23-0430 Wakati Wa Kanisa La Efeso

Ujume: 60-1205 Wakati Wa Kanisa La Efeso

PDF

pakua – m4a

pakua – amr

BranhamTabernacle.org

Mpendwa Dhahabu Safi Iliyofuliwa,

Jinsi gani Ninavyoshukuru kuungana pamoja na kila mmoja wenu, tukiingia katika Roho na kumsikiliza Mungu akizungumza nasi, mdomo kwa sikio. Hakuna mwisho kwa kile anachotufunulia. Mioyo yetu imejaa furaha. Nafsi zetu zinabubujika. Anawezaje mtu kuelewa kile tunachosikia?

Sikilizeni tu kile Bwana Mwenyewe anachotuambia: “Ninyi ndio Kanisa Langu la kweli, Bibi-arusi Wangu. Kwangu mimi, mmefananishwa na dhahabu SAFI. Haki yenu ni haki yangu. Sifa zenu ni sifa ZANGU mwenyewe tukufu. Utambulisho wenu wenyewe unapatikana ndani Yangu. Kile MIMI NIKO, mnakihakisi. Kile NILICHO NACHO, mnakidhihirisha.

KWANGU mimi, hakuna kosa ndani yenu, ninyi ni watukufu ndani na nje. Tangu mwanzo hadi mwisho, ninyi ni kazi Yangu…na kazi ZANGU zote ni kamilifu.

Hamtasimama kamwe hukumuni, kwa sababu dhambi haiwezi kuhesabiwa kwenu. Hata kabla ya misingi ya dunia, kusudi Langu lilikuwa ni kushiriki Uzima Wangu wa Milele pamoja NANYI.

Je, mtu anawezaje kufahamu Maneno haya? Akili zetu zinawezaje kufahamu kile kinachotendeka? Ni nini kimefunuliwa? Wazia jambo hilo, hatupaswi kulia mioyoni mwetu na kusema, “Loo, laiti ningalikuwa kule nyuma katika wakati wa kwanza wakati mitume walipotumwa kwanza.” HAKUNA haja ya sisi kuangalia nyuma, kwa sababu Yeye, ambaye habadiliki kamwe katika tabia au katika njia zake, Yeye yuko katikati yetu SASA, akizungumza nasi na kutuambia kuwa Yeye ni yeye yule jana, leo na hata milele. Huu ni wakati MKUU zaidi katika historia ya ulimwengu kuishi ndani yake.

Tunapigwa na kutakaswa, na kujazwa na mateso ambayo Kristo aliacha. Tunahesabiwa kama kondoo wa kuchinjwa. Tunauawa siku nzima. Tunateseka sana, lakini katika hayo yote, hatulipizi kisasi, wala hatusababishi wengine wateseke. Kwake, sisi ni dhahabu safi iliyofuliwa, sio kukunjwa, sio kuvunjwa, sio kuharibiwa, bali kufanywa kitu chenye uzuri na furaha milele kwa majaribu na majaribio ya maisha haya.

Sasa Yeye anawaonya wengine wote, “Rudini kwenye Upendo wenu wa Kwanza”. Jinsi gani Wanavyopaswa kuwa waangalifu kwani hupaswi kubadilisha HATA NENO MOJA, hata nukta au dashi. Hiyo ilikuwa ndio hila ya asili ya Shetani katika bustani ya Edeni. Neno moja tu likiongezwa, Neno moja tu likiondolewa, basi ni Mpinga-Neno.

Katika wakati huu wa mwisho anatuonya kutakuwa na manabii wengi wa uongo watakaotokea, wakiwaambia watu ya kwamba wasipowaamini wao na yale wanayosema , mtapotea.

KUNA NJIA MOJA PEKEE ya kuwa na Hakika HAKUNA KITU Kilichoongezwa, hakuna kilichoondolewa, hakuna kilichobadilishwa… kwa kusikiliza SAUTI YA MUNGU safi…KUBONYEZA PLAY.

Mshukuru Bwana kwa ajili ya mhudumu wa kweli, aliyefundishwa kwa uaminifu, ambaye si tu anawaambia kondoo wao umuhimu wa kusikiliza Ujumbe kila siku majumbani mwao, bali kwa kuwa viongozi wa kweli, kuweka Ujumbe Huu, Sauti Hii, Kanda Hizi, NAFASI YA KWANZA NA ILIYO YA KWANZA KABISA kwa watu walio katika makanisa yao.

Kwa kusema mambo haya, naeleweka vibaya na ninatuhumiwa kwa kuyagawa makanisa na kuwaambia watu wasiende makanisani. Hiyo si kweli. NENO linawatoa watu kutoka katika makanisa haya ambayo hayaweki kanda NAFASI YA KWANZA katika makanisa yao. Wana njaa ya kusikia Neno kutoka kwa Nabii wa Mungu. Wanajisikia HUO ndio Ujumbe na Sauti iliyo muhimu zaidi wanayotaka kusikiliza. Wanajisikia Ni Mapenzi Makamilifu ya Mungu kuzicheza kanda kanisani mwao.

Daima nimewaambia watu, “NENDENI KANISANI”. Wanapouliza: “Je, unahisi wahubiri bado wanaweza kuhubiri?” “Ndiyo.” Sijawahi kusema ama kuwazia kwamba hawapaswi. Kwa urahisi Ninawaambia wahubiri, waalimu, wachungaji, “Fanyeni kile Mungu alichowaitia, LAKINI TAFADHALINI, iwekeni hiyo Sauti yenyewe ya Mungu iliyo kwenye Kanda NAFASI YA KWANZA, SI HUDUMA YENU”.

Huo ndio UFUNUO WANGU. Wao yawabidi wafanye vile WANAVYOJISIKIA KUONGOZWA KUFANYA. Nina haki ya kuhubiri na kufundisha kile ninachojisikia. Kama Wao wanataka kusema Ndugu Branham kamwe hakuwahi kusema Kubonyeza Play Kanisani, Sauti yenyewe hasa ya Mungu wanayodai kuwa wanaifuata, hiyo ni juu yao.

Roho Mtakatifu ndiye, na daima amekuwa, akimwongoza Bibi-arusi Wake. Tunaamini Yeye anatuambia, “BONYEZENI PLAY, KAENI NA NABII WANGU, SAUTI YANGU, ROHO WANGU MTAKATIFU.”

Vema, tutakuwa na mashindano ya jambo hilo, basi, kama nabii Eliya kabla ya hapo . Na iwapo wewe ni mwana wa Mungu, utakaa pamoja na nabii wa Biblia hii. Ni Neno. Angalia ile saa, huo wakati.

Nabii wa Biblia ni nani, Neno, Roho Mtakatifu!

Roho Mtakatifu ndiye Nabii wa wakati huu; Yeye analihakikisha Neno Lake, akilithibitisha . Roho Mtakatifu alikuwa ndiye Nabii wa wakati wa Musa. Roho Mtakatifu alikuwa Nabii wa wakati wa Mikaya. Roho Mtakatifu, aliyeliandika Neno, anakuja na kulithibitisha Neno.

Roho Mtakatifu wa wakati huu anatuongoza Kupitia nabii Wake, kama jinsi alivyofanya katika kila wakati. Mungu kamwe habadilishi mpango Wake.

Kwa hiyo, unaalikwa kuja kuungana nasi katika kile tunachojisikia kuwa ndio Mpango wa Mungu kwa kumsikiliza Roho Mtakatifu akizungumza kupitia nabii Wake, na kutuongoza anapotuletea Ujumbe: 
Wakati Wa Kanisa La Efeso 60-1205 , saa 6:00 SITA MCHANA. Masaa ya Jeffersonville. ( ni saa 1:00 MOJA JIONI ya Tanzania na Kenya pia .)

Ndugu. Joseph Branham

Maandiko ya kusoma Kwa ajili ya maandalizi ya Kusikiliza Ujumbe :

Matendo 20:27-30
Ufunuo 2:1-7