njia ya Mungu iliyoandaliwa, na uko katika mapenzi Yake makamilifu.

Mimi ndiye tu ninayekuwa karibu wakati anapoyafanya. Mimi nilikuwa tu sauti aliyoitumia Yeye, kusema jambo Hilo. Haikuwa yale niliyojua; ni yale niliyojitolea kwake tu , aliyozungumza kupitia .

Hayo ndiyo yote Bibi-arusi anayotaka na anayohitaji. Sauti Moja. Nabii mmoja. Ujumbe Mmoja. Mjumbe mmoja.

Ee Baba, jinsi tunavyoshukuru kwa neema na rehema zako kwetu. Ulituambia hakuna lisilowezekana kwako. Hakuna lisilowezekana kwetu sisi. Kwa maana yote yanawezekana kwao waaminio, nasi TUNAAMINI.

Njoo uungane nasi Jumapili saa 06:00 SITA MCHANA , saa za Jeffersonville, (ni Saa 2:00 MBILI USIKU ya Tanzania na Kenya pia.) tukiwa na Sauti iliyochaguliwa ya Mungu ikituambia yote kuhusu  Watiwa-Mafuta katika Wakati wa Mwisho 65-0725M.

Ndugu.  Joseph Branham

23-0108 Chakula Cha Kiroho Kwa Wakati Wake

UJUMBE: 65-0718e Chakula Cha Kiroho Kwa Wakati Wake

PDF

pakua

BranhamTabernacle.org

Wapendwa Watafuta Madini ,

Kuna kisima kinachofoka maji cha Ufunuo ambacho kinabubujika ndani yetu zaidi ya hapo awali. Tumesikia Ujumbe huu maisha yetu yote, na daima tumeamini kila Neno, lakini SASA imedhihirishwa ndani yetu zaidi kabisa ya hapo awali.

Sasa huu ndio wakati wake , sasa ni majira yake tunakula mambo ya siri ya Mungu ambayo ulimwengu umefichwa. Kitu kile watu wanachokicheka, ndicho kitu tunachokiomba. Kile kitu ambacho watu wanaita “wenda wazimu,” tunakiita “Kikuu!”
Mungu ametufunulia kuna njia moja tu iliyoandaliwa ya kuwa Bibi-arusi Wake, KUBONYEZA PLAY.

Lakini Mungu ashukuriwe, tuna Chakula kilichofichwa, Chakula cha kiroho, hata tunaishi kwa fadhili na rehema za ufunuo wa Yesu Kristo katika siku hizi za mwisho, akijithibitisha Mwenyewe miongoni mwa watu Wake.

Kwa kila Ujumbe anaousikia Bibi-arusi, Yeye hututhibitishia hayo ni Mapenzi yake makamilifu. Sio kile TUNACHODHANI Anasema, wala si kile TUNACHODHANI Inamaanisha , NI HASA KABISA Yale yeye Asemayo na bado wengine hata hawawezi kuliona; wamepofushwa. Mungu amelificha. Wanalitazama moja kwa moja, lakini hawalioni. Kwetu sisi, NDIYO YOTE TUYAONAYO.

Tunapokusanyika kila wiki, ni vigumu kungoja kusikia kile Atakachoenda kutuambia na kutufunulia. Jumapili hii, yeye hatatupa vijisehemu fulani vidogo vya vito vya thamani vilivyofichwa, Yeye atatupa jiwe kubwa la madini na KULlLIPUA tena na tena ili kuhakikisha tunalipata.

. Huyo nabii alikuwa amekaa kwa muda mrefu sana katika Uwepo wa Mungu, Manabii wa Agano la Kale, ama wa wakati wo wote, walipoishi katika Uwepo wa Mungu mpaka wakawa Neno, Ujumbe wao ni Neno Lenyewe . Pia, kumbukeni, yeye alisema, “BWANA ASEMA HIVI.”

. Tunaona ya kwamba mtu anapokuja, ametumwa kutoka kwa Mungu, amechaguliwa na Mungu, akiwa na BWANA ASEMA HIVI ya kweli, ujumbe huo na mjumbe huyo ni mmoja na kitu kimoja.

. Basi wakati mtu anapokuja na BWANA ASEMA HIVI , yeye na Ujumbe huo ni mmoja .

. Mbingu zinatangaza jambo hilo, Biblia inalitangaza, Ujumbe unalitangaza. Yote ni jambo lile lile.

. Nabii, Neno, Ujumbe; mjumbe, Ujumbe, na Ujumbe, walikuwa mmoja.

. Mtu ye yote na ujumbe wake ni mmoja .

Nena kuhusu Mgodi wa Dhahabu.

Ikiwa una hata chembe ya Ufunuo , nadhani yeye analiweka wazi kweli hilo; Ujumbe na mjumbe ni MMOJA . Je, unasikia alichosema… MMOJA !! Basi Enyi Wahudumu, hamwezi kumtenganisha mjumbe na Ujumbe.

Unatakiwa kumweka MJUMBE kanisani mwako pamoja na UJUMBE aliouleta vinginevyo wewe haukubali UJUMBE WOTE. WEWE SI BIBI-ARUSI.

Loo! Tena, jambo hilo linaufanya Ujumbe na mjumbe kuwa ni kitu kimoja. Chakula cha kiroho kiko tayari, na kiko katika wakati wake sasa.

Kwetu sisi, tunaoamini saa ya Mungu tunayoishi, mjumbe Aliyemtuma, kila Neno alilonena; mambo haya ni Chakula kilichofichwa.

Jinsi tunavyoupenda Ujumbe huu, na unapowazia tu, “Kunawezaje kuwa mengine zaidi?” Yeye Anaweka jiwe la kifuniko juu Yake kwa kutuambia sisi ni nani sasa.

Hivi hamwoni mamlaka ya Mungu aliye hai katika Kanisa lililo hai, Bibi-arusi ? Wagonjwa wanaponywa, wafu wanafufuliwa, viwete wanatembea, vipofu wanaona, Injili inatangazwa katika nguvu Zake, kwa maana Ujumbe na mjumbe ni kitu kimoja. Neno liko ndani ya Kanisa, katika mtu.

Neno Hilo NDANI YETU . Sisi ni Ujumbe. Tunayo mamlaka. Ujumbe huu na sisi NI MMOJA!! Nena kuhusu kububujika tena na tena na tena.

Bibi-arusi ni sehemu ya Mume, Kanisa ni sawa na Kristo. “Kazi nizifanyazo Mimi ninyi nanyi mtazifanya.”

Sisi ni sehemu ya Mume!!

SISI NI SAWA NA KRISTO!!

Unafikiri inasikika sasa vizuri , na kuubariki moyo wako kwa kusoma tu nukuu hizi, subiri tu mpaka uisikie Sauti ya Mungu ikikuelezea hizo mdomo kwa sikio Jumapili hii saa 6:00 SITA MCHANA , saa za Jeffersonville,( ni Saa 2:00 MBILI USIKU ya tanzania na Kenya pia) tunaposikia: 65-0718E. Chakula Cha Kiroho Kwa Wakati Wake.

Umealikwa kuja kuungana nasi. Kama huwezi, BONYEZA PLAY wakati wowote, Ujumbe wowote, mahali popote, na umsikie mjumbe wa Mungu akikuletea Ujumbe wa Mungu.

Ndugu. Joseph Branham.

Ndivyo ilivyo leo, ya kwamba Chakula cha Uzima ambacho watoto wanakula, kinafuata Ujumbe wa Mungu, kuwahifadhi katika wakati wa ukame.

Maandiko ya kusoma kabla ya Kusikiliza Ujumbe :

1 Wafalme 17:1-7
Amosi 3:7
Yoeli 2:28
Malaki 4:4
Luka 17:30
Yohana 14:12