23-0611 Wale Wanawali Kumi, Na Wayahudi Mia Na Arobaini Na Nne Elfu

Ujume: 60-1211M Wale Wanawali Kumi, Na Wayahudi Mia Na Arobaini Na Nne Elfu

PDF

pakua – mp3

pakua – amr

BranhamTabernacle.org

Wapendwa, Wapendao Mana,

Tuna furaha kwa sababu kwamba tunaweza kula Chakula kisicho na mfupa wala mbegu ndani yake. Mikate myembamba ilishuka kutoka Mbinguni, iitwayo “Mana,” inafunika kila mahali kwa utamu wa Mbinguni.

Kwa Ufunuo wa Kiroho, Yeye ametufunulia kuna mahali pamoja tu tunaweza kupata hii Mana Safi isiyo na mbegu: kwa kuisikia Sauti ya Mungu aliyoiandaa kwa ajili ya Bibi-arusi Wake.

Ni ombi lake la daima katika kila wakati kwamba makanisa waisikie Sauti ya Bwana. Katika Wakati huu wa mwisho, ombi Lake ni la nguvu zaidi kuliko wakati mwingine wo wote ; kwa maana hii ndio siku ya Kuja kwa Bwana. Ametuonya, kwa dharura yote, kwamba hatuna budi kuisikia Sauti Yake ya kweli, iliyothibitishwa.

Loo! kuna sauti nyingi sana ulimwenguni—shida nyingi sana na mahitaji yanapaza sauti yapate kushughulikiwa; lakini kamwe hakutakuweko na sauti iliyo muhimu sana na inayostahili kushughulikiwa kama sauti ya Roho. Kwa hiyo, “Yeye aliye na sikio la kusikia, na alisikie Neno hili ambalo Roho ayaambia makanisa.”

Hilo hapo, onyo lake kwa makanisa, jinsi gani ilivyo muhimu kusikia SAUTI ya Roho. Hakika hapo ndipo adui atakaposhambulia, akijaribu kuondoa kwa watu umuhimu wa kuisikia SAUTI HIYO.

Yeye anatuambia kuna SAUTI NYINGI. Kuna shida nyingi sana na mahitaji, yanapaza sauti yapate kushughulikiwa, lakini usisahau kamwe, lazima usikie SAUTI YAKE ILIYOTHIBITISHWA.

Ikiwa niliwahudhi kwa kusema hivyo, nisameheni, lakini, nilihisi yaweza kuwa huko ni kuchukizwa, lakini, mimi ni Sauti ya Mungu kwenu.

Hilo hapo jibu: MIMI NI SAUTI YA MUNGU KWENU.

Ni wazi sana kwa Bibi-arusi Wake. Halijafichwa, Liko papo hapo wazi kabisa; mtu yeyote anaweza kulisoma. Mimi Siwaambii watu jambo ambalo Yeye Hakusema… mimi silibuni jambo hili. Yeye anatuambia waziwazi ni jambo gani lililo muhimu zaidi tunalopaswa kufanya. Mapenzi makamilifu ya Mungu ni KUSIKIA SAUTI YAKE NA YEYE NDIYE SAUTI YA MUNGU KWETU.

Ndugu na dada, sisemi kuwa hamwezi kuwasikia wachungaji wenu. Sisemi kwamba ni wa uwongo ama ni makosa ikiwa watahudumu. Ni wazi Bwana ametuweka hapa ili tuwe msaada kwa Bibi-arusi na kuwaelekeza ninyi KURUDI kwenye Neno la asili; kuiweka Sauti hiyo mbele zenu kuwa iliyo muhimu zaidi mnayopaswa kuisikia. Tunatakiwa kurudi kwenye MAPENZI MAKAMILIFU YA MUNGU. Yule Adamu aliyerejeshwa kikamilifu, akilindwa na Neno. Mungu alinena kila siku na Adamu mdomo kwa sikio katika ile Bustani, na leo hii, Yeye Anafanya jambo lile lile.

Tunapaswa kuwa tukisimama katika pengo na kusema, “Sisi ni ndugu!” Hatujagawanyika, Sisi sote ni mwili mmoja; Mmoja katika tumaini na fundisho, (Fundisho la Biblia.)

Sisi ni ndugu. Mimi Sijaribu kuyagawanya Makanisa, ninajaribu kutuleta pamoja kwa jambo PEKEE linaloweza kumleta Bibi-arusi pamoja. Hatuwezi sote kukubaliana na MTU YOYOTE, AMA KUNDI LA WAHUDUMU; wote wametofautiana, na wanasema mambo yaliotofautiana. Kuna malaika-mjumbe wa saba MMOJA tu . Kuna Sauti ya Mungu MOJA tu . Sauti ambayo Mungu ameiandaa kwa ajili ya Bibi-arusi Wake kwenye kanda.

Nitakuwa wazi. Ufunuo wangu ni: Kusikiliza Sauti ya Mungu kwenye kanda NDIO MAPENZI MAKAMILIFU YA MUNGU.

Kama katika siku za Samweli, wakati watu walipomwendea na kumwambia walitaka mfalme wakuwatawala. Ilihuzunisha moyo wake. Alimwendea Mungu na kumwambia kile walichotaka. Mungu alimwambia Samweli, hawakukukataa wewe, Samweli, wamenikataa Mimi, ili Nisiwe mfalme juu yao .

Je, Yeye alikuwa akiwatawala namna gani? KWA NABII WAKE, SAMWELI. Hayo yalikuwa ndio MAPENZI YAKE MAKAMILIFU, nao wakamkataa. Ili uwe Bibi-arusi Wake ni lazima Urudi kwenye Mapenzi Makamilifu ya Mungu. Huwezi kuwa na MAPENZI MAKAMILIFU 2.

Jinsi gani ningependa Bibi-arusi wote wakusanyike pamoja kutoka ulimwenguni kote ili kusikia Sauti ya Mungu wote kwa wakati mmoja. Si kwa sababu “Mimi” nasema hilo, bali kwa sababu Mungu ANAFANYA HIVYO. Ndilo jambo pekee la kumkusanya Bibi-arusi Wake pamoja.

Ninakualika uje kusikiliza pamoja na sehemu ya Bibi-arusi, Jumapili saa 06:00 SITA MCHANA, saa za Jeffersonville( Ni saa 1:00 MOJA JIONI ya Afrika Mashariki), kusikia: Wale Wanawali Kumi, Na Wayahudi Mia Na Arobaini na Nne Elfu 60-1211M.

Ikiwa huwezi kuungana nasi, mtie moyo mchungaji wako msikilize Sauti ya Mungu Jumapili hii asubuhi kanisani mwenu. Je! Waweza kuwazia, Bibi-arusi kote ulimwenguni, katika kila kanisa, kila nyumba, ama popote ulipo, wakisikia Mana Mpya ikifunika kila mahali kwa utamu wa Mbinguni.

Ndugu. Joseph Branham