22-1120 Mahali Alipopachagua Mungu Pa Kuabudia

Ujume: 65-0220 Mahali Alipopachagua Mungu Pa Kuabudia

PDF

pakua – m4a

pakua – amr 8 MB (use Firefox to download)

BranhamTabernacle.org

Mpendwa Bi Yesu Kristo,

Jinsi tunavyopenda kusikia majina yetu yakiitwa. Kufikiri tu, sisi ndio wale Anaowajia. Bibi-arusi wa Kifalme kwa Mwana aliyeahidiwa wa Kifalme. Uzao wake maalumu wa Kifalme wa Ibrahimu ambao umekuwa mkweli na mwaminifu kwa kila Neno.

Hatujafanya uzinzi, wala hata kukonyezana, na neno lingine lo lote; tumejiweka tu wasafi na tumekaa na kila Neno.

Kuna wanawake Wakristo wengi wazuri ulimwenguni leo, wanawake waaminifu; Bali kuna Bi Yesu Kristo mmoja tu. Sisi ndio tunaenda Nyumbani pamoja Naye. Sisi ndio Mke wake Aliyeteuliwa .

Alituambia katika Neno Lake kwamba angekuja mara nyingine tena, kama jinsi tu alivyokuja hapo awali. hapo yeye alisimama, akijifunua katika mwili wa mwanadamu, akisoma Neno na kutuambia, “Leo Maandiko haya yametimia machoni penu,” nasi tukamtambua, na tukawa Bi Yesu Kristo wake.

Imefunuliwa kwetu ya kwamba M-w-a-n-a yule yule wa Mungu aliyetokea mashariki na kujithibitisha Mwenyewe kama Mungu aliyefanyika mwili ndiye M-w-a-n-a yule yule wa Mungu aliyeko katika kizio cha magharibi cha dunia ambaye anajitambulisha Mwenyewe kati ya Bibi-arusi wake. Ile nuru ya jioni ya Mwana imekuja.

Na kama ningeuliza swali kuhusu cho chote, yapaswa kuwe na jibu la kweli. Kwaweza kuwe na lililo la karibu nalo; lakini yapaswa kuwe na jibu la kweli, la moja kwa moja kwa kila swali. Kwa hiyo, basi, kila swali linalozuka maishani mwetu, yabidi kuwe na jibu la kweli na sahihi.

Katika wakati wetu kuna maswali mengi na mabishano miongoni mwa watu.

. Je, ni muhimu jinsi gani kusikiliza kanda za nabii wa Mungu?

. Je, ni muhimu jinsi gani kusikia na kuamini kila Neno?

. Yakini yetu ni nini? Je! Ni yale aliyosema kwenye kanda, ama Roho Mtakatifu humwongoza kila mtu kuamua lipi ni Neno na lipi si Neno.

. Je, ni lazima tuwe na mtu, au kundi la watu, kutuvunjia-vunjia ?

. Je! Neno linasema baada ya Yeye kumtuma Eliya nabii, Yeye atatuma kundi la watu ambalo halina budi kuwafafanulia Hilo?

. Je, tunahitaji mtu fulani wa kutufasiria Neno au kulivunja-vunja ?

. Je, tunapaswa kuzisikiliza tu kanda katika nyumba zetu, magari, na vituo vya mafuta, na kisha kumsikia mhudumu tunapoenda kanisani?

. Je, tucheze kanda katika makanisa yetu?

. Je, ni Sauti ya Mungu kwa ajili ya wakati wetu au la?

Sasa, kama ni swali la Biblia, basi lapaswa liwe na jibu la Biblia. Halingepaswa kuweza kuja kutoka kundi la watu, kutoka kwenye ushirika wo wote ule, au kutoka kwa mwalimu fulani, au kutoka kwa madhehebu fulani. Lapaswa litoke moja kwa moja katika Maandiko…

Kwa hiyo, ikiwa tunataka kupata jibu sahihi kwa maswali yetu, ni lazima twende kwenye Maandiko. Kisha, ni lazima tuamue, ni nani aliye mfasiri wa Kiungu wa Maandiko. Je, kila mtu anajiamulia kivyake?

Nabii haimaanishi kunena Neno tu, bali pia ni kutabiri, na ni mfasiri wa Kiungu wa Neno, Neno la Kiungu lililoandikwa.

Kwa hiyo kama nabii ndiye mfasiri wa Kiungu wa Maandiko, basi kile nabii huyo alichosema ni Neno la Mungu kwa Bibi-arusi Wake ambalo limekwisha kufasiriwa, NI HAYO TU.

Hilo haliondoi wahudumu, au nafasi ambayo Mungu amewaitia. Wameitwa na Mungu kudumisha Neno hilo lililonenwa na nabii wa Mungu mbele ya kundi lao. Wawaelekeze watu wao kwa huyo mjumbe na Ujumbe wa Saa hii.

Kila neno wanalohubiri lazima lipimwe kwa Maneno ambayo nabii wa Mungu aliyosema kwenye kanda. Hawapaswi kubadilisha, wala hata kuweza kufasiri hata NENO MOJA. Maandiko ya Mungu yanafasiriwa TU na nabii Wake.

Sasa, kila moja yao, bila shaka, ungeweza kuona wazo lao, nami siwezi kuyalaumu. Kila moja hudai kwamba wao ndio ile kweli, wana ile kweli. Na watu ambao ni washiriki wa makanisa hayo wanapaswa kuiamini hiyo, kwa sababu wamesalimisha kikomo cha—chao, kikomo chao cha Milele, juu ya mafundisho ya kanisa lile. Nayo yanatofautiana sana, moja kwa lingine, mpaka inazusha maswali mbalimbali mia tisa na kitu.

Ikiwa Ujumbe huu ulionenwa na nabii wa Mungu si Yakini yako, bali ni kile ambacho mtu ama watu fulani wasemayo ndio Neno, Basi kikomo chako cha Milele kinategemea yale WANAYOSEMA.

Maneno yangu yanaonekana kupingana kabisa na ye yote na wahudumu wote. Siwapingi. Ninaamini Mungu ameweka watu halisi katika Kanisa Lake na kuyaangalia makundi Yake kuweka Ujumbe huu mbele yao. Ninaamini wanahubiri na kuamini Ujumbe huu. Lakini kwa nini hawataki kumweka Ndugu Branham nyuma ya mimbara zao Kama Sauti iliyo muhimu sana yakusikia? Kwa nini wanaweka huduma yao kuwa sawa na, pia muhimu kama ile Sauti?

Malaki 3 ilisema, “Namtuma mjumbe Wangu mbele ya uso Wangu kuitengeneza njia.” Na yule ambaye alipelekwa kuitengeneza ile njia, alimtambua Yeye pale. “Huyo Ndiye! Hakuna kosa. Huyo Ndiye! Ninaona ishara ikimfuata Yeye. Najua kwamba huyo Ndiye; Nuru ikishuka kutoka Mbinguni na kukaa juu Yake.” Ilikuwa dhahiri, huyo alikuwa Ndiye.

Basi, ndugu yangu, nataka kukuuliza wewe jambo fulani, katika kufunga. Tungeweza kusema hivi. Hivi katika Malaki 4, hatukuahidiwa tai mwingine, Nguzo ya Nuru itafuata , kuonyesha kanisa lililokosea siku hii kwamba Yeye ni Waebrania 13:8, “yeye yule jana, leo, na hata milele”? Hivi hatukuahidiwa mwingine atakayeruka aje kutoka nyikani?

Je, tunapaswa kufuata nini? Nguzo hiyo ya Nuru. Hiyo Nguzo ya Nuru ni nani? Yule tai, Malaki 4. Ni nani aliyekuwa na Nguzo ya Moto juu ya kichwa chake kumthibitisha yeye alikuwa nani? William Marrion Branham.

Kila wakati tunapokusanyika, hatuna budi kuiweka Sauti hiyo mbele ya watu. Ni lazima tuipe Sauti ya Mungu NAFASI YA KWANZA. Si kumwabudu mtu huyo, bali kumwabudu yule Mungu Aliye Katika mtu huyo.

Huyo ndiye mtu ambaye Mungu amechagua kumwongoza Bibi-arusi Wake. Mtu huyo ndiye mtu ambaye Mungu amechagua kufasiri Neno Lake. Mtu huyo ndiye mtu ambaye Mungu amechagua kufunua kwake siri zake zote. Mtu huyo ndiye ambaye Mungu alisema, “Wafanye watu WAKUAMINI ”, SI MTU MWINGINE YE YOTE AU ASEMAYO MTU AWAYE YOTE YULE, WEWE, WILLIAM MARRION BRANHAM . Mtu huyo ndiye atakayetutambulisha kwa Yesu Kristo.

Mwanamume au mwanamke anayeongeza lo lote kwa yale ninayosema, haamini yale nisemayo.

Njoo na uwe Bi Yesu Kristo pamoja nasi Jumapili hii saa 06:00 SITA MCHANA , saa za Jeffersonville, ( Ni Saa 2:00 MBILI USIKU ya Tanzania) tunaposikia kinywa cha Mungu kilichochaguliwa kikinena na kutuambia:  Mahali Alipopachagua Mungu Pa Kuabudia 65-0220 .

Ndugu. Joseph Branham

Maandiko ya kusoma kabla ya kusikiliza Ujumbe :

Kumbukumbu la Torati 16:1-3
Kutoka 12:3-6
Malaki Sura ya 3 & 4
Luka 17:30
Warumi 8:1
Ufunuo 4:7