23-0514 Wakati Wa Kanisa La Pergamo

Ujume: 60-1207 Wakati Wa Kanisa La Pergamo

PDF

pakua – m4a

pakua – amr

BranhamTabernacle.org

Wapendwa watoto wa Nabii,

Sisi ni Neno lililodhihirishwa, tukitiwa nguvu na Roho, tukisikia Sauti ya Mungu, kama anavyotutangazia, sisi ni BIBI-ARUSI WAKE.

Baba amelipatia Kanisa lake karama TISA za Roho, na huduma-TANO, lakini Yesu alisema: Katika KILA wakati nitamwandikia mtu MMOJA TU. ni Mjumbe MMOJA tu kwa kila wakati atakayepokea yale ninayouambia wakati huo. MJUMBE HUYO MMOJA ndiye mjumbe wa Kanisa la kweli.

Yeye anazungumza kwa niaba ya Mungu kwa ufunuo. Ujumbe huo ndipo unatangazwa kwa wote, lakini unapokelewa tu na kundi fulani linalostahili kwa njia fulani. Kila mtu binfsi wa kundi hilo ni yule aliye na uwezo wa kusikia yale Roho anayosema kwa njia ya mjumbe huyo. Wale wanaosikia hawapati ufunuo wao wa Kipekee, wala kundi fulani halipati ufunuo wao wa pamoja, BALI KILA MTU ANASIKIA NA KUPOKEA AMBAYO HUYO MJUMBE AMEISHAPOKEA TAYARI KUTOKA KWA MUNGU.

Jinsi tunavyopaswa kuwa waangalifu kusikia sauti MOJA, kwa kuwa Roho hana ila sauti moja ambayo ni sauti ya Mungu.

Kuna SAUTI MOJA YA MUNGU nayo haihitaji kuthibitishwa kama zile TISA, wala kuchujwa kama zile TANO; ni SAUTI MOJA TU, NENO SAFI!!

Je, tunaweza kuwasikiliza wahudumu wengine? Ndiyo, lakini msingi ni kusema TU yale yaliyonenwa na nabii. Wengine wanaweza, na wanapaswa, kuhimiza, kufundisha na kuhubiri; lakini Mungu ametutengenezea njia leo ZAIDI YA SIKU NYINGINE YOYOTE. Tunaweza kusikia yale hasa Mungu anayoliambia Kanisa.

Yeye alituambia tunapaswa kuwa waangalifu sana. YEYE ALITUAMBIA, SI MIMI, ya kwamba wao wanaongeza hapa, ama wanaondoa pale, na mara ujumbe si Halisi tena. Wakati tunaposikiliza kanda, Ni Neno kwa Neno, Bwana Asema hivi.

Thibitisho la Roho akaaye ndani ya mtu lilikuwa ni kukubali na KUFUATA yale nabii wa Mungu aliyotangazia huo wakati wake akiliweka kanisa kwenye utaratibu.

Ndio maana TUNAFUATA, na kusema, mchungaji wetu ni malaika-mjumbe wa saba na tunataka tu kusikia yale yeye anayosema. Kwetu sisi, Ni Mana Iliyofichwa.

Ufunuo ulimwagwa juu ya malaika-mjumbe wetu. Ufunuo wa Neno ulitolewa na kuandikiwa YEYE kwa ajili ya wakati wetu. Yeye ana Ufunuo mkubwa zaidi kidogo wa kile Kristo Alicho; wito wa juu zaidi kidogo, kuliko wengine wote. Ikiwa hatuwezi kuishi juu zaidi ya mchungaji wetu, basi sisi tunamtaka William Marrion Branham kama mchungaji wetu.

Tunajua wengine hawataona yale tunayoona, na Hawataamini mambo tunayoamini, lakini bado ni ndugu na dada zetu, nasi tutaishi Milele nao. Lakini lazima tubaki waaminifu kwa kile tunachoamini kuwa ni njia ambayo Mungu ametuonyesha kumwabudu na kumfuata.

Ni vyepesi sana kwa wengine kusema tunamwinua sana mjumbe, lakini kwa kweli, tunamnukuu yeye tu. Yakubidi kumshutumu hilo Bwana. Kwa maana ni Sauti ya Mungu inayosema mambo haya.

Hebu na tufungue mioyo na akili zetu na tusome yale Roho aliyotuambia kupitia malaika Wake:

Anayekuja ulimwenguni hivi karibuni, yule malaika mkuu wa Nuru atakayetujia, atakayetuongoza tutoke, Roho Mtakatifu mkuu, akija mamlakani, naye atatuongoza kwa Bwana Yesu Kristo. Labda hatajua hilo, bali atakuwa hapa moja ya siku hizi. Atafanya…Mungu atamtambulisha. Haitambidi kujitambulisha mwenyewe, Mungu atamtambulisha. Mungu atamthibitisha aliye Wake. Hivyo ndivyo Yeye alivyosema wakati Yesu alipokuwa hapa wala hawakumtambua, mnaona. Alisema, “Nisipozitenda kazi za Baba Yangu, basi msiniamini; bali nikizitenda kazi za Baba Yangu, wala hamwezi kuniamini Mimi, basi ziaminini zile kazi.” Hiyo ni kweli?

Je, Yeye si anajiita malaika mkuu wa Nuru wa wakati huu? Tunajua ni Roho Mtakatifu ndani yake, lakini yeye alisema: Labda hatajua hilo, bali atakuwa hapa moja ya siku hizi. Roho Mtakatifu hatamjua Yeye ni nani? Haitambidi kujitambulisha mwenyewe; Mungu atamtambulisha.

Kwa hiyo Yeye anasema, nabii wa wakati wetu ndiye malaika mkuu wa Nuru atakayetuongoza tutoke na kwa Yesu Kristo kwa njia ya Roho Mtakatifu kupitia yeye. Huo hapo Ufunuo wa Wakati wetu.

Ni nani atakayemtambulisha Bibi-arusi kwa Bwana? MCHUNGAJI WETU.

Lakini huyu nabii atakuja, na kama vile yule mtangulizi wa kule kuja kwa kwanza alivyopaza sauti, “Tazama Mwana-Kondoo wa Mungu aichukuaye dhambi ya ulimwengu,” vivyo hivyo bila shaka naye atapaza sauti, “Tazama Mwana-Kondoo wa Mungu anayekuja katika utukufu.” Atafanya jambo hili, kwa maana kama vile Yohana alivyokuwa mjumbe wa ile kweli kwa wateule, ndivyo alivyo na huyu mjumbe wa mwisho kwa wateule na kwa bibi-arusi aliyezaliwa kwa Neno.

Kuzijua Kweli hizi, na kuwa na Ufunuo MKAMILIFU wa Yeye katika siku hii, tumekuwa Bibi-arusi Wake aliyezaliwa kwa Roho, aliyejazwa na Roho.

FURAHI BIBI-ARUSI, HUYU NDIYE SISI TULIYE!

Wakati mtu aliyezaliwa kwa Roho, aliyejazwa na Roho anapoingiza Neno hilo ndani ya moyo wake na kuliweka kwenye kinywa chake kwa imani, mbona hilo ni kama tu Mungu akinena. Kila mlima hauna budi kuondoka. Shetani hawezi kusimama mbele ya mtu huyo.

Sasa upatanifu mkamilifu wa kweli upo kati ya Bwana Arusi na sisi, Bibi-arusi Wake. Yeye ametuonyesha Neno Lake la uzima, nasi tumelipokea. Hatutalitilia shaka kamwe. Kwa hiyo, hakuna kitu kinachoweza kutudhuru, hata kifo chenyewe.

FURAHI BIBI-ARUSI, HUYU NDIYE SISI TULIYE!

Neno limo ndani ya bibi-arusi (kama vile lilivyokuwa ndani ya Mariamu). Bibi-arusi ana nia ya Kristo kwa kuwa anajua kile Yeye anachotaka kifanywe kwa Neno. Anatekeleza maagizo ya Neno katika jina Lake kwa kuwa yeye anayo “Bwana asema hivi.” Ndipo Neno linahuishwa na Roho nalo linatimia. Kama vile mbegu ambayo imepandwa na kumwagiwa maji, inafikia mavuno kamili, ikitimiza kusudi lake.

Tumefika kwenye mavuno kamili na sasa tunatimiza kusudi Lake. Sisi hufanya tu mapenzi yake. Hakuna ye yote anayeweza kutufanya tutende vinginevyo. Tuna “Bwana Asema hivi,” la sivyo tunanyamaza. Tunajua ya kwamba ni Mungu ndani yetu, akifanya kazi, akilitimiza Neno Lake Mwenyewe.

Tunashangilia, kwani nabii alituona ng’ambo ya pazia la wakati sote tulipoziinua sauti zetu na kupaza sauti kwa upatanifu, “Tunategemea hilo!”

Njoo ukusanyike pamoja nasi Jumapili saa 6:00 SITA MCHANA, saa za Jeffersonville, ( ni saa 1:00 MOJA JIONI ya Tanzania )tunaposikia Sauti ya Mungu ikituletea siri ya: Wakati wa Kanisa la Pergamo 60-1207.

Ndugu. Joseph Branham

Maandiko ya Kusoma kwa maandalizi ya Kusikiliza Ujumbe :

Hesabu 23:8-9
Ufunuo 2:12-17, 17:1-5, 17:15