23-0423 Ono La Patimo

Ujume: 60-1204E Ono La Patimo

PDF

pakua – m4a

pakua – amr

BranhamTabernacle.org

Wapendwa, Wapenzi Wa Neno la Mungu,

Inapendeza jinsi gani kuweza kuongea na kila mmoja wenu kama Wapenzi wa Neno la Mungu. Hakuna kitu kinachoweza kupachukua mahali Pake. Kuwa na nafasi ya kumsikiliza Bwana wetu kila siku ya maisha yetu, akisema nasi kupitia midomo ya mwanadamu, na kutuambia Yeye ni nani na SISI NI NANI. Hakuna mahali, hakuna sauti, hakuna kanisa, na hakuna mtu anayeweza kukuambia mambo haya kama SAUTI YA MUNGU.

Alituambia uvuvio wa Neno ulikuwa kwenye kanda. Yote tunayopaswa kufanya ni Kubonyeza Play na Roho Mtakatifu anakijaza chumba. Mjumbe wetu alikuwa akivuta Uzima, na nuru, kutoka kwenye rasilimali za bakuli hilo kuu. Utambi wake ulikuwa umezamishwa humo ndani.

Maisha yake yanawaka moto wa Roho Mtakatifu. Utambi wake (uhai) umezamishwa ndani ya Kristo. Kupitia huo utambi anaunyonya uzima ule ule wa Kristo, na kwa huo, anatupa mwangaza sisi, Bibi-arusi.

Kisha anatuambia sio tu kwamba utambi wa mjumbe Wake mwenye nguvu upo mle, bali sote tunanyonya kutoka kwenye chanzo kimoja. Sote tumetumbukizwa kwenye bakuli moja. Tumekufa kwa nafsi zetu na uhai wetu umefichwa katika Mungu kwa njia ya Kristo, umetiwa muhuri na Roho Mtakatifu.

Hakuna mtu anayeweza kututoa kutoka kwenye mkono Wake. Maisha yetu hayawezi kuchezewa. Uhai unaoonekana unawaka na kuangaza ndani yetu, ukitoa nuru na madhihirisho ya Roho Mtakatifu. Maisha yetu ya ndani, yasiyoonekana yamefichwa ndani ya Mungu na kulishwa kwa Neno la Bwana. Tunao Ufunuo wa Yesu Kristo katika siku yetu.

Jinsi gani Neno linavyolisha nafsi zetu. Hakuna lakulinganishwa nalo. Jinsi gani ameandaa njia ambayo Bibi-arusi, kutoka ulimwenguni kote, wanaweza kukusanyika pamoja ili kusikia Sauti ya Mungu kwa wakati mmoja. Haijalishi wakosoaji ama wanaoshuku wanasema nini, Mungu ametengeneza njia na ni harufu nzuri ya manukato Kwake. Ndio kwanza Atuambie kwamba atatukusanya pamoja sote mwishoni mwa siku ya tatu. Utukufu!!

Hebu sote na tukusanyike pamoja Jumapili hii saa 06:00 SITA MCHANA , saa za Jeffersonville,( ni saa 1:00 MOJA JIONI Ya Tanzania)kusikia Sauti ya Mungu ikituletea Ufunuo wa Neno tunaposikia: Ono la Patmo 60-1204E.

Kwanza, ni lazima TUINGIE KATIKA ROHO kama tutakavyosikia;

Ile sauti iliyotangaza Neno Lake katika Bustani ya Edeni na juu ya Mlima Sinai, sauti ambayo ilisikika pia katika utukufu mkuu wa Mlima wa Kugeuzwa Sura, ilikuwa inatangaza mara nyingine tena, na wakati huu kwa yale makanisa saba pamoja na ufunuo mkamilifu na wa mwisho wa Yesu Kristo.

Ndugu. Joseph Branham

Maandiko ya kusoma ili kujitayarisha Kusikiliza Ujumbe.

Kumbuka kusoma na kusikiliza kitabu cha Nyakati Saba za Kanisa.

Isaya 28:8-12
Danieli 7:8-14
Zekaria 4:1-6
Malaki 4:1-2, 4:5
Mathayo 11:28-29, 17:1-2
Yohana 5:22
Waebrania 4:3-4, 4:7-10, 4:12
Ufunuo 1:9-20, 19:11-15