All posts by admin5

24-0114 Yeye Aliye Ndani Yenu

UJUMBE: 63-1110E Yeye Aliye Ndani Yenu

PDF

pakua – m4a

pakua – amr

BranhamTabernacle.org

Wapendwa Waamini wenye Imani Kamilifu,

Kila siku mioyo yetu inaenda mbio kwa matarajio makubwa. Tunangojea ile saa ifike ya kule Kuja Kwake hivi karibuni. Hofu zote zimetoweka. Hakuna kujiuliza-uliza tena, “Je! sisi ni Bibi-arusi Wake”? Imetiwa nanga ndani ya mioyo yetu zaidi ya hapo nyuma, SISI NI BIBI-ARUSI WAKE.

Tumeshikwa katika hali ya Kimbinguni, tukisikiliza huduma ya Yesu Kristo, aliyefanyika mwili upya katika Kanisa Lake. Ujumbe huu umethibitishwa kotekote na Neno la Mungu, hivi kwamba hawezi kuwa ni mwanadamu, haina budi kuwa ni Mungu akinena mdomo kwa sikio na Bibi-arusi Wake.

Sisi tunaamini si mwanadamu anayenena nasi kwenye kanda hizi, ni Mungu.

Ninachojaribu kusema, “Usife moyo.” Usimruhusu Shetani akuambie ubaya kunihusu mimi; sababu ana mengi. Bali wewe shikilia matumaini hayo; sababu, usipoyashikilia, haitatendeka. Usiniangalie mimi, kama mwanadamu; mimi ni mwanadamu, nimejaa makosa. Bali tazama yale ambayo ninayosema kumhusu Yeye. Ni Yeye. Yeye Ndiye.

Yakubidi kuamini na kuwa na matumaini katika yale ANAYOSEMA, LA SIVYO HAITATENDEKA. Hatumwangalii nabii wa Mungu kama mwanadamu, kama wengi wanavyofikiri tunafanya hivyo. Tuko nyuma ya pazia la mwili wa mwanadamu, na yote tunayoyaona na kusikia ni Mungu akinena kupitia midomo ya mwanadamu, NA TUNAYO MATUMAINI NA KUAMINI KILA NENO.

Huo ndio Ufunuo wa Yesu Kristo kwa ajili ya siku hii. Kuamini kuwa ni Mungu, si mwanadamu, anayenena kwenye kanda. Ukilikosa jambo hilo, rafiki, umeukosa Ujumbe wa wakati huu na huwezi kuwa Bibi-arusi.

Shetani anaweka fasiri yake kwenye jambo hilo, na asilimia 99% ya wakati ananukuu Ujumbe kama tu vile alivyomfanyia Hawa, bali Hawa aliamriwa kukaa na Neno; yale Adamu aliyomwambia ndio Mungu aliyosema, si yale ambayo mtu mwingine aliyosema ati yalimaanisha. Hawa alipaswa kukaa na Sauti ya Mungu.

Hii ndio siku iliyo kuu ambayo ulimwengu umewahi kujua. Maisha ya Yesu Kristo, yale aliyoishi na kujifunua Mwenyewe katika maisha ya nabii Wake, sasa yanaishi katika mwili ndani YETU, Bibi-arusi Wake.

Tunafanya vile hasa Yeye alivyotuamuru kufanya: kukaa na Neno kwa kukaa na Sauti ya Mungu iliyo kwenye kanda. Ndio huduma ya kanda ya Mungu na mpango wa Mungu wa siku hii.

Ikiwa kweli unaamini William Marrion Branham alikuwa ndiye malaika-mjumbe wa saba aliyechaguliwa na Mungu, yule ambaye Mungu alimchagua kunena na kufunua siri zote zilizofichwa katika Neno, aliye Sauti ya Mungu kwa kizazi hiki, mtu aliyekuwa na imani kuliko mtu mwingine yeyote yule, yule ambaye malaika wa Bwana alimwambia “ikiwa utawafanya watu WAKUAMINI, hakuna kitu kitakachosimama mbele ya maombi yako”, basi Jumapili hii itakuwa siku kuu kuliko.

HAKUNA KITU ambacho kinachoweza kamwe kuuondoa Ufunuo wa Ujumbe Huu kwetu sisi, HAKUNA. Hatuwezi KAMWE kuutilia shaka. Kama Yeye aliusema, sisi tunauamini. Huenda tusiuelewe Wote, lakini tunauamini hata hivyo.

Yesu mwenyewe alituambia: “Yeye aliye ndani yenu ni mkuu kuliko yeye aliye katika ulimwengu.” hebu hilo na lizame mioyoni mwetu. Roho Wake anaishi ndani yetu. Je, twaweza kulishika hilo? Sasa hivi, unaposoma Barua hii, Roho Mtakatifu, Mungu Mwenyewe, Nguzo ya Moto, anaishi na kukaa ndani yetu? Tunajuaje kuwa hiyo ni kweli? MUNGU ALISEMA HIVYO!!

Shetani anaendelea kutuambia kwamba sisi ni watu walioshindwa. Na yuko sahihi, ndivyo tulivyo. Anatukumbusha, hatupo mahali tunapotakiwa kuwa katika Neno. Sahihi tena, hatuko. Tunafanya mambo tunayojua vyema kuliko kuyafanya. Tusamehe Bwana, yuko sahihi.

Lakini hata pamoja na makosa yetu yote, madhaifu yetu yote, kushindwa kwetu kote, haibadilishi ukweli wa mambo, SISI NI BIBI-ARUSI. TUNAAMINI KILA NENO!

Hatujitazami sisi wenyewe ama chochote tunachoweza kufanya, sisi ni mchafuko. Sisi tunajua tu kwamba Yeye alituchagua na kutupa Ufunuo wa Neno Lake na hakuna kitu kinachoweza kuuondoa Ufunuo huo kwetu. Huo umewekwa ndani ya mioyo na roho zetu.

Yeye alituambia inatupasa kuwa na IMANI KAMILIFU. Tunayo Bwana, IMANI KAMILIFU katika Neno Lako. Tuna imani katika Yale Nabii Wako aliyosema kuwa ni Bwana Asema Hivi. Si neno lake, bali Neno lako kwetu sisi.

Nabii Wako alituambia chochote tunachohitaji, kama tu tutaamini, na kuwa na imani katika Neno Lako, tunaweza kupata chochote tunachohitaji. TUNAAMINI.

Bwana, ninalo hitaji. Ninakuja mbele Zako nikiwa na imani yote niliyo nayo katika Neno Lako, kwa maana haiwezi kushindwa. Lakini leo, Bwana, siji mbele Zako nikiwa tu na imani yangu, bali na imani uliyompa malaika-mjumbe wako wa saba mwenye nguvu.

Ee Bwana Mungu, nakuomba uturehemu. Na jalia kila mwanamume na mwanamke ambaye ameketi sasa, ambaye ana namna yo yote ya maradhi au mateso; na kama vile Musa alivyojitupa mwenyewe katika pengo, kwa ajili ya watu, usiku wa leo ninaweka moyo wangu mbele Zako, Bwana. Na kwa imani yote niliyo nayo, ambayo iko ndani Yako, ambayo Wewe umenipa, ninawapa.

Nami ninasema: nilicho nacho, nawapa wasikizi hawa! Kwa Jina la Yesu Kristo wa Nazareti, kataeni magonjwa yenu, kwa sababu Yeye aliye ndani yenu ni mkuu, kuliko huyo Ibilisi anayejaribu kuyatwaa maisha yenu. Ninyi ni wana wa Mungu. Mmekombolewa.

Imekwisha. Neno Lake haliwezi kushindwa. Chochote tunachohitaji, tunaweza kukipokea.

Njooni muungane nasi Jumapili saa 6:00 SITA MCHANA, saa za Jeffersonville, ( Ni saa 2:00 MBILI USIKU ya Afrika Mashariki) kupokea baraka hii kuu na upako kutoka kwa Mungu pindi sehemu ya Bibi-arusi watakapokusanyika kutoka duniani kote kusikiliza Sauti ya Mungu akiweka IMANI yake pamoja na IMANI yetu.

Ndugu. Joseph Branham

63-1110E Yeye Aliye Ndani Yenu

24-0107 Nafsi Zilizo Kifungoni Sasa

UJUMBE: 63-1110M Nafsi Zilizo Kifungoni Sasa

PDF

pakua – m4a

pakua – amr

BranhamTabernacle.org

Wapendwa Watu Waliotengwa,

Mungu amekuja katika wakati wetu na kujifunua katika mwili wa mwanadamu, katika mtu aitwaye William Marrion Branham, ili aweze kulitimiza Neno Lake. Huo ndio Ufunuo wa Yesu Kristo katika wakati wetu.

Kuisikiliza Sauti hiyo na kuamini kila Neno ndiyo Njia pekee iliyoandaliwa na Mungu kwa ajili ya siku hii. Alituma ulimwenguni watu wengi waliopakwa mafuta na Roho wake Mtakatifu, lakini Yeye alituma na kunena kupitia mtu mmoja tu kufunua Neno Lake na kumwongoza Bibi-arusi Wake.

Yeye kamwe habadilishi Mpango Wake wala Njia Yake ya kufanya mambo. Jinsi alivyolifanya mara ya kwanza, Yeye hulifanya jinsi hiyo kila wakati. Yeye huwaongoza watu Wake Mwenyewe, kwa Nguzo ya Moto.

Usisahau kamwe, WEWE NI Bibi-arusi mteule wa Mungu na hakuna kitu shetani anachoweza kufanya au kusema ambacho kinaweza kuliondoa hilo kutoka kwako, HAKUNA! Alikuchagua wewe tangu asili kabla ya kuwekwa misingi ya ulimwengu. Alikujua tangu wakati huo, nawe ulikuwa pamoja Naye. Alijua jina lako. Alijua kila kitu kukuhusu. Alijua heri na shari zako. Alijua kushindwa kwako, makosa yako, na bado alikupenda na kukuchagua wewe kwa kuwa ulikuwa sehemu yake.

Nafsi yako inaweza tu kujilisha kwenye Neno Lake. Hakuna kinachoweza kukutosheleza ila Neno Lake. Unapenda kusoma Neno Lake na kumtafakari Yeye, ukiomba kutoka katika kilindi cha moyo wako. Unaposikia Sauti Yake ikizungumza nawe moja kwa moja, inakuinua hadi ng’ambo ya pazia la wakati. Kwa maana unajua umeketi naye katika ulimwengu wa roho wakati anaponena nawe mdomo kwa sikio, akifunua Neno lake, akikukumbusha, WEWE NI BIBI-ARUSI WANGU.

Ibilisi aweza kukutwanga na kukutwanga. Waweza kushushwa moyo sana wakati mwingine na kuhisi wewe ni aliye shindwa kabisa; ujisikie kana kwamba umemkosa Yeye zaidi ya yeyote yule. Wewe ndiye mbaya zaidi kuliko wabaya wote, lakini mahali fulani, chini kabisa ndani ya nafsi yako, unasikia ile Sauti Ndogo Tulivu ikikuambia: “Hakuna kitu kinachoweza kukutenganisha na MIMI, WEWE NI NENO LANGU. Nililiweka jina lako kwenye Kitabu Changu Cha Uzima cha Mwana-Kondoo, Mimi Mwenyewe .”

Naweza kusema nini kuwatia moyo leo?

Kaeni tu katika Neno. BONYEZENI PLAY kila siku na mwisikie Sauti ya Mungu ikisema Bwana Asema hivi na kuwaambia; Ninawaunganisha katika Neno Langu. Mnaweza kushinda CHOCHOTE, kwa maana Neno Langu linaishi na kukaa ndani yenu. Nimewathibitishieni, mnayo IMANI KAMILIFU. Mmeiweka ile Ishara, nayo imewaweka katika Kudhikika. Nitasimama nyuma ya Neno Langu. Nitafanya kile nilichosema kuwa nitafanya.

Maneno Yake ni ya ajabu jinsi gani anayosema nasi kwenye Kanda. Tunajua si mtu fulani, mtu wa kimwili ambaye yuko miongoni mwetu. Ni Mungu wa Milele anayezungumza nasi, Bibi-arusi Wake.

Mnaalikwa kuungana na Bibi-arusi Jumapili hii saa 06:00 MCHANA, saa za Jeffersonville,( Ni saa MBILI USIKU ya Afrika Mashariki ) tunapokusanyika kusikiliza ile Sauti Ndogo Tulivu:  63-1110M Nafsi Zilizo Kifungoni Sasa.

Ndugu. Joseph Branham

Maandiko ya kusoma kabla ya ibada:

Mwanzo 15:16
Mathayo 23:27-34
Yohana 4:23-24 / 6:49 / 14:12
1 Petro 3:18-22
2 Petro 2:4-5
Yuda 1:5-6

23-1231 Kukata Tamaa

UJUMBE: 63-0901E Kukata Tamaa

PDF

pakua – m4a

pakua – amr

BranhamTabernacle.org

Baba mpendwa,

Tumecheza muda mrefu vya kutosha. Tumehudhuria kanisa muda mrefu vya kutosha. Tangu kuusikia Ujumbe, ile Ishara, imemtupa Bibi-arusi Wako katika hali ya kudhikika.

Tunajua jambo fulani linakaribia kutukia. Wakati umekaribia. Tunataka Uje ututoe katika ulimwengu huu. Tunataka kuwa pamoja na Wewe. Tunahisi hali ya kudhikika ndani kabisa ya nafsi zetu.

Je! hivi tutalizungumzia tu? Je! tumedhikika vya kutosha? Je! tunakulilia Wewe mchana na usiku kama tunavyopaswa?

Loo, Kanisa, amka na ujitikise! Finya dhamira yako, amka katika saa hii! Hatuna budi kukata tamaa ama tutaangamia! Kuna jambo linalokuja kutoka kwa Bwana! Ninajua jambo hilo kwamba ni BWANA ASEMA HIVI. Kuna jambo linalokuja, na ni afadhali tukate tamaa. Ni kati ya uzima na mauti. Litapita katikati yetu wala hatutaliona.

Tunajua inahitaji hali ya kudhikika kukuleta Wewe jukwaani. Hatuna budi Tulipate sasa hivi ama tuangamie. Bwana, tujalie tudhikike kuliko hapo awali, ndipo utajitokeza jukwaani na kuja kumchukua Bibi-arusi Wako anayengoja.

Tusaidie Baba kujiingiza kwa nguvu. Si kutembea tu na kuingia ndani Yake kwa urahisi, bali kujiingiza ndani yake kwa nguvu. Sio tu kulizungumzia na kuendelea na maisha yetu ya kila siku. Tunataka kukutafuta kwa mioyo yetu yote, kwa roho zetu zote na kwa akili zetu zote. Bwana, tusaidie.

Tunajua tumekukosa mara nyingi, Bwana, lakini ulituambia kama tukishindwa, hilo halina uhusiano wo wote na jambo hilo; sisi ni wenye kushindwa kwanza, lakini tuna Wewe umesimama hapo na mkono wenye nguvu na unaweza kutushika chini na kutuinua juu ya maji.

Nabii alitutangazia ya kwamba Wewe ungepita juu yetu wakati tu unapoona ile Ishara ikiwa imewekwa. Bwana, tumefuata maagizo Yako na tumeiweka ile Ishara na kufanya nyumba zetu kuwa Kanisa la Kanda, tukisikiliza na kuamini kila Neno.

Yeye hutambua tu I—Ishara. Huo ndio Ujumbe wa wakati huu! Huo ndio Ujumbe wa siku hizi! Huo ndio Ujumbe wa wakati huu! Katika Jina la Yesu Kristo, upokeeni!

Sisi tuna Hakika kabisa, na tunaamini na kuweka kila kitu kulingana na yale nabii aliyotuambia.

Tunaamini kila kitu kinafanyika na hutokea kwa wakati Wako mkamilifu. Hakuna kitu kilicho nje ya mahali. Tumeiona miujiza Yako yote, nasi tumesikia na kuja chini ya ushahidi wa ile Ishara.

Sasa wakati tukiwa chini ya ushahidi wa ile Ishara, tutaula Ushirika Jumapili hii katika hali ya kudhikika. Kwa maana tunajua Wewe uko tayari kutoa hukumu.

Jalia tuule kama mfano wa Pasaka, wakati ilipoliwa kwa dharura, katika wakati wa kudhikika. Tupo katika kudhikika tena leo Baba.

Tunashukuru, Bwana, kwamba tunaweza kutazama nyuma kwenye mwaka huu na kuona yote ambayo umetufanyia. Umelifunua Neno Lako na kutupa Ufunuo juu ya Ufunuo kuliko hapo awali.

Sasa tunajua sisi ni wana na binti Zako. Sisi ndiye Bibi-arusi-Neno kamilifu Wako ambaye Umemngojea kwa muda mrefu sana. Ni Wewe, unayeishi na kukaa ndani yetu. Ulituchagua, ukatujua sisi tangu zamani na sasa unakuja kutuchukua.

Bwana, jalia tukutafute mchana na usiku. Na tuwe wenye kudhikika sana kukulilia Wewe. Jalia tujiingize kwa nguvu zaidi ya tulivyowahi kufanya hapo awali. Huu ukawe ndio mwaka wewe utakaokuja kutuchukua. Tunakupenda Baba, na tunataka kuwa katika Mapenzi yako makamilifu. Njoo uwe nasi tunapoungana saa 11:00 KUMI NA MOJA JIONI, saa za Jeffersonville, kuizunguka Sauti Yako na kukusikia Wewe ukituambia jinsi ya kuingia katika : Kudhikika (Kukata Tamaa) 63-0901E. Kisha uwe pamoja nasi tunaposhiriki katika kudhikika, Meza ya Bwana.

Hizi ndizo siku kuu za maisha yetu Baba. Kwa maana tunajua Unakuja upesi kutupeleka kwenye Makao yetu ya Baadaye pamoja nawe. Tunatazamia kila siku kwa hamu kubwa wale watakatifu ambao wametutangulia. Tunajua pindi tuwaonapo, ule wakati wa kuja kwako umefika….UTUKUFU!!!

Tuko katika hali ya Kudhikika kwa ajili ya siku hiyo, Baba.

Ndugu. Joseph Branham.

Maandiko ya kusoma kabla ya ibada:

Kutoka 12:11
Yeremia 29:10-14
Luka 16:16
Yohana 14:23
Wagalatia 5:6
Yakobo 5:16

23-1224 Kwa Nini Bethlehemu Mdogo?

UJUMBE: 58-1228 Kwa Nini Bethlehemu Mdogo?

PDF

BranhamTabernacle.org

Mpendwa Bibi-arusi Aliyeweka Ile Ishara,

Ningependa sote tujitayarishe kwa ajili ya ibada ya kipekee sana ya Ushirika wa Nyumbani katika Mkesha wa Mwaka Mpya, Jumapili, Tarehe 31 Desemba. Tutausikia Ujumbe, 63- 0901E Kudhikika, ambao Ndugu Branham anaingia katika ibada ya Ushirika na ya kutawadhana Miguu kuelekea mwisho wa kanda.

Kwenye Voice Radio Ujumbe utachezwa(kwa Kiingereza peke yake), na mfuate mpangilio wa ibada kama jinsi tulivyofanya katika ibada zilizopita za Ushirika wa Nyumbani, ikiwemo muziki wa piano wakati wa sehemu ya ibada ya Ushirika, na Nyimbo za Injili wakati wa Kutawadhana Miguu. Tutaanza ibada saa 11:00 KUMI NA MOJA JIONI. majira ya Jeffersonville. Kwa wale ninyi mlio nchi za ng’ambo, tafadhali jisikieni huru kuicheza kanda hii na kushiriki Ushirika katika masaa ya nchi zenu ili mshiriki Ushirika kabla ya saa sita usiku ya 2023.

Siwezi kufikiri njia bora zaidi tunayoweza kuumaliza mwaka huu wa 2023, na kuuanza mwaka mpya wa kumfanyia kazi Bwana katika 2024, kuliko kunyamaza mbele zake, kudhikika zaidi Kwa ajili yake, kushiriki Meza Yake, kuombea na kusameheana mmoja kwa mwingine, kuiosha miguu ya watakatifu Wake, na kulisikia Neno Lake. Hii itakuwa jioni ya kipekee iliyoje.

Zilizoorodheshwa hapa chini ni anuani za njia za kupata na kutayarisha divai na mkate wa Ushirika.

Ninashukuru sana kwamba Bwana ameiandaa njia kwa sisi kuungana pamoja kwa ajili ya hili tukio takatifu jinsi hii. Hakika natazamia kukutana nanyi nyote Mezani Pake.

Jumapili hii, tutasikia ujumbe wa Krismasi: Kwa nini Bethlehemu Mdogo? 58-1228 saa 6:00 SITA MCHANA. saa za Jeffersonville.( Ni saa 2:00 MBILI USIKU ya Afrika Mashariki)

Mungu awabariki,

Ndugu Joseph Branham

Jumapili, Desemba 24, 2023

58-1228 Kwa Nini Bethlehemu Mdogo?
saa 6:00 SITA MCHANA. Saa za Jeffersonville ( Ni saa 2:00 MBILI USIKU ya Afrika Mashariki )

Jumapili, Desemba 31, 2023

63- 0901E Kudhikika/pamoja na Ushirika wa Nyumbani na Kutawadhana Miguu
Saa 11:00 KUMI NA MOJA JIONI saa za Jeffersonville

https://branhamtabernacle.org/en/streaming/viewservice/259609A1-17BB-458F-A4AC-C3EBFF4D53E8

https://branhamtabernacle.org/en/articles/view/1212021_InstructionsToObtainCommunionWineFeetWashingBins

23-1217 Ile Ishara

UJUMBE: 63-0901M Ile Ishara

PDF

BranhamTabernacle.org

Mpendwa Kipenzi Changu,

Moyo wangu unabubujika tu ninapowaona ninyi nyote mkikusanyika pamoja kuizunguka Sauti Yangu, mkisikia Neno Langu, ninapozungumza nanyi kupitia malaika Wangu.

Inanifurahisha sana kujua kwamba mnao Ufunuo wa ni nani niliyemchagua kuwa Sauti Yangu kwenu. Kuamini kila Neno alilonena halikuwa neno lake, bali Neno Langu kwenu.

Hiyo ilikuwa ni ya muhimu sana Kwangu, Nikaifanya irekodiwe na kuhifadhiwa kwa ajili yenu, ili mweze kuisikia tena na tena. Sikutaka kamwe msahau nilichosema kutoka moyoni Mwangu. Nilijua ya kwamba hiyo ingekuwa ndio njia pekee ningeweza kuwapa ninyi ile Imani Kamilifu mliyohitaji, ili tuweze kuwa pamoja.

Daima nimemtumia mtu mmoja kunena na kulifunua Neno Langu kwa Bibi-arusi Wangu. Jinsi ile tu nilivyofanya na Musa. Kile alichoagiza, ndicho alichopata, kwa maana alinena tu Maneno Yangu. Hata nilimwambia yeye, nitakufanya wewe mungu. Utakuwa mungu, na Haruni atakuwa nabii wako. Nitachukua sauti yako, nami nitaumba kwa kukutumia wewe. Nami nitanena, nao watu hawawezi kuikana. Lolote UTAKALOSEMA, litatendeka.

Sasa mmeipata Imani Kamilifu katika Neno Langu, si kwamba mnatambua tu ni nani Niliyewatumia kuwa Sauti Yangu, lakini sasa mnatambua kwamba Neno Langu linaishi na kukaa ndani yenu, hilo limekupa IMANI KAMILIFU.

Mnajua ninyi ni nani.
Mnakaa ndani Yangu, na Neno Langu ndani yenu. Ombeni mtakalo; nanyi mtapewa. katika Jina Langu mtatoa pepo; si, Mimi nitatoa, NINYI MTATOA. Kama NINYI mkiuambia mlima huu; si kama Mimi Nikiuambia, Kama NINYI mkiuambia mlima huu.

Adui yako hana nguvu tena juu yako. Wewe na Neno Langu ni MMOJA. Ikiwa una watoto ama wapendwa wako ambao hawako mahali wanapopaswa kuwa, wadai. Kama Ilifanya kazi kwako, basi itumie IMANI yako KAMILIFU katika NENO LANGU KAMILIFU linalokaa ndani yako, nawe waweza kupokea uombacho.

Lo, nimengoja kwa muda mrefu sana wewe kujitambua ni nani. Kukuona ukijiweka mwenyewe tayari kwa kulisikia Neno Langu. Nimefurahishwa sana hatimaye wakati huo umefika.

Hilo Neno Kamilifu nililonena na kuwahifadhia ninyi ndilo Ishara Yangu kwa kila mwamini leo. Ni Roho Mtakatifu; si damu, kemia, bali ni Roho Wangu Mtakatifu, Neno Langu, linaloishi na kukaa ndani yenu.

Saa ambayo hiyo Ishara haina budi kuonyeshwa waziwazi imewadia. Huna budi kuibeba Ishara pamoja nawe usiku na mchana; sio tu Jumapili, huna budi Kubonyeza Play wakati wote.

Yeye hutambua tu I—Ishara. Huo ndio Ujumbe wa wakati huu! Huo ndio Ujumbe wa siku hizi! Huo ndio Ujumbe wa wakati huu! Katika Jina la Yesu Kristo, upokeeni!

Nje huko kuna jumbe nyingi, lakini Sauti Yangu ndio Ujumbe wa wakati huu. Huna budi kupokea na kuamini kila Neno. Haina budi kuwekwa wakati wa jioni.

Ninyi kote ulimwenguni, mnaosikiliza kwenye kanda, ishara ya wakati huu iko hapa. Kuna Ishara ambayo haina budi kuwekwa, na haingalikuja wakati mwingine wo wote …mnalipata?

Njoo uiweke ile Ishara Yangu maishani mwako pamoja na Bibi-arusi wangu Jumapili hii saa 6:00 saa SITA MCHANA, saa za Jeffersonville (Ni saa 2:00 MBILI USIKU ya Afrika Mashariki ) tunapousikia Ujumbe Wangu kwa Bibi-arusi: ile Ishara 63-0901M.

Ndugu. Joseph Branham

Maandiko ya kusoma kabla ya kusikiliza Ujumbe:

Mwanzo 4:10
Kutoka sura ya 12
Yoshua sura ya 12
Matendo 16:31 / 19:1-7
Warumi 8:1
1 Wakorintho 12:13
Waefeso 2:12 / 4:30
Waebrania 6:4 / 9:11-14 / 10:26-29 / 11:37 / 12:24 / 13:8, 10-20
Yohana 14:12

23-1210 Imani Kamilifu

UJUMBE: 63-0825E Imani Kamilifu

PDF

BranhamTabernacle.org

Mpendwa Bibi-arusi mwenye Imani Kamilifu,

IMANI yetu huja kwa kusikia, kulisikia Neno. Neno humjia nabii.

Nabii ni:

Neno lililofanyika mwili! Haleluya! Neno likitenda kazi katika mwili wa mwanadamu, kwa ishara za kimwili kwa ishara za vitu, kwa ishara za Kimaandiko, kikamilifu, kuwaleteeni Imani Kamilifu kwa ajili ya Kunyakuliwa Kukamilifu.

Sisi tunafanya kile hasa Neno linasema tufanye kwa kuisikia Sauti ya Mungu pekee iliyothibitishwa ikinena na kufunua Neno Lake kupitia mwili wa mwanadamu ili kutupa Imani Kamilifu.

Inakupasa…masikio yako ni bubu kwa kinginecho chote isipokuwa neno analosema Roho. Unaona? “Kwake yeye aliye na sikio ( linalosikiza ), aone neno ambalo Roho ayaambia makanisa”; yeye aliye na mahali pa kusikizia, ambapo panapokea neno ambalo Roho ayaambia makanisa. Waona?

Sisi ndio mahali pake pa kusikizia ambapo panalipata na kuliamini kila Neno. Anapotupa amri: “Semeni tu yale yaliyo kwenye hizo kanda. MIMI NI Sauti ya Mungu kwenu. Mnaniita mimi mchungaji wenu, nanyi mwanena vema, maana ndivyo Nilivyo.” Sisi tunayatekeleza. Cho chote Asemacho, hamna tashwishi kamwe tunatembea moja kwa moja. Lolote Bwana anenalo kupitia nabii Wake, hamna mtu ulimwenguni anayeweza kutushawishi vinginevyo, tunaendelea vivyo hivyo.

Sasa unafikia Imani Kamilifu , ukamilifu mtimilifu usioweza kushindwa. Imani hiyo haishindwi.

Sasa tunayo Imani Kamilifu katika Neno Lake. Sisi hatujitazami wenyewe. Hatuogopi lolote, kama Ayubu. Hatuogopi kuyatazama mawimbi makubwa na kuzama ndani ya maji kama Petro. Siku hizo zimepita. SASA tunalitazama lile Neno Kamilifu linaloishi na kukaa ndani yetu. Tunafikia asili ya Bibi-arusi. Tunafikia katika hali ya kunyakuliwa.

Tunapoomba, tunaamini kwamba tunapokea kile tunachoomba, nasi tutakipokea; tutapewa. Wakati, mahali, hakuna kitu kitakachokibadilisha. Tunajua imetendeka. imekwisha Tayari. Tunajuaje? Kwa sababu si Neno letu, bali ni NENO LAKE, ambalo amesema na kutupa sisi. Tuna NGUVU NA IMANI KAMILIFU YA KULINENA.

Kama vile Yesu alivyofanya kwa ajili yake Mwenyewe, tunatambua mahali petu; sisi ni nani. Jambo pekee tunalopaswa kufanya basi, ni kuwa na imani na kile tulicho. Tuwe na imani katika kile NENO linasema tulicho! Ndipo Neno la Mungu linakuja ndani yetu na kujidhihirisha Lenyewe; kwa maana sisi ni waamini. Na mwamini ni “imani ya Mungu inayotenda ndani yetu.”

Na sasa, tunakuwa watiwa mafuta kwa Roho yuyo huyo, masihi watiwa mafuta, masihi wa siku za mwisho, kuangaza ufufuo wa Yesu Kristo; kuonyesha ya kwamba si mfu, bali yuko katika umbo la Roho Mtakatifu, yu ndani ya watu Wake, akitembea kati ya Bibi-arusi Wake, akimfanyia mapenzi, akijimwaga Mwenyewe Kwake. Wanakuwa mmoja kwa ajili ya Karamu ya Arusi; na ishara zile zile, zilizoahidiwa na Mungu yule yule, katika Neno lile lile zinafanya madhihirisho yale yale Yake.

Hamna kilichobaki kwetu ila kuliamini, na kwa Kuliamini ndiyo hakika ya mambo inayoumba Imani Kamilifu. Sikiliza hilo tena, KWA KULIAMINI NDIYO HAKIKA YA MAMBO INAYOUMBA IMANI KAMILIFU.

Je! kunacho kiungo katika mwili wako kinachotilia shaka hata Neno moja: HAPANA
Je! unaamini kila Neno: Ndiyo
Je! Amekupa Ufunuo wa Ujumbe huu: Ndiyo
Je! Ni Bibi-arusi peke yake ndio watakaokuwa na huo Ufunuo wa kweli: Ndiyo
Je! unajua wewe ni Bibi-arusi Wake: Ndiyo
Je! Alisema kwa kuamini kila Neno itakupa Imani Kamilifu: Ndiyo
BASI WEWE NDIYE BIBI-ARUSI-NENO MWENYE IMANI KAMILIFU!!

Ee Bwana tuandae zaidi ya wakati mwingine tunapokusanyika pamoja Jumapili hii kusikia Neno lako. Tusaidie tusijitazame wenyewe tena, bali tu kuamini Neno Lako ulilonena kwa ajili yetu. Tumeuona Mvuto wa Tatu ukitenda kazi nasi tunajua unakaa ndani yetu. Yatubidi tuwe tunalinena na kuliamini Neno Lako.

Tunajua unamjia hivi karibuni Bibi-arusi-Neno Wako mkamilifu. Lolote tunalohitaji, Baba, LOLOTE TUNALOHITAJI, tunajua tutalipokea. Kwa maana Ni Neno Lako ambalo umekwisha kulinena kwa ajili yetu. Hakuna lingine lakufanya ila KULIAMINI tu. Tunaliamini Baba, tunaliamini. Sasa hebu na tulitendee kazi NENO LAKO.

Tunakiri kushindwa kwetu, dhambi na makosa yetu yote. Tutazame kupitia Damu ya Mwanao ambapo tunahesabiwa haki kwa Neema na rehema zako. Jalia kuwe na badiliko ndani ya Bibi-arusi Wako zaidi ya hapo awali. Na Utumiminie Roho wako Mtakatifu na kutupa yote tunayohitaji.

Wagonjwa wataponywa magonjwa yote. Aliyerudi nyuma atarudi kwenye Neno. Bibi-arusi wako ulimwenguni kote wataona njia yako iliyoandaliwa kwa ajili ya siku hii na kuamini.

Kama huna mtu wa kukuwekea mikono…wewe jiwekee mikono yako mwenyewe…wewe ni mwaminio. Umekuwa Neno; unakuwa Neno, unapolipokea Neno.

Njoo Bwana Yesu, Bibi-arusi Wako anajiweka mwenyewe tayari kwa kukaa katika uwepo wa Neno Lako, kuivishwa. Tunataka kupambwa na kuvikwa kwa Neno lako.

Njoo ututie mafuta zaidi ya hapo kabla Jumapili hii saa 6:00 SITA MCHANA, saa za Jeffersonville, ( Ni saa 2:00 MBILI USIKU ya Afrika Mashariki ) wakati sehemu ya Bibi-arusi wako inapokusanyika kukusikiliza WEWE ukinena na kutufunulia jinsi ya kupata: Imani Kamilifu 63-0825E.

Ndugu. Joseph Branham

Maandiko ya kusoma kabla ya ibada:

Marko 11:22-26 / 16:15-18
Yohana 14:12 / 15:7
Waebrania 11:1 / 4:14
Yakobo 5:14
1 Yohana 3:21

23-1203 Ninawezaje Kushinda?

UJUMBE: 63-0825M Ninawezaje Kushinda?

PDF

BranhamTabernacle.org

Mpendwa Yungiyungi la Kidimbwini,

Jinsi gani mioyo yetu ilivyoruka kwa furaha Jumapili tulipomsikia Bwana wetu akinena na kutuambia kile kinachotendeka sasa hivi. Tunaungana na Neno na kuwa MMOJA Naye. Hivi karibuni sana tutaungana na watakatifu waliotutangulia kuwa WAMOJA nao. Kisha sisi sote pamoja tutaungana na Kristo kama MMOJA kwenye Karamu ya Arusi ya Mwana-Kondoo.

Ni furaha iliyoje iliyojaza nafsi zetu wakati Alipotuambia kuwazia kwamba katika dakika moja, katika kufumba na kufumbua jicho, ulimwengu hata hautajua kinachoendelea; lakini kwa ghafula, tutawaona mbele ya macho yetu wapendwa wetu walioondoka, nasi tutaungana nao tena.

Ni matarajio yaliyoje yanayojaza mioyo yetu kuwazia, kwa ghafula, tutawaona wamesimama mbele yetu baba zetu, mama zetu, kaka, dada, waume, wake, watoto, hata nabii wetu. TUTAWAONA, KATIKA MWILI!!

Tutajua papo hapo, hili NDILO; wakati umefika, tumefaulu, IMEKWISHA. Nena kuhusu changamko kwa Ufunuo!! Nikiliwazia na kulinena tu sasa hivi, naweza kuwasikia mkipaza sauti, UTUKUFU, HALELUYA, JINA LA BWANA LIHIMIDIWE.

Ni Wakati wa jinsi gani tunaokuwa nao, tukila barua hizi za mapenzi tulizoachiwa. Barua za mapenzi tunazoweza kuzichomoa wakati wowote tunapotaka na kuzisoma tena na tena na tena. Si hivyo tu, bali na KUBWA ZAIDI, tunaweza KUMSIKIA Bwana wetu Mwenyewe akisema kupitia midomo ya mwanadamu na kutuambia, “Nilizihifadhi barua hizi za mapenzi kwa ajili yako tu, kipenzi Changu. Nilijua wakati ungefika ambao ungehitaji kunisikia Mimi nikikuambia jinsi ninavyokupenda na kwamba wewe ni Wangu.”

“Nilitaka kukuambia kila siku adui anapokushambulia, unapopitia mitihani na majaribu yako yote, WEWE NI WANGU. Tayari nimelipa ile gharama. Tayari nimeshinda chochote kile…umenisikia kipenzi? CHOCHOTE unachokihitaji, nimekwisha kushinda kwa ajili yako, kwa sababu Nakupenda”.

“Nilikujua kabla hata ulimwengu haujawepo. Wewe ulikuwa sehemu Yangu WAKATI HUO. Hukumbuki hilo sasa, lakini Mimi ninakumbuka. Usisahau nilichokuambia, wewe ni Mwili wa Mwili Wangu, Roho wa Roho Yangu, Mfupa wa Mfupa Wangu”.

“Ule wakati umefika sasa ambao nimekuwa nikiwaambia. Hakutakuwa na huzuni tena, hakutakuwa na mitihani na majaribu tena; siku hizo zimekwisha. Sasa ni sisi sote tu pamoja Milele yote”.

“Jipe moyo. Endelea kusonga. Kule Kupambazuka kwa siku ile kumekaribia. Mvutano wote unaopitia kila siku ni wa kukuleta karibu na Mimi”.

“Wakati jambo lolote linapokujia, na unaanza kuhisi umevunjika moyo sana, umechoka na huwezi, na kuonekana kama huwezi kuendelea mbele, inakubidi usisahau kamwe, Mimi Niko hapo pamoja nawe. Neno Langu linaishi ndani yako. Wewe ni Neno Langu.”

“Niliwaambia, mnene Neno. Lo lote mtakalo, mkisali, aminini ya kwamba mtalipokea, nanyi mtalipata. Mtapewa jambo hilo. Tayari Mimi nimekwishawashindia jambo hilo”.

Maneno haya yanamaanisha nini kwetu. Yanatuhifadhi kila siku. Linaziinua Roho zetu na kutuweka katika ulimwengu wa Roho pamoja Naye. Tunamwishia tu Mungu na Neno Lake. Tuna kusudi moja, hilo ni Yesu Kristo. Nje ya Hilo, hakuna jambo lingine linalojalisha.

Tumelipata lile Ono. Pazia limevutwa nyuma nasi tunamwona Yeye, Neno Lake lililofanyika mwili, akizungumza nasi kupitia midomo ya mwanadamu. Tuna mapenzi na Neno hili, Ujumbe huu, Sauti hiyo.

Njoo uungane nasi Jumapili saa 6:00 SITA MCHANA, saa za Jeffersonville,( Ni saa 2:00 MBILI USIKU ya Afrika Mashariki ) upate uzoefu uliyo mkuu maishani mwako. Usikie jinsi ya kushinda kila vita ambavyo Shetani anatupa mbele yako. Ujaze moyo wako kwa furaha na shangwe kujua wewe ni Bibi-arusi wa Yesu Kristo.

Ndugu. Joseph Branham

63-0825M Ninawezaje Kushinda?

Maandiko ya Kusoma kabla ya ibada :

Ufunuo 3:21-22

23-1126 Wakati Wa Kuungana Na Ishara Yake

UJUMBE: 63-0818 Wakati Wa Kuungana Na Ishara Yake

PDF

pakua – m4a

pakua – amr

BranhamTabernacle.org

Mpendwa Mwili wa Mwili Wake, Neno la Neno Lake, Uhai wa Uhai Wake, Roho wa Roho Wake,

Ndugu na dada zangu wapendwa, Hebu someni kauli hiyo moja tena na tena. Someni kile Mungu Mwenyewe alichomaliza kuwaita. Hivi angewezaje mtu yeyote kuandika kwa maneno ya kibinadamu tu kuwa hayo yana maana gani kwetu. Haiwezekani kuyaeleza. Kama tungeweza kuyafahamu kikamilifu na kuyatumia, kwa mioyo yetu yote, nia na roho zetu zote, ninaamini kweli Unyakuo ungepaswa kutukia.

Kuna nini cha kuogopa? Kuna nini cha kuhofia? Shetani anatushambulia, anatutesa, anatutupia magonjwa, anashambulia akili zetu kwa kila namna ya mawazo mabaya, lakini hakuna kitu kinachoweza kutudhuru. Je, kuna jambo lolote linaloweza kumdhuru Yesu? HAPANA, basi wala hakuna kitu cha kutudhuru. Ndio kwanza Amesema: SISI NI Mwili Wake, Neno Lake, Uhai Wake, Roho Wake.

Ni furaha na uradhi uliyoje tulio nao mioyoni mwetu tunapotafakari yale ambayo Yeye amekuwa akituambia. Ufunuo ambao Mungu amekuwa akitufunulia, mzigo wa kanda, baada ya mzigo wa kanda, baada ya mzigo wa kanda. Roho Mtakatifu anabubujika ndani yetu kama Kisima kikuu kinachofoka maji.

Sisi tumechaguliwa tangu zamani Kuliona na Kulisikia. Hatuta na hatuwezi kuanguka wala kupotoshwa. Tuko njiani kukutana na Uongozi wetu, Mkombozi wetu, Mume wetu, Mfalme wetu, Bwana wetu, Mpenzi wetu, Mwokozi wetu, katika Mahali palipoandaliwa pa kukutania!

Hebu sikilizeni hili tena: Utimilifu kamili wa Uungu kwa jinsi ya mwili unakaa ndani YETU, Kanisa Lake, ule utangulizi. Yote aliyokuwa Mungu, aliyamimina ndani ya Kristo; na yote aliyokuwa Kristo, yalimiminwa ndani ya Kanisa; sisi, Bibi-arusi Wake. Sio jambo litakalotendeka siku moja, AMESEMA LINAFANYIKA NDANI YETU SASA HIVI.

Je, waweza kuwazia, tangu mwanzo kabisa wa wakati, Mungu hakuwahi kutoa siri Yake kuu ya ajabu ambayo ilikuwa niani Mwake kwa mtu yeyote, hadi leo hii. Kwa nini alifanya hivyo? Kwa sababu Yeye alikuwa anangojea kutujulisha SISI katika siku hizi za mwisho kama alivyoahidi. Alikuwa anatusubiri sisi. Alijua kuwa sisi ndio watu pekee tungaliweza, na tungeweza, KULIELEWA KIKAMILIFU….UTUKUFU!! !

Alituchagua sisi tuwe Bibi-arusi wake kwa sababu alijua kwamba hatutaanguka. Tungeshikilia Neno hilo haidhuru ulimwengu wote ungesema nini kulihusu. Tungeshikilia Neno hilo na NENO hilo PEKE YAKE! Sisi tumechaguliwa tangu zamani kusimama hapo. SISI tumefanywa wana wenye mamlaka na Yesu Kristo.

Kunayo mengi zaidi. Sikilizeni kwa makini….jichune. Kichwa (Mungu) na Mwili (Sisi) umekuwa kitu kimoja. Ni Mungu aliyedhihirishwa ndani YETU.

  • Mungu na Kanisa Lake wao ni MMOJA, “Kristo ndani YENU.”
  • Sisi NDIO Ufunuo Mkuu wa Mungu.
  • Sisi hata tunalibeba Jina Lake; Jina Lake ni Yesu, yule Mtiwa Mafuta.
  • SISI NDIO Mwili uliotiwa mafuta wa Kristo.
  • SISI TUNA mdhihirisha Mungu kama jinsi ule mwili ulivyofanya.

Sisi ndio Bibi-arusi Wake, tumetiwa mimba kwa Roho Wake. Kanisa, linalozaa watoto, lililotiwa mimba kwa Roho Wake likibeba Jina Lake; likibeba Uhai Wake. Tuna jibu la Shetani. Uongozi uko hapa. Kristo, Bwana aliyefufuka, yuko hapa katika Nguvu zile zile za kufufuka Kwake alizowahi kuwa, akijidhihirisha Mwenyewe ndani yetu, Bibi-arusi-Neno Lake Lililonenwa.

Mungu sasa anamuunganisha Bibi-arusi Wake pamoja. Anawaunganisha kutoka ulimwenguni kote kwa Neno Lake, jambo pekee litakalomleta Bibi-arusi Wake pamoja. Roho Mtakatifu anaongoza na kumkusanya Bibi-arusi Wake. Katika kila wakati, nabii alikuwa ndiye Roho Mtakatifu kwa ajili ya siku zao.

Liwazieni jambo hili. Wakati Watu wanaposema kuwa tunampa sifa nyingi mno malaika-mjumbe wa saba, kumbuka, Mungu Mwenyewe alizikabidhi SIRI ZAKE ZOTE alizokuwa nazo Niani Mwake kabla hata ulimwengu haujawepo, kwa malaika-mjumbe Wake wa saba. Mungu Mwenyewe alikuwa na imani na mtu huyu asilimia 100%, hata akauweka Mpango wake mkuu wa wakati wa mwisho mikononi mwake. Alimpa yeye…SIKILIZENI, AKAMPA YEYE Ufunuo wa siri Zake zote kwa mtu huyo. Alimpa mtu huyo Ufunuo wa mambo ambayo hata hayakuandikwa. Alisema chochote kile alichosema duniani kilikuwa ni muhimu sana, kingerudisha mwangwi mbinguni.

Hakuna tashwishi kwamba Mungu aliwatuma watu wakuu waliojazwa na Roho Mtakatifu katika ulimwengu huu. Lakini kila mmoja wa watu hawa, hata ikiwa wamejazwa na Roho Mtakatifu, wanaweza kuwa makosani. Mungu kamwe hakuthibitisha kile wanachosema kuwa Bwana Asema hivi, na kuwaambia muamini kila neno lao. Kulikuwa na mtu mmoja tu aliyekuwa na mamlaka hayo kutoka kwa Mungu, malaika-mjumbe Wake wa saba.

Unaweza, na unapaswa, kuwa na mchungaji. Lakini kama huyo mchungaji hakuambii ya kwamba SAUTI YA MUNGU iliyo kwenye kanda ndiyo SAUTI iliyo MUHIMU SANA KUSIKIA, na kuipa nafasi ya KWANZA mbele yenu kwa kusikiliza kanda pamoja nanyi, si kwamba tu yeye awaambie ati nabii anasema hivi, basi mchungaji mliye naye hafai.

Yeyote anayekuongoza, hata kama unadai kuwa ni Roho Mtakatifu, ni afadhali awe anakuunganisha na Ujumbe huu, Ile Sauti, kwani Ndiyo sauti Pekee inayoweza kusema, “MIMI NI SAUTI YA MUNGU KWENU”.

Kama umechaguliwa tangu zamani Kuliona, Utaliona. Ikiwa hujachaguliwa tangu zamani Kuliona, hutaliona kamwe; hujaandikiwa kuliona.

Tunaona mataifa yakiungana, tunaona ulimwengu ukiungana, tunaona makanisa yakiungana. Tunaona Bibi-arusi akiungana, akiungana na Neno. Kwa nini? Neno ni Mungu. Na kama Neno…Kama vile Bwana Arusi (akiwa ni Neno), na Bibi-arusi (akiwa ni msikiaji wa Neno), wanakuja pamoja katika Muungano. Wanaungana kama vile arusi. Unaona, wanajiandaa kufanya arusi, nao—nao wanakuwa mmoja. Neno linakuwa wewe, wewe unakuwa Neno. Yesu alisema, “Katika siku hiyo mtaijua. Yote aliyo Baba, ndivyo nilivyo Mimi; na yote niliyo Mimi, ndivyo mlivyo ninyi; na yote mliyo ninyi, ndivyo nilivyo Mimi. Katika siku hiyo mtajua ya kwamba Mimi niko ndani ya Baba Yangu, Baba ndani Yangu, Mimi ndani yenu, nanyi ndani Yangu.”

Ninawaalika mje kuungana nasi kuizunguka Sauti ya Mungu Jumapili hii saa 6:00 SITA MCHANA, saa za Jeffersonville, ( ni saa2:00 MBILI USIKU ya Afrika Mashariki), tunaposikia, Wakati Wa Kuungana na Ishara Yake 63-0818

Ndugu. Joseph Branham

Maandiko ya kusoma kabla ya ibada:

Zaburi 86:1-11
Mathayo 16:1-3

23-1119 Kristo Ni Siri Ya Mungu Iliyofunuliwa

UJUMBE: 63-0728 Kristo Ni Siri Ya Mungu Iliyofunuliwa

PDF

pakua – m4a

pakua – amr

BranhamTabernacle.org

Mpendwa Kitovu Cha Moyo Wa Nabii,

Wao ndio—ndio wamezaliwa Kwako, kwa Roho na kwa Neno la Kweli. Nami naomba ya kwamba utawabariki, Bwana, na kuwaweka wameunganishwa pamoja kwa karibu na vifungo vya upendo wa Kristo.

Jitayarisheni, tutakuwa na baraka, upako na Ufunuo kuliko awali. Twaweza kulihisi jambo hilo katika nafsi zetu, jambo fulani linakaribia kutukia. Wakati uko tayari. Tumechangamshwa sana kwa furaha na tuko chini ya matarajio makubwa ya aina yake. Bibi-arusi ulimwenguni kote anakusanyika pamoja ili kusikia kutoka kwenye kiti cha enzi cha Mungu Ujumbe ambao utatupeleka kwenye viwango vipya, na kutujaza, na kujaza, na kisha kutujaza upya na Roho Wake Mtakatifu.

Maandiko yanaenda kutimia. Onyo limefanyika. Hukumu iko karibu. Bwana anakuja kumwita Bibi-arusi Wake kwenda kwenye Karamu yetu ya Arusi. Ule wito wa mwisho umepita. Ujio wa Mungu umefika. ANAKUJA KUTUCHUKUA.

Sisi ndio ile mbegu iliyochaguliwa tangu zamani ambayo huliona na kulikubali. Dhambi zetu zimeangamizwa, zimekwisha. Zimetupwa kwenye wino wa Damu ya Yesu Kristo, wala hazitakumbukwa tena. MUNGU amezisahau ZOTE. Tunasimama kama mwana na binti wa Mungu, mbele za Mungu. Ndivyo tulivyo SASA…si tutakuwa; SASA sisi ni wana na binti za Mungu.

Tunatambua kitu kimoja, NENO. KANDA HIZI. UJUMBE HUU. Hayo ni mamoja.

Na mara moja, muda mfupi tu uliopita, ulipoonyesha lile ono, hii maskani ndogo hapa, karibu kuweka Chakula akiba, kwamba utakuja wakati ambapo haya yote yangehitajika … “Weka Chakula hiki akiba hapa kwa ajili ya huu wakati.”

Huu ndio wakati. Hiki ndicho Chakula. Sisi ndio watu hao. Sisi tunao Ufunuo.

Wengine wanaweza kuukosa umuhimu wa Huduma ya Kanda. Sisi sisi sivyo. Ni maisha yetu, ni kila kitu kwetu. Ni zaidi ya uhai kwetu. Tunapokuwa na swali kuhusu jambo fulani, hatuendi kumwomba mtu atufafanulie, ama atutafutie. Sisi tunafanya vile hasa malaika wa Mungu alivyotuagiza kufanya ikiwa tutashindwa kuelewa au tukiwa na swali.

Mnalipata? Mkishindwa, rudini kwenye kanda hii tena. Sijui nitakuwa nanyi kwa muda gani zaidi. Kumbukeni, hii ndiyo Kweli, ya BWANA ASEMA HIVI. Ndiyo Kweli. Ni Maandiko.

Mkishindwa, rudini kwenye kanda.

Msitukasirikie, hivyo ndivyo YEYE ALIVYOSEMA…PAMOJA NA, hii ndiyo KWELI YA BWANA ASEMA HIVI . Yeye hakusema kiasi chake, baadhi Yake, ama wakati mtu fulani anapofasiri kile kilicho na ambacho si Neno lililotiwa mafuta. KANDA HIZI NI BWANA ASEMA HIVI.

Huenda wewe usilipate, ama kulielewa, ama bado halijafunuliwa kwako . Lakini kwetu sisi, haya ndiyo YEYE anayotuambia kupitia nabii Wake.

Unajua jinsi unavyomwambia mke wako mambo, unajua, msichana mdogo utakayemwoa. Unampenda sana, unamwambia tu siri, na kumweka karibu nawe, na kukupenda wewe na kadhalika. Unajua jinsi ilivyo. Hivyo ndivyo Mungu, Kristo, analifanyia Kanisa. Mnaona? Anamjulisha siri, siri tu. Sio hawa wafanya utani; ninamaanisha Mke Wake.

Nasi tunayazingatia yote. Loo jinsi gani Bibi-arusi alivyo mwenye furaha na changamko la shangwe kabla tu ya arusi yake. Hatuwezi kabisa kusimama kimya. Tunazihesabu dakika …. sekunde. Yeye anaendelea kutuambia tena na tena jinsi gani anavyotupenda.

Shetani anaendelea kutushambulia kuliko awali, lakini kile hajajiandaa, ni kwamba sasa TUNAJIJUA sisi ni nani. Hakuna shaka tena, SISI NI NENO LILILONENWA. Tunaweza, na tuna, nena Neno. Tuna jibu la Shetani. Mungu amejithibitisha Mwenyewe. Mungu amejihakikisha Mwenyewe. Sisi ni Neno Lake lililo hai nasi tuna nena kwa mamlaka yote aliyotupa.

Naye huyu hapa leo, katika Neno Lake, akidhihirisha jambo lile lile alilofanya kule. Hawezi kutambua uongozi mwingine. La, bwana. Hakuna askofu, hakuna chochote. Anatambua Uongozi mmoja, huo ni Kristo, naye Kristo ni Neno. Loo, jamani! Whiu! Napenda hilo. Uh! Naam, bwana.

Sisi ni raia wa Ufalme, nao huo Ufalme ni Neno la Mungu lililofanyika Roho na Uzima katika maisha yetu wenyewe. Kwa hiyo, sisi ni Neno Lake lililo hai.

Hili Hakika lanena YOTE enyi marafiki, IKIWA UNA UFUNUO WA KWELI WA KULIPOKEA NA KULIAMINI.

Sasa angalieni. Angalieni sasa, wameunganishwa pamoja chini ya Uongozi mmoja, kwa namna ile ile, mfano wa Israeli wa kale. Sasa mnalipata? Kama Israeli wa kale; Mungu mmoja, aliyethibitishwa kwa Nguzo ya Moto, na kujifunua Mwenyewe kupitia nabii, kuwa Neno. Mungu yeye yule, Nguzo ile ile ya Moto, kwa njia ile ile; Hawezi kubadili njia Yake . Hilo ni… Kamili tu kama iwezavyo kuwa.

Nabii…Hebu hilo lizame ndani kilindini. Mungu Mmoja, aliyethibitishwa kwa Nguzo ya Moto, kupitia nabii, kuwa Neno la siku hiyo, Naye hawezi kubadilika.

Ningeweza kuendelea na kuendelea, na tungeweza kufurahia na kushiriki nukuu baada ya nukuu; nasi tutafanya hivyo, kutoka kote ulimwenguni Jumapili hii saa 6:00 SITA MCHANA, saa za Jeffersonville, (ni saa 2:00 MBILI USIKU ya Afrika Mashariki ) tunaposikia:  Kristo Ni Siri ya Mungu Iliyofunuliwa 63-0728.

Ndugu. Joseph Branham

Maandiko ya kusoma kabla ya ibada:

Mathayo 16:15-17
Luka Sura ya 24
Yohana Mtakatifu 5:24 / 14:12
1 Wakorintho Sura ya 2
Waefeso Sura ya 1
Wakolosai Sura ya 1
Ufunuo 7:9-10

23-1112 Mungu Hamwiti Mtu Hukumuni Bila Ya Kumwonya Kwanza

UJUMBE: 63-0724 Mungu Hamwiti Mtu Hukumuni Bila Ya Kumwonya Kwanza

PDF

BranhamTabernacle.org

Mpendwa Kamani, Springi kuu, Mkulima na Mke nyumbani,

Chochote kile ambacho Mungu alichokupa kufanya, una utumishi kwa jambo hilo. Huna budi kuwajibika kwa hilo kwa Mungu. Haijalishi adui aweza kukuambia kuwa wewe ni mdogo jinsi gani, wewe ni muhimu sana kwa Mungu hivi kwamba saa Yake kuu haiwezi kusonga bila wewe.

Alikuita, akakuchagua, alikukusudia tangu awali, na akakupa Ufunuo wa Ujumbe Wake mkuu wa wakati wa mwisho. Ana imani na wewe asilimia 100%. Wewe ndiwe yule Bibi-arusi mwenyewe wa Yesu Kristo, Kipenzi Chake, naye Anakupenda sana.

Daima amewaonya watu kote katika mataifa, “Tubuni, la sivyo mtaangamia,” “Rudini kwenye Neno,” “Jitayarisheni, kuna jambo linaenda kutukia.” Wakati huo hatimaye umefika. Mungu anakuja kumchukua Bibi-arusi Wake, kama vile tu alivyotuahidi Angefanya. Ameliita Gurudumu Lake kutoka kwenye gurudumu.

Wengi wameanguka kutoka kwenye Ujumbe mkuu wa Mungu wa wakati wa mwisho leo hii, wakisema, “yale aliyosema yangetukia, hayakufanyika. Mambo yote yako vile vile.” Ilikuwa ni vizazi vingi vilivyopita kabla ya unabii mwingi wa manabii wa Mungu kutimia. Lakini yalitendeka hata hivyo, kama tu walivyosema, Neno kwa Neno.

Biblia yake inatuambia hivi: “Kama ilivyokuwa katika siku za Nuhu, ndivyo itakavyokuwa katika kuja Kwake Mwana wa Adamu.” Kabla Mungu hajatuma hukumu kuuangamiza ule ulimwengu uliotangulia gharika, Mungu alimtuma nabii ulimwenguni. Nabii huyo alifanya nini?

Akawatayarisha watu kwa ajili ya wakati huo. Nuhu aliwatayarisha watu, nao ulikuwa ni wito wa rehema kabla ya hukumu.

Nuhu aliwatayarisha watu kabla ya hukumu kuja aliowaonya kuihusu. Ilikuwa ndio Njia ya Mungu iliyoandaliwa kwa ajili ya siku hiyo.

Nabii wa Mungu alituambia kwamba Mungu kamwe habadilishi mpango Wake. Yale aliyoyafanya wakati huo, anayafanya vivyo hivyo leo hii. Sisi tutakaa tu na MPANGO WA MUNGU ULIYOANDALIWA KWA AJILI YA SIKU HII NA KUBONYEZA PLAY.

Kama ilivyokuwa wakati huo, watu husema tunaweka mkazo sana kwa nabii wa Mungu; Ni Roho Mtakatifu, si William Branham. Tunasema, AMINA, hatumsikilizi huyo mtu , tunasikiliza tu YALE ALIYOSEMA.

Roho Mtakatifu ndiye Nabii wa wakati huu; Yeye analihakikisha Neno Lake, akilithibitisha. Roho Mtakatifu alikuwa ndiye Nabii wa wakati wa Musa. Roho Mtakatifu alikuwa Nabii wa wakati wa Mikaya. Roho Mtakatifu, aliyeliandika Neno, anakuja na kulithibitisha Neno.

Lakini Ndugu Branham ndio kwanza awaambie juma lililopita;

Sasa, mnaona, daima nimewaomba mwe waangalifu kwa yale mnayosikiliza. Mnaona? Kuna mengi sana ambayo ni upande tu wa kibinadamu.

Sisemi ya kwamba Bwana aliniambia jambo hilo. “Mimi” naamini, unaona. Na naamini halipaswi kufanywa.

Kwangu mimi na nyumba yangu, nitachukua yale malaika-mjumbe wa saba wa Mungu ANAYOAMINI, ANAYOWAZIA AU HATA ANAYOJISIKIA kuliko ya mhudumu mwingine yeyote, askofu ama mtu.

Ni nani ambaye Mungu aliwahi kumtuma kuhukumu kile nabii Wake anachoamini, anachohisi ama hata anachofikiria ndicho ama halijavuviwa?…Hebu niwaambieni ni nani ninayefikiri.

Mwangalieni Kora, katika siku ambazo Mungu alimtuma Musa na ujumbe, naye Kora na Dathani wakawazia, wakamwendea Musa, na kusema, “Sasa, hebu kidogo, unajichukulia mengi kupita kiasi! Unafikiri wewe ndiwe changarawe ya pekee ufukoni; bata kidimbwini, ndiwe wa pekee. Nitakufahamisha wapo watu wengine walio watakatifu, pia!”

Onyo, hukumu iko karibu. Rudini kwenye NENO LA ASILI. Rudini kwenye Sauti ya Mungu iliyothibitishwa kwa ajili ya siku yetu. Rudini kwa nabii wa Mungu. Ujumbe huu, Sauti Yake. Inapaswa kuwa ya KWANZA na kuwa jambo lililo muhimu zaidi kwenu.

Bila shaka wengine wana sauti, na wito, kuhubiri na kufundisha Ujumbe huu. Bali Kanda hizo, Sauti hiyo, haina budi kuwa ndio Sauti iliyo muhimu sana mnayopaswa kuisikia katika nyumba zenu, magari yenu, na muhimu zaidi, kanisani mwenu, kama mnataka kuwa Bibi-arusi wa Mungu.

Njooni msikie hiyo Sauti pamoja nasi Jumapili saa 6:00 SITA MCHANA, saa za Jeffersonville,( ni saa 2:00 MBILI USIKU ya Afrika Mashariki ) Wakati nabii wa Mungu anapouonya ulimwengu kwamba Kuja kwa Bwana kumekaribia. Hii inaweza kuwa ndio mara ya mwisho.

Ndugu. Joseph Branham

Mungu Hamwiti Mtu Hukumuni Bila Ya Kumwonya Kwanza. 63-0724

Maandiko ya kusoma kabla ya ibada:

Isaya 38:1-5
Amosi Sura ya 1