Category Archives: Uncategorized

21-0613 Mfalme Aliyekataliwa

UJUMBE: 60-0515M Mfalme Aliyekataliwa

PDF

BranhamTabernacle.org

TAI WANAKUSANYIKA PAMOJA

Wapendwa marafiki wapendwa, wapenzi wa Injili, watoto waliyomzalia Mungu,

Ninashukuru sana tunamsikiliza mchungaji wetu. Sisi ni kondoo anaowachunga. Sisi ni kanisa lake. Kanda hizi zimerekodiwa na kuhifadhiwa kwa ajili yetu. Sisi ni Rafiki za malaika_mjumbe wake wa saba, na wapendwa wapenzi wa Injili. Sisi ni watoto wake aliyomzalia Mungu.

Siku moja ujumbe huu uliangaza mbele yetu na tukamsikia Yesu Kristo yeye yule jana, leo, na hata milele. Imetosheleza ladha yetu, na tunatamani zaidi. Ujumbe huu, Neno Lake, Sauti Yake, ni Bwana Yesu Kristo. Ni yote tunayohitaji, yote tunayotaka, yote tuliyonayo.

Ikiwa ufunuo wowote utawasilishwa kwetu ambao ni kinyume na Neno lililoandikwa, hatutaupokea kamwe, kwa sababu ndivyo Shetani alivyomfanyia Hawa. Alikuwa na Neno, lakini alikuwa akitafuta nuru Fulani mpya, na Shetani aliiona kwamba hawa anayo. Hatutaki kamwe kuongeza chochote kwenye Neno, au kuondoa lolote kutoka kwenye Neno; bali liache tu jinsi lilivyo. Dumu sawa sawa na Neno, kwa maana kitu chochote kilicho kinyume ni kutokuamini. Lazima TUDUMU NA HUDUMA YA KANDA.

“ Sijahubiri cho chote maishani mwangu ambacho nilionea aibu. Mimi sitaagiza kanda zo zote zirudishwe, wala rekodi zo zote. Nitadumu na anayosema Roho Mtakatifu. Hayo nitaishi nayo na kufa nayo.” Mimi sijaribu kuzungumzia juu yangu binafsi, sasa, bali ninajaribu tu kuwapa mfano wa yanayoendelea kusudi mpate kuona na kufahamu. Ni watu kutaka kuongozwa na mwanadamu.

Kanda hizi ni kile ambacho Roho Mtakatifu anachosema kumwongoza Bibi-arusi Wake. Tunaishi kwa kila Neno na tutakufa kwa kila Neno, kwa maana Ni Bwana Asema Hivi. Tutasimama na Neno la Mungu hata ikiwa itagharimu kila kitu kilicho katika maisha yetu; tutadumu na Neno.

Kila kanda tunayosikia inatuleta karibu zaidi na yeye na kufunua Neno lake zaidi. Daima ni kile hasa tunachohitaji kwa siku hiyo. Hatutaki mwana wa Kishi atuongoze, tunataka njia ya Mungu iliyoandaliwa: Nabii wake.

Ombi letu Ni, ” Ee Mungu, Usituache kamwe tupatane kwa Neno moja. Tujalie tudumu sawasawa katika Neno hilo na kuliishi. Hatujali nini kinachokuja ama kinachokwenda, kile mtu ye yote afanyacho ,tujalie tudumu na Neno lako.”

Vita vinazidi kuwa vigumu na vigumu kila siku. Shetani yuko katika ghasia kubwa zaidi ya hapo awali. Anajua wakati wake umekwisha, siku zake sasa zimehesabiwa. Ana ulimwengu chini ya udhibiti wake, kwa hiyo anamshambulia Bibi-arusi.

Wakati mwingine vita huwa vigumu sana. Tunapata uchovu sana na kuchoka tukipaza sauti.

Nina hamu ya kwetu sana na nina huzuni na nataka kumwona Yesu; Ningetaka kusikia hizo kengele tamu za bandari zikilia; Ingeangaza njia yangu na kutowesha hofu zote; Bwana, hebu tuangalie ng’ambo ya pazia la wakati. Bwana, hebu niangalie ng’ambo ya pazia la huzuni na hofu; Hebu niiangalie hiyo nchi yenye jua na inayong’aa. Ingetia nguvu imani yetu na kutowesha hofu zote; Bwana, hebu na waangalie ng’ambo ya pazia la wakati.

Baba alijua kwamba tungedhoofika na kuchoka, kama nabii Wake. Kwa hiyo asubuhi moja alimuamsha mtumishi Wake, ili kumtia moyo. Akamwacha aangalie na aende Ng’ambo ya Pazia la Wakati.

Ndipo akamrudisha kutuambia jinsi kutakavyokuwa. Hapakuwa na wivu. Hakukuweko na uchovu. Hakukuweko na kifo ama magonjwa kule. Kupatikana na Mauti hakungeweza kutufanya kuzeeka tena. Ilikuwa zaidi ya ukamilifu.

Ndipo Bibi-arusi akamchukua, na kumweka yeye juu ya mahali pamoja pa juu na kupaza sauti akisema:

“ Tunajua jambo hilo, nasi tunajua tunarudi pamoja nawe siku moja duniani.” Kasema, “Yesu atakuja, nawe utahukumiwa kulingana na Neno ulilotuhubiria sisi. Halafu, kama ukikubalika wakati huo, ambapo utakubalika,” kisha kasema, “basi wewe utatukabidhi Kwake kama tunu yako ya huduma yako.”

Kwa hivyo, wakati Bibi-arusi atakaporudi duniani, tutakuwa tunarudi pamoja naye, nabii wa Mungu, na ATATUKABIDHI “KWAKE” KAMA TUNU YA HUDUMA YAKE. Kwa hiyo, lazima tudumu pamoja na huduma ya Kanda.

Nadhani ni muhimu kuingiza hapa kile tulichomsikia nabii akisema wiki chache tu zilizopita:

kanda hizi zinaenda tu…Ninazungumzia kusanyiko langu, ndugu. Mimi siwajibiki na wale Mungu aliokupa kuwachunga; mimi ninawajibika na aina ya Chakula ninachowalisha watu hawa. Hiki ni kwa ajili ya Maskani haya pekee. Mnaona? Sasa, kama watu wanataka kusikiliza kanda, hiyo ni juu yao. Bali mimi ninawazungumzia wale Mungu alionipa.

Ndio maana tunadumu na hizi kanda. Ndio maana tunasema William Marrion Branham ndiye mchungaji wetu. Ndio maana tunasema sisi ni kusanyiko lake. Sisi ndiyo wale Mungu aliyompa. Ndio, sisi ni MMOJA WAO, UTUKUFU.

Ikiwa ungependa kuwa sehemu ya kusanyiko lake, BONYEZA PLAY . Ikiwa ungependa kusikia kanda hizi pamoja nasi, tunakualika uungane nasi Jumapili saa 8:00 nane, mchana, saa za Jeffersonville, (ni saa 3:00 tatu , usiku ya Tz), wakati tutakapoungana na waaminio wengine kutoka kote ulimwenguni kusikia: Mfalme Aliyekataliwa 60-0515M .

Ndugu. Joseph Branham

TD: Nimekuwa katika maombi kwa ajili ya kile kingefuata ambacho Baba angependa tusikilize . Nilijisikia kama alikuwa akiniongoza kuucheza, “Mfululizo wa Kufanywa Wana Wenye Mamlaka.” Nilianza kuomba na kutafuta mapenzi yake. Nilipomaliza kuomba, niliinuka, nikafungua biblia yangu bila mpangilio na kuanza kusoma, ilikuwa ni Wagalatia 4: 1-7. Baba alinihakikishia na kujibu maombi yangu kwa mara nyingine tena.

Mimi na wafanyikazi wa VGR tutachukua muda wa kupumzika kwa wiki 3 zijazo. Wakati wa likizo, nitakuwa nakutumia barua fupi ya uthibitisho wa ujumbe ambao tutakaosikiliza.

Tafadhali nikumbuke mimi na wafanyikazi wa VGR katika maombi yako.

Maandiko ya kusoma kabla ya kusikia ujumbe

1 Samweli Sura ya 8

Mtakatifu Marko 16: 15-18

21-0530 Kristo Amefunuliwa Katika Neno Lake Mwenyewe

UJUMBE: 65-0822M Kristo Amefunuliwa Katika Neno Lake Mwenyewe

PDF

BranhamTabernacle.org

21-0502 Makao Ya Baadaye Ya Bwana Arusi Wa Mbinguni Na Bibi-Arusi Wa Duniani

UJUMBE: 64-0802 Makao Ya Baadaye Ya Bwana Arusi Wa Mbinguni Na Bibi-Arusi Wa Duniani

PDF

pakua – m4a

pakua – amr

BranhamTabernacle.org

21-0418 Kutambua Siku Yako Na Ujumbe Wake

UJUMBE: 64-0726M Kutambua Siku Yako Na Ujumbe Wake

PDF

pakua – amr

BranhamTabernacle.org

Mpendwa Bibi_arusi aliyekatwa atoke,

Mungu alitambua kwamba kulikuwa na watu duniani ambao aliowakusudia Uzima. Alitambua kuwa huu ndio wakati wa kutuma Ujumbe Wake kupitia mjumbe Wake kumwita Bibi-arusi Wake atoke. Amefanya hivyo. Sasa Bibi-arusi Wake ametambua siku yetu na Ujumbe Wake, na ametambua sisi ni nani, kuzaliwa asili kwa Neno.

Sisi ni yule Bibi-arusi ambaye aliyekuja katika onyesho la Awali mbele ya nabii. Bibi-arusi aliyefanana sana na yule aliyepita mwanzoni. Alipotuona, moyo wake uliruka kwa furaha, kwa kujua kwamba kuna Bibi-arusi ambaye atayekaa na Neno. Alipotuona, tulifanywa kwa kitu kimoja, na kuvikwa kwa kitu kimoja kama yule aliyekuwako mwanzo: Alfa na Omega. Sisi ni yule Bibi-arusi Neno kamilifu.

Mungu amembangua Bibi-arusi Wake atoke, amemkatatilia mbali na makanisa mengine yote kupitia nabii Wake, kwa Neno. Sasa, baada ya miaka elfu mbili, na kulingana na Neno Lake lililoahidiwa kwamba angefanya katika siku za mwisho, Ameizuru kambi tena. Ameizuru kambi kudhihirisha Neno Lake kwa ajili ya leo hii, kama vile alivyofanya katika siku za Musa. Kama ilivyokuwa wakati huo, ndivyo ilivyo sasa. Huyo hakuwa Musa aliyetenda hayo; Musa alikuwa mwanadamu. Ilikuwa ni Kristo.

Ilifanyaje? Iliwasumbua makuhani, kuona hao watu wakiondoka makanisani na kwenda zao. Akasema, “kama ye yote wenu akihudhuria mikutano yake, mtatengwa na ushirika. Tutawafukuza moja kwa moja kutoka katika dhehebu. “
Angalia, “Kama vile Yane na Yambre pia walivyompinga Musa,” atakuja moja kwa moja, baadhi yao. Sio, sasa, yeye hazungumzi kuhusu Mmethodisti, Mbaptisti, hapa; wao wako nje ya picha. Unaona?

Lakini ni kitu gani kinachotukia kwa Bibi-arusi? Tunakusanyika pamoja kutoka kote ulimwenguni. Tumeundwa kutoka kote nchini; kutoka New York, kutoka Massachusetts, Maine, Tennessee, Georgia, Alabama, na kote nchini na ulimwenguni kote. Sisi ni Tai tunakusanyika pamoja. “Kutakuwa na Nuru yapata wakati wa jioni.”

Kama kijana mdogo siku zote nilijiuliza, “Bwana, utaletaje Kanisa lako pamoja kama ulivyofanya Kanisa Lako la kwanza?” “Ninasoma katika Neno lako, Wewe kila wakati uliwaleta pamoja wakati ulipotaka kuwaunganisha.” “Je! Utamleta kila mmoja huko Jeffersonville?” “Utafanyaje jambo hilo?” “Je! Sote tutahitaji kukusanywa mahali pamoja?”

Sasa imefunuliwa kwangu, Sio katika makao ya kimwili ambapo Bibi-arusi Wake wanakusanyika pamoja , sio Mlima Mtakatifu, mahali Patakatifu, BIBI-ARUSI ANAKUSANYIKA KWENYE NENO LAKE, kwa kuwa hapo ndipo MAHALI PEKEE ambapo Bibi-arusi anaweza kuungana.

Mungu ameusimamisha ulimwengu ili alitimize Neno lake. Shetani anajaribu kulizuia; kujaribu kulifanyia mzaha. Anajaribu kuwafanya watu waogope kwamba ikiwa watazisikiliza Kanda, watatengwa na Ushirika, watapotea. Lakini hawezi kuzuia kile kinachotokea.

“Ondoka njiani! Nina Ujumbe wa Mfalme. ” Amina. “Mimi ni Mjumbe wa Mfalme,” Neno lililothibitishwa. Nikawazia, “Shetani, ondoka njiani! Nina Ujumbe wa Mfalme. Sina budi kwenda.”
Ni Ujumbe wa Mfalme. Hebu na tuutambue, wapendwa, kwa kuwa tumeitwa kukusanyika pamoja kwa ajili ya kupigwa kwa Baragumu. “Kwa maana Baragumu ya Bwana italia, ndipo hakutakuwa na wakati baada ya hayo.”

Hakuna furaha kubwa, hakuna upako mkubwa zaidi, kuliko kukaa pamoja katika makao ya kimbinguni na Bibi-arusi kote ulimwenguni, tukisikiliza Sauti ya Mungu ikinena kupitia mjumbe wake aliyethibitishwa na kunena Neno la Uzima wa Milele.

Kumbuka katika ono langu? Nilisema, “Ikiwa watu wa Paulo wataingia, na wangu pia wataingia, kwa sababu nimefanya vile hasa alivyofanya.” Ninadumu kabisa nalo. Hao mamilioni walitupa mikono yao, wakisema, “Tunategemea jambo hilo!”

Tai watakusanyika tena Jumapili hii saa 8:00 mchana, saa ya Jeffersonville,(Ni saa 3:00 usiku ya TZ), kumsikia Kristo mwenyewe akizungumza nasi kupitia mjumbe wake aliyethibitishwa. Neno tunalotegemea. Njoo uungane nasi tunapomsikia akiuonya ulimwengu kwamba lazima wawe : Kutambua Siku Yako na Ujumbe Wake 64-0726M

Ndugu. Joseph Branham

Maandiko ya kusoma kabla ya kusikia Ujumbe:

Hosea 6
Malaki 4:5-6
2 Timotheo 3