23-0618 Wakati wa Kanisa La Laodikia

Ujume: 60-1211E Wakati wa Kanisa La Laodikia

PDF

pakua – m4a

pakua – amr

BranhamTabernacle.org

Wapendwa Waamini wa Neno lisilokosea,

Jinsi gani imekuwa ni jambo lakupendeza sana kusikia na kusoma Nyakati hizi Saba za Kanisa. Kwa kila Ujumbe tunaousikia, kila sura tunayosoma, Yeye anatupa Ufunuo zaidi. Tunajiona waziwazi tukishuka kuja kupitia kila wakati wa kanisa…Bibi-arusi Wake, ambaye alidumu na Neno la asili.

Katika nyakati zote tunaziona roho hizo mbili kwa uwazi; Udanganyifu na uongo wa Shetani, kulipotosha Neno la Mungu, kuwadanganya, kuwapotosha na kuwashinda watu. Lakini wakati wote kumekuwa na kundi dogo la Mungu la watu waaminifu, Bibi-arusi Wake, wakishikilia kila Neno.

Wakati wote kuna onyo moja la daima linalotolewa kwa watu, yawabidi KUDUMU NA NENO. Mara tu unapopata kutoka nyuma ya Neno hilo, unanaswa katika utando wa buibui mkuu wa Shetani; kama Hawa alivyofanya tangu mwanzo. Alishindwa kulitumia Neno. Adamu alishindwa katika kutolitii Neno moja kwa moja. Lakini Yesu, katika Maisha Yake binafsi, akishindana na nafsi yake, alishinda kwa utii kwa Neno la Mungu.

Alisema kama tunataka kuketi katika kiti Chake cha enzi, lazima tuwe Neno lililo hai. Maombi yetu, kufunga kwetu, au hata toba zetu hazitatupa majaliwa hayo. Bibi-arusi NENO tu ndiye atakayejaliwa.

Kunayo mengi ningependa kusema, na nukuu nyingi ningependa kuzishiriki na kila mmoja wenu; hayaishi. Ninajua Ujumbe Huu unawaka katika kila mojawapo wa mioyo yenu na mnapenda kila Neno, jinsi tu nami ninavyolipenda. Yote Tunayotaka kufanya ni kuzungumza na kulishiriki. Tunataka ulimwengu ujue: Ndiyo, sisi ni watu wa kanda. Ndiyo, sisi tunabonyeza Play . Ndiyo, sisi tunaamini ile Sauti iliyo kwenye kanda hizi ndio itakayomkamilisha Bibi-arusi. Ndiyo, kanda ndizo zitakazomuunganisha Bibi-arusi. Ndiyo, Kubonyeza Play ndio Mapenzi Makamilifu ya Mungu. Ndiyo, mimi ndiye Bibi-arusi Wake.

Ninajua mimi ninarudia Kwa barua nyingi, lakini nina furaha sana, ninashukuru kweli, ni hakika … ni jambo lisilo na shaka, huu ndio Mpango wa Mungu kwa Bibi-arusi Wake.

Kwa kila Ujumbe tunaousikia, tunashangaa kwa mshangao, Wao Wanakosaje kuona, kusoma au kusikia yale tunayosikia? Liko papo hapo, kwenye kanda, kanda baada ya kanda, baada ya kanda. Inanifanya nijisikie kuwaambia wao kama vile Yesu alivyomwambia Nikodemo: “Je! wewe u mwalimu wa Israeli, na mambo haya huyafahamu?”

Hebu Sikiliza jinsi gani malaika huyu anavyolifanya rahisi.

Juu ya msingi wa tabia za wanadamu peke yake, mtu ye yote anajua ya kwamba palipo na watu wengi kuna hata na maoni yasiyopatana juu ya mambo madogo-madogo ya fundisho muhimu ambalo wote wanashikilia pamoja.

Juu ya msingi wa tabia za wanadamu PEKE YAKE, hakuna ufahamu wa kiroho unaohitajika, mtu ye yote anajua watu wawili watakuwa na maoni yasiyopatana juu ya MAMBO MADOGO- MADOGO ya fundisho muhimu.

Wote wanaweza kukubaliana na kusema kama watu hawafanyi wanalosema wao, ama wakiondoka, basi maangamizi yatafuata. Lakini nabii wa kweli daima atamwongoza mtu kwenye Neno na kuwafunga watu kwa Yesu Kristo naye hatawaambia watu wamwogope yeye ama yale anayosema, Lakini waogope yale Neno lisemayo.

Neno linasemaje? Nitawapelekea Eliya nabii. Katika siku za SAUTI. Kutakuwa na nabii wa Neno MMOJA…MMOJA tu…kwa kuwa Mungu ameukabidhi Ufunuo kwa HUYO MMOJA PEKE YAKE. Yeye ndiye atakayemrudisha Bibi-arusi Wangu.

Jinsi kulivyo na sauti nyingi hivi na maoni mengi na nukuu nyingi, mtu anawezaje kuwa na HAKIKA?

Ni nani basi atakayekuwa na mamlaka ya kutokosea ambayo itarudishwa katika wakati huu wa mwisho, kwa kuwa wakati huu wa mwisho utarudi kwenye kumdhihirisha Bibi-arusi wa Neno Halisi?

Huyo ndiye ambaye Bibi-arusi anataka kumsikiliza, huyo aliye na mamlaka ya kutokosea; kwa maana Yeye atakuwa ndiye wa KUMRUDISHA Bibi-arusi. Yeye Hatakuwa na maoni yasiyopatana, Yeye ni Neno.

Swali: Bwana, tunataka kujua, ni nani mtu huyo atakayekuwa na Maneno ya kutokosea?

Nitakwambia ni nani atakayekuwa nalo. Itakuwa ni nabii aliyethibitishwa kinaganaga, ama hata aliyethibitishwa kinaganaga zaidi kuliko nabii ye yote katika nyakati zote tangu Henoko hata siku hii, kwa sababu mtu huyu itambidi kuwa na huduma ya jiwe la kifuniko , na Mungu atamtambulisha. Haitambidi kujitetea , Mungu atamtetea kwa sauti ya ishara. Amina.

Jibu: William Marrion Branham.

Hebu nikutie moyo leo Ewe Bibi-arusi Mteule. HUWEZI, NA HAUTA, PUMBAZWA. Je, ulilipata jambo hilo? Hakuna mtu anayeweza kukupumbaza. Paulo hangeweza kumpumbaza mteule ye yote, kama angalikuwa amekosea. Hata katika wakati ule wa kanisa la kwanza la Efeso, wateule hawakuweza kupumbazwa. Waliwajaribu mitume wa uongo na manabii wa uongo na kuwaona kuwa ni waongo na Wakawaondosha.

UTUKUFU EWE BIBI-ARUSI …. Wewe ni Kondoo WAKE nawe unaisikia Sauti yake na kumfuata YEYE. WEWE NI BIBI-ARUSI-NENO LILILO HAI!!

Hakuna kitu kilicho kikuu zaidi kuliko kujua Maneno haya. Kujua ndani ya moyo wako na nafsini mwako, kuwa wewe ni Bibi-arusi Wake. Siku zile ambazo ulimwengu ulikuwa ukingoja zimefika. Bibi-arusi anajitambua naye anafanyika MMOJA NA YEYE; sisi ni UUMBAJI MPYA WA MUNGU.

Kwa mara nyingine tena ninawasihi, ISIKILIZENI SAUTI YA MUNGU siku ya Jumapili, popote mkutanikapo. Haijalishi ni Ujumbe gani Mnaousikiliza mradi tu mnasikiliza Sauti ya Mungu iliyothibitishwa. Sauti hiyo ilikuwa ndio Sauti ambayo Mungu aliyoiita na kuichagua kumrudisha na kumkusanya Bibi-arusi Wake.

Kwa makanisa yote, watu wote, mnaalikwa kusikiliza pamoja nasi Jumapili hii saa 06:00 SITA MCHANA.,masaa ya Jeffersonville,( ni saa 1:00 MOJA JIONI ya Afrika Mashariki) tunaposikia:  Wakati wa Kanisa la Laodikia 60-1211E.

Ndugu. Joseph Branham