21-0801 Kuthibitisha Neno Lake

Ujumbe: 65-0426 Kuthibitisha Neno Lake

PDF

pakua

BranhamTabernacle.org

Tai wanakusanyika Pamoja.

Wapendwa Watoto Wachanga Wanaoweza kujifunza,

Ni Hali ya kimbinguni jinsi gani tulikuwa tumeketi siku ya Jumapili wakati Bibi-arusi wa Kristo alipokusanyika pamoja katika Uwepo wa Roho Mtakatifu. Tungeweza kuhisi Ikihuisha miili yetu inayokufa.

Hakuna upako mkuu zaidi, hakuna hali kuu zaidi, kuliko wakati Ukibonyeza Play na kusikia Sauti ya Mungu ikizungumza nawe. Mungu ameweka masikio yetu kusikia na kuamini kila Neno, kwani si mwingine isipokuwa El, Elah, Elohim, Yule aliyekuwepo, anayejitosheleza, mwenye nguvu, akiongea na kila mmoja wetu na kutufunulia sisi Kuwa ni wana na binti zake waliodhihirishwa.

Jinsi gani ilivyokuwa yenye nguvu wakati Uzao wa Mungu uliochaguliwa awali, kutoka kote ulimwenguni, walipoweka mikono yao mitakatifu juu ya mmoja kwa mwingine. Nyumba zetu na makanisa yetu yalijazwa na Uwepo wa Roho Mtakatifu. Imani yetu ilikuwa imejengwa, kwani tulijua ni nani anayesema nasi. Kisha akatuambia kuwa ile nguvu ya kuhuisha ilikuwa NDANI YETU. Tuliamini kwa mioyo na roho zetu zote, kwa sababu alisema hivyo.

Ndipo akatuambia tuseme, “Bwana Mungu, naamini kwa moyo wangu wote.” Tulirudia kila Neno kutoka kwenye kina cha mioyo yetu. Alisema, “Ugonjwa hauwezi kusimama katika kundi kama hili.” Roho yetu ilifurahi tuliposikia Maneno haya, kwa maana tulijua kilichokuwa kinatendeka.

Alisema, “Kila mtu anayemtaka Roho Mtakatifu, inua mikono yako, POPOTE ULIPO unayetaka hilo… ninaamini kwamba Mungu atamjaza kila mmoja wenu, SASA HIVI, na Roho Mtakatifu.”
Wakati huo huo, tulijazwa, na kujazwa upya, na Roho Wake Mtakatifu, Sauti ya Mungu ilitamka hivyo.

Kisha kwa wale ambao waliyohitaji uponyaji katika miili yao, Alisema, “Ninakuamuru, katika Jina la Yesu Kristo, simama kwa miguu yako na kukubali uponyaji wako.” Wakati huo huo, kila mwamini, kutoka kote ulimwenguni, ambaye alikuwa na IMANI na aliamini, ALIPONYWA.

Je! Hili lilitendeka wapi? Katika kundi moja dogo la watu lililokusanyika pamoja? Hapana, ilikuwa kutoka ULIMWENGUNI kote wakati Bibi-arusi alipoketi pamoja katika Ulimwengu wa Roho kusikiliza Sauti ya Mungu kwa ajili ya siku yetu.

HAIWEZEKANI kwa mtu yeyote, au kundi la watu, kumuunganisha Bibi-arusi namna hiyo. Ni Roho Mtakatifu peke yake ndiye anayeweza kufanya hivyo kwa kunena kupitia mjumbe wake aliyeandaliwa kwa ajili ya siku hii. Ujumbe huu ni BWANA ASEMA HIVI. Hakuna kushangaa, hakuna kubahatisha, Mungu amethibitisha hii ndiyo njia yake iliyoandaliwa kwa ajili ya leo hii.

Tunalo pumziko na amani jinsi gani. Hatujawahi kamwe kuwa na wasiwasi au kuhoji kile tunachoambiwa. Hatujawahi kamwe kurudi kwenye Neno kulikagua, maana tunasikiliza Neno la Mungu lililothibitishwa kwa ajili ya siku yetu. Tunaketi tu, tukifungulia mioyo yetu, akili na roho zetu, na kusema AMINA, AMINA, AMINA.

Hapana, hatustahili. Hapana, hatuelewi kila kitu. Lakini Tuna AMINI kila Neno. Alisema hiyo ilikuwa ndiyo ishara ya kweli kwamba una Roho Mtakatifu, na ni Bibi-arusi Wake peke yake ndiye atakayeamini na kukaa na kila Neno. SISI NDIYO BIBI_ARUSI HUYO….Haleluya !.

Linapita juu ya wanaodhaniwa kwamba wana akili nyingi sana, na unalifunulia watoto wachanga wanaoweza kujifunza .

Ninashukuru sana ya kuwa mimi ni mtoto mchanga Ninayeweza kujifunza.

Amethibitisha kupitia karne zote Kuwa yeye alikuwa Nani katika kila kizazi. Yeye alithibitisha jambo Hilo kupitia kwa manabii Wake. Alilithibitisha hilo wakati alipokuja katika mwili, akachukua dhambi zetu na kutundikwa msalabani, kisha akafufuka na Akamtuma Roho Mtakatifu.

Sasa amethibitisha katika siku yetu kwa kurudi na kujifunua mwenyewe katika mwili wa mwanadamu Kwa mara nyingine tena kama alivyoahidi angefanya katika Neno Lake. Alijithibitisha kuwa ni Mwana wa Adamu, huduma ya Yesu Kristo Mwenyewe, ikiwa imefichwa katika mwili wa mwanadamu.

Na sasa, sura Yake ya mwisho, sababu yenyewe ya mpango huu mkuu, kuja kwetu, Bibi-arusi Wake aliyerejeshwa Kikamilifu, aliyethibitishwa, ambaye aliyekaa Na Neno.

Je! Ungalipenda Kuwa kwenye mlima siku hiyo wakati Yesu alipoongea na wale 5000? Je! Ungalipenda kumwona akiuthibitishia ulimwengu kuwa Yeye alikuwa nani kwa kutoa mikate na samaki? Je! Ungalipenda kukaa chini ya upako huo, kusikia tu Sauti Yake ikifariji moyo wako kwa Maneno Yake ya Uzima wa Milele?

Unaweza, ikiwa unaamini Ujumbe huu kwa moyo wako wote.

Njoo uketi pamoja nasi chini ya upako huo juu ya mlima Jumapili hii saa 8:00 Nane mchana, saa za Jeffersonville ( Ni saa 3:00 tatu usiku ya Tanzania), na umsikie Mungu akiuthibitishia ulimwengu kuwa Yeye ni nani katika siku yetu. Luka 17:30 Akinena nawe na kukuambia B-R-A-N-H-A-M ni Sauti Yangu iliyothibitishwa na iliyochaguliwa kwako. Njoo umsikie Yeye: Kuthibitisha Neno Lake 65-0426 .

Ndugu. Joseph Branham

Maandiko ya kusoma:

Mathayo Mtakatifu 11: 4-19 / 28:20
Marko Mtakatifu 11: 22-26
Luka Mtakatifu 8: 40-56 / 17:30
Yohana Mtakatifu 14:12
Waebrania 4: 12-15 / 13: 8
Malaki 4