Category Archives: Uncategorized

23-0430 Wakati Wa Kanisa La Efeso

Ujume: 60-1205 Wakati Wa Kanisa La Efeso

PDF

pakua – m4a

pakua – amr

BranhamTabernacle.org

Mpendwa Dhahabu Safi Iliyofuliwa,

Jinsi gani Ninavyoshukuru kuungana pamoja na kila mmoja wenu, tukiingia katika Roho na kumsikiliza Mungu akizungumza nasi, mdomo kwa sikio. Hakuna mwisho kwa kile anachotufunulia. Mioyo yetu imejaa furaha. Nafsi zetu zinabubujika. Anawezaje mtu kuelewa kile tunachosikia?

Sikilizeni tu kile Bwana Mwenyewe anachotuambia: “Ninyi ndio Kanisa Langu la kweli, Bibi-arusi Wangu. Kwangu mimi, mmefananishwa na dhahabu SAFI. Haki yenu ni haki yangu. Sifa zenu ni sifa ZANGU mwenyewe tukufu. Utambulisho wenu wenyewe unapatikana ndani Yangu. Kile MIMI NIKO, mnakihakisi. Kile NILICHO NACHO, mnakidhihirisha.

KWANGU mimi, hakuna kosa ndani yenu, ninyi ni watukufu ndani na nje. Tangu mwanzo hadi mwisho, ninyi ni kazi Yangu…na kazi ZANGU zote ni kamilifu.

Hamtasimama kamwe hukumuni, kwa sababu dhambi haiwezi kuhesabiwa kwenu. Hata kabla ya misingi ya dunia, kusudi Langu lilikuwa ni kushiriki Uzima Wangu wa Milele pamoja NANYI.

Je, mtu anawezaje kufahamu Maneno haya? Akili zetu zinawezaje kufahamu kile kinachotendeka? Ni nini kimefunuliwa? Wazia jambo hilo, hatupaswi kulia mioyoni mwetu na kusema, “Loo, laiti ningalikuwa kule nyuma katika wakati wa kwanza wakati mitume walipotumwa kwanza.” HAKUNA haja ya sisi kuangalia nyuma, kwa sababu Yeye, ambaye habadiliki kamwe katika tabia au katika njia zake, Yeye yuko katikati yetu SASA, akizungumza nasi na kutuambia kuwa Yeye ni yeye yule jana, leo na hata milele. Huu ni wakati MKUU zaidi katika historia ya ulimwengu kuishi ndani yake.

Tunapigwa na kutakaswa, na kujazwa na mateso ambayo Kristo aliacha. Tunahesabiwa kama kondoo wa kuchinjwa. Tunauawa siku nzima. Tunateseka sana, lakini katika hayo yote, hatulipizi kisasi, wala hatusababishi wengine wateseke. Kwake, sisi ni dhahabu safi iliyofuliwa, sio kukunjwa, sio kuvunjwa, sio kuharibiwa, bali kufanywa kitu chenye uzuri na furaha milele kwa majaribu na majaribio ya maisha haya.

Sasa Yeye anawaonya wengine wote, “Rudini kwenye Upendo wenu wa Kwanza”. Jinsi gani Wanavyopaswa kuwa waangalifu kwani hupaswi kubadilisha HATA NENO MOJA, hata nukta au dashi. Hiyo ilikuwa ndio hila ya asili ya Shetani katika bustani ya Edeni. Neno moja tu likiongezwa, Neno moja tu likiondolewa, basi ni Mpinga-Neno.

Katika wakati huu wa mwisho anatuonya kutakuwa na manabii wengi wa uongo watakaotokea, wakiwaambia watu ya kwamba wasipowaamini wao na yale wanayosema , mtapotea.

KUNA NJIA MOJA PEKEE ya kuwa na Hakika HAKUNA KITU Kilichoongezwa, hakuna kilichoondolewa, hakuna kilichobadilishwa… kwa kusikiliza SAUTI YA MUNGU safi…KUBONYEZA PLAY.

Mshukuru Bwana kwa ajili ya mhudumu wa kweli, aliyefundishwa kwa uaminifu, ambaye si tu anawaambia kondoo wao umuhimu wa kusikiliza Ujumbe kila siku majumbani mwao, bali kwa kuwa viongozi wa kweli, kuweka Ujumbe Huu, Sauti Hii, Kanda Hizi, NAFASI YA KWANZA NA ILIYO YA KWANZA KABISA kwa watu walio katika makanisa yao.

Kwa kusema mambo haya, naeleweka vibaya na ninatuhumiwa kwa kuyagawa makanisa na kuwaambia watu wasiende makanisani. Hiyo si kweli. NENO linawatoa watu kutoka katika makanisa haya ambayo hayaweki kanda NAFASI YA KWANZA katika makanisa yao. Wana njaa ya kusikia Neno kutoka kwa Nabii wa Mungu. Wanajisikia HUO ndio Ujumbe na Sauti iliyo muhimu zaidi wanayotaka kusikiliza. Wanajisikia Ni Mapenzi Makamilifu ya Mungu kuzicheza kanda kanisani mwao.

Daima nimewaambia watu, “NENDENI KANISANI”. Wanapouliza: “Je, unahisi wahubiri bado wanaweza kuhubiri?” “Ndiyo.” Sijawahi kusema ama kuwazia kwamba hawapaswi. Kwa urahisi Ninawaambia wahubiri, waalimu, wachungaji, “Fanyeni kile Mungu alichowaitia, LAKINI TAFADHALINI, iwekeni hiyo Sauti yenyewe ya Mungu iliyo kwenye Kanda NAFASI YA KWANZA, SI HUDUMA YENU”.

Huo ndio UFUNUO WANGU. Wao yawabidi wafanye vile WANAVYOJISIKIA KUONGOZWA KUFANYA. Nina haki ya kuhubiri na kufundisha kile ninachojisikia. Kama Wao wanataka kusema Ndugu Branham kamwe hakuwahi kusema Kubonyeza Play Kanisani, Sauti yenyewe hasa ya Mungu wanayodai kuwa wanaifuata, hiyo ni juu yao.

Roho Mtakatifu ndiye, na daima amekuwa, akimwongoza Bibi-arusi Wake. Tunaamini Yeye anatuambia, “BONYEZENI PLAY, KAENI NA NABII WANGU, SAUTI YANGU, ROHO WANGU MTAKATIFU.”

Vema, tutakuwa na mashindano ya jambo hilo, basi, kama nabii Eliya kabla ya hapo . Na iwapo wewe ni mwana wa Mungu, utakaa pamoja na nabii wa Biblia hii. Ni Neno. Angalia ile saa, huo wakati.

Nabii wa Biblia ni nani, Neno, Roho Mtakatifu!

Roho Mtakatifu ndiye Nabii wa wakati huu; Yeye analihakikisha Neno Lake, akilithibitisha . Roho Mtakatifu alikuwa ndiye Nabii wa wakati wa Musa. Roho Mtakatifu alikuwa Nabii wa wakati wa Mikaya. Roho Mtakatifu, aliyeliandika Neno, anakuja na kulithibitisha Neno.

Roho Mtakatifu wa wakati huu anatuongoza Kupitia nabii Wake, kama jinsi alivyofanya katika kila wakati. Mungu kamwe habadilishi mpango Wake.

Kwa hiyo, unaalikwa kuja kuungana nasi katika kile tunachojisikia kuwa ndio Mpango wa Mungu kwa kumsikiliza Roho Mtakatifu akizungumza kupitia nabii Wake, na kutuongoza anapotuletea Ujumbe: 
Wakati Wa Kanisa La Efeso 60-1205 , saa 6:00 SITA MCHANA. Masaa ya Jeffersonville. ( ni saa 1:00 MOJA JIONI ya Tanzania na Kenya pia .)

Ndugu. Joseph Branham

Maandiko ya kusoma Kwa ajili ya maandalizi ya Kusikiliza Ujumbe :

Matendo 20:27-30
Ufunuo 2:1-7

23-0423 Ono La Patimo

Ujume: 60-1204E Ono La Patimo

PDF

pakua – m4a

pakua – amr

BranhamTabernacle.org

Wapendwa, Wapenzi Wa Neno la Mungu,

Inapendeza jinsi gani kuweza kuongea na kila mmoja wenu kama Wapenzi wa Neno la Mungu. Hakuna kitu kinachoweza kupachukua mahali Pake. Kuwa na nafasi ya kumsikiliza Bwana wetu kila siku ya maisha yetu, akisema nasi kupitia midomo ya mwanadamu, na kutuambia Yeye ni nani na SISI NI NANI. Hakuna mahali, hakuna sauti, hakuna kanisa, na hakuna mtu anayeweza kukuambia mambo haya kama SAUTI YA MUNGU.

Alituambia uvuvio wa Neno ulikuwa kwenye kanda. Yote tunayopaswa kufanya ni Kubonyeza Play na Roho Mtakatifu anakijaza chumba. Mjumbe wetu alikuwa akivuta Uzima, na nuru, kutoka kwenye rasilimali za bakuli hilo kuu. Utambi wake ulikuwa umezamishwa humo ndani.

Maisha yake yanawaka moto wa Roho Mtakatifu. Utambi wake (uhai) umezamishwa ndani ya Kristo. Kupitia huo utambi anaunyonya uzima ule ule wa Kristo, na kwa huo, anatupa mwangaza sisi, Bibi-arusi.

Kisha anatuambia sio tu kwamba utambi wa mjumbe Wake mwenye nguvu upo mle, bali sote tunanyonya kutoka kwenye chanzo kimoja. Sote tumetumbukizwa kwenye bakuli moja. Tumekufa kwa nafsi zetu na uhai wetu umefichwa katika Mungu kwa njia ya Kristo, umetiwa muhuri na Roho Mtakatifu.

Hakuna mtu anayeweza kututoa kutoka kwenye mkono Wake. Maisha yetu hayawezi kuchezewa. Uhai unaoonekana unawaka na kuangaza ndani yetu, ukitoa nuru na madhihirisho ya Roho Mtakatifu. Maisha yetu ya ndani, yasiyoonekana yamefichwa ndani ya Mungu na kulishwa kwa Neno la Bwana. Tunao Ufunuo wa Yesu Kristo katika siku yetu.

Jinsi gani Neno linavyolisha nafsi zetu. Hakuna lakulinganishwa nalo. Jinsi gani ameandaa njia ambayo Bibi-arusi, kutoka ulimwenguni kote, wanaweza kukusanyika pamoja ili kusikia Sauti ya Mungu kwa wakati mmoja. Haijalishi wakosoaji ama wanaoshuku wanasema nini, Mungu ametengeneza njia na ni harufu nzuri ya manukato Kwake. Ndio kwanza Atuambie kwamba atatukusanya pamoja sote mwishoni mwa siku ya tatu. Utukufu!!

Hebu sote na tukusanyike pamoja Jumapili hii saa 06:00 SITA MCHANA , saa za Jeffersonville,( ni saa 1:00 MOJA JIONI Ya Tanzania)kusikia Sauti ya Mungu ikituletea Ufunuo wa Neno tunaposikia: Ono la Patmo 60-1204E.

Kwanza, ni lazima TUINGIE KATIKA ROHO kama tutakavyosikia;

Ile sauti iliyotangaza Neno Lake katika Bustani ya Edeni na juu ya Mlima Sinai, sauti ambayo ilisikika pia katika utukufu mkuu wa Mlima wa Kugeuzwa Sura, ilikuwa inatangaza mara nyingine tena, na wakati huu kwa yale makanisa saba pamoja na ufunuo mkamilifu na wa mwisho wa Yesu Kristo.

Ndugu. Joseph Branham

Maandiko ya kusoma ili kujitayarisha Kusikiliza Ujumbe.

Kumbuka kusoma na kusikiliza kitabu cha Nyakati Saba za Kanisa.

Isaya 28:8-12
Danieli 7:8-14
Zekaria 4:1-6
Malaki 4:1-2, 4:5
Mathayo 11:28-29, 17:1-2
Yohana 5:22
Waebrania 4:3-4, 4:7-10, 4:12
Ufunuo 1:9-20, 19:11-15

23-0416 Ufunuo Wa Yesu Kristo

Ujume: 60-1204M Ufunuo Wa Yesu Kristo

PDF

pakua – m4a

pakua – amr

BranhamTabernacle.org

Mpendwa mti wa bibi-arusi,

Ni yubile iliyoje aliyonayo Mti wa Bibi-arusi. Mioyo na roho zetu zinawaka ndani yetu kuliko hapo awali. Anatembea na kuzungumza nasi, akifunua Neno Lake. Mambo yanatokea haraka sana hatuwezi kuendana nayo.

Tunalisikia Neno kamilifu la Mungu likidhihirishwa na Mti mkamilifu wa Nabii, ukihubiri Neno kamilifu la Nabii, likizaa tunda kamilifu la Nabii, kwa Neno kamilifu la Mungu.

Kila kitu kilichoharibiwa na kuliwa na wale wajumbe wanne wa mauti walioua Mti, sasa kimerudishwa tena na wajumbe wanne wa Uzima. Si wajumbe WATANO, si wajumbe wa huduma tano, si kundi; WAJUMBE wanne ndio wameurudisha Mti wa Bibi-arusi.

Tangu mwanzo wa wakati, Mungu amengojea siku na majira haya yatimie ili aweze kuliona tunda lake, katika wakati Wake, kwa majira ya nabii. Sisi ndio Tunda hilo. Haya ndio majira yenyewe. Wakati wa mavuno umefika.

Wikiendi hii ya Pasaka ilikuwa kama hakuna Pasaka nyingine ambayo mtu yeyote amewahi kuiona. Hatutakuwa kamwe jinsi tulivyokuwa. Uwepo kama huo wa Bwana. Nilikuwa nikingojea Unyakuo kufanyika sekunde yoyote.

Katika Biblia, Daudi alisema Maneno haya: Walinizua mikono na miguu yangu. Naweza kuihesabu mifupa yangu yote: Wao wanitazama na kunikodolea macho.

Watu walikuwa wamesoma na kusikia kifungu hicho kwa mamia ya miaka, lakini Yesu alipokuwa akining’inia pale mbele ya macho yao msalabani, Bibi-arusi lazima yawezakuwa alimtazama na kutambua, Leo, Maandiko Haya Yametimia mbele ya macho yetu.

Jinsi ambavyo lazima walijisikia walipotambua kwamba walikuwa wanaona, kwa macho yao, Maandiko hayo yakitimizwa, na walikuwa sehemu ya Neno lililoandikwa.

Ndio sisi SASA. Tunaishi katika siku ambazo Maandiko yote ya mwisho yanatimizwa mbele ya macho yetu; na sisi ni sehemu ya Maandiko hayo.

Yeye anatembea moja kwa moja kati yetu. Ni mwisho wa siku ya tatu. Ametokea na kutuonyesha ishara ya kufufuka kwake. Ni yeye yule jana, leo, na hata milele. Sisi ni matunda hai ya Uwepo Wake. Amedhihirishwa na anaonekana kwetu sote, Kanisa Lake.

YEYE ANALIFANYAJE JAMBO HILO?

Nabii ameondolewa kutoka katika dunia hii, Lakini Roho Mtakatifu yuko kwenye kanda, naye anaenda kwenye mataifa na ulimwenguni kote. NI HUDUMA HAI YA BWANA YESU KRISTO. Anamkusanya Bibi-arusi Wake wote pamoja kwa jambo moja pekee linaloweza, na litakalofanya hivyo: Neno Lake. Sauti yake. KUBONYEZA PLAY!

Leo, Maandiko haya Yametimia.

Yeye ndiye Mti wa Bwana-arusi kutoka katika Bustani ya Edeni. Lakini Mti wa Bwana-arusi bila wakike, hauwezi kuzaa matunda; Hana budi kuwa na Mti wa Bibi-arusi. Huyo ni WEWE. Mlizaliwa kwa kitu kile kile. Neno limefanyika mwili ndani YENU. Maisha yale yale yaliyo ndani ya Bwana-arusi yako sasa hivi ndani YENU.

Bibi-arusi anapaza sauti: Haleluya, Amina, Utukufu!!

Je, ni mambo gani aliyotuwekea akiba hapo mbele?

Lakini sababu ya wakati huu maalum ilikuwa ni kwamba tungeninii…Juu ya moyo wangu Roho Mtakatifu alikuwa ameweka ilani hii ya kusadiki, kwamba, “Kanisa katika siku hizi linapaswa kupata Ujumbe huu.” Kwa sababu, ninaamini ya kwamba ndio Ujumbe ulio muhimu sana wa Biblia, kwa sababu unamfunua Kristo katika Kanisa Lake kwenye wakati huu.

Kwa hiyo, Bibi-arusi atakuwa anakusanyika Jumapili hii saa 06:00 SITA MCHANA , saa za Jeffersonville ,(Ni saa 1:00 MOJA JIONI ya Tanzania ) tunaposikia: Ufunuo Wa Yesu Kristo 60-1204M.

Ningependa kuwahimiza msikie, au kusoma, kila wiki katika Kitabu cha Nyakati za Kanisa, sura ambayo tumesikia kila Jumapili. Tutakuwa tukichapisha audio kwa Kiingereza kwenye Lifeline – Redio ya Sauti kila siku kwa nyakati tofauti, lakini jisikie huru kukisoma, kukisiklizia na kukisoma wiki nzima wakati wowote.

Hebu na tushangilie na kufurahi. Msiukazie ulimwengu huu na dhambi na fadhaa zinazotuzunguka pande zote. Hebu tusherehekee kwa yote anayotufanyia kila siku.

Katika siku za Musa, nina hakika watu waliendelea kumuuliza Musa,
“Tutaondoka lini mahali hapa? Tutatoka lini hapa?”

Naweza tu kumsikia Musa akiwatuliza watu na kusema:

“Mungu akiwa tayari. Lakini kwa sasa, furahieni yote anayowafanyia NINYI”.

Je! Mna vyura nyumbani mwenu? HAPANA.
Je! Mna nzige zilazo mimea yenu? HAPANA
Je! Mna maji ya kunywa yenye damu? HAPANA. Mnakunywa maji safi ya kisima kinachobubujika. Ninyi kaeni kitako tu na mfurahie yote Anayofanya na kuwafunulia.

Ni kifo, maangamizi na hukumu kwao. Lakini kwako wewe, hizi ni siku zilizo kuu zaidi duniani. Kuwa mwenye furaha, amani na shangwe. Msifu tu Bwana kwa yote anayofanya, na utarajie yale atakayofanya hapo mbele.

Ndugu. Joseph Branham

23-0407 Ukamilifu

Ujume: 57-0419 Ukamilifu

PDF

pakua – m4a

pakua – amr

BranhamTabernacle.org

Molingami Mwasi na Libala, tika ete biso nyoso elongo toyangana lelo mpe toyoka Liteya Bobongi be 57-0419. Ekozala koleka na Voice Radio na 12:30 nsima ya nzángá, ntango ya Jeffersonville, kasi mpo baoyo na ngambo na nivale minene, bómiyoka ba nsómi koyoka na ntango nyoso ekoki na manáka ya libota na bino

Ndeko Joseph Branham

23-0406 IBADA MAALUM YA USHIRIKA

Ujume: 57-0418 IBADA MAALUM YA USHIRIKA

pakua – m4a

pakua – amr

BranhamTabernacle.org

Mpendwa Mti wa Bibi-arusi Uliyorudishwa,

Kwa muda wa mwaka mzima, nimetazamia kwa hamu wikendi ninayoweza kufungia nje ulimwengu kabisa, kuzima vifaa vyangu vyote, kuomba siku nzima, kusikia Sauti Yake ikizungumza na moyo wangu, kushiriki Ushirika Naye, na kuweka wakfu upya maisha yangu kwa ukamilifu Kwa ajili ya Huduma yake. KILA SIKU inapaswa kuwa siku ya Pasaka kwetu, lakini wikendi hii ni tukio la kipekee sana, fursa takatifu; wakati uliotengwa kwa Bibi-arusi kukusanyika pamoja na Kuabudu. NIMESISIMKWA SANA kuhusu jambo hilo Enyi marafiki. Siwezi kungoja zaidi ili kujifungia na Mungu mahali pa siri, hapo katika Roho, nikiutazama Uso Wake; nikiungana na Bibi-arusi wa Kristo ulimwenguni kote, tukiketi katika mahali pa mbinguni. Lihimidiwe Jina la Bwana! Kwa kweli inapaswa kuwa wikendi inayotarajiwa sana na takatifu katika maisha yetu.

Loo, hebu tusimame dakika moja tu zaidi hapa. “Mahali pa Mbinguni.” Sasa, si popote pale, bali mahali pa Mbinguni. Tumekusanyika katika “Mbingu,” ina maana kwamba hapo ndipo mahali pa mwaminio. Basi, kama nimeomba vya kutosha, nawe umeomba vya kutosha, au kanisa limeomba vya kutosha, na tuko tayari kwa Ujumbe, nasi tumekusanyika pamoja kama watakatifu, walioitwa wakatoka, waliobatizwa na Roho Mtakatifu, wamejazwa na baraka za Mungu, wameitwa, wakateuliwa, wameketi pamoja mahali pa Mbinguni sasa, sisi ni wa Kimbinguni katika nafsi zetu. Roho zetu zimetuleta katika hali ya Kimbinguni. Loo, ndugu! Haya basi, hali ya Kimbinguni! Loo, nini kingetokea usiku wa leo, kungetokea nini usiku wa leo kama tungekuwa tumeketi hapa katika hali ya Kimbinguni, huku Roho Mtakatifu anatembea katika kila moyo ambao umezaliwa upya na ukawa kiumbe kipya katika Kristo Yesu? Dhambi zote zikiwa chini ya Damu, katika ibada kamilifu, huku tumemwinulia Mungu mikono yetu na mioyo yetu imeinuliwa, tumeketi katika mahali pa Mbinguni katika Kristo Yesu, tukiabudu pamoja katika mahali pa Mbinguni.

Je, umewahi kuketi mahali kama hapo? Loo, mimi nimeketi hata ningelia kwa furaha na kusema, “Mungu, kamwe usiniache nikaondoka hapa.” Mahali pa Mbinguni tu katika Kristo Yesu!

Akitubariki na Nini? Uponyaji wa Kiungu, kutangulia kujua, ufunuo, maono, nguvu, lugha, tafsiri, hekima, maarifa, baraka zote za Kimbinguni, na furaha isiyoneneka na iliyojawa na Utukufu, kila moyo umejazwa na Roho, tukitembea pamoja, tukiketi pamoja katika mahali pa Mbinguni, hakuna wazo moja baya kati yetu, hakuna hata sigara moja inayovutwa, hakuna nguo moja fupi, hakuna jambo hili, lile au lingine, hakuna wazo moja baya, hakuna aliye na neno dhidi ya mwingine, kila mtu akizungumza katika upendo na upatanifu, kila mtu katika moyo mmoja na mahali pamoja, “ndipo kukaja ghafla toka Mbinguni uvumi kama wa upepo wa nguvu ukienda kasi.” Haya basi, “Ametubariki kwa baraka zote za rohoni.”

Bwana Yesu pokea ibada zetu kwako wikendi hii ya Pasaka. Hebu na tuingie katika mahali pa mbinguni katika Kristo Yesu; na tupasue kuingia katika Patakatifu pa Patakatifu. Hakuna wazo moja baya, hakuna kizubaishi chochote, bali kwa nia moja, katika Mahali pamoja; basi kuwe na sauti kutoka Mbinguni ikija kama uvumi wa upepo wa nguvu uendao kasi katika kila moja ya nyumba zetu. “Njoo Bwana Yesu”, tuko tayari kukuona uso kwa uso.

Kwa maana Bibi-arusi amerudishwa kupitia Ujumbe wa Nuru ya jioni ya siku yetu; kupitia Ujumbe wa Malaki 4. Tunakushukuru Bwana kwa dhihirisho kamili la Kristo katika Kanisa Lake, si kanisa lililojengwa kwa mikono, bali dhihirisho kamili la Kristo aliyedhihirishwa ndani ya mtu, nabii wako, kwa ishara kuu na maajabu, naye amefunua Neno lote la Mungu tena. Na sasa linaishi ndani ya Bibi-arusi Wako ulimwenguni kote. Asante kwa kutuwezesha kuishi ili kuona Nuru hii kuu ya jioni, kulingana na unabii.

Basi Nuru ya jioni imetokea kwa ajili gani? Nuru ya jioni ni ya nini? Kurudisha. Whiu! Mnalipata? [Kusanyiko linasema, “Amina.”—Mh.] Nuru ya jioni ni kwa ajili ya kusudi lile lile la Nuru ya asubuhi, kurudisha kile kilichokatiliwa mbali na Nyakati za Giza, kupitia Roma. Mungu anaenda kurudisha, kwa kuangaza Nuru ya jioni (ya nini?), kulirudisha Neno lote la Mungu tena, dhihirisho kamili la Kristo katika Kanisa Lake. Kila kitu alichofanya Yeye, vile vile hasa alivyofanya, itakuwa hivyo tena katika Nuru ya jioni. Mnaona ninayomaanisha? Loo, hilo si ni zuri sana? [“Amina.”] Na kujua ya kwamba tunaishi papa hapa kuiona sasa, Nuru ya jioni, kulingana kabisa na unabii.

Bibi-arusi wa kweli haishii katika Kuhesabiwa haki, ingawa anajua dhambi zake ni kana kwamba hakuwahi kuzitenda kamwe; Yeye haishii katika Utakaso, ingawa Ametakaswa na kutengwa kwa ajili ya utumishi; Haishii katika Pentekoste, ingawa amepokea ubatizo wa Roho Mtakatifu; bali anaendelea hadi kwenye NENO LA SIKU YETU: Malaki 4, Neno Lenyewe lililofanyika mwili tena katika mwanadamu. Ile, “Nitarudisha asema Bwana,” ambayo italeta Imani ya Kunyakuliwa kwa Bibi-arusi. Na Neno hilo lililodhihirishwa linaweza TU kuja kwa kuzisikia Kanda, Jina Lake la ajabu na lisifiwe.

Mmoja wao, Martin Luther, yeye alianza kuiangaza Nuru. Kulikuwako na Nuru ndogo, nguvu kidogo sana, ya kuhesabiwa haki.

Ndipo akaja Wesley, nguvu zaidi, utakaso.

Baada ya Wesley, akaja aliye na nguvu zaidi kuliko yeye, Pentekoste, ule ubatizo wa Roho Mtakatifu, katika nabii mwingine mkuu. Unaona?

Lakini katika siku za mwisho, za Malaki 4, Eliya atakuja pamoja na Neno lile lile. “Neno la Bwana lilimjia nabii.” Katika Nuru za jioni, atatokea, apate kurudisha na kurejesha. Kitu gani? “Kuirudisha mioyo ya watoto iirudie Imani ya Mungu.” Nuru ya nne!

Njooni mkusanyike kulizunguka Neno, majumbani mwenu, wakati wa wikendi ya Pasaka na hebu tumwabudu Bwana. Zimeni simu zenu isipokuwa kupiga picha, kusikiliza Nukuu ya Leo, na kuzicheza kanda kwenye programu ya The Table , programu ya Lifeline, au anuani ya kupakulia.

Ningependa sote tuungane kwenye ratiba ifuatayo:

ALHAMISI

Ilikuwa ni Alhamisi usiku ambapo Bwana Yesu alikuwa na Karamu ya Mwisho pamoja na wanafunzi wake, katika ukumbusho wa Pasaka kabla ya kule kutoka kwa wana wa Israeli. Ni fursa iliyoje tuliyo nayo ya kufanya ushirika na Bwana katika nyumba zetu, kabla ya wikendi yetu takatifu, na kumwomba yeye atusamehe dhambi zetu, na kutupa sisi sote kile tunachohitaji katika safari yetu.

Mungu, chunguza mioyo yetu sasa. Je, ile Damu iko humo Bwana? Kama haimo, twaomba kuwa—kuwa utaiweka sasa hivi, ukiondoa dhambi zetu na kuzifunika, nazo zitatengwa nasi, Bwana, dhambi za ulimwengu huu, ili tuwe watakatifu na wa kupendeza mbele za Baba yetu sasa tunapokuja kula ule—ule mwili wa Damu iliyomwagwa ya Mwana-Kondoo wetu, Mwana wa Mungu, Mwokozi wetu.

Asante kwa kuturuhusu kuishi katika kuona Nuru hii kuu ya jioni, kulingana na Unabii.

Kwa ndugu na dada zangu wa nchi za ng’ambo,

Hebu sote tuanze saa 12:00 KUMI NA MBILI jioni . kwa masaa ya nchi na eneo unaloishi, kusikia Ushirika 57-0418. na kisha tuende katika Ibada yetu maalumu ya Ushirika itakayokuwa ikicheza kwenye programu ya Lifeline ama unaweza kupakua Ujumbe kwa Kiingereza ama lugha zingine kwa kubofya kwenye anuani hapa chini.

Kufuatilia Ujumbe, tutakusanyika na familia zetu majumbani mwetu na kushiriki Meza ya Bwana.

Hivi karibuni tutakuwa na anuani ya kupakua vyote kanda na ibada ya Ushirika, au, itapatikana kwenye Voice Radio .

IJUMAA

Hebu tuende katika maombi pamoja na familia zetu saa  3:00 TATU asubuhi ( ni saa 10:00 KUMI jioni ya Tanzania)., na kisha tena saa   6:00 SITA mchana( ni saa 1:00 MOJA JIONI ya Tanzania ), tukimualika Bwana kuwa pamoja nasi na kujaza nyumba zetu na Roho Mtakatifu tunapojiweka wakfu Kwake.

Mawazo yetu na yarudi huko nyuma hadi siku ile pale Kalvari, zaidi ya miaka 2000 iliyopita, na kumwona Mwokozi wetu akining’inia msalabani, na kisha tujitoe vivyo hivyo kufanya daima yale yanayompendeza Baba:

Sasa tunaona ya kwamba ilimwakisi kikamilifu. Yule Mchongaji sasa alikuwa amelifanya Neno kuakisi kwenye kile Kipeo tena, kilichoitwa Mwanawe, Mungu, Imanueli. Wazia tu, ya kwamba, mtu ambaye amejidhili sana mpaka Mungu akajitambulisha Mwenyewe mle ndani, katika mwili huo, Naye akawa…Yeye na Mungu wakawa mmoja. “Mimi na Baba Yangu ni Mmoja. Baba Yangu anaishi ndani Yangu. Mimi daima hufanya lile linalomfurahisha Baba.”

Vipi kama Mkristo siku hizi angeweza kuwa na ushuhuda kama huo? Ungekuwa ni kipeo papa hapa Yuma, mtaani. Kama wewe ni dobi mwanamke huko nje nyuma beseni la kufulia, ungali utakuwa ni kipeo kwa Mungu, wakati unapoweza kusema, “Daima nafanya kile kinachompendeza Mungu,” na ulimwengu mzima unaweza kuona ka—kazi ya Yesu Kristo ikiakisi ndani yako.

Kisha saa  6:30 Sita na Nusu Mchana.,(  ni saa 1:30 MOJA na NUSU jioni ya Tanzania ), tuungane pamoja katika nyumba zetu ili kusikia, Ukamilifu 57-0419.

Kisha Hebu na tuungane tena pamoja katika maombi saa 9:00 TISA alasiri.( ni saa 4:00 Nne Usiku ya Tanzania). katika ukumbusho wa kusulubiwa kwa Bwana wetu.

JUMAMOSI

Hebu sote kwa mara nyingine tena tuungane katika maombi saa 3:00 TATU Asubuhi ( ni saa 10:00 kumi jioni ya Tanzania )., na  saa 06:00 SITA Mchana( ni saa 1:00 Moja jioni ya Tanzania)., na tutayarishe mioyo yetu kwa ajili ya mambo makuu atakayotutendea miongoni mwetu.

Bwana! Tafadhali, Bwana! Loo, naweza nikaimba kupita kiasi. Huenda nikahubiri kupita kiasi. Huenda nikapaza sauti kupita kiasi. Huenda nikalia kupita kiasi. Lakini kamwe sitaomba kupita kiasi. Ee Mungu, nichunguze na unijaribu.

Nilikuwa tu nikizungumza, muda mfupi uliopita, kuhusu madimbwi ya kina kirefu, jinsi yanavyoziakisi nyota; tia kina cha Roho wako ndani yetu, Bwana, kama nabii Daudi alivyosema, “Uniongoze kando ya maji matulivu,” sio maji yanayotiririka. Maji matulivu, niongoze huko, Bwana. Ninyamazishe.

Kisha saa  6:30 SITA na NUSU Mchana ( ni Saa 1:30 moja na Nusu jioni ya Tanzania )., Sote tutakusanyika pamoja kusikia NENO:
Kuzikwa 57-0420.

Hii itakuwa SIKUKUU ILIYO MUHIMU ilioje kwa Bibi-arusi Wake ulimwenguni kote.

Kisha tuungane tena pamoja katika maombi saa 9:00 TISA alasiri . ( ni Saa 4:00 Nne Usiku ya Tanzania )

JUMAPILI

Ni Siku kamilifu jinsi gani kusikia na kushiriki Kurejeshwa Kwa Mti wa Bibi-arusi. Kwanza Hebu na tuamke mapema kama vile Ndugu Branham alivyofanya asubuhi ile wakati rafiki yake mdogo, yule robin, alipomwamsha
saa 11:00 KUMI na MOJA asubuhi .. Hebu na tumshukuru Bwana kwa kumfufua Yesu kutoka kwa wafu:

Saa kumi na moja asubuhi ya leo, rafiki yangu mdogo mwenye kifua chekundu aliruka dirishani akaniamsha. Ilionekana kana kwamba moyo wake mdogo ungepasuka, akisema, “Amefufuka.”

Saa  3:00 TATU asubuhi .( ni saa 10:00 kumi jioni ya Tanzania)  hebu na tuungane kwa mara nyingine tena katika mnyororo wetu wa maombi, tukiombeana sisi kwa sisi na kujitayarisha kuisikia Sauti ya Mungu.

Saa  6:30 Sita na Nusu mchana .(ni Saa 1:30 Moja na Nusu jioni ya Tanzania )tutakusanyika pamoja kusikia Ujumbe wetu wa Pasaka:  Kurudishwa Kwa Mti wa Bibi-arusi 62-0422.

Baada ya Ibada hii, Hebu na tuungane tena katika maombi, tumshukuru kwa WIKENDI YA AJABU ALIOTUPATA KUWA PAMOJA NAYE NA PAMOJA NA BIBI-ARUSI WAKE ULIMWENGUNI KOTE.

Kwa ndugu na dada zangu walio nchi za ng’ambo, kama mwaka jana,

Ningependa kuwaalika kuungana nasi kwa matukio haya kwa saa za Jeffersonville, kwa vipindi vyote vya maombi kwenye ratiba hii na kwa kanda itakayochezwa   Jumapili Alasiri . Ninatambua, hata hivyo, kwamba kucheza Kanda Alhamisi, Ijumaa, na Jumamosi alasiri katika wakati wa Jeffersonville kungekuwa vigumu sana kwa wengi wenu, kwa hivyo tafadhali jisikie huru kucheza Jumbe hizo wakati wowote wa mchana unaokufaa. Ningependa, hata hivyo, tuungane wote pamoja Jumapili saa 6:30 Sita na Nusu mchana., saa za Jeffersonville, ( Ni saa 1:30 moja na Nusu jioni ya Tanzania )ili kusikia Ujumbe wetu wa Jumapili kwa pamoja.

Ningependa pia kukualika wewe na watoto wako kuwa sehemu ya karatasi za vipindi vya Creations na video za Maelekezo, na majaribio ya YF, ambayo familia yako yote inaweza kufurahia pamoja. Tunaamini mtayapenda kwa kuwa yote yanahusu NENO tutakalosikia wikendi hii.

Kwa ratiba ya wikendi, taarifa kuhusu kujiandaa kwa ajili ya ibada ya Ushirika, nyenzo zitakazohitajika kwa ajili ya vipindi vya Creations, majaribio ya Pasaka, na taarifa nyinginezo, tazama anuani zilizopo hapa chini.

Ni heshima kubwa kwangu kukualika wewe na familia yako kukusanyika pamoja na Bibi-arusi duniani kote kwa wikendi iliyojaa KUABUDU, SIFA NA UPONYAJI. Ninaamini kweli ni wikendi ambayo itabadilisha maisha yako milele.

Ndugu Joseph Branham

23-0402 Unyakuo

Ujume: 65-1204 Unyakuo

PDF

pakua – m4a

pakua – amr

BranhamTabernacle.org

Mpendwa Neno Juu ya Neno,

Makanisa mengi yametatizika, yana mshangao , yameduwazwa, yamepigwa na butwaa, yamefadhaika, yamechanganyikiwa na hata kushangazwa na kile kinachoendelea kwa hawa “ Watu wa Kanda ” kutoka ulimwenguni kote kila Jumapili.

Ni Muungano Usioonekana wa Bibi-arusi wa Kristo, tukiketi katika uwepo wa Mwana, kuivishwa, tukijiweka wenyewe tayari. Bwana Arusi Wetu wa Mbinguni amekuwa akituambia yote kuhusu Makao yetu ya Baadaye Pamoja Naye.

Majuma machache tu yaliyopita Alituambia: “Dunia hii si Makao yako, ni Edeni ya Shetani, nami nitaiteketeza kwa moto. Wewe ni kipenzi changu, ambaye Nimekuchagua kabla ya kuwekwa misingi ya ulimwengu kuwa Bibi-arusi wangu. Sasa, Jumapili hii nitakuambia yote kuhusu Unyakuo Wangu unaokuja hivi karibuni.”

Tuko chini ya matarajio makubwa sana. Tunaweza kulihisi jambo hilo hewani. Mambo yanatukia haraka sana.

Vile vile hasa Biblia ilivyosema ingetendeka katika siku hii, inatendeka, siku baada ya siku. Mbona, inalundikana upesi sana huko nje, katika yale majangwa, na mambo yanayotendeka, hata nisingeweza kufuatilia jambo hilo. Tuko karibu na kule Kuja kwa Yesu, kuunganishwa na Kanisa Lake, ambapo Neno linafanyika Neno.

Haya yote yanatendeka kwa ajili yetu, Bibi Mteule wake, Bibi-arusi wa siku hii. Sisi ndio pekee tunaoona mambo haya yakijifunua.

Ametuchagua tangu zamani kwa ajili ya wakati huu na hakuna mtu yeyote anayeweza kupachukua mahali petu. Sasa Sisi ni wana na binti waliodhihirishwa ili tuweze kushirikiana Naye; hicho ndicho yeye Anachotaka.

SISI ni Neno juu ya Neno, chembe hai juu ya chembe hai, Uhai juu ya Uhai, na kimo kikamilifu cha Bibi-arusi wa Bwana Yesu Kristo.

Kama unalo hitaji, litamke . Wewe ni Neno juu ya Neno. Usiangalie utusitusi huu katika ulimwengu unaotuzunguka; magonjwa, maradhi, mauaji, kukata tamaa, ukichaa wa watu ambao hawajui ikiwa wao ni mwanamume au mwanamke. SISI NI BIBI-ARUSI , tuliochaguliwa tangu zamani , tumehesabiwa haki, Bibi-arusi aliyedhihirishwa wa Bwana Yesu Kristo.

Usiogope LOLOTE. Kuwa mwenye furaha na kushangilia. Muda umekaribia. Tunajiandaa kuondoka kwenye nyumba hii ya wadudu, UTUKUFU !!!

Njoo ujiweke tayari pamoja nasi kwa ajili ya Unyakuo , Jumapili saa 06:00 SITA MCHANA , saa za Jeffersonville ( ni saa 1:00 MOJA JIONI ya Tanzania). Kamwe Hutabaki kama ulivyokuwa.

Ndugu. Joseph Branham.

Maandiko ya kusoma Kabla ya Kusikiliza Ujumbe :

Zaburi 27:1-5

23-0326 Muungano Usioonekana Wa Bibi-Arusi Wa Kristo

Ujume: 65-1125 Muungano Usioonekana Wa Bibi-Arusi Wa Kristo

PDF

pakua – m4a

pakua – amr

BranhamTabernacle.org

Mpendwa Bibi Mteule,

Ungetoa nini ili Bwana Yesu aje kuingia nyumbani mwako Jumapili hii, aketi kwenye kochi lako, akuangalie machoni na anene nawe moja kwa moja?

Husingeweza kuzungumza. Usingependa kuzungumza. Yote ungalitaka kufanya ni kumwangalia yeye tu na kulia. Ungeogopa hata kufungua mdomo wako. Ungeweza kusema nini? Katika mawazo yako ungekuwa unawazia, Bwana, sistahili kabisa kwako Wewe kuwa hapa nyumbani mwangu. Mimi ni wa chini kabisa kuliko walio chini. Nimekukosea mara nyingi sana Bwana, lakini Bwana, nakupenda sana.

Ndipo ungetambua moyoni mwako, Anajua kabisa yale ninayowazia, hakuna kitu kilichofichwa Kwake. Anazijua kabisa siri za moyo wangu.

Unapotazama katika Macho Yake ya thamani, ungeona huo upendo na huruma. Angeweza kuzungumza nawe bila hata kufungua kinywa chake. Ungekuwa ukiwazia, Yeye yuko hapa, nyumbani mwangu, pamoja nami.

Moyo wako ungeanza kwenda mbio hata zaidi, ulipoona Akiwa karibu kutamka kitu fulani kwako. Mara moja, ile Sauti tamu sana ambayo hujawahi kuisikia ingesema, “ mpendwa, kipenzi changu ,usihofu, jina lako limo kwenye Kitabu changu cha Uzima cha Mwana-Kondoo. Si kitabu cha zamani cha ndoa yako ya kawaida, bali Kitabu Changu kipya cha Bibi-arusi. Ni cheti chako cha ndoa na Mimi.

Kipenzi, si kwamba tu umesamehewa dhambi zako zote na kushindwa kwako, Bali kwangu mimi , UMEHESABIWA HAKI. Machoni mwangu, hujawahi kufanya lolote baya.

Wewe ni mwana na binti yangu wa thamani, mwadilifu, asiye na dhambi. Unasimama bila doa; Bibi-arusi Wangu asiyeghoshiwa ambaye ameoshwa kwa Maji ya Damu Yangu Mwenyewe.

Kabla hata hakujakuwa na mwezi, nyota, au molekuli, ulikuwa mwana na binti yangu. Wewe ni onyesho la kimwili la sifa zilizokuwa ndani Yangu hapo mwanzo.

Jeni yako ya kiroho ilikuwa ndani Yangu kwa sababu wewe ni dhihirisho la sifa Zangu, mawazo Yangu. Ulikuwa ndani Yangu hata kabla ya kuwekwa misingi ya ulimwengu.

Wewe ni Bibi-arusi Wangu wa kiroho ambaye umekuwa ukikaa katika Uwepo wa Mwana, kuivishwa, kwa kusikiliza Neno Langu. Sasa umeanza kuwa na uamsho, kurudi na kujiweka sawa na Neno Langu. Wewe ni Bibi-arusi wangu, bibi-Mteule.

Sasa mnao muungano wa kiroho pamoja nami. Mwili wako unakuwa Neno, na Neno linafanyika mwili; likidhihirishwa na kuthibitishwa. Vile vile hasa nilivyowaambia ingetendeka katika siku hii, inatendeka, siku baada ya siku. Neno likifanyika Neno.

Mnao Ufunuo wa kweli wa siku hii ya mwisho: kukusanyika pamoja kwa Bibi-arusi Wangu kwa Ujumbe Huu. Hakuna wakati mwingine niliouahidi hilo. Niliwaahidi ninyi jambo Hilo, katika wakati huu: Malaki 4, Luka 17:30, Yohana Mtakatifu 14:12, Yoeli 2:38.

Tutakuwa na Sikukuu ya Kutoa shukrani Jumapili hii nitakapowaeleza hata na zaidi. Nitatumia muda mwingi, nikishiriki na kusherehekea Neno Langu pamoja nanyi. Nitawahakikishieni tena kwamba kwa kukaa na Neno Langu, nabii Wangu, Sauti Yangu, Kubonyeza Play, mko katika Mapenzi Yangu makamilifu .

Niliwaambia wao katika Neno Langu, Nasimama mlangoni, nabisha. Mtu yeyote akiisikia SAUTI yangu, na akaufungua mlango, nitaingia kwake, nami nitakula pamoja naye, na yeye pamoja nami. Wengi hawatasikiliza na kufungua mlango wao, lakini kwa Ufunuo, ninyi mmefungua mlango wenu na kunikaribisha ndani.

Hawakubaliani na kuicheza Sauti Yangu katika makanisa yao. Iwapo wangemwacha tu Roho Mtakatifu achunguze nia zao kwa Neno, wangekubali. Mwache Kristo, Neno lililotiwa mafuta, achunguze dhamiri yako mwenyewe. Mwache yeye aingie ndani yako, uone kama Hiyo ni kweli ama sivyo.

Niliwaambia halitakuwa dhehebu litakalowakusanya pamoja, wao hawawezi kukubaliana kwenye Neno moja au mawili katika Biblia. Je! Niliwahi kamwe kuwaambia litakuwa kundi la watu? Hapana! Niliwaambia ulikuwa ni Ujumbe wa Mtu MMOJA; na mkasikiliza na kutii.

Kwa sababu hawakusikiliza na kukubali mpango wangu wa asili tangu mwanzo, Nikawatumia wahubiri, waalimu, mitume, wachungaji na manabii. Lakini walitumwa kuwaelekeza watu KURUDI kwenye Mpango wangu wa asili na mkamilifu, Malaika Wangu mwenye nguvu. Kwa maana ni Sauti ya Mungu kwenu.

Wametiwa mafuta, lakini MIMI nina NABII-MJUMBE MMOJA WA KUWAONGOZA NINYI. ROHO MTAKATIFU ​​NDIYE NABII. Je, sijawaambia mara nyingi, NENO LANGU LILILONENWA KUPITIA KWAKE HILO HALIHITAJI KUFASIRIWA, USIONGEZE KWALO AU KUONDOA CHOCHOTE ALICHOSEMA, SEMA TU YALE ALIYOSEMA KWENYE HIZO KANDA ? Huyo ndiye nabii, Roho Mtakatifu anayewaongoza.

Yeye ndiye niliyemtuma kuwaita muwe Bibi-arusi Wangu. Yeye ndiye wa kuwatambulisha ninyi Kwangu. Yeye ndiye niliyesimama naye nilipomwonyesha kukaguliwa kwenu kimbele, Bibi-arusi Wangu. Niliwaambia yote kumhusu yeye katika Ufunuo niliposema, MIMI Yesu nimemtuma MALAIKA WANGU kuwashuhudia ninyi mambo haya KATIKA MAKANISA. Ni MIMI, natumia tu mwili wake na sauti yake kuzungumza nanyi.”

Ni siku ya ajabu jinsi gani tunayo kuwa nayo pamoja Naye. Hatujawahi kuwa wenye furaha au kuridhika zaidi hivi maishaini mwetu. Hii ndio YENYEWE . Hili ndilo tumekuwa tukingojea maisha yetu yote.

Hakuna kivuli cha shaka katika mioyo yetu ama akili zetu. Kwa maana kwa kila Ujumbe tunaosikia, anatuambia tuko katika Mapenzi yake makamilifu. Kuna Sauti moja tu itakayowaunganisha ninyi, kuwakamilisha, na kuwaleta pamoja…Mimi, MIMI NIKINENA KUPITIA NABII WANGU. SI MANENO YAKE, NI MANENO YANGU. NI NJIA YANGU ILIYOANDALIWA.

Meza imeandaliwa. Imejaa Makabeji, na matanipu, na mafigili…NENO JUU YA NENO, JUU YA NENO. Tutakuwa na Sikukuu ya Kutoa shukrani ambayo Haijawahi kutokea. Kutakuwa na yubile duniani kote wakati Bibi-arusi watakapokusanyika kandokando ya Meza zao ili kusikiliza Sauti ya Mungu ikinena nao. Nyumba zetu na makanisa yetu yatajazwa na uwepo wake. Tutaduwaa isipokuwa Utukufu, Haleluya zetu, jina la Bwana lihimidiwe.

Njoo uwe sehemu ya Kukusanyika huku kwa Familia ya Bibi-arusi kutoa Shukrani, anapotulisha. Usichelewe, kwani tutaanza kusherehekea Jumapili, saa 06:00 SITA kamili MCHANA , saa za Jeffersonville. ( ni Saa 1:00 MOJA kamili JIONI ya Tanzania na Kenya pia ) Kwa maana aliniambia angekuwepo.

NAKUJA na nitakuwa nikiwaambia yote kuhusu Muungano wenu Usioonekana wa Bibi-arusi wa Kristo 65-1125.

Nitawaoneni Pale Mezani.

Ndugu. Joseph Branham

AKA: Bibi Mteule Wake

23-0319 Kuchagua Bibi-Arusi

Ujumbe: 65-0429e Kuchagua Bibi-Arusi

PDF

pakua – m4a

pakua – amr

BranhamTabernacle.org

Mpendwa, Mmoja Katika Milioni Moja,

Nimekuwa nikikusubiri kwa muda mrefu sana. Wewe ni Kipenzi changu wa moyo, na ninakupenda sana. Kama nilivyokuahidi, nimekuwa nikikutengenezea Makao mapya ambapo tutaishi pamoja katika Milele yote. Nimeweka kila kitu jinsi kabisa unavyovipenda.

Sasa Ninaweza kukutazama na kuona, wewe ni picha halisi yangu mimi . Una tabia Yangu hasa, Mwili Wangu, Mifupa Yangu, Roho Wangu yeye yule, kila kitu Changu jinsi ile ile , sawa kabisa. Umekuwa mmoja na Mimi.

Nilimtuma malaika Wangu mwenye nguvu duniani kukuita wewe kutoka katika Edeni ya Shetani. Nilimtuma ili aweze kueleza mawazo Yangu, sifa Zangu, na kuwaambia kuhusu mambo yajayo. Nilitumia kinywa chake na sauti yake kujieleza. Baada ya yeye kuyasema, naliyatimiza, kwa maana Mbingu na nchi zitapita, bali Neno Langu kwenu halitashindwa kamwe.

Nilijua uliponisikia nikizungumza, kwa kutumia sauti ya malaika Wangu, ungejua ndani kabisa ya moyo wako, huyo hakuwa yeye, ilikuwa ni Mimi nikizungumza nawe. Ilikuwa ni Mimi nikikutumia barua ya mapenzi, nikikuambia, Nimekuchagua kuwa Bibi-arusi Wangu kipenzi.

Machoni Mwangu, hakuna aliye kama wewe. Hakuna anayeweza kupachukua mahali pako. Umebaki mkweli na mwaminifu Kwangu. Ninapokutazama, Moyo Wangu unachangamka kwa furaha.

Wakati Nilipokuambia, kuwa mwangalifu sana kipenzi , kile unachosikiliza, kutakuwa na wapakwa mafuta wengi wanaotumia Maneno Yangu, lakini ni wa uwongo. Nawe ulielewa onyo Langu kwa Ufunuo na ukakaa mkweli na mwaminifu kwa Sauti Yangu.

Nilijisikia vizuri sana mlipoomba kwa bidii kuhusu ni kanisa la aina gani mnaloshiriki. Niliwaambia mfanye chaguo sahihi, na nikawapa mifano ya jinsi kanisa kamilifu lilivyo. Mlikumbuka niliposema hayo huwa yana roho, na mchague kanisa kamilifu.

Hata niliwaambia kuwa wangalifu sana ni nani aliye mchungaji wako. Kwa hiyo mnaweza kufikiria jinsi moyo Wangu ulivyoruka kwa furaha nilipowaona mmekaa na mchungaji Niliyemtuma kuwaleta ninyi Kwangu. Mlijua ni Roho Wangu Mtakatifu akiishi ndani ya nabii Wangu kuwaongoza ninyi Kwangu.

Nakumbuka siku mliyokuwa na furaha sana, na kuchangamshwa kweli, wakati nilipomwita malaika Wangu mahali pa juu ili niweze kumwonyesha ninyi mkikaguliwa Kimbele . Tulikuwa tumesimama hapo tukiwatazama mkipiga hatua taratibu ya Twendeni Askari wa Kristo mbele Yetu.

Alipenda jinsi nyote mlivyokuwa mmevalia vazi lenu la taifa mlikotoka ; kama Uswisi , Ujerumani, na kutoka kote ulimwenguni. Kila mmoja mkiwa na nywele zenu ndefu zilizotengenezwa vizuri. Sketi zenu zilikuwa ndefu nadhifu. Nilijisikia vizuri na kufurahi sana kuwaonyesha ninyi nyote kwake, ili aweze kurudi na kuwatia moyo na kuwaambia aliwaona Kule.

Kila jicho lilitutazama Sisi. Wakati wasichana wachache, nyuma ya mstari, walianza kuangalia huku na huko mahali pengine, yeye alipiga kelele , “Msifanye hivyo! Msiache hatua hizo!”

Wakati Nilipowaambia Ninawahifadhia chakula ninyi mpate kula, mlijua kabisa nilichokuwa nazungumzia. Mlitaka kuwa Bibi-arusi-Neno Bikira Wangu . Sijawahi kuwapata mkitaniana na mtu mwingine yeyote. Daima imekuwa ni Mimi, Neno Langu. Hilo lilinifurahisha sana Mimi.

Nimewachagua , NINYI , kuwa Bibi-arusi Wangu. Ninawapenda sana, kama vile ninyi mnavyonipenda Mimi. Msivunjike moyo, jipeni ​​moyo, iweni wenye furaha , Shangilieni, siku ile inakaribia upesi nitakapokuja kuwachukua. Ni Wakati mzuri vipi Tutakaokuwa nao .

Ninyi Wengine, TUBUNI, dunia inanguruma. Siku moja Los Angeles itazama chini ya bahari, Kama vile nilivyowaambia ingekuwa. Ghadhabu yangu inakokomoa papa hapa chini yake. Sitazuia ufuko huo muda zaidi tena. Utatiririka ndani ya bahari kina cha maili moja, kote kote mpaka kwenye Bahari ya Salton. Itakuwa mbaya zaidi kuliko siku ya mwisho wa Pompeii.

Naenda kuisafisha dunia hii kwa moto hivi karibuni. Nitaua kila kitu Kilicho juu yake na chini yake. Mnayaona yale yanayoendelea ulimwenguni kote, kama nilivyowaambia. Mnamwona Bibi-arusi Wangu akiungana pamoja kulizunguka Neno Langu, kama vile nilivyowaambia.

Sasa huu ndiyo wakati Wenyewe . Sasa haya ndiyo majira yenyewe. Jiandaeni!

Ile saa ya ghadhabu Yake iko juu ya nchi. Kimbieni wakati kungali na wakati wa kukimbia, na mwingie ndani ya Kristo.


Mmealikwa kuja kuungana nasi, sehemu ya Bibi-arusi Wake, tunapojiweka wenyewe tayari kwa ajili ya Kuja Kwake, kwa kusikia Sauti ya Mungu ikisema nasi na kutuletea Ujumbe: Kuchagua Bibi-arusi 65-0429E Jumapili hii saa 06:00 SITA MCHANA saa za Jeffersonville.( Ni saa 1:00 MOJA JIONI ya Tanzania na Kenya pia )

Ndugu. Joseph Branham

Maandiko ya Kusoma Kabla ya Kusikiliza Ujumbe :

Mwanzo 24:12-14
Isaya 53:2
Ufunuo 21:9