23-0416 Ufunuo Wa Yesu Kristo

Ujume: 60-1204M Ufunuo Wa Yesu Kristo

PDF

pakua – m4a

pakua – amr

BranhamTabernacle.org

Mpendwa mti wa bibi-arusi,

Ni yubile iliyoje aliyonayo Mti wa Bibi-arusi. Mioyo na roho zetu zinawaka ndani yetu kuliko hapo awali. Anatembea na kuzungumza nasi, akifunua Neno Lake. Mambo yanatokea haraka sana hatuwezi kuendana nayo.

Tunalisikia Neno kamilifu la Mungu likidhihirishwa na Mti mkamilifu wa Nabii, ukihubiri Neno kamilifu la Nabii, likizaa tunda kamilifu la Nabii, kwa Neno kamilifu la Mungu.

Kila kitu kilichoharibiwa na kuliwa na wale wajumbe wanne wa mauti walioua Mti, sasa kimerudishwa tena na wajumbe wanne wa Uzima. Si wajumbe WATANO, si wajumbe wa huduma tano, si kundi; WAJUMBE wanne ndio wameurudisha Mti wa Bibi-arusi.

Tangu mwanzo wa wakati, Mungu amengojea siku na majira haya yatimie ili aweze kuliona tunda lake, katika wakati Wake, kwa majira ya nabii. Sisi ndio Tunda hilo. Haya ndio majira yenyewe. Wakati wa mavuno umefika.

Wikiendi hii ya Pasaka ilikuwa kama hakuna Pasaka nyingine ambayo mtu yeyote amewahi kuiona. Hatutakuwa kamwe jinsi tulivyokuwa. Uwepo kama huo wa Bwana. Nilikuwa nikingojea Unyakuo kufanyika sekunde yoyote.

Katika Biblia, Daudi alisema Maneno haya: Walinizua mikono na miguu yangu. Naweza kuihesabu mifupa yangu yote: Wao wanitazama na kunikodolea macho.

Watu walikuwa wamesoma na kusikia kifungu hicho kwa mamia ya miaka, lakini Yesu alipokuwa akining’inia pale mbele ya macho yao msalabani, Bibi-arusi lazima yawezakuwa alimtazama na kutambua, Leo, Maandiko Haya Yametimia mbele ya macho yetu.

Jinsi ambavyo lazima walijisikia walipotambua kwamba walikuwa wanaona, kwa macho yao, Maandiko hayo yakitimizwa, na walikuwa sehemu ya Neno lililoandikwa.

Ndio sisi SASA. Tunaishi katika siku ambazo Maandiko yote ya mwisho yanatimizwa mbele ya macho yetu; na sisi ni sehemu ya Maandiko hayo.

Yeye anatembea moja kwa moja kati yetu. Ni mwisho wa siku ya tatu. Ametokea na kutuonyesha ishara ya kufufuka kwake. Ni yeye yule jana, leo, na hata milele. Sisi ni matunda hai ya Uwepo Wake. Amedhihirishwa na anaonekana kwetu sote, Kanisa Lake.

YEYE ANALIFANYAJE JAMBO HILO?

Nabii ameondolewa kutoka katika dunia hii, Lakini Roho Mtakatifu yuko kwenye kanda, naye anaenda kwenye mataifa na ulimwenguni kote. NI HUDUMA HAI YA BWANA YESU KRISTO. Anamkusanya Bibi-arusi Wake wote pamoja kwa jambo moja pekee linaloweza, na litakalofanya hivyo: Neno Lake. Sauti yake. KUBONYEZA PLAY!

Leo, Maandiko haya Yametimia.

Yeye ndiye Mti wa Bwana-arusi kutoka katika Bustani ya Edeni. Lakini Mti wa Bwana-arusi bila wakike, hauwezi kuzaa matunda; Hana budi kuwa na Mti wa Bibi-arusi. Huyo ni WEWE. Mlizaliwa kwa kitu kile kile. Neno limefanyika mwili ndani YENU. Maisha yale yale yaliyo ndani ya Bwana-arusi yako sasa hivi ndani YENU.

Bibi-arusi anapaza sauti: Haleluya, Amina, Utukufu!!

Je, ni mambo gani aliyotuwekea akiba hapo mbele?

Lakini sababu ya wakati huu maalum ilikuwa ni kwamba tungeninii…Juu ya moyo wangu Roho Mtakatifu alikuwa ameweka ilani hii ya kusadiki, kwamba, “Kanisa katika siku hizi linapaswa kupata Ujumbe huu.” Kwa sababu, ninaamini ya kwamba ndio Ujumbe ulio muhimu sana wa Biblia, kwa sababu unamfunua Kristo katika Kanisa Lake kwenye wakati huu.

Kwa hiyo, Bibi-arusi atakuwa anakusanyika Jumapili hii saa 06:00 SITA MCHANA , saa za Jeffersonville ,(Ni saa 1:00 MOJA JIONI ya Tanzania ) tunaposikia: Ufunuo Wa Yesu Kristo 60-1204M.

Ningependa kuwahimiza msikie, au kusoma, kila wiki katika Kitabu cha Nyakati za Kanisa, sura ambayo tumesikia kila Jumapili. Tutakuwa tukichapisha audio kwa Kiingereza kwenye Lifeline – Redio ya Sauti kila siku kwa nyakati tofauti, lakini jisikie huru kukisoma, kukisiklizia na kukisoma wiki nzima wakati wowote.

Hebu na tushangilie na kufurahi. Msiukazie ulimwengu huu na dhambi na fadhaa zinazotuzunguka pande zote. Hebu tusherehekee kwa yote anayotufanyia kila siku.

Katika siku za Musa, nina hakika watu waliendelea kumuuliza Musa,
“Tutaondoka lini mahali hapa? Tutatoka lini hapa?”

Naweza tu kumsikia Musa akiwatuliza watu na kusema:

“Mungu akiwa tayari. Lakini kwa sasa, furahieni yote anayowafanyia NINYI”.

Je! Mna vyura nyumbani mwenu? HAPANA.
Je! Mna nzige zilazo mimea yenu? HAPANA
Je! Mna maji ya kunywa yenye damu? HAPANA. Mnakunywa maji safi ya kisima kinachobubujika. Ninyi kaeni kitako tu na mfurahie yote Anayofanya na kuwafunulia.

Ni kifo, maangamizi na hukumu kwao. Lakini kwako wewe, hizi ni siku zilizo kuu zaidi duniani. Kuwa mwenye furaha, amani na shangwe. Msifu tu Bwana kwa yote anayofanya, na utarajie yale atakayofanya hapo mbele.

Ndugu. Joseph Branham