21-1121 Kiu

UJUMBE: 65-0919 Kiu

PDF

pakua

BranhamTabernacle.org

Tai wanakusanyika Pamoja.

Mpendwa Bibi Mteule,

Muungano mkuu wa mwisho unafanyika kwa ajili ya Unyakuo. Roho Mtakatifu anamleta Bibi-arusi Wake pamoja kutoka katika mataifa yote; kutoka Pwani ya Magharibi hadi Pwani ya Mashariki, kutoka Kaskazini hadi Kusini, kutoka pembe nne za dunia.

Anatukusanya pamoja katika makanisa yetu na katika nyumba zetu kupitia Mawimbi Bora sana. Ni bora hata zaidi kuliko njia ya kurusha matangazo. Ni mawasiliano ya simu. Tunaweka vipokezi au maikrofoni, ama chochote kile, katika chumba, na ni sawa sawa tu na kusimama katika chumba pamoja na nabii Wake. Ni njia iliyoandaliwa na Mungu kwa ajili ya siku hii kumuunganisha na kumleta Bibi-arusi Wake pamoja na, “Bwana Asema Hivi”.

Miaka hamsini na sita iliyopita, Mungu alianza mpango wake wa kuwakusanya Bibi-arusi Wake pamoja ili waweze kumsikia akinena kupitia malaika Wake mwenye nguvu kwa wakati mmoja. Hata aliifanya huduma tano yake kusitisha kuhudumu na kuwakusanya watu wao pamoja, nao Wakajiunganisha Kwa Radio katika makanisa yao, kwani alitaka Bibi-arusi Wake aisikie Sauti Yake wote kwa wakati mmoja. Mpango wake mkuu ulikuwa umeanza. Haijawahi kamwe kuwezekana katika historia ya ulimwengu. Nabii wake alijua jambo Hilo na alifurahishwa sana. Sasa Mungu angeweza kusema moja kwa moja na Bibi-arusi Wake wote kwa wakati mmoja. Wote wangeweza kusikia wenyewe, Mungu akizungumza nao moja kwa moja, na haingehitaji fasiri yoyote.

Leo, ulimwengu uko katika mshangao. Kwa nini watu kutoka duniani kote, wakiwa na majira tofauti ya maeneo Yao ; 6:00 sita mchana., 8:00 Nane mchana., 2:00 mbili usiku., usiku wa manane, wanakusanyika pamoja wote kwa wakati mmoja ili kusikia Ujumbe ambao wanaweza kusikiliza wakati wowote. Nini kinachovutia?

Imefunuliwa kwao kwamba huu ni mpango wa Mungu, njia iliyotolewa na Mungu ya kuwaunganisha kiroho. Ni Mungu akitayarisha kuzungumza na Bibi-arusi Wake wote kwa wakati mmoja.

HAKUNA kingine ila Sauti ya Mungu, Neno Lake, Ujumbe Huu, ulionenwa na nabii Wake ungeweza kufanya hivyo. Hakuna mtu, wala kitu kingine chochote, ambacho Bibi-arusi wote wanaweza kukubaliana kwacho.

Mtu fulani anaweza kusema, “Mimi humsikiliza mchungaji wangu anaponukuu na kuhubiri Neno kama tu vile Ndugu Branham alivyosema afanye.” Bwana asifiwe. Hilo ni zuri na umebarikiwa sana kuwa na mchungaji anayedumu na Neno. Ameitwa kuweka kundi pamoja na kukupa na kukuelekeza kwenye Neno, Lakini hilo silo ninalozungumzia. Huna budi kuwa na Yakini, Neno la mwisho. Maneno Ambayo SOTE TUNAWEZA KUKUBALIANA KWAYO. Kadiri alivyoitwa na kupakwa mafuta jinsi mtu ye yote awezavyo kuwa, hakuna neno la mtu yeyote ambalo ni kamilifu, na hakuna huduma ya mtu yeyote inayoweza kumuunganisha Bibi-arusi.

“Hilo ni wazo lako tu na maoni yako. Thibitisha hilo kwa Neno, Ndugu Joseph”.

Kwa sababu ukiwa na watu wawili, una maoni mawili . Yapasa kuwe na yakini Moja ya mwisho , na yakini yangu ni Neno, Biblia . kama mchungaji hapa wa kanisa, Yakini yangu ni Neno, nami ninataka … ninajua ninyi, ndugu zetu, kwa namna fulani
mnanichukua mimi kama Yakini yenu kwa yale…mradi ninamfuata Mungu kama Paulo alivyosema katika Maandiko, “Mnifuate mimi kama ninavyomfuata Kristo .”

Hivyo basi, wakati nabii anaponena, ni Yakini kwa Bibi-arusi. Ujumbe Wake si neno lake yeye, wala si fasiri yake yeye ya Neno. Ni Mungu akifasiri Neno Lake Mwenyewe kwa njia Yake pekee aliyoiandaa ya kufanya hivyo: kwa nabii Wake.

Ikiwa unasema unaamini Ujumbe Huu.
Ikiwa unasema unaamini nukuu hii.
Ikiwa unasema na kuamini kuwa wewe ni Bibi-arusi wa Kristo, Basi kile kilichonenwa kwenye kanda lazima kiwe Yakini Yako.

Hivi, ni nini kingine kinachoweza kumleta Bibi-arusi wa Kristo wote pamoja isipokuwa Yakini yetu? HAKUNA KINGINE. Hizo Kanda ni Sauti Yake, Neno Lake, Yakini Yetu. Nabii alituambia kwamba nabii Kwa ajili ya wakati huu ni Roho Mtakatifu. Roho Mtakatifu huchagua mtu MMOJA, Sauti MOJA kufunulia Neno Lake na Sauti hiyo inamuunganisha Bibi-arusi Wake kwa njia Yake aliyoiandaa kwa ajili ya siku hii, KWA KUBONYEZA PLAY .

Ninajaribu sana niwezavyo kudumu kwa unyofu na Neno , kwa ajili ya hawa ambao wamewekwa mikononi mwangu kwa ajili ya Mungu , maana kondoo huhitaji chakula cha kondoo, bila shaka. “Kondoo wangu huisikia Sauti Yangu.” Na hilo ndilo tunaloishi kwalo, kila Neno litokalo…Si yote…Si Neno moja mara hii na mara nyingine; bali kila Neno litokalo kinywani mwa Mungu, hilo ndilo ambalo watakatifu wanapaswa kuishi kwalo.

Tunapaswa kuishi kwa kila Neno litokalo katika kinywa cha Mungu. Je, kinywa cha Mungu kilichothibitishwa kwa ajili ya wakati huu ni kipi? Mimi? Mimi si Malaika- Mjumbe wa 7 wa Mungu aliyethibitishwa , wala kinywa Cha Mungu si mchungaji wako wala mtu ye yote yule; Ni Mungu akitumia sauti ya WILLIAM MARRION BRANHAM.

Tutahukumiwa kwa Ujumbe ALIONENA kwenye kanda. Si kwa Fasiri ya mtu mwingine ye yote ama kuhubiri kile alichonena, Bali kwa Neno KWENYE KANDA. Kama wapakwa mafuta na Roho Mtakatifu jinsi tuwezavyo kuwa, tunaweza kukosea. Sisemi muhudumu yeyote ni wa uwongo au amekosea; tumeitwa kuhubiri, na kufundisha, na kukaa na Neno, Lakini wito wetu ni kuwaelekeza ninyi KWENYE NENO, na NENO PEKEE LILILOTHIBITISHWA KIKAMILIFU liko kwenye Kanda.

Tunayo mengi sana, kama Bibi-arusi wa Kristo, ya kushukuru.

je kama tungaliijaza bahari kwa wino, Na kama mbingu zote zimetengenezwa kwa karatasi; Kama kila shina duniani lingekuwa ni kalamu, Na kila mtu awe kazi yake ni mwandishi; Kuuandika upendo wa Mungu aliye juu Kungeikausha bahari yote; Ama kama gombo hilo lingechukua nafasi yote, Hata kama limetandazwa kutoka mbingu hadi mbingu.

Tunakaribia kuwa na juma kuu la Shukrani la maishani mwetu.
Sikukuu ya Chakula cha Kiroho cha kujaza Nafsi. Sikukuu ambapo Bibi-arusi ataungana na kuketi pamoja katika Uwepo wa Jua kuivishwa.

Mungu atanena kupitia mjumbe wake na kutuambia:

. Sisi ni Bibi Mteule wake.

. Majina yetu yako kwenye Kitabu cha Uzima cha Mwana-Kondoo.

. Hatuna dhambi.

. Tulihesabiwa haki kabla ya kuwekwa misingi ya ulimwengu.

. Sisi ndio walioitwa watoke na wateule.

. Sisi ndio ambao mpango mzima wa Mungu umekuwa ukingojea.

. Sisi ni Bibi-arusi safi, mwema, asiye na dhambi wa Mwana wa Mungu aliye hai.

. Sisi ni wakamilifu mbele zake.

Hakuna mwisho wa kuyaandika yale yote ambayo Roho Mtakatifu anakwenda kutufunulia na kututendea.

Nena kuhusu Shukrani !!!

Nimehisi kushinikizwa katika Roho yangu kutoka kwa Bwana ili tuweke wakfu juma zima, kuanzia Jumapili hii, kwa ajili ya Shukrani kwa Bwana.

Iliyoambatishwa hapa ni kalenda yenye siku, masaa na Jumbe tutakazosikia.

Kama unavyoweza kuona, Jumapili sote tutaungana pamoja katika muda wetu wa kawaida wa saa 8:00 Nane mchana, saa za Jeffersonville, ( ni saa 4:00 nne usiku ya Tanzania) , ili kusikia Ujumbe: Kiu 65-0919.

Jumatatu Hadi Jumatano , ningependa tusikie Jumbe 3 zinazofuata ambazo Ndugu Branham alizileta katika mfuatano, mwaka wa 1965. Tutakuwa tukizituma kwenye Voice Radio (Radio ya Sauti, iliyopo kwenye app ya Lifeline ya vgr ) saa 3:00 tatu Asubuhi saa za Jeffersonville,( ni saa 11:00 kumi na Moja jioni ya Tanzania) na tena saa 1:00 Moja jioni, saa za Jeffersonville,( ni saa 9:00 Tisa usiku ya Tanzania).

Najua itakuwa vigumu kwa wengi kusikiliza kwa wakati uliowekwa kutokana na ratiba zao za kazi au majukumu mengine, lakini tunatumai mnaweza kusikiliza wakati mmojawapo Kwa pamoja na familia zenu.

Kisha Alhamisi , mwezi wa 11, tarehe 25, ningependa tuungane pamoja saa 8:00 Nane mchana, saa za Jeffersonville, ( ni saa 4:00 nne usiku ya Tanzania ) kuanza wikendi yetu nzuri ya Kutoa Shukrani tunapounganishwa tena ili kusikia Sauti ya Mungu ikituletea Ujumbe wa kwanza wa wikendi yetu: Muungano Usioonekana wa Bibi-arusi wa Kristo 65-1125.

Ilikuwa ni baraka ya pekee kwangu kutambua itakuwa miaka 56 iliyopita, hadi siku ya leo, ambapo Mungu alinena kupitia nabii Wake kutuletea mfululizo huu wa Jumbe. Ilikuwa pia miaka 56 tangu kuzaliwa kwa Ndugu Branham mwaka wa 1909, hadi mwaka wa 1965, ambapo alizinena Jumbe hizi.

Tungefanya nini kama tungejua Ndugu Branham atakuwepo Shreveport, LA wikendi hii ili kutuletea Jumbe hizi? Hakuna ….Namaanisha HAKUNA kitu kingaliweza kutuzuia kwenda. Mungu ana mpango kwa ajili ya Bibi-arusi Wake leo, na HAKUNA kitakachotuzuia.

Naamini kila mmoja wenu Yuko chini ya matarajio makubwa kwa juma hili zuri tutakalokuwa pamoja na Bwana; kumshukuru, kumsifu na kumwabudu kwa ajili ya yote aliyoyafanya, na yote anayokwenda kufanya kwa ajili ya kila mmoja wetu, BIBI MTEULE WAKE.

Ndugu. Joseph Branham