All posts by admin5

21-1121 Kiu

UJUMBE: 65-0919 Kiu

PDF

pakua

BranhamTabernacle.org

Tai wanakusanyika Pamoja.

Mpendwa Bibi Mteule,

Muungano mkuu wa mwisho unafanyika kwa ajili ya Unyakuo. Roho Mtakatifu anamleta Bibi-arusi Wake pamoja kutoka katika mataifa yote; kutoka Pwani ya Magharibi hadi Pwani ya Mashariki, kutoka Kaskazini hadi Kusini, kutoka pembe nne za dunia.

Anatukusanya pamoja katika makanisa yetu na katika nyumba zetu kupitia Mawimbi Bora sana. Ni bora hata zaidi kuliko njia ya kurusha matangazo. Ni mawasiliano ya simu. Tunaweka vipokezi au maikrofoni, ama chochote kile, katika chumba, na ni sawa sawa tu na kusimama katika chumba pamoja na nabii Wake. Ni njia iliyoandaliwa na Mungu kwa ajili ya siku hii kumuunganisha na kumleta Bibi-arusi Wake pamoja na, “Bwana Asema Hivi”.

Miaka hamsini na sita iliyopita, Mungu alianza mpango wake wa kuwakusanya Bibi-arusi Wake pamoja ili waweze kumsikia akinena kupitia malaika Wake mwenye nguvu kwa wakati mmoja. Hata aliifanya huduma tano yake kusitisha kuhudumu na kuwakusanya watu wao pamoja, nao Wakajiunganisha Kwa Radio katika makanisa yao, kwani alitaka Bibi-arusi Wake aisikie Sauti Yake wote kwa wakati mmoja. Mpango wake mkuu ulikuwa umeanza. Haijawahi kamwe kuwezekana katika historia ya ulimwengu. Nabii wake alijua jambo Hilo na alifurahishwa sana. Sasa Mungu angeweza kusema moja kwa moja na Bibi-arusi Wake wote kwa wakati mmoja. Wote wangeweza kusikia wenyewe, Mungu akizungumza nao moja kwa moja, na haingehitaji fasiri yoyote.

Leo, ulimwengu uko katika mshangao. Kwa nini watu kutoka duniani kote, wakiwa na majira tofauti ya maeneo Yao ; 6:00 sita mchana., 8:00 Nane mchana., 2:00 mbili usiku., usiku wa manane, wanakusanyika pamoja wote kwa wakati mmoja ili kusikia Ujumbe ambao wanaweza kusikiliza wakati wowote. Nini kinachovutia?

Imefunuliwa kwao kwamba huu ni mpango wa Mungu, njia iliyotolewa na Mungu ya kuwaunganisha kiroho. Ni Mungu akitayarisha kuzungumza na Bibi-arusi Wake wote kwa wakati mmoja.

HAKUNA kingine ila Sauti ya Mungu, Neno Lake, Ujumbe Huu, ulionenwa na nabii Wake ungeweza kufanya hivyo. Hakuna mtu, wala kitu kingine chochote, ambacho Bibi-arusi wote wanaweza kukubaliana kwacho.

Mtu fulani anaweza kusema, “Mimi humsikiliza mchungaji wangu anaponukuu na kuhubiri Neno kama tu vile Ndugu Branham alivyosema afanye.” Bwana asifiwe. Hilo ni zuri na umebarikiwa sana kuwa na mchungaji anayedumu na Neno. Ameitwa kuweka kundi pamoja na kukupa na kukuelekeza kwenye Neno, Lakini hilo silo ninalozungumzia. Huna budi kuwa na Yakini, Neno la mwisho. Maneno Ambayo SOTE TUNAWEZA KUKUBALIANA KWAYO. Kadiri alivyoitwa na kupakwa mafuta jinsi mtu ye yote awezavyo kuwa, hakuna neno la mtu yeyote ambalo ni kamilifu, na hakuna huduma ya mtu yeyote inayoweza kumuunganisha Bibi-arusi.

“Hilo ni wazo lako tu na maoni yako. Thibitisha hilo kwa Neno, Ndugu Joseph”.

Kwa sababu ukiwa na watu wawili, una maoni mawili . Yapasa kuwe na yakini Moja ya mwisho , na yakini yangu ni Neno, Biblia . kama mchungaji hapa wa kanisa, Yakini yangu ni Neno, nami ninataka … ninajua ninyi, ndugu zetu, kwa namna fulani
mnanichukua mimi kama Yakini yenu kwa yale…mradi ninamfuata Mungu kama Paulo alivyosema katika Maandiko, “Mnifuate mimi kama ninavyomfuata Kristo .”

Hivyo basi, wakati nabii anaponena, ni Yakini kwa Bibi-arusi. Ujumbe Wake si neno lake yeye, wala si fasiri yake yeye ya Neno. Ni Mungu akifasiri Neno Lake Mwenyewe kwa njia Yake pekee aliyoiandaa ya kufanya hivyo: kwa nabii Wake.

Ikiwa unasema unaamini Ujumbe Huu.
Ikiwa unasema unaamini nukuu hii.
Ikiwa unasema na kuamini kuwa wewe ni Bibi-arusi wa Kristo, Basi kile kilichonenwa kwenye kanda lazima kiwe Yakini Yako.

Hivi, ni nini kingine kinachoweza kumleta Bibi-arusi wa Kristo wote pamoja isipokuwa Yakini yetu? HAKUNA KINGINE. Hizo Kanda ni Sauti Yake, Neno Lake, Yakini Yetu. Nabii alituambia kwamba nabii Kwa ajili ya wakati huu ni Roho Mtakatifu. Roho Mtakatifu huchagua mtu MMOJA, Sauti MOJA kufunulia Neno Lake na Sauti hiyo inamuunganisha Bibi-arusi Wake kwa njia Yake aliyoiandaa kwa ajili ya siku hii, KWA KUBONYEZA PLAY .

Ninajaribu sana niwezavyo kudumu kwa unyofu na Neno , kwa ajili ya hawa ambao wamewekwa mikononi mwangu kwa ajili ya Mungu , maana kondoo huhitaji chakula cha kondoo, bila shaka. “Kondoo wangu huisikia Sauti Yangu.” Na hilo ndilo tunaloishi kwalo, kila Neno litokalo…Si yote…Si Neno moja mara hii na mara nyingine; bali kila Neno litokalo kinywani mwa Mungu, hilo ndilo ambalo watakatifu wanapaswa kuishi kwalo.

Tunapaswa kuishi kwa kila Neno litokalo katika kinywa cha Mungu. Je, kinywa cha Mungu kilichothibitishwa kwa ajili ya wakati huu ni kipi? Mimi? Mimi si Malaika- Mjumbe wa 7 wa Mungu aliyethibitishwa , wala kinywa Cha Mungu si mchungaji wako wala mtu ye yote yule; Ni Mungu akitumia sauti ya WILLIAM MARRION BRANHAM.

Tutahukumiwa kwa Ujumbe ALIONENA kwenye kanda. Si kwa Fasiri ya mtu mwingine ye yote ama kuhubiri kile alichonena, Bali kwa Neno KWENYE KANDA. Kama wapakwa mafuta na Roho Mtakatifu jinsi tuwezavyo kuwa, tunaweza kukosea. Sisemi muhudumu yeyote ni wa uwongo au amekosea; tumeitwa kuhubiri, na kufundisha, na kukaa na Neno, Lakini wito wetu ni kuwaelekeza ninyi KWENYE NENO, na NENO PEKEE LILILOTHIBITISHWA KIKAMILIFU liko kwenye Kanda.

Tunayo mengi sana, kama Bibi-arusi wa Kristo, ya kushukuru.

je kama tungaliijaza bahari kwa wino, Na kama mbingu zote zimetengenezwa kwa karatasi; Kama kila shina duniani lingekuwa ni kalamu, Na kila mtu awe kazi yake ni mwandishi; Kuuandika upendo wa Mungu aliye juu Kungeikausha bahari yote; Ama kama gombo hilo lingechukua nafasi yote, Hata kama limetandazwa kutoka mbingu hadi mbingu.

Tunakaribia kuwa na juma kuu la Shukrani la maishani mwetu.
Sikukuu ya Chakula cha Kiroho cha kujaza Nafsi. Sikukuu ambapo Bibi-arusi ataungana na kuketi pamoja katika Uwepo wa Jua kuivishwa.

Mungu atanena kupitia mjumbe wake na kutuambia:

. Sisi ni Bibi Mteule wake.

. Majina yetu yako kwenye Kitabu cha Uzima cha Mwana-Kondoo.

. Hatuna dhambi.

. Tulihesabiwa haki kabla ya kuwekwa misingi ya ulimwengu.

. Sisi ndio walioitwa watoke na wateule.

. Sisi ndio ambao mpango mzima wa Mungu umekuwa ukingojea.

. Sisi ni Bibi-arusi safi, mwema, asiye na dhambi wa Mwana wa Mungu aliye hai.

. Sisi ni wakamilifu mbele zake.

Hakuna mwisho wa kuyaandika yale yote ambayo Roho Mtakatifu anakwenda kutufunulia na kututendea.

Nena kuhusu Shukrani !!!

Nimehisi kushinikizwa katika Roho yangu kutoka kwa Bwana ili tuweke wakfu juma zima, kuanzia Jumapili hii, kwa ajili ya Shukrani kwa Bwana.

Iliyoambatishwa hapa ni kalenda yenye siku, masaa na Jumbe tutakazosikia.

Kama unavyoweza kuona, Jumapili sote tutaungana pamoja katika muda wetu wa kawaida wa saa 8:00 Nane mchana, saa za Jeffersonville, ( ni saa 4:00 nne usiku ya Tanzania) , ili kusikia Ujumbe: Kiu 65-0919.

Jumatatu Hadi Jumatano , ningependa tusikie Jumbe 3 zinazofuata ambazo Ndugu Branham alizileta katika mfuatano, mwaka wa 1965. Tutakuwa tukizituma kwenye Voice Radio (Radio ya Sauti, iliyopo kwenye app ya Lifeline ya vgr ) saa 3:00 tatu Asubuhi saa za Jeffersonville,( ni saa 11:00 kumi na Moja jioni ya Tanzania) na tena saa 1:00 Moja jioni, saa za Jeffersonville,( ni saa 9:00 Tisa usiku ya Tanzania).

Najua itakuwa vigumu kwa wengi kusikiliza kwa wakati uliowekwa kutokana na ratiba zao za kazi au majukumu mengine, lakini tunatumai mnaweza kusikiliza wakati mmojawapo Kwa pamoja na familia zenu.

Kisha Alhamisi , mwezi wa 11, tarehe 25, ningependa tuungane pamoja saa 8:00 Nane mchana, saa za Jeffersonville, ( ni saa 4:00 nne usiku ya Tanzania ) kuanza wikendi yetu nzuri ya Kutoa Shukrani tunapounganishwa tena ili kusikia Sauti ya Mungu ikituletea Ujumbe wa kwanza wa wikendi yetu: Muungano Usioonekana wa Bibi-arusi wa Kristo 65-1125.

Ilikuwa ni baraka ya pekee kwangu kutambua itakuwa miaka 56 iliyopita, hadi siku ya leo, ambapo Mungu alinena kupitia nabii Wake kutuletea mfululizo huu wa Jumbe. Ilikuwa pia miaka 56 tangu kuzaliwa kwa Ndugu Branham mwaka wa 1909, hadi mwaka wa 1965, ambapo alizinena Jumbe hizi.

Tungefanya nini kama tungejua Ndugu Branham atakuwepo Shreveport, LA wikendi hii ili kutuletea Jumbe hizi? Hakuna ….Namaanisha HAKUNA kitu kingaliweza kutuzuia kwenda. Mungu ana mpango kwa ajili ya Bibi-arusi Wake leo, na HAKUNA kitakachotuzuia.

Naamini kila mmoja wenu Yuko chini ya matarajio makubwa kwa juma hili zuri tutakalokuwa pamoja na Bwana; kumshukuru, kumsifu na kumwabudu kwa ajili ya yote aliyoyafanya, na yote anayokwenda kufanya kwa ajili ya kila mmoja wetu, BIBI MTEULE WAKE.

Ndugu. Joseph Branham

21-1114 Nguvu Za Mungu Za Kugeuza

UJUMBE: 65-0911 Nguvu Za Mungu Za Kugeuza

PDF

pakua

BranhamTabernacle.org

Tai Wapendwa , hebu sote tukusanyike pamoja na kusikia Ujumbe  65-0911 Nguvu za Mungu za Kugeuza Jumapili hii saa 8:00 nane Mchana, saa za Jeffersonville.( Ni saa 4:00 nne usiku ya Tanzania).

Ndugu Joseph Branham

Maandiko ya kusoma:

Mwanzo Sura ya 4 yote

Isaya 9:6 / 14:12-14

Mathayo 5:6 / 24:24

Yohana Mtakatifu 1:1

Warumi 12:1-2

2 Wathesalonike 2:3-4

Waebrania 10:26-27

Ufunuo Sura ya 3 yote

21-1107 Edeni ya Shetani

UJUMBE: 65-0829 Edeni ya Shetani

PDF

pakua

BranhamTabernacle.org

Mpendwa Bibi-arusi Aliyeangazwa,

Kama Siku ile iliyokwisha kupita, tulikuwa tumeunganishwa na Yeye akaja katika nyumba zetu na akawa pamoja nasi. Kote katika mataifa, sehemu ya Mwili wa Kristo, Ambayo nabii Wake amepewa haki ya kuilisha, waliketi pamoja katika ulimwengu wa roho Alipokuwa YEYE akisema nasi kupitia malaika Wake mkuu ambaye amemtuma; kuuangaza ulimwengu kwa Roho Wake Mtakatifu kupitia yeye, kumwita Bibi-arusi Wake atoke.

Mungu alituma, katika mlango huu wa 18, malaika mwenye nguvu, baada ya siri hiyo kujulikana, malaika mwenye nguvu, ama, mjumbe….

Mungu alimtuma malaika, mjumbe (kufanya nini?) kuwaita watoke. “Tokeni!” Ujumbe wa Wakati huu!…

Tokeni kwake! Mungu alituma wengi…malaika mkuu, ama, mjumbe. Na Nuru yake haikuwa kwenye maficho, iliangaza duniani kote… Kuiangaza nchi, na kuwaita watu Wake watoke kwake.

Sasa, mnajua jambo hilo ni Kweli. Mjumbe fulani alitumwa kutoka Mbinguni, kuwaita watu wa Mungu watoke Babeli. Na Nuru Yake ikaangaza nchi, Roho Mtakatifu aliye mkuu .

Wiki iliyopita mhudumu fulani aliliambia kusanyiko lake kwamba Mimi nilitaka watu waamini kwamba Ndugu Branham alikuwa ndiye malaika wa Ufunuo 18, lakini akadai kuwa huyo alikuwa ni malaika kutoka Mbinguni, na asingeweza kuwa Ndugu Branham. Kama huyo ndugu angalifanya tu kile nabii ALILOMWAMBIA afanye, kulichunguza jambo hilo kwa Neno, na SI kwa ufahamu wake, ANGESIKIA, KWAMBA KWA KWELI, ALIKUWA NI NDUGU BRANHAM ALIYESEMA YEYE ALIKUWA NDIYE MALAIKA HUYO .

…Angalia, huyu ni malaika wa Nuru, kumbukeni, malaika wa mwisho, ni malaika katika wakati wa kanisa wa Laodikia. Ni mjumbe wa Laodikia, huyo, ni wa mwisho, kwa kuwa mlango unaofuata tu ni mlango wa 19, ambao ni kuja kwa Bibi-Arusi .

Ndugu na dada zangu, NINACHUKIA kusema mambo haya na kuyabainisha. Kama vile Ndugu Branham asemavyo, “Naeleweka vibaya sana ”. Mimi Simaanishi kuwa ni wahudumu wote wanaosema mambo haya, wala siamini wahudumu wote ni wauongo, au hawapaswi kuhudumu. HAPANA, lakini walio wengi sana wanawadanganya watu kwa kuweka umuhimu zaidi katika huduma yao kwa kuhubiri Neno, badala ya kubonyeza play na watu wao na kusikia HASA kile nabii alichosema.

kama umechaguliwa tangu awali, unaliona. Hakuna njia ya kulificha toka kwako. Utaangalia na kusema, “ ni dhahiri sana mbele ya uso wangu! Ninaliangalia moja kwa moja. Ninaliona. Hili hapa, lile Neno; kila Neno, Neno kwa Neno. limedhihirishwa mbele yangu na nafsi yangu yote imefungamanishwa ndani yake.”

Hebu niwape nukuu hii ndugu zangu wahudumu, ambayo inaeleza yale tu mimi, na kanisa ambalo Bwana amenipa kuwa mchungaji, tunaamini kuhusu kucheza kanda kanisani.

Na sasa kumbukeni, kama hili linanaswa…Sijui. Siwezi kumwona ye yote. Naam, naweza, naweza kumwona Ndugu Terry kule kwenye—kwenye chumba cha kurekodia. Na kama hili linanaswa; kwa ajili ya wahudumu wo wote mahali po pote, wakati wo wote, hili halielekezwi kwa madhumuni ya kudharau mafundisho yenu, hili hata halielekezwi kwa kondoo wenu. Ujumbe huu, na Jumbe zote zingine ambazo ninazungumzia, zinaelekezwa kwenye kusanyiko langu. Si kwa ajili ya kusanyiko lako isipokuwa wawe wanataka kulipokea. Bali limeelekezwa kwa watu hawa hapa.

Watu hununua kanda hizi. Watu kila mahali ulimwenguni huzinunua na kuzicheza. Mara nyingi wananiandikia. Na sikuzote mimi huwarejesha, kama wao ni washiriki wa kanisa fulani, “ Mwoneni mchungaji wenu.”

Wananitazama Mimi kama mchungaji wao Wa mahali hapa , ndiomana ninawaambia, “NINAAMINI KUZIPOKEA KANDA NA KUBONYEZA PLAY . Ndugu Branham ndiye mchungaji wetu. Sisi ni sehemu ya Kusanyiko lake ”.

Sasa, ewe mchungaji , nataka ujue jambo hilo, ya kwamba, ninazungumza haya kwa ajili ya kusanyiko langu peke yake. Nami nina haki ya kutenda jambo hilo, kwa maana nimewekwa na Roho Mtakatifu kuwachunga kondoo hawa. Na ole wangu kama siwaambii ninayofikiria ni Kweli, na jinsi ninavyofikiri linakuja. Bali si kwa ajili ya ulimwengu wala kwa makanisa mengine. Ninyi fanyeni lo lote ambalo Mungu anawaambia mtende. Siwezi kuwajibieni, wala ninyi hamwezi kunijibia .
Lakini kila mmoja wetu hana budi kujibu mbele za Mungu, kwa ajili ya huduma yetu

Sina budi kujibu kwa Mungu kwa ajili ya huduma aliyonipa. Kwa kila hali ya utu wangu naamini ni lazima ucheze Sauti ya Mungu katika kanisa lako kwa njia ya Jumbe zilizorekodiwa . Ni njia iliyoandaliwa na Mungu kwa ajili ya siku hii kuivisha Bibi-arusi Wake. Ndiyo njia PEKEE kwa Bibi-arusi kuunganishwa na kukamilishwa.

Ujumbe tutakaosikia Jumapili ulinenwa na kurekodiwa kwa ajili ya LEO HII. Ni Chakula Cha Kiroho Kwa Wakati wake. Hebu na tufungue mioyo yetu ili Roho Mtakatifu aweze kututia mafuta ili tusikie kile alichokuwa anatuonya tutazamie katika siku hizi za mwisho.

Alitueleza roho zote mbili zitadhihirishwa kikamilifu katika siku hii ya mwisho. Alitueleza ingefanana sana hata ingewadanganya wateule kama yamkini. Siku hiyo ndiyo hii.

Angalia, wakati Yesu alipokuja—unaona, Shetani alikuwemo katika kundi lile la waalimu wa Kiyaudi na marabi na makuhani, akijaribu kuwaambia washike Torati ya Musa, ambapo Neno lenyewe lilisema—kwamba katika siku hiyo, Mwana wa Adamu angefunuliwa. Unaona? Kwamba angejifunua Mwenyewe . Kwa hiyo walikuwa wakijaribu…kadiri ambavyo waliwaweka wa kidini, na katika Torati ya Musa…unaona alilotenda ? Alikuwa akijaribu kuwaambia, “Sehemu hiyo ya Neno ni sawa kabisa, lakini mtu huyu siye mtu yule.” Unaona jinsi alivyo mdanganyifu ? Hiyo ndiyo hiyo siku yenyewe hasa ya udanganyifu.

HATUWEZI kudanganywa, sisi ni Bibi-arusi. Sisi NI watoto wa Mungu. Sisi NI sehemu ya sifa ya Mungu iliyokuwa ndani Yake, tulifanyika mwili kama vile Yeye alivyofanyika mwili, ili tuweze kuwa na ushirika sisi kwa sisi kama familia ya Mungu duniani. Hatulikumbuki jambo hilo kwa sasa, lakini tulikuwa huko. Alijua jambo hilo. Na alitaka tuwe hivyo ili aweze kuwasiliana nasi, aseme nasi na kutupenda, na kupeana nasi mikono,
UTUKUFU!!!

Hakuna tena, “NADHANI MIMI ni Bibi-arusi Wake. NATUMAI MIMI ni Bibi-arusi Wake.” TUNAJUA SISI NI BIBI-ARUSI WAKE .

Roho Mtakatifu anatenda kazi ndani yetu . Ni Uzima. Si msisimko wa mwili; sio namna fulani ya uhakika wa matendo ya kimwili, bali ni Mtu, Yesu Kristo, Neno la Mungu lililowekwa katika mioyo yetu kuhuisha kila neno la wakati huu.

Unakaribishwa kuungana nasi kwa kuunganishwa Jumapili saa nane 8:00 mchana , saa Jeffersonville, ( ni saa nne 4:00 usiku ya Tanzania), Roho Mtakatifu anapotuangazia kwa Neno Lake lililonenwa kupitia malaika Wake, na kutuletea Ujumbe: Edeni ya Shetani 65-0829

Ndugu. Joseph Branham.

Maandiko ya kusoma

2 Timotheo 3:1-9

Ufunuo 3:14

2 Wathesalonike 2:1-4

Isaya 14:12-14

Mathayo 24:24

21-1031 Chujio La Mtu Mwenye Busara

Ujume: 65-0822e Chujio La Mtu Mwenye Busara

PDF

pakua – m4a

pakua – amr

BranhamTabernacle.org

Wapendwa Waamini wa Biblia,

Ni siku tukufu jinsi gani tunayoishi. Mioyo yetu inawaka ndani yetu anapozungumza nasi kila siku njiani. Kristo amefunuliwa kwetu kwa Neno Lake. Ni Ufunuo wa Yesu Kristo, Neno Mwenyewe aliyedhihirishwa katika mwili. Ni Sauti ya Mungu ikimwita Bibi-arusi Wake atoke.

Tunao Mkataa, neno la mwisho, Yakini yetu; ni Neno Lake, Biblia. Sasa kama “Biblia” ndiyo Yakini yetu, hebu na tuone kile nabii alichosema Biblia ilichokuwa .

Yeye Alisema Mungu aliandika Biblia kwa kutumia manabii pekee yao. Hiyo ndiyo ilikuwa njia Yake ya kufanya jambo hilo. Hiyo ndiyo njia Aliyokuwa nayo ya kuleta Neno Lake kwa watu: kupitia midomo ya manabii Wake. Neno Lake lilimjia nabii peke yake .

Nabii alikuwa ameelekeza nia yake daima kwenye yale Mungu aliyosema; si vile mwanadamu alivyofikiri, vile huo wakati ulivyofikiri, vile kanisa lilivyofikiri, vile ufalme ulivyofikiri. Bali Vile Mungu alivyofikiri, yeye alitamka tu mawazo ya Mungu kwa Neno, wakati Mungu alipoyafunua mawazo Yake kwake, yeye aliyatamka kwa Neno lililoandikwa.

Kwa hiyo, Biblia nzima si maneno ya mwanadamu, wala haikuandikwa na mwanadamu, kuletwa na mwanadamu, ama wala haiwezi kufunuliwa na mwanadamu. Ni Neno la Mungu hufunuliwa na Mungu Mwenyewe, Hujifasiria Mwenyewe. Neno Lake.

Sasa manabii hawa walisema, “Si mimi. Sina uhusiano wowote nalo, bali ni BWANA ASEMA HIVI.” Kwa hivyo, Biblia ni BWANA ASEMA HIVI kupitia manabii. Manabii hawa hawakunena tu na kuandika Neno, lakini pia alikuwa Mfasiri wa Kiungu wa Neno hilo lililoandikwa.

Kwa hiyo, Biblia ni mawazo hasa ya Mungu yaliyoandikwa na manabii. Nabii ndiye mfasiri pekee wa kiungu wa Biblia. Ujumbe, Neno, Biblia na mjumbe ni kitu kimoja . Hivyo, tutahukumiwa kwa fasiri ya Biblia iliyonenwa na nabii.

” Wewe ulitumwa kuwa kiongozi na Mungu atakuja, na atakapokuja, Yeye atakuhukumu kulingana na yale uliyowafundisha, kwanza; kama wataingia ama hawataingia. Tutaingia kulingana na mafundisho yako .”

Je hivi yeye amesema NINI? Atahukumiwa kwanza kwa yale YEYE aliyotufundisha. Tunaweza TU kuingia kulingana na mafundisho YAKE. Kwa hiyo ni jinsi gani ilivyo muhimu kusema tu yale yaliyo kwenye kanda kwani tutahukumiwa kwa NENO LAKE KWENYE KANDA; ambayo ni fasiri ya Biblia.
Je, utaamini kikomo chako cha Milele juu ya kile mtu fulani anachosema? Sio Bibi arusi!! Sisi Tutafanya na kusema nini?

Ndipo hao wote wakapaza sauti kwa pamoja, “Tunajua hilo! Tunastarehe kwa uhakika.”

Kwa hiyo, Bibi-arusi anastarehe juu ya kila Neno ambalo nabii alilonena, ambayo ilikuwa ni fasiri ya mawazo ya Mungu yaliyoandikwa na manabii, na katika siku hizi za mwisho yamenenwa na Mungu Mwenyewe kupitia midomo ya nabii Wake.

“Wewe utatukabidhi Kwake, na ndipo tutarudi duniani tena, tukaishi milele.”

Ee wandugu na wadada, amkeni kabla hamjachelewa. Huu ni wito Wake wa mwisho. Fungua moyo wako na uone jinsi unavyopaswa kusikiliza Sauti ya Mungu kwenye kanda. Ikiwa tutahukumiwa kwa Ujumbe ambao Mungu alinena kupitia mjumbe Wake kwenye kanda, unawezaje kutokuona jinsi ilivyo muhimu, na njia pekee ya kuwa sahihi na kuwa mstari mmoja na Neno Lake, ni kwa kusikia Sauti ya Mungu kwenye kanda.

Ndiyo, Mungu ameita huduma tano , lakini hawana budi kuweka umuhimu wa kuzisikiliza kanda zaidi ya huduma yao. Sisemi kwamba mchungaji wako hawezi kuhubiri au kufundisha. Sisemi kuacha kwenda kanisani; unapaswa kwenda kanisani, lakini wakati mchungaji wako haweki kanda, Sauti ya Mungu ambayo utahukumiwa kwayo, kuchukua nafasi ya kwanza na kuwapa hiyo kusikiliza, una chujio mbaya.

Hebu Jiulize, wakati mhudumu anapokuambia, unapaswa kucheza kanda tu nyumbani kwako na sio kanisani, je! Hilo linaingia akilini? Hakika, hujadanganganywa kiasi hicho . Sauti ile ile na Neno utakayohukumiwa kwayo inapaswa TU kusikilizwa majumbani mwenu na si kanisani? Ndugu Branham kamwe hakusema kucheza kanda kanisani, lakini unapaswa kunisikiliza mimi tu kama mchungaji wako unapokuja kanisani. hivi una hata chembe ya ufunuo kweli ?

Ni jambo gani linaloweza kuwa muhimu zaidi mnapokutanika pamoja katika kanisa lenu kumwabudu Bwana, kukua katika ufahamu wa Neno, kumkaribia Mungu zaidi, kuliko kuivishwa kwa kusikia sauti PEKEE…PEKEE iliyothibitishwa ya Mungu.

Je, ungeweza kuwazia Yoshua akiwaambia Israeli wote, najua tunayo maneno halisi ambayo Musa aliyonena, lakini Musa hakuwahi kusema tunapokutanika pamoja kwamba tunapaswa kusoma maandishi yake. Ninawaongoza sasa na mimi nitawaambia maneno ya Musa.

Kisha akasoma maneno yote ya torati, baraka na laana, sawasawa na yote yaliyoandikwa katika kitabu cha torati .

Wala Hapakuwa na neno lo lote katika yote aliyoamuru Musa, ambalo Yoshua hakulisoma mbele ya mkutano wote wa Israeli, pamoja na wanawake, na watoto, na wageni waliokaa kati yao .

Kwa maneno mengine, kama Yoshua angekuwa na kinasa sauti katika siku zake, alipowakusanya watu pamoja ange BONYEZA PLAY.

Malaki 4 amekuja na BWANA ASEMA HIVI, nawe utahukumiwa kwa kila neno lililonenwa kwenye hizo kanda . Ujumbe huu ni chujio lako. Sikiliza na uishi, kataa na ufe.

Je, tunawezaje kuchukua nafasi wakati kikomo chetu cha Milele kina uwalakini? Tunahitaji kuwa daima tunasikia Neno; katika nyumba zetu, katika magari yetu, wakati wakufua nguo, tunapofundisha watoto wetu, tunapoosha magari yetu, tunapokuwa matembezi, na muhimu zaidi, tunapokusanyika katika makanisa yetu.

Unakaribishwa kuungana na sehemu ya Bibi-arusi Wake, inayoamini KILA NENO kwenye kanda, tunaposikia Ujumbe: Chujio la Mtu Mwenye Busara 65-0822E , Jumapili saa 8:00 nane mchana , saa za Jeffersonville ( ni saa 3:00 tatu Usiku ya Tanzania) . Au mtie moyo mchungaji wako acheze kanda kanisani mwako ili wewe pia uweze kusikia Sauti ile ile itakayokutambulisha kwa Bwana wetu Yesu Kristo, na kisha tutarudi duniani tena ili kuishi milele. HAIWEZEKANI KUWA BORA ZAIDI YA HIYO.

Ndugu. Joseph Branham

21-1024 Kristo Amefunuliwa Katika Neno Lake Mwenyewe

Ujume: 65-0822m Kristo Amefunuliwa Katika Neno Lake Mwenyewe

PDF

pakua

BranhamTabernacle.org

Mpendwa Bibi-arusi mwenye changamko,

Hatujawahi kamwe kuwa na furaha kama hiyo , au kuridhika zaidi katika maisha yetu. Tunachangamko kwa Ufunuo zaidi ya hapo awali. Ulimwengu unaporomoka. Watu wameingia wendawazimu kabisa. Tunaona vitu ambavyo tumesikia juu ya maisha yetu yote sasa yakitukia mbele ya macho yetu.

Kila Ujumbe tunaosikia upo katika wakati mkamilifu kabisa na kile hasa tunachohitaji kusikia. Ni Chakula Cha Kiroho Kwa Wakati Wake. Tumeridhika Sio mawazo ya mwanadamu, wala Siyo Maneno ya mwanadamu, Ni Maneno ya Mungu Asemayo kupitia Mwanadamu, kumwita Bibi-arusi Wake atoke.

Tunaweza kusema kutoka kwenye kina cha mioyo yetu:

. Ujumbe huu ni Bwana Asema hivi.

. Ni njia iliyotolewa na Mungu kwa ajili ya wakati huu.

. Hauhitaji fasiri yoyote.

. Ni Maneno yasiokosea.

Kusikiliza mifululizo hii ya mwisho ya Ujumbe imekuwa jambo kuu maishani mwangu. Nataka tu kushiriki nukuu baada ya nukuu na kila mmoja. “Je! Ulisikia nukuu hii… sijawahi kuisikia namna hiyo hapo awali… nilisikiliza kanda hiyo mara 4 katika siku chache zilizopita na sikuwahi kulinasa kama nilivyofanya leo hii. Ujumbe huu ni wa sasa zaidi kuliko wakati ulipohubiriwa miaka 56 iliyopita ”.

Hakuna kitu chochote kama ile furaha kubwa ya kujua unasikiliza Sauti safi ya Mungu iliyothibitishwa. Hakuna haja ya wewe kujiami. Hakuna haja ya kujiuliza, je! Hili Linalingana na Neno.? Hivi Hayo ni mawazo yake au ni fasiri yake? Napaswa niende kulikagua kwenye Neno.

Sio sisi, sisi
tunaketi tu, tunapumzika, na kusema AMEN kwa kila Neno, kwani tunajua kila tunachokisikia ni BWANA ASEMA HIVI.

Haiwi vizuri au rahisi kuliko hivyo.

Nimekuwa nikiomba na kumtafuta Bwana naye ananiongoza kuendelea na jumbe hizi za mwisho ambazo nabii alizonena. Najua tumesikiliza Jumbe hizi zifuatazo miezi michache iliyopita, lakini kila wakati tunapozisikia Yeye hutufunulia mengi zaidi na zaidi .

Ninapofikiria juu ya Bibi-arusi Wake, wamekusanyika pamoja kutoka kote ulimwenguni, wakingojea kwa shahuku kubwa kuuanza Ujumbe wao kumsikia Mungu akizungumza nao kwa midomo ya nabii Wake, mimi hufurahi sana. Je! Yeye atatufunulia nini leo hii?

Kuna uamsho mkuu unaotendeka kote ulimwenguni. Bibi-arusi anapaaza sauti , akisema: “Tunataka kusikia kanda. Tunataka kubonyeza play. Tunataka kuungana na Bibi-arusi kwenye Neno ”.

Tunaungana na kuketi pamoja katika Uwepo wa Mwana, kuivishwa , tukijiandaa kwa ajili ya Unyakuo. Ningependa kukualika uje kuivishwa pamoja nasi saa 8:00 nane Mchana , saa za Jeffersonville, ( ni saa 3:00 tatu usiku ya Tanzania) tunapomsikia Mungu akizungumza na Bibi-arusi Wake na kuleta Ujumbe, Kristo Amefunuliwa Katika Neno Lake Mwenyewe 65-0822M .

Ndugu. Joseph Branham

Maandiko ya kusoma kabla ya kusikiliza Ujumbe:

Kutoka 4: 10-12

Isaya 53: 1-5

Yeremia 1: 4-9

Malaki: 4: 5

Luka Mtakatifu 17:30

Yohana Mtakatifu 1: 1 /1:14 / 7: 1-3 / 14:12 / 15:24 / 16:13

Wagalatia 1: 8

2 Timotheo 3: 16-17

Waebrania 1: 1-3 / 4:12 / 13: 8

2 Petro 1: 20-21

Ufunuo 1: 1-3 / 10: 1-7 / 22: 18-19

21-1017 Nawe Hujui

UJUMBE: 65-0815 Nawe Hujui

PDF

pakua – m4a

pakua – amr 11MB (use Firefox to download)

BranhamTabernacle.org

Tai wanakusanyika Pamoja.

Tai Wapendwa Wanaokusanyika,

Loo, ni kipindi cha namna gani, ni wakati wa jinsi gani! Hakuna kitu ambacho kimeachwa bila kutimia . Tai wa Mungu wanakusanyika kwenye Mzoga. Unabii unatimia. Hakuna hata wakati mmoja ambapo imekosea, wala haitakosea, kwa kuwa sisi, tuliochaguliwa tangu zamani kuliona, tunaliona.

Tangu Baba alipompeleka Nabii Wake Nyumbani, Bibi-arusi Wake hajawahi kuungana kwenye Sauti Yake kama ilivyo leo hii. Alichagua njia ambayo Neno Lake lingekuja, na hiyo ilikuwa kwa manabii Wake, ambao walichaguliwa na kuteuliwa kimbele . Nasi tumeridhika, na kushawishika, ya kwamba huyu ni Yesu Kristo akijitambulisha Mwenyewe , akijitambulisha Mwenyewe katika unabii.

Jinsi Ilivyokuwa kwamba aliwaongoza wana wa Israeli kupitia jangwani, katika safari yao, kama mfano wa watu walioitwa watoke leo hii. Huyu hapa, kwa utafiti wa kisayansi, hata alijitambulisha mwenyewe mbele ya sayansi. Na kwa matendo Yake yenyewe na kwa unabii Wake mwenyewe, mambo ambayo yametabiriwa kwake yeye kuyafanya katika siku hii, kumfanya Yeye kuwa yeye yule jana, leo, na hata milele, yamethibitishwa kikamilifu. Je! Haitoshi kufanya mioyo yetu kuwaka ndani yetu?

Kama Hao mitume wa siku hiyo, tumekusudiwa Uzima, Jambo tu litupasalo kufanya ni kuifanya Sauti Yake ijulikane; Na sauti hiyo ni mawazo ya Mungu mwenyewe yaliyotamkwa. Tunaamini kila sehemu yake . Si lazima tuthibitishe lo lote kisayansi, ama kumuuliza Msadukayo ye yote ama Mfarisayo, ama Mtu Yeyote yule, juu ya jambo hilo. Yeye Alilisema hilo nasi tunaliamini. kondoo Wake huisikia Sauti Yake, ikinena kupitia Nabii wake.

Ujumbe huu ni Sauti ya Mungu kwenye kanda. Ndiyo Ufunuo wote wa Yesu Kristo, Agano la Kale na lile Jipya yakiwekwa pamoja. Siri zote zimefunuliwa. Hatuongezi kwenye hilo au kuondoa kutoka Kwake. Tunafanya hasa kama vile Yeye alivyotuamuru tufanye, DUMUNI NA NENO.

Haya basi. Ni huyo mtu wa ndani. Huyo wa ndani ambaye ataliitikia Neno, atadumu na Neno, haidhuru.

Alitabiri na kutuambia nini kingetokea.
Ulimwengu mzima ungerundikana katika ukichaa, na utaendelea kuwa mbaya na mbaya na mbaya, hata watakuwa kundi la wenye kichaa.

Alisema ile saa imekaribia wakati tutakapoona jambo fulani likitukia, jambo fulani litatukia. Na Jumbe Hizi zote Zilikuwa utangulizi na Zimekuwa zikiweka msingi kwa ajili ya Ujumbe mfupi, na wa haraka ambao utatikisa mataifa yote. Ninaamini sasa tunayaona mambo haya yakitukia sasa hivi.

Nami najua ya kwamba, baada ya kuondoka kwangu kutoka dunia hii, hizo kanda na vitabu vitaendelea kuwepo, na wengi wenu ninyi watoto wadogo mtaona, katika siku zijazo, ya kwamba jambo hili ni Kweli kabisa, kwa maana nanena katika Jina la Bwana .

Hebu na tusikilize na tuangalie kwa undani maelezo yote ya ndoto ambazo nabii alizotuambia . Jinsi walivyomwona amesimama kwenye mwamba uliotandaa kutoka mashariki kwenda magharibi, katika umbo lililochongoka kama piramidi, jinsi alivyokuwa juu ya farasi ambaye hawajawahi kuona kitu kingine kama yeye maishani mwao mwote; farasi mkubwa sana mweupe, mwenye manyoya ya shingoni yamening’inia chini.

Jinsi Wingu jeupe lilivyokuja na likamchukua na likamuondoa , kisha Baada ya kitambo kidogo likamketisha upande wa mbele wa ile meza naye alikuwa mweupe kama theluji Alikuwa Amesimama pale Akinena kwa mamlaka. Hakukuweko na kukisia katika jambo hilo. Kila mtu alifahamu yale hasa Aliyokuwa Anasema.”

“ Nitapanda farasi kupitia njia hii tena !”

Ninaamini tunaliona Jambo hilo Likitendeka leo hii. Jumbe hizi Zimepanda farasi kupitia njia ile tena . Mungu anawaita Tai wake pamoja kutoka kote ulimwenguni. Wanaungana kwenye Neno Lake, Sauti Yake, Ujumbe Huu.

Ulimwengu ni uchi, mnyonge, wenye Mashaka, kipofu, nao haujui. Lakini Bibi-arusi amevikwa Neno, mwenye utukufu wa Roho, akifurahi kwa Neema yake, na tunaweza kuona na kujua sisi ni nani: BIBI-ARUSI WAKE .

Alitueleza kwa kadiri alivyojua, hakuona chochote cha kuzuia, wakati huu, Kuja kwa Bwana Yesu, nje ya utayari wa Kanisa Lake.

Enyi Tai, hebu na Tujifanye wenyewe tayari. Ninakualika kukusanyika pamoja nasi kwenye Mzoga Jumapili saa 8:00 Nane Mchana , saa za Jeffersonville,( Ni saa 3:00 tatu Usiku ya Tanzania), kusikia Sauti ya Mungu kwa ajili ya wakati wetu ikitufanya tayari kwa Unyakuo unaokuja hivi karibuni tunaposikia: 65-0815 Nawe Hujui .

Ndugu. Joseph Branham

Maandiko ya kusoma :

Ufunuo 3: 14-19
Wakolosai 1: 9-20

21-1010 Matukio Yakidhihirishwa Na Unabii

UJUMBE: 65-0801e Matukio Yakidhihirishwa Na Unabii

PDF

pakua – m4a

pakua – amr 11MB (use Firefox to download)

BranhamTabernacle.org

Tai wanakusanyika Pamoja.

Mpendwa Kundi dogo Bibi-arusi Neno Bikira wa Kristo,

Sisi ni Bibi-arusi Neno wake tukisubiri Bwana harusi Neno wetu na fungate yake ya utawala wa miaka Elfu . Tutasikiliza Sauti moja tu . “Kondoo Wangu wanaijua Sauti Yangu. Mgeni Hawatamfuata. ” Sauti yake ni nini?

Sauti ya mtu ye yote ni neno lake. Nalo ndilo Hili, Biblia, neno moja lisiongezwe Kwake au kuondolewa Kwake. Dumuni waaminifu tu kwa Sauti hiyo. “Mgeni hawatamfuata,” madhehebu.

Sauti hiyo ni Sauti Yake, izungumzayo kwenye Kanda kupitia Mfasiri pekee wa Kiungu wa Neno Lake, nabii Wake, William Marrion Branham. Ni Yesu Kristo akinena kupitia midomo ya mwanadamu. Sisi Hatujali maneno ya mwanadamu, mawazo ya mwanadamu au Fasiri ya mwanadamu, Tunaijali tu Sauti iliyothibitishwa kwa ajili ya wakati wetu. Ni BWANA ASEMA HIVI.

Mungu aliiongoza mikono ya nabii wetu. Mungu aliyaongoza macho yake katika maono. Hakuweza kusema kitu chochote ila kile alichokuwa anaangalia. Asingeweza kunena kitu, Maana Mungu Alitawala kabisa ulimi wake, kidole chake, kila kiungo cha mwili wake kilikuwa katika utawala Mkamilifu wa Mungu. Si ajabu kwamba Biblia ilisema manabii Wake walikuwa miungu; walikuwa ni sehemu ya Mungu! Yeye Alikuwa ndiye Neno la Mungu lililodhihirishwa kwa ajili ya wakati wetu.

Biblia hii inatabiri, kwa unabii, ni siku gani tunayoishi, na wakati gani tunaoishi, na ni matukio ya namna gani yanayopaswa kutukia. Inatabiri jambo hilo kikamilifu kabisa, wala haijakosea hata kizazi kimoja, wakati wote. Hakuna hata wakati mmoja ambapo imekosea, wala haitakosea, kwa kuwa waliochaguliwa tangu zamani kuliona wataliona. Ni Neno Likiungana na Neno

Katika Kila wakati, watu wanamwachilia mtu aweke fasiri yao kwenye Neno hili, na inawafanya watu wasione matukio yaliyotukia. Jambo lile lile limefanyika kwa Mafarisayo na Masadukayo.

Waliwaambia watu, “Sisi tumetiwa mafuta na Mungu. Mnatuhitaji sisi kuwambieni kile Neno linachosema. Mnatuhitaji sisi tuwafasirie ninyi. ”

Kama ilivyokuwa katika siku hiyo ndivyo ilivyo leo hii. Upande wa kudanganya ni kwamba wamepakwa mafuta na Roho Mtakatifu. Wana wito kutoka kwa Mungu kufanya huduma ya Neno. Wapo kuwaambia watu kile nabii alichosema, lakini wengi wao huweka FASIRI YAO KWAKE kwa kufanya huduma yao kuwa muhimu zaidi kuliko Sauti ya Mungu.

Angalia jinsi wanavyotaka kujaribu kukusanya watu pamoja kwenye huduma yao, kwenye fasiri yao ya kile manabii wa Mungu walichosema, lakini hawawezi kufanya jambo hilo.

Wanaficha na kuwatisha watu ili kuhalalisha kutocheza kanda katika makanisa yao kwa kusema, “Hao watu wanaweka mkazo sana kwa mtu huyo na wanamwabudu yeye na sio Yesu Kristo. Ni udhehebu kusikiliza ujumbe sote kwa wakati mmoja kutoka sehemu moja. Ndugu Branham hakuwahi kusema chezeni kanda kanisani ”, hivyo kuepuka hasa sababu Yenyewe, hawataki tu kucheza kanda katika makanisa yao. Huduma yao, ufahamu wao, wito wao, ni muhimu zaidi kuliko kusikiliza kanda kanisani. Hawatathubutu kusema kuwa, HAPANA , lakini vitendo vyao vinawasemea.

Mhudumu yeyote wa kweli, anayedai kuamini huu ni Ujumbe wa kweli wa wakati wa mwisho, ni Sauti ya Mungu kwa ajili ya wakati wetu, hangekuwa kamwe na Udhuru wa kutocheza kanda katika kanisa lao. CHUNGUZA TAMSHI HILO PAMOJA NA BIBI-ARUSI NENO.

Sijawahi kusema ni lazima kila Mtu asikilize saa 8:00 nane mchana , saa za Jeffersonville, la sivyo wewe si Bibi-arusi, KAMWE. Sijawahi kumwabudu mtu . Ni Yesu Kristo ndiye anayepokea utukufu wote. Ninamwabudu Mungu aliye ndani ya huyo Mtu kama vile NENO lilivyotuambia tufanye. Jinsi gani walivyo wadanganyifu na vipofu . Soma tu Maandiko ndugu yangu, liko papo hapo.

Ibilisi ANAJUA kwamba mhudumu yeyote, au kundi la wahudumu, HAWAWEZI KAMWE kumuunganisha Bibi-arusi; Hata hawakubaliani wao kwa wao. Kama tu vile Wamethodisti, Wabaptisti, Wapresbyteri na Wapentekoste, anawezaje yeyote mmoja wao au mchanganyiko wao kumuunganisha Bibi-arusi… HAWAWEZI kabisa.

KITU PEKEE KINACHOWEZA KUMUUNGANISHA BIBI-ARUSI NI SAUTI YA MUNGU KWENYE KANDA .. ​​NA INAFANYA HIVYO !

Adui analichukia jambo hilo, kwa hivyo anajaribu kuliangamiza, lakini haitawezekana kufanya hivyo ….UTUKUFU!

Kama kawaida, wao daima, katika mwisho wa wakati, wameingia katika mchafuko kama huo kwa wanatheolojia wao na makasisi mpaka daima_ ni mchafuko. Daima fasiri yao ni mbaya, hakuna hata wakati mmoja imeshindwa kuwa mbaya. Wala hakuna hata wakati mmoja Neno la Mungu limeshindwa kuwa kweli. Hiyo ndiyo tofauti.

Kuna njia moja rahisi tu ya kuwa na hakika, Dumu na Neno, Sauti ya Mungu iliyo kwenye kanda. Soma Biblia yako, itakuambia ni matukio gani yatakayotokea katika siku hii. Itakuambia juu ya malaika Wake mwenye nguvu ambaye atakuja katika siku hii. Itakuambia kudumu na Sauti Hiyo, Kudumu na mjumbe Wake Aliyemchagua.

Ikiwa Shetani anachukia Kitabu chochote cha Biblia, ni kitabu cha Ufunuo. Kiliandikwa na Kristo mwenyewe. Halafu kulingana na roho hiyo, Kristo mwenyewe lazima aweke msisitizo mwingi kuhusu malaika wake wa 7.

Baada ya hayo naliona malaika mwingine akishuka kutoka mbinguni, mwenye Mamlaka kuu; na nchi ikaangazwa kwa utukufu wake.

Kristo Mwenyewe alisema dunia nzima iliangazwa kwa UTUKUFU WAKE. Yeye Hakusema iliangazwa kwa “Utukufu Wangu”. Halafu kulingana na uelewa wako, unamshtaki Kristo mwenyewe kwa yeye kuweka msisisitizo mwingi juu ya Mjumbe wake malaika wa 7.

Mjumbe huyo wa duniani alifanana sana na Kristo mwenyewe, Yohana alijaribu kumwabudu, MARA MBILI, lakini akasema, “HAPANA!, Mwabudu Mungu.” Hilo ndilo hasa tunalofanya, kumwabudu Mungu. Hatuwekei mkazo sana juu ya mtu huyo, tunasema tu kile KRISTO NENO ALICHOSEMA…. “Nchi ikaangazwa kwa utukufu wake”. Hilo Linatupa Changamko Kwa Ufunuo.

Mungu hujichagulia Mwenyewe, kwa kuchagua tangu zamani, akawachagua manabii kwa ajili ya kila wakati. Angalia jambo hilo. Yeye huweka tabia ya huyo nabii ipate kulingana na wakati huo. Mnaona, Yeye huweka mtindo wake, cho chote afanyacho. Yeye humweka kama ana elimu ama hana elimu. Yeye humwekea vipawa, namna atakavyohubiri, karama atakazokuwa nazo. Na Ujumbe wa wakati huo fulani, Mungu alichagua tangu zamani kitu hicho maalum kitendeke wala hakuna kitu kingine kinachoweza kuchukua mahali pake .

Cheza kanda, kanda yoyote , Jumapili, hakuna kinachoweza kuchukua mahali pake. Ikiwa unataka kuungana na Maskani ya Branham tunaposikiliza kanda, unakaribishwa na umealikwa kuungana nasi Jumapili saa 8:00 Nane mchana, saa za Jeffersonville,( ni saa 3:00 tatu Usiku ya Tanzania) tunaposikia: Matukio Yakidhihirishwa Na Unabii 65-0801E .

Ndugu. Joseph Branham

Maandiko:

Mwanzo: 22: 17-18

Zaburi: 16:10 / Sura 22 yote/ 35:11 / 41: 9

Zekaria 11:12 / 13: 7

Isaya: 9: 6/40: 3-5 / 50: 6/53: 7-12

Malaki: 3: 1/sura ya 4 yote

Yohana Mtakatifu 15:26

Luka Mtakatifu : 17:30 / 24: 12-35

Warumi: 8: 5-13

Waebrania: 1: 1/13: 8

Ufunuo: 1: 1-3 / Sura ya 10 yote

21-1003 Mungu Wa Wakati Huu Mwovu

UJUMBE: 65-0801m Mungu Wa Wakati Huu Mwovu

PDF

pakua – m4a

pakua – amr 13MB (use Firefox to download)

Mpendwa Bibi-arusi Changamko kwa Ufunuo,

Ni nini kilikuwa kinatukia kote ulimwenguni wikendi hii iliyopita? Ni kitu gani kilikuwa kinatendeka? Vifijo hivyo vyote vilikuwa ni vya nini? Bibi-arusi kutoka kote ulimwenguni waliungana pamoja, na kutengeneza milima kwa plasta, udongo, mchanga na vijiti. WakiKukusanyika kwenye mioto iwakayo , kuimba nyimbo za ibada na kumsifu Bwana. Vijana kwa wazee wote namna moja, wakiwa wamevaa fulana sinazosema Changamko Kwa Ufunuo. Walikuwa kutoka Michigan hadi Florida, kutoka Maine hadi California, kutoka Amerika Kaskazini hadi Amerika Kusini, Ulaya, Afrika, Asia, Australia, kila kona ya dunia. Walikuwa wakisikiliza kwa kuunganishwa katika nyumba zao, wakisikia Sauti ya Mungu ikiwazungumzia moja kwa moja.

Nini kilichovutia? Uzao wa Mungu uliochaguliwa tangu awali ambao hauwezi kufanya vinginevyo isipokuwa kufuata Ujumbe wa wakati huu , ambao wanaamini kila Neno lililonenwa na kinywa cha Mungu, walikuwa wamekusanyika pamoja katika sifa, katika kuabudu, na katika kusherehekea tukio kuu lililotukia katika siku yetu juu ya Mlima Sunset.

Ilikuwa ni Mungu akithibitisha Neno Lake. Ndio maana ya kelele zote hizi . Angalia, ni Mungu akitimiza Neno Lake lililoahidiwa tena, la Ufunuo 10: 1 hadi 7, “Na katika siku za kutangazwa kwa Ujumbe wa malaika wa saba, siri ya Mungu itatimia .”

Ilikuwa ni Mungu akifanya historia. Ilikuwa ni Mungu akitimiza unabii. Lilikuwa jibu la unabii wa nabii. Na tulitamani kuwapo pale ili kupata na kusikia chochote ambacho Yeye alichofanya kupitia nabii Wake.

Tunapuuza ukosoaji wa Asiyeamini na waamini wa kujifanya. Hatuna hoja nao. Tuna jambo moja la kufanya, hilo ni kuamini na kupata kila sehemu yake tuwezayo. Tunakusanyika pamoja kila wiki kama wa moja kusikia Sauti ya Mungu, tunapongojea kuja kwa Masihi.

Ni Saa kuu jinsi gani tunayoishi. Kuona Maandiko yanatimizwa katika maisha yetu. Lakini Alituonya katika Neno Lake kwamba upako wa uwongo ungefanana sana, ungewapoteza KAMA Yamkini walio wateule wa Mungu. Lakini Mungu asifiwe, haitawezekana kumpoteza Bibi-arusi Wake, kwa maana wao watadumu na ile Sauti ya Mungu ya asili, iliyodhihirishwa, na iliyothibitishwa na hawatabadilisha nukta moja au yodi moja. Hawataongeza fasiri yao wenyewe Kwake, lakini kirahisi wataamini KILA NENO.

Tunapaswa kuwa waangalifu sana jinsi gani kama WATAFANANA SANA . Tunashangaa, je yatakuwa ni haya makanisa ya kimadhehebu? Wao Wanaonekana wako nje mbali sana na hata hawafanani. Basi Atakuwa ni nani?

Sasa, makanisa tu baridi, ya kawaida, magumu, na kadhalika, ya theolojia za kujitengenezea, hayo hayangeweza; walio Wateule wasingewajali. Lakini ni kule juu karibu sana na jambo lililo halisi. Kuacha tu Neno moja ndivyo tu unavyopaswa kufanya.

Alisema Hawa hakuondoka tu kirahisi akasema siamini Mungu.Yeye aliamini kosa. Shetani yeye alikubali hilo lilikuwa Neno la Mungu, lakini shida ilikuwa aliweka fasiri yake mwenyewe kwake na ilimfanya hawa aamini uwongo na alihukumiwa nao.

Jalada limeondolewa. Piramidi imefunguliwa. Maandiko yamefunuliwa. Ufunuo Amepewa Bibi-arusi. Ni Yesu Kristo yeye yule jana, leo na hata milele.

Hilo Linamfanya Shetani atukasirikie sana. Anajua amefikia mwisho wake. Yeye Anataka tujiulize sisi ni akina nani. Tunapitia mitihani na majaribu magumu kuliko tulivyowahi kupitia. Wakati mwingine tunajiuliza, kwa nini haya yote yanatutokea?

Sababu yake ni kwamba, ni kumjaribu Yeye, Bibi-arusi Wake. Ni ku-…Wakati amedhihirishwa, akajaribiwa, kuthibitishwa, akathibitishwa kwa Shetani

Utukufu !!! Majaribu na mitihani yetu ni Yeye tu akimthibitishia Shetani SISI NDIYE BIBI-ARUSI WAKE ALIYETHIBITISHWA

Tunaona sasa, wakati huu mwovu ni kuthibitisha, kwa Shetani, Yeye si kama Hawa, ya kwamba Yeye si mwanamke wa namna hiyo. Naye atajaribiwa kwa Neno Lake , Bibi-arusi, kama bibi-arusi wa Adamu alivyojaribiwa kwa Neno. Na bibi-arusi wa Adamu aliamini kila sehemu ya Neno, lote, ila akachanganyikiwa kwenye ahadi moja .

Lakini hatutachanganyikiwa hata kwa Neno moja au kufuata mapokeo yao, Fasiri zao za Neno, tutadumu na NENO LA ASILI.

Kama tuna kinasasauti, tutakusanya kundi la watu pamoja, na tuicheze, na kusikiliza kwa makini, kama vile alivyotuambia tufanye!

Ni kama tu vile uhai wako wa kawaida na tabia inavyoridhiwa na kuzaliwa kwa asili kwa baba yako, ndivyo alivyo Roho wa Mungu, aliyechaguliwa tangu kuwekwa misingi ya ulimwengu.

Tunashukrani jinsi gani kwamba Roho wa Mungu, kuzaliwa kwetu, kulichaguliwa kabla ya kuwekwa misingi ya ulimwengu kuwa na Ufunuo wa Kweli wa Ujumbe Huu.

Unakaribishwa kuja kupata Changamko lile lile kwa ufunuo pamoja nasi Jumapili saa 8:00 nane mchana , saa za Jeffersonville , (ni saa 3:00 tatu Usiku ya Tanzania) tunaposikia: 65-0801M Mungu Wa Wakati Huu Mwovu.

Ndugu. Joseph Branham

Maandiko ya kusoma:

Mathayo Mtakatifu 24/27: 15-23

Luka Mtakatifu 17:30

Yohana Mtakatifu 1: 1 / 14:12

Matendo 10:49

1 Wakorintho 4: 1-5 / 14 sura yote

2 Wakorintho 4: 1-6

Wagalatia 1: 1-4

Waefeso 2: 1-2 / 4:30

2 Wathesalonike 2: 2-4 / 2:11

Waebrania sura ya 7

1 Yohana Sura ya 1 / 3:10 / 4: 4-5

Ufunuo 3:14 / 13: 4 / Sura ya 6-8 na 11-12 / 18: 1-5

Mithali 3: 5

Isaya 14: 12-14