All posts by admin5

23-1022 Mbona Unalialia? Nena!

UJUMBE: 63-0714M Mbona Unalialia? Nena!

PDF

pakua – m4a

pakua – amr

BranhamTabernacle.org

Wapendwa maskani za Mungu,

Mimi ni Kanisa Lake. Wewe ni Kanisa Lake. Sisi tu maskani ambamo Mungu anakaa ndani yake. Sisi ni Kanisa la Mungu aliye hai; Mungu aliye hai akiishi katika nafsi zetu. Matendo yetu ni matendo ya Mungu. Utukufu!!

Sote tunakusanyika pamoja, katika maeneo madogo kutoka kote ulimwenguni; sote tukikusanyika pamoja ilipo Sauti ya Mungu, Neno Lake la siku hii.

Ni ajabu sana. Hakuna kufungwa kwa kitu kingine, ila kwa Yesu Kristo na Neno Lake. Hilo Ndilo, mwisho wa maneno. Tumeketi pamoja katika ulimwengu wa Roho tukikamilishwa na Sauti ya Mungu mwenyewe.

Tunaenda kabisa. tunaenda sote kwenye Nchi ya Ahadi. Kila mmoja wetu! Hata kama wewe ni mke wa nyumbani, u yaya mdogo, mama kizee, babu ama kijana mwanamume, chochote ulicho, tutaenda sisi sote. Hakutakuwa hata na mmoja wetu atakayeachwa nyuma. Kila mmoja wetu ataenda, na “hatutazuiwa na kingine chochote.”

Tunaamini kwamba tunapaswa kuwa wote pamoja. Kundi moja kubwa lililoungana la Mwili wa Yesu Kristo, linalongojea kule Kuja kwenye utukufu. Hatungepaswa kutengana, lakini mwanadamu ametoka kwenye njia iliyowekwa ya mafundisho ya Injili.

Yabidi kuwe njia fulani ya kuonyesha kabisa ni ipi iliyo kweli na iliyo makosa. Na njia pekee utakayotenda, ni kutokuweka fasiri yo yote kwenye Neno, lisome tu jinsi lilivyo na uliamini hivyo. Kila mtu anaweka fasiri yake mwenyewe, na inalifanya linene jambo lingine tofauti. Kuna SAUTI YA MUNGU MOJA tu KWA BIBI-ARUSI. BONYEZA PLAY!

Nayasema kwa kanda hii na kwa wasikizaji hawa; nasema hili chini ya uongozi wa Roho Mtakatifu, “Ni nani aliye upande wa Bwana? Na aje chini ya Neno hili.”

Neno la siku yetu lina Sauti. Nabii wetu ndiye Sauti hiyo. Sauti hiyo ndilo Neno lililo hai kwa ajili ya siku yetu. Tulichaguliwa tangu zamani kuisikia Sauti hiyo na kuona saa hii, na hakuna kitu kitakachotuzuia kuisikia Sauti hiyo.

Imani yetu inaiona hiyo na kuchagua kuisikia hiyo bila kujali mtu yeyote anasema nini. Sisi hatushushi darubini yetu kutazama upande mwingine. Tunaweka kipini chetu cha kulengea shabaha katikati ya Neno kabisa na masikio yetu yametuniwa kwenye Sauti hiyo.

Kwa kujiweka wakfu Kwako Bwana, kutoka mioyoni mwetu hadi Masikioni Mwako, haya ni maombi yetu ya dhati.

Kusudi maisha yetu yapate kubadilika tangu leo na kuendelea, tupate kuwa na mawazo mema. Tutajaribu kuishi vizuri sana na kuwa wanyenyekevu pia tukiamini yale tunayomwomba Mungu, Mungu atampa kila mmoja. Nasi hatutanena maovu sisi kwa sisi ama dhidi ya mtu ye yote. Tutawaombea adui zetu na kuwapenda; tuwafanyie mema wanaotufanyia mabaya. Mungu ndiye Hakimu wa asiye na makosa na aliye na makosa.

Ninawaalika mje kutia mafuta Imani yenu kwa kuisikia Sauti ya Mungu pamoja nasi Jumapili, saa 6:00 SITA MCHANA, saa za Jeffersonville,( ni saa 1:00 MOJA JIONI ya Afrika Mashariki ) tunaposikia: Mbona Unalialia? Nena! 63-0714M.

Ndugu. Joseph Branham

23-1015 Lile Shtaka Na Ushirika wa Nyumbani Na Kutawadhana Miguu

UJUMBE: 63-0707M Lile Shtaka

PDF

pakua – m4a

pakua – amr

BranhamTabernacle.org

Mpendwa Bibi-arusi wa Kanisa la Nyumbani,

hebu sote tukusanyike pamoja na kusikiliza Ujumbe, Lile Shtaka 63-0707m, Jumapili hii saa 11:00 KUMI NA MOJA JIONI, saa za Jeffersonville. ( Ni saa 6:00 SITA USIKU ya Afrika Mashariki )

Hebu basi na tujitayarishe kwa nafasi iliyo takatifu ya kushiriki Meza ya Bwana majumbani mwetu mara tu baada ya huo Ujumbe huku tukisikiliza 63-0707e Ushirika. Kisha tutakuwa na Ibada ya Ushirika na kutawadhana miguu itafuata. Kama vile Lile shtaka, kanda ya Ushirika itachezwa kwenye Voice Radio (kwa Kiingereza peke yake), ikifuatiwa na muziki wa piano, nukuu ya kutambulisha kutawadhana miguu, na Nyimbo za Injili, kama kawaida tufanyavyo katika ibada za Ushirika za Nyumbani.

Zilizoorodheshwa hapa chini ni anuani za njia za kupata ama kuandaa divai na mkate wa Ushirika.

Ninashukuru sana kwamba Bwana ametuandalia njia ya kumwalika Mfalme wa wafalme katika kila moja ya nyumba zetu kwa siku iliyo maalum sana pamoja Naye. Hakika ninatazamia kukutana nanyi nyote Mezani Pake.

Mungu awabariki,

Ndugu Joseph Branham

Instructions for Baking Bread / Making Wine

Instructions to obtain Communion Wine / Feet Washing Bins

Kampeni za uinjilishaji za kasisi William Branham

Sanduku la Posta 325
Jeffersonville, Indiana

Julai 13, 1964

Ndugu mpendwa Gagnon;
Salamu katika Jina la Bwana.

Ilikuwa ni furaha kusikia kutoka kwako leo hii, na ninaamini kwamba u mzima, ukimtumikia Bwana.

Ilikuwa furaha kuisoma barua yako, na kuona unyoofu wako kwa kuniuliza maswali yafuatayo. Kwa msaada wa Bwana, nitajaribu kukujibu hilo. Kwanza, kuhusu ushirika, Ndiyo, Shiriki, huhitaji kuwa mhudumu ili kufanya jambo hilo; Divai iko sawa. Kuhusu swali kuhusu nambari 666, ni kuhusu tu njia yako ya kuzaliwa tu, na haimaanishi chochote kile, kwa sababu sasa wewe ni mtoto wa Bwana aliyezaliwa mara ya pili.

Natumai nitasikia kutoka kwako tena hivi karibuni.

Katika huduma yake,

Ndugu Branham

BB/wpb

KUMBUKA: Swali nililomuuliza Ndugu Branham ni hili:

Nilimwambia sisi hatuna mhudumu, nasi tulitaka kujua ikiwa ilikuwa ni sawa kwangu kuhudumia ushirika. Pia, ikiwa ilikuwa ni sawa kutumia divai ya “kosher”.

AA Gagnon

23-1008 Je, Maisha Yako Yanaistahili Injili?

UJUME: Je, Maisha Yako Yanaistahili Injili? 63-0630E

PDF

pakua – m4a

pakua – amr

BranhamTabernacle.org

Wapendwa kundi la Nabii wa Mungu,

Tuombe.

Baba wa Mbinguni, jinsi tunavyoshukuru kwa ajili ya wakati mwingine wa kukusanyika pamoja kutoka kote ulimwenguni upande huu wa Umilele. Kuwa katika nia moja na umoja pamoja Nawe; tukiiskia Sauti yako ikituzungumzia. Tunatarajia kwa mara nyingine tena kuhuishwa upya kwa nguvu kuja kutoka Kwako, zipate kututia moyo na nguvu kwa ajili ya safari iliyoko mbele.

Tunakusanyika pamoja ili kuipokea Mana iliyotolewa kwa ajili yetu. Ile Mana ya kiroho uliyoihifadhi ili itupe nguvu kwa ajili ya safari. Ndilo jambo PEKEE linaloweza kutuhifadhi katika siku zijazo.

Ulituambia, kabla hujaliweka Kanisa Lako katika utaratibu, itabidi utukusanye pamoja, mahali pamoja, na kwa nia moja. Ndipo ungemtuma Roho wako Mtakatifu kwetu kwa ajili ya uongozi; si baraza fulani la ekumeni, si kundi fulani la watu, bali Roho Wako Mtakatifu atuzungumzie mdomo kwa sikio.

Wewe ulinena kupitia malaika wako na kutuambia:

“Ninawatakeni mkae na mchungaji wenu na mdumu na Mafundisho ambayo yamefundishwa hapa. Dumuni na Neno hili, msiliache! Dumuni moja kwa moja na Neno hata iweje, dumuni na Neno hilo!”

Baba, tunalitii Neno Lako nasi tunakaa na mchungaji wetu. Ni Sauti ya Mungu kwa ajili ya siku hii tu ndiye anenaye Neno Lako lililo safi ambalo limethibitishwa na kudhihirishwa kwa ajili ya siku yetu.

Ulituambia kama ilivyokuwa katika siku za Sodoma, ndivyo itakavyokuwa katika Kuja kwake Mwana wa Adamu; kwamba tungekuwa na mambo mawili ya kutuongoza, na ulimwengu wote uliyosalia ungekuwa na mambo mawili. Mambo yao mawili walikuwa wahubiri wawili.

Lakini kwa ajili ya Kanisa Lako la kiroho, Bibi-arusi Wako mteule, aliyechaguliwa tangu zamani, mambo yetu mawili yangekuwa ni Wewe, kudhihirishwa katika mwili wa kibinadamu, kutuongoza kwa Nguzo ya Moto.

Acha upepo uvume vikali. Acha tufani itikise. Tuko salama, milele. Tunapumzika papo hapo kwenye Neno Lako. Wakati umefika. Kule kutoka kwa kiroho kumewasili. Tunatembea na kuzungumza nawe kila siku, tukisikia Sauti Yako. Tuko katika ushirika wa daima na Wewe.

Tunataka kuwa Mikono Yako, Macho Yako, Ulimi Wako. Wewe ni mzabibu, sisi ni matawi Yako. Tutie nguvu, Baba, ili tuzae matunda yako. Nia yetu pekee ni kuwa na maisha yanayoistahili Injili Yako.

Jihakisi Mwenyewe kupitia sisi, Baba, ili kuendeleza kazi Yako na kutimiza Neno Lako lililoahidiwa. Nia yetu ni kuwa wajumbe Wako wa siku hii, ili kuitimiza haki yote.

Tunataka kukusikia Wewe ukituambia:

Ombi langu ni kwamba, kwa wale walioko kwenye redio ama kwenye…kwenye maeneo ya kanda, na wale waliopo hapa. Mungu wa neema yote, wa Mbinguni, na atuangazie sisi sote Roho Wake Mtakatifu, kusudi sisi, tangu usiku huu, kuendelea, tunaweza kuishi maisha ambayo Mungu angesema, “Nimependezwa. Ingieni katika furaha za Milele ambazo zimewekwa tayari kwa ajili yenu tangu kuwekwa misingi ya ulimwengu.” Mungu wa Mbinguni na atume baraka Zake juu yenu nyote.

UTUKUFU…hao ni sisi Baba, Bibi-arusi Wako katika maeneo ya kanda. Hakika Wewe unatutumia baraka zako na kutufunulia Neno lako, ukituambia kwa kila Ujumbe tunaousikia, Wewe umependezwa, SISI NI BIBI-ARUSI WAKO.

Ikiwa ungependa kumsikia mchungaji wetu, mchungaji wa Mungu kwa ulimwengu mzima ambaye Yeye alimtuma kumwita atoke na kumwongoza Bibi-arusi Wake, njoo uungane nasi Jumapili saa 6:00 SITA MCHANA, saa za Jeffersonville, ( ni saa 1:00 MOJA JIONI ya Afrika Mashariki ) kumsikia Yeye akinena Maneno ya Uzima wa Milele, anapotuletea Ujumbe kutoka kwa Mungu: Je, Maisha Yako Yanaistahili Injili? 63-0630E.

Ndugu. Joseph Branham

Tangazo Maalum: Bwana akipenda, Jumapili ijayo usiku, tarehe 15 Oktoba. tutakuwa na Ibada ya Ushirika ya nyumbani na Kutawadhana Miguu.

23-1001 Kutoka Kwa Tatu

UJUME: 63-0630M Kutoka Kwa Tatu

PDF

pakua – m4a

pakua – amr

BranhamTabernacle.org

Mpendwa Bibi-arusi wa Kutoka,

Mambo haya tunayoyaona yakitukia leo yasingeweza kutokea miaka ishirini iliyopita, ama miaka arobaini iliyopita; ni leo tu ndio yanafanyika. Hii ndio ile saa! Huu ndio wakati! Sasa ndio wakati wake wa kutimizwa. Mungu aliliahidi, NA NDILO HILI HAPA.

Sisi tuna ufahamu wa kiroho; uovu wa taifa hili umetimia. Ile saa imefika. Ni wakati wa kwenda kwenye ile Nchi ya ahadi. Sio nchi nyingine tu ya kuendea, bali Makao yetu ya Baadaye ambayo tumekuwa tukiyangojea.

Hebu Wazia jambo hilo, kile kinachotuongoza ni zaidi ya nabii. Ni Mungu aliyedhihirishwa katika mwili miongoni mwetu, pamoja na Neno Lake kuthibitisha jambo hilo. Nabii ambaye aliyefanya mara elfu zaidi ya nabii mwingine ye yote. Ni Nguzo ya Moto inayotuongoza kwenda kwenye ile Nchi ya ahadi, Utawala wa Miaka Elfu.

Yeye alimchagua nabii wetu na akampa ishara ya kimbinguni ya Nguzo ya Moto, ili asikosee. Yale nabii aliyosema ni Maneno hasa ya Mungu Mwenyewe. Alimchukua nabii wetu, akamfundisha, kisha akamrudisha kwetu pamoja na ile Nguzo ya Moto, ili ajithibitishe Mwenyewe kwetu, na kutupa Ufunuo mkamilifu wa Neno Lake lote.

Kama tunataka kwenda kwenye hiyo Nchi ya ahadi, hatupaswi kusahau kamwe, Mungu hawezi, na hatabadilisha mpango Wake. Yeye ni Mungu, Naye hawezi. Alituambia Yeye kamwe hatajishughulisha na Kundi. Hajawahi kamwe. Yeye hutushughulikia kama mtu mmoja-mmoja. Yeye alituahidi katika Neno Lake angetutumia Malaki 4 atuongoze kwenda kwenye Nchi hii, Naye ametutumia.

Lakini, unaona, Ahabu alikuwa na mfumo aliodhani ulikuwa ni wa Bwana. Akasema, “Nina mia nne wa hao, walioelimishwa na kufundishwa.” Nao wanadai kwamba ni manabii wa Kiebrania, kama vile makundi ya wahudumu yanavyodhani siku hizi.

Wengi hawataki kulikubali, lakini kama Eliya wa kale, Mjumbe-malaika wa saba wa Mungu, mchungaji wetu, ndiye mchungaji wa ulimwengu wote kumwongoza Bibi-arusi Wake.

Yeye ni Malaki 4:5, na Ufunuo 10:7. Yeye ndiye kutimizwa kwa Maandiko yote ambayo Biblia ilitabiri kumhusu. Ni Ujumbe huu, Sauti hii, ambayo ni Sauti ya Mungu inayomwita Bibi-arusi Wake. Ndiyo Ramani ya Mungu kwa ajili ya siku hii.

Ni Nguzo ile ile ya Moto, kwa mfumo ule ule uliotiwa mafuta. Mungu yeye yule akifanya mambo yale yale.

Sasa Neno limefanyika mwili na linaishi kati yetu katika miili yetu, Bibi-arusi Neno Wake.

Hebu na tumlilie na kumshukuru, tumsifu, tumwabudu, kwa yote aliyotenda: Kutuokoa, kutuchagua tangu zamani, kutuhesabia haki.

Yale Anayotufanyia sasa hivi; Yanatupa Ufunuo na Ufunuo, akituambia sisi ni nani. Na yote atakayotufanyia…Kuja kutuchukua kuwa Bibi-arusi Wake na kutupeleka kwenye Makao yetu ya Baadaye Aliyotuandalia, na kuwa pamoja Naye katika Milele yote.

Chochote tunachohitaji, mlilie Yeye. Hilo ndilo analotaka watoto Wake wafanye. Kumlilia Yeye mpaka tumeridhika na kupata kile tunachokihitaji.

Njoo ukaungane na sehemu ya Bibi-arusi Wake Jumapili saa 6:00 SITA MCHANA, saa Jeffersonville, ( Ni saa 1:00 MOJA JIONI ya Afrika Mashariki ) na umsikie mchungaji wa Mungu kwa ulimwengu, William Marrion Branham, akituambia yote kuhusu: Kutoka kwa Tatu 63-0630M.

Ndugu. Joseph Branham

Maandiko ya kusoma kabla ya Ujumbe:

Kutoka 3:1-12
Mwanzo Sura ya 37 yote
Mwanzo Sura ya 43 yote

23-0924 Kimulimuli Chekundu Cha Dalili Ya Kuja Kwake

UJUME: 63-0623E Kimulimuli Chekundu Cha Dalili Ya Kuja Kwake

PDF

pakua – mp3 (VGR dynamic audio)

pakua – amr

BranhamTabernacle.org

Mpendwa Bibi-arusi Asiye na Hofu,

ONYO!! ONYO!! Taa nyekundu inamemetesha. Kule kushushwa kwa pazia kumefika. Yatubidi tuweke kila kitu kando, KILA KITU, na tuwe tayari. Tumefika mwisho. Ule wakati ambao tulikuwa tukiungojea tangu mwanzo umefika. Unabii sasa unatimizwa.

Mungu alimwinua mjumbe-tai Wake mwenye nguvu juu sana katika mbingu kutazama miaka sitini ng’ambo ya mwaka 1963 hadi leo, Septemba mwaka 2023, kuyaona yote ambayo yangetendeka katika siku yetu… hali ambayo ulimwengu ungekuwemo, ukosefu wa uadilifu wa wanawake, kanisa na hali yake, wazimu wa watu; mwovu, kipofu, uchi, kahaba mkuu katika matawi yote ya serikali, ufisadi katika siasa, naye ametuonya ni yapi yangetukia.

Sasa tunaliona hilo likidhihirishwa mbele ya macho yetu vile hasa alivyotuambia ingekuwa. Sisi ndio wale walioyaona mambo haya yote yakitimia. Kila kitu kiko mahali pake. Limekuwa chungu kubwa mno la uchafu.

Ulimwengu wote uko katika hali ya hofu. Wanajua hakuna tumaini lililobakia. Inazidi kuwa mbaya kila siku. Hofu imetanda uso wa Dunia. Uchumi umekwisha, mauaji ya bila sababu, wanawake wanataka kuwa wanaume, wanaume wanataka kuwa mwanamke. Cho chote na kila kitu kinakubaliwa. kitu gani kinaweza kutokea wakati wo wote? Wanajua ni kama volkeno; Kitalipuka sekunde yo yote. Unaliona jambo hilo kwenye nyuso zao, katika matendo yao, HAKUNA TUMAINI, HOFU.

Hata makanisa yanayojiita ya Kikristo yanakumbatia watu waliobadili jinsia kuwa wachungaji, viongozi wa kiroho wa watu. Imekuwa mbaya zaidi kuliko Sodoma na Gomora. Shetani na ufalme wake wanaungana na kuwa kitu kimoja. Yeye amelifikia lengo lake.

LAKINI UTUKUFU KWA MUNGU, katikati ya mchafuko huo wote na hofu, Baba ametuhifadhi, SISI, kundi lake la watu teule, Bibi-arusi kipenzi Wake, salama Mikononi Mwake nasi tuna muungano wa Kiroho pamoja Naye zaidi ya wakati wo wote ule. Huu ni wakati mkuu zaidi wa maisha yetu. Ni ajabu. Ni tukufu. Ni la kimbinguni. Ni zaidi ya maneno ambayo tungeweza kueleza.

Miili yetu inafanyika Neno, nalo Neno linafanyika mwili; linadhihirishwa, linathibitishwa. Vile vile hasa Biblia ilivyosema ingetendeka katika siku hii, inatendeka, siku baada ya siku.

Mambo yanatukia na kutendeka upesi sana hivi kwamba hatuwezi hata kufuatilia jambo hilo. Tuko karibu sana na kule Kuja kwa Bwana wetu Yesu; kuunganishwa Naye, ambapo Neno linafanyika Neno.

Pamoja na mambo haya yote yanayotukia kutuzunguka pande zote, HATUJAWAHI KAMWE KUWA NA FURAHA, kuridhika zaidi ama kutosheka zaidi hivi. Mioyo na nafsi zetu zinabubujika kwa furaha isiyotamkika na iliyojaa utukufu. Ni kitendawili.

Tunapata faraja kuliko wakati mwingine wo wote ule, tukijua kwamba tangu mwanzo kabisa, tulichaguliwa tangu zamani kuwa mwana na binti wa Mungu.

SISI ni Bibi-arusi mwadilifu wa Kristo, aliyeoshwa kwa Damu ya Kristo. Mwana wa Mungu wa thamani, mwadilifu, asiye na dhambi akiwa amesimama na Bibi-arusi Neno asiye na doa, asiyeghoshiwa, aliyemwosha kwa Maji ya Damu Yake Mwenyewe. Sisi tulichaguliwa tangu zamani katika kifua cha Baba kabla ya mwanzo wa wakati; kama vile alivyokuwa Yeye ….UTUKUFU!! HALELUYA!

Sisi si hivyo tu tulivyo, lakini hivi karibuni tunaenda kwenye arusi huko mbinguni, tukiwa tumevaa utepe wa arusi ya waliochaguliwa tangu zamani. Alitujua SISI…Hebu tafakari tu juu ya hilo, ALITUJUA kabla ya kuwekwa misingi ya ulimwengu, kwa hiyo akatuvisha utepe wa arusi PALE na akaliandika JINA LETU KWENYE KITABU CHAKE CHA UZIMA CHA MWANA-KONDOO, si tu kusamehewa, bali KUHESABIWA HAKI.

Kuna njia moja tu ya kuwa na haya yote, yakubidi uje kwa Njia pekee iliyoandaliwa na Mungu. Neno la asili, BONYEZA PLAY.

Tunashukuru sana tunao Ufunuo huu. Ni wazi sana kwetu. Mwili na damu havikutufunulia jambo Hilo, lakini Baba yetu wa Mbinguni na hakuna maneno katika msamiati wetu wa kumwelezea jinsi tunavyompenda Yeye kwa ajili ya Jambo hilo….NEEMA YA AJABU.

Hakuna cha kulinganishwa na kuisikia Sauti ya Mungu ikikuzungumzia mdomo kwa sikio. Furaha inayofurika mioyo yetu. Hakuna kushangaa, hakuna kubahatisha, hakuna, hata si kutumaini, TUNAJUA, NI BWANA ASEMA HIVI. Huwezi kuwa na uhakika huo wa 100% mahali pengine popote isipokuwa kwenye kanda.

Ningependa kukualika uje uungane pamoja nasi tunapoisikia Sauti ya Mungu ikituambia yote kuhusu siku tunayoishi, wakati yeye anaponena kupitia nabii-tai Wake mwenye nguvu na kutuletea Ujumbe: Kimulimuli Chekundu cha Dalili ya Kuja Kwake 63-0623E.

Tutakusanyika kutoka kote ulimwenguni saa 6:00 SITA MCHANA, saa za Jeffersonville ( ni saa 1:00 MOJA JIONI ya Afrika Mashariki). Kama huwezi kuungana nasi pamoja, popote pale ulipo, lo lote lile ufanyalo, Bonyeza Play na uyasikie Maneno ya Uzima wa Milele.

Ndugu. Joseph Branham

Maandiko ya kusoma kabla ya kusikiliza Ujumbe:

Mathayo 5:28 / 22:20 / Sura ya 24 yote
2 Timotheo Sura ya 4 yote
Yuda 1:7
Mwanzo Sura ya 6 yote

23-0917 Kusimama Katika Pengo

UJUME: 63-0623M Kusimama Katika Pengo

PDF

pakua – m4a

pakua – amr

BranhamTabernacle.org

Wapendwa Wateule,

Bwana wetu Yesu anatupenda sana, hata ikampendeza Yeye kututumia nabii katika siku yetu. Mmoja yule ambaye alimwamini asilimia mia moja. Mmoja yule Yeye angeweza kuja na kuishi ndani yake, ili aweze kujifunua Mwenyewe kupitia ule mwili wa mwanadamu kumwita Bibi-arusi Wake.

Nabii wake alitupenda sana hata akatuahidi, sisi, na Mungu, ya kwamba Ujumbe wo wote mpya ungetoka kwenye maskani yake ndogo. Angeurekodi, kuuhifadhi, ili Bibi-arusi wa Mungu apate Chakula cha Kiroho cha kufanyia karamu, hata alipokuwa ameondoka.

Mungu alimpenda malaika-nabii Wake sana Yeye alimsaidia nabii Wake kulitimiza neno lake kwetu.

Baada ya Mungu kunena kupitia malaika Wake mwenye nguvu na kuifunua kikamilifu na kutufasiria sisi Biblia nzima, ndipo akakifungua kilele cha Mwamba ulio kama piramidi, ambao hata haukuandikwa, na kulifunua hilo kwa malaika Wake, ili aweze kutupa sisi siri Zake zote zilizofichwa, Bibi-arusi Wake.

Mungu hata alitoa ono kwa Ndugu Roberson, ambapo aliona Nguzo ya Moto ikimtwaa nabii Wake na kumpeleka Magharibi, kisha ikamrudisha na kumweka mbele ya Meza ambapo alikuwa amekwisha badilishwa.

Ndipo Roho Mtakatifu akanena na kumwambia,
“Huyu ni mtumishi Wangu. Nami nimemwita kuwa nabii kwa wakati huu, kuwaongoza watu kama tu Musa alivyofanya. Naye amepewa mamlaka, angeweza kunena kitu kiwepo.”

Wito wa Musa ulikuwa ni upi? Yeye alipaswa kufanya kitu gani? Mungu alikuwa amemwagiza Musa kuwaongoza watu hadi nchi ya ahadi. Lakini waliinuka watu waliokuwa wameamua kwamba wangeingilia agizo ambalo Mungu alimpa Musa, wakisema, “Umejitwalia madaraka mengi mno wewe. Wewe, ukijaribu kujifanya mtu wa pekee katika kundi hili ambaye ana mamlaka yote.”

Tendo hili lilimuudhi Mungu sana mpaka akamwambia Musa, “Jitenge ukaondoke miongoni mwao. Nitaliua tu kundi hilo lote, na kuanza kizazi kipya kwako.” Naye Musa akaanguka mbele za Mungu na kusema yeye itambidi kuja juu yake.

Kama Mungu angeamua kuwaangamiza watu katika siku yetu, ni nani angesimama kama Musa kwa ajili ya watu? Tungempata wapi mtu ambaye angesimama, au angeweza kusimama, ambaye Mungu angemkubali kama Yeye alivyomkubali Musa? Kuna maisha ya mtu mmoja tu duniani yaliyo muhimu sana kwa Mungu kuizuia hasira yake, malaika wake wa saba mwenye nguvu.

Mungu daima amekuwa na mpango. Bibi-arusi Wake atautambua mpango huo naye atadumu nao Neno kwa Neno. Wao wanajua inawabidi wadumu na Sauti hiyo ambayo Mungu ameichagua kuwaongoza kufika kwenye Nchi ya Ahadi.

Mungu alinena kupitia nabii wake naye akatoa nafasi ya kutosha ya kwenda mwelekeo tofauti upendao, kama vile Nuhu alivyowafanyia yule njiwa na kunguru ndani ya safina. Lakini kama tu vile njiwa ambaye daima alirudi ndani ya Safina, Bibi-arusi daima atarudi kwenye Ujumbe, Sauti hiyo, KANDA.

Nabii wa Siku yetu alikuwa nani? Kumekuwa na manabii wenye nguvu hapo awali ambao Mungu alikuwa amewaita na kuwatuma kuongoza watu wake kote katika nyakati: Ibrahimu, Musa, Eliya, Elisha, lakini hakuna hata mmoja wao aliyekuwa kama huyu nabii mwenye nguvu wa siku yetu. Yeye Aliitwa kuwepo kwenye huduma ya juu zaidi kuliko hao wote. Yeye ndiye ambaye Mungu alimchagua kufunua siri zake zote. Yeye ndiye ambaye Mungu alimchagua kunena kitu fulani kiwepo pasipo na kitu. Yeye ndiye aliyechaguliwa kufunua Mvuto wa Tatu. Yeye ndiye ambaye Mungu alimchagua kumwongoza Bibi-arusi Wake.

Sisi ni watu waliobarikiwa jinsi gani, Bibi-arusi mteule wa Mungu. Tunawezaje kushushwa chini? Tunawezaje kuwa na huzuni? Shetani anajaribu kutukatisha tamaa, lakini tunao ushindi, tuko ndani tumetiwa muhuri, salama ndani ya Safina. Milango imefungwa. Hakuna kinachoweza kutudhuru. Sisi ni Adamu Wake aliyerejeshwa.

Anakuja kwa ajili yetu, Bibi-arusi Wake mteule. Kutakuwa na baadhi yetu ambao haitawalazimu kuonja kifo, lakini watabadilishwa mara moja, kufumba na kufumbua. UTUKUFU!!

Kama vile kila mmoja wenu, nimechangamshwa sana, wakati kila siku, Neno Lake, Ufunuo wangu aliyonipa, unazidi kuwa mkuu zaidi na zaidi. Niko chini ya matarajio makubwa. Ikiwa Yeye hatakuja leo, huenda kesho, lakini najua Yeye yuaja hivi karibuni sana na Anakuja KWA AJILI YANGU NA KWA AJILI YAKO.

Njoo uungane nasi Jumapili saa 06:00 SITA MCHANA, saa za Jeffersonville,( ni saa MOJA JIONI ya Afrika Mashariki ), tunaposikia Chakula ambacho kimehifadhiwa mahali pamoja padogo tunapotazama na kusikia: Kusimama Katika Pengo 63-0623M. Tutauanza Ujumbe huu kwenye namba ndogo ya 27.

Ndugu. Joseph Branham

Maandiko ya Kusoma Kabla ya Kusikiliza Ujumbe:

Hesabu 16:3-4

23-0910 Muhuri Wa Saba

UJUME: 63-0324E Muhuri Wa Saba

PDF

pakua – m4a

pakua – amr

BranhamTabernacle.org

Mpendwa Bibi-arusi wa Kanda,

Ni siku ya namna gani tunayoishi! Ni wakati mkuu jinsi gani! Zile siri, mafumbo, yote yanayofunuliwa kwetu kila siku. Hatuoni tu yale ambayo tumeyapita, tunajua ile saa hasa tunayoishi na yale hasa yaliyo mbele.

Tunaambiwa mstari kwa mstari kile kitakachotokea. Yeye anatuambia waziwazi sisi ni nani, ni akina nani watakaokuwapo kule, na hata kile tutakachofanya. Wale Wayahudi 144,000, lile kanisa lililotakaswa kwa Dhiki, watenda kazi katika mashamba ya mizabibu ambao watakaoleta heshima na utukufu wao katika mji ule.

Lakini basi anatuambia huyo hatakuwa wewe…loo la, wewe ni Bibi-arusi Wangu, uko pamoja Nami katika Mji ule. Wewe hutakuwa huko nje ukifanya kazi katika mashamba ya mizabibu, wewe ni kipenzi changu. Wewe u Malkia Wangu pamoja Nami, Mfalme wako. Ninyi ndio wale moja ya mia ya hao moja kwa tano niliyowachagua kabla ya kuwekwa misingi ya ulimwengu. Nimepatengeneza Mahali hapa KWA AJILI YENU TU…NA JINSI TU MNAVYOLIPENDA.

Kuwazia tu, tunakusanyika kuizunguka Meza yake anapozungumza nasi wiki baada ya wiki, siku baada ya siku, saa baada ya saa, akitufunulia Neno Lake lote la ajabu. Yeye anatuambia tena na tena sisi ni nani; jinsi gani Yeye anavyotupenda; kile kilichokuwa, kile kilicho sasa, na kile kitakachotukia.

Hakuna maneno ya kuelezea jinsi inavyomaanisha kwetu, ama jinsi tunavyojisikia wakati tunapomsikia Yeye akituambia mambo haya. Wakati Tunapobonyeza Play na kuisikia Sauti hiyo, tunaondoka katika ulimwengu huu na mara moja tunaketi katika ulimwengu wa Roho pamoja Naye. Nafsi zetu zinafarijiwa. Tunajisikia Roho Mtakatifu akijaza utu wetu wote kwa Roho Wake. Ni furaha isiyoweza kuelezeka. Mungu anazungumza NASI. Kila Neno lililonenwa kwenye kanda hizo, Yeye alinena kwa ajili yetu. Yeye anajua hasa kile ambacho tungehitaji kusikia na wakati ambao tuliyohitaji kulisikia… na mara nyingi tunahitaji kulisikia tena na tena…. na kila wakati HUFURIKA NAFSI ZETU.

Sisi hatuchoki kumsikia yeye akituambia kuhusu Maono, Ndoto, Bwana Asema Hivi, ng’ambo ya pazia, akituona sisi tumevaa nguo ndefu nyeupe, Mvuto wa Tatu, kuwaumba kindi, Ule Upanga wa Mungu uliyoenea mkononi mwake barabara, chakula kilichohifadhiwa, tukiwa tumewekwa kwa Mkuu wa Meza, Ngurumo, Malaika wenye nguvu wakija na kumtwaa juu, yule malaika wa saba wakipekee aliyemaanisha kitu cha zaidi kwake, ishara ya milele ya vilele saba vya milima vinavyoendeleza herufi BRANHAM, semeni tu hasa yale yaliyo kwenye kanda hizo, ninayo Maneno ya kutoweza kukosea, Yeye ameitiwa wito wa juu zaidi, nitawaambia UFUNUO WANGU, Mimi ni Sauti ya Mungu kwenu, shikilieni kabisa hayo mafundisho ya kanda, nitawaita BIBI-ARUSI, aiko, iyo, dafuta… sisi tunayapenda YOTE.

Hili ndilo ono langu. Sauti ya Mungu iliyo kwenye kanda ndio Mapenzi makamilifu ya Mungu, MWISHO WA MANENO. Kuzicheza kanda ndio Mapenzi makamilifu ya Mungu, MWISHO WA MANENO. Wewe unaweza kuwasikia wahubiri, waalimu, mitume, manabii, wachungaji, LAKINI kanda ndizo, na zinatakiwa kuwa, Sauti iliyo muhimu sana unayotakiwa kuisikia, MWISHO WA MANENO. Sauti iliyo kwenye kanda ndio Sauti pekee ambayo Mungu Mwenyewe aliyosema, MSIKIENI YEYE, MWISHO WA MANENO.

Ndugu na dada zangu, simpingi mtu ye yote, Mimi niko kwa ajili ya Sauti hiyo tu. Inatupasa, na mimi, nawapenda wote wanaotangaza kwamba wanapenda na kuamini Ujumbe huu. Hata kama mnajisikia kwamba ninawaambia watu vibaya kuwaambia kubonyeza play, Ninawapenda na ninaamini mnanipenda. Sote tunataka kuwa katika Mapenzi yake Makamilifu. Tafadhali endelea kufanya yale Mungu aliyokuitia kufanya; hubiri, fundisha, kuwa mchungaji, wewe liambie tu kundi lako ni Sauti gani iliyo muhimu sana wanayotakiwa kuisikia.

Ni Sauti hiyo tu iliyo kwenye kanda isemayo jambo lile lile KILA WAKATI. Haibadiliki kamwe. Bibi-arusi anaweza TU KUSEMA AMINA kwa kila Neno lililo kwenye kanda, lakini Bibi-arusi hawezi kusema AMINA kwa kila neno ambalo mwanadamu ye yote asemalo, MWISHO WA MANENO.

Kama huamini jambo hilo, wewe si Bibi-arusi. Ikiwa unaamini jambo hilo, basi hutakuwa na shida kuwaambia kundi lako kwamba kuzisikiliza kanda ndiyo Sauti iliyo muhimu zaidi wanayotakiwa kuisikia.

Kwa Mimi kutoa kauli hizi nimesikia kutoka kwa wahudumu wengi tofauti ambao wanasema kwamba ninawaambia watu wasiwasikilize wachungaji wao na kuyaacha makanisa yao, HIYO SI KWELI. Siwezi kusema jambo hilo na siamini jambo hilo.

Ni kweli wengi wanasema mambo ambayo sijawahi kamwe kusema, wala kuamini. Siwezi kuwajibishwa kwa ajili yao, lakini tu kwa yale niliyosema na yale ninayoamini. Nimezungumza waziwazi na kuyaweka katika mfumo wa barua yale ninayoamini. Wao / ninyi mnapindisha kwa manufaa yenu yale ninayosema /na ninayomaanisha.

Bibi-arusi wote watakuwa wakisema jambo lile lile. Hakuna watu wawili wasemao jambo lile lile. Sauti Moja. Nabii mmoja. Bibi-arusi Mmoja.

Mimi Siamini kwamba yakubidi kuusikia Ujumbe kwa wakati mmoja kabisa, kama wanavyofanya waamini wengi ulimwenguni kote, ili uwe Bibi-arusi Wake, lakini Naamini unapaswa kuisikia Sauti ya malaika-mjumbe wa saba Jumapili asubuhi…ipe hiyo sauti nafasi ya KWANZA.

Unaalikwa kusikiliza pamoja nasi: Muhuri wa Saba 63-0324E, Jumapili saa 06:00 SITA MCHANA, saa za Jeffersonville, ( ni saa 1:00 MOJA JIONI ya Afrika Mashariki) Wakati sehemu ya Bibi-arusi kutoka kote ulimwenguni watakaposikia Sauti hiyo kwa wakati mmoja kabisa.

Ndugu. Joseph Branham

Maandiko ya kusoma kabla ya Kusikiliza Ujumbe:

Kumbukumbu la Torati 29:16-19
1 Wafalme 12:25-30
Ezekieli 48:1-7, 23-29
Mathayo 24:31-32
Ufunuo 7 yote
Ufunuo 8:1
Ufunuo 10:1-7
Ufunuo 14 yote

23-0903 Maswali Na Majibu Juu Ya Mihuri

UJUME: 63-0324M Maswali Na Majibu Juu Ya Mihuri

PDF

pakua – m4a

pakua – amr

BranhamTabernacle.org

Mpendwa Ndugu Branham,

Ninaamini kwa moyo wangu wote wewe ndiye malaika-mjumbe wa Saba wa Mungu aliyetumwa kumwita Bibi-arusi Wake atoke. Wewe ni Sauti ya Mungu uliye na Bwana Asema Hivi kwa ulimwengu. Ninaamini wewe ndiye yule aliyemchagua kumfunulia siri zote za Biblia. Ninaamini kila Neno unalosema kwenye hizo kanda.

Nina swali moyoni mwangu ambalo ningependa kukuuliza. Kuna watu wengi sana, sauti nyingi sana, zinazosema mambo mengi tofauti kuhusu kile tunachopaswa kufanya ili kuwa Bibi-arusi wa Kristo. Ninataka kuwa katika Mapenzi yake makamilifu. Nataka kuwa na Imani kamilifu. Simpingi mtu yeyote, lakini nataka kusikia wewe unasemaje.

Ni kitu gani kitakachomkusanya Bibi-arusi pamoja na kutupa Imani ya kunyakuliwa tunayohitaji?

Nami naamini ya kwamba, kupitia Ngurumo hizo Saba, zitafunuliwa katika siku za mwisho ili kumkusanya Bibi-arusi pamoja kwa ajili ya kupata imani ya kunyakuliwa.

Ndugu Branham, Je, zile Ngurumo Saba ambazo ni sawa na siri saba zimekwisha kufunuliwa? Je, zilifunuliwa katika zile Muhuri Saba, ila bado hazijajulikana kwetu kama zile Ngurumo?

La, zilifunuliwa katika zile Muhuri Saba; hivyo ndivyo zile ngurumo zilivyokuwa. Ilibidi zifunue…Zile Ngurumo Saba zilizotoa sauti zao na hakuna ye yote angetambua ilikuwa nini…Yohana alijua zilikuwa nini, lakini yeye alikatazwa kuandika habari zake. Yeye alisema, “Bali yule malaika wa saba, katika siku za kupiga baragumu yake, zile siri saba za zile Ngurumo Saba zitafunuliwa.” Na yule malaika wa saba ndiye mjumbe wa ule Wakati wa Saba wa Kanisa.

Utukufu kwa Mungu. Hilo hapo jibu langu. Siri ya zile Ngurumo Saba imefunuliwa. Ni Sauti ya Mungu iliyo kwenye kanda na sasa inamuunganisha Bibi-arusi pamoja na kutupa ile IMANI YA KUNYAKULIWA, tunayohitaji.

Asante, Ndugu Branham, kwa kujibu swali langu. Nilijua kuwa jibu la swali nililokuwa nalo moyoni mwangu lingekuwa kwenye kanda.

Hayo ndiyo yote ninayohitaji kujua. Nitaendelea Kubonyeza Play kila siku na kupokea IMANI YA KUNYAKULIWA zaidi.

Njoo upokee Imani ya Kunyakuliwa pamoja nasi Jumapili hii saa 6:00 SITA MCHANA, saa za Jeffersonville, ( ni saa 1:00 MOJA JIONI ya Afrika Mashariki ) tunaposikia: Maswali na Majibu Juu ya Mihuri. 63-0324M.

Ndugu. Joseph Branham