All posts by admin5

24-1020 Wakati Wa Kanisa La Efeso

UJUMBE: 60-1205 Wakati Wa Kanisa La Efeso

PDF

BranhamTabernacle.org

Mpendwa Bibi-arusi Wa Kweli,

Ni wakati mzuri sana jinsi gani tulio nao huku Uzima Wake ukitiririka na kudundadunda ndani na kupitia kwetu, ukitupa uzima. Bila ya Yeye, hakungekuwa na uzima wo wote. Neno Lake ndilo pumzi yetu.

Katika siku hii kuu ya giza, sisi ndio kundi Lake la mwisho ambalo limeinuka; Bibi-arusi Wake wa kweli wa siku ya mwisho ambaye atamsikiliza Roho peke yake, Sauti ya Mungu kwa ajili ya siku yetu. 

Jinsi tunavyopenda kumsikia Yeye akituambia, “Kwangu Mimi, umefananishwa na dhahabu safi iliyofuliwa. Haki yako ni haki Yangu. Sifa zako ndio sifa Zangu zenye utukufu. Wewe ndiye Bibi-arusi Wangu wa Kweli wa kupendeza.”

Kama vile vita vyetu vinavyoonekana kuwa vigumu zaidi na zaidi kila wiki, sisi Tunabonyeza Play tu ili kumsikia Yeye akizungumza nasi kwa utamu sana na kutuambia, “Usijali, wewe unaistahili injili Yangu. Wewe ni kitu cha uzuri na furaha. Ninapenda kukutazama pindi unapomshinda adui kwa majaribu na majaribio ya maisha haya.”

Ninaiona taabu yako ya upendo; ni wito mkuu maishani mwako kunitumikia Mimi. Nilijua kabla ya kuwekwa misingi ya ulimwengu ya kwamba wewe ungemtambua malaika Wangu mwenye nguvu ambaye ningemtuma awe Sauti Yangu kwako; jinsi ambavyo usingedanganyika wakati ambapo wale mbwa-mwitu wakali wakija huku wakijaribu kudai ufunuo sawasawa. Wewe Hungetoka kwenye Neno Langu, hata kidogo, HATA KWA NUKTA MOJA. Wewe ungekaa na Neno Langu, Sauti Yangu.

Ungeona wakati ninapokufunulia Neno Langu jinsi gani ule Mzabibu wa Kweli na mzabibu wa uongo ile iliyoanza katika Bustani ya Edeni jinsi ingekua pamoja kote katika nyakati zote. 

Kile kilichoanza katika kanisa la kwanza kingeendelea katika kila wakati. Jinsi ambavyo katika wakati wa kwanza wa kanisa, ule mzabibu wa uongo wa Shetani ungeanza kujiingiza ndani, na kuwashinda washirika kwa roho yake ya unikolai. Lakini jinsi gani ninavyolipenda hili kwamba wewe tu, Bibi-arusi Wangu mteule, hutadanganywa. 

Wiki hii, Nitaliangazia Neno Langu ndani yenu kwa kuifichua ile siri kuu ya ule uzao wa nyoka. Nitawafunulia kwa undani yote yaliyotukia katika bustani ya Edeni; jinsi ambavyo Shetani alivyojichanganya katika jamii ya binadamu. 

Litakuwa wazo la kufurahisha sana wakati mtakapotambua kwamba Mimi, Ule Mti wa Uzima katika Bustani ya Edeni, ambao usingeweza kukaribiwa hadi sasa kwa sababu ya kuanguka kwa Adamu, sasa mmepewa ninyi, washindi Wangu. 

Hii ndiyo itakuwa thawabu yako. Nitakupa haki ya bustani ya Mungu; ushirika wa daima na Mimi. Kamwe hautatengana na Mimi. Po pote Niendapo, wewe, Bibi-arusi Wangu utakwenda. Kile kilicho Changu Mimi, Nitakishiriki na wewe, Mpendwa Wangu.

Jinsi gani mioyo yetu inavyoenda mbio ndani yetu wakati tunapoyasoma maneno haya. Tunajua ule utimilifu wa ahadi zake unakaribia upesi, na ni vigumu kwetu kusubiri. Na hebu tuharakishe kulitii Neno Lake na hapo tuthibitishe kustahili kwetu kushiriki utukufu Wake.

Ningependa kuwaalika mje kuungana nasi wakati tunapoendelea na somo letu kuu la Nyakati Saba za Kanisa, ambapo Mungu anapotufunulia Neno Lake kwa njia Yake aliyoiandaa, malaika-mjumbe Wake wa saba. 

Ndugu. Joseph Branham

Jumapili saa 6:00 sita MCHANA, saa za Jeffersonville. (Ni Saa 1:00 MOJA JIONI ya Afrika Mashariki)
60-1205 Wakati Wa Kanisa La Efeso

24-1013 Ono La Patimo

UJUMBE: 60-1204E Ono La Patimo

PDF

BranhamTabernacle.org

Mpendwa Bibi-arusi Neno Mkamilifu, 

Ni kitu gani kinachotukia ndani ya Bibi-arusi kote ulimwenguni? Tunaingia katika Roho, tukiinuka na kupaza sauti, “Utukufu! Haleluya! Bwana asifiwe!” Mungu anatusafirisha na kulifunua Neno Lake kwa Bibi-arusi Wake.

Mambo ambayo tumeyasoma na kuyasikia maisha yetu yote sasa yanadhihirika. Uhuishaji mkuu unatendeka. Tumeangaziwa na Neno kuliko wakati wowote. 

Tunalihisi ndani kabisa ya nafsi zetu. Kuna kitu fulani cha tofauti, kuna kitu kinatendeka. Tunamhisi Roho Mtakatifu akitutia mafuta, akiijaza mioyo na akili zetu kwa Neno Lake. 

Tunaweza kumsikia Yeye akisema nasi: Najua adui anapigana nanyi kuliko hapo awali, lakini msiogope enyi watoto wadogo, NINYI NI WANGU. Ninawapa upendo Wangu, ujasiri na uwezo. Mnene tu Neno, nami nitalitimiza. Mimi ni pamoja nanyi siku zote.

Katika somo letu kuu la Ufunuo wa Yesu Kristo, tuko chini ya matazamio makubwa kila wiki nini kifuatacho Atakachotufunulia. Neno lake ndilo kimbilio letu pekee, amani na faraja yetu. Tunasikiliza kwa makini tena na tena na tena. Kila aya ndogo tunayosoma, tunataka kupiga kelele na kupaza sauti wakati Neno linapofunuliwa mbele ya macho yetu. Imani ya Kunyakuliwa inakuja juu ya Bibi-arusi, ikizijaza nafsi zetu.

Hebu wazia, hakuna mahali pengine ulimwenguni unapoweza kwenda, ila papo hapo kwenye vidole vyako, kuisikia Sauti ya Mungu ikisema nawe na kulifunua Neno Lake. 

Jinsi ambavyo Mungu alivyoliondoa lile pazia, akalivuta, na kumruhusu Yohana atazame ndani na kuona kile ambacho kila wakati wa kanisa ungefanya, na kuyaandika katika Kitabu na kututumia sisi. Ndipo, wakati utimilifu wa wakati ulipotimia, Mungu alitutumia sisi malaika Wake wa saba mwenye nguvu kukinena, na kufunua yote Ilichomaanisha. 

Yohana aliandika kile alichokiona, lakini hakujua maana yake. Yesu hata hakulijua hilo wakati alipokuwa hapa duniani. Hakuna mtu katika nyakati zote aliyejua, mpaka siku hii, wakati huu, watu hawa, SISI, Bibi-arusi Wake.

Jinsi ambavyo ametufunulia kwamba hizo taa saba zilikuwa zikifyonza uhai na nuru kutoka kwenye hazina ya hilo bakuli kuu. Alitueleza jinsi ambavyo kila mmoja walivyokuwa wametumbikiza tambi zao mle. Kila mjumbe wa wakati wa kanisa alikuwa amewashwa moto na Roho Mtakatifu na utambi wake ukiwa umetumbukizwa ndani ya Kristo, akifyonza uzima halisi wa Kristo na kuitoa Nuru hiyo kwa kanisa. Na sasa, mjumbe wetu wa siku ya mwisho, aliye mkuu kuliko wajumbe wote, alikuwa na maisha yale yale na Nuru ile ile iliyodhihirishwa na maisha yaliyofichwa pamoja na Kristo katika Mungu.

Kisha malaika wetu mwenye nguvu anatuambia kuwa si tu kwamba kila mjumbe alionyeshwa hapo, BALI KILA MMOJA WETU NASI PIA, waamini wa kweli wa Mungu. Kila mmoja wetu pia anawakilishwa wazi wazi hapo. Kila mmoja wetu anafyonza kutoka kwenye chemchemi ile ile kama wale wajumbe. Sote tumetumbukizwa kwenye bakuli lile lile. Tumekufa kwa nafsi zetu na maisha YETU yamefichwa pamoja na, na ndani ya, Kristo Yesu Bwana wetu. 

Jinsi Yeye anavyotutia moyo kwa kusema hakuna mtu anayeweza kututoa sisi kutoka katika Mkono wa Mungu. Maisha yetu hayawezi kuchezewa. Maisha yetu yanayoonekana yanawaka moto na kuangaza, yakitoa nuru na madhihirisho ya Roho Mtakatifu. Maisha yetu ya ndani, yasiyoonekana yamefichwa ndani ya Mungu na kulishwa kwa Neno la Bwana. 

Vita ni vikali. Adui anashambulia kwa hasira kuliko hapo awali, akijaribu awezavyo kutuvunja moyo, kutupiga kabisa, lakini hawezi kulifanya hilo.  Mungu Mwenyewe ananena nasi kupitia midomo ya mwanadamu naye anatuambia, SISI NI BIBI-ARUSI WAKE, ALIYEMCHAGUA, na hilo linamshinda shetani KILA WAKATI. 

Bwana wetu Mkamilifu, akinena Neno Lake Kamilifu, akitoa Amani Kamilifu, kwa Bibi-arusi Wake Mkamilifu.

Kama kawaida, tunaualika ulimwengu mzima uje kuchovya utambi wao ndani ya BAKULI KUU, Ujumbe huu, ambao umehifadhiwa na kutunzwa kwa ajili ya Bibi-arusi. Tutakuwa tukipiga mayowe na kupaza sauti saa 6:00 Sita MCHANA, saa za Jeffersonville, (Ni saa 1:00 Moja JIONI ya Afrika Mashariki) tunapoisikia Sauti ya Mungu ikinena na kufunua yaliyotukia katika: Ono la Patimo 60-1204E.

Ndugu. Joseph Branham 

24-1006 Ufunuo Wa Yesu Kristo

UJUMBE: 60-1204M Ufunuo Wa Yesu Kristo

PDF

BranhamTabernacle.org

Wapendwa Jeshi la Mungu Lisiloweza Kushindwa,

Sisi ndio wale ambao Baba aliyowachagua na kuwapa UFUNUO WA KWELI wa Yeye Mwenyewe; KANISA Lake la KWELI na pekee. Wale aliowachagua watende KAZI Yake KUBWA ZAIDI. Kwa maana kwa Roho Wake, tunaweza kuitambua na kuipinga roho ya mpinga-Kristo ya Shetani. Yeye HANA NGUVU mbele ZETU, kwa sababu sisi ni Jeshi Lake Lisiloweza Kushindwa.

Shetani anachukia ufunuo wote. LAKINI SISI TUNAUPENDA. kwa maana sisi ni wapenzi wa Neno la Mungu lililofunuliwa. Tukiwa na ufunuo wa kweli maishani mwetu, milango ya kuzimu haiwezi kutushinda, tunamshinda adui. Kila pepo yuko chini ya miguu yetu. Sisi ni Mmoja na Yeye nasi tunaweza kunena Neno, kwa maana sisi ni Neno Lake.

Bwana ameliweka hilo moyoni mwangu kwamba tujifunze na kuzisikia Nyakati Saba za Kanisa. Zitakuwa Wiki kuu sana kwa kila mmoja wetu. Atakuwa akitufunulia Neno Lake kuliko hapo awali, kwa nguvu zake za ushindi.

Huu sasa ndio wakati. Haya ndio majira yake. Atakuwa akituhuisha, akitutia moyo, kwa kutupa Changamko kwa Ufunuo, nalo Litaiwasha moto mioyo yetu!!

Ufunuo wa Yesu Kristo ni Kitabu cha kinabii ambacho kinaweza tu kueleweka na tabaka fulani la watu walio na ono la kinabii, SISI, Bibi-arusi Wake. Inahitaji Ufunuo wa KWELI kujua kwamba unasoma na kuisikia Sauti ya Mungu inayotoka kwa malaika-mjumbe Wake aliyemchagua, akitupa mafundisho ya kimbinguni.

Ni Ufunuo wa Yesu Kristo aliopewa Yohana kwa ajili ya Wakristo wa nyakati zote. Ndicho kitabu pekee katika Biblia nzima ambacho kimeandikwa na Yesu Mwenyewe, kwa kumtokea mwandishi Yeye Mwenyewe.

Ufunuo 1:1-2, “Ufunuo wa Yesu Kristo, aliopewa na Mungu awaonyeshe watumwa wake mambo ambayo kwamba hayana budi kuwako upesi; naye akatuma kwa mkono wa malaika Wake na kumwonyesha mtumwa Wake Yohana: aliyelishuhudia Neno la Mungu, na ushuhuda wa Yesu Kristo, yaani, mambo yote aliyoyaona.

Kitabu cha Ufunuo ni mawazo ya Mungu kabisa yaliyoandikwa na Mungu Mwenyewe. Lakini Yeye alituma na kumwonyesha mtumwa Wake Yohana kupitia malaika Wake. Yohana hakujua maana Yake; aliandika tu kile alichokiona na kusikia.

Lakini leo, Mungu alimtuma malaika Wake mwenye nguvu duniani kufunua Ufunuo huu Mkuu kwa Bibi-arusi Wake, ili tuweze kusoma na kusikia yale yaliyokuwa yametukia katika nyakati zote za kanisa. Tunaweza kuliona lile kundi Lake dogo lile lililodumu mwaminifu na wa kweli kwa Neno katika kila Wakati.

Mungu alinena kupitia malaika Wake na kusema ya kwamba katika siku hizi za mwisho, wakati Sauti ya mjumbe Wake wa wakati wa saba wa kanisa itakapoanza kupiga baragumu, Yeye atafunua siri za Mungu kama zilivyofunuliwa kwa Paulo. Wale wanaompokea nabii huyo katika jina lake mwenyewe watapokea matokeo mema ya huduma ya nabii huyo.

Utukufu, sisi ni Bibi-arusi wa Kubonyeza Play wa Mungu ambaye tumempokea nabii huyo katika jina lake mwenyewe, nasi tunapokea matokeo mema. Tunaamini ni Sauti ya Mungu inayonena na kumwongoza Bibi-arusi Wake.

Lo, Kanisa, kile tutakachosoma na kukisikia katika wiki zijazo. Kwake Yeye, sisi tunafananishwa na dhahabu SAFI. Kile alicho Yeye, ndicho tulicho. Sisi ndio Mzabibu Wake wa Kweli. Tumeshinda. Tumefanywa wakamilifu, tumeimarishwa, tumetiwa nguvu. Tumechaguliwa kwa Upendo Wake wa Kuchagua. Hakuna cha kuogopa. Sisi ndio kundi lile lililomsikia mjumbe na Ujumbe wake na Kuutwaa na Kuuishi.

Kila wiki tutakuwa tunasema, “Je, mioyo yetu haiwaki ndani yetu wakati Yeye anaponena na kutufunulia Neno lake njiani”.

Ukitaka kuuhisi upako wa Roho Wake Mtakatifu, kupokea Ufunuo zaidi wa Neno la Mungu, na unataka kuketi katika uwepo wa Mwana kuivishwa, na kupokea Imani ya Kunyakuliwa, njoo uungane nasi Jumapili saa 6:00 Sita MCHANA, saa za Jeffersonville.(Ni saa 1:00 Moja JIONI ya Afrika Mashariki), tunapoanza somo letu kuu juu ya: Ufunuo Wa Yesu Kristo 60-1204M.

Ndugu. Joseph Branham

Ningependa kukuhimiza usikie, au kusoma, kila wiki Kitabu cha Maelezo ya nyakati za Kanisa, sura tuliyomaliza kusikiliza kila Jumapili.

24-0929 Ufunguo Wa Mlango

UJUMBE: 62-1007 Ufunguo Wa Mlango

PDF

BranhamTabernacle.org

Wapendwa Wenye Ufunguo wa Imani,

“Mimi ndiye Mlango wa zizi la kondoo. Mimi ndimi Njia, Njia pekee, Kweli, na Uzima, na mtu haji kwa Baba ila kwa njia ya Mimi. Mimi ndimi Mlango wa vitu vyote, na imani ndiyo ufunguo unaofungua mlango ili uweze kuingia.”

Kuna mkono mmoja tu unaoweza kuushikilia ufunguo huu, na huo ni mkono wa IMANI. IMANI ndiyo ufunguo pekee unaofungua ahadi zote za Mungu. IMANI katika kazi yake iliyokwisha kumalizika inaufungua kila mlango kwa kila hazina iliyo ndani ya Ufalme wa Mungu. IMANI ni Ufunguo malaya mkuu wa Mungu ambao unaufungua KILA MLANGO KWA BIBI-ARUSI WAKE nasi tunaushikilia huo Ufunguo katika MKONO wetu wa IMANI.

Ufunguo huo wa imani uko mioyoni mwetu, nasi tunasema, “Ni Neno la Mungu; Ni ahadi za Mungu kwa ajili yetu, nasi tunaushikilia ufunguo.” Na kisha, kwa kila sehemu ya imani tuliyo nayo, bila kutilia shaka hata chembe moja, tunaufungua kila mlango unaosimama kati yetu na baraka ambazo Mungu alizonazo kwa ajili yetu. Inazima jeuri ya moto. Inaufungua uponyaji kwa wagonjwa. Inaufungua wokovu wetu. Tumefika kwenye Mlango na lolote tunalofanya kwa neno au kwa tendo, tunayafanya yote katika Jina Lake, tukijua kwamba tunao ufunguo wa imani; nao ni ufunguo uliotengenezwa kwa Maandiko.

Sisi hatujali kile mtu yeyote anachowazia, kuna jambo moja la hakika: Mungu alituita SISI, alituchagua SISI tangu awali, alitufunulia SISI Neno Lake, alituambia sisi ni nani, nasi tumeyakinia kulifuata Neno Lake, kwa sababu Yeye ametuita sisi tuwe Bibi-arusi Wake.

Baba alizishikilia nyota Zake saba, wajumbe Wake saba, kwa zile nyakati saba mkononi Mwake. Amewashika mkononi Mwake, hivyo wanahusishwa na nguvu Zake. Hicho ndicho mkono unachomaanisha. Unamaanisha nguvu za Mungu! Na mamlaka ya Mungu.

Tumelishika Neno lake katika mikono yetu ya Imani, ikimaanisha uweza na mamlaka ya Mungu vipo MIKONONI MWETU naye ametupa UFUNGUO wa kuufungua kila mlango kwa kila jambo tunalohitaji. Ni Ufunguo Maalum ambao utaufungua KILA MLANGO.

Sasa ninajua kwa nini Mungu alitupa vidole 5 katika kila mkono; sio 4, sio 6, lakini 5, kwa hivyo kila wakati tunapoitazama mikono yetu tutakumbuka, tunayo ILE IMANI ya kuufungua kila mlango.

Ni ishara ya milele kwa jamii ya binadamu kwa hivyo sisi hatutasahau kamwe; daima tutakumbuka na kujipa moyo, kwamba tunaishikilia IMANI hiyo mikononi mwetu. Naye ataiinua imani yetu ya mbegu ya haradali na kutupa ILE IMANI YAKE KUU KATIKA NENO LAKE LISILOWEZA KUSHINDWA KAMWE, LA MILELE LISILOSHINDWA KAMWE!!!

Tunaweza kuinua mikono yetu Mbinguni, kuvinyoosha vidole vyetu 5 kwa kila mkono na kumwambia, “Baba, tunaamini na tunayo IMANI katika kila Neno ulilonena. Ni Ahadi Yako, Neno Lako, nawe Utatupatia Ile IMANI TUNAYOHITAJI ikiwa tu tutaamini….nasi TUNAAMINI.”

Kwa vile tutakuwa na ibada yetu ya Ushirika hadi ifikapo Jumapili jioni, ningependa kuwahimiza mchague Ujumbe wa kusikiliza pamoja na Kanisa lako, familia, au mtu binafsi, Jumapili asubuhi, kwa wakati unaofaa kwako. Hakika hakuna njia bora ya kuitathmini Imani yetu kuliko kusikia Neno; kwa maana IMANI huja kwa kusikia, kulisikia Neno, nalo Neno huja kwa nabii.

Hebu Basi tuungane wote kwa pamoja saa 11:00 kumi na moja JIONI. (kwa masaa ya nchi yako) ili kusikiliza Ujumbe, 62-1007 Ufunguo wa Mlango. Kama ilivyotangazwa, ningependa kuifanya hii kuwa Ibada Maalum ya Ushirika, ambayo itakuwa ikicheza kwenye Redio ya Sauti (Voice Radio) saa 11:00 kumi na moja JIONI. (Masaa ya Jeffersonville). Mnaweza kupakua na kucheza ibada kwa Kiingereza au lugha zingine kwa kubofya hapa: BOFYA HAPA.

Sawa na ibada zingine za Ushirika wa Nyumbani katika wakati uliyopita, mwishoni mwa kanda Ndugu Branham ataombea mkate na divai. Kutakuwa na muziki wa piano kwa dakika kadhaa ili mkamilishe sehemu ya ibada ya Ushirika. Kisha, Ndugu Branham atasoma Maandiko yanayohusu kutawadhana miguu, na Nyimbo za Injili zitafuata usomaji wake kwa dakika kadhaa, ili muweze kukamilisha sehemu ya ibada ya kutawadhana miguu.

Ni fursa iliyoje tuliyo nayo kumwalika Bwana wetu Yesu kula pamoja na kila mmoja wetu katika nyumba zetu, makanisani, au popote ulipo. Niombeeni wakati mnapozungumza Naye, kama ilivyo hakika nitakuwa nikiwaombea.

Mungu awabariki,

Ndugu Joseph Branham

TANGAZO LA IBADA YA USHIRIKA WIKI HII

Ilitumwa jana: Jumatatu, tarehe 23 Septemba, 2024

Ndugu na dada,

Ningependa tuwe na Ibada nyingine ya Ushirika na Kutawadhana Miguu Jumapili hii, tarehe 29 Septemba, Bwana akipenda. Kama tulivyofanya wakati uliyopita, ningewahimiza muanze saa 11:00 KUMI NA MOJA JIONI. kwa masaa ya nchi zenu. Ingawa Ndugu Branham alisema mitume wao walifanya Ushirika kila wakati walipokutana pamoja, Yeye alipendelea kuufanya wakati wa jioni, naye akautaja kama Meza ya Bwana.

Ujumbe na ibada ya Ushirika itakuwa kwenye Redio ya Sauti, na pia kutakuwa na anuani ya faili la kupakuliwa kwa wale ambao hawawezi kuipata Redio ya Sauti Jumapili asubuhi.

Kwa waamini wa eneo la Jeffersonville, tutakuwa na divai ya Ushirika tena itakayopatikana kwa ajili ya kuja kuchukua. Tangazo litatoka hivi karibuni kueleza mahali, siku na saa.

Hakika niko chini ya matarajio kwa sisi kushika agizo hili la thamani ambalo Bwana alilotuachia. Ni fursa ilioje kwetu sisi kuandaa nyumba zetu na kuifungua mioyo yetu kwa ajili ya Mfalme wa Wafalme aingie na kula pamoja nasi Mezani Pake.

Mungu awabariki,

Ndugu Joseph

https://branhamtabernacle.org/en/bt/A9/109403

24-0922 Edeni Ya Shetani

UJUMBE: 65-0829 Edeni Ya Shetani

PDF

BranhamTabernacle.org

Mpendwa sifa ya Mungu,

Sisi ndio sifa halisi ya Baba yetu wa Mbinguni; kwa maana tulikuwa ndani yake hapo mwanzo. Hatukumbuki hilo sasa, lakini tulikuwa pamoja Naye, na Yeye alitujua. Alitupenda sana hata akatufanya kuwa mwili, ili aweze kuwasiliana nasi, kuzungumza nasi, kutupenda, hata kutushika mikono.

Lakini Shetani alikuja na kupotosha Neno la asili la Mungu, Ufalme Wake, na mpango Wake kwa ajili yetu. Aliwapotosha wanaume na wanawake na kufanikiwa katika kupotosha na kuuteka ulimwengu huu tunaoishi. Ameufanya ulimwengu kuwa ufalme wake, bustani yake ya Edeni.

Ni saa danganyifu na yenye hila iliyowahi kuwako. Ibilisi ameweka kila mtego wa ujunja awezao; maana yeye ni mdanganyifu mkuu. Mkristo hana budi kuwa mwangalifu zaidi leo kuliko alivyowahi kuwa katika wakati wowote.

Lakini wakati huohuo, ndio wakati uliyo mzuri zaidi ya nyakati zote, kwa sababu tunaelekea kwenye ule Utawala wa Miaka Elfu mkuu. Bustani yetu ya Edeni inakuja hivi karibuni, ambamo tutakuwa na upendo mkamilifu na ufahamu mkamilifu wa upendo wa Mungu. Tutakuwa hai na salama pamoja Naye katika Edeni yetu Milele yote.

Yesu alituambia katika Mathayo 24 tunapaswa kuwa waangalifu jinsi gani katika siku hii. Alituonya kwamba ingekuwa ni siku ya udanganyifu sana iliyowahi kuwepo, “inafanana sana hata ingewadanganya wale Walioteuliwa na Mungu kama yamkini”; kwa kuwa ujanja wa Ibilisi utawafanya watu waamini ya kwamba wao ni Wakristo, wakati wao sio.

Lakini wakati huu pia ungemtoa Bibi-arusi Neno safi wake ambaye hangedanganyika na asingeweza kudanganywa; kwa maana wangedumu na Neno Lake la asili.

Kama Yoshua na Kalebu, Nchi yetu ya ahadi imeanza kuonekana kama vile yao ilivyoanza kuonekana. Nabii wetu alisema Yoshua maana yake ni, “Yehova-Mwokozi”. Alimwakilisha kiongozi wa wakati wa mwisho ambaye atakuja kwa kanisa, kama vile Paulo alivyokuja kama kiongozi wa kwanza.

Kalebu aliwakilisha wale waliomtii Yoshua. Kama vile wana wa Israeli, Mungu alikuwa amewaanzisha kama bikira kwa Neno Lake; bali wao walitaka kitu tofauti. Nabii wetu alisema, “vivyo hivyo na kanisa hili la siku za mwisho nalo.” Kwa hiyo, Mungu hakuwaacha Waisraeli waingie katika nchi ya ahadi mpaka wakati Wake Mwenyewe uliokusudiwa ulipowadia.

Watu walimsonga Yoshua, kiongozi wao waliyepewa na Mungu, na kusema, “Hiyo nchi ni yetu, hebu na twende tukaitwae. Yoshua, umeshindwa, lazima umepoteza agizo lako. Huna ile nguvu uliyokuwa nayo. Ulikuwa ukisikia kutoka kwa Mungu na kujua mapenzi ya Mungu, na kutenda kwa haraka. Una kasoro fulani wewe.”

Yoshua alikuwa nabii aliyetumwa na Mungu, naye alijua ahadi za Mungu. Nabii wetu alituambia:

“Mungu aliuweka uongozi mzima katika mikono ya Yoshua kwa sababu alikuwa amedumu na Neno. Mungu aliweza kumwamini Yoshua lakini si hao wengine. Kwa hiyo itajirudia katika siku hizi za mwisho. Shida ile ile, usumbufu ule ule.”

Kama vile Mungu alivyofanya na Yoshua, Yeye aliuweka UONGOZI MZIMA mikononi mwa malaika-nabii Wake, William Marrion Branham; kwa maana alijua angeweza kumwamini yeye, lakini si hao wengine. Ilibidi kuwe na Sauti Moja, Kiongozi Mmoja, Neno Moja la mwisho, wakati huo, na SASA HVI.

Ninapenda jinsi nabii alivyotuambia kutakuwa na maelfu mara maelfu ambao watakaozisikia kanda. Alisema kuwa hizo kanda NI HUDUMA. Kutakuwa na baadhi yetu tutakaoingia kwa siri Majumbani na makanisani tukiwa na kanda (huduma yake) ili kuupata Uzao wa Mungu uliochaguliwa tangu awali.

Tuliporudi na kusema, Bwana, tumetii maagizo yako, nako kulikuwa na watu tuliowapata tulipozicheza kanda walioamini. Sasa tumehubiri jambo hilo, kote ulimwenguni, Je, utatimiza hilo?

Yeye atasema: “Hilo ndilo Mimi nililowatuma kufanya.”

Mungu atalitimiza hilo. Nyumba yako kamwe haitaporomoka. Wakati Mungu atakapotoa ishara ya kukiangamiza kitu hicho chote, familia yako yote, mali zako zote, zitakuwa salama nyumbani mwako. Unaweza kusimama humo. Haikulazimu kuchungulia dirishani, wewe Bonyeza Play tu huku vita vikiendelea.

Maneno yako yalionekana, nami nikayala; na maneno yako yalikuwa ni furaha kwangu, na shangwe ya moyo wangu; maana nimeitwa kwa jina lako, Ee Bwana, Mungu wa majeshi.

Ninakualika uje uungane nasi wakati tunapokula huduma kuu ya Mungu, hai, ya wakati wa mwisho, Jumapili hii saa 6:00 SITA MCHANA, saa za Jeffersonville,(Ni saa 1:00 Jioni ya Afrika mashariki) tunaposikia yote yanayohusu: Edeni ya Shetani 65-0829.

Hebu tuishi mpaka kuja Kwake Bwana kama ikiwezekana. Hebu na tutende kila kitu kilicho katika uwezo wetu kwa upendo, na uelewano—kuelewa kwamba Mungu anauchunguza ulimwengu, siku hii ya leo, kutafuta kila kondoo aliyepotea. Hebu tuzungumze nao kwa maombi ya upendo yaliyokolea chumvi na Neno la Mungu, ili tuweze kumpata huyo wa mwisho kusudi tupate kwenda nyumbani, na tutoke katika Edeni hii ya kale ya Shetani hapa, Bwana.

Ndugu. Joseph Branham

Maandiko ya kusoma kabla ya kusikiliza Ujumbe:

2 Timotheo 3:1-9
Ufunuo 3:14
2 Wathesalonike 2:1-4
Isaya 14:12-14
Mathayo 24:24

24-0915 Chujio La Mtu Mwenye Busara

UJUMBE: 65-0822E Chujio La Mtu Mwenye Busara

PDF

BranhamTabernacle.org

Mpendwa Bi. Yesu Kristo,

Roho wa Mungu aliye hai, tupulizie. Hebu tuchukue Chujio lako nasi tuishi chini ya Hilo, Bwana. Tupulizie hewa safi ya Roho Mtakatifu ndani ya mapafu yetu na ndani ya nafsi zetu kila siku. Tunaweza tu kuishi kwa Neno Lako; kila Neno litokalo katika kinywa Chako kwa ajili ya wakati huu tunaoishi.

Sisi tumeonja mambo Yako ya Mbinguni nasi tuna Neno Lako mioyoni mwetu. Tumeliona Neno Lako likidhihirishwa mbele yetu, na nafsi yetu yote imesitiriwa ndani Yake. Ulimwengu huu, na mambo yote ya Ulimwengu yamekufa kwetu.

Sisi ni chembechembe iliyo hai, mbegu Neno ambayo iliyokuwa ndani Yako tangu mwanzo Tukisimama hapa tukiivuta ile mbegu yako ya Uzima. Mbegu yako imo mioyoni mwetu kwa kujua kwako tangu awali. Ulituchagua tangu awali tusivute kupitia chochote kile, ila Neno Lako, Sauti Yako, kwenye kanda.

Ule wakati wa jicho umefika; hakuna kilichosalia ila Kuja Kwako kumjia Bibi-arusi Wako. Chujio letu ni Neno Lako, Malaki 4, Bwana Asema Hivi.

Hebu tulipande Neno Lako mioyoni mwetu, na tuazimie ya kwamba hatutageuka mkono wa kulia ama wa kushoto, bali tuishi tukiwa waaminifu Kwake siku zote za maisha yetu. Baba, tutumie juu yetu Roho Mtakatifu wa Uzima, na alihuishe Neno Lako kwetu, ili tupate kukudhihirisha Wewe.

Shauku ya mioyo yetu ni kuwa wana na binti wa kweli Kwako. Tumeketi katika uwepo wa Sauti Yako, tukiivishwa, tukijifanya wenyewe tayari kwa ajili ya Karamu yetu ya Harusi pamoja nawe hivi karibuni.

Mataifa yanavunjika. Ulimwengu unavurugika. Matetemeko ya ardhi yanaitikisa California kama vile Wewe ulivyotuambia ingefanya. Tunajua hivi karibuni Kipande kinene cha maili elfu moja na mia tano, upana wa maili mia tatu ama mia nne kitazama, labda maili arobaini ndani ya ule ufa kule. Mawimbi yataruka mpaka mkoa wa Kentucky, Na wakati kitakapozama, kitaitikisa dunia sana mpaka kila kitu juu yake kitaanguka chini.

Onyo lako la mwisho linaendelea. Ulimwengu uko katika machafuko kamili, lakini wakati wote Bibi-arusi Wako anapumzika ndani Yako na Neno Lako, ameketi pamoja katika ulimwengu wa roho unapozungumza nasi, na kutufariji njiani.

Jinsi gani tunavyoshukuru, Baba, kwamba tunaweza kwa urahisi “Kubonyeza Play” na kuisikia Sauti Yako ikizungumza nasi, kututia moyo na kutuambia:

Msiogope, enyi kundi dogo. Yote niliyo Mimi, ninyi ni warithi wake. Nguvu Zangu zote ni zenu. Uwezo Wangu ni wenu ninaposimama katikati yenu. Sikuja kuleta hofu na kushindwa, bali upendo na ujasiri na uwezo. Nimepewa mamlaka yote nanyi mnaweza kuitumia. Ninyi neneni Neno Nami nitalitimiza. Hilo ni agano Langu wala haliwezi kushindwa kamwe.”

Ee Baba, hatuna cha kuogopa. Unatupa upendo wako, ujasiri na uwezo wako. Neno Lako liko ndani yetu kulitumia tunapolihitaji. Tunalinena, na Wewe Utalitimiza. Ni agano Lako, nalo haliwezi KUSHINDWA KAMWE.

Maneno yapatikayo na mauti hayawezi kueleza jinsi gani tunavyojisikia, Baba, lakini tunajua Wewe unaona ndani ya mioyo na roho zetu; kwa maana sisi ni sehemu Yako.

Jinsi gani tunavyoshukuru kwamba Umeiandaa njia kwa ulimwengu kuisikia Sauti Yako katika wakati huu wa mwisho. Kila wiki, Wewe unaualika ulimwengu mzima uje kuungana kumsikia malaika-mjumbe wako wakati Wewe unapotulisha Chakula cha Kondoo ambacho kimehifadhiwa ili kutudumisha hadi Utakaporudi kutuchukua.

Tunakupenda Baba.

Ndugu. Joseph Branham

Ujumbe: 65-0822E Chujio La Mtu Mwenye Busara

Muda: Saa 06:00 SITA MCHANA, Saa za Jeffersonville(Ni saa 1:00 MOJA JIONI ya Afrika mashariki)

Maandiko: Hesabu 19:9 / Waefeso 5:22-26

24-0908 Kristo Amefunuliwa Katika Neno Lake Mwenyewe

UJUMBE: 65-0822M Kristo Amefunuliwa Katika Neno Lake Mwenyewe

PDF

BranhamTabernacle.org

Mpendwa Maskani ya Branham,

Jinsi gani macho yetu yalivyobarikiwa; maana yanaona. Jinsi gani masikio yetu yalivyobarikiwa; maana yanasikia. Manabii na watu wenye haki walitamani kuona na kusikia yale tuliyoyaona na kuyasikia, lakini hawakuyaona. Sisi vyote viwili TUMEONA NA KUISIKIA SAUTI YA MUNGU.

Mungu Mwenyewe alichagua kuiandika Biblia Yake kupitia manabii Wake. Mungu Mwenyewe pia alichagua kufunua siri Zake zote katika wakati huu wa mwisho kwa Bibi-arusi Wake kupitia nabii Wake. Ni sifa Zake, Neno Lake lililodhihirishwa, likifanya jambo hilo lote kuwa sehemu Yake.

Pindi wakati wetu ulipowadia, Yeye alimwasilisha nabii Wake akawasili wakati uo huo. Alimvuvia na kunena kupitia yeye. Ilikuwa ndiyo njia Yake iliyokusudiwa tangu zamani na iliyoandaliwa ya kufanya jambo hilo. Kama vile Biblia, Ni Neno la Mungu, na si neno la mwanadamu.

Ni lazima tuwe na Yakini, mkataa; Neno la mwisho. Baadhi ya watu husema Biblia ndio Yakini yao, si yale yanayosemwa kwenye kanda; kana kwamba zinasema kitu tofauti. Ni ajabu sana jinsi Mungu ameuficha Ufunuo wa kweli wa Neno Lake kwa wengi sana, lakini ameufunua na kuuweka wazi sana kwa Bibi-arusi Wake. Wengine hawawezi kujizuia, wamepofushwa na hawana Ufunuo kamili wa Neno la Mungu lililofunuliwa.

Mungu alisema katika Neno Lake (Biblia) kupitia nabii Wake na kutuambia, “Mungu, ambaye alisema zamani na baba zetu katika manabii kwa sehemu nyingi na kwa njia nyingi”. Hivyo, manabii wa Mungu waliiandika Biblia. Haikuwa wao, bali Mungu akinena kupitia wao.

Alisema katika siku yetu Yeye angemtuma Roho wake wa kweli ili atuongoze katika kweli zote. Yeye hatanena kwa shauri lake mwenyewe; lakini yote atakayoyasikia atayanena, na mambo yajayo atatuonyesha.

Ujumbe uliyo kwenye kanda ndio kweli za Mungu zilizofunuliwa. Haihitaji fasiri yoyote. Ni Mungu akilifasiri Neno Lake Mwenyewe wakati anapolinena kwenye kanda.

Hakuna mwendeleo katika yale watu wengine wanachozungumza, Ila tu kile Mungu anenacho. Kile kinachosemwa kwenye kanda ndio Sauti pekee ambayo HAITABADILIKA KAMWE. Watu hubadilika, mawazo hubadilika, fasiri hubadilika; Neno la Mungu halibadiliki kamwe. Ndio Yakini ya Bibi-arusi.

Nabii anatupa mfano wa rifarii kuwa ndio yakini katika mchezo wa mpira. Neno lake ndilo la mwisho. Huwezi kulihoji. Kile anachosema, ndivyo hivyo, Mwisho wa maneno. Sasa rifarii ana kitabu cha sheria ambacho lazima akipitie. Kinamwambia mahali yalipo maeneo ya mpira kawaida au goli, ni wakati gani salama kwako na wakati gani uko nje; sheria ni zipi kwa mchezo wa mpira.

Anasoma na kukisoma kitabu hicho ili anaponena, na kufanya uamuzi wake, hiyo ndiyo sheria, hilo ndilo neno la mwisho. Hamna budi kudumu na kile anachosema, hakuna swali, hakuna mabishano, chochote anachosema, hivyo ndivyo kinavyopaswa kuwa nacho hakiwezi kubadilishwa. Utukufu.

Ndugu Branham hakusema hupaswi kuhubiri, au kufundisha; kinyume chake, yeye alisema muhubiri, na kuwasikiliza wachungaji wenu, lakini Sauti ya Mungu iliyo kwenye kanda haina budi kuwa Yakini yenu.

Kunapaswa kuwe na nguzo ya kushikilia; kwa maneno mengine, mkataa. Kila mtu hana budi kuwa na mkataa huo. Ni neno la mwisho. Mungu ametoa mahali pamoja tu pa kulipata hilo, Sauti ya Mungu kwenye kanda. Ndio fasiri ya kiungu ya Neno la Mungu. NDILO NENO LA MWISHO, ILE AMINA, ILE BWANA ASEMA HIVI.

Yesu Mwenyewe alisema tunawaita “miungu,” walionena Neno Lake; nao walikuwa miungu. Alisema wakati manabii walipotiwa mafuta na Roho wa Mungu, walilileta Neno la Mungu sawasawa. Ilikuwa ni Neno la Mungu likinena kupitia kwao.

Hiyo ndiyo sababu nabii wetu alikuwa jasiri sana. Aliongozwa na Roho Mtakatifu kunena Neno la Mungu lisilokosea. Mungu alikuwa amemchagua kwa ajili ya wakati wetu. Akauchagua Ujumbe ambao angeunena, hata tabia ya nabii wetu na kile kingetukia katika wakati wetu.

Maneno aliyonena, vile alivyotenda, imewapofusha wengine, lakini imeyafungua macho yetu. Yeye hata alimvalisha kwa namna ya mavazi aliyovaa; tabia yake, shauku yake, kila kitu jinsi tu ilivyompasa kuwa, alichaguliwa tu kikamilifu kwa ajili yetu sisi, Bibi-arusi wa Mungu.

Ndiyo maana, wakati TUNAPOKUSANYIKA PAMOJA, Ni Sauti ndio tunayotaka kuiweka KUWA YA KWANZA kuisikia. Tunaamini kwamba tunalisikia Neno Safi lililonenwa kutoka kwa mjumbe mteule na aliyechaguliwa wa Mungu.

Tunajua wengine hawawezi kuliona au kulielewa hilo, lakini yeye alisema alikuwa akilizungumzia kusanyiko lake peke yake. Yeye hakuwajibika na wale ambao Mungu aliowapa wengine kuwachunga; yeye aliwajibika tu na aina ya Chakula anachotulisha sisi.

Ndiyo maana tunasema sisi ni Maskani ya Branham, kwa sababu yeye alisema Ujumbe ulikuwa kwa ajili ya watu wake tu katika Maskani, lile kundi dogo lililotaka kuzipata na kuzisikiliza kanda. Alikuwa anawazungumzia wale Mungu aliyompa kuwaongoza.

Yeye alisema, “kama watu wanataka kutengeneza chakula cha kisasa na kadhalika huko nje, wewe pata ufunuo kutoka kwa Mungu kisha ufanye yale ambayo Mungu anakwambia ufanye. Nitafanya jambo lilo hilo. Bali Jumbe hizi, kwenye kanda, ni kwa ajili ya kanisa hili peke yake.”

Jinsi gani alivyolifanya Hilo rahisi kweli kweli kwa Bibi-arusi Wake kuliona na kuisikia Sauti ya Mungu na kufuata maagizo Yake.

Iwapo ungependa kuungana nasi kuisikia Sauti hiyo, tutakuwa tukisikiliza sote kwa wakati mmoja Jumapili hii saa 6:00 SITA MCHANA, saa za Jeffersonville,(Ni saa 1:00 MOJA JIONI masaa ya Afrika mashariki): 65-0822M – “Kristo Amefunuliwa Katika Neno Lake Mwenyewe”.

Ikiwa huwezi kuungana nasi, nakuhimiza usikilize Ujumbe huu wakati wowote uwezapo.

Ndugu. Joseph Branham

Maandiko ya kusoma kabla ya kusikiliza Ujumbe:

Kutoka 4:10-12
Isaya 53:1-5
Yeremia 1:4-9
Malaki 4:5
Luka Mt. 17:30
Yohana Mt.1:1 / 1:14 / 7:1-3 / 14:12 / 15:24 / 16:13
Wagalatia 1:8
2 Timotheo 3:16-17
Waebrania 1:1-3 / 4:12 / 13:8
2 Petro 1:20-21
Ufunuo 1:1-3 / 10:1-7 / 22:18-19

24-0901 Nawe Hujui

UJUMBE: 65-0815 Nawe Hujui

PDF

BranhamTabernacle.org

Ndugu na Dada Wapendwa,

Kaeni karibu na Kristo. Hebu niwaonye sasa, kama mhudumu wa Injili, juu ya jambo hili. Msichukue upumbavu wo wote. Msiwazie cho chote. Kaeni moja kwa moja pale mpaka huu wa ndani wa ndani umetiwa nanga kwenye Neno, mpaka uwe ndani ya Kristo kabisa, kwa maana hicho ndicho kitu pekee ambacho kitaninino…Kwa maana, tuko katika wakati wa udanganyifu sana tuliopata kuishi ndani yake. “Utawapoteza walio Wateule kama yamkini,” kwa maana wana upako, wanaweza kufanya cho chote kama wengine wao.

Baba, Ulituonya kwamba tunaishi katika wakati wa udanganyifu zaidi ya nyakati zote. Roho hizo mbili ulimwenguni zingefanana sana, ingewadanganya walio wateule, kama yamkini. Lakini Bwana asifiwe, isingewezekana kutudanganya sisi, Bibi-arusi Wako; tutakaa na Neno Lako.

Sisi ni Uumbaji Wako Mpya, nasi hatuwezi kudanganywa. Tutakaa na Sauti Yako. Tutaitikia na kushikilia kila Neno, bila kujali mtu yeyote anasema nini. Hakuna njia nyingine isipokuwa Njia Yako iliyoandaliwa; Bwana Asema Hivi kwenye kanda. 

Wakati nabii Wako alipokuwa hapa duniani, yeye alijua jinsi gani ilivyokuwa muhimu kwa Bibi-arusi kusikia kila Neno lililonenwa, kwa sababu hiyo yeye alimuunganisha Bibi-arusi Wako kwa mawasiliano ya simu. Alituunganisha pamoja kwenye Sauti Yako iliyothibitishwa ya Neno Lililonenwa.

Yeye alijua hapakuwepo na upako mkuu kuliko Sauti Yako. 

Huko nje kwenye mawimbi ya simu hii, naomba Roho Mtakatifu aliye mkuu aingie katika kila kusanyiko. Jalia Nuru ile ile Takatifu tunayoiangalia papa hapa kanisani, jalia imwangukie kila mmoja, na kila mtu.

Kila kitu ambacho Bibi-rusi Wako anachohitaji kwa ajili ya kule Kuja Kwako kilinenwa, kikahifadhiwa na kufunuliwa kwa Bibi-arusi Wako na malaika Wako; hilo ni Neno Lako. Ulituambia ikiwa tuna maswali yoyote, twende kwenye kanda. Ulituambia William Marrion Branham alikuwa ndiye Sauti Yako kwetu. Kunawezaje kuwa na swali niani mwa Bibi-arusi Wako jinsi gani ilivyo muhimu kuiweka Sauti Yako kama Sauti iliyo muhimu zaidi Anayoweza kuisikia? Hakuna swali Bwana, kwa Bibi-arusi Wako.

Nabii wako alituambia juu ya ndoto ambapo alisema, “Nitapanda farasi kupitia njia hii tena.” Hatujui hilo linamaanisha nini, lakini kwa hakika Bwana, Sauti Yako imepanda farasi kwa njia ya mawimbi ya hewa leo tena, ikinena, na kumwita Bibi-arusi Wako atoke kutoka kote ulimwenguni.

Unaalikwa uje uungane nasi, Maskani ya Branham, Jumapili saa 6:00 SITA MCHANA, saa za Jeffersonville,(Ni saa 1:00 MOJA JIONI ya Afrika mashariki) tunaposikiliza Sauti ya Mungu kupitia mawimbi ya hewa ikituletea Ujumbe: 65-0815 – “Nawe Hujui”.

Ndugu. Joseph Branham

  Maandiko ya kusoma:

Ufunuo 3:14-19
Wakolosai 1:9-20

24-0825 Matukio Yakidhihirishwa Na Unabii

UJUMBE: 65-0801E Matukio Yakidhihirishwa Na Unabii

PDF

BranhamTabernacle.org

Tai Wapendwa,

Palipo na Mzoga, tai wanakusanyika. Ni wakati wa jioni, na unabii umetimizwa mbele ya macho yetu. Mioyo yetu inawaka ndani yetu tunapomwalika katika makanisa yetu, nyumba zetu, na vibanda vyetu vya udongo huko msituni. Atazungumza nasi na kulifunua Neno Lake. Tunaona njaa na kiu ya Mungu zaidi.

Yeye amechagua njia ile Neno lake lingetujia; ni kwa nabii Wake, ambaye Yeye alimchagua tangu zamani na kumtenga tangu zamani. Alimchagua William Marrion Branham kuwa mtu wa wakati huu kuwashika wateule Wake wa wakati huu, SISI, Bibi-arusi Wake.

Hakuna mtu mwingine anayeweza kupachukua mahali pake. Tunapenda jinsi anavyojieleza; ii, siho, iyo, pepa, dafuta, ni Mungu akizungumza masikioni mwetu. Mungu, akinena kupitia midomo ya mwanadamu, akifanya yale hasa Yeye aliyosema angefanya. Hilo latosha!

Mungu aliongoza mikono na macho yake katika maono. Yeye hakuweza kusema kitu chochote ila kile alichokuwa akikiangalia. Mungu alitawala kabisa ulimi wake, kidole, hata kila kiungo cha mwili wake kilikuwa katika utawala mkamilifu wa Mungu. Alikuwa ndiye kinywa chenyewe cha Mungu.

Mungu alijua kimbele katika wakati huu kanisa lingeingia kwenye mchafuko. Kwa hiyo, Yeye alikuwa na nabii Wake tayari kwa ajili ya wakati wetu, kumwita na kumwongoza Bibi-arusi Wake aliyechaguliwa kwa Neno Lake lililothibitishwa.

Katika mpango Wake mkuu, Yeye pia alijua angempeleka nabii Wake Nyumbani kabla ya Kuja Kwake, kwa hiyo Alihakikisha ameirekodi Sauti Yake na kuihifadhi, ili Bibi-arusi Wake mteule daima wangeweza kuwa na Bwana Asema Hivi kiganjani. Basi wasingekuwa na swali kamwe. Hakukuwa na fasiri iliyohitajiwa, Neno safi na bikira tu waliloweza kulisikia wakati wote.

Alijua kungekuwa na sauti nyingi na machafuko mengi katika siku za mwisho.
Wiki tatu zilizopita amezungumza nasi na kuweka saa tunayoishi. Alituambia kuhusu manabii wa uongo ambao wangetokea na kuwadanganya wateule, kama yamkini.

Jinsi gani huyu mungu wa kizazi hiki alivyoipofusha mioyo ya watu. Na jinsi ambavyo Mungu Mwenyewe alisema kupitia kwa nabii Zake ya kwamba mambo haya yangetukia katika Wakati huu wa Laodikia. Alituambia hakuna kitu ambacho kimeachwa bila kutimia.

Amejitambulisha Mwenyewe mbele zetu kwa mambo yale yaliyotabiriwa kumhusu Yeye kuyafanya katika siku hii. Matendo yake yenyewe yametuthibitishia Yeye ni yeye yule jana, leo, na hata milele. Ni Sauti ya Mungu, ikizungumza na, na kuishi ndani ya, Bibi-arusi Wake.

Je! unaamini Ujumbe huu ni Waebrania 13:8? Kuwa ni Neno lililo hai? Kuwa ni Mwana wa Adamu akijifunua Mwenyewe katika mwili? Basi unabii utatendeka Jumapili hii ikiwa utaamini na kutii.

Kitu fulani kitakuwa kikitendeka ulimwenguni kote ambacho hakijawahi kutokea katika historia ya dunia. Mungu atakuwa akinena kupitia midomo ya mwanadamu, akizungumza na Bibi-arusi Wake kila mahali ulimwengu mzima wote kwa wakati mmoja. Atatufanya tuwekeane mikono na kuombeana mmoja kwa mwingine wakati yeye anapotuombea sisi wote.

Ninyi mlio huko nje kwenye simu, kama mmekwisha amini kwa moyo wenu wote, wahudumu wakiwa wanawawekea mikono, na wapendwa wenu wakiwawekea mikono, kama mnaamini kwa moyo wenu wote ya kwamba imekwisha, imekwisha.

Chochote tunachohitaji, Mungu atatupa ikiwa tu tutaamini… NASI TUNAAMINI. SISI NDIO BIBI-ARUSI WAKE MWAMINIFU. Itatendeka. Nguzo ya Moto itakuwa popote tutakapokusanyika na kumpa kila mmoja wetu chochote tunachohitaji, ni BWANA ASEMA HIVI.

Jalia Nuru ile ile Takatifu tunayoiangalia papa hapa kanisani, jalia imwangukie kila mmoja, na kila mtu, na jalia waponywe wakati huu. Tunamkemea adui, Ibilisi, katika Uwepo wa Kristo; tunamwambia huyo adui, ya kwamba ameshindwa na—na mateso yaliyompata badala yetu, yale mauti ya Bwana Yesu na ushindi wa ufufuo katika siku ya tatu; na ushuhuda Wake uliothibitishwa ya kwamba Yeye yuko hapa kati yetu usiku wa leo, akiwa hai, baada ya miaka elfu moja mia tisa. Jalia Roho wa Mungu aliye hai aujaze kila moyo kwa imani na nguvu, na nguvu za kuponya kutokana na kufufuka kwa Yesu Kristo, Ambaye ametambulikana sasa kwa Nuru hii kuu inayolizunguka kanisa, katika Uwepo Wake. Katika Jina la Yesu Kristo, tujalie kwa ajili ya utukufu wa Mungu.

Wewe ni Bibi-arusi Wake. Hakuna kinachoweza kuliondoa hilo kutoka kwako, HAKUNA CHOCHOTE. Shetani ameshindwa. Unaweza kuhisi una kijiko tu kilichojaa Yeye, hicho ndicho tu unachohitaji, NI HALISI. NI YEYE. WEWE NI WAKE. NENO LAKE HALIWEZI KUSHINDWA.

Liamini, likubali, lishikilie, haliwezi kushindwa. Huna nguvu lakini una mamlaka yake. Sema, “Nimeichukua Bwana, ni yangu, Wewe umenipa hiyo nami sitamwacha Shetani aichukue.”

Tutakuwa na wakati ulioje. Hakuna mahali pengine ningependa kuwa. Roho Mtakatifu atatuzunguka sote. Tumepewa Ufunuo zaidi. Mioyo iliyovunjika. Kila mtu aliponywa. Hatuwezije kusema, “Je! Mioyo yetu haikuwaka ndani yetu, nayo haiwaki sasa, kujua kwamba sasa tuko katika uwepo wa Yesu Kristo aliyefufuka, utukufu na sifa vina yeye milele.

Ndugu. Joseph Branham.

Tunaalika ulimwengu wote uje kuungana nasi:

Muda: saa 06:00 SITA MCHANA masaa ya Jeffersonville(ni saa 1:00 MOJA JIONI masaa ya Afrika mashariki)
Ujumbe: 65-0801E Matukio Yakidhihirishwa Na Unabii

Maandiko ya kusoma kabla ya kusikiliza Ujumbe:

Mwanzo: 22:17-18
Zaburi: 16:10 / Sura ya 22 / 35:11 / 41:9
Zekaria 11:12 / 13:7
Isaya: 9:6 / 40: 3-5 / 50:6 / 53:7-12
Malaki: 3:1 / sura ya 4
Yohana 15:26
Luka Mt: 17:30 / 24:12-35
Warumi: 8:5-13
Waebrania: 1:1 / 13:8
Ufunuo: 1:1-3 / Sura ya 10