23-0507 Wakati Wa Kanisa La Smirna

Ujume: 60-1206 Wakati Wa Kanisa La Smirna

PDF

pakua – m4a

pakua – amr

BranhamTabernacle.org

Wapendwa Waamini Wa Kweli,

Sisi ni kama wana wa Israeli waliotoka Misri na wakakoma karibu na Nchi ya Ahadi. Sote tumesafiri pamoja. Sote tumeona miujiza ile ile ya Mungu; sote tumeshiriki mana ile ile na maji kutoka kwenye Mwamba uliopigwa. Sote  tumedai kuwa tunafuata Nguzo ya Moto. Lakini WAWILI TU ndio waliofika kwenye Nchi ya Ahadi wakati huo. Kwa nini? WAWILI TU NDIO WALIOKUWA WA KWELI AMA WAAMINI HALISI. Tofauti ilikuwa ni kitu gani kati ya wakati huo na sasa? Waamini wa kweli walidumu na Neno.

Kuna kundi moja tu maalum sana la watu ambao wanaweza kusikia yale Roho anayosema. Kundi moja maalum linalopokea Ufunuo wa kweli. Kundi hilo ni la Mungu. Wanasikia yale Roho anayosema na wameyapokea.

Sisi ndio kundi hilo maalum ambalo lina Roho wa Mungu. Sisi ndio tuliozaliwa na Mungu. Sisi ndio tuliobatizwa katika mwili wa Bwana Yesu Kristo kwa Roho Wake.

Ushuhuda wa kweli ni KUSIKIA Yale Roho asemayo. Roho ananena. Roho anafundisha. Hivyo ndivyo hasa Yesu alivyosema angefanya atakapokuja. Yohana 14:26, “Naye atawafundisha yote, na kuwakumbusha yote niliyowaambia.”

Yesu alituahidi kwamba angekua akiishi ndani ya kila mmoja wetu. Angetuongoza, kutusimamia na kutuelekeza kama watu binafsi. Lakini miaka 72 iliyopita leo, Mungu alinena kupitia malaika Wake mwenye nguvu na kuutangazia ulimwengu, “Mimi ni Sauti ya Mungu kwenu”. Aliambia kila kiumbe hai “Mimi, Roho Mtakatifu, nina SAUTI nitakayoitumia kusema nanyi na kuzifunua siri zangu zote”. Hakuwahi kamwe kupata nafasi ya Sauti Yake kurekodiwa ili tuweze kusikia Sauti Yake ikituzungumzia mdomo kwa sikio.

Kwa kusikia Sauti yake kwenye hizo kanda haitakubidi kushangaa, kutumaini, au hata kuomba kujua ikiwa kile unachosikia kama ni kweli. KILA mtu anachopaswa kufanya ni Kubonyeza Play, nao wanaweza kusikia Sauti ya Mungu ikiwatangazia, “Bwana Asema hivi”.

Je, unahitaji uponyaji: Bonyeza Play.
Unahitaji kuolewa: Bonyeza Play.
Unahitaji kuzikwa: Bonyeza Play.
Una swali moyoni mwako: Bonyeza Play. Una jambo unalopitia na unahitaji ushauri nasaha: Bonyeza Play.
Una uamuzi muhimu unaohitaji kufanya: Bonyeza Play.
Hujui ufanye nini na maisha yako: Bonyeza Play na usikilize Sauti ya Mungu, Roho Mtakatifu, aseme nawe mdomo kwa sikio.

Roho Mtakatifu ndiye nabii wa wakati huu. Aliuambia ulimwengu, hii ndiyo Sauti Niliyoichagua tangu asili iwe Sauti Yangu kwenu. Nitawajaza wengine na Roho wangu Mtakatifu, nami Nimewatuma kuwasaidia, Lakini Mimi Nina Sauti Moja tu ninayotangaza kuwa SAUTI YANGU. Hata nimepiga picha yangu pamoja naye ili kuuthibitishia ulimwengu, Msikieni Yeye.

Tafadhali msinielewe vibaya. Ndiyo, kuna watu wa Mungu waliojazwa na Roho Mtakatifu ambao amewaita kuwasaidia watoto Wake. Naomba ya kuwa mimi ni mmoja wao. Wao pia wanaweza kuwapa ushauri, faraja, na kuwaongoza katika safari ya maishani. Mungu amewaweka hapa kwa kusudi. Lakini ushauri uliyo MUHIMU zaidi, faraja na uongozi unaoweza kupokea ni Sauti ya Mungu ikizungumza nawe kwa Kubonyeza Play. Chochote ninachowaambia, ama mtu mwingine ye yote, lazima kwanza kitoke kwenye Sauti ya Mungu iliyo kwenye kanda.

Hakuna kitu kilicho muhimu zaidi katika maisha yako, kuliko kusikiliza Sauti ya Mungu ikisema nawe. Jiulize, je, kuna jambo lolote katika ulimwengu huu KUBWA ZAIDI ningaliweza kufanya, au ni muhimu zaidi katika maisha yangu, kuliko kusikiliza SAUTI ya Mungu iliyothibitishwa? Je, ni Kumsikiliza ndugu Joseph, HAPANA. Je, ni Kumsikiliza mtu mwingine yeyote, HAPANA. Hakuna CHOCHOTE KILICHO KIKUBWA ZAIDI YA SAUTI HIYO.

Ikiwa mtu yeyote ana Ufunuo wowote na wanaye Roho Mtakatifu katika maisha yao wanapaswa kusema AMINA. Hakuna kitu chochote kikubwa zaidi katika ulimwengu huu kuliko Kubonyeza Play .

Tunapaswa kuwa waangalifu jinsi gani katika wakati huu wa mwisho kukaa na Neno hilo. Kuanzia maneno ya papa, anayedai kuwa Halifa wa Mungu, hadi kubadilisha nukta moja ama deshi ya kile kilichonenwa. Machoni pa Mungu, WOTE ni UPINGA-NENO, UPINGA-KRISTO.

Sisi hatutaki kuwa kama watu wa siku za Samweli.

Wakati walipomwendea Samweli na kuomba wapewe mfalme, Samweli alifadhaika sana hata roho yake karibu izimie. Mungu alikuwa anawaongoza watu Wake kupitia kwa nabii huyu aliyewekwa wakfu, aliyethibitishwa kwa Maandiko naye akaona kwamba alikuwa amekataliwa…

Tunaifurahia miujiza, hekima, chakula na ulinzi wa Mungu. Tunauamini. Tunaupenda. Na isitoshe hatutaki kuukosa. Ni kwamba tu tanataka mfalme wa kutuongoza vitani…

“…TUNATAKA MFALME AMBAYE NI MMOJA WETU APATE KUTUONGOZA.”

Ndipo Mungu akamwambia Samweli. “Unaona, wao hawakukukataa wewe, lakini wamenikataa MIMI nisiwatawale.”

Kinyume Chake, sisi tunajisikia kama vile Elisha wakati akizungumza na Eliya. Eliya ALIMWAMBIA WAZIWAZI, (leo ingekuwa Kile alichosema kwenye kanda,) wewe kaa hapa niendapo. Elisha hangefanya hivyo, na hangeweza kufanya hivyo, alikuwa na UFUNUO wa Neno la Wakati Wake.

Sasa, tunawaona wakiendelea na safari, kuja shuleni. Naye akasema, “Kaa hapa sasa. Kuwa hapa, na utulie uwe mwalimu mzuri wa theolojia, na kadhalika. Na pengine, siku moja, unaweza kuwa mkuu wa chuo hapa. Lakini sina budi kushuka kwenda mbele kidogo.”

57 Unaweza kumwazia mtu wa Mungu akiridhika kuwa mkuu wa chuo, wakati Nguvu za Mungu zikiwa pale pale alipokuwa amesimama? La, bwana. Akasema, “Kama Bwana aishivyo na roho yako iishivyo, sitakuacha.” Napenda hilo.

Kaa nalo, haidhuru umeshushwa moyo kiasi gani, hata kama inatoka kwa mama yako, baba yako, au kutoka kwa mchungaji wako. Kaa Naye.

Kama Bwana aishivyo, nitakaa na Sauti ya Mungu kwa Kubonyeza Play, kwa maana ni Bwana Asema Hivi Kwangu.

Njoo uungane na kundi letu, Jumapili saa 06:00 SITA MCHANA, saa za Jeffersonville, (Ni saa 1:00 MOJA JIONI Ya Tanzania na Kenya pia)tunapokusanyika ili kuisikia Sauti Yake ikizungumza nasi na kutuletea Ufunuo wa: Wakati wa Kanisa la Smirna 60-1206.

Ndugu. Joseph Branham

Maandiko ya Kusoma kabla ya Kusikiliza Ujumbe :

Ufunuo 2:8-11