23-0625 Hii Ndiyo Ishara Ya Mwisho, Bwana?

Ujume: 62-1230E Hii Ndiyo Ishara Ya Mwisho, Bwana?

PDF

pakua – m4a

pakua – amr

BranhamTabernacle.org

Mpendwa Bibi-arusi Neno kwa Neno,

Hakuna nabii, hakuna mtume, kamwe, katika wakati wo wote, aliyewahi kuishi katika wakati kama huu tunaoishi sasa. Huu ndio wa mwisho. Ile Nguzo ya Moto imerudi. Ile Nguzo ya Moto ambayo iliwaongoza wana wa Israeli; Ile ile iliyompiga Sauli ikamwangusha akienda zake Dameski. Ile ile imekuja na Nguvu ile ile, ikifanya mambo yale yale, na ikifunua Neno lile lile, ikidumu Neno kwa Neno na Biblia!

Siri zote zilizofichwa zilifunuliwa kwake yeye. Je, umeona, Siri ZOTE. Hakuna jipya, hakuna kilichoachwa, hakuna kitakachofunuliwa kutoka kwa mtu mwingine ye yote; YOTE yalifunuliwa kwa malaika-mjumbe Wake wa saba na hayo tumepewa SISI, Bibi-arusi Wake, kwenye Kanda.

Ndiyo YOTE Bibi-arusi anayohitaji; ANGALIA TENA, YOTE BIBI-ARUSI ANAYOHITAJI . Wengine wanahitaji vitu vingine, nao wamepewa vitu hivyo. Lakini tunachohitaji sisi kimerekodiwa na tumepewa hicho kwenye Kanda NACHO kinatupa IMANI ya Kunyakuliwa.

Sisi ndilo kanisa lile ambalo Bwana Mungu alimpa. Haya ndiyo makao yake makuu. Hapa ndipo Yeye alipotuambia tukae. Si jengo, KANDA. Sisi ndio kundi lile la watu wanaoamini, na wenye njaa na wanaoshikilia kila Neno. Alituambia tukae hapa na tuliangalie lile Jiwe Jeupe, Jiwe gumu sana, NENO KWENYE HIZI KANDA.

Sauti kutoka Mbinguni ilinena naye na kusema, “Lete Chakula. Kihifadhi mle ndani. Hiyo ndiyo njia pekee ya kuwaweka hapa, ni kuwapa Chakula”. Yeye Hakusema tafuteni kitu kingine, ama ya kwamba kutakuwa na mafunuo mapya kutoka kwa mtu mwingine; angalieni CHAKULA HIKI KILICHOHIFADHIWA KWENYE KANDA, KAENI HAPO.

Lakini kama tu vile walivyofanya katika ndoto zote alizofunua, baadhi yao wakaenda huko; baadhi yao wakachukua njia moja, na wengine nyingine. Wachache sana ndio waliobakia na wakaendelea kuangalia kile ambacho YEYE aliwaambia.

Sasa linganisha hilo na zile nyingine, zile ndoto. Hili lilikuwa ono. Kile chakula; hiki hapa. Mahali penyewe ni hapa.

Asingeweza kuwa wazi zaidi kwa Bibi-arusi Wake zaidi ya hapo. Hili lilikuwa ono, si ndoto, ONO. Chakula kiko hapa: KANDA. Mahali penyewe ni hapa: KANDA. Tunafanya vile hasa alivyotuambia tufanye: Kuzisikiliza KANDA!

Inahitaji Ufunuo wa Kiroho kuelewa mambo haya. Itahitaji Ufunuo wa Kiroho kuamini na kuelewa yote atakayotuambia Jumapili hii. Utakuwa ni wakati uliyotukuka kwa Bibi-arusi.

Kuna mambo mengi sana Mungu anatuambia na kutufunulia kwenye Ujumbe huu. Ninataka kunakili nukuu baada ya nukuu na kuwapeni, lakini najua atawafunulia kila kito cha thamani kwa sababu alisema huyu ndiye ninyi mlikuwa:

Hili ndilo kanisa ambalo Bwana Mungu alinipa. Hapa ndipo makao makuu yangu. Hapa ndipo ninapokaa…kuna kundi la watu hapa wanaoamini na wana njaa na wangali wanashikilia.

Sisi ndio kundi hilo ambalo lina njaa na linaloshikilia. Watu Wengi hawatuelewi na wanatufanyia mzaha, lakini hiyo ni sawa, tunawapenda na kuwaombea; bali sisi tunataka SAUTI MOJA tu kutuongoza.

Nisamehe, lakini sina budi kukupa nukuu hii.

“Aanzapo kupiga baragumu, siri itatimizwa”. Sasa, angalia: Basi wakati umewadia wa kufunuliwa kwa zile Sauti za Muhuri Saba za Ufunuo 10. Mnaelewa? Wakati siri zote za kile Kitabu zimemalizika, na Biblia ilisema hapa kwamba angetimiza zile siri .

Nani ambaye angetimiza zile siri? Mchungaji wako? Kundi? Mimi? Malaika-Mjumbe wa Saba: William Marrion Branham. Hakuna mtu kabla yake, kipindi chake, ama baada yake. ANGETIMIZA ZILE SIRI.

Huenda ikawa ni wakati wa mwisho. Huenda ikawa wakati umewadia wa pinde za mvua kupita angani na tangazo toka mbinguni likisema, “Wakati umekwisha.” Kama ndivyo ilivyo, hebu na tujiandae, marafiki, kumlaki Mungu wetu.

Ndiyo, Bwana, tunataka kujiandaa kukulaki wewe. Tunataka kufanya yote tuwezayo. Tunataka kuwa katika Mapenzi Yako makamilifu. Tafadhali tuambie Baba, tufanye nini ili tuweze kujiandaa?

Kumekwisha wekwa chakula kingi sana sasa; hebu na tukitumie. Hebu na tukitumie sasa.

Asante Baba kwa Chakula ulichokihifadhi kwa ajili ya Bibi-arusi Wako na ule Ufunuo Wake. Tunakitumia kila siku.

Naomba msamaha kwa kanisa langu dogo hapa, ambako Wewe umenituma kulielekeza na kuliongoza. Wabariki, Bwana. Nimetenda kulingana na yale maono na ndoto na kadhalika vimesema kadiri nijuavyo mimi. Nimehifadhi chakula chote, vizuri nijuavyo, kwa ajili yao , Bwana. Hata iwe nini, Bwana, sisi tu Wako.

Asante Bwana, umetuambia kwa mara nyingine tena, umekihifadhi Chakula chote tunachohitaji kwa safari yetu.

Ni Vigumu kwangu kungojea kusikia, Hii ​​Ndiyo Ishara ya Mwisho, Bwana? 62-1230E, pamoja na kila mmoja wenu Jumapili saa 06:00 SITA MCHANA saa za Jeffersonville.( Ni saa 1:00 MOJA JIONI masaa ya Afrika Mashariki),Najua mambo yatafunuliwa kwetu zaidi ya hapo awali. Hii inaweza kuwa mara ya mwisho sisi kusikia jambo hili.

Vipi kama ni kitu cha kutujulisha jinsi ya kuingia katika imani ya kunyakuliwa! Sio? (Tutakimbia na kuruka juu ya kuta?) Kuna jambo lililo tayari kutukia, na hii miili ya kale iliyoharibika, mipotovu, itabadilishwa? Naweza kuishi nipate kuliona, ee Bwana? Lipo karibu sana kwamba nitaliona? Hiki ndicho kizazi kile? Mabwana, ndugu zanguni, ni wakati gani? Tuko wapi?”

Ndugu. Joseph Branham