21-0724 Mahali Pa Kuabudia Palipoandaliwa Na Mungu

Ujume: 65-0425 Mahali Pa Kuabudia Palipoandaliwa Na Mungu

PDF

pakua

BranhamTabernacle.org

Tai wanakusanyika Pamoja.

Wapendwa Waliyouishwa ,

Jinsi gani tunavyopenda kukusanyika pamoja kila wiki kula Manna ya Kiroho aliyowaandalia Bibi-arusi Wake. Inatupa nguvu tunayohitaji kwa ajili ya safari yetu. Ni Maisha yenyewe ya Masihi, yaliyodhihirishwa, yakifanya Kanisa Lake liwe tayari kwa Unyakuo.

Nguzo ya Moto imetuita kutoka, na inatuongoza kwenda kwenye Nchi ya Ahadi, chini ya upako wa nabii Wake Mwenye nguvu, William Marrion Branham.

Ndugu Branham sio ile Nguzo ya Moto. Yeye Ndiye kiongozi aliyepakwa mafuta, chini ya ile Nguzo ya Moto. Nguzo ya Moto inathibitisha tu Ujumbe wake kwa ishara na maajabu. Ni Roho wake Mtakatifu Mkuu aliyejidhihirisha kati yetu na ni mara elfu zaidi ya manabii wengine wote wa hapo awali.

Hivi huwezi kumwona Mwana wa Adamu, Mwana wa Adamu katika mfano wa Ujumbe wa kinabii, akirudi tena katika Kanisa Lake, katika unabii, akimfunua Yesu Kristo kwamba ni yeye yule jana, leo, na hata milele? Halijawahi kufanyika kote katika wakati huu, mpaka kufikia saa hii.

Akili zetu za Kiroho zimelishika. Tunaliona na tunaamini kila Neno. Ujumbe Huu, Kanda hizi, ni Njia iliyoandaliwa na Mungu ili kuikamata akili hiyo huko nje ambapo mbegu hiyo imepandwa. Tumesikia Sauti hiyo na Nuru imetugusa na tumetwaa Uzima.

Inatuketisha katika makao ya kimbinguni, SASA HIVI. Sio tutakuwa, tuko sasa. Tayari tumefufuliwa, Nguvu tendaji na mitambo ipo kazini. Imetuhuisha katika Uwepo wa Mungu, alipo Roho Wake. Sio kile utakachokuwa, tayari uko! Ni shetani tu akijaribu kutufumba kutoka Kwenye hilo.

Swali: Je! Umekuwa Hai?
J: Ndio

Swali: Je! Kristo amekuwa halisi kwako?
J: Ndio

Swali: Je! Nguvu za Mungu zimedhihirishwa?
J: Ndio

Swali: Je! Uko katika Kanisa hilo, Kanisa lililoandaliwa na Mungu?
J: Ndio

Swali : Unakuaje ndani Yake, unajuaje kuwa umehuishwa ndani Yake?
J : Mawazo yetu yote; Utu wetu wote, uko ndani ya Kristo. Kristo yuko katikati yetu, akijithibitisha kuwa hai, akithibitisha kuwa yuko hapa.

Sisi ni nyama ya nyama Yake, na mfupa wa mfupa Wake, mwili wa mwili Wake, Jina la Jina Lake, Bibi-arusi Wake. Tuko ndani yake. Sisi ni mwili Wake na mifupa yake.

Hatuwezi kufa, tumehuishwa. Nguvu ile ya kuhuisha iliyotufufua kutoka kwenye maisha ya dhambi, na kubadilisha Utu wetu, imetufufua kwa uwezekano katika Kristo Yesu, ambapo, ufufuo utatuleta katika ukomavu kamili.

Tumezaliwa mara ya pili na kuzaliwa upya, tumebatizwa na Roho Mtakatifu, ndani ya Yesu Kristo. Tumehuishwa kwa kila Neno. Tunaitikia kila Neno kwa “amina”.

Tunapokusanyika pamoja katika Yesu Kristo; kwa nia moja, na kwa umoja , chochote tunachohitaji, ikiwa tutakuwa na IMANI na kuamini, Yeye atatupatia.
Hebu na tutambue ya kwamba Yeye atakuwa katika kila moja ya nyumba zetu, makanisa yetu, au mahali popote tutakapokusanyika, kwani sisi ni wana na binti zake, Kanisa la Bibi-arusi Wake.

Ninajua Yeye yuko hapa. Nina hakika Yeye yuko hapa. Ninajua ya kwamba sasa kuna nguvu za kuhuisha ndani ya Kanisa kumponya kila mtu anayeketi hapa .

Je! Unaamini Ujumbe huu? Je! Unaamini ni Njia ya Mungu ya leo? Je! Unaamini ni Mwana wa Adamu akijifunua mwenyewe katika mwili wa mwanadamu? Je! Unaamini kila Neno?

Ikiwa unahitaji uponyaji wa mwili, uponyaji wa roho, au CHOCHOTE ambacho unaweza kuhitaji, basi ninakupa changamoto kuamini sauti ya Mungu iliyotiwa mafuta nakuthibitishwa kwa ajili ya siku yetu:

Jalia sasa ya kwamba nguvu hizo za kuhuisha zitaihuisha imani yao, Bwana, kwa yale wanayofanya. Kuna mwamini aliyeweka mikono yake juu ya mwamini, mwili kwa mwili, nguvu kwa nguvu. Na ni nguvu za Mungu, kwa mwana wa Mungu ama binti ya Mungu, kwa Mwana wa Mungu. Ee Mungu, jalia Shetani awaachilie watu hawa! Jalia waponywe alasiri ya leo, kwa nguvu hizo za kufufuka, kuhuisha kwa Uwepo uliotambulishwa, Yesu Kristo. Katika Jina la Yesu Kristo, na iwe hivyo!

Njoo uungane nasi chini ya: Mahali Pa Kuabudia Palipoandaliwa na Mungu 65-0425, na upokee uponyaji wako, utiwe mafuta na Roho Mtakatifu, roho yako ifurahi unapoketi katika makao ya kimbinguni na kumsikia Mwana wa Adamu akizungumza Jumapili hii saa 8:00 Nane mchana , saa za Jeffersonville ( ni saa 3:00 Tatu usiku ya Tanzania).

Ndugu. Joseph Branham

Maandiko ya kusoma kabla ya kusikia Ujumbe:

Kumbukumbu la Torati 16: 1-6
Malaki 4: 5
Mathayo Mtakatifu 1:23
Marko Mtakatifu 16:17
Luka Mtakatifu 17:30
Yohana Mtakatifu 4:23 / 10: 1-7
Warumi 8: 1-11
1 Wakorintho 12:13
Waefeso 1:21
1Wathesalonike 4:16
Waebrania 13: 8
Ufunuo 22:19