21-0808 Je! Mungu Hubadilisha Nia Yake?

Ujumbe: 65-0427 Je! Mungu Hubadilisha Nia Yake?

PDF

pakua

BranhamTabernacle.org

Tai wanakusanyika Pamoja.

Mpendwa Bibi_arusi wa Mapenzi Makamilifu,

Ee Mungu mpendwa, hatutaki mapenzi Yako ya kuruhusia, Baba. Jalia tutembee katika mapenzi Yako makamilifu. Hebu tuninii tu—tusichukue tu Neno moja hapa na pale, na kulifanya liafikiane na fundisho fulani la sharti ama kanuni fulani ya imani, ama jambo fulani. Hebu na tuchukue Neno jinsi lilivyo, tukiamini Injili kamili, yote ambayo Yesu alitufundisha kufanya .

Hiyo ndiyo hamu yetu kubwa na ya kina kabisa, ni kuwa katika mapenzi Makamilifu ya Mungu. Hatutaki kamwe kumchukiza, bali kumpendeza katika yote tunayosema na tunayofanya. Tunataka kuwa wana na binti zake wenye Mamlaka na waliyodhihirishwa.

Ni wapi tunapata kujua jinsi ya kuwa katika mapenzi yake Makamilifu na kumpendeza? Ni Lazima tuende kwenye Neno Lake, kwani tunajua Neno Lake ndio kweli na uzima. Neno Lake daima ni lile lile, mpango Wake daima ni ule ule, kwani Yeye hawezi kubadilika.

Neno linatuambia, jinsi alivyofanya mambo mara ya kwanza, atafanya vile vile kila wakati. Lazima yeye abaki vile vile milele. Kusudi lake daima limekuwa lile lile. Matendo yake daima yamekuwa yale yale . Jinsi anavyofanya mambo, jinsi anavyowaponya watu, na jinsi anavyowaongoza watu Wake, daima atabaki vile vile .

Biblia inatuambia katika Neno Lake lisilobadilika kuwa Neno la Bwana huja kwa manabii Wake peke yao. Yeye kamwe hawafunulii makasisi ama mwanatheolojia, manabii Wake tu. Alisema pia hakufanya neno lolote mpaka kwanza alipowaonyesha hilo manabii wake .

Mwanadamu daima amekuwa akitaka mfumo uliotengenezwa na mwanadamu, kundi la watu kuwaongoza. Lakini hiyo kamwe haikuwa njia ya Mungu , Yeye daima alimtuma kiongozi wa kiungu aliyeitwa, nabii aliyeteuliwa akiwa na Neno kuwaongoza watu Wake. Nabii huyo alithibitishwa na alichaguliwa kuwa kiongozi wao wa saa hiyo.

Mungu alichagua na kuweka viongozi wengine wengi waliowekwa wakfu waliojazwa na Roho Mtakatifu; na wana nafasi zao, lakini aliwaonya hao viongozi, “Kaeni mbali na hiyo Nguzo ya Moto.” Je! Nguzo hiyo ya Moto hufanya nini… HUONGOZA WATU MCHANA NA USIKU.

Kisha Neno linatuambia, “Kama ilivyokuwa katika siku za Sodoma, Hivyo ndivyo itakavyokuwa siku Ile atakayofunuliwa Mwana wa Adamu .” Kulingana na Neno Lake katika Malaki 4, na Maandiko mengi, atarudi tena katika Kanisa Lake katika umbo la mwili; katika watu, katika wanadamu, kwa njia ya kuwa nabii.

Tutamtambuaje nabii huyu? Yeye atathibitisha yeye ni nani kwa Neno. Yeye atajua siri za mioyo. Atawafunulia watu Neno lote. Atathibitishwa na Nguzo ya Moto kumwongoza Bibi-arusi. Mungu hata atapigwa picha pamoja na nabii wake.

Wengine watakuwa kama Yohana kwenye kisiwa cha Patmo na kujaribu kumwabudu, lakini atasema, “Angalia usifanye hivyo, mimi ni mjoli wako, na wa manabii, mwabudu Mungu.” Bibi-arusi atajua sio kumwabudu yeye, yule mtu, lakini kumwabudu Mungu KATIKA MTU HUYO.

Atatambua kuwa ndiye yule aliyechaguliwa na Mungu kunena Maneno ya kutokukosea. Atatambua kuwa alikuwa yule malaika_mjumbe wa 7 aliyechaguliwa na Mungu. Ulimwengu utaona na kusikia Sauti ya Mungu ikinena kupitia Yeye na utaona Adamu wa kwanza aliyerejeshwa Kikamilifu.

Atamwongoza Bibi-arusi kwa Nguzo ya Moto. Atakuwa akipata taarifa yake kutoka kwa Logos na kumpa Bibi_arusi njiani mwao kuelekea nchi ya ahadi. Bibi-arusi atakuwa na Ufunuo na kutambua huyu ni mjumbe aliyeandaliwa na Mungu. Hii ndio njia iliyoandaliwa na Mungu. Haya ni MAPENZI MAKAMILIFU ya Mungu .

Njoo uungane nasi Jumapili saa 8:00 Nane Mchana, saa za Jeffersonville (Ni saa 3:00 Tatu Usiku ya Tanzania), Kusikia: Je! Mungu Hubadilisha Nia Yake? 65-0427.

Ndugu. Joseph Branham

Hesabu 22:31