UJUMBE: 60-1211E Wakati wa Kanisa La Laodikia
- 26-0913 Wakati wa Kanisa La Laodikia
- 24-1208 Wakati wa Kanisa La Laodikia
- 23-0618 Wakati wa Kanisa La Laodikia
- 20-1227 Wakati wa Kanisa La Laodikia
- 19-0310 Wakati wa Kanisa La Laodikia
- 16-0410 Wakati wa Kanisa La Laodikia
Tai wanakusanyika Pamoja.
26.12.2020
Mpendwa Bibi-arusi Neno Mkamilifu,
Bibi-arusi anafurahi sana na mwenye Matarajio makuu tunapojiandaa kusikia Ujumbe wa jiwe la kifuniko wa wakati wa mwisho wa kanisa, Laodikia. Ni wakati mkuu zaidi wa nyakati Zote , na Mjumbe mkuu zaidi wa nyakati zote, ambaye anakusanya watu wakuu zaidi wa nyakati zote.
Hakujawahi kuwa na siku kama siku tunayoishi. Ulimwengu unaweza kusikia Sauti ya Mungu kama vile andiko lilivyotabiri katika Neno Lake. Ufunuo 10: 7, Katika siku za SAUTI. Angalia, SI MASAUTI(sauti nyingi), BALI SAUTI.
Mungu aliahidi kumtuma malaika mwenye nguvu katika wakati huu wa mwisho kufunua siri zote ambazo alikuwa amezificha tangu kuwekwa misingi ya ulimwengu. Atakuwa malaika_mjumbe aliyethibitishwa kuliko mwingine yeyote, kwa maana amechaguliwa kumwita Bibi-arusi Wake Atoke.
Wengi watamkataa. Wengine watasema huwezi kuamini yote anayosema; Ila tu anaposema Bwana asema hivi. Kuna makosa katika ujumbe wake. Sio yeye tu, kuna wengine walioitwa na kupakwa mafuta kumuongoza Bibi-arusi na kufunua kweli.
Neno linasema kutakuwa na kundi teule la watu ambao wataamini kila Neno mjumbe huyu kutoka kwa Mungu alilosema; kwa kuwa agizo lake lilikuwa “Wafanye watu WAKUAMINI”.
Kwa hiyo, ni lazima tuamini baadhi tu ya yale aliyosema? Je! Neno linasema, “Nitakutumia Eliya nabii kisha tena nitakutumia watu wengine kukuambia lipi ni Neno na lipi sio Neno?”
Maneno yangu yatashindwa, lakini Maneno ya Mungu hayawezi kushindwa. Hebu na tusome ni Mamlaka gani MUNGU ATAKAYOMPA Malaika wake wa Saba.
Ni nani basi atakayekuwa na nguvu ya kutokushindwa ambayo itarejeshwa katika wakati huu wa mwisho, kwani wakati huu wa mwisho utarejea kudhihirisha Bibi-arusi Neno Safi? Hiyo inamaanisha tutakuwa na Neno mara nyingine tena kama lilivyotolewa kikamilifu, na kueleweka kikamilifu katika siku za Paulo. Nitakuambia ni nani atakayekuwa nalo. Atakuwa nabii aliyethibitishwa kabisa, au hata na zaidi amethibitishwa kabisa kuliko nabii yeyote katika nyakati zote tangu Enoko hadi leo hii, kwa sababu mtu huyu atakuwa na huduma kuu ya kinabii ya jiwe La kifuniko, na Mungu atamweka wazi. Hataitaji kuongea mwenyewe, Mungu ataongea kwaajili yake kwa sauti ya ishara. Amina.
Utukufu !! Haleluya !! Sauti tunayoisikiliza tunapo BONYEZA PLAY, imetolewa kikamilifu, na inaeleweka kikamilifu, NA INAONGEA MANENO YASIOSHINDWA. (Webster: isioweza kukosea.)
Ni pumziko la jinsi gani Bibi_arusi alilonalo tunaposikiliza Neno safi la Mungu. Hakuna kubashiri, hakuna kushangaa, hakuna haja ya kwenda kumsikia huyu, au kwenda kumsikia yule; tunayo yote KATIKA SAUTI MOJA KWENYE KANDA.
hebu na tuende kutafuta na kung’asha vitu muhimu zaidi na tuone kile Mungu anachosema juu ya malaika wetu.
-Yeye atasikia tu kutoka kwa Mungu na
-Atakuwa na “Bwana asema hivi” na kunena kwa niaba ya Mungu. Yeye
-Atakuwa kinywa cha Mungu.
-Atawarudisha wateule wa siku za mwisho.
-Atairudisha kweli.
Sasa na tuang’aizie baadhi ya vitu muhimu wakati anapozungumza kutuhusu sisi, kundi hilo maalum aliloita, aliloteua na kuchagua kuamini kila Neno; Bibi_arusi wake.
-Na hao wateule walio pomoja naye katika siku hiyo watakuwa ndio wanaomdhihirisha Bwana kwa kweli na watakuwa ndio Mwili wake na kuwa sauti yake na kutenda kazi zake. Haleluya! Je! Unaliona hilo?
-Katika wakati huu wa mwisho kuna watu wengine nchini, ambao chini ya mjumbe wao watakuwa ndio sauti ya mwisho kwa wakati wa mwisho.
-Kanisa si “kinywa” cha Mungu tena. Ni kinywa chake lenyewe
-Sauti ya Mungu itakuwa ndani ya bibi_arusi. Ndio Iko, kwa maana inasema katika sura ya mwisho ya Ufunuo mstari wa 17, “Roho na bibi_arusi wasema, Njoo.”
-Amempa bibi_arusi Sauti.
-Wateule hawawezi kudanganywa
Ongea juu ya kupumzika, ametupa Sauti yake na hatuwezi kudanganywa, sisi ni MMOJA na yeye.
Sasa, thawabu yetu ya kukaa wa kweli kwa nabii huyo na kuamini kila Neno kwa kusikiliza Sauti hiyo.
-Hao wanaompokea nabii huyo katika jina lake mwenyewe watapokea matokeo mema ya huduma ya nabii huyo. Na hao wanaomsikia watabarikiwa na kuwa sehemu ya bibi-arusi wa siku ya mwisho anayetajwa katika Ufunuo 22:17, “Roho na bibi_arusi wanasema, Njoo.”
Ikiwa ungependa kupokea thawabu hiyo, njoo uungane nasi Jumapili hii saa 2:00 mchana saa ya Jeffersonville ( saa 22:usiku ya TZ), kusikia: Wakati wa Kanisa la Laodikia 60-1211e, au vile Napenda kuuita, Hadithi ya Maisha yangu.
Ndugu. Joseph Branham
Malaki 4: 1-6
Mtakatifu Mathayo 2: 14-15, 17: 9-13
Mtakatifu Luka 1: 14-17
Warumi 11: 15-27
Ufunuo 3: 14-22