23-0604 Wakati Wa Kanisa La Filadelfia

Ujume: 60-1210 Wakati Wa Kanisa La Filadelfia

PDF

pakua – m4a

pakua – amr

Mpendwa Bibi Yesu Kristo,

Je! hilo halisikiki lakupendeza? Mwana-Kondoo na Bibi-arusi Wake wametulia milele katika ukamilifu wote wa Mungu. Ati tutoe sifa ya jambo hilo? Tunalifikiri. Tunaliota. Tunasoma kile Neno lisemacho kulihusu. Tunamwona Yeye akishiriki Utakatifu Wake NASI. Ndani yake, tumekuwa haki halisi ya Mungu.

Inatuletea furaha jinsi gani wakati tunapobonyeza Play, na kumsikia Mungu Mwenyewe akizungumza nasi kupitia malaika Wake mwenye nguvu na kutuambia mambo haya.

Hakuna kitu cho chote katika maisha haya, hata kiridhishe namna gani, kiwe kizuri na chema vipi, ila utapata jumla ya ukamilifu wote katika Kristo. Kila kitu hufifia kabisa mbele Zake.

Yeye anatuambia tutakuwa na jina jipya, Jina Lake. tutapewa jina lake wakati atakapotupeleka kwake. Itakuwa lakupendeza sana kuliko tunavyoweza kuwazia. Tutaenda popote Bwana-arusi alipo. Hatutaachwa Naye kamwe. Hatutaondoka Ubavuni mwake. Tutashiriki kiti cha enzi pamoja naye. Tutatiwa taji kwa utukufu na sifa zake.

Na wakati anapojithibitisha Mwenyewe kwa ulimwengu, na ulimwengu wote unasujudu miguuni Pake, wakati huo ulimwengu wote utasujudu miguuni pa watakatifu, ikithibitisha ya kwamba walikuwa sahihi katika msimamo wao pamoja Naye. Mungu na abarikiwe milele!

Yeye alitujua tangu zamani kwa uamuzi wa Kiungu ya kwamba tungekuwa Bibi-arusi Wake. Yeye Alituchagua SISI; hatukumchagua Yeye. Yeye ndiye Aliyetuita SISI ; hatukuja kwa hiari yetu. Yeye Alitufia SISI. Alitusafisha katika Damu Yake Mwenyewe. Yeye Alitununua SISI . Sisi ni mali yake, na wake peke yake. Tumejitoa Kwake kabisa naye Anakubali jukumu hilo. Yeye ni kichwa CHETU. Yeye Ananena nasi kupitia malaika wake nasi tunatii, kwani hiyo ndiyo furaha yetu.

Tangu mwanzo hata mwisho, Ujumbe ulio kwenye kanda yote ni MUNGU kwetu SISI. Hebu hayo Maisha na yawe ndani YETU. Hebu na iwe ni Damu yake inayotuosha SISI. Hebu iwe ni Roho Wake anayetujaza SISI. Hebu na liwe ni Neno lake ndani ya moyo na mdomo WETU. Na yawe ni Mapigo Yake yanayotuponya SISI. Na iwe ni Yesu, na Yesu peke yake. Si kwa matendo ya haki, ambayo tumefanya. Kristo ndiye uzima wangu. Ujumbe huu ni uzima wetu, kwa maana ni Kristo.

Loo! kuna sauti nyingi sana ulimwenguni—shida nyingi sana na mahitaji yanapaza sauti yapate kushughulikiwa; lakini kamwe hakutakuweko na sauti iliyo muhimu sana na inayostahili kushughulikiwa kama sauti ya Roho. Kwa hiyo, “Yeye aliye na sikio la kusikia, na alisikie Neno hili ambalo Roho ayaambia makanisa.”

Mungu anayo Sauti kwa ajili ya siku hii. Imethibitishwa na Nguzo ya Moto kuwa ni Sauti ya Mungu. Kamwe hakutakuwa na Sauti ILIYO MUHIMU SANA NA YENYE THAMANI SANA KUSHUGHULIKIWA kama ile Sauti iliyo kwenye kanda kwa ajili ya siku ya leo.

Njoo uungane nasi Jumapili saa 06:00 SITA MCHANA, saa za Jeffersonville. ( Ni saa 1:00 MOJA JIONI ya Afrika Mashariki )Tuna mfuko mzima wa maandiko uliyojaa Asali. Tutaiweka kwenye Mwamba, si juu ya kanisa lolote; juu ya Mwamba, Kristo Yesu. Basi ninyi kondoo anzeni kuiramba. Hakika mtapata afya mara moja. Shida zote za dhambi zitakwisha utakapouramba Mwamba. Hivyo tu ndivyo unavyopaswa kufanya, njoo uisikie Sauti ya Mungu ikituambia yote kuuhusu: Wakati wa Kanisa la Filadelfia 60-1210.

Ndugu. Joseph Branham